Tuesday, 27 September 2022
BENKI YA CRDB YAKABIDHI VITI NA MEZA KWA AJILI YA WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI MAMA SAMIA KAHAMA
BENKI YA LETSHEGO YAZINDUA HUDUMA MPYA KWA AJILI YA WAJASIRIAMALI NA WASTAAFU
SAMIA SCHOLARSHIP KUANZA RASMI KWA WAHITIMU WENYE UFAULU WA JUU MITIHANI YA KIDATO CHA SITA TAHASUSI ZA SAYANSI
Baadhi ya wadau wa Elimu waliohudhuria kwenye kikao maalum cha Menejimenti ya Wizara ya elimu nchini Jijini Dodoma .
Na Dotto Kwilasa,DODOMA
UFADHILI WA TEA KATIKA UJENZI WA MABWENI WACHANGIA UFAULU WA WANAFUNZI.
TBS YATOA MAFUNZO KWA WADAU WA ZAO LA MUHOGO MKOA WA LINDI NA MTWARA
NAIBU WAZIRI KATAMBI ATOA MAAGIZO KWA WAAJIRI NA VIONGOZI WA MATAWI TUGHE
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi ,Vijana,Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe Probass Katambi amewataka Viongozi wa matawi Tughe kuhakikisha wanatoa Elimu juu ya mafao kwa watumishi wastaafu kabla ya kustaafu.
Mhe. Katambi ameyasema hayo jijini Mwanza alipokuwa akifungua semina ya waajiri na viongozi wa matawi ya TUGHE iliyolenga kuondoa changamoto zisizo na tija mahala pa kazi.
Katambi alisema kuwa changamoto za wastaafu nyingi zinazotokea baada ya kustaafu serikalini, zinatokana na uelewa mdogo pamoja na uwajibikaji duni.
Katika ufunguzi wa semina hiyo,Naibu Waziri pia ameingeza kuwa Mwajiri asipoitisha vikao vya baraza la wafanyakazi kwa mujibu wa sheria TUGHE, wizara ipatiwe taarifa ili ifuatilie na kubaini sababu ya ukiukwaji huo.
“Nawashangaa sana wanao hujumu mahala pa kazi wakijua wanaikomoa serikali hapana ni wanahatarisha nafasi zao za ajira,sioni sababu za kuvujisha siri za ofisi kinachotakiwa ni kufanya kazi kwa uzalendo mkubwa kwajili ya taifa letu”. Aliongeza Mhe. Katambi.
Aidha Waziri aliwaagiza kuwa mafunzo watayopata wayatumie ipasavyo katika kuendesha mabaraza ya wafanyakazi yenye tija.
“Hakikisheni mnashauri ipasavyo waajiri wenu ili kuondoa tabia ya ukiukaji wa sheria na kanuni zinazounda mabaraza ya wafanyakazi , kila taasisi ya umma iwe na Baraza la wafanyakazi linalofanya vikao vyake kwa mujibu wa sheria”. Amesema Mhe. Katambi.
Sambamba na hayo Naibu waziri Katambi amewapongeza Viongozi wa matawi Tughe kwa kuitisha semina hiyo kwani jambo hilo litakuwa na tija na masilahi mapana kwa serikali na taasisi zote .
“Kwa yale mtakayo kubaliana hapa na kuyajadili kwa pamoja yatatusaidia sana kutika kutafuta fursa Zaidi na kubadilisha changamoto kuwa fursa, haki na wajibu wa mwajiri uko upande pia ya mwajiriwa haki ya mwajiri ni wajibu wa mwajiriwa na wajibu wa mwajiriwa ni haki ya mwajiri”. Amesema Waziri Katambi.
Monday, 26 September 2022
PROF. MKENDA ATAKA MABORESHO YA MITAALA YA ELIMU KUENDANA NA KASI YA MABADILIKO YA SEKTA HIYO
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda
Na Dotto Kwilasa, DODOMA.
SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imewataka wadau wa elimu nchini wanaoshiriki katika kikao maalum cha Menejiment ya wizara na wadau wa elimu kutoa maoni ya kuboresha sera na mitaala ya Elimu ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya sekta hiyo muhimu Duniani.
Waziri mwenye dhamana ya Elimu nchini Prof. Adolf Mkenda amesema hayo wakati akizungumza leo jijini Dodoma na kusema kuwa kikao hicho ni kutekeleza Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani.
Amefafanua kuwa agizo hilo alilitoa Mnamo Tarehe 22 Aprili 2022 Bungeni ambapo alitaka kufanyike marekebisho ya sera ya Elimu ya mwaka 2014 pamoja na mitaala iliyopo kwa maslahi ya Taifa na Watu wake.
Prof. Mkenda amesema kuwa huwezi kuzungumzia ubora wa elimu bila kufanya mageuzi na mabadiliko katika sera na mitaala ili kuendana na kasi ya maendeleo ya Dunia kwani kwa sasa taaluma na ujuzi zinakwenda sambamba.
"Tunapokwenda kufanya mageuzi ya elimu ni lazima twende na adhma ya Mhe. Rais aliyeagiza kuwa mbali tu na kujikita katika elimu ya taaluma tujikite pia katika Ujuzi hivyo ni lazima tuhakikishe tunatoa mawazo ambayo itasaidia kuboresha elimu yetu sio kushusha ubora,"amesema Prof. Mkenda.
Na kuongeza kuwa "Suala la elimu sio la Tanzania peke yake ni la kidunia hivyo lazima tufanye mageuzi ili kuendani na kasi ya mabadiliko katika sekta ya elimu duniani,"amesema.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Abdugulam Hussein amesema vijana lazima waandaliwe kitalamu na kiubunifu ili waweze kulitetea Taifa kimaendeleo na kushindana kimasoko.
Pia Mhe. Ali Abdugulam Hussein amesema kuwa swala la sera na mitaala ya elimu ndio kila kitu katika maboresho ya elimu hivyo kukifanyika makosa katika mapitiao haya yanaweza kulipoteza taifa.
"Sera na mitaala ni vyanzo muhimu katika elimu ya nchi yeyote duniani hivyo niwaombe washiriki wa kikao hiki maalum mtoe mawazo huku mkijua kuwa michango yenu ndio itakayokuja na sera na mitaala madhubuti,"amesema Mhe. Ali Abdugulam Hussein.
Dhima ya sera mpya na mitaala ya Elimu nchini ni kuinua ubora wa Elimu na Mafunzo na Kuweka Mifumo na Taratibu zitakazowezesha Kupata idadi Kubwa ya Watanzania walioelimika na wanaopenda kujielimisha zaidi ili waweze kuchangia katika kufikisha Malengo ya Maendeleo ya Taifa.