Thursday, 15 June 2023

TGNP YAKUTANISHA WADAU KATIKA KIJIWE CHA KAHAWA KUFUATILIA MUBASHARA HOTUBA YA HALI YA UCHUMI NA BAJETI YA TAIFA IKISOMWA BUNGENI


Mkuu wa Program kutoka TGNP Bi. Clara Kalanga akifungua Mjadala na Uchambuzi wa Bajeti ya Taifa ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 maarufu Jukwaa la ‘Kijiwe cha Kahawa’ kwa niaba ya Mkurugenzi wa TGNP, leo Alhamis Juni 15,2023 katika ukumbi wa TGNP jijini Dar es salaam 


Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) limekutanisha wadau wa masuala ya jinsia katika Mjadala na Uchambuzi wa Bajeti ya Taifa ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 maarufu ‘Kijiwe cha Kahawa’ ili kuwapa fursa kufuatilia mubashara Hotuba ya Hali ya Uchumi wa taifa 2022/2023 na Mpango wa Maendeleo ya taifa kwa mwaka 2023/2024 pamoja na Hotuba ya Bajeti ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 ikiwasilishwa Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.


Akifungua Mjadala na Uchambuzi wa Bajeti ya Taifa ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 maarufu Jukwaa la ‘Kijiwe cha Kahawa’  kwa niaba ya Mkurugenzi wa TGNP, Mkuu wa Program kutoka TGNP Bi. Clara Kalanga leo Alhamis Juni 15,2023 katika ukumbi wa TGNP jijini Dar es salaam amesema lengo la Jukwaa la Kijiwe cha Kahawa ambalo limekuwa likiandaliwa na TGNP kwa miaka minne sasa ni kuwapa fursa wadau mbalimbali kufuatilia hutoba ya bajeti Mubashara na kuweza kutoka maoni na mapendekezo yao yatakayowezesha uboreshaji wa utekelezaji wake kwa mrengo wa kijinsia.


“Kwa mwaka huu dhima ya Kijiwe cha Kahawa ni kuhamasisha dhana ya ushirikishwaji kwa makundi yote ili kuandaa na kutekeleza bajeti zenye mrengo wa kijinsia ‘Promoting inclusive budgetary process for a gender responsive 2023/2024 budget”,amesema Kalanga.


Ameeeza kuwa Kijiwe cha Kahawa ni mojawapo ya majukwaa ya TGNP kujenga nguvu za pamoja ili kuleta chachu ya mabadiliko chanya ya kisera, kiutendaji na kifikra.


“Kukutana kwetu hapa ni kwa ajili ya kuhamasisha nguvu za pamoja katika kudai utengwaji wa bajeti kwa mrengo wa kijinsia ili kutatua changamoto za makundi mbalimbali katika jamii hasa yale yaliyo pembezoni kama vile wanawake, wanaume maskini, watu wenye ulemavu na vijana”,ameongeza Kalanga.


Amesema kwa miaka 30 sasa TGNP imekuwa mstari wa mbele katika kujenga uwezo na ushawishi juu ya bajeti yenye mrengo wa kijinsia na imekukuwa ikijihusisha na mchakato wa bajeti kila mwaka kwa kuwawezesha wanawake na makundi yaliyo pembezoni katika ngazi za jamii kushiriki kikamilifu kupitia mchakato wa fursa na vikwazo (O&OD) unaofanyika katika ngazi ya jamii kuweza kuibua vipaumbele vyao na pia kuwaunganisha na mjadala wa kitaifa ili kudai utengwaji wa rasilimali kwa ajili ya masuala ya jamii kwa ujumla.


“Tunaipongeza serikali kwa kutuonesha nia ya kuendeleza usawa wa kijinsia nchini kwa kuchukua hatua katika kutekeleza baadhi ya mapendekezo ambayo tumekuwa tukiyatoa kupiti chambuzi zetu za bajeti na kupitia ushiriki wa wadau mbalimbali. Hata hivyo tunaiomba serikali kutumia matokeo haya katika mipango na bajeti ili vipaumbele viendane na mahitaji ya makundi husika”,amesema Kalanga.


“Tunatambua na tunaendelea kupongeza jitihada za serikali yetu katika kuridhia utekelezaji wa mikataba mbalimbali ya kitaifa,kikanda na kitaifa ili kuendeleza usawa wa kijinsia nchini. Ili kuweza kutekeleza kwa ufanisi mikataba hii na sera na mipango mingineyo, Bajeti yenye mrengo wa kijinsia ni suala la msingi”ameongeza.


Amefafanua kuwa ikiwa rasilimali za kutosha hazitatengwa, hazitatolewa na kutekelezwa kwa wakati, kufikia usawa wa kijinsia na maendeleo endelevu itakuwa ni ndoto.

Wakichangia hoja wakati wa majadiliano hayo, wadau hao wameipongeza serikali kwa kuanzisha huduma za kibingwa za matibabu katika Hospitali huku wakionesha wasiwasi juu ya huduma hizo za kibingwa kuwanufaisha wananchi waliopo maeneo ya pembezoni ambako hata zahanati tu hazipo na zingine zikiwa zinakabiliwa na changamoto mbalimbali.
Mkuu wa Program kutoka TGNP Bi. Clara Kalanga akifungua Mjadala na Uchambuzi wa Bajeti ya Taifa ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 maarufu Jukwaa la ‘Kijiwe cha Kahawa’ kwa niaba ya Mkurugenzi wa TGNP, leo Alhamis Juni 15,2023 katika ukumbi wa TGNP jijini Dar es salaam. Picha na Kadama Malunde 1 blog
Mkuu wa Program kutoka TGNP Bi. Clara Kalanga akifungua Mjadala na Uchambuzi wa Bajeti ya Taifa ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 maarufu Jukwaa la ‘Kijiwe cha Kahawa’
Mkuu wa Program kutoka TGNP Bi. Clara Kalanga akifungua Mjadala na Uchambuzi wa Bajeti ya Taifa ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 maarufu Jukwaa la ‘Kijiwe cha Kahawa’
Mkuu wa Program kutoka TGNP Bi. Clara Kalanga akifungua Mjadala na Uchambuzi wa Bajeti ya Taifa ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 maarufu Jukwaa la ‘Kijiwe cha Kahawa’
Mkuu wa Program kutoka TGNP Bi. Clara Kalanga akifungua Mjadala na Uchambuzi wa Bajeti ya Taifa ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 maarufu Jukwaa la ‘Kijiwe cha Kahawa’
Wadau wa masuala ya Kijinsia wakiwa katika Ukumbi wa TGNP Mabibo Jijini Dar es salaam wakisikiliza mubashara Hotuba ya Hali ya Uchumi wa taifa 2022/2023 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2023/2024 ikiwasilishwa Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.
Wadau wa masuala ya Kijinsia wakiwa katika Ukumbi wa TGNP Mabibo Jijini Dar es salaam wakisikiliza mubashara Hotuba ya Hali ya Uchumi wa taifa 2022/2023 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2023/2024 ikiwasilishwa Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.
Wadau wa masuala ya Kijinsia wakiwa katika Ukumbi wa TGNP Mabibo Jijini Dar es salaam wakisikiliza mubashara Hotuba ya Hali ya Uchumi wa taifa 2022/2023 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2023/2024 ikiwasilishwa Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.
Wadau wa masuala ya Kijinsia wakiwa katika Ukumbi wa TGNP Mabibo Jijini Dar es salaam wakisikiliza mubashara Hotuba ya Hali ya Uchumi wa taifa 2022/2023 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2023/2024 ikiwasilishwa Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

Wadau wa masuala ya Kijinsia wakiwa katika Ukumbi wa TGNP Mabibo Jijini Dar es salaam wakisikiliza mubashara Hotuba ya Hali ya Uchumi wa taifa 2022/2023 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2023/2024 ikiwasilishwa Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.



Share:

PICHA ZA MATUKIO NHIF ILIVYOSHIRIKI MAONYESHO YA BIASHARA NA UTALII YA 10 YA JIJINI TANGA


Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Macrina Clemence kulia akitoa elimu kwa mmoja wa wananchi waliofika kwenye Banda lao wakati wa maonyesho  ya 10 ya Biashara na Utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga 
Wananchi wakiwa kwenye Banda ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakipatiwa huduma mbalimbali wakati wa maonyesho hayo
Wananchi wakiendelea kupata huduma kwenye Banda ya NHIF
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JUNI 152023


































Share:

Wednesday, 14 June 2023

MAHAKAMA YAZUIA KIKUNDI CHA VIJANA VICTORY FARMERS KUSAFIRISHA MBOLEA YA SAMADI MANYONI

 



Na Mwandishi wetu

Mahakama ya wilaya ya Manyoni mkoani Singida imetoa amri ya zuio la muda kwa  kwa kikundi cha Vijana Victory Farmers kusafirisha Mbolea ya Samadi iliyokusanywa kutoka kwa wafugaji katika kijiji cha Ngaiti wilayani Manyoni.

Zuio hilo ni kutokana na kesi ndogo iliyofunguliwa kwa hati ya dharura na kampuni ya Maisha Transport limited baada ya kikundi hicho kukiuka mkataba baina yao


Kesi ya maombi madogo namba 3 ya mwaka 2023 ya kuzuia usafirishaji wa Mbolea hiyo baada ya ukiukwaji wa mkataba kwa kuuza mbolea hiyo kwa kampuni nyingine.

Kikundi hicho kiliingia mkataba wa mwaka 1  mwezi Januari 2023 na kampuni ya Maisha kwa kuuziana mbolea ya Samadi ambayo ilikusanywa kwenye kijiji cha Ngaiti wilayani Manyoni kutoka kwa wafugaji kwa makubaliana ya malipo ya shilingi  milioni 30 kwa trip 79 za Semi trela.

Hakimu mfawidhi wa Mahakama  ya wilaya ya Manyoni, Alisile Mwankejela amesema uamuzi huo umefuatia kufunguliwa kesi ya maombi madogo namba 3 ya 2023 kwa hati ya dharura juu ya usafirishwaji wa Mbolea hiyo.

 

Wakili wa upande wa madai John Chigongo amesema amepoka maamuzi hayo kwa moyo mkunjufu kwani yamewanusuru wateja wake kupata hasara wakati wakisubiri maamuzi ya kesi ya madai namba 2 ya mwaka 2023.

Kesi ya madai namba 2 ya mwaka 2023 inatarajia kusikilizwa tarehe 30.6.2023 katika Mahakam ya wilaya ya Manyoni mkoani Singida.
Share:

SERIKALI YASISITIZA KUFANYA KAZI KWA KARIBU NA VYAMA VYA WAFANYAKAZI




Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Mhe. Ummy Nderiananga, akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti maalum (Chadema), Mhe. Sophia Mwakagenda kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu leo Juni 14,2023 bungeni jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu, DODOMA

SERIKALI imesema itaendelea kufanya kazi kwa karibu na vyama vya wafanyakazi kwa kusuluhisha migogoro iliyopo kwenye baadhi ya vyama.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Mhe. Ummy Nderiananga ametoa kauli hiyo bungeni Juni 14, 2023 alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti maalum (Chadema), Mhe. Sophia Mwakagenda kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

Katika swali lake, Mbunge huyo amehoji serikali inatoa kauli gani kuhusu ulazima wa kujiunga na vyama na itoe tamko la kuruhusu mwalimu kujiunga kujiunga na chochote anachoridhika nacho.

Akijibu swali hilo, Ummy amesema zipo katiba zinazoongoza vyama vya wafanyakazi na serikali inafahamu kuna baadhi ya vyama vina migogoro na serikali itaendelea kufanya kazi kwa karibu na vyama hivyo kwa kuboresha mapungufu yaliyopo na kusuluhisha migogoro.

“Niwatoe hofu walimu waendelee kukiamini chama chao cha walimu na sisi serikali tupo pamoja nao,”amesema.
Share:

AGRI THAMANI YAENDESHA SEMINA KWA WAHARIRI KUHUSU MASUALA YA ULINZI WA TAARIFA ZETU ZA AFYA

Mwanzilishi na Mwenyekiti wa asasi isiyo ya kiserikali, Agri Thamani Foundation Mbunge Mhe.Neema Lugangila akizungumza na wahariri wa Vyombo vya Habari nchini wakati wa Semina ya Wahariri kuhusu kuzungumzia masuala ya ulinzi wa taarifa zetu za Afya. Je, namna gani taarifa za afya zinakusanywa, kuhifadhiwa, kutumiwa na kutupwa?. Semina iyo imefanyika leo Juni 14,2023 Jijini Dar es Salaam

Mwanzilishi na Mwenyekiti wa asasi isiyo ya kiserikali, Agri Thamani Foundation Mbunge Mhe.Neema Lugangila akizungumza na wahariri wa Vyombo vya Habari nchini wakati wa Semina ya Wahariri kuhusu kuzungumzia masuala ya ulinzi wa taarifa zetu za Afya. Je, namna gani taarifa za afya zinakusanywa, kuhifadhiwa, kutumiwa na kutupwa?. Semina iyo imefanyika leo Juni 14,2023 Jijini Dar es Salaam
Meneja wa Utetezi na Kampeni (Transform health) Bi.Beatrice Okech akizungumza katika Semina ya Wahariri kuhusu kuzungumzia masuala ya ulinzi wa taarifa zetu za Afya. Je, namna gani taarifa za afya zinakusanywa, kuhifadhiwa, kutumiwa na kutupwa?. Semina iyo imefanyika leo Juni 14,2023 Jijini Dar es Salaam
Meneja wa Taasisi ya Agri Thamani Bi.Mwasiti Kazinja akizungumza katika Semina ya Wahariri kuhusu kuzungumzia masuala ya ulinzi wa taarifa zetu za Afya. Je, namna gani taarifa za afya zinakusanywa, kuhifadhiwa, kutumiwa na kutupwa?. Semina iyo imefanyika leo Juni 14,2023 Jijini Dar es Salaam
Mwanzilishi na Mwenyekiti wa asasi isiyo ya kiserikali, Agri Thamani Foundation Mbunge Mhe.Neema Lugangila akiwa kwenye picha ya pamoja na wahariri wa Vyombo vya Habari nchini wakati wa Semina ya Wahariri kuhusu kuzungumzia masuala ya ulinzi wa taarifa zetu za Afya. Je, namna gani taarifa za afya zinakusanywa, kuhifadhiwa, kutumiwa na kutupwa?. Semina iyo imefanyika leo Juni 14,2023 Jijini Dar es Salaam
Mwanzilishi na Mwenyekiti wa asasi isiyo ya kiserikali, Agri Thamani Foundation Mbunge Mhe.Neema Lugangila akiwa kwenye picha ya pamoja na wahariri wa Vyombo vya Habari nchini wakati wa Semina ya Wahariri kuhusu kuzungumzia masuala ya ulinzi wa taarifa zetu za Afya. Je, namna gani taarifa za afya zinakusanywa, kuhifadhiwa, kutumiwa na kutupwa?. Semina iyo imefanyika leo Juni 14,2023 Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Wahariri wa Vyombo vya habari wakiwa katika semina kuzungumzia masuala ya ulinzi wa taarifa zetu za Afya. Je, namna gani taarifa za afya zinakusanywa, kuhifadhiwa, kutumiwa na kutupwa?. Semina iyo imefanyika leo Juni 14,2023 Jijini Dar es Salaam

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Share:

NDUGU ZANGU WARUDISHA MIRATHI NA KUOMBA MSAMAHA

Mafundisho ya wazazi juu ya upendo wa wengine yaliingia vizuri nikafanya upendo kuwa kitu kikubwa sana juu ya vyote nilivyo navyo. Alfajiri ya Jumamosi nikiwa safarini kuelekea kwa wazazi walezi walionisimamia ubatizo nikapokea ujumbe rudi nyumbani tunakuhitaji.

Haikuwa kitu cha kawaida kwani sikuzoea kuandikiwa ujumbe isipokuwa kupokea simu na mazungumzo ya moja kwa moja mara zote inapotokea shida yoyote ile.

Nilishtuka nikateremka kwenye gari nikatoa taarifa ya kuahirisha safari na taratibu za kurudishwa nauli zangu zilianza, nilipojaribu kupiga simu za wazazi zilipokelewa na vilio kisha zikakatwa bila ya upande wa pili kutoa majibu yoyote. Nilifanya ivyo zaidi ya mara tatu lakini ilikuwa ni hali upande wangu na vilio upande wapili. Nikagundua kuna shida na tayari akili yangu ikabadilika papohapo.


Mara baada ya kufika nyumbani zilikuwa ni taarifa za msiba mama na baba wamefariki wakiwa shambani kwa kuangukiwa na miti ya radi.Nililipokea likaniumiza lakini sikuwa na la kufanya tuliwazika tukalia msiba ukaisha.

Siku ya tatu baada ya msiba nilishangaa kuona kila aliyekuwa ndugu wa baba na mama wakigawana mali na mimi kama kaka mkubwa wa familia yetu waliniacha bila lolote na hawakutaka nishiriki chochote katika vikao vyao wakidai kuwa hizo zilikuwa mali zao walilzorithishwa na baba yao yaani babu yangu.


Kwa upendo nilio kuwa nao na jinsi nilivyo funzwa na wazazi wangu majirani walinionea huruma haikusaidia kwa kuwa tayari mali zote zilikwisha toweka nyumbani.Tuliishi katika hali ngumu sana tukifuatilia taratibu za mirathi mahakamani bila ya kupewa msaada wowote.

Miezi saba baada ya kusikilizwa kwa kesi yangu mahakamani mara mbili bila ya kushinda sasa mama yangu wa ubatizo alifunga safari akaja kunitembelea na kuniambia mwanangu nitakupa msaada ambao nitaomba uuamini na uufanye kwa makini.

Alinipa nambari za whatsapp +243 990 627 777 za daktar.Mazungumzo tukafanya kiundani nikamtafuta katika tovuti zake https://bakongwadoctors.com/.Akaniahidi ndani ya muda mchache kila jambo litakuwa sawa kama nitafuata maelekezo yake.

Alinitumia dawa na kisha nikazipokea katika dawa hizo kulikuwamo na kibandiko chenye maelekezo ya matumizi sahihi ya dawa ambayo daktari alisisitiza sana niyafuate kikamilifu.

Nikatumia dawa nikawa sawa ndani ya masaa machache wanafamilia walianza kunipigia simu wakitaka kurudisha mali kwani hazikuwa zikiwahusu walisema kuwa zilikuwa chini ya uangalizi wangu kwani zilikuwa ni halali kutoka kwa babu yangu hakika nasema asante sana kwa daktari BAKONGWA.
Share:

NEC YATANGAZA UCHAGUZI MDOGO KATIKA KATA 14


Mkurugugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Ramadhan Kailima, akizungumza jijini Dodoma leo Juni 14,2023 wakati akitangaza taarifa ya uchaguzi mdogo wa Udiwani katika Kata 14 za Tanzania bara.


*************

Na Mwandishi Maalum, Dodoma
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika Kata 14 za Tanzania Bara utakaofanyika tarehe 13 Julai mwaka 2023.

Akitangaza Uchaguzi huo mdogo jijini Dodoma leo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ramadhani Kailima amesema uchaguzi huo unafanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa.

Amefafanua kuwa Waziri ametoa taarifa hiyo kwa kuzingatia matakwa ya Kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292.

“Kutokana na taarifa hiyo, Tume kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, inatoa taarifa kwa Umma kuhusu uwepo wa uchaguzi mdogo wa adiwanikatika kata 14 za Tanzania Bara”alisema Kailima.

Kailima amezitaja kata hizo kuwa ni Kata ya Ngoywa iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Kata ya Kalola iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Uyui zote za Mkoani Tabora na Kata Sindeni Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Kata ya Potwe Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Kata ya Kwashemshi Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe na Kata ya Bosha Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga zote za Mkoa wa Tanga.

Kata zingine ni Kata ya Mahege katika Halmashauri ya Kibiti mkoa wa Pwani, Kata ya Bunamhala katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Kata ya Njoro na Kalemawe katika Halmashauri ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kata ya Mnavira katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mkoa wa Mtwara, Kataya Kinyika katika Halmashauri ya Wilaya ya mkoa wa Njombe.

Kailima ametaja Kata zingine zitakazo fanya uchaguzi ni Kata ya Magubike katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro na Kata ya Mbede katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe ya mkoa wa Katavi.

Amesema ratiba ya uchaguzi huo itaanza na utoaji wa fomu za uchaguzi kwa wagombea kuanzia tarehe 24 hadi 30 Juni , 2023 huku uteuzi wa wagombea watakao wania nafasi hizo ukifanyika Juni 30 mwaka huu.

Kailima amesema vyama vitakavyopata uteuzi vitaanza kampeni za Uchaguzi tarehe 01 hadi 12 Julai na siku ya kupiga kura itakuwa tarehe 13 Julai mwaka 2023.

“Tume inatumia nafasi hii kuvikumbusha vyama vya siasa, wagombea na wadau wote wa uchaguzi uzingatia Sheria, Kanuni, Maadili ya Uchaguzi, Taratibu, Miongozo na maelekezo katika kipindi cha uchaguzi huu mdogo” alisema Kailima.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger