Monday, 19 June 2023

Picha : RC MNDEME AKUTANA NA MACHINGA...SAKATA LA BANDARI MOTOO!! "SHINYANGA HATUDANGANYIKI"

Mkuu wa  Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na Machinga mkoa  wa Shinyanga kupitia Shirikisho la Umoja wa Machinga Mkoa wa Shinyanga na Taifa.


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa `Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amekutana na kuzungumza na wajasiriamali wadogo mkoa wa Shinyanga kupitia Shirikisho la Umoja wa Machinga Mkoa wa Shinyanga ambapo ametumia fursa kutoa ufafanuzi kuhusu azimio la kuridhia Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kupitia Kampuni yake ya DP World kuhusu Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi wa Bandari Tanzania huku Machinga wakiunga mkono suala la uwekezaji katika Bandari.

Mkutano huo umefanyika leo Jumatatu Juni 19,2023 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambapo wajasiriamali hao wadogo na viongozi wao ngazi ya Mkoa na taifa wamehudhuria mkutano huo.


Akizungumzia kuhusu azimio la kuridhia Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kupitia Kampuni yake ya DP World kuhusu Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi wa Bandari Tanzania, Mkuu huyo wa Mkoa amesema Mkataba huo una manufaa makubwa katika mkoa wa Shinyanga na taifa kwa ujumla kwa sababu mkoa wa Shinyanga upo jirani na masoko ya nchi jirani.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na Machinga

“Sisi Shinyanga ni lango la kiuchumi, uwekazaji haukuanza leo, kwanini watu wanapotosha kwa malengo gani?, Rais wetu ni Mzalendo, tumuache afanye kazi, tusifanye upotoshaji”,amesema Mndeme.

Amesema kutokana na kwamba Kampuni ya DP World kwa kuzingatia uzoefu wake katika uendeshaji wa shughuli za bandari barani Afrika, Asia, Ulaya na Amerika ya Kaskazini na Kusini,Uwekezaji huo katika Bandari ya Dar es salaam utaleta manufaa katika kupunguza muda wa meli kukaa nangani kutoka siku 5 mpaka masaa 24 na kupunguza gharama za utumiaji wa Bandari na kufungua masoko ya kimkakati katika eneo la bidhaa na biashara ya usafirishaji ndani ya nchi na kanda jirani.


“Shinyanga hatudanganyiki, Machinga hatudanganyiki, tunataka bidhaa zije kwa spidi. Rais wetu anania nzuri ya kutaka bidhaa ziwahi kuja machinga wapate bidhaa wauze, wanataka kutukatisha tamaa, hili halikubaliki. Haiwekezani tumkatishe tamaa Rais wetu”,ameongeza Mndeme.

Mndeme amesema serikali inaendelea kushirikiana na Machinga katika kuliletea maendeleo taifa hivyo kuwaomba wafanyabiashara hao kuepuka kutumiwa vibaya na watu wasioitakia mema nchi ya Tanzania.

Masoko yanaendelea kujengwa na sasa hivi hakuna biashara hazifungwi. Mhe. Rais Samia ameleta shilingi Bilioni 612 kwa ajili ya maendeleo mkoani Shinyanga. Naomba msikubali kutumika na watu wasiotutakia mema,wenye nia mbaya. Tumuunge mkono Mhe. Rais Samia, Amani yetu tusiivuruge”,amesema Mndeme.
“Kama mtu anataka ugomvi na mimi akamate machinga, atakuwa haki yangu, fuateni sharia na taratibu za kufanya biashara. Nyie Machinga wa mkoa wa Shinyanga mnajielewa vizuri, mna hofu ya Mungu. Nawaahidi hakuna machinga atakayesumbuliwa Shinyanga, serikali ipo pamoja na nyinyi ilimradi mnazingatia sheria”,amesema Mndeme.

“Niwaombe katika masoko yetu, tutaweka sehemu kwa ajili ya faragha ya wanawake kunyonyesha watoto, anafanya biashara lakini pia mtoto naye anapata haki yake”,ameongeza.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wafanyabiashara kuwa mstari wa mbele kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Akisoma tamko la  Umoja wa wafanyabiashara ndogondogo (Machinga)  Mkoa wa Shinyanga kuhusu mapendekezo ya kuridhia mkataba baina ya serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya kuendeleza na kuboresha utendaji kazi wa Bandari Tanzania , Mwenyekiti wa Shirikisho Mkoa wa Shinyanga Boniphace Petro amesema wameridhia azimio hilo kwa maslahi ya taifa.

"Tumepokea maelezo ya awali kuhusu mapendekezo ya kuridhia Mkataba baina ya serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendeshaji  na uboreshaji  kazi wa Bandari Tanzania. Mhe. Mkuu wa Mkoa ametupitisha katika maelezo ya mapendekezo ya kuridhia mkataba na tumeelewa lengo la serikali ni jema kwani serikali inapambana kutuletea maendeleo katika nchi yetu",amesema Mwenyekiti huo wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Mkoa wa Shinyanga.

"Sisi Machinga Mkoa wa Shinyanga tunabariki na kuridhia makubaliano ya Uwekezaji katika bandari huku tukilaani vikali wale wanaokosoa makubaliano na kupotosha jamii kwa uchochezi wa maneno yasiyo na tija. Tunaahidi kuwa mabalozi wema katika maeneo yetu na tutakuwa sehemu ya wanaoelezea kwa nia njema juhudi za maendeleo zinazofanywa na Serikali katika nchi yetu. Tunatanguliza shukrani zetu kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutupambania na kutuletea maendeleo  katika mkoa wetu na nchi yetu kwa ujumla”,amesema.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na wajasiriamali wadogo mkoa  wa Shinyanga kupitia Shirikisho la Umoja wa Machinga Mkoa wa Shinyanga na Taifa. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na wajasiriamali wadogo mkoa wa Shinyanga kupitia Shirikisho la Umoja wa Machinga Mkoa wa Shinyanga na Taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na wajasiriamali wadogo mkoa wa Shinyanga kupitia Shirikisho la Umoja wa Machinga Mkoa wa Shinyanga na Taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na wajasiriamali wadogo mkoa wa Shinyanga kupitia Shirikisho la Umoja wa Machinga Mkoa wa Shinyanga na Taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na wajasiriamali wadogo mkoa wa Shinyanga kupitia Shirikisho la Umoja wa Machinga Mkoa wa Shinyanga na Taifa.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Mkoa wa Shinyanga Boniphace Petro akisoma tamko
Mwenyekiti wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Mkoa wa Shinyanga Boniphace Petro akisoma tamko
Mwenyekiti wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Mkoa wa Shinyanga Boniphace Petro akisoma tamko
Wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini

Wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Share:

MUME WANGU APONA KIFUNGO CHA MAISHA KWA KOSA LA KUSINGIZIWA

Familia yetu yenye jumla ya watu sita pamoja na dada wa kazi tumeishi kwa furaha katika kipindi chote tukitegema kulishwa na mume wangu katika kazi zake za utafutaji huko Shirika la Reli.

Nilizoea kuona mume wangu anafanya kazi usiku na mchana kwa wiki kwa kuwa shirika lile lilikuwa limejiwekea taratibu za ufanyaji kazi kwa awamu yaani shift. Miaka ishirini na nne ya kwenye ndoa nimeshuhudia mume wangu akifanya kazi pasina tatizo lolote lile ofisini kwake.

Kwa kweli bila ya msaada wa daktari BAKONGWA ningempoteza mume wangu gerezani. Siku mmoja ikiwa ni ajabu sana kwa mume wangu kufanya kazi mchana na usiku yaani kwa siku mmoja akafanya shift zote mbili nilishtuka lakini sikutaka kujua nini kina mchanganya. Jioni ya chakula aliinita na kuniambia kuwa anahitaji apumzike kwa hivyo sauti za radio zisiwe juu sana.

Kesho ya siku hiyo baada ya tukio hilo asubuhi yake tulishangazwa kuona askari wanne waliovaa nguo za askari wa wanyamapori wakisindikizwa na mwenyekiti wa mtaa tunapoishi wamekuwa wageni nyumbani pale.


Mara moja walimuwekea mume wangu pingu mikononi mwangu na kumchukuwa huku wakituacha sisi kwa hasira wakitupa maneno kuwa amekuwa akishirikiana na majangiri pembe za ndovu katika safari za treni ziendazo mikoani.

Tulidharilika mtaani kwa tukio hilo lakini hatukuwa na la kufunya, kulingana na sheria kali zilizowekwa dhidi ya ujangiri hakukuwa na wasaa wa kutafuta shuhuda bali walimtupa mahabusu mara moja wakituahidi kuwa kesi yetu itasikilizwa mahakamani baada ya wiki mbili kusudi tupishe sherehe za sikukuu za kitaifa.

Nilijitahidi kufanya maombi na kutafuta haki katika ngazi za serikalini hususani katika ofisini zake za kazi lakini hatukupata msaada. Sheria kali iliyokuwa mbele yetu kwa makosa hayo ya ilikuwa kifungo cha maisha kwa kuhujumu uchumi wa malighafi za wanyamapori, nilijihisi kutomfahamu mume wangu kabisa.

Siku ya hukumu ikakaribia nikiwa mwenye kukata tamaa kwani kila jambo nimejaribu bila ya kufaulu nilitembelewa na shemeji yangu na kuniambia nimtafute daktari bakongwa huko whatsapp +243990627777 na tovuti zake https://bakongwadoctors.com  nitembelee kabla ya kusikilizwa hukumu ya mume wangu mahakamani.

Nilimtafuta daktari haraka haraka tukampa maelekezo ya kutosha kuhusu mambo yaliyokuwa yanatuchanganya yeye akatia msisitizo kuwa kila kitu kitakuwa sawa tuondoe shaka akatoa maelekezo ya dawa za kutumia na kuahidi kuwa ndani ya siku mbili kabla ya hukumu nitumie dawa zile, alinitumia dawa zile zikanifikia nikazipokea ambapo ndani yake kulikuwa na kikiratasi chenye maelekezo ya matumizi ya dawa hizo

Tena nikafanya hivyo, nilishangaa sana ile siku ya hukumu jina la mume wangu kusomwa na kusemwa kuwa uchunguzi umefanyika na kuonekana kuwa amesingiziwa na viongozi wake wa juu huko ofisini kwake aliachiliwa huru.Kwa kweli ninasema asante sana daktari tulikuwa tukimpoteza baba kwa bila ya sababu.


Share:

Sunday, 18 June 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JUNI 192023



























Share:

ZUNGUSHA GURUDUMU LA BAHATI SLOTI YA STICKY 777!!


Sloti ya Sticky 777

 

Unawaza ni biashara gani ya kuzungusha pesa yako na ikakulipa haraka Zaidi, basi usiwaze hilo limeisha, ukiwa na Meridianbet kasino ya mtandaoni unapata fursa ya kuzungusha pesa yako kwenye gurudumu la bahati, na ukishinda unapewa papo hapo, ni sloti ya Sticky 777.

 

Alama kubwa zaidi kwenye sloti hii ni Sticky 777 ambayo ina malipo makubwa kwenye mchezo wa kawaida wa kasino ya mtandaoni. Ukizipata alama za 3,4 &5 utapata Gurudumu la Bahati. Kasino ya mtandaoni inakupa faida mara 1000 ya dau lako.

 

Sloti ya Sticky 777 pia ina alama nyingine kama vile almasi, kengele na matunda kama vile tikiti maji, nanasi, limao na mengine mengi. Unaweza kupata ushindi mkubwa kama alama 3 au zaidi ya hizi zitakusanywa. Katika mistari 10 ya malipo, unaweza kushinda almasi na kengele zenye thamani kubwa lakini pia, unaweza kushinda miti ya matunda maarufu.

Zungusha Gurudumu la Bahati ya kasino ya mtandaoni kwenye Sloti ya Sticky 777.

 

Sloti ya Sticky 777 ina uwezo wa kurudia kuzungusha gurudumu, sifa hii inatokea pale ambapo wilds mbili zitatokea kwenye reels. Baadhi ya bonasi za gurudumu la bahati zinapatikana katika mfumu huu; alama tatu zitakupeleka katika gurudumu la bahati la hatua ya kwanza ambapo utaweza kupata faida mara 50 zaidi ya dau lako.

 

Alama 4 zitakupeleka katika gurudumu la bahati la hatua ya 2 ambapo utaweza kupata faida mara 125 ya dau lako. Alama 5 zitakupeleka kwenye hatua ya 3 ambapo utaweza kupata faida mara 1000 zaidi ya dau lako.

 

Mchezaji ataweza kusogea kwenye hatua inayofuata endapo gudurumu litasimama likiwa na mishale katika hatua mojawapo kati ya hatua mbili. Kusonga mbele hakutoi zawadi ya pesa lakini ni mwanzo wa kusogea kwenye hatua zilizo na zawadi kubwa zaidi.

 

Kwa ujumla Sloti ya Sticky 777 kupitia Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet ina machaguo mbalimbali. Unaweza kuchagua ubashiri/Gamble ili kuongeza ushindi wako mara mbili zaidi.

 

NB: Kubwa kuliko ni kwamba ukijisajili Meridianbet unazawadiwa mizunguko ya bure kucheza kasino ya mtandaoni, jisajili hapa.


Share:

HUDUMA ZA MSIMBOMILIA ZITAONGEZA THAMANI YA BIDHAA ZETU- WAZIRI GWAJIMA






Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitaifa wa maonesho ya wiki ya Msimbomilia kwenye viwanda jijini Dar es Salaam.


Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1 Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Majukwaa ya Uwezeseshaji Wanawake Kiuchumi, Fatma Kange,,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitaifa wa maonesho ya wiki ya Msimbomilia kwenye viwanda jijini Dar es Salaam.


Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa kitaifa wa maonesho ya wiki ya Msimbomilia kwenye viwanda jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,akikagua bidhaa mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kitaifa wa maonesho ya wiki ya Msimbomilia kwenye viwanda jijini Dar es Salaam.




Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa kitaifa wa maonesho ya wiki ya Msimbomilia kwenye viwanda jijini Dar es Salaam.

Na WMJJWM, Dar es Salaam

Serikali imesema itaendelea kushirikiana na taasisi inayosimamia utoaji wa huduma za Msimbomilia na Ufuatiliki GS1 Tanzania kuweka utaratibu wa kuchangia kuwawezesha wanawake wajasiriamali ili kujikwamua kiuchumi kwa kuzipatia bidhaa wanazozalisha Barcodes.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kitaifa wa maonesho ya wiki ya Msimbomilia kwenye viwanda jijini Dar es Salaam.

Waziri Gwajima amesema kutokana na umuhimu wa msimbomilia ikiwemo kufanya bidhaa kutambulika kimataifa na kuingia kwenye maduka madogo na makubwa Serikali iliamua kusimamia na kushiriki katika mchakato wa kuanzishwa kwa taasisi itakayosimamia kisheria utoaji wa huduma za Msimbomilia na Ufuatiliki katika bidhaa zinazozalishwa nchini na nje ya nchi, kwani awali kulikuwa na changamoto ya bidhaa zinazozalishwa nchini kukosa utambuzi katika mifumo ya kimataifa ya Kidigitali.

"Nafurahi kusikia kuwa GS1 Tanzania imeanza kuchukua hatua za dhati za kuhakikisha kuwa bidhaa za Kitanzania pia zinaweza kuingia kwenye Maduka Makubwa ya Kisasa kwa kuanzisha Programu ya Mafunzo katika Halmashauri zote Nchini kupitia OR-TAMISEMI kwa kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali zenye majukumu yanayoendana na kuwajengea uwezo wajasiriamali kama vile TRA, TBS, TRDO, SIDO, TANTRADE na TCCIA ambazo zote zina majukumu ya kuhakikisha elimu ya viwango, utambuzi wa bidhaa na masoko kuwa zinawafikia wananchi wote kwa kuanzia ngazi ya Halmashauri".

Dkt. Gwajima ameongeza kuwa, awali ukosefu wa huduma ya msimbomilia nchini ulifanya bidhaa kutotambulika katika mifumo ya kimataifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wakati wa mauzo hivyo Serikali kukosa mapato kupitia ongezeko la thamani kwenye bidhaa zinazouzwa kwa njia ya reja reja.

Waziri Dkt. Gwajima amebainisha kwamba Tanzania ni kati ya nchi chache Afrika kupata leseni ya Shirika la GS1 Global lenye hati miliki ya huduma ya msimbomilia ambapo nchi nyingine ni Algeria, Misri, Ivory Coast, Kenya, Libya, Mauritius, Morocco, Nigeria, Senegal, Afrika Kusini hali inayochangia Tanzania kutoa huduma hiyo kwa nchi zinazoizunguka na kupanua wigo wa wateja.

Ametoa wito kwa Uongozi na Menejimenti ya GS1 Tanzania kuwa na mikakati ya kuzifikia nchi jirani kuhakikisha wanatumia Msimbomilia (Barcodes) za Tanzania ili kuongeza pato na kuitangaza nchi.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1 Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Majukwaa ya Uwezeseshaji Wanawake Kiuchumi, Fatma Kange amebainisha changamoto ya wafanyabiashara wengi kukosa maeneo ya uzalishaji wa bidhaa zao na kuiomba Serikali kuona namna ya kuwapa maeneo.

"Wazalishaji wengi bado wanafanyia shughuli zao nyumbani, hivyo tunaomba tukipata eneo la ekari 10 tu popote hapa Dar es salaam".
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 182023

 











Share:

Saturday, 17 June 2023

Video Mpya : BHUDAGALA MWANAMALONJA - MBYALA


Bhudagala Ng'wana Malonja ameachia ngoma mpya inaitwa Mbyala
Tazama Video Hapa chini
Share:

Live : UWASILISHWAJI WA BAJETI KUU YA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024

Share:

WAZIRI MKENDA AITAKA TET KUWEKA MAZINGIRA ENDELEVU YA WALIMU WANAOMUDU VIZURI STADI ZA UFUNDISHAJI SHULE ZA UMMA NA BINAFSI

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akizungumza wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Stadi za Ufundishaji kwa Walimu wa Elimu ya Awali na Msingi iliyofanyika jijini Dar es salaam.

Na.Mwandishi Wetu-Dar es Salaam

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameitaka Taasisi ya Elimu Tanzania kuweka mazingira endelevu ya kutambua walimu wanaomudu vizuri stadi za ufundishaji kwenye shule za umma na Binafsi.

Waziri Mkenda ametoa rai hiyo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Stadi za Ufundishaji kwa Walimu wa Elimu ya Awali na Msingi ambapo amesema Walimu wanahitaji motisha mbalimbali ikiwemo katika kutambua katika kazi wanayofanya

Amesema ubora wa elimu hapa nchini pamoja na mageuzi ya elimu bila kuwa na walimu wenye hamasa itakuwa ni kazi bure.

“Ningependa kwenye hili la kutambua stadi za ufundishaji TET muweke mazingira endelevu, najua kwa sasa Mradi wa BOOST umewezesha na mmefika katika halmashauri 26 nataka muende kwenye halmashauri zote na Tuzo hizi ziwe endelevu na kazi hii mfanye pamoja na Wizara ili hata baada ya Mradi iweze kuendelea ”amesema Prof. Mkenda

Prof. Mkenda amewaeleza walimu kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa walimu na kwamba Sera mpya ya elimu itaendeleza mafunzo kazini kwa walimu na itasisitiza fursa za walimu kusoma.

Waziri Mkenda ametumia fursa hiyo kuishukuri Benki ya dunia kwa namna inavyofadhili miradi mbalimbali ya elimu hapa nchini na pia kwa kuwezesha hafla ya utoaji wa Tuzo kwa washindi wa Stadi za Ufundishaji kwa Walimu wa Elimu ya Awali na Msingi kupitia Mradi wa BOOST.

Nae Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania Preeti Arora amesema Ushindani wa ujuzi wa kufundisha ni moja ya njia bora za maendeleo ya kitaaluma ya mwalimu na kwamba inaweza kuwa sehemu na sehemu ya mpango wa MEWAKA kwani Ushindani huwapa walimu fursa ya kuonyesha ujuzi wao na kujifunza kutoka kwa wenzao.

“Kwa kushiriki katika ushindani, waalimu wanahamasishwa kuendelea kuboresha mbinu zao za kufundisha, kupanua maarifa yao, na kuendeleza mikakati mpya ya kushiriki na kuhamasisha wanafunzi wao kujifunza. Hii inasababisha ukuaji wao wa kitaaluma na huongeza ubora wa jumla wa elimu, hongera walimu wote mlioshinda,” amesema mkurugenzi huyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt. Aneth komba amesema utoaji wa tuzo hii ni ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa BOOST ambao unafadhiliwa na Benki ya Dunia na unalenga kuboresha uwezo wa walimu katika ufundishaji na ujifunzaji wa wanafunzi kupitia Mafunzo Endelelevu ya Walimu Kazini (MEWAKA).

“Shindano la Stadi za Ufundishaji kwa Walimu wa Elimu ya Awali na Msingi lilianza mwezi wa nne kwa kukusanya na kutathmini video za walimu zenye maudhui ya ufundishaji na ujifunzaji wa kuhesabu pamoja na Somo la Hisabati katika Halmashauri 26 zinazotekeleza Mradi wa BOOST,” amesema Dkt. Komba.

Amesema pamoja na washindi kupata fedha, cheti na wengine ngao video zao zitarekodiwa upya katika studio za TET na kupakiwa katika mfumo wa ujifunzaji na ufundishaji wa LMS na hivyo kuzidi kuleta chachu ya ufundishaji unaozingatia ujenzi wa umahiri.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akizungumza wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Stadi za Ufundishaji kwa Walimu wa Elimu ya Awali na Msingi iliyofanyika jijini Dar es salaam.


Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt. Aneth komba ,akizungumza wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Stadi za Ufundishaji kwa Walimu wa Elimu ya Awali na Msingi iliyofanyika jijini Dar es salaam.


Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (hayupo pichani),akizungumza wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Stadi za Ufundishaji kwa Walimu wa Elimu ya Awali na Msingi iliyofanyika jijini Dar es salaam.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akikabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Stadi za Ufundishaji kwa Walimu wa Elimu ya Awali na Msingi iliyofanyika jijini Dar es salaam.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa hafla ya utoaji Tuzo za Stadi za Ufundishaji kwa Walimu wa Elimu ya Awali na Msingi iliyofanyika jijini Dar es salaam.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger