Monday, 10 October 2022

RAIS RUTO ATUA TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akishuka kutoka katika ndege alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini.

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akishuka kutoka katika ndege akipokea shada la Maua kutoka kwa Mtoto Tracy-Chantelle Mmbando alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto na Mke wake Mama Rachel Ruto wakizungumza na watoto Joseph Mmbando na Tracy-Chantelle Mmbando baada ya kupokea maua walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchin
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akisalimiana na mmoja wa maafisa waliofika ukatika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kumpokea alipowasili nchini kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu.
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax wakielekea katika chumba cha mapumziko katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili nchini kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto (kulia) Mama Rachel Ruto (wa pili kushoto) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Alfred Mutua (wa kwanza kushoto) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchin.


**********************************


Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya Siku mbili. Mhe. Dkt. Ruto ambaye ameambatana na mke wake Mama Rachel Ruto, amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wa jijini Dar es Salaam.


Baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wa Dar es Salaam Mhe. Dkt. Ruto alikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake na kuelekea hotelini kwa mapumziko.

Tarehe 10 Oktoba 2022 asubuhi, Mhe. Dkt. Ruto atawasili katika Ikulu ya Dar es salam ambapo atpokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo pamoja na mambo mengine viongozi hao watakuwa na mazungumzo rasmi ambayo yatakayohusisha wajumbe wa pande zote mbili.

Baada ya kukamilika kwa mazungumzo hayo rasmi viongozi hao watazungumza na waandishi wa habari kuhusiana na walichojadili katika ziara hiyo na baadaye watahudhuria dhifa ya kitaifa ambayo Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuandalia mgeni wake Mhe. Dkt. Ruto.


baada ya kumalizika kwa Dhifa hiyo ya Kitaifa, Mhe. Dkt. Ruto na ujumbe wake wanatarajiwa kuondoka kurejea nchini Keny

a.
Share:

Sunday, 9 October 2022

SIMBA SC YAENDELEA KUFANYA VIZURI KIMATAIFA, YAICHAPA 3-1 PRIMEIRO DE AGOSTO


NA EMMANUEL MBATILO

KLABU ya Simba imefanikiwa kuinyuka timu ya Primeiro de Agosto Fc kwa mabao 3-1 mchezo ambao ulipigwa kwenye nchini Angola hivyo nakuwa na faida kwa Simba ambaye atasubiri kucheza mchezo wa marudiano ili aweze kufuzu hatua ya makundi.

Simba Sc iimepata mabao kupitia kwa wachezaji wake Clautos Chama, Israel Mwenda pamoja na mshambuliaji wao hatari Moses Phiri.

Simba Sc ilianza kupata bao la kwanza dakika za mwanzo kipindi cha kwanza kupitia kwa kiungo wao Chama na kuwapeleka mapumziko wakiwa mbele kwa bao 1-0.

Bao la timu ya Primeiro de Agosto Fc lilifungwa dakika za lala salama kupitia kwa mkwaju wa penati.
Share:

BARRICK BULYANHULU YAKABIDHI MASHINE ZA BIOHAZARD SAFETY CABINET HOSPITALI YA WILAYA YA KAHAMA NA KITUO CHA AFYA BUGARAMA


Mkuu wa wilaya ya Kahama,Festo Kiswaga (kulia) akikata utepe wakati wa hafla ya mgodi wa Barrick Bulyanhulu kukabidhi Mashine 2 za Biohazard safety cabinet katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga na kituo cha afya cha Bugarama iliyofanyika mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Josephat John, wengine ni Maofisa wa Serikali wilayani humo.
Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Josephat John. (kushoto) akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Mashine (Biohazard safety cabinet) mbili zenye thamani ya shilingi milioni 30 kwa hospitali ya Manispaa ya kahama na kituo cha afya cha Bugarama mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Bw. Festo Kiswaga. Wengine ni Maofisa wa Serikali wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya Kahama,Festo Kiswaga (aliyesimama) akiongea na wageni waalikwa katika hafla ya kupokea msaada wa mashine mbili za Biohazard safety cabinet zilizotolewa na Barrick kwa ajili ya hospitali mbili mkoani Shinyanga iliyofanyika mwishoni mwa wiki,wengine pichani ni maofisa waandamizi wa Barrick na Serikali mkoani humo.
Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu,Josephat John (aliyesimama) akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Mashine (Biohazard safety cabinet) mbili zenye thamani ya shilingi milioni 30 kwa hospitali ya Manispaa ya Kahama na kituo cha afya cha Bugarama mwishoni mwa wiki. (Wa tatu kutoka kulia) ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Bw. Festo Kiswaga. Wengine ni Maofisa wa Barrick na Serikali wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga, akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu, waliohudhuria katika hafla hiyo.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Barrick, wakijiandaa kumpokea Mkuu wa Wilaya ya Kahama wakati wa hafla hiyo.
Mwonekano wa mashine ya Biohazard safety cabinet
Mkuu wa wilaya ya Kahama,Festo Kiswaga (Kulia) akisalimiana na Diwani wa kata ya Bugarama Prisca Msoma ambaye alimwakilisha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala katika hafla hiyo.

***


Mgodi ya Barrick Bulyanhulu, umetoa msaada wa mashine mbili za kuzuia kusambaa bacteria hatarishi kwenye maabara (Biohazard safety cabinet), kwa hospitali ya manispaa ya Kahama na kituo cha afya cha Bugarama kilichopo wilayani Msalala mkoani Shinyanga, vyenye thamani ya shilingi ya milioni 30 ukiwa ni mwendelezo wake wa kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha huduma za afya katika jamii.

Katika hafla ya kukabidhi msaada huo mwishoni mwa wiki iliyofanyika katika Hospitali ya wilaya ya Kahama, Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi Bulyanhulu, Josephat John, alikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mheshimiwa Festo Kiswaga, vifaa hivyo vya kusaidia katika maabara.

Akiongea katika hafla hiyo Kaimu Meneja Mkuu wa Barrick Bulyanhulu Josephat John, alisema "Tunajivunia kutoa vifaa hivi maalum ili kuimarisha miundombinu ya matibabu katika jamii zinazozunguka migodi ya kampuni na huu ni mwendelezo wa jitihada za kampuni kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha huduma katika sekta ya afya nchini.”

Akipokea Mashine hizo, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Bw. Festo Kiswaga ameishukuru Kampuni ya Barrick Kwaa kushirikiana na Serikali katika jitihada zake za kuboresha afya kwa jamii.

“Barrick hamjawa nyuma, mmekuwa mstari wa mbele kila wakati, serikali inapokuwa na jambo, mmekuwa mkifungua mikono yenu. Asanteni sana kwa kuiunga mkono serikali kwa jambo hili jema la kuleta vifaa hivi vya kisasa ambavyo vitasaidia kuboresha huduma za maabara katika hospitali zetu”, alisema Kiswaga.

Kiswaga ametoa wito kwa wananchi kutunza afya zao pia ameutaka uongozi wa Hospitali ya Manispaa ya Kahama na Kituo cha Afya cha Bugarama kuhakikisha wanasimamia vyema matumizi na utunzaji wa vifaa hivyo.

Naye Diwani wa Kata ya Bugarama, Prisca Msoma, ambaye alimwakilisha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala, aliipongeza kampuni ya Barrick kwa jitihada ambazo Imekuwa ikifanya kuunga mkono jitihada za Serikali za kukabiliana na changamoto mbalimbali kwenye jamii ikiwemo kuboresha sekta ya afya.
Share:

WAFUGAJI WALIOHAMIA MSOMERA WAUNGA MKONO JUHUDI ZA UHIFADHI




Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi

Wafugaji wa Jamii ya kimasaii waliohamia katika kijiji cha Msomera Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga wamesema wameamua kwa hiari yao wenyewe kuhamia Msomera kuunga Juhudi za uhifadhi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Wafugaji hao ambao wamehamia eneo hilo wakitoka katika mamlaka ya hifadhi Ngorongoro wamesema watalitumia eneo hilo kwa kwa shughuli za ufugaji na kilimo tofauti na mwanzo walipokuwa katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ambapo fulsa hiyo hawakuipata.

Hayo wamesema leo Oktoba 09 katika kijiji cha Msomera  baadhi ya wafugaji Wa Jamii ya kimasaii mara baada ya kuwasili kwa kundi la kumi na mbili katika Kijiji cha Msomera Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga, wafugaji hao wamesema wanamuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Jitihada zake za kukuza ufadhi na utalii alizoanza kujionyesha katika Nchi yetu.

Share:

WAFUGAJI WANAOMILIKI SILAHA HARAMU WATAKIWA KUZISALIMISHA POLISI


Na Mwandishi wetu Jeshi la Polisi

Kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa Mifugo nchini ACP SIMON PASUA amewataka wafugaji wanaomiliki silaha kinyume na utaratibu kuzisalimisha Jeshi la Polisi na maeneo yaliyoainishwa ili wawekewe utaratibu mzuri wa kuzimiliki kihalali ambapo amesema kuwa muda wa msamaha wa Afrika umebaki mchache hivyo amewataka wajitokeze kusalimisha silaha ambazo wanamiliki kinyume na utaratibu.


Kamanda wa Polisi Kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo nchini kamishina msaidizi wa Polisi ACP SIMON PASUA amesema zaidi ya mifugo elfu kumi mia saba thelathini na nane imewasili katika kijiji hicho ikiwa ni awamu ya kumi na mbili.


ACP PASUA amesema Jeshi hilo linaendelea kuwahakikishia wananchi wanaohamia katika Kijiji cha Msomera kuwa Mifugo yao iko salama ambapo amewataka kufuata matumizi bora ya ardhi ili kuepusha Migogoro ya wakulima na wafugaji.


Kamanda Pasua amebainisha kuwa zoezi la kuhamisha mifugo katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro linaendelea kwa kushirikiana na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.
Share:

MATUKIO MBALIMBALI YA PICHA: KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA POSTA DUNIANI


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) akitembelea mabanda mbalimbali ya maonesho wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani tarehe 9 Oktoba 2022, katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Matukio mbalimbali wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani tarehe 9 Oktoba, 2022, katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC).

Mgeni Rasmi ni Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Moses Nnauye (mb)

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akiwa na Viongzi mbalimbali katika maadhimisho ya siku ya Posta duniani katika ukumbi wa Julius Nyerere Internationa Convention Centre, jijini Dar es Salaam Oktoba 09, 2022.Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Posta duniani katika ukumbi wa Julius Nyerere Internationa Convention Centre, jijini Dar es Salaam Oktoba 09, 2022. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Kate Kamba akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Posta duniani katika ukumbi wa Julius Nyerere Internationa Convention Centre, jijini Dar es Salaam Oktoba 09, 2022. Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Macrise Mbodo akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Posta duniani katika ukumbi wa Julius Nyerere Internationa Convention Centre, jijini Dar es Salaam Oktoba 09, 2022.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Selemani Kakoso, akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Posta duniani katika ukumbi wa Julius Nyerere Internationa Convention Centre, jijini Dar es Salaam Oktoba 09, 2022.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO, WHMTH)
Share:

WAZIRI MKENDA AKERWA KUSUASUA UJENZI VETA-SIMIYU

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia  Prof Adolf Mkenda akizungumza na watendaji chuo Cha Veta Simiyu.


Na Mwandishi wetu, Simiyu.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda (Mb) amekerwa na kusuasua kwa ujenzi wa chuo cha ufundi stadi-VETA mkoani Simiyu.


Ameagiza wataalamu wote wa usimamizi wa chuo hicho ambao ni kutoka chuo cha ufundi Arusha waweke kambi mkoani Simiyu ili kukagua na kukamilisha haraka ujenzi huo.


Waziri Mkenda ameametoa maagizo hayo mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Simiyu leo tarehe 8 Octoba 2022.


“Tungependa kuona chuo cha ufundi Arusha kikisimamia kazi hadi watu binafsi wawatafute kwa ajili ya kwenda kusimamia ujenzi, lakini hapa sidhani kama wamefikia kiwango kizuri, wamejitahidi lakini hawajafikia kwahiyo siridhiki” Amekaririwa Waziri Mkenda


Chuo cha Ufundi stadi VETA-Simiyu ni miongoni wa vyuo vinne ambavyo vimesalia kukamilika ujenzi wake ili mikoa yote iwe na vyuo vya Ufundi VETA, Waziri Mkenda ameitaja mikoa hiyo kuwa ni Simiyu, Rukwa, Njombe, na mkoa wa Songwe ambao fedha tayari zimepatikana kwa ajili ya kuanza ujenzi.


Prof Mkenda amesisitiza umuhimu wa kuzingatia ubora katika ujenzi wa Vyuo hivyo na kuhakikisha kuwa miradi yote inakamilika kwa wakati kama ilivyokusudiwa na serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan.


Pia, Waziri Mkenda amesema kuwa changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na usafiri, serikali itaendelea kuzitatua.


Kadhalika, Waziri Mkenda amesema kuwa kwa sasa Wizara imejipanga kuanza ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi katika wilaya zote nchini hivyo kama ujenzi wa usimamizi wa vyuo vya mikoa unasuasua ni wazi kuwa kusimamia Wilaya zote nchini haitakuwa kazi rahisi.




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger