Tuesday, 2 August 2022

RAIS WA MAREKANI JOE BIDEN ATOA KAULI NZITO JUU YA KIFO CHA KIONGOZI WA KUNDI LA KIGAIDI LA AL QAEDA


Ayman al- Zawahiri akiwa na aliyekuwa Kiongozi wa kundi la Al-Qaeda Osama Bin Laden
Ayman al-Zawahiri aliyekuwa kiongozi wa kundi la lkigaidi la Al- Qaeda

***
RAIS wa Marekani Joe Biden amelihutubia Taifa hilo na kutoa kauli nzito juu ya kifo cha kiongozi wa kundi la kigaidi la Al Qaeda Ayman al-Zawahiri, aliyeuawa na ndege ya Marekani isiyokuwa na Rubani.

Rais Biden amesema kuwa kifo cha al- Zawahiri ni malipo ya unyama alioufanya kwa wananchi wa Taifa hilo kufuatia kuhusika katika utekelezaji wa shambuliola kigaidi la Septemba 11 mwaka 2001 ambalo liliua zaidi ya raia 3000 nchini humo.

Rais wa Marekani Joe Biden

“Kiongozi wa ugaidi hayupo tena.” Alinukuliwa akisema Rais Biden ambaye aliendelea kwa kusisitiza kuwa kifo cha gaidi huyo kinarudisha tena faraja kwa familia za wahanga wa shambulio la Septemba 11.

Rais huyo wa Marekani amesisitiza kuwa Afghanistan haitakuwa tena makazi ya ugaidi baada ya shambulio hilo kutekelezwa ikiwa ni mwaka mmoja tangu vikosi vya Marekani vindoke nchini humo.

Aidha kiongozi huyo wa kundi la kigaidi ambaye ana asili ya Misri aliuawa majira ya asubuhi wakati akiwa katika nyumba yake kwenye mji wa Kabul ambapo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Rais Biden ni kwamba hakuna mtu mwingine yeyote yule kutoka katika familia ya al- Zawahiri aliyeathirika au kujeruhiwa katika shambulio hilo.


Al-Zawahiri aliuawa vipi?

Maafisa wa Marekani wamesema Zawahiri alikuwa amesimama kwenye veranda ya nyumba yake ya mafichoni. Ghafla, ndege isiyokuwa na rubani- inayofahamika kama drone- ikadondosha makombora mawili.


Taarifa inasema kuwa kombora lilimpiga Zawahiri ambaye alikuwa amesimama nyumbani kwake.


Ndugu wengine wa familia ya Ayman Al-Zawahiri walikuwepo pamoja naye katika eneo hilo, lakini hakuna mtu mwingine aliyeuawa wala kujeruhiwa katika shambulio hilo, na kiongozi wa Al-Qaeda akafa mara moja pale peke yake, maafisa walisema.
Share:

BIMA YA KILIMO YA NBC YAWAVUTIA WADAU WA KILIMO MAONESHO YA NANENANE MBEYA


Mkurugenzi wa Wateja wadogo wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke (Kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Benki Kuu Tanzania tawi la Mbeya Bw Ibrahimu Malogoi alipotembelea banda la maonesho ya kilimo la benki ya NBC inayoshiriki Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.


Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo, Lariba na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa (kulia) akibadilishana mawazo na wadau wa kilimo waliotembelea banda la maonesho ya kilimo la benki hiyo inayoshiriki Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.


Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Mbeya Bi Asia Mselemu (kulia) akibadilishana mawazo na wadau wa kilimo waliotembelea banda la maonesho ya kilimo la benki hiyo inayoshiriki Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.


Maofisa wa benki ya NBC wakitoa ufafanuzi kuhusu huduma zinazotolewa na benki hiyo kwa wadau mbalimbali waliotembelea banda la maonesho ya kilimo la benki hiyo inayoshiriki Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.


Timu ya maofisa wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa Wateja wadogo wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke (wa tano kulia), Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo, Lariba na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa (wa tano kushoto) na Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Mbeya Bi Asia Mselemu (wan ne kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye banda la maonesho ya kilimo la benki hiyo inayoshiriki Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.

.....................................

Na Mwandishi Wetu-Mbeya

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeendelea kung’ara kwenye Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya, huku huduma ya Bima ya Kilimo inayotolewa na benki hiyo kwa wakulima ikiwa ni moja ya vivutio vikubwa miongoni mwa washiriki wanaotembelea maonesho hayo.

Akizungumza kwenye maonesho hayo yaliyozinduliwa jana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango, Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo, Lariba na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa alisema ushiriki wa benki hiyo kwenye maonesho hayo ni muendelezo wa jitihada zake za kuendelea kujiweka karibu zaidi na wadau wa sekta hiyo muhimu.

“Kupitia Maonesho haya tunapata fursa ya kutangaza huduma zetu zinazohusiana na sekta nzima ya kilimo pamoja na kupokea mrejesho wa huduma hizo kutoka kwa wakulima.’’

Alisema ushiriki wa benki hiyo kwenye sekta ya kilimo unahusisha mkakati mkubwa wa benki hiyo unaolenga kuinua sekta ya kilimo nchini unaofahamika kama ‘NBC Shambani’ unaohusisha mnyororo wote wa sekta ya kilimo kuanzia kwa mkulima, mchakataji wa mazao ya kilimo hadi msambazaji.

“Zaidi pia tunalenga kuhakikisha tunashirikiana vema na serikali katika kutimiza adhma ya msingi kabisa ya kuhakikisha tunaongeza kwa kasi ukuaji wa sekta ya kilimo nchini ikiwa ni sambamba na kuboresha maisha ya wakulima wenyewe,’’ alibainisha.

Akizungumzia baadhi ya huduma zinazotolewa na benki hiyo mahususi kwa wakulima Bw Urassa aliitaja huduma ya Bima kwa wakulima inayotolewa na benki hiyo kwa kushirikiana na kampuni ya Bima ya Jubilee Insurance inayolenga kuwalinda wakulima, wavuvi na wafugaji nchini dhidi ya hasara pindi wanapopata majanga mbalimbali yanayoweza kuathiri uzalishaji wao.

“Benki ya NBC tuinatambua vema sekta ya kilimo na zaidi tunatambua mchango wa wa wakulima katika uchangiaji wa uchumi wa nchi na kwa msingi huu tumeona ni vema kuja na Bima ya mazao kwa wakulima. Katika kuthibitisha ufanisi wa huduma hii, ni hivi karibuni tu kwa kushirikiana na wenzetu kampuni ya Bima ya Jubilee Insurance tuliwafidia wakulima wa tumbaku mkoani Tabora ambao mazao yao yaliathiriwa na hali ya hewa,’’ alibainisha.

Zaidi, aliongeza kuwa benki hiyo pia inawawezesha wakulima kwa kuwapatia pembejeo za kilimo kwenye baadhi ya mazao hususani yale ya kimkakati ikiwemo pamba, kahawa na tumbaku lengo likiwa ni kuongeza tija kwenye sekta hiyo muhimu.

“Kupitia mpango wetu wa NBC Shambani tumekuwa tukishirikiana na wadau mbalimbali katika kutoa mikopo mbalimbali kwa wakulima ikiwemo ya zana mbalimbali za kilimo ikiwemo matrekta na mashine nyingine nyingi,’’ alitaja huku akiwaomba wadau mbalimbali wa kilimo waliohudhuria maonesho hayo kutembelea banda la benki hiyo ili kupata ufafanuzi na huduma mbalimbali zinazohusiana na sekta hiyo.
Share:

RAIS WA ZAMBIA MHE.HAKAINDE HICHILEMA AWASILI NCHINI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal one Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya siku moja nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema wakati Nyimbo za Taifa (Tanzania na Zambia) zikipigwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal one Jijini Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal one Jijini Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema wakati wakisalimiana na viongozi mbalimbali waliofika kwenye mapokezi katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal one Jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema wakati wakiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za asili na matarumbeta vilivyokuwa vikitoa burudani wakati wa mapokezi katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal one Jijini Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal one Jijini Dar es Salaam.

PICHA NA IKULU
Share:

HALMASHAURI 100 ZAKUSANYA MAPATO YA NDANI KWA 100%

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe Innocent Bashungwa akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa kuhusu Mapato na Matumizi ya Ndani ya Halmashauri kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 leo Agosti 2,2022 Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe Innocent Bashungwa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa kuhusu Mapato na Matumizi ya Ndani ya Halmashauri kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 leo Agosti 2,2022 Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu mpya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Prof. Riziki Shemdoe akizungumza na wakuu wa Mikoa pamoja na Makatiibu Tawala wa Mkoa wakati wakitoa taarifa kuhusu Mapato na Matumizi ya Ndani ya Halmashauri kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 leo Agosti 2, 2022 Jijini Dar es Salaam Wakuu wa Mikoa wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe Innocent Bashungwa wakati akitoa taarifa kuhusu Mapato na Matumizi ya Ndani ya Halmashauri kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 leo Agosti 2, 2022 Jijini Dar es Salaam Wakuu wa Mikoa wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe Innocent Bashungwa wakati akitoa taarifa kuhusu Mapato na Matumizi ya Ndani ya Halmashauri kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 leo Agosti 2, 2022 Jijini Dar es Salaam

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

****************************

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe Innocent Bashungwa amesema katika mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri 100 zimekusanya mapato ya ndani kwa asilimia 100 au zaidi ya lengo la mwaka.

 Ameyasema hayo leo Agosti 2 , 2022 Jijini Dar-es-Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu Mapato na Matumizi ya Ndani ya Halmashauri kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022.

Bashungwa amesema, Halmashauri 78 zimekusanya kati ya asilimia 80 hadi asilimia 99, na Halmashauri 7 zimekusanya kati ya asilimia 58 hadi 79. Halmashauri zilizofikia malengo ya mwaka zimeongezeka kutoka Halmashauri 57 katika mwaka wa fedha 2020/21, hadi kufikia Halmashauri 100 katika mwaka wa fedha 2021/22.


Amefafanua kuwa ulinganisho wa ufanisi wa ukusanyaji wa mapato ya ndani, kwa kigezo cha asilimia ya makusanyo, unaonesha kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha imeongoza katika Halmashauri zote kwa kukusanya asilimia 247 ya makisio yake ya mwaka, ikifuatiwa na Halmashauri za Wilaya ya Mlele asilimia 185, na Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro asilimia 158.


Vilevile, Waziri Bashungwa amesema , Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli imekuwa ya mwisho kwa kukusanya asilimia 58 ya makisio yake ya mwaka, ikifuatiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe asilimia 67, na Halmashauri ya Wilaya ya Bunda asilimia 70 ya makisio yake ya mwaka.

Ameendelea kusema kuwa katika kuzipima Halmashauri zote kwa Kigezo cha wingi wa mapato (pato ghafi), jumla ya Halmashauri 35 zimekusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 5. Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekusanya mapato mengi zaidi kuliko Halmashauri zote, kwa kukusanya Shilingi Bilioni 75.3 ikifuatiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Shilingi Bilioni 47.3, na Halmashauri ya jiji la Dodoma Shilingi Bilioni 45.1.


Bashungwa amesema, Halmashauri 4 zimekusanya chini ya Shilingi Bilioni 1 ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli imekua ya mwisho kwa kukusanya Shilingi Milioni 599.7, ikifuatiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Shilingi Milioni 692.1, Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Shilingi Milioni 792.3, na Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Shilingi Milioni 880.2.

Aidha, Halmashauri 4 zilizokusanya chini ya shilingi bilioni 1 zimeonekana kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato. na haakuna Halmashauri iliyokusanya chini ya asilimia 50 kwa miaka yote miwili mfululizo
Share:

PAKUA APP YA MALUNDE 1 BLOG...Imeboreshwa zaidi

Share:

Monday, 1 August 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE AGOSTI 2,2022













Share:

WASIOJULIKANA WAMUUA MUUZA DUKA BAADA YA KUNUNUA PIPI NA SODA SHINYANGA

Picha haihusiani na habari hapa chini

Mwanamke aliyetambulika kwa jina la Kabula Ngasa mwenye umri wa miaka 60, mkazi wa kijiji cha Nyida Kata ya Nyida katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga , ameuawa na watu wasiojulikana kwa kukatwa panga sehemu mbalimbali za mwili wake.

Mwenyekiti wa kijiji cha Nyida Kidoto Maganga ameiambia Redio Faraja kuwa, tukio hilo limetokea majira ya saa tatu usiku wa kuamkia leo Jumatatu Agosti 1,2022, wakati Marehemu akiwa nyumbani kwake katika kijiji hicho.

Taarifa zaidi zinabainisha kuwa, watu waliofanya mauaji hayo walikuwa ni wawili ambao walifika nyumbani kwa Marehemu mapema na kujifanya wateja katika kibanda chake cha bidhaa ndogo ndogo kilichopo hatua chache kutoka kwenye nyumba yake ambapo mwanzoni waliagiza Pipi na baadaye Soda na kuhudumiwa.

Baada ya dakika chache kupita walimtuma mjukuu wake anayesoma darasa la nne aliyekuwa naye kibandani kuwafuatia maji ya kunywa ndani, ambapo baada ya kurudi na maji walimpiga kwa ubapa wa panga hali iliyosababisha aanguke chini.

Alipoamka alikimbia kwa Mama yake ambaye anaishi jirani na kumweleza kinachoendelea, lakini inaelezwa kuwa Mama wa mtoto huyo aliogopa kutoka nje kwa vile Mume wake hakuwepo na hivyo watu hao wakatumia mwanya huo kumshambulia marehemu kwa Panga sehemu mbalimbali za mwili wake mpaka alipofariki dunia.

Diwani wa kata ya Nyida Selemani Seregeti , amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo huku kamanda wa Polisi wa mkoa wa Shinyanga George Kyando akibanisha kuwa,bado hajapata taarifa za tukio hilo kwa sababu yuko nje ya ofisi kikazi.

CHANZO - RADIO FARAJA BLOG

Share:

NYUKI WAVAMIA SHULE, WAJERUHI WALIMU NA WANAFUNZI


Picha haihusiani na habari hapa chini

KUNDI la nyuki ambalo halikujulikana limetokea wapi limezua taharuki baada ya kuvamia Shule ya Msingi ya Kamena Wilaya ya Liwale mkoani Lindi na kujeruhi walimu na wanafunzi.

Taarifa kutoka wilayani humo na kuthibitishwa na mmoja wa walimu wa shule hiyo, Rehema Mwaitenda, zinaeleza tukio hilo lilitokea saa nane mchana, Julai 26, mwaka huu.

Mwaitenda alisema siku ya tukio, yeye na walimu wenzake wakiwa wanaendelea na majukumu yao ya kikazi, kundi hilo la nyuki lilivamia shuleni hapo na kuwashambulia walimu na wanafunzi.


Alisema katika uvamizi huo, wanafunzi wanane pamoja na walimu wawili walikimbizwa Hospitali ya Wilaya mjini Liwale na kupatiwa matibabu baada ya kung’atwa na nyuki hao.

Chanzo - Nipashe
Share:

MWENGE WA UHURU WAMULIKA MRADI WA MAJI NYAMILANGANO UNAOTEKELEZWA NA RUWASA KAHAMA


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, akikata Utepe kwenye Mradi wa Majisafi na salama wa Nyamilangano Halmashauri ya Ushetu ambao unatekelezwa na RUWASA.

Na Marco Maduhu, USHETU

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, ameweka jiwe la Msingi katika Mradi wa Majisafi na salama Katika kijji cha Ididi Kata ya Nyamilangano Ushetu wilayani Kahama ambao utaondoa adha ya ukosefu wa maji kwa wananchi.



Mradi huo wa Maji umewekewa Jiwe hilo la Msingi Julai 31,2022 na Mwenge wa Uhuru, huku wananchi wakionyesha furaha ya kupata mradi huo wa Majisafi na salama, ambao unatekelezwa na Wakala wa Majisafi na usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) wenye thamani ya Sh.milioni 350.

Akizugumza wakati wa uwekaji wa jiwe hilo la Msingi Kiongozi huyo wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, amesema mradi huo wa Maji una manufaa makubwa kwa wananchi, kuwaondolea adha ya ukosefu wa Maji na kuagiza ukamilishwe kwa wakati.

"Mradi huu wa maji ni mzuri tumeukagua ila naagiza ukamilishwe kwa wakati, ili wananchi wapate huduma ya Maji haraka na kutekeleza dhamira ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan ya kumtua ndoo kichwani Mwanamke," amesema Geraruma.

Naye Meneja Wakala wa Majisafi na usafi wa Mazingira RUWASA wilayani Kahama Magili Maduhu, amesema mradi huo wa Maji ni wa Kisima kirefu na utekelezaji wake kwa sasa ni asilimia 85 na unatarajiwa kukamilika mwaka huu na utanufaisha wananchi 5,296.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani, amesema mradi huo wa maji ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa wananchi wa Nyamilangano na vijiji jirani na kuwataka wananchi wautunze mradi huo.

Pia amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan katika mwaka wa fedha (2022-2023) ametoa kiasi cha fedha Sh.bilioni 1.8 kwa ajili ya kukamilisha miradi yote ya Maji ambayo ipo Halmashauri ya Ushetu.

Nao baadhi ya wananchi wa Nyamilangano akiwamo Sophia Boniphace ,wameishukuru Serikali kwa kutekeleza mradi huo wa Majisafi na salama ambao umewaondolea changamoto pia ya Mgogoro ya kifamilia sababu ya kufuata Maji umbali mrefu.

Aidha, Mwenge huo wa Uhuru leo umekabidhiwa mkoani Tabora.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma akizungumza wakati akiweka jiwe la Msingi kwenye Mradi wa Maji wa Nyamilangano Halmashauri ya Ushetu ambao umetekelezwa na RUWASA.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani akizungumza kwenye mradi huo wa Maji.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, akizungumza kwenye mradi huo wa Maji.
Meneja wa RUWASA wilayani Kahama Mhandisi Magili Maduhu, akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mradi huo wa Maji.
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Juliety Payovela, akitetea jambo na mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, akiweka jiwe la Msingi kwenye Mradi wa Maji wa Nyamilangano Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama ambao unatekelezwa na RUWASA.
Tenki la kuhifadhia Maji kwenye Mradi wa Maji wa Nyamilangano Halmshauri ya Ushetu.

Mwenge wa Uhuru ukiwa kwenye Mradi wa Maji wa Nyamilangano Halmashauri ya Ushetu.

Share:

MAFURIKO YAUA WATU 10

Watu kumi wamepoteza maisha nchini Uganda kufuatia mafuriko makubwa mashariki kwa taifa hilo la ukanda wa Afrika Mashariki, shirika la Msalaba Mwekundu lilisema Jumapili.

Mvua kubwa ilisababisha mito kufurika na maji kusambaa hadi katika maboma ya watu na barabara huku Red Cross ikielezea uwezekano wa idadi ya maafa kuongezeka.

 Waliofariki ni waathiriwa wa mvua kubwa iliyohushudiwa usiku wa Jumamosi katika wilaya za Kapchorwa na Mbale. Video zinaonyesha wakaazi waliojawa na hofu wakikimbilia usalama wao huku viwango vya maji vikiongezeka katika kijiji kimoja na kuangusha nyumba na migomba ya ndizi.

Kwa mujibu wa kamishna wa Mbale Ahamada Waashaki, mwanajeshi ni mmoja wa watu waliongamizwa na mafuriko hayo. 

"Watu wengi hawajulikani waliko na wanahofiwa kuaga dunia. Kuna uharibifu mkubwa. Barabara zimezibwa, nyumba kumezwa kwa sababu ya mvua kubwa iliyoanza usiku wa jana (Jumamosi) hadi asubuhi hii (Jumapili)," Ahamada Waashaki aliambia shirika la habari la AFP.

 Waziri Mkuu Robinah Nabbanja alitembelea Mbale, eneo ambalo linapatikana takriban kilomita 300 mashariki mwa jiji kuu la Kampala.

 "Polisi na wanajeshi wa majini watafika kusaidia katika uokoaji na kutafta miili ya walioaga dunia tunapotoa msaada kwa wale walioathirika," ofisi ya waziri mkuu ilisema. 

AFP inaripoti kuwa wanahabari wawili waliiambia kuwa waliona miili ikielea katika maji hayo yaliyojaa matope kabla ya kuopolewa na polisi. Magari kadhaa pia yalisombwa pamoja na vitu vya nyumbani wakaazi wakikimbilia maeneo ya juu kwa usalama wao.
Share:

MFUNGWA ATOROKA POLISI UCHI AKIOGA

Polisi jijini Nairobi wanamsaka mfungwa mwenye umri wa miaka 19, ambaye alitoroka katika Kituo cha Polisi cha Viwandani.

Katika kisa hicho cha Jumatano, Julai 27, Erickson Khata aliomba ruhusa ya kuoga na afisa aliyekuwa kwenye zamu alimsindikiza kuchota maji na kuoga.

Hata hivyo, Khata alitumia fursa hiyo kutoroka baada ya afisa aliyekuwa amemsimamia kujinafasi ili kumpa faragha. DCI inasema kuwa mfungwa huyo alitoroka akiwa amevalia suruali ya ndani pekee yake, na kuacha nyuma nguo zake zote.

"Afisa huyo alishuku kuwa kila kitu kilikuwa si sawa baada ya mtungi wa maji ya kumwagika kusimama ghafla, na kufuatiwa na kimya cha kishindo. Alipokwenda kuangalia, alikumbana na beseni la maji yaliyopakwa nusu, kipande cha sabuni na nguo za mfungwa, bila mfungwa kuonekana,” wapelelezi walieleza.

Khata alikuwa amezuiliwa katika gereza la mgao wa ulinzi wa juu jijini Nairobi baada ya kulalamika kuwa yeye ni mtoto mdogo.

Ni hadi alipopelekwa katika Hospitali ya Mbagathi, mnamo Julai 26, ambapo vipimo vilifanywa na kuthibitishwa umri wake ulikuwa wa miaka 19. 

Kesi hiyo ilitakiwa kutajwa mahakamani siku aliyotoweka bila kujulikana aliko.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger