Friday, 7 October 2022

DC SHEKIMWERI AIPONGEZA TANESCO DODOMA KWA KUTOA HUDUMA KWA WATEJA


MKUU wa Wilaya ya Dodoma,Jabir Shekimweri,akizungumza wakati wa kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kwa Shirika la TANESCO Mkoa wa Dodoma hafla iliyoendana sambamba na ukataji wa keki pamoja na uchangiaji damu iliyofanyika leo Oktoba 7,2022 jijini Dodoma.


MKUU wa Wilaya ya Dodoma,Jabir Shekimweri,akisisitiza jambo wakati wa kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kwa Shirika la TANESCO Mkoa wa Dodoma hafla iliyoendana sambamba na ukataji wa keki pamoja na uchangiaji damu iliyofanyika leo Oktoba 7,2022 jijini Dodoma.


Meneja wa TANESCO mkoa wa Dodoma, Mhandisi Donasiano Shamba,akitoa taarifa ya shirika hilo mkoa wa Dodoma wakati wa kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kwa Shirika la TANESCO Mkoa wa Dodoma hafla iliyoendana sambamba na ukataji wa keki pamoja na uchangiaji damu iliyofanyika leo Oktoba 7,2022 jijini Dodoma.


MENEJA Masoko wa TANESCO Bw.Kassim Chowo,akizungumza wakati wa kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kwa Shirika la TANESCO Mkoa wa Dodoma hafla iliyoendana sambamba na ukataji wa keki pamoja na uchangiaji damu iliyofanyika leo Oktoba 7,2022 jijini Dodoma.


Mhandisi wa miradi na mitambo, kutoka kampuni ya Kilimo Pyxus, Muhoja Manane,akizungumza wakati wa kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kwa Shirika la TANESCO Mkoa wa Dodoma hafla iliyoendana sambamba na ukataji wa keki pamoja na uchangiaji damu iliyofanyika leo Oktoba 7,2022 jijini Dodoma.


Mwenyekiti wa wafanyakazi wa Shirika hilo kupitia Chama cha Wafanyakazi (TUICO), Ramadhan Butallah,akizungumza wakati wa kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kwa Shirika la TANESCO Mkoa wa Dodoma hafla iliyoendana sambamba na ukataji wa keki pamoja na uchangiaji damu iliyofanyika leo Oktoba 7,2022 jijini Dodoma.


BAADHI ya watumishi wa TANESCO wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,Jabir Shekimweri (hayupo pichani) wakati wa kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kwa Shirika la TANESCO Mkoa wa Dodoma hafla iliyoendana sambamba na ukataji wa keki pamoja na uchangiaji damu iliyofanyika leo Oktoba 7,2022 jijini Dodoma.


MKUU wa Wilaya ya Dodoma,Jabir Shekimweri,akipata maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano Tanesco Mkoa Dodoma Sarah Libogoma,wakati wa kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kwa Shirika la TANESCO Mkoa wa Dodoma hafla iliyoendana sambamba na ukataji wa keki pamoja na uchangiaji damu iliyofanyika leo Oktoba 7,2022 jijini Dodoma.


MKUU wa Wilaya ya Dodoma,Jabir Shekimweri,akikata keki wakati wa kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kwa Shirika la TANESCO Mkoa wa Dodoma hafla iliyoendana sambamba na uchangiaji damu iliyofanyika leo Oktoba 7,2022 jijini Dodoma.


MKUU wa Wilaya ya Dodoma,Jabir Shekimweri,akiwalisha keki wafanyakazi wa TANESCO,Wateja waliohudhuria kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kwa Shirika la TANESCO Mkoa wa Dodoma hafla iliyoendana sambamba na ukataji wa keki pamoja na uchangiaji damu iliyofanyika leo Oktoba 7,2022 jijini Dodoma.


MKUU wa Wilaya ya Dodoma,Jabir Shekimweri,akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TANESCO mara baada ya kuzungumza kwenye kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kwa Shirika la TANESCO Mkoa wa Dodoma hafla iliyoendana sambamba na ukataji wa keki pamoja na uchangiaji damu iliyofanyika leo Oktoba 7,2022 jijini Dodoma.


WAFANYAKAZI wa TANESCO wakichangia damu wakati wa kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kwa Shirika la TANESCO Mkoa wa Dodoma hafla iliyoendana sambamba na ukataji wa keki pamoja na uchangiaji damu iliyofanyika leo Oktoba 7,2022 jijini Dodoma.

.................................

Na.Alex Sonna-DODOMA

MKUU wa Wilaya ya Dodoma,Jabir Shekimweri amelipongeza shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Dodoma kwa kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi pamoja na kuendelea kuboresha huduma kwa wateja.

Hayo ameyasema leo Oktoba 7, 2022 jijini Dodoma wakati wa kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kwa Shirika hilo, ambapo amesema kuwa TANESCO wamekuwa ni kiungo muhimu katika kutoa huduma bora kwa wananchi.

“Niwapongeze kwa kuhitimisha wiki ya huduma kwa mteja, utoaji wa huduma ukiimarishwa hasa kwenye shirika hili muhimu, kutaleta tija kwa jamii, nawapongeza kwa kupiga hatua sana kwenye utendaji kazi wenu,”amesema Shekimweri

Aidha Shekimweri amesema kuwa kutokana na shirika hilo kupitia katika mifumo mipya ya kidijitali wanapaswa kwenda na kasi na viwango katika kutoa huduma iliyobora kwa wateja wao.

''Mnatakiwa kwenda sambamba na kasi ya ubunifu ili kuweza kutimiza malengo ya Serikali kwa wananchi na wadau wengine ambao ndio wateja wanaofikiwa na huduma hiyo.''amesema

Amewataka watumishi wa shirika hilo kufanya kazi kwa ari, ushirikiano, ubunifu na kujituma kwa hali ya juu ili kuweza kutimiza malengo ya Serikali kwa wateja.

Aidha Shekimweri ameshiriki zoezi la kukata keki na watumishi wa TANESCO na wateja waliohudhuria hafla hiyo.

Kwa upande wake Meneja wa TANESCO mkoa wa Dodoma, Mhandisi Donasiano Shamba, ametaja maboresho mbalimbali yaliyofanyika ndani ya miezi tisa iliyopita yanayolenga kutoa huduma bora kwa wateja wake.

Mhandisi Shamba amesema shirika hilo limekuwa likitekeleza mpango mkakati wa miezi 18 wenye vipaumbele saba ili kutoa huduma bora kwa wananchi.

Amesema kupitia mfumo wa kidigitali wa kuomba kuunganishiwa umeme bila kumlazimu mteja kwenda ofisini (Nikonekt), shirika hilo limepokea maombi ya wateja zaidi ya 19,000 na tayari wananchi zaidi ya 10,000. wameunganishiwa umeme.

“Maboresho yamefanyika katika huduma za dawati la dharura ambapo wateja wanapiga simu kwenye kituo kikuu cha miito ya simu na wanapata huduma ndani ya muda mfupi zaidi” amesema Mhandisi Shamba.

Naye Mhandisi wa miradi na mitambo, kutoka kampuni ya Kilimo Pyxus, Muhoja Manane, amesema TANESCO imepiga hatua katika kuwahudumia wateja ikilinganishwa na kipindi cha nyuma.

Awali, Mwenyekiti wa wafanyakazi wa Shirika hilo kupitia Chama cha Wafanyakazi (TUICO), Ramadhan Butallah, amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wateja wanapata huduma bora.

''Wateja wanapewa huduma kulingana na mwongozo wa mkataba wa huduma kwa mteja kwa kuhamasisha wafanyakazi kuwahudumia vyema wananchi.''amesema

TANESCO Mkoa wa Dodoma wameshiriki katika zoezi la kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya kusheherekea wiki ya huduma kwa mteja inayoadhimishwa kila mwaka kuanzia wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba
Share:

BOSI WANGU KANIONGEZEA MSHAHARA MARA NNE

Share:

MABANGO YENYE UJUMBE MZITO KWENYE TAMASHA LA JINSIA 2022 'KEKETENI RUSHWA'



Washiriki wa Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali kuhusu Mila Kandamizi ambazo ni kikwazo cha kufikia haki za uchumi na maisha endelevu leo Ijumaa Oktoba 7,2022 katika viwanja vya Kwasa Kwasa wilayani Same.

Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini limeandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na wadau wanaotetea haki za wanawake na usawa wa jinsia na wanaharakati binafsi kwa ufadhili wa Ubalozi wa Watu wa Canada, Sweeden, Coady Institute Canada na Seedchange.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Washiriki wa Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali kuhusu Mila Kandamizi ambazo ni kikwazo cha kufikia haki za uchumi na maisha endelevu leo Ijumaa Oktoba 7,2022 katika viwanja vya Kwasa Kwasa wilayani Same.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA OKTOBA 7,2022







 

0

Share:

Thursday, 6 October 2022

WAZIRI JAFFO ATEMBELEA BANDA LA PSSSF MAONESHO YA SEKTA YA MADINI GEITA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jaffo (kushoto) akizungumza na Kaimu Meneja wa PSSSF Mkoa wa Geita Bw. Kiwamba Saidi (kulia) wakati Waziri huyo alipotembelea katika Banda la Mfuko huo katika Maonesho ya tano ya Sekta ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya Bombambili EPZA Geita.

Waziri Jaffo amekuwa mgeni rasmi wa siku ya leo Oktoba 6,2022 ambapo ameiagiza PSSSF kuweka vifaa maalum vya kutunzia taka (Dustbins) katika maeneo mbalimbali nchini kwa namna ambavyo PSSSF watapendekeza ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya 6 ya Rais Samia Suluhu Hassan ya utunzaji wa Mazingira.

Aidha Waziri Jaffo ameipongeza PSSSF kwa kazi nzuri wanayofanya ya kulipa mafao kwa wakati na kuwawezesha wastaafu kuwa na uhakika wa maisha yao baada ya kustaafu.

(Picha Na: Hughes Dugilo)

Kaimu Meneja wa PSSSF Mkoa wa Geita Bw. Kiwamba Saidi (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jaffo (kushoto) alipofika kwenye Banda la Mfuko huo kujionea shughuli wanazozifanya katika Maonesho ya Madini Geita.

Kaimu Meneja wa PSSSF Mkoa wa Geita Bw. Kiwamba Saidi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Mfuko huo katika Banda lao.
Share:

MAFUNZO YA KUENDELEZA UJUZI YATENGENEZA AJIRA KWA VIJANA NA WANAWAKE MKOANI MBEYA.


Mwakilishi kutoka Benki ya Dunia (WB) Bi. Innocent Mulindwa (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo wakati wa ziara katika kampuni ya RiversBank Fish Farm Wilayani Rungwe

Mkurugenzi wa Kampuni ya RiversBank Fish Farm Pius Nyambacha (mwenye kofia) akifurahia jambo na ujumbe uliofanya ziara katika mashamba yake ya kufugia samaki

Wajumbe kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Mamlaka ya Elimu Tanzania na Benki ya Dunia (WB) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kampuni ya RiversBank Fish Farm

************************

Mafunzo ya Kuendeleza Ujuzi yanayotolewa kupitia ruzuku ya Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) unaoratibiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) yametengeneza fursa za ajira kwa mamia ya vijana na akinamama katika wilaya ya Rungwe, Jijini Mbeya kupitia mradi wa kufuga samaki.

Mkurugenzi wa shamba la kufugia samaki la RiversBank Fish Farm, Pius Nyambancha ambalo ni miongoni mwa taasisi zilizofadhiliwa na SDF amebainisha hayo alipozungumza na ujumbe kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mamlaka ya Elimu Tanzania (TE) na wawakili wa Benki ya Dunia (WB)ambao ni wafadhili wa Mradi huo wa Kuendeleza Ujuzi (SDF).

Amesema ruzuku ya SDF imemwezesha kufuga samaki kitaalam ikiwa ni pamoja na kumpa uwezo wa kuzalisha vifaranga hivyo kumwongezea uzalishaji ambapo katika kipindi cha miezi tisa amezalisha kilo 600 za samaki na hivyo kujiongezea kipato.

Kupitia ruzuku ya SDF, Kampuni ya RiversBank Fish Farm ilipata ufadhili wa Shs. Milioni 131.2 ambazo zimewezesha uboreshaji wa miundombinu ya uzalishaji vifaranga vya samaki, ufugaji wa kisasa, ununuzi wa vifaa vya kisasa vya ufugaji pamoja na kuendesha mafunzo kwa vijana na akina mama 427 Wilayani Rungwe.

Nyambacha ameongeza kuwa, baada ya kujengewa uwezo na SDF amefanikiwa kutengeneza ajira kwa watanzania 726.

Ujumbe kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, TEA na Benki ya Dunia (WB) uko mkoani Mbeya kwa ziara ya siku nne ya ukaguzi wa miradi katika taasisi zilizonufaika na ufadhili wa SDF
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger