Sunday, 27 March 2022

RAIS SAMIA ARIDHIA VIJIJI 67 MAENEO YA HIFADHI KUBAKI MOROGORO

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na viongozi pamoja na watendaji wa mkoa wa Morogoro wakati wa ziara ya Mawaziri wa Kisekta kupeleka mrejesho wa Uamuzi wa Baraza la Mawaziri juu ya utatuzi wa wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 tarehe 26 Machi 2022.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Merry Masanja akizungumza katika kikao baina ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta na uongozi wa mkoa wa Morogoro wakati wa ziara ya Kamati hiyo kutoa Mrejesho wa Uamuzi wa Baraza la Mawaziri kuhusu utatuzi wa wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 tarehe 26 Machi 2022. .

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Allan Kijazi akichangia hoja katika kikao baina ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta na uongozi wa mkoa wa Morogoro wakati wa ziara ya Kamati kupeleka mrejesho wa Uamuzi wa Baraza la Mawaziri juu ya utatuzi wa wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 tarehe 26 Machi 2022. .

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Martine Shigella akizungumza katika kikao baina ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta na uongozi wa mkoa wa Morogoro wakati wa ziara ya Kamati kupeleka mrejesho wa Uamuzi wa Baraza la Mawaziri juu ya utatuzi wa wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 tarehe 26 Machi 2022. .

Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Morogoro Frank Minzikunte akichangia hoja kwenye kikao baina ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta na uongozi wa mkoa wa Morogoro wakati wa ziara ya Kamati kupeleka mrejesho wa Uamuzi wa Baraza la Mawaziri juu ya utatuzi wa wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 tarehe 26 Machi 2022.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mvomero mkoani Morogoro Yusufu Makunja akichangia hoja katika kikao baina ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta na uongozi wa mkoa wa Morogoro wakati wa ziara ya Kamati kupeleka mrejesho wa Uamuzi wa Baraza la Mawaziri juu ya utatuzi wa wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 tarehe 26 Machi 2022.

***********************

Na Munir Shemweta, WANMM MOROGORO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameridhia vijiji 67 vilivyokuwemo maeneo ya hifadhi katika mkoa wa Morogoro kubaki ili kuwawezesha wananchi wake kuendelea na shughuli zao bila matatizo.

Hatua hiyo ya Rais Samia ni juhudi za za Serikali ya Awamu ya Sita kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975.

Kamati ya Mawaziri wa Kisekta inayoongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula iko katika ziara ya kutembelea mikoa mbalimbali ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji mapendekezo ya Baraza la Mawaziri kuhusu utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji na mitaa 975.

Baadhi ya Mapendekezo hayo ni kubakisha vijiji na vitongoji 366 vilivyomo ndani ya hifadhi, kubainisha maeneo ya hifadhi yaliyopoteza sifa ili kugawiwa kwa wananchi na kuhakiki pamoja na kurekebisha mipaka kati ya hifadhi za misitu, wanyama na makazi.

Pia yapo mapendekezo ya kumega baadhi ya hifadhi na kugawia wafugaji na wakulima, kufanya mapitio ya sheria zinazohusiana na matumizi ya ardhi, kupitia upya sheria ya vyanzo vya maji inayozungumzia mita 60 na kufutwa kwa mashamba yasiyoendelezwa.

Akizungumza na uongozi na watendaji wa mkoa wa Morogoro kuhusiana na migogoro ya matumizi ya ardhi katika mkoa huo mwishoni mwa wiki, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alisema mkoa huo unahusisha vijiji 81 kati ya 975 yenye migogoro ya matumizi ya ardhi.

‘’Katika kutafuta suluhu ya migogoro ya matumizi ya ardhi kwenye mkoa huu, viijiji 67 vitabaki katika maeneo yake na vijiji/mitaa 14 vitafanyiwa tathmini’’ alisema Dkt Mabula.

Moja ya eneo lenye mgogoro wa matumizi ya ardhi mkoani Morogoro ni Bonde la Mto Kilombero linalohusisha Pori Tengefu na Hifadhi ya Misitu inayochangia maji kwenye Mto Rufiji unaotumika pia kupeleka maji kwenye mradi wa kimkakati wa Bwawa la Mwl Nyerere.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, pamoja na maamuzi hayo ya serikali kila taasisi itakuwa na jukumu la kuhakikisha inalinda maeneo yake ya ardhi ili yasiweze kuvamiwa tena na wananchi.

Aidha, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alitoa maagizo kwa Watendaji wa Serikali kuhakikisha taratibu zinafuatwa katika kusimamia utekelezaji wa maamuzi yanayotolewa na serikali kwa kuwa kutosimamiwa vyema kwa maamuzi hayo kumechangia kwa kiasi kikubwa uwepo migogoro ya matumizi ya ardhi kwenye maeneo mbalimbali.

Alionya wananchi wenye tabia ya kuvamia mashamba yanayofutwa na serikali na kuzitaka mamlaka za upangaji ambazo ni halmashauri kuhakikisha maeneo hayo yanapangiwa ile mipango wa matumizi ya ardhi kabla ya kuanza kutumika.

‘’Pale ambapo serikali imefuta mashamba, mashamba hayo lazima yarudi kwenye mikono ya halmashauri ili mpango wa matumizi uweze kuandaliwa’’ alisema Dkt Mabula.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Merry Masanja mbali na kuwapongeza wakuu wa wilaya kwa kazi kubwa wanayoifanya katika wilaya zao alisema bado kuna changamoto katika usimamizi wa maeneo hasa yale ya hifadhi.

‘’Kuna changamoto nyingi zinazosababishwa na watendaji wa serikali hasa katika maeneo ya hifadhi hapa morogoro kuna vijiji 46 vimesajiliwa ndani ya maeneo ya hifadhi’’ alisema Merry Masanja.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Hamis Chillo alieleza umuhimu wa kutolewa elimu kwa wananchi kuhusiana na masuala ya hifadhi na kusisitiza kuwa busara lazima itumike katika kutekeleza maamuzi yanayotolewa na serikali.

‘’Watu wanahitaji kupata elimu ya uhifadhi na wakiipata taaluma katika masuala hayo basi utekelezaji maamuzi ya serikali itakuwa rahisi kutekelezwa, busara lazima itumike’’ alisema Chillo.
Share:

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA TAWA KWA KUSIMAMIA VIZURI MIRADI YA MAENDELEO PORI LA AKIBA SWAGASWAGA


KAMATI ya Kudumu ya Bunge,Ardhi,Maliasili na Utalii wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Pori la akiba la Swagaswaga,Joseph Reuben kabla ya kuanza kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Pori la Akiba la Swagaswaga lililopo katika wilaya za Chemba na Kondoa.


KAMATI ya Kudumu ya Bunge,Ardhi,Maliasili na Utalii wakiedelea kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Pori la Akiba la Swagaswaga lililopo katika wilaya za Chemba na Kondoa.


KAMATI ya Kudumu ya Bunge,Ardhi,Maliasili na Utalii wakimsikiliza Mkandarasi Johannes Nyamasiriri wakati wakikagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Pori la Akiba la Swagaswaga lililopo katika wilaya za Chemba na Kondoa.


KAMATI ya Kudumu ya Bunge,Ardhi,Maliasili na Utalii wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Pori la akiba la Swagaswaga,Joseph Reuben wakati wakikagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Pori la Akiba la Swagaswaga lililopo katika wilaya za Chemba na Kondoa.


KAMATI ya Kudumu ya Bunge,Ardhi,Maliasili na Utalii wakikagua kisima cha maji kinatumia na wananchi waliopo karibu na Pori la Akiba Swagaswaga wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Pori la Akiba la Swagaswaga lililopo katika wilaya za Chemba na Kondoa.


MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge,Ardhi,Maliasili na Utalii Mhe.Ally Makoa,akiipogeza TAWA kwa usimamizi mzuri wa matumizi ya fedha mara baada ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Pori la Akiba la Swagaswaga lililopo katika wilaya za Chemba na Kondoa.


MAKAMU Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge,Ardhi,Maliasili na Utalii Mhe.Shaban Shekilindi akizungumza mara baada ya kukagua na kujionea maendeleo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Pori la Akiba la Swagaswaga lililopo katika wilaya za Chemba na Kondoa.


MKURUGENZI wa Idara ya Wanyamapori Dk.Maurus Msuha,akiipongeza Kamati hiyo kwa kutembelea na kujionea maendeleo ya miradi mbalimbali katika Pori la Akiba Swagaswaga lililopo wilaya za Chemba na Kondoa.


KAIMU Kamishna wa Uhifadhi katika Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Mabula Nyanda,akieleza majukumu yanayotekelezwa na TAWA wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge,Ardhi,Maliasili na Utalii ya kukagua na kujionea miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Pori la Akiba la Swagaswaga lililopo katika wilaya za Chemba na Kondoa.


Meneja wa Pori la akiba la Swagaswaga,Joseph Reuben,akitoa taarifa ya utedaji kazi ya Pori la Akiba Swagaswaga kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge,Ardhi,Maliasili na Utalii ilipofanya ziara ya kukagua na kujionea miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Pori la Akiba la Swagaswaga lililopo katika wilaya za Chemba na Kondoa.


KAMANDA wa Uhifadhi Pori la Akiba Mkungunero Khadija Malongo,akiiomba kamati hiyo iweze kutembelea Pori la Mkungunero wakati wa ziara ya kukagua na kujionea miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Pori la Akiba la Swagaswaga lililopo katika wilaya za Chemba na Kondoa.


SEHEMU ya watumishi wa TAWA,Waandishi na waheshimiwa wabunge wakifatilia hotuba mbalimbali.


KAMATI ya Kudumu ya Bunge,Ardhi,Maliasili na Utalii wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa TAWA mara baada ya kumaliza ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Pori la Akiba la Swagaswaga lililopo katika wilaya za Chemba na Kondoa.

................................................

Na Alex Sonna-KONDOA

KAMATI ya Kudumu ya Bunge,Ardhi,Maliasili na Utalii imeipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa kusimamia vizuri ujenzi wa miradi ya maendeleo katika Pori la Akiba la Swagaswaga lililopo katika wilaya za Chemba na Kondoa .

Miradi ambayo imekaguliwa na kamati hiyo ni Ujenzi wa Ofisi, ujenzi wa nyumba za watumishi, kisima kinachotumia pampu za kisasa pamoja na ujenzi wa nyumba za kulala wageni 'Hostel' yote ikigharimu kiasi cha shilingi billioni 1.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miradi hiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Ally Makoa amesema wameridhishwa na matumizi ya fedha zilitolewa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza miradi hiyo.

“Tunamshukuru Rais kwa kuleta fedha nyingi katika Wizara za Ardhi na ile ya Maliasili na Utalii naipongeza Wizara ya Maliasili kwa kuzisimamia vizuri fedha hizo.Niwatakie kila la heri na mwambie Waziri (Dkt Damas Ndumbaro) Kamati imeridhishwa na kazi na tukiingia katika bajeti tutaendelea kumshawishi mheshimiwa Rais (Samia Suluhu Hassan) aongeze fedha,”amesema.

Aidha,Makoa ambaye ni Mbunge wa Kondoa Mjini amesema kuna maeneo machache katika Mkoa wa Dodoma ambayo yakiwekezwa nguvu yanaweza kunyayuka kiutalii likiwemo pori la Swagaswaga na Mkungunero.

Vilevile,Mwenyekiti huyo ameitaka Wizara hiyo kusimamia fedha ambazo zinatolewa na Rais Samia ili awe na imani na kuweza kuongeza fungu lingine.

“Tukifanya vizuri ndio atatuletea fedha zaidi lakini kama kutakuwa na ‘mazongezonge’ kwenye fedha anazoleta wakati mwingine hataongeza tunatarajia fedha yoyote itakayoletwa itatumika kisawasawa,”amesema.

Aidha ameipongeza TAWA kwa kuwa na mahusiano mazuri na jamii ambazo zipo pembezoni mwa mapori ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za maji katika vijiji.

Kwa upande wake,Kaimu Kamishna wa Uhifadhi kutoka TAWA,Mabula Nyanda Amesema utekelezaji wa mradi huo utasaidia Mamlaka kutimiza lengo la kuongeza idadi ya watalii na mapato yatokanayo na utalii kama ilivyoanishwa katika ilani ya CCM.

“Tunaishukuru Serikali kwa kuendelea kutatua migogoro kati ya hifadhi na wananchi ambayo imesaidia kuboresha mahusiano baina ya pande hizi mbili,”amesema.

Naye,Meneja wa Pori la akiba la Swagaswaga,Joseph Reuben amesema katika kuhakikisha migogoro kati ya wananchi na wahifadhi inapungua wameendelea kutoa elimu ya uhifadhi kwa wananchi wa vijiji vinavyopakana na hifadhi.

Amesema kwa kipindi cha Julai 2017 hadi Desemba 2021 wamefanikiwa kuelimisha jumla ya wananchi 4604 katika vijiji 18 ambapo amedai elimu hiyo imetolewa kwa kushirikiana na Afisa Wanyamapori na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa Wilaya za Chemba na Kondoa.
Share:

Saturday, 26 March 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MACHI 27,2022

Share:

HOPES FOR THE BASKETBALL SPORT REVIVED AS SUPER GROUP-OWNED BETWAY CONTINUES TO RENOVATE FACILITIES


Betway, a leading international online betting and gaming brand, has renovated and launched another basketball facility at the Leaders Club Grounds in Dar es Salaam. The launch that took place on Saturday, 26 March 2022, is the continuation of the Super Group-owned brand’s sports facilities renovation pilot project that aims at renovating five basketball facilities in Dar es Salaam.


Through the project, Betway renovates basketball facilities in strategic public sports and recreational centres with a view of adding value to the basketball sport in the country. To make sure the renovated facilities are properly maintained for sustainable use, Betway has collaborated with the Tanzania Basketball Federation (TBF), the government body responsible for the administration of basketball in the country. TBF plays a significant role in making sure the facilities are meaningfully utilised for basketball competitions and other related sports activities.

A variety of sports and networking activities that brought together over 250 individuals and stakeholders from the basketball sport industry accompanied the inaugural events. The main event of the bonanza was a basketball match between two female teams, Dar Queens and Dar Divas, for a TSh 500,000 reward. Betway prioritised women as part of the annual 8 March celebration of Women's Day.


Speaking to the attendees of the launch event, Betway Tanzania’s Marketing Manager, Calvin Mhina, highlighted key improvements covered by Betway.

"We took the responsibility to upgrade this (Leaders Club) court looking at the value it will add to the game since it is one of the most famous sports and recreational centers in Dar es Salaam. At Betway, we believe in community development as part of our core responsibilities and we will keep supporting the sports community in all aspects of sports development,” said Mhina.


Mwenze Kabinda, the TBF’s secretary-general, commended the move by Betway as he admitted that the upgrade of the court will add great value to the game.

“For us (TBF) who are responsible for the development of the sport, it excites us to see stakeholders such as Betway invest in improving infrastructures which are key to guaranteeing the development of any sport. We are thankful for the project and this brings a challenge to us as a responsible authority to come up with more tournaments to make sure the courts are in use,” commented Mwenze.

Basketballers, fans, and stakeholders who took part in the bonanza had a great time watching the game and taking part in the other amusing events. Players shared their delight about the court modifications they saw and experienced during the launch game.


About the Betway Group

Betway is part of Super Group: the global digital company which provides first class entertainment to the worldwide betting and gaming community.

Super Group (SGHC) Limited is the holding company for leading global online sports betting and gaming businesses: Betway, a premier online sports betting brand, and Spin, a multi-brand online casino offering. Listed on the New York Stock Exchange (NYSE ticker: SGHC), the group is licensed in over 20 jurisdictions, with leading positions in key markets throughout Europe, the Americas and Africa. The group’s successful sports betting and online gaming offerings are underpinned by its scale and leading technology, enabling fast and effective entry into new markets. Its proprietary marketing and data analytics engine empowers it to responsibly provide a unique and personalized customer experience. For more information, visit www.sghc.com


Betway Group is a leading provider of innovative and exciting entertainment across sports betting, casino and esports betting. Launched in 2006, the company operates across a number of regulated online markets. Betway prides itself on providing its customers with a bespoke, fun and informed betting experience, supported by a safe, secure, fair and responsible environment.

Betway is a member of several prominent industry-related bodies, including International Betting Integrity Association (IBIA), iGaming European Network (iGEN), the Independent Betting Adjudication Service (IBAS), Sports Wagering Integrity Monitoring Association (SWIMA) and the Betting and Gaming Council (BGC), and is ISO 27001 certified through the trusted international testing agency eCOGRA. Betway Tanzania, powered by Media Bay Limited is Licensed and regulated by the Ministry of Finance and Planning Gaming Board of Tanzania.

For more information about Betway please visit: www.betway.co.tz
Share:

WACHAWI WA UKRAINE WATANGAZA KUMROGA RAIS WA URUSI



Vifaa vya kichawi
**
Kwa mjibu wa shirika la habari la UNIAN likiinukuu taarifa ya duka la Witch Cauldron lililopo mjini Kiev, limesema wachawi wa Ukraine wanakusudia kufanya matambiko matatu yatakayomuondoa madarakani Rais wa Urusi Vladimir Putin.

"Mnamo Machi 31, siku ya 29 ya mwezi, siku ya rushwa na laana, sisi, wachawi wa Ukraine kwa kushirikiana na washirika wa kigeni, tutafanya ibada ya kumwadhibu adui wetu - Vladimir Putin," wachawi hao walichapisha kwenye akaunti yao ya Instagram.

Wachawi hao wamesema tambiko hilo litafanywa kwa awamu tatu; ya kwanza itafanyika Ukraine katika Mlima wa Bald nje ya Kiev, hadi sasa, baadhi ya wachawi 13 wameonyesha nia ya kushiriki katika mpango huo.

Tambiko la pili litafanyika "Avic" Ibada hiyo inatarajiwa kuhitimishwa kwa kuunda "gunia la jiwe" kwa rais wa Urusi, ambaye atakabiliwa na kutengwa, kuondolewa madarakani na kupoteza uungwaji mkono ndani ya watu anao waongoza.

Hata hivyo, wachawi hao hawakutaja ni lini hasa tambiko hilo litaanza, shirika la utangazaji la Urusi lilisema katika taarifa yake mapema Ijumaa kuwa mipango ya wachawi tayari imekosa nguvu kwa kuingia dosari.
Share:

URUSI YATHIBITISHA WANAJESHI WAKE 1,351 KUUAWA UKRAINE


Wizara ya ulinzi ya Urusi imetoa taarifa kuhusu vifo va wanajeshi wake pamoja na majeruhi – kwa mara ya pili tu – ikidai kuwa wanajeshi wake 1,351 wameuawa na wengine 3,825 kujeruhiwa, shirika la habari la Ria Novosti linaripoti.

Vyanzo vya kijeshi vya Ukraine vimekadiria kuwa wanajeshi 15,000 wa Urusi wameuawa, ingawa idadi hiyo inaweza kujumuisha majeruhi pamoja na vifo. Idara ya ujasusi ya Marekani imesema huenda wanajeshi wa Urusi waliouawa katika vita hiyo ni zaidi ya nusu ya idadi hiyo inayodaiwa na Ukraine.

Taarifa ya kwanza kutoka wizara ya ulinzi ya Urusi kuhusu majeruhi ilikuwa tarehe 2 Machi, na ilisema kuwa wanajeshi 498 waliuawa tangu uvamizi huo ulioingia mwezi wa pili sasa.

Gazeti la Komsomolskaya Pravda (KP) lilichapisha makala mtandaoni iliyonukuu wizara ya ulinzi ikisema wanajeshi 9,861 wa Urusi waliuawa katika mzozo huo.

Baadaye, sehemu ya makala hiyo iliondolewa na mhariri wa KP aliiambia BBC kuwa taarifa hizo zilitokana na udukuzi.
Share:

UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI YA TaSUBa

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MACHI 26,2022

Magazetini leo Jumamosi March 26,2022




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger