Saturday, 17 December 2022

Picha : KAMPENI YA KUPINGA RUSHWA YA NGONO YAZINDULIWA SHINYANGA...MBIO ZA BAISKELI ZANOGESHA MIAMBA WAKICHUANA


Waendesha Baiskeli wanawake wanaokimbia na ndoo kichwani wakichuana wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waendesha baiskeli kundi A la wanaume wakichuana vikali wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amezindua Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono yenye kauli mbiu ‘ Kuwa Jasiri Kataa Rushwa ya Ngono’ inayoendeshwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Karibu Tanzania Organization (KTO) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Vyuo 54 vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs).

Uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono umefanyika leo Jumamosi Desemba 17,2022 katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga ukiambatana na utoaji wa elimu ya Rushwa ya Ngono kwa njia ya michezo ya Baiskeli ambapo wanamichezo wa mbio za baiskeli kupitia Chama Cha Mbio za Baiskeli Mkoa wa Shinyanga wameshindana na kuondoka na zawadi mbalimbali.

Miongoni mwa mbio za baiskeli zilizofanyika ni mbio za wanawake wanaokimbia na ndoo za maji kichwani wakizunguka uwanja wa CCM Kambarage, mbio za wanawake kuzunguka uwanja wa CCM Kambarage, mbio za wanaume waliogawanywa katika makundi matatu (A,B,C) kuzunguka uwanja huo na washindi kuanzia namba moja hadi 10 wameondoka na zawadi ya pesa taslimu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo, Kamanda Magomi amelipongeza Shirika la KTO kwa kuanzisha Kampeni ya Kupinga Rushwa ya ngono likishirikiana na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi nchini Tanzania (FDCs) na TAKUKURU akieleza kuwa Rushwa ya Ngono inapaswa kupingwa na kila mtu kwani inarudisha nyuma maendeleo ya nchi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi.

“Rushwa ya Ngono inaanzia nyumbani na kazini ambapo watu wenye mamlaka wanatumia mamlaka yao vibaya wakitaka wapewe rushwa ya ngono ambapo rushwa hii inamuumiza zaidi mwanamke. Huko mtandaoni pia wanawake wanaombwa rushwa ya ngono pale wanapotishiwa picha zao kusambazwa mtandaoni. Rushwa ya ngono inasababisha tupate wataalamu wasio na sifa lakini pia inaua kutokana na kuchangia maambukizi ya magonjwa ya zinaa ukiwemo UKIMWI na inamfanya muathirika wa rushwa ya ngono kuwa mtumwa wa ngono”,amesema Kamanda Magomi.


“Rushwa ya ngono ni unyanyasaji, kunyamazia kimya rushwa ya ngono ni kunyima haki. Kila mtu aguswe na athari za rushwa, kila mmoja apaze sauti. Naomba wananchi mtoea taarifa polisi na TAKUKURU kuhusu vitendo vya rushwa ya ngono na rushwa zingine. Tukipata taarifa hizo tutazishughulikia kwa weledi na usiri mkubwa”,ameongeza Kamanda Magomi.

Kwa upande wake, Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Bi. Mwamba Masanja amesema rushwa ya ngono siyo fursa ya kujinufaisha na kitu/jambo/ huduma hivyo ni lazima kila mmoja anatakiwa kuwa mstari wa mbele kupinga rushwa ya ngono na rushwa zingine kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Mkurugenzi wa Shirika la Karibu Tanzania Organization (KTO) Maggid Mjengwa amesema wanaendesha Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono kwenye vyuo 54 vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs) na wameamua kutumia mchezo wa mbio za baiskeli kutoa elimu kuhusu masuala ya rushwa ya ngono ili wawe mabalozi wa kupinga rushwa ya ngono.

“Tupo hapa kwa ajili ya kupinga rushwa ya ngono, KTO tunaamini kuwa silaha kubwa ya kupinga rushwa ya ngono ni kujenga uelewa kwa jamii juu ya rushwa ya ngono ndiyo maana hapa leo tunashuhudia mbio za baiskeli. Tunajenga uelewa kupitia michezo Waendesha baiskeli watakuwa mabalozi wa kueneza elimu ya madhara ya rushwa ya ngono. Naomba kila mmoja apinge rushwa ya ngono kwani jambo hili linamhusu kila mwananchi”,amesema Mjengwa.
Waendesha Baiskeli wakitimua vumbi wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, John Tesha amesema Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inagusa jamii hivyo kuwaomba wananchi kutoa taarifa za vitendo vya rushwa katika jamii.


Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi, Bi. Maria Mkanwa amesema chuo hicho pamoja na vyuo vingine vya maendeleo ya wananchi kwa kushirikiana na KTO wanaendelea kutoa elimu ya kupinga rushwa ya ngono pamoja na kutoa Proramu mbalimbali kwa ajili ya kumwendeleza mwanamke kijana.


Mwakilishi wa Bodi ya KTO, Khalfani Mshana amesema vyuo 54 vya Maendeleo ya Wananchi vimeendelea kushirikiana na KTO na TAKUKURU kutoa elimu ya kupinga rushwa ya ngono kwa kuendesha Programu mbalimbali ikiwemo Programu ya Elimu Haina Mwisho ambayo ni Programu maalumu ya kuendeleza maarifa kwa wanawake vijana waliokatishwa masomo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ujauzito pamoja na wale ambao hawakupata nafasi ya kuendelea na masomo ya sekondari, watasoma masomo ya sekondari kupitia mfumo usio rasmi, masomo ya ufundi, ujasiriamali na stadi za maisha bure.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati akizindua Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono yenye kauli mbiu ‘ Kuwa Jasiri Kataa Rushwa ya Ngono’ inayoendeshwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Karibu Tanzania Organization (KTO) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Vyuo 54 vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs) leo Jumamosi Desemba 17,2022 katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati akizindua Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati akizindua Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati akizindua Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Mwakilishi wa Bodi ya KTO, Khalfani Mshana akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Mwakilishi wa Bodi ya KTO, Khalfani Mshana akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Mkurugenzi wa Shirika la Karibu Tanzania Organization (KTO) Maggid Mjengwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Mkurugenzi wa Shirika la Karibu Tanzania Organization (KTO) Maggid Mjengwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Mkurugenzi wa Shirika la Karibu Tanzania Organization (KTO) Maggid Mjengwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, John Tesha akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, John Tesha akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Bi. Mwamba Masanja  akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Bi. Mwamba Masanja  akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi, Bi. Maria Mkanwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Mtoa huduma za kisheria ngazi ya jamii, Anne Deus kutoka kituo cha Msaada wa Kisheria Community Edivication Organization (CEO) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Waendesha Baiskeli kundi C wakishindana mbio wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Waendesha Baiskeli kundi C wakishindana mbio wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Waendesha Baiskeli wanawake wanaokimbia na ndoo kichwani wakijiandaa kuanza mbio wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Waendesha Baiskeli wanawake wanaokimbia na ndoo kichwani wakichuana wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Waendesha Baiskeli wanawake wanaokimbia na ndoo kichwani wakichuana wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Mwendesha Baiskeli maarufu Makirikiri akishangilia baada ya kushika nafasi ya kwanza kundi la wanawake wanaokimbia na ndoo kichwani wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Waendesha Baiskeli kundi B wakitimua vumbi wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.

Mwendesha Baiskeli Paul Maiga akishangilia baada ya kushika nafasi ya kwanza kundi B la Wanaume wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.

Wanafunzi wa Chuo cha Buhangija FDC wakitoa burudani ya Igizo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Wanawake waendesha baiskeli bila ndoo kichwani wakitimua vumbi wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.

Mwendesha Baiskeli maarufu Futi Mbili akishangilia baada ya kushika nafasi ya kwanza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Vijana wa kundi la Kambi ya Nyani wakitoa burudani wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Waendesha baiskeli kundi A la wanaume wakichuana vikali wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Waendesha baiskeli kundi A la wanaume wakichuana vikali wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Waendesha baiskeli kundi A la wanaume wakichuana vikali wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs.
Waendesha baiskeli kundi A la wanaume wakihitimisha mbio baada ya kuzunguka uwanja wa CCM Kambarage mara 35 wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Rushwa ya Ngono inayoendeshwa na Shirika la KTO kwa kushirikiana na TAKUKURU na FDCs. Kulia ni Mshindi wa kwanza George Izengo
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akikabidhi zawadi ya shilingi 50,000/=  Mwendesha Baiskeli Makirikiri baada ya kuibuka mshindi wa kwanza mbio za baiskeli huku umebeba ndoo ya maji kichwani kuzunguka uwanja wa CCM Kambarage mara 15
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akikabidhi zawadi ya shilingi 50,000/=  Mwendesha Baiskeli Futi Mbili baada ya kuibuka mshindi wa kwanza mbio za wanawake kuzunguka uwanja wa CCM Kambarage mara 15
Zawadi zikiendelea kutolewa kwa washindi
Zawadi zikiendelea kutolewa kwa washindi
Zawadi zikiendelea kutolewa kwa washindi
Zawadi zikiendelea kutolewa
Zawadi zikiendelea kutolewa 
Zawadi zikiendelea kutolewa
Wadau wakifuatilia burudani uwanjani
Wadau wakifuatilia burudani uwanjani
Wadau wakifuatilia burudani uwanjani
Wadau wakifuatilia burudani uwanjani
Wadau wakifuatilia burudani uwanjani
Wadau wakifuatilia burudani uwanjani
Wadau wakifuatilia burudani uwanjani
Wadau wakifuatilia burudani uwanjani.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:

KAMATI YA MAWAZIRI 8 WA KISEKTA YAWASILI MKOANI KAGERA


Kamati ya Mawaziri Nane wa Kisekta imewasili rasmi mkoani Kagera kwa ajili ya kuongea na wakazi wa vijiji vinne vya kata ya Rutoro kuhusu uamuzi wa Baraza la Mawaziri juu ya vijiji hivyo ambavyo vimo ndani ya eneo la Ranchi ya Kagoma wilayani Muleba mkoa wa Kagera.

Kamati hiyo inaongozwa na mwenyekiti wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba ndaki na Makamu wake Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete.

Wengine ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. David Silinde, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde, Naibu Waziri wa Maji Mhe. Eng. Maryprisca Mahundi, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Khamis Chilo.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI DESEMBA 17,2022









Share:

Friday, 16 December 2022

WALIMU NCHINI WATAKIWA KUPUNGUZA MATUMIZI YA VIBOKO NA VITISHO KWA WANAFUNZI


Rai imetolewa kwa walimu wote wa shule za msingi na sekondari na vyuo nchini kupunguza matumizi ya viboko na vitisho kwa wanafunzi kama njia ya kufanya wafaulu katika masomo yao kwa kuwa huo si mtazamo sahihi.

Rai hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Elimu, Dkt. Lyabwene Mtahabwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa siku mbili wa wadau wa Mradi wa Kuendeleza Elimu ya Ualimu (TESP) ambapo alimwakilisha Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Francis Michael

Ameongeza kuwa walimu wanatakiwa wafahamu kuwa watoto wote hawana uwezo unaofanana hivyo wanatakiwa kuwachukulia watafute mbinu mbalimbali za kumsaidia kila mmoja.

"Maendeleo ya kweli katika nchi huletwa na elimu bora, elimu bora huletwa na walimu bora na walimu bora sifa yao kuu ni upendo kwa wanafunzi na wadau wengine wa elimu. Mwalimu ni kioo cha jamii, amejaa hekima na busara na ni kimbilio la watu wote," amesema Dkt. Mtahabwa.

Amesema lengo la mkutano huo ni kutafakari namna ambavyo mradi umekuwa ukitekelezwa na kujadili jinsi ya kuimarisha na kuendeleza mambo yaliyotekelezwa kwa mafanikio baada ya mradi kuisha.

"Kwa hiyo siku hizi mbili tutaangalia nini kimefanyika kupitia Mradi huu wa TESP na kisha kuweka mikakati ya namna ya kuendeleza mradi huu," ameongeza Dkt. Lyabwene.

Mratibu wa Mradi wa TESP, Cosmas Mahenge amesema mradi huo unaofadhiliwa na Serikali ya Canada umejikita katika kuimarisha elimu ya ualimu, hasa katika ngazi ya Astashahada na Stashahada za Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali na kwamba una jumla ya zaidi ya Shilingi bilioni 90.

Ametaja kazi kubwa zilizofanywa na mradi huo kuwa ni kutoa mafunzo kwa Wakufunzi zaidi ya 1,300, kununua vifaa vya TEHAMA kwa vyuo vyote 35 vya umma na kuviunganisha katika mkongo wa taifa wa mtandao.

Nyingine ni ujenzi wa Chuo cha mfano cha Ualimu Kabanga, ujenzi na ukarabati katika vyuo saba, kukarabati na kujenga maktaba za kisasa, maabara za Tehama na za sayansi, kuimarisha uongozi kwa kuwapa mafunzo ya uongozi kwa viongozi na maafisa Wizara ya Elimu Makao Makuu lengo likiwa kuimarisha mfumo wa kusimamia elimu ya ualimu.

Naye Mwenyekiti wa Wakuu wa vyuo vya Serikali, Tanzania Bara Agustine Sahili amesema wamenufaika na mradi huo kwa kupata mafunzo kwa wakufunzi wa vyuo vyote.

Ameongeza kuwa manufaa mengine waliyopata ni vyuo kujengewa na kukarabatiwa miundombinu ikiwemo maktaba mpya na maabara za Tehama na za sayansi.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Canada, Rasmatta Barry ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa utekelezaji wa mradi huo ambao amesema umezingatia masuala ya mazingira na jinsia kwa kiasi kikubwa.
Share:

TBS YAKABIDHI LESENI NA VYETI 59 KWA WAZALISHAJI WA BIDHAA MKOANI MBEYA


SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limekabidhi Leseni na Vyeti vya ubora hamsini na tisa (59) na kati ya hivyo, leseni na vyeti 39 (66.1%) vimetolewa kwa wajasiriamali wadogo ambapo leseni na vyeti hivyo vimetolewa kwa wazalishajiwa bidhaa ambazo zimekidhi viwango.

Vyeti na leseni hizo ni kwa ajili ya bidhaa za vyakula, vipodozi, vifaa vya ujenzi, chaki, gesi, makaa ya mawe na vifungashio.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo iliyofanyika leo Desemba 16,2022 mkoani Mbeya, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bi. Mwajuma Nyamkomola amesema

Aidha amesema serikali imekuwa ikiwahudumia wajasiriamali wadogo katika kupata huduma za TBS bila malipo na gharama za ukaguzi na upimaji kwa kipindi cha miaka mitatu (3) ya mwanzo.

"Naipongeza Serikali kwa kuendelea kutambua uhitaji wa kuendelea kuwalipia wajasiriamali wadogo hata baada ya kipindi cha miaka mitatu kwisha kutokana na hali ngumu ya biashara inayosababisha kutofikia uwezo wa kuanza kujilipia. Hatua hii inasaidia katika kuinua na kukuza viwanda hapa nchini". Amesema

Amesema serikali za Mkoa na Halmashauri wanaendelea kushirikiana na taasisi wezeshi ikiwemo TBS kuhakikisha wanakua kuanzia kuwa na bidhaa zenye viwango ili kupata soko kiurahisi na kumudu ushindani.

Ameipongeza TBS kwa kufanya hafla hizo katika Kanda zake kwa kuanzia katika mkoa wangu wa Mbeya. Kwa niaba ya mikoa ya wenzangu, naamini fursa hii ya kufanyika hafla katika mikoa italeta hamasa na chachu ya wazalishaji Zaidi ya waliohudhuria hapa, kuzalisha bidhaa zenye ubora na bila shaka wataongezeka katika kuomba kuthibitisha bidhaa zao kwa TBS.

Pamoja na hayo ametoa wito kwa wazalishaji wote ambao hawajapata leseni na vyeti vya ubora walioko katika mikoa ya Kanda za Nyanza za Juu Kusini na Magharibi mwa Tanzania ambako ofisi za TBS zipo, waendelee kufuata taratibu za shirika ili nao waweze kupata alama za ubora kwa ajili ya usalama wa mlaji na kuyafikia masoko ya ndani na nje ya nchi.

Hata hivyo amewahasa waliopata leseni na vyeti vya ubora kuwa muwe mabalozi wazuri katika matumizi ya Viwango ili kufikia lengo la Tanzania ya viwanda na muendelee kuzalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya Viwango kwa mustakabali wa afya za watumiaji na kukuza soko la ndani na nje ya nchi.

Share:

WANASHERIA, WAENDESHA MASHTAKA NA WAPELELEZI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII WAPATIWA MAFUNZO JIJINI MWANZA


Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Lucy E Saleko akizungumza kabla ya kuanza kwa Mafunzo kwa Wanasheria,Waendesha mashtaka na wapelelezi walioko chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii Jijini Mwanza.
Baadhi ya Wanasheria,Waendesha mashtaka na wapelelezi walioko chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Mahakimu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Maliasili na Utali, Lucy E, Salekoi kwenye Mafunzo ya Wataalamu hao yanayofanyika Jijini Mwanza.


Na John Bera - Mwanza

Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Kitengo cha Huduma za Sheria imeendesha mafunzo kwa Wanasheria,Waendesha mashtaka na wapelelezi walioko chini ya Wizara hiyo ili kuwajengea uwezo kuhusu Sheria za kisekta na Sheria Mtambuka kwa lengo la kupunguza matukio ya ujangili wa mazao ya misitu na wanyamapori kwenye maeneo yaliyohifadhiwa.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo leo jijini Mwanza, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi. Lucy Saleko  amesema kuwa mafunzo hayo yameandaliwa na Kitengo cha Sheria chini ya udhamini wa Mradi wa Kuzuia na Kupambana na ujangili wa wanyamapori na Biashara haramu ya nyara na mazao ya misitu (CPIWT Project), UNDP na Global Environmental Facility (GEF) chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia.


“Sisi kama kitengo cha Sheria ambao ndio waratibu wakuu wa mafunzo haya tumekuwa tukipata changamoto hususan kwenye makosa ya ujangili na mifugo kukamatwa kutokana na watu kuingiza hifadhini, mafunzo haya ni muhimu pale mashauri yanapopelekwa mahakamani kuhakikisha ushahidi unatolewa wa mtu aliyeingiza mifugo hifadhini haukwami", amesisitiza Lucy Saleko.


Amesema kutokana mafunzo hayo,Wanasheria,Waendesha mashtaka na wapelelezi walioko chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii wataongeza ujuzi katika kudhibitisha vielelezo vya ushahidi na kukusanya taarifa za ushahidi wawapo mahakamani.
Share:

MAMA AUA WANAE WAWILI, AJINYONGA


Miili ya mama na wanaye

Amina Maketu mwenye umri wa miaka 34 amewaua watato wake wawili wenye umri wa miaka 9 na mwingine ana umri wa mwaka 1 na miezi 8 na kisha yeye mwenyewe kujinyonga huku chanzo cha tukio hilo ikiwa ni ugomvi wa ardhi uliotokea kwenye familia yake.

Akielezea tukuio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Michael Chilya, amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Desemba 15,2022, katika mtaa wa Namanditi A, Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, huku sababu ya kutokea tukio hilo ikiwa ni ugomvi wa ardhi alikuwa anagombea yeye na ndugu zake ambapo marehemu ameacha ujumbe unaoeleza kuwa ameamua kujiua yeye na kuua watoto wake ili watoto wake wasipate tabu.

Akieleza kwa masikitiko makubwa Peter Komba ambaye ni mume wa marehemu amesema anasikitishwa na kitendo cha mke wake huyo kuwaua watoto wake kwani hakuwa na ugomvi naye licha ya kutengana naye.

Chanzo - EATV
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger