Wednesday, 31 August 2022

TAKRIBANI TANI TISA ZA BIDHAA ZENYE VIAMBATA SUMU ZATEKETEZWA



*********************

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeteketeza bidhaa za aina mbalimbali zenye viambata sumu ambazo hazikidhi matakwa ya viwango za uzito wa tani tisa zenye thamani ya shilingi milioni 400.

Akizungumza Mkuranga Mkoani Pwani kaimu Mkurugenzi,usimamizi na utekelezaji wa sheria wa TBS, Dkt, Candida Shirima, amesema kuwa shehena ya bidhaa zilizoteketezwa zina uzito wa tani 9 na nyingi ni vipodozi vyenye viambata sumu ambayo vimeshapingwa marufuku kwa mijibu wa sheria ya viwango sura 130.

Dkt Shirima amesema kuwa viambata sumu hivyo ni aina ya Zebaki,hydroquinone na steroids ambayo ni hatari kwa afya ya watumiaji wa vipodozi kwani husababisha madhara mbalimbali kama vile ya ngozi muwasho, ngozi kuwa nyekundu, laini,saratani madhara ya figo na uzazi.

Aidha ameitaka jamii kuepuka kutumia vipodozi vyenye viambata sumu na vilivyopigwa marufuku kama ambavyo imekuwa ikishauriwa na kusisitizwa na mamlaka hiyo pamoja na wataalamu wa afya ili kulinda afya.

Pia amewataka wananchi kuangalia muda wa matumizi kwenye bidhaa hususani vyakula kabla ya kununua au kuzitumia huku wafanyabishara kuhakikisha kuwa wanazingatia sheria na kanuni na viwango ili kutoingiza nchini,kuzalisha,kuuza au kusambaza bidhaa zisizokidhi vigezo vya ubora na usalama ili kuwalinda watumiaji na kukuza uchumi wa nchi.

Kwa upande wake Kaimu Meneja Kanda ya Mashariki wa TBS, Fransis Mapunda amesema kuwa bidhaa hizo zilizotekezwa wamezikamata katika maeneo mbalimbali ikiwemo mkoani Morogoro, Pwani na Zanzibar huku akiwataka wafanyabishara kutokujihusisha na bidhaa zisizokidhi vigezo.

"Zoezi la ukaguzi ni endelevu katika maeneo yote hivyo sehemu yoyote mtu atakayejihusisha na biashara ambazo hazikidhi matakwa ya sheria atakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa sheria zilizowekwa kwa masilahi mapana ya taifa kwa ujumla"amesema Mapunda

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO AGOSTI 31,2022



Magazetini leo Jumanne August 31 2022





































Share:

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MUHEZA ASIMAMISHWA KAZI KUPISHA UCHUNGUZI


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI),Mheshimiwa Innocent Bashungwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga,Nassib Bakari Mmbaga kwa utendaji kazi usioridhisha.
Share:

ATUPWA JELA MIAKA 4 KWA KUMCHAPA VIBOKO KARANI WA SENSA




Amos Nyang'waji

Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Amos Nyang'waji (25), mkazi wa Kijiji cha Matui wilayani Kiteto mkoani Manyara, amehukumiwa kwenda jela miaka minne kwa kosa la kumcharaza viboko Karani wa Sensa na kuharibu kishikwambi chake wakati akitekeleza majukumu yake.


Hukumu hiyo imetolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Kiteto, na Hakimu Mosi Sasy, ambapo awali akisoma mashtaka hayo, Mwendesha Mashtaka ya Polisi Joseph Kijo, amesema Agosti 25, 2022, katika Kijiji hicho cha Matui wilayani Kiteto mtuhumiwa Amosi Nyang'wali akiwa nyumbani kwa kaka yake alimpiga Karani wa Sensa aliyefahamika kwa jina la Cecilia Paulo.

Alipotakiwa kujitetea mtuhumiwa huyo alisema yeye ana tatizo la akili lililomfanya atende kosa hilo ambapo Hakimu Sasy alisema, kwa kawaida kosa la kwanza la shambulio la mwili anapaswa kwenda jela miaka mitano na kosa la pili la kuharibu mali ni jela miaka saba lakini baada ya kuiomba Mahakama impunguzie adhabu aliamriwa kwenda jela miaka 4 na faini laki 7 na fidia laki 5

Hakimu Sasy amesema adhabu hiyo iwe fundisho kwa wengine wenye tabia ya kukwamisha kazi za serikali na hata kuharibu mali ya serikali ambayo inatumia kodi ya wananchi kuwahudumia.

CHANZO - EATV
Share:

BENKI YA NBC, KOLA PRODUCTS WATOA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA VIJANA WA DON BOSCO

Na Mwandishi Wetu - Malunde 1 blog

Benki ya Taifa ya Biashara ya NBC kwa kushirikiana na Kola Products wametoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana wa Wasalesia wa Don Bosco wanaotoka mikoa saba ya Tanzania.

Elimu hiyo imetolewa leo Jumanne Agosti 30,2022 wakati wa Kongamano la Vijana wa Wasalesia wa Don Bosco (Salesian Youth Movement - SYM) lililofanyika katika shule ya Don Bosco Didia mkoani Shinyanga ambalo limehudhuriwa na vijana Wanaotoka mikoa ya Shinyanga, Dodoma, Arusha , Kilimanjaro, Morogoro, Dar es Salaam na Iringa pamoja na wawakilishi kutoka Kenya ambako nyumba za Don Bosco zinapatikana.

Meneja wa Benki ya NBC tawi la Shinyanga Joyce Chagonja amewaomba vijana hao kuchangamkia fursa ya mikopo yenye gharama nafuu kutoka kwenye benki yao ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kuingiizia mapato serikali.


Naye Meneja Biashara wa Benki ya NBC Fedrick Rutta amewasihi vijana hao kuhakikisha wanakwenda kufanya kwa vitendo mafunzo ya ujasiriamali waliyopewa ili kuweza kujipatia kipato na hatimaye kuweza kuajiri watu wengine ili kutatua changamoto ya ajira.

Akifundisha kwa vitendo juu ya utengenezaji wa sabuni za maji, Mkurugenzi wa Kola Products , Josephine Charles amewasihi vijana hao wachangamkie fursa ya utengenezaji sabuni kwa sababu ni rahisi kuitengeneza, mtaji ni mdogo naa soko ni rahisi kupatikana.

Mkuu wa shule ya Sekondari Don Bosco Didia Fr. Felix Wagi ameishukuru Benki ya NBC na Kola Products kwa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana hao.


Aidha amesema kongamano hilo hufanyika kila baada ya Miaka 2 kwa lengo la kuwaleta vijana hao wa madhehebu mbalimbali ya kikristo pia waislamu kuweza kujifunza mambo yanayohusu Maisha, wito, uchumi na hali ya Utandawazi.


"Kongamano hili ambalo mara zote hufanyika kwa siku tano, huratibiwa na kufadhiliwa na shirika la Don Bosco wakisaidiana na wadau mbalimbali pia michango ya ushiriki kutoka kwa vijana.Mwaka huu kongamano hili limefanyika mkoa wa Shinyanga katika shule ya Don Bosco Didia na kuhudhuriwa na Vijana 285 na walezi wao", amesema Fr. Wagi.
Meneja wa Benki ya NBC tawi la Shinyanga Joyce Chagonja akizungumza wakati wa Kongamano la Vijana wa Wasalesia wa Don Bosco (Salesian Youth Movement - SYM) lililofanyika katika shule ya Don Bosco Didia mkoani Shinyanga. Wa kwanza kushoto ni Afisa Mauzo wa Benki ya NBC Patrick Mashenene akifuatiwa na Meneja Biashara wa Benki ya NBC Fedrick Rutta
Meneja wa Benki ya NBC tawi la Shinyanga Joyce Chagonja akizungumza wakati wa Kongamano la Vijana wa Wasalesia wa Don Bosco (Salesian Youth Movement - SYM) lililofanyika katika shule ya Don Bosco Didia mkoani Shinyanga.
Meneja Biashara wa Benki ya NBC Fedrick Rutta akizungumza wakati wa Kongamano la Vijana wa Wasalesia wa Don Bosco (Salesian Youth Movement - SYM) lililofanyika katika shule ya Don Bosco Didia mkoani Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kola Products , Josephine Charles akizungumza wakati wa Kongamano la Vijana wa Wasalesia wa Don Bosco (Salesian Youth Movement - SYM) lililofanyika katika shule ya Don Bosco Didia mkoani Shinyanga.
Mkuu wa shule ya Sekondari Don Bosco Didia Fr. Felix Wagi akizungumza wakati wa Kongamano la Vijana wa Wasalesia wa Don Bosco (Salesian Youth Movement - SYM) lililofanyika katika shule ya Don Bosco Didia mkoani Shinyanga 
Kongamano la Vijana wa Wasalesia wa Don Bosco (Salesian Youth Movement - SYM) likiendelea

Kongamano la Vijana wa Wasalesia wa Don Bosco (Salesian Youth Movement - SYM) likiendelea

Mkurugenzi wa Kola Products , Josephine Charles (kulia) akifundisha kwa vitendo juu ya utengenezaji wa sabuni za maji. 
Mkurugenzi wa Kola Products , Josephine Charles (kulia) akifundisha kwa vitendo juu ya utengenezaji wa sabuni za maji.
Mkurugenzi wa Kola Products , Josephine Charles (kulia) akifundisha kwa vitendo juu ya utengenezaji wa sabuni za maji.
Vijana wakitengeneza sabuni za maji.
Vijana wakitengeneza sabuni za maji.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger