Monday, 19 September 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU SEPTEMBA 19,2022





















Share:

Sunday, 18 September 2022

WAANDAAJI WA MAUDHUI YA NDANI WACHAGIZWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA TEHAMA KUZALISHA MAUDHUI BORA YA NDANI

*TCRA yashauriwa kuanzisha tuzo za wazalishaji maudhui bora

Na Mwandishi Wetu

Waandaaji wa Maudhui ya ndani yakiwemo maudhui ya burudani, elimu, Habari, Sanaa na michezo wamekumbushwa kuwa uwepo na ukuaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ni fursa muhimu itakayowezesha kukuza sanaa na hatimae kukuza tija na kudumisha utamaduni unaojenga jamii imara.

Akizungumza wakati akifungua Warsha iliyowakutanisha Wadau wa Uzalishaji wa Maudhui ya Ndani wakiwemo Vituo vya Utangazaji, Waandaaji na Wasambazaji wa maudhui, wanazuoni wanaopika watayarishaji maudhui na waandaaji wa maudhuio ya kwenye mtandao Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) alisisitiza kuwa uwepo wa teknolojia mpya ya habari unawezesha wazalishaji maudhui kuifikia hadhira kubwa zaidi.Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb.) akiongoza kikao na Kamati ya Maudhui ya TCRA muda mfupi baada ya kufungua Warsha ya Waandaaji na Watayarishaji wa Maudhui iliyofanyika kwa siku mbili jijini Dar es salaam, ikiratibiwa na TCRA. Picha na: TCRA

“Ni ukweli usiopingika kwamba sasa mabadiliko ya teknolojia ya Habari na Utangazaji yametupeleka kwenye dunia nyingine ambayo usambazaji wa maudhui hauna mipaka. Kwa sasa unaweza kupokea maudhui kutoka sehemu yoyote duniani ili mradi unakifaa stahiki cha kupokelea maudhui. Makampuni makubwa ya kimataifa yanashindana kutengeneza na kusambaza Tamithiliya, Cartoon za Watoto, vichekesho (Comedy), Miziki, Makala na maudhui mengi yenye vionjo na tamaduni kutoka nchi mbalimbali. Ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa tunatumia teknolojia iliyopo kuhakikisha kuwa na sisi tunaingia kwenye ulimwengu wa ushindani na utandawazi ambapo utavutia Watanzania na wananchi wengine walioko nje ya mipaka ya nchi yetu ili nao waweze kutazama na kueneza Utamaduni wetu na vilevile kuongeza pato la taifa,” alisisitiza Waziri Nape.

Alibainisha kuwa jamii imekumbwa na changamoto ya kulishwa maudhui kutoka nchi za mbali ambayo kwa kiasi kikubwa hayazingatii maadili na utamaduni wa Mtanzania na hivyo yamechangia sana kuharibu utamaduni wa ndani.

“Kila Jamii inayo maadili yake tofauti na jamii nyingine. Sisi kama jamii ya Watanzania tunao utamaduni wetu, mila na desturi ambazo zinatutofautisha na jamii nyingine za kigeni. Waandaaji na watayarishaji wa maudhui mnayo dhamana kubwa ya kuhakikisha kwamba utamaduni wetu,mila na desturi zetu zinadumishwa na hazipotoshwi kabisa ili hata watoto wetu wanaozaliwa kizazi hadi kizazi wawe na cha kujivunia katika nchi yao kupitia vipindi ama habari wanazozipata kupitia vyombo vya Habari na utangazaji,” aliongeza.

Akizungumzia lengo la kuandaa Warsha hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari alibainisha kuwa, Mamlaka hiyo imeamua kuwaleta pamoja wadau hao kwa kuzingatia kuwa wanayo nafasi kubwa ya kuiwezesha nchi kupata maudhui ya ndani yanayokidhi ubora.

“Kwa kuelewa umuhimu wa maudhui ya ndani TCRA imeamua kuratibu warsha hii ya siku mbili ili kujadili mustakabali mwema wa uzalishaji wa maudhui ya ndani yenye ubora,” aliongeza Mkurugenzi Mkuu wa TCRA.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbas akifunga warsha hiyo ya siku mbili alisisitiza kuwa Wizara hiyo itahakikisha inashirikiana na wadau wote wa maudhui kuhakikisha maudhui ya ndani yanapatikana kwa wingi ili kuviwezesha vituo vya utangazaji na usambazaji wa maudhui kufikisha maudhui ya ndani yenye kuisaidia nchi.

Miongoni mwa taasisi zilizowakilishwa kwenye Warsha hiyo ni pamoja na TASUBA, BASATA, Chuo Kikuu cha Dar es salaam-Shule ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma, Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM), Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari(WHMTH), Wazalishaji wa maudhui ya mtandaoni, Wakusanyaji na Wasambazaji wa maudhui, Watayarishaji binafsi wa maudhui, Vyombo vya Utangazaji, Waandishi wa Habari miongoni mwa makundi mengine yaliyoshiriki Warsha hiyo, iliyoazimia kwamba kila upande uwajibike, huku TCRA ikitolewa mwito na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Nnauye, kutafakari uwezekano wa kuanzisha tuzo maalum kwa wazalishaji bora wa maudhui ya ndani.

Share:

BENKI CRDB YAFANYA TAMASHA MAALUM LA KUTOA ELIMU YA BIMA YA VYOMBO VYA MOTO 'KUWA MSHUA’


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe (wapili kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Kitengo cha Bima Benki ya CRDB, Moureen Majaliwa wakati wakitembelea mabanda katika tamasha la kutoa elimu ya bima kwa vyombo vya moto lililoandaliwa na Benki ya CRDB na kufanyika kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. Wengine pichani ni Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Bonaventure Paul (kulia) pamoja na Meneja Mwandamizi wa Mawasiliano na Mahusiano wa Benki ya CRDB, Emmanuel Kiondo.

======== ======== =======

Benki ya CRDB imezindua rasmi kampeni maalum ya elimu ya bima ya vyombo vya moto iliyopewa jina la ‘Kuwa Shua’ tamasha lililofanyika kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.

Akizungumza katika tamasha hilo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe alisema ili kuchochea ukuaji wa sekta ya bima na kuongeza ujumuishi wa sekta hii yaani “Insurance Inclusion,” Serikali kupitia Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha imekuwa ikiandaa programu mbalimbali za elimu kwa umma juu ya umuhimu wa matumizi ya bima.

"Ni imani yangu kuwa kampeni hii ya mwaka huu ya “Kuwa Shua” itawajengea uelewa wamiliki wa vyombo vya moto umuhimu wa kukata bima dhidi ya majanga yanayoweza kutokea, niipongeze Benki yetu ya CRDB kwa kutekeleza kwa vitendo agizo hili la ufikishaji wa elimu ya bima kwa wateja wenu na wananchi. Nafahamu mwaka jana mliendesha kampeni ya “Bima Unachokithamini” mkitoa elimu ya umuhimu wa bima katika nyanja mbalimbali". alisema Gondwe.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Bima ya Sanlam, Ernest Selestine (watatu kushoto) wakati akitembelea mabanda katika tamasha la kutoa elimu ya bima kwa vyombo vya moto lililoandaliwa na Benki ya CRDB na kufanyika kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es salaam. Tamasha hilo liliwaleta pamoja wadau mbalimbali wa vyombo vya moto kama Kampuni za Bima, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), Msuluhishi wa Migogoro ya Bima, Jeshi la Polisi, gereji pamoja na maduka ya vifaa mbalimbali za vyombo hivyo. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Bima Benki ya CRDB, Moureen Majaliwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe (watatu kulia) akipata maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya Bima ya Strategis, Lilian Malakasuka (katikati) wakati akitembelea mabanda katika tamasha la kutoa elimu ya bima kwa vyombo vya moto lililoandaliwa na Benki ya CRDB na kufanyika kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es salaam. Tamasha hilo liliwaleta pamoja wadau mbalimbali wa vyombo vya moto kama Kampuni za Bima, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), Msuluhishi wa Migogoro ya Bima, Jeshi la Polisi, gereji pamoja na maduka ya vifaa mbalimbali za vyombo hivyo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Bima Benki ya CRDB, Moureen Majaliwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe akipata maelezo kutoka kwa Maafisa wa Shirika la Bima nchini wakati alipotembea banda lao katika tamasha la kutoa elimu ya bima kwa vyombo vya moto lililoandaliwa na Benki ya CRDB na kufanyika kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe furahi jambo na Maafisa wa Shirika la Bima la Zanzibar wakati alipotembea banda lao katika tamasha la kutoa elimu ya bima kwa vyombo vya moto lililoandaliwa na Benki ya CRDB na kufanyika kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe akipata maelezo kutoka kwa Mdau mkuu wa ukarabari wa magari, Edwin Mactemba wakati alipotembea banda lake katika tamasha la kutoa elimu ya bima kwa vyombo vya moto lililoandaliwa na Benki ya CRDB na kufanyika kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es salaam.




Share:

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI ...MHANDISI KHATIB APELEKWA TCRA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:

  1. Amemteua Bw. Sosthenes Laurent Kewe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Tanzania (TIB). Bw. Kewe ni Mshauri Binafsi wa Uendelezaji wa Sekta Binafsi za Fedha, Dar es Salaam.

2.Amemteua Mhandisi Othman Sharif Khatib kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Bw Khatib anachukua nafasi ya Dkt. Jones Kilembe ambaye uteuzi wake umetenguliwa. Bw. Khatib ni Mhandisi Mstaafu (TCRA).

3.Amemteua Dkt. David Nkanda Manyanza kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI). Dkt. Manyanza ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Development Solution Consultancy (T) Limited.

4.Amemteua Bi. Hawa Abdulrahman Ghasia kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Masoko Kariakoo. Bi Ghasia ni Mbunge mstaafu.

5.Amemteua Bw. Sylvester Jospeh Kainda kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani. Bw. Kainda ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Morogoro.

Uteuzi huu unaanza mara moja.

Share:

SIMBA SC YAENDELEZA UBABE KIMATAIFA, YAICHAPA NYASA BIG BULLETS 2-0



**********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU ya Simba imefanikiwa kutinga hatua inayofuata Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufanikiwa kuichapa Nyasa Big Bullets mabao 2-0 na kufikia jumla ya mabao 4-0 baada ya mechii ya kwanza Simba Sc akiwa ugenini kupata mabao 2-0.

Simba Sc imepata mabao kupitia kwa Moses Phiri ambaye amepachika mabao yote mawili na kuiwezesha timu yake kutinga hatua inayofuata Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba Sc inatinga hatua inafuata na kuungana na wenzake Yanga Sc ambao nao jana walifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuwachapa Zalan Fc kwa jumla ya mabao 9-0.
Share:

SERIKALI YAIPONGEZA BARRICK KWA KUTEKELEZA SERA YA USHIRIKISHAJI WANANCHI KATIKA MNYORORO WA SEKTA YA MADINI (LOCAL CONTENT) KWA VITENDO


Kamishna wa Tume ya Madini ,Janeth Lekashingo (katikati) akifunga warsha ya ya ushirikishwaji wananchi katika mnyororo wa sekta ya madini (Local Content iliyofanyika katika mgodi wa Bulyanhulu mwishoni mwa wiki (Kushoto) ni Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Jan Jacobs (kulia) ni Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Madini kutoka tume hiyo,Bw.Venance Kasiki.
Meneja wa Barrick nchini, Georgia Mutagahywa, akitoa mada wakati wa semina ya ushirikishwaji wananchi katika mnyororo wa sekta ya madini (Local Content iliyofanyika katika mgodi wa Bulyanhulu mwishoni mwa wiki,(Kulia) ni Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Jan Jacobs.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada wakati wa semina hiyo
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada wakati wa semina hiyo
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada wakati wa semina hiyo
Washiriki katika picha ya pamoja na Kamishna wa Tume ya Madini

***
Kamishna wa Tume ya Madini nchini, Janeth Lekashingo, ameipongeza kampuni ya madini ya Barrick kwa jitihada inazofanya kuhakikisha inatekeleza sera ya ushirikishwaji wananchi katika mnyororo wa sekta ya madini (Local Content) kwa lengo la kuwanufaisha Watanzania wanaoishi jirani na migodi yake.

Akifunga semina ya siku mbili iliyohusu ushirikishwaji wananchi katika mnyororo wa sekta ya madini (Local Content) iliyoandaliwa na Twiga Minerals Corporation na kufanyika katika mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu, Bi. Lekashingo, alisema Barrick ni miongoni mwa makampuni ambayo yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza sera hii kwa vitendo.


 Semina hiyo ilihusisha wafanyakazi wa Barrick na Maofisa kutoka Tume ya Madini ambao walitoa mada mbalimbali kuhusiana na uendeshaji wa shughuli za uchimbaji madini nchini kwa kufuata sheria na miongozo ya Serikali.


"Nawapongeza sana kwa kuwa mstari wa mbele katika kutekeleza sera hii kwa vitendo na pia kufanikisha miradi ya maendeleo katika maeneo yanayozunguka migodi yenu kupitia fedha za uwajibikaji katika jamii (CSR)", alisema Lekashingo.

Alisema moja ya majukumu ya Tume ya Madini ni kusimamia wadau katika sekta ya madini kuhakikisha wanatekeleza sera hii hususani katika utoaji wa zabuni kwa makampuni ya wazawa yaliyosajiliwa na tume hiyo na makampuni ya nje yanayoshirikiana na wazawa ikiwemo suala la kutoa ajira kwa wazawa.

Aliongeza kusema Tume ya Madini iko tayari kutoa ushauri wa kitaalamu bure kwa Barrick na wadau wengine katika sekta ya madini kuhakikisha sera hii inatekelezwa na kufanikisha lengo lake la kuwawezesha watanzania kunufaika na sekta ya madini.

Akiwasilisha mada ya utendaji wa shughuli za Barrick, Meneja wake nchini Georgia Mutagahywa, alisema hadi kufikia sasa takribani asilimia 70% ya watoa huduma katika migodi ya Barrick nchini ni Watanzania.

“Kampuni imefanikiwa kutekeleza sera hii kwa vitendo katika maeneo ya ajira, utoaji wa zabuni, sambamba na kuendesha miradi ya kusaidia jamii katika maeneo yanazozunguka migodi yake nchini kupitia fedha zilizotengwa kwa ajili ya kuhudumia jamii (CSR)” ,alisema Mutagahywa.

Aliongeza kuwa Barrick, tayari imeanzisha programu ya kuwaendeleza wafanyabiashara wa ndani,(Local Business Development Programme (LBD) inayosimamiwa na mgodi wa North Mara, ambayo ni mhimili wa kusimamia kanuni hii na kuhakikisha watanzania wananufaika nayo kwa asilimia kubwa kwa kuboresha maisha yao kupitia uwekezaji katika sekta ya madini, na fursa zilizopo kwenye sekta hii na tayari baadhi ya wafanyabiashara wamepatiwa mafunzo katika awamu ya kwanza.


Watendaji kutoka Tume ya Madini pia walipata fursa ya kutembelea mgodi wa Bulyanhulu na kujionea shughuli za uchimbaji zinazofanywa na Barrick kwa kutumia teknolojia za kisasa zenye viwango vya kimataifa vilevile walitembelea kituo cha afya za Bugarama wilayani Msalala ambacho kimeboreshwa na kuwa cha kisasa kupitia fedha za Uwajibikaji wa jamii zilizotolewa na kampuni hiyo.

Serikali ya Tanzania iliunda sera ya Local content mwaka 2017 ikilenga sekta ya madini, mafuta na gesi ili kuhakikisha uchimbaji wa madini na mapato yake yanawanufaisha watanzania.

Sera hiyo na kanuni zake inalenga kupanua uwanda wa kibiashara kwenye uchumi wa Tanzania, kutengeneza nafasi za ajira kwa kuhamasisha maendeleo ya taaluma na uwezo wa watanzania kushiriki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi nchini.


Share:

DOWNLOAD/ INSTALL UPYA APP YA MALUNDE 1 BLOG

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI SEPTEMBA 18,2022











Share:

Saturday, 17 September 2022

TBS YASHIRIKI VIWANGO SPORTS BONANZA

Watumishi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakicheza drafti katika Bonanza la Michezo kwa wafanyakazi wa Shirika hilo lililofanyika leo Septemba 17,2022 katika viwanja vya Chuo cha Ardhi Jijini Dar es Salaam.Watumishi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakicheza bao katika Bonanza la Michezo kwa wafanyakazi wa Shirika hilo lililofanyika leo Septemba 17,2022 katika viwanja vya Chuo cha Ardhi Jijini Dar es Salaam. Watumishi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakicheza mpira wa miguu katika Bonanza la Michezo kwa wafanyakazi wa Shirika hilo lililofanyika leo Septemba 17,2022 katika viwanja vya Chuo cha Ardhi Jijini Dar es Salaam. Watumishi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakicheza Volley ball katika Bonanza la Michezo kwa wafanyakazi wa Shirika hilo lililofanyika leo Septemba 17,2022 katika viwanja vya Chuo cha Ardhi Jijini Dar es Salaam. Watumishi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakicheza mpira wa pete katika Bonanza la Michezo kwa wafanyakazi wa Shirika hilo lililofanyika leo Septemba 17,2022 katika viwanja vya Chuo cha Ardhi Jijini Dar es Salaam.

Watumishi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakicheza mchezo wa kuvuta kamba katika Bonanza la Michezo kwa wafanyakazi wa Shirika hilo lililofanyika leo Septemba 17,2022 katika viwanja vya Chuo cha Ardhi Jijini Dar es Salaam.

********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), leo Septemba 17,2022 wameshiriki siku ya Bonanza la Michezo kwa wafanyakazi wa Shirika hilo dhumuni kuu likiwa nikuwakutanisha watumishi wa TBS katika michezo ili kuboresha afya na kujenga mahusiano mazuri miongoni mwa watumishi.

Akizungumza wakati wa Bonanza hilo lililofanyika Jijini Dar es Salaam, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi TBS, Bw.Twalib Mmbaga amesema katika Bonanza hilo ambalo wameliita kwajina la 'Viwango Sports Bonanza'ni tukio linaloshindanisha watumishi wa shirika la viwango Tanzania katika michezo mbalimbali kama vile mpira wa miguu, mpira wa pete, mpira wa wavu, kuvuta kamba na michezo ya jadi ambapo mashindano hayo yanashindanishwa kiidara.

"Kupitia michezo hii watumishi wanapata burudani na kupunguza msongo wa mawazo unaoweza kutokana na kukosa nafasi ya kufanya mazoezi au kushiriki michezo mbalimbali". Amesema

Aidha amewapongeza wanaviwango waliojitokeza siku hiyo na walioona umuhimu wa kushiriki katika michezo hiyo ili kuboresha afya zao na kujenga mahusiano mazuri kati ya watumishi kwani utekelezaji mzuri wa majukumu ya kila siku hutegemea afya ya mwili na akili.

Pamoja na hayo ameipongeza menejimenti ya TBS kwa jitihada ilizozifanya kuweza kufanikisha Viwango Sports Bonanza kwani haikuwa rahisi ikizingatiwa kuwa shughuli kama hii inahitaji uwepo wa bajeti ili kufanikisha.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger