Saturday, 17 June 2023

Picha : ASKOFU BUGOTA AWEKA JIWE LA MSINGI NYUMBA YA KIASKOFU KANISA LA AICT DAYOSISI TEULE YA KAHAMA


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota ameweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga iliyopo mtaa wa Shunu kata ya Nyahanga Manispaa ya Kahama.


Askofu Bugota ameweka jiwe la Msingi la Mradi wa ujenzi wa nyumba ya Kiaskofu leo Jumamosi Juni 17,2023 ambayo ni moja ya kazi za kitume zikiwa ni utekelezaji wa mpango mkakati wa Kanisa la AICT ambao unajishughulisha na malengo matano ya Kimkakati (Waefeso 2:10).

Akizungumza wakati akiweka jiwe hilo la msingi, Askofu Bugota amewapongeza na kuwashukuru waumini wa Kanisa la AICT ‘The Champions’ walioanzisha hoja ya kujenga nyumba ya Kiaskofu huku akisisitiza kuwa nyumba hiyo itafunguliwa mwezi Agosti,2023 wakati wa wiki ya maombi.


“Hii ni hatua nzuri na kubwa sana baada ya kupewa Dayosisi teule ya Shinyanga na Simiyu. Wakati tunafanya wiki ya maombi mwezi Agosti, Askofu Mkuu atafungua nyumba hii ili tulale humu”,amesema Askofu Bugota.
Muonekano wa nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga

“Tunamshukuru sana Mungu kila mahali kanisa la AICT tumekuwa na watu ambao tunawaita The Champions wanaanzisha maono hata kama wengine tunafuata baadae kwa kusuasua lakini nashukuru sana kwa taarifa hii sasa kwamba huduma hii iliyoanzishwa na The Champions leo hii imekuwa huduma inayoungwa mkono na waumini wote”,amesema Askofu Bugota.


Ameeleza kuwa Baraza la Utendaji la AICT katika vikao vyake vya kawaida lilitoa ushauri katika Sinodi kuu iliyopita kwamba kanisa liendelee kupanua huduma ya injili nchini kwa hiyo Dayosisi ya Shinyanga imepewa jukumu la kuanzisha Dayosisi mbili mpya ambazo ni Kahama na Simiyu na tayari wameshaunda kikosi kazi cha kushughulikia uanzishwaji wa hizo Dayosisi.


“Kwa hiyo tunapoweka jiwe la msingi katika nyumba hii tunataka kutambulisha tu kwamba msingi wetu sisi kama waumini ni Yesu Kristo, huo ndiyo msingi imara, na kama Yesu atakuwa sehemu ya msingi katika Maisha yetu, tunaamini hata changamoto nyingi za kijamii tunazopambana nazo leo zitakuwa hazipo, maana Yesu hutengeneza upendo, Maisha ya uadilifu na anatupa pia matumaini ya milele na hata kama tunapita katika changamoto za Maisha Yesu ndiyo anabaki wa kutegemewa”,ameongeza Askofu Bugota.
Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota.

Tutumie nafasi hii kumsimamisha Yesu katika Maisha ya watu. Nyinyi wenyewe mnashuhudia wakati ambapo tunazungumzia ukatili wa Maisha, mmomonyoko wa maadili katika taifa hili. Serikali na sisi viongozi wa dini umekuwa wimbo wa mchana na usiku kukemea maovu hayo.


Tunaona tamaduni zinabadilika na tunaingia kwenye makosa ambayo kwa kweli hata ubinadamu haupo, leo hii wanaume kwa wanaume wanaweza kuoana au wanawake kwa wanawake wanaweza kufunga ndoa, katika mamlaka ya Mungu ni kinyume cha neno la Mungu. Sisi waumini na watumishi wa Mungu tutasimama katika neno hilo hadi siku ya kufa kuwaambia watu kuwa huo ni uovu na siyo msingi wa neno la Mungu”,amesema Askofu Bugota.


Akisoma taarifa fupi ya ujenzi wa nyumba ya utumishi (Kiaskofu), Katibu wa Kanisa la AICT Jimbo la Kahama Mjini, John Mtumai amesema mpaka sasa nyumba hiyo ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 80% inakadiriwa kutumia rasilimali vitu vya ujenzi na rasilimali fedha kiasi cha shilingi Milioni 100.


Amefafanua kuwa kutokana na mwamko mkubwa wa kanisa wenye kiu ya maendeleo ya kanisa, Ono la kujenga nyumba hiyo ilianza na wadau wa maendeleo ambao ni wazalendo wa kanisa wachache walionunua kiwanja na kukikabidhi kwa kanisa kisha ujenzi ulianza kwa kasi.


“Nitumie fursa hii kuwatambua wabeba maono wa kazi hii kubwa kwa kanisa na kuleta hamasa kwa kanisa letu la AICT ni Mwinjilisti Mathias Mtolo, Amos Sospeter, Charles Daudi Machali na Elisha Amos. Watumishi hawa wa Mungu wamefanya kazi kubwa sana kiu yao ni kuona kanisa letu linapata maendeleo na huduma ya Krsito na hivyo kuwepo kwa hamasa katika makanisa yetu ndani na nje ya Jimbo la Kahama na sasa kazi hii inaungwa mkono na kanisa lote la AICT”,ameeleza Mtumai.

“Pamoja na kazi hii ya ujenzi wa nyumba hii ambayo ni makazi ya Askofu mtarajiwa wa Dayosisi tarajiwa ya Kahama ambaye atakaa humo, mipango mingine ya muhimu kuanza nayo ni ujenzi wa nyumba moja ya katibu wa Dayosisi teule ya Kahama ambapo tayari kiwanja kipo”,amesema Mtumai.

Mtumai ameitaja mipango mingine ni kununua magari matatu ya ofisi ya Dayosisi teule (mpango upo), kuanzisha vitega uchumi vya dayosisi mfano shule, hospitali, vituo vya kati ambayo vitaleta maendeleo katika kanisa sambamba na eneo la kujenga ofisi za dayosisi na Kanisa la Uaskofu (Cathedtral) ambapo kiwanja kipo mtaa wa Malunga – Kahama chenye ukubwa wa hekari tatu na kina ramani ya mipango miji.

Sambamba na uwekaji jiwe la msingi la nyumba ya Kiaskofu pia kumefanyika harambee kwa ajili Ujenzi wa nyumba ya Kiaskofu katika Kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga itakayofunguliwa mwezi Julai 2023 kwa ajili ya kuweka vigae na kumalizia ujenzi wa nyumba ya kiaskofu Dayosisi teule ya Kahama ambayo itafunguliwa mwezi Agosti 2023.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota akizungumza wakati akiweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga leo Jumamosi Juni 17,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota akiongoza ibada wakati akiweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga leo Jumamosi Juni 17,2023. 
Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota (wa tatu kushoto) akikata utepe wakati akiweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga leo Jumamosi Juni 17,2023. 
Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota (wa tatu kushoto) akikata utepe wakati akiweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga leo Jumamosi Juni 17,2023. 
Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota (wa tatu kushoto) akikata utepe wakati akiweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga leo Jumamosi Juni 17,2023. 
Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota akiweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga leo Jumamosi Juni 17,2023. 
Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota akiweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga leo Jumamosi Juni 17,2023. 
Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota akisoma maandishi baada ya kuweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga leo Jumamosi Juni 17,2023. 
Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota akiomba baada ya kuweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga leo Jumamosi Juni 17,2023. 
Muonekano wa nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga
Muonekano wa nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga
Muonekano wa nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga
Viongozi na waumini wa Kanisa la AICT wakiongozwa na Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota wakiwasili katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga
Viongozi na waumini wa Kanisa la AICT wakiwa katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama mkoani Shinyanga
 Katibu wa Kanisa la AICT Jimbo la Kahama Mjini, John Mtumai akisoma taarifa fupi ya ujenzi wa nyumba ya utumishi (Kiaskofu) Dayosisi teule ya Kahama

Katibu wa Kanisa la AICT Jimbo la Kahama Mjini, John Mtumai akisoma taarifa fupi ya ujenzi wa nyumba ya utumishi (Kiaskofu) Dayosisi teule ya Kahama
Katibu wa Maendeleo , Mipango na Uchumi Kanisa la AICT Jimbo la Kahama Mjini, Mwinjilisti Mathias Mtolo akizungumza wakati Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota akiweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama. Wengine ni wabeba maono wa kazi hiyo ya ujenzi wa nyumba ya kiaskofu
Mhasibu Msaidizi wa kamati ya uchumi, mipango na maendeleo ya Kanisa la AICT Kahama Mjini, Charles Daudi Machali akizungumza wakati Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota akiweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama. 
Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota akiongoza maombi baada ya kuweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama

Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zachayo Enock Bugota akiongoza maombi baada ya kuweka Jiwe la Msingi katika Nyumba ya Utumishi ya Kiaskofu ya Dayosisi teule ya Kahama
Muonekano wa Kanisa la AICT Kahama Mjini
Muonekano wa Kanisa la AICT Kahama Mjini

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog



Share:

TBS YAKABIDHI VYETI NA LESENI 264 KWA WAZALISHAJI WA BIDHAA AMBAZO ZIMEKIDHI MATAKWA YA VIWANGO

Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt.Athuman Ngenya akikabidhi vyeti na leseni kwa wazalishaji wa bidhaa ambazo zimekidhi matakwa ya Viwango. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 17,2023 Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam

******************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limekabidhi vyeti na leseni 264 vikiwemo vyeti na leseni 257 za kuthibitisha ubora wa bidhaa pamoja na vyeti saba (7) vya kuthibitisha ubora wa mifumo (Management system certification).

vyeti na leseni zimetolewa kwa wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa kukidhi matakwa ya Viwango kwa kipindi cha kuanzia mwezi Oktoba, 2022 hadi Mei, 2023.

Akizungumza na Waandishi wa habari katika hafla hiyo ambayo imefanyika leo Juni 17,2023 Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt.Athuman Ngenya amesema leseni na vyeti 107 ambayo ni sawa na asilimia 41.6 vilitolewa kwa wajasiriamali wadogo wadogo.

Vyeti na leseni zilizotolewa ni za bidhaa za vyakula, vipodozi, vifaa vya ujenzi, vilainishi, vifaa vya umeme, trela, vibebeo, vifungashio pamoja na mifumo ya utoaji huduma.

Aidha amesema kwa kipindi cha kuanzia mwezi Oktoba 2022 mpaka Mei, 2023 wamekwisha sajili maeneo (maduka, maghala, magari) 1,394 ya kuuza, kuhifadhi au kusambaza bidhaa za vyakula na vipodozi. Pia, kwa kipindi hicho wameweza kusajili bidhaa 1255 za vyakula na vipodozi toka nje ya nchi.

Pamoja na hayo amewasisitizia wajasiriamali hao kuwa mabalozi wazuri katika matumizi ya Viwango ili kufikia lengo la Tanzania ya viwanda hasa katika kipindi hiki ambapo Tanzania tupo uchumi wa kati.

Hafla hiyo imebeba kauli mbiu ya ubora ya mwaka huu wa 2022/2023 inayosema “Dhamira bora fanya kwa usahihi”. Kauli mbiu hiyo ni ujumbe tosha kwa wazalishaji kuwa ubora wa bidhaa unaanza na nia njema ya kuzalisha bidhaa kwa kuzingatia matakwa ya sheria, kanuni na miongozo iliyopo kwa hiari na kwa usahihi, ili kuhakikisha watumiaji wanapata bidhaa bora muda wote.


Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt.Athuman Ngenya akikabidhi vyeti na leseni kwa wazalishaji wa bidhaa ambazo zimekidhi matakwa ya Viwango. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 17,2023 Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt.Athuman Ngenya akizungumza katika hafla ya utoaji vyeti na leseni kwa wazalishaji wa bidhaa ambazo zimekidhi matakwa ya Viwango. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 17,2023 Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora TBS, Bw.Lazaro Msasalaga akizungumza katika hafla ya utoaji vyeti na leseni kwa wazalishaji wa bidhaa ambazo zimekidhi matakwa ya Viwango. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 17,2023 Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam

Meneja wa Uthibitishaji bidhaa TBS, Bi.Amina Yasini akizungumza katika hafla ya utoaji vyeti na leseni kwa wazalishaji wa bidhaa ambazo zimekidhi matakwa ya Viwango. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 17,2023 Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam

Share:

Friday, 16 June 2023

MACHIFU WAZEE NA VIONGOZI WA DINI SHINYANGA WABARIKI UWEKEZAJI BANDARI YA DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Baraza la wazee, viongozi wa dini na Machifu Mkoani Shinyanga wameuunga mkono makubaliano ya uwekezaji kwenye bandari ya Dar es salaam kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kupitia Kampuni yake ya DP World wenye lengo la kuanzisha ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii katika Uendelezaji wa Maeneo ya Bandari Nchini.


Tamko hilo limetolewa leo Juni 16,2023 kwenye kikao na uongozi wa mkoa huo katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni Siku chache baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha azimio la kuridhia Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kupitia Kampuni ya DP World kuhusu Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi wa Bandari Tanzania.

Akisoma tamko hilo lililopitishwa kwa makubaliano ya watu wote na kusomwa na Chief wa Kizumbi Chief. Charles Njange amesema wamekubaliana na kuunga mkono makubaliano ya uwekezaji uliofanywa baina ya nchi hizo mbili na kulaani wale wanaopotosha jamii juu ya makubaliano hayo kwa uchochezi wa maneno yasiyokuwa na tija na staha.

“Sisi wazee, viongozi wa dni na machifu wa Mkoa wa Shinyanga tunakubali na kuunga mkono makubaliano haya yaliyofanywa na serikali yetu ya awamu ya sita, kwani haya ni mahusiano mazuri ya kiuchumi baina ya nchi hizi mbili, lengo la serikali yetu ni jema kwani serikali inapambana kutuletea maendeleo katika nchi yetu”, amesema Chief. Charles Njange.

"Wazee tunalaani kitendo cha baadhi ya watu wachache wanaotaka kumpaka matoke Rais Dkt. Samia Suluhu Hasan kwa kusema ameuza bandari kwa falme za kiarabu,inatupasa kutumia busara ya kawaida na kuwakataza wengine wanaopotosha, tuungane na viongozi wetu kuleta maendeleo katika nchi yetu, tunabariki na kuunga mkono jitihada hizo", ameongeza Chifu  Charles Njange.


Awali akizungumza wakati wa kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme ameeleza manufaa yatakayopatikana ndani ya mkoa kutokana na makubaliano ya uwekezaji wa bandari ya Dar es salaam ambapo amesema kuwa ndani ya mkoa wa Shinyanga kuna bandari kavu mbili zitakazotoa fursa za ajira kwa vijana mpaka sasa mkoa wa Shinyanga umepokea Shilingi Bilioni 612.3 kwa ajili ya shughuli za kimaendeleo.


Nao baadhi ya wazee walioudhuria kikao hicho akiwemo Fransisca Ngokolo na Mohamed Mkambala wamesema kuwa maendeleo ya nchi yanaletwa na juhudi zinazofanywa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo Shinyanga ni moja ya Mikoa inayonufaika na fedha za serikali kwenye miradi mbalimbali hivyo wataendelea kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita.
Chief wa Kizumbi Chief. Charles Njange akisoma tamko wakati wa kikao.
Baadhi ya washiriki walioudhuria kikao hicho.

Baadhi ya washiriki walioudhuria kikao hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza wakati wa kikao hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude wakati wa Kikao.
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Habibu akichangia wakati wa kikao hicho.
Share:

KATIBU MKUU UTUMISHI AWAHIMIZA WATUMISHI WA e-GA KUWA WAADILIFU


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Juma Mkomi, amewataka watumishi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kuzingatia maadili ya utumishi wa umma ili kulinda maslahi ya taifa.


Mkomi alitoa kauli hiyo hivi karibuni, wakati wa kikao kazi cha watumishi wa e-GA na viongozi wa Wizara kilicholenga kujadili utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka.


Alisema kuwa, watumishi wa e-GA wanashiriki katika kazi muhimu zinazohusu mifumo na miundombinu muhimu ya TEHAMA serikalini hivyo, wanapaswa kuwa waadilifu kwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, pamoja na kutunza siri ili kulinda maslahi ya nchi.



"Nyinyi ndio mnahusika na mifumo ya serikali ikiwemo mifumo nyeti inayohusu rasilimali na usalama wa taifa, hakikisheni nafasi mliyonayo mnaitumia kutekeleza majukumu yenu tu kwa uadilifu na kutunza siri ili kulinda taifa letu", alisema.


Vilevile aliwapongeza watumishi hao kwa weledi na utendaji kazi mzuri katika utekelezaji wa majukumu yao, hali ambayo inachangia ukuaji wa Serikali Mtandao katika taasisi za umma.


"Napokea simu nyingi sana aidha kutoka kwa Makatibu Wakuu au Wakuu wa taasisi za umma, wakiomba vijana kutoka e-GA hii inaonesha ni jinsi gani mlivyo wazuri katika utendaji kazi wenu" alisisitiza.


Ili kuongeza ufanisi na ubunifu katika TEHAMA, Mkomi aliutaka uongozi wa Mamlaka kuwajengea uwezo watumishi wake kwa kuwapa mafunzo ya muda mrefu na mfupi ndani na nje ya nchi.


Alisema, teknolojia hukua na kubadilika kila mara, hivyo ni vema Mamlaka ikaweka utaratibu wa kuwajengea uwezo watumishi wake ili kuweza kukabiliana na mabadiliko hayo.


Kikao kazi hicho kilifanyika katika Ofisi za e-GA zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, na kuongozwa na Mhe. George Simbachawene Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Naibu Waziri Mhe. Ridhiwani Kikwete pamoja na Katibu Mkuu Bw. Juma Mkomi.
Share:

RAIS SAMIA AHUTUBIA MKUTANO WA EITI ATAKA UWEKEZAJI WENYE MANUFAA SEKTA YA MADINI


Dakar

Rais Samia Suluhu Hassan amehutubia kwa njia ya mtandao mkutano wa kimataifa wa Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Sekta ya Madini, Mafuta na Gesi Asilia (EITI) uliofanyika Jijini Dakar, Senegal.


Mkutano huo ulifanyika chini ya udhamini wa Rais Macky Sall wa Senegal, Bodi ya EITI na wadau wa sekta za uziduaji.


Katika hotuba yake fupi aliyowasilisha mbele ya washiriki zaidi ya 1,500 toka nchi zaidi ya 90; Rais Samia alisistiza umuhimu wa wavunaji wa raslimali za madini kuhakikisha kuwa uwekezaji wao unawanufaisha wananchi wanaoishi katika maeneo husika.


Amesisitiza umuhimu wa mataifa yenye rasilimali kuwa na uwazi kwenye uwekaji na kuweka hadharani kumbukumbu za uzalishaji wao zinazoonyesha mchango stahiki wanaochangia jamii na pato la taifa. 


Kwa sasa nchi 57 duniani ni wanachama hai wa EITI, huku Tanzania ikiwa miongoni mwao kupitia taasisi yetu ya TEITI.


Ujumbe wa Tanzania uliowakilisha taifa letu kwenye Mkutano huo uliongozwa na Dkt. Steven Kiruswa, Naibu Waziri wa Madini.


Wajumbe sita walioambatana na naibu waziri ni Dkt. Abdulrahaman Mwanga, Kamishna wa Madini, Mhe. Danstan Kitandula, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, pamoja na Mhe. Jesica Kishoa, Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini. 


Wengine ni Bi Mariam Mgaya, Kaimu Mtendaji wa TEITI, Ndugu Ludovic Utouh, Mwenyekiti wa Kamati ya TEITI na Ndugu Adam Anthony, Mjumbe wa Kamati ya TEITI.


Mkutano huu ambao ulifunguliwa na Waziri Mkuu wa Senegal kwa niaba ya Rais Macky Sall pia ulihudhuriwa na mawaziri wakuu toka nchi mbali mbali sambamba na waliohudhuria kwa njia ya mtandao akiwemo Tony Blair, Waziri Mkuu mstaafu wa Uingereza.


Katika mkutano huo, ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Dkt. Kiruswa uliwasilisha mada kuhusu fursa za uwekezaji katika sekta ya madini nchini Tanzania.

Share:

SLOTI YA ODD ONE OUT INAKUPA USHINDI MKUBWA


 


Sloti ya Odd One Out

Ligi nyingi zimeisha na kupisha dirisha la usajili ili kujiimarisha Zaidi kwa msimu ujao, nataka kusema na wadau wa kubeti, Meridianbet kasino ya mtandaoni ni chimbo jingine la kuendelea kupiga hela haswa kwa wachezaji wa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti kama hii ya Odd One Out.



Kupitia sloti hii, Meridianbet kasino ya mtandaoni inakupa njia 243 za kutengeneza ushindi, unaanzaje kushindwa kuwa bilionea? Mchezo huu una mfumo wa safu 5 kwa 3, huku ukiwa na mpaka mistari 243 ya ushindi.



Namna ya Kucheza sloti ya Odd One Out

Ukifungua Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, tafuta mchezo wa Odd One Out. Weka dau lako kwa mfumo wa sarafu yaani “coin”. Baada ya hapo bonyeza kitufe cha alama ya mzunguko kilichopo katikati kuanzisha mchezo wa kasino ya mtandaoni. Baada ya hapo subiria ushindi mnono.



Njia za Ushindi Katika Sloti ya Odd One Out

Kasino ya mtandaoni hii ina alama nyingi, lakini kuwa makini. Alama ya chungwa inaweza kukupa mpaka sarafu 400!



Sloti ya Odd One Out, inaweza kukupa zawadi nyingi zaidi ya pesa! unapocheza Odd One Out utapata bonasi ya mizunguko ya bure, na alama ya Wild ambayo inakupa ushindi mnono kwa kukupa mara mbili ya ushindi wako endapo utaipata katika ushindi wako. Usisahau kuwa, mchezo huu pia unaweza kukurudishia mpaka 96.04% ya dau lako!



Wkati mismu wa ligi nyingi umemaliza, ni muda sasa wa kuelekeza nguvu kwenye kucheza kasino ya mtandaoni ili kukusanya maokoto mengi Zaidi, na kubwa Zaidi sloti nyingi za Meridiabet zinakupa bonasi kibao.


NB: Kingine ni kwamba ukijisajili Meridianbet unazawadiwa mizunguko ya bure kucheza kasino ya mtandaoni, jisajili hapa.

 

 


Share:

GGML YATOA ELIMU YA HAKI WAJIBU MAADHIMISHO SIKU YA MTOTO WA AFRIKA


Regina Mabula Afisa uhusiano kutoka GGML akizungumza na Watoto kuhusu siku yam toto wa Afrika
Rebbeca Manace kutoka Jeshi la Polisi dawati la Jinsia Geita Akitoa elimu juu ya haki za Watoto

*****


Na Mwandishi Wetu

KATIKA kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imeshirikiana na wadau mbalimbali likiwemo Jeshi la Polisi kitengo cha dawati la jinsia pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Geita kutoa elimu mbalimbali juu ya haki na wajibu wa mtoto katika jamii katika maeneo yanayozunguka mgodi ikiwemo Bugulula, Kasota na Nyawilimilwa.


Katika maadhimisho hayo ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 16 Juni, GGML imefanya kampeni mbalimbali kutoa elimu juu ya haki za mtoto wa Afrika na wajibu wake ndani ya jamii.


Akizungumza mjini Geita kwa niaba ya GGML Meneja mwandamizi anayesimamia mahusiano ya jamii kutoka GGML, Gilbert Mworia amesema kuwa watoto ni sehemu muhimu katika jamii ambayo inapaswa kushirikishwa katika nyanja mbalimbali za maendeleo.


“Siku ya mtoto wa Afrika ni muhimu kwa kila mmoja wetu kwa kuwa inatukumbusha umuhimu wa kundi hili ndani ya jamii yetu. Watoto ni taifa la sasa na kesho, tunapaswa kuwalinda kwa kuwapatia haki zao za msingi ikiwemo elimu. 


“GGML itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali yenye kuwanufaisha watoto ndani ya mkoa wa Geita na Tanzania kwa ujumla ikiwemo ujenzi wa shule, vituo vya afya, miundombinu na miradi endelevu yenye tija kwa maendeleo endelevu,” alisema akitoa wito kwa wazazi na walezi kutoruhusu watoto kuingia maeneo ya migodi kutafuta kipato kwa kuwa ni mazingira hatarishi.


Akitoa elimu kwa watoto na wazazi katika Shule ya Msingi Kamlale iliyopo kata ya Nyawilimwila katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Rehema Kabanda amesema kuwa serikali itaendelea kuhamasisha matumizi bora ya kidigitali ili kumwepusha mtoto na masuala yasiyo na tija katika jamii.


“Kauli mbiu ya Siku ya Mtoto wa Afrika inasisitiza kuzingatia usalama wa mtoto katika ulimwengu wa kidigitali.Tunatoa wito kwa wazazi na walezi kuwaongoza vyema watoto wao juu ya matumizi salama ya kidigitali kwa kuwa ni chanzo cha mmomonyoko wa maadili ndani ya jamii na kuathiri maendeleo yetu wote,” alisema Rehema Kabanda.


Siku ya Mtoto wa Afrika ni siku inayosherehekewa kila mwaka tarehe 16 Juni, ilianza kuadhimishwa mwaka 1991 ilipoteuliwa na Umoja wa Afrika kuenzi michango ya watoto walioshiriki katika maandamano katika mji wa Soweto, Afrika Kusini mwaka 1976 pamoja na kujengea jamii uelewa juu ya umuhimu wa elimu bora kwa watoto.


Katika siku hiyo, maelfu ya watoto katika nchi ya Afrika Kusini walikusanyika katika mji wa Soweto kwa ajili ya maandamano yenye malengo ya kudai elimu bora. Mamia ya watoto walipigwa risasi na kuuliwa wakati watoto zaidi ya elfu moja walijeruhiwa.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNI 162023


Share:

Thursday, 15 June 2023

WABAKAJI MAARUFU WAJIKUTA WAKITOKWA MOSHI PUANI



Huwa ni jambo la ovyo sana mtu anapopata ushawishi wa kuiba kitu cha mtu mwingine ambacho hakukifanyia kazi, tabia ya wizi ni tishio kwa maendeleo ya jamii na imepelekea watu wengi kuogopa hata kuwekeza kwenye biashara ndogondogo.

Katika kauti ya Busia genge la wezi watano lilionyeshwa cha mtema kuni baada ya kuiba Pikipiki, kulingana na walioshuhudia kisa hicho, genge hilo lilikuwa limesumbua wakazi wa eneo hilo kwa muda sana.

Maduka yao yalikuwa yakivunjwa, bidhaa zao kuibiwa, kina mama walikuwa wakibakwa kila walipokuwa wakirejea nyumbani na hata watu kadhaa walikuwa wameuawa kutokana na ukatili wa genge hilo. Uwepo wa hilo genge kwenye mitaa ya Busia ama kwa hakika ulikosesha wakaazi wa eneo lile usingizi.

Hata hivyo, siku hiyo genge lilo lilirejesha Pikipiki ya Bwana mmoja wakiwa wameibeba bengeni, kilichoshangaza wengi, ni wezi wale walikuwa wakila nyasi kama ng'ombe huku wakitoa moshi kwenye pua.

Wezi wale walipofika kwa yule bwana mwenye pikipiki ndivyo mambo yaliwazidi unga kwani walianza kula mchanga huku wakivua nguo na kubaki uchi. Wazee kwa vijana, kina mama kwa watoto walijitokeza kujionea tamthilia ya bure kabisa, Wanahabari nao hawakuwachwa nyuma.

Mwenye Pikipiki ile alipohojiwa alisema kwamba alikuwa amechoka na genge lile kwani lilikuwa limeangaisha mtaa ule kwa muda mrefu sana, basi umati ulikuwa ukishangilia sana, Polisi walijaribu kusambaratisha umati ule lakini waliambulia patupu.

Wanahabari waliendelea kumhoji mwenye Pikipiki ile na akawaambia kuwa African Doctors ndiye alikuwa fundi aliyemsaidia kuwanasa jamaa wale. Aliongeza kwamba ili wezi wale warejee kwenye hali yao ya kawaida inatakiwa African Doctors wajulishwe kwanza ndio watatoa muongozo.

Baada ya dakika chache African Doctors walipigiwa simu na wezi wale walitakiwa walipe Ksh90,000 ile waweze kurejea katika hali yao ya kawaida.

Basi jamaa yule mwenye pikipiki aliwatafuta ndugu wa genge lile na mwishowe akawapata na kuwaarifu jinsi African Doctors walivyosema, basi nao walilipa kitita cha fedha ambacho waliambiwa na hapo mambo yakarejea kama kawaida kwani African Doctors hakusita na kurekebisha mambo.

Tangu siku ile wizi wa Pikipiki na vitu vingine katika mji ule umepungua sana kwani kila mtu anaheshimu mali ya mwenzake, mtu yeyote anayesumbuliwa na wizi anaweza kuwasiliana na African Doctors na kupata ufumbuzi mara moja.

African Doctors wamekita mizizi katika eneo nzima la Afrika mashariki kwa ueledi wake wa kutibu magonjwa kama vile kifaa, msukumo wa damu na mengineyo, pia wanasuluhisha migogoro ya ndoa na mahusiano.

Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com au watumie email; africandoctorheals@gmail.com

Mwisho.


Share:

KASINO YA MTANDAONI SLOTI YA WILD WILD RICHES

 

Sloti ya Wild Wild West Riches

Nikisema Meridianbet nyumba ya mabingwa namaanisha, kwanini nasema hivyo! Ni ujio wa sloti ya kijanja ya Wild Wild West Riches hii ni sloti ya kitajiri inayopatikana kasino ya mtandaoni ya Meridiannbet, unapata bonasi kibao.


Kupitia sloti ya Wild Wild West Riches, unaweza kupata faida mpaka mara 4608 ya dau lako kupitia Jakipoti Bonanza kwenye sloti hii. Unasubiri nini?


Jinsi ya Kucheza Sloti ya Wild Wild West Riches

Mambo ni mazuri Zaidi Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. unapocheza sloti ya Wild West Riches, unatakiwa kuangaza macho yako kwenye mtungi wenye dhahabu. Mtungi huu utakupatia bonasi ya kukusanya pesa/Money Collect.


Unaweza kuvuna pesa kibao au kuzidishiwa dau lako maradufu kila unapoipata bonasi hii. Kumbuka, bonasi ya Money Collect inaweza kuzidisha dau lako mpaka mara 500.


Nikikwambia Meridianbet ni nyumba yenye bonasi kubwa, namaanisha! Hawaishii hapo tu. Kupitia sloti ya Wild Wild West Riches, una nafasi ya kushinda mpaka mizunguko 20 ya bure kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Karibu ujiunge na familia ya Mabingwa wa Michezo ya Kubashiri!


Kumbuka unaweza kushinda mara dufu na jakipoti kibao za kasino ya mtandaoni ya Meridianbet kushirikiana na waandaaji wake. Endelea kufurahia kasino ya mtandaoni na kujiweka karibu zaidi na ushindi.

 

NB: Kubwa kuliko ni kwamba ukijisajili Meridianbet unazawadiwa mizunguko ya bure kucheza kasino ya mtandaoni, jisajili hapa.



Share:

SLOTI YA MKWANJA NI HII HAPA!


 

 Umewahi kucheza michezo ya kasino ya mtandaoni? Ubashiri wa michezo ni maarufu sana kwa mamilioni ya watu kote duniani. Hili ndilo dhumuni kubwa la Meridianbet kwenye sloti hii, kuleta ubashiri wa michezo kwenye kiwanda cha sloti.

 

Inapatikana kwenye Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet pekee. Lucky Betting Shop ni mashine ya sloti inayofurahisha na kukupa zawadi kedekede kwenye michezo. Kumbuka, sio ubashiri wa kasino ya mtandaoni ila ni ubashiri madukani. Inaonesha uhalisia wa dukani ikiwa ni pamoja na tiketi za ubashiri ambazo zinakupa mchanganyiko wa ushindi.

 

Lucky Betting Shop ni sloti bora kwa mashabiki wote wa michezo ya kasino ya mtandaoni. Hii haifanani na michezo ya sloti. Lakini, imeweka utaratibu wa kubashiri kwenye mfumo wa sloti, mashine yake imetengenezwa kwa upekee.

 

Kujaza Tiketi za Ubashiri

 

Sloti ya Lucky Betting Shop ina malipo 1024. Kiwango cha chini cha kubeti ni sarafu 25. Kila ushindi unazidishwa kwa sarafu ya ubashiri na unalipa kuanzia kushoto kwenda kulia. Utofauti upo kwenye ushindi uliotawanywa ambao unalipwa popote.

 

Alama za Lucky Betting Shop ni pamoja na vifaa vya ubashiri wa michezo. Kila kitu kinafanyika kwenye Lucky Betting Shop ambapo unaweza kushinda kutoka kwenye michezo mingi.

 

Washirika wa kadi ni alama za chini na ushindi, wakati watupaji na wafanyakazi wanalipa zaidi. Tiketi ya kubashiri ni ya mwitu, ikibadilisha alama zote katika mchanganyiko wa kushinda isipokuwa kutawanyika.

 

Alama zina malipo mchanganyiko. Zinaweza kutokea katika ukubwa kamili au nusu. Zinapotokea katika ukubwa nusu, zinalipa kutokana na jedwali la malipo. Mwanamke nyuma ya kaunta analipa mara 250 ya dau lako. Mtupaji yupo chini zaidi kwenye orodha, analipa mara 100 ya mchanganyiko uleule.

 

Kwenye mchezo wa mwanzo, machaguo yanaweza kuongezwa kwenye reels kati ya 50x na 250x ya dau lako. Kuna nafasi moja tu ya kushinda kwenye reel iliyoongezwa. Sifa hii hii inapatikana kwenye mizunguko ya bure ambapo utaweza kushinda kwa tabiri za kushangaza.

 

Bonasi Unaipata.

 

Sloti ya Lucky Betting Shop ina mizunguko ya bure ambayo inaweza kupatikana sehemu yeyote ya reels. Utapata jumla ya mizunguko 15 ya bure ambayo inawezakurudiwa. Mchezo unatumia reels maalumu kwenye mzunguko huu. Mizunguko ya bure inachezwa muda wa kubashiri.

 

Kuna sifa nyingine ambayo inawafurahisha zaidi wapenzi wa michezo ya kubashiri haswa kasino ya mtandaoni. Inaitwa Tiketi ya ubashiri na inaweza kupatikana kwa kubofya kwenye bet slip chini kabisa kwenye pembe ya kushoto.

 

Huu ni ubashiri wa ziada ambao unaweza kufanyika mwanzoni mwa mchezo. Unaweza kuwa na tiketi 2 zinazoweza kutumika. Ili kutumia sifa hii unatahitajika kwanza kuchagua alama moja kati ya tatu na idadi ya mizunguko.

 

Kwamfano, unaweza kuchagua mfanyakazi au mtupaji kutokea mara 21 au 25 kwenye mizunguko 12. Kisha unachagua ubashiri wako upande wa kulia na kuanza mchezo. Kama utaweza kupata alama zako kama ulivyochagua kwenye mizunguko 12, utashinda tiketi yako ikiwa imezidishwa.

 

NB: Kubwa kuliko ni kwamba ukijisajili Meridianbet unazawadiwa mizunguko ya bure kucheza kasino ya mtandaoni, jisajili hapa.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger