Wednesday, 7 September 2022

DC MBONEKO AHAMASISHA WANANCHI KUENDELEA KUPATA CHANJO YA UVIKO - 19

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye kikao cha kuhamasisha chanjo ya UVIKO-19 katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye kikao cha kuhamasisha chanjo ya UVIKO-19 katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amewahamasisha wananchi kuendelea kujitokeza kupata chanjo ya UVIKO-19, ili kuimarisha kinga za miili yao, na kuepuka kupata madhara makubwa pale watakapoambukizwa virusi vya Corona.

Mboneko amebainisha hayo leo Septemba 7, 2022 wakati akifungua kikao cha uhamasishaji wananchi kupata chanjo ya UVIKO-19 katika Kata Nne za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, ambazo ni Lyamidati, Mwenge, Imesela, na Mwamala.

Amesema baada ya watu kupata chanjo ya UVIKO-19 maambukizi ya virusi vya Corona yamepungua hapa nchini, ambapo mtu akipata chanjo hawawezi kudhurika zaidi tofauti na wale ambao hawakupata chanjo hususani pale watakapopata maambukizi.

“Tunamshukuru Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutuletea chanjo za UVIKO-19 na kujali afya za wananchi wake, na wananchi wakiwa na afya njema watafanya vizuri shughuli za maendeleo,”amesema Mboneko.

“Wakati wa utoaji chanjo ya UVIKO-19 anzeni pia na Makundi maalum, wakiwemo wazee, wenye magonjwa sugu na watumishi, na pale penye changamoto nipeni taarifa ili tuitatue na zoezi hili lifanikiwa kwa asilimia 100 kwa kuchanja wananchi wengi,”ameongeza.

Katika hatua nyingine Mboneko ameonya upotoshaji juu ya chanjo ya UVIKO-19  na kubainisha kuwa chanjo ni salama na zinatolewa bure, na kuwataka wataalam watoe elimu ya kutosha kwa wananchi ili zoezi hilo lifanikiwe kama ilivyofanyika kwenye chanjo ya Polio.

Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Dk. Nuru Yunge, amesema wamefanya kikao hicho cha kampeni ya kuhamasisha chanjo ya UVIKO-19 kwa kushirikiana na Shirika la USA PeaceCorps kwa kuanza na Kata Nne wilayani humo.

Amesema katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga lengo lao lilikuwa ni kuchanja watu chanjo ya UVIKO-19, 218,929 lakini watu waliopata chanjo kamili wilayani humo ni 120,107 na waliopata dozi moja ni 47,359.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Dk. Nuru Yunge akizungumza kwenye kikao cha kuhamasisha wananchi kupata chanjo ya UVIKO-19.

Kikao cha hamasa chanjo ya UVIKO-19 kikiendelea.

Kikao cha hamasa chanjo ya UVIKO-19 kikiendelea.

Kikao cha hamasa chanjo ya UVIKO-19 kikiendelea.

Kikao cha hamasa ya chanjo ya UVIKO-19 kikiendelea.

Kikao cha hamasa chanjo ya UVIKO-19 kikiendelea.

Kikao cha hamasa chanjo ya UVIKO-19 kikiendelea.

Kikao cha hamasa ya chanjo ya UVIKO-19 kikiendelea.

Kikao cha hamasa chanjo ya UVIKO-19 kikiendelea.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akipiga picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kufungua kikao cha hamasa ya chanjo ya UVIKO-19 Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.

Share:

APIGWA HADI KUFA NA MMEWE KISA KACHELEWA KURUDI NYUMBANI AKITAFUTA MAREJESHO YA KIKOBA

Aisha Ramadhani (Marehemu)

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia Peter Mwakiposile kwa tuhuma za kumuua mkewe Aisha Ramadhani mkazi wa Chidachi kwa kupigwa hadi kufa, kwa kosa la kuchelewa kurudi nyumbani akitafuta fedha za Marejesho la kikundi cha kikoba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma ACP Martin Otieno ameeleza kuwa mtuhumiwa yupo chini ya ulinzi wakati akisubiri taratibu za kufikishwa mahakamani huku mwili wa marehemu Aisha Ramadhani ukiwa umehifadhiwa chumba cha kuhifadhia maiti kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa taratibu za mazishi.

Mama wa marehemu Aisha Ramadhani amesimulia kuwa alipigiwa simu na mkwe wake Peter Mwakiposile wakati akitekeleza unyama huo ambapo ilisikika sauti ya marehemu ikiomba msaada kitendo ambacho kilipuuzwa na mumewe huku watoto wa marehemu wakisema mama yao aliondoka nyumbani saa 12 jioni na kurudi saa 2 usiku baada ya kwenda kuomba fedha kwa rafiki yake kwa ajili ya rejesho ndipo baba yao akaanza kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake.

Chanzo - EATV
Share:

HATIMAYE WILLIAM RUTO AWASILIANA NA UHURU KENYATTA

Uhuru Kenyatta na William Samoei Ruto

NI muda ulipita tangu Rais mteule awasiliane na Uhuru Kenyata baada ya watu hao wawili kuhitirafiana kutokana na Uhuru kuamua kumsapoti mpinzani wa Ruto Bw. Raila Odinga.

Katika hotuba aliyoitoa baaada ya kuidhinishwa na mahakama kuwa rais alieleza kua wanamuda mrefu tangu awasiliane na Rais Kenyata.

Ujumbe aliouchapisha Ruto kwenye Ukurasa wa Twitter

Lakini kupitia mtandao wa twitter Bw Ruto amesema ameweza kuwasiliana na Uhuru Kenyata na kuweza kuelezana kuhusu sherehe za kimila kama jadi yao pamoja na demokrasia.

Imeandikwa:Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao
Share:

Tuesday, 6 September 2022

YANGA YATOKA SARE NA AZAM FC LIGI KUU YA NBC

MABINGWA watetezi Yanga wametoka nyuma na kutoka sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Matajiri wa Chamazi Complex Azam FC mchezo wa ligi Kuu ya NBC uliochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Shujaa wa Yanga ni Feisal Salum (Fei Toto) aliyetokea benchi na kwenda kufunga mabao yote mawaili dakika ya 56 na 77.

Azam FC walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa beki wao kisiki,Daniel Amoah dakika ya 24 akifunga bao kwa kichwa akimalizia faulo ya Ayubu Lyanga baada ya Yannic Bangala kumchezea rafu Prince Dube.

Hadi timu zinakwenda mapumziko Azam Fc walikuwa mbele ya bao hilo moja .

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko mnamo dakika ya 65 Malickou Ndoye aliifungia bao la pili Azam FC huku Yanga wakikosa Penalti iliyoadakwa na golikipa wa Azam FC iliyopigwa na Shaban Djuma baada ya Lusanjo Mwaikenda kumchezea rafu Benard Morrison.

Kwa Matokeo hayo Yanga wamefikisha mechi 40 wakicheza bila kufungwa na wanapanda mpaka nafasi ya kwanza wakiwa na Pointi 7 huku Azam Fc wakifikisha Pointi 5 Mechi nyingine imechezwa uwanja wa CCM Kiruma wenyeji Geita Gold wametoshana nguvu ya kufungana bao 1-1 na Kagera Sugar.

Ligi hiyo itaendelea kesho Simba watacheza na KMC katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Share:

RC MJEMA ASHUHUDIA UWEKAJI SAINI WA MIKATABA ZABUNI YA UJENZI WA BARABARA… "FEDHA ZIPO, MKAJENGE KWA WAKATI, VIWANGO"

Meneja Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) mkoa wa Shinyanga Mhandisi Oscar Gilbert Mlekwa (kulia) akibadilishana Mikataba ya Zabuni ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja mkoa wa Shinyanga na Mkurugenzi wa Kampuni ya MIDA Women Group, Milka Marisham.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema, amesema hatakubali kuona utekelezaji mbovu wa ujenzi wa miradi ya maendeleo huku akiwataka Wakandarasi wanaojenga miundo mbinu ya barabara kujenga kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa.

Dkt. Mjema amesema hayo leo Jumanne Septemba 6, 2022 wakati akishuhudia hafla ya Usainishaji Mikataba 15 ya Zabuni ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja mkoa wa Shinyanga kati ya Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) na Wakandarasi watatu yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6.

Wakandarasi hao watatu wazawa waliosaini Mkataba na TARURA ni MIDA Women Group, Joline Women Group na Corsyne Consult Ltd ambao watajenga barabara za kiwango cha changarawe na madaraja kwenye maeneo mbalimbali mkoani Shinyanga.

Dkt. Mjema amesema jumla ya shilingi Bilioni 2.6 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya barabara hivyo anachotaka ni ujenzi kufanyika kwa wakati na kwa kuzingatia ubora unaotakiwa.

“Fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara zipo, nendeni mkajenge barabara za viwango na mtekeleze kwa wakati uliopangwa. Tunataka barabara za viwango zitakazodumu kwa miaka 20 na siyo mwaka mmoja tu barabara inakuwa mbovu mnaanza kuzikarabati, hilo hatutaki. Ninyi ni wakandarasi wazawa fanyeni kazi zenu kwa ufanisi mkubwa na mshindane na Wakandarasi kutoka Nje ya nchi,”amesema Mjema.

“Tunataka kupokea barabara zenye viwango vya juu. Nategemea barabara zote ziwe na viwango. Hatutakubali kuona wala kupokea ujenzi wa barabara ambayo ipo chini ya kiwango,”ameongeza Mjema.

Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Ramadhani Masumbuko amesema amefurahi kuona Wakandarasi wazawa akibainisha kuwa kutokana na kwamba miundombinu ya barabara ni kiungo muhimu cha ukuaji wa uchumi ana imani kuwa Wakandarasi hao wazawa watatekeleza miradi hiyo kwa ufanisi mkubwa huku akiwataka TARURA kuwa makini kusimamia ujenzi wa miundo mbinu kwa hatua zote.

Naye Meneja Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) mkoa wa Shinyanga Mhandisi Oscar Gilbert Mlekwa amesema kati ya bajeti iliyotengwa kwa Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ni shilingi 15,321,240,000/= na kwamba mikataba hiyo iliyosainiwa ni ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha changalawe na madaraja katika wilaya za Kahama, Shinyanga na Kishapu.

“Nawapongeza Wakandarasi walioshinda zabuni hizi nawaasa watekeleze miradi hii kwa kuzingatia ubora na muda uliopangwa. Barabara hizi zikiboreshwa zitachochea sana ukuaji wa uchumi wa wananchi kwa mkoa wetu na kuboresha sana sekta za kilimo na utalii”,amesema Mhandisi Mlekwa.

Katika hatua nyingine amesema TARURA Mkoa wa Shinyanga inahudumia mtandao wa barabara wenye urefu wa Km 5,220.02, kati ya hizo barabara za lami ni Km 1,414.70 na barabara za udongo ni Km 3,767.19.

Nao Wakurugenzi wa Makampuni hayo ya Ukandarasi Flora Charles Gabba wa Kampuni ya Joline Women Group na Denis Kisoka wa Kampuni ya Corsyne Ltd na Milka Marisham wa Kampuni ya MIDA Women Group wameipongeza Serikali kwa kujali Wakandarasi wazawa na kuwapatia kazi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara huku wakiahidi kutowaangusha na kutekeleza kazi zao kwa kiwango bora na kuikamilisha kwa wakati.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akizungumza leo Jumanne Septemba 6, 2022  katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHY COM) Mjini Shinyanga wakati akishuhudia hafla ya Usainishaji Mikataba 15 ya Zabuni ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja mkoa wa Shinyanga kati ya Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) na Wakandarasi watatu yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema akizungumza wakati akishuhudia hafla ya Usainishaji Mikataba 15 ya Zabuni ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja mkoa wa Shinyanga kati ya Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) na Wakandarasi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6. 

Meneja Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) mkoa wa Shinyanga Mhandisi Oscar Gilbert Mlekwa akizungumza wakati wa hafla ya Usainishaji Mikataba 15 ya Zabuni ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja mkoa wa Shinyanga kati ya TARURA na Wakandarasi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6. 

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akizungumza wakati wa hafla ya Usainishaji Mikataba 15 ya Zabuni ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja mkoa wa Shinyanga kati ya TARURA na Wakandarasi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6. 
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo akizungumza wakati wa hafla ya Usainishaji Mikataba 15 ya Zabuni ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja mkoa wa Shinyanga kati ya TARURA na Wakandarasi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6. 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema (katikati) akizungumza wakati akishuhudia hafla ya Usainishaji Mikataba 15 ya Zabuni ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja mkoa wa Shinyanga kati ya Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) na Wakandarasi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6. 
Afisa Sheria wa Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Shinyanga, Male Samson Mathias (kulia) akizungumza wakati wa hafla ya Usainishaji Mikataba 15 ya Zabuni ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja mkoa wa Shinyanga kati ya TARURA na Wakandarasi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6. 
Mkurugenzi wa Kampuni ya MIDA Women Group, Milka Marisham akisaini Mikataba ya Zabuni ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja mkoa wa Shinyanga iliyosainiwa kati ya Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) na Wakandarasi.
Afisa Sheria wa Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA)Mkoa wa Shinyanga, Male Samson Mathias (mwenye suti nyeusi) na  Meneja Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) mkoa wa Shinyanga Mhandisi Oscar Gilbert Mlekwa wakisaini Mikataba ya Zabuni ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja mkoa wa Shinyanga iliyosainiwa kati ya Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) na Wakandarasi.
Meneja Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) mkoa wa Shinyanga Mhandisi Oscar Gilbert Mlekwa akisaini Mikataba ya Zabuni ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja mkoa wa Shinyanga iliyosainiwa kati ya Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) na Wakandarasi.
Meneja Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) mkoa wa Shinyanga Mhandisi Oscar Gilbert Mlekwa (kulia) akibadilishana Mikataba ya Zabuni ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja mkoa wa Shinyanga na Mkurugenzi wa Kampuni ya MIDA Women Group, Milka Marisham.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Joline Women Group,  Flora Charles Gabba (kushoto) akisaini Mikataba ya Zabuni ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja mkoa wa Shinyanga iliyosainiwa kati ya Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) na Wakandarasi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Joline Women Group,  Flora Charles Gabba (kushoto) akisaini Mikataba ya Zabuni ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja mkoa wa Shinyanga iliyosainiwa kati ya Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) na Wakandarasi. Kulia ni Meneja Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) mkoa wa Shinyanga Mhandisi Oscar Gilbert Mlekwa.
Zoezi la kusaini Mikataba ya Zabuni ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja mkoa wa Shinyanga iliyosainiwa kati ya Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) na Wakandarasi likiendelea.
Meneja Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) mkoa wa Shinyanga Mhandisi Oscar Gilbert Mlekwa akisaini Mikataba ya Zabuni ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja mkoa wa Shinyanga iliyosainiwa kati ya Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) na Wakandarasi.
Meneja Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) mkoa wa Shinyanga Mhandisi Oscar Gilbert Mlekwa (kulia) akibadilishana Mikataba ya Zabuni ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja mkoa wa Shinyanga na Mkurugenzi wa Kampuni ya Joline Women Group,  Flora Charles Gabba.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Corsyne Ltd, Denis Kisoka (kushoto) akisaini Mikataba ya Zabuni ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja mkoa wa Shinyanga iliyosainiwa kati ya Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) na Wakandarasi.
Meneja Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) mkoa wa Shinyanga Mhandisi Oscar Gilbert Mlekwa akisaini Mikataba ya Zabuni ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja mkoa wa Shinyanga iliyosainiwa kati ya Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) na Wakandarasi.
Afisa Sheria wa Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA)Mkoa wa Shinyanga, Male Samson Mathias (mwenye suti nyeusi) akisaini Mikataba ya Zabuni ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja mkoa wa Shinyanga iliyosainiwa kati ya Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) na Wakandarasi.
Meneja Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) mkoa wa Shinyanga Mhandisi Oscar Gilbert Mlekwa (kulia) akibadilishana Mikataba ya Zabuni ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja mkoa wa Shinyanga na Mkurugenzi wa Kampuni ya Corsyne Ltd, Denis Kisoka
Wadau wakiwa kwenye hafla ya Usainishaji Mikataba 15 ya Zabuni ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja mkoa wa Shinyanga kati ya Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) na Wakandarasi watatu yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6.

TBS YAWANOA MAAFISA KUTOKA MAABARA ZA UBORA NA UCHUNGUZI KUHUSU VIPIMO MWANZA

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Mhe. Amina Makilagi kufungua mafunzo kwa wafanyakazi kutoka taasisi za maabara za ubora na uchunguzi yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika ukumbi wa TMDA Buzuruga Mwanza mapema leo

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Mhe. Amina Makilagi akifungua mafunzo kwa wafanyakazi kutoka maabara za ubora na uchunguzi kuhusu sayansi ya vipimo yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango (TBS)mapema leo katika ukumbi wa TMDA Mwanza.

Washiriki wa mafunzo kutoka maabara za ubora na uchunguzi wakifuatilia mafunzo ya sayansi ya vipimo yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ambayo yamefanyika leo Nyamagana mkoani Mwanza.

*********

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Mhe. Amina Makilagi amefungua mafunzo kwa wafanyakazi kutoka maabara za ubora na uchunguzi kuhusu sayansi ya vipimo yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Mhe. Makilagi amefungua mafunzo hayo Jumanne Septemba 06, 2022 katika ukumbi wa TMDA Buzuruga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe. Adam Malima.

Mhe. Makilagi ametumia fursa hiyo kuipongeza TBS kwa kuandaa mafunzo hayo kwani yatakuwa chachu ya kuongeza ufanisi katika maabara zinazofanya vipimo vya ubora na uchunguzi na kutoa majibu sahihi.

"Mwanza ni Mkoa wa kimkakati unaokua kwa kasi, tuna miradi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi na afya hivyo baada ya mafunzo haya tunategemea kuona mkifanya vipimo vitakavyotoa majibu sahihi na ya kuaminika" amesema Mhe. Makilagi.

Naye Mkurugenzi Mkuu TBS, Dkt. Athuman Ngenya amesema washiriki wa mafunzo hayo watajengewa uwezo kuhusu sayansi ya vipimo (Metrolojia) pamoja na mchakato wa kuangalia ubora wa bidhaa katika vipimo (Ugezi) kwani hizo ni nyenzo muhimu katika uzalishaji akisema "ukikosea vipimo hata bidhaa yako haiwezi kuwa na ubora".

Baadhi ya washiriki akiwemo Mkuu wa Kitengo cha Mizani TANROADS Mkoa Mwanza, Mhandisi Joseph Kalala pamoja Mwakilishi wa Maabara ya SGS, Suma Mwakyembe wamesema mafunzo hayo ni muhimu na yatasaidia kuleta mabadiliko ya kiutendaji katika taasisi zao.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger