Saturday, 5 March 2022

RAIS SAMIA AKUTANA NA MBOWE IKULU.....WAKUBALIANA KUFANYA SIASA ZA KISTAARABU NA KIUNGWANA

 






Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe alipowasili Ikulu Jijini Dar Es salaam leo tarehe 04 March 2022 .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe alipowasili Ikulu Jijini Dar Es salaam leo tarehe 04 March 2022




Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MACHI 5,2022






Share:

Friday, 4 March 2022

KAMPUNI ILIYOPEWA ZABUNI YA KISAMBAZA MABOMBA UJENZI WA MIRADI YA MAJI KANDA YA ZIWA YATAHADHARISHWA

Wizara ya Maji imeitaka Kampuni iliyopewa zabuni ya kusambaza mabomba kwenye ujenzi wa miradi ya maji Kanda ya Ziwa inayotekelezwa na Serikali kupitia fedha za Uviko 19, kuhakikisha inafikisha mabomba hayo kwa wakati kwenye maeneo ya miradi, ili kuepuka kukwamisha miradi hiyo na hatimaye lengo la Serikali la kuwafikishia wananchi maji safi na salama liweze kufikiwa.


Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi ametoa rai hiyo wakati akikagua mradi wa maji wa Bunamala Mbugani wilayani Itilima mkoani Simiyu na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo.

Amesema katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uviko 19, ni lazima wananchi wahakikishiwe upatikanaji wa maji safi na salama ambayo yatawasaidia kujikinga na maradhi hayo.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA MACHI 4,2022

Magazetini leo Ijumaa March 4 2022
Mabilionea wa Dubai wavutiwa na Sekta ya Gesi
Share:

Thursday, 3 March 2022

UMOJA WA MATAIFA WAITAKA URUSI KUSIMAMISHA MARA MOJA MASHAMBULIZI NCHINI UKRAINE



Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) limepiga kura kwa wingi ya kuunga mkono azimio la kuitaka Urusi kusimamisha mara moja mashambulizi nchini Ukraine na kuyaondoa majeshi yake yote nchini humo.

Mataifa mengi wanachama wa umoja huo yameonyesha kuliunga mkono azimio hilo. Kura hiyo iliyoitwa “uvamizi dhidi ya Ukraine” ilipigwa katika kikao cha dharura cha baraza hilo. Kwenye kura hiyo mataifa 141 yaliunga mkono azimio hilo, na kupingwa na mataifa matano, na 35 hayakuwepo kwenye mchakato wa kupiga kura.


Urusi iliungwa mkono na Belarus, Syria, Korea Kaskazini na Eritrea, dalili inayoashiria namna taifa hilo lilivyotengwa kimataifa kufuatia uvamizi huo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliwaambia waandishi wa habari baada ya kura hiyo kwamba ujumbe wa UNGA uko wazi na ni dhahiri kwamba Urusi inatakiwa kusimamisha mashambulizi Ukraine mara moja na kufungua milango ya mazungumzo na diplomasia.

Balozi wa Cuba ambayo haikuwepo kupiga kura Pedro Luis Cuesta amelaumu kuhusu mzozo huo akisema umechochewa na matamanio ya Marekani ya kupanua jumuiya ya NATO eneo la mashariki na kuelekea kwenye mipaka ya Urusi pamoja na kupeleka silaha za kisasa nchini Ukraine huku ikipuuza wasiwasi wa Urusi juu ya usalama wake.

Kabla ya kura hiyo, balozi wa Ukraine kwenye umoja huo Sergiy Kyslytsya alisema vikosi vya Urusi vimeingia kwenye ardhi ya Ukraine sio tu kuwaua baadhi ya watu lakini pia kuchukua haki ya Ukraine ya kuendelea kuwepo na kuongeza kuwa uhalifu ni wa kutisha mno.

Maandishi yanayomaanisha “inusuru Ukraine” huko Bulgaria kama moja ya njia ya kupeleka ujumbe wa kupinga taifa hilo kuvamiwa.


Balozi wa Urusi, Vassily Nebenzia yeye aliuomba umoja huo kulikataa azimio hilo akidai mataifa ya magharibi yaliongeza shinikizo lisilo kifani sambamba na vitisho vya wazi ili kuungwa mkono. Azimio hilo pia limelaaini uhusika wa Belarus kwamba ilitumia nguvu dhidi ya Ukraine.

Na huko Jerusalem, kansela wa Ujerumani Olaf Cholz pamoja na waziri mkuu wa Israel Naftali Bennet jana walisisitizia wajibu wao katika kuhakikisha kunafanyika mazungumzo ya amani kati ya Urusi na Ukraine.


Scholz alithibitisha wajibu wa Ujerumani kwa usalama wa Israel akisema tayari taifa lake lilishaweka wazi kuhusu hilo na kuongeza kuwa kwa pamoja na Israel walikuwa na nia ya dhati kushirikiana ili kuhakikisha mazungumzo zaidi ya amani kati ya Urusi na Ukraine, huku Bennet akisema wanawajibika pia kuzuia umwagikaji wa damu.

Nchini Ufaransa, rais Emmanuel Macron amesema Ulaya imeingia kwenye enzi mpya baada ya Urusi kuivamia Ukraine. Amesema katika hotuba yake kupitia televisheni kwamba kutokana na hali hiyo wanalazimika kufanya maamuzi na kurudia mwito kwa Ulaya kusimamia usalama wake badala ya kutegemea wengine. Macron aidha amelimwagia sifa jeshi la Ukraine lakini akionya kwamba siku zijazo huenda zikawa ngumu zaidi.


Mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich atangaza kuiuza klabu hiyo na kupeleka fedha kwa wahanga wa vita, Ukraine

Mjini The Hague, mahakama ya kimataifa ya makosa ya uhalifu ICC imetangaza kuanzisha uchunguzi rasmi wa wa uhalifu wa kivita unaofanyika dhidi ya watu wa Ukraine. Mwendesha mashitaka mkuu wa ICC Karim Khan amesema tayari ameifahamisha ofisi ya rais wa ICC kuhusu hatua yake ya kuendeleza uchunguzi na tayari wameanza kukusanya vithibitisho. Ikumbukwe tu kwamba Urusi haijasaini Mkataba wa Rome ulioanzisha mahakama hiyo.


Huko Uingereza, mmiliki wa klabu ya klabu ya Premier ya Chelsea Roman Abramovich ameamua kuiweka mauzoni timu hiyo na kuahidi fedha zitakazopatikana atazitoa kwa wahanga wa vita nchini Ukraine.

Kulingana na ofisi ya haki za binaadamu ya Umoja wa Mataifa, watu 227 wamekufa na 525 kujeruhiwa hadi usiku wa kuamkia jana nchini Ukraine.
Share:

BABA AMUUA MTOTO WAKE KWA SHOKA AKIGOMBANA NA MKEWE




Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia mwanaume aitwaye Anderson Clemence (35), mkazi wa kijiji cha Kafunjo, Kata ya Kamagambo wilayani Karagwe kwa tuhuma za kumuua mtoto wake Hansen Anderson, mwenye umri wa miezi minne kwa shoka.


Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Wankyo Nyigesa, amesema kuwa baba huyo alikamatwa Machi 01, 2022 na kwamba chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi baina yake na mke wake.

Amesema kuwa wakati wakigombana mtuhumiwa alirusha shoka ili kumpiga mke wake na badala yake likampiga mtoto huyo aliyekuwa amebebwa mgongoni na mama yake mzazi.
Share:

NAIBU WAZIRI MARYPRISCA : MIRADI YA MAJI FEDHA ZA UVIKO-19, IKAMILIKE KWA WAKATI


Naibu Waziri wa Maji MaryPrisca Mahundi, akizungumza kwenye mradi wa maji Mkula, mara baada ya kukagua mradi wa Maji Badugu wilayani Busega mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Maji Maryprisca Mahundi, akitembelea mradi wa maji Nyakabindi, kushoto ni mkuu wa wilaya ya Bariadi Lupakisyo Kapange, pamoja na Mwenyekiti wa Halshauri ya mji wa Bariadi David Masanja (mwenye shati jeupe) ambaye pia ni diwani wa kata ya Nyakabindi, kulia ni Mtendaji wa kata ya Nyakabindi

Na COSTANTINE MATHIAS, Busega.

Naibu Waziri wa Maji Maryprisca Mahundi amewaagiza Mameneja wa Wilaya wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) nchi nzima, kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa kwa fedha za Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi Uviko-19 inakamilika kabla ya mwezi Juni mwaka huu.

Amesema kuwa hakutakuwa na nafasi ya maelezo wala kuongeza muda kwa Meneja yeyote ambaye atashindwa kukamilisha miradi hiyo kwa muda muafaka, ambapo ameagiza miradi yote inatakiwa kukamilika mwezi Mei mwaka huu.

Naibu Waziri huyo ametoa maagizo hayo leo (jana) Mkoani Simiyu, ambapo akiwa Wilayani Busega amemtaka meneja wa Ruwasa wilayani humo anayetekeleza miradi miwili ya Uviko -19 kuhakikisha inakamilika kwa muda.

Amesema kuwa miradi yote ya Uviko-19 mbali na kukamilika ujenzi wake, inatakiwa kutoa maji na wananchi wanaanza kutumia na siyo kukamilika kwa kujengwa tu bali inatakiwa kabla ya muda huo ianze kutoa maji.

Amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameleta fedha hizo kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa Uviko, ambapo moja ya njia za mapambano ni wananchi kunawa mikono kwa maji safi na tiririka.


“Kunawa maji safi na tiririka ni lazima kila radi ukamilike ujenzi wake kwa asilimia 100 na siyo kukamilika alafu tunaambiwa kuna kitu fulani hakijakamilika, hapana …tunataka maji yatoke na wananchi waanze kutumia,” amesema Mahundi

“Kwenye hii miradi kama Wizara hatuna Excuse (msamaha) kwa Meneje yeyote wa Wilaya, wala hatuna muda wa ziada kwa ambaye mradi utashindwa kukamilika kwa muda, tunataka miradi ikamilike kabla ya mwezi wa tano na itoe maji kwa wananchi,” ameongeza Naibu Waziri.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji ndani ya Wilaya Busega Meneja wa RUWASA Wilaya hiyo Mhandisi Samson Gagala amesema kuwa walipokea zaidi ya Sh. Milioni 450 fedha za Uviko -19 kwa ajili ya kutekeleza miradi miwili ya maji.


Mhandisi Gagala amesema kuwa miradi hiyo inatekelezwa katika vijiji vya Badugu na Kalemela ambapo ujenzi wake kwa miradi yote miwili umefikia kiwango cha asilimia 25.

“ Kukamilika kwa miradi hii yote miwili itahudumia zaidi ya wananchi 8000, lakini katika Wilaya tunayo mingine ambayo inajengwa kwa fedha za lipa kulingana na matokeo (P4R) zaidi ya Sh. Milioni 900.'' amesema.

Kwa upande wake Meneja Miradi kutoka Jonta Investment Ltd anayetekeleza mradi wa Badugu, Mhandisi Juma Bangula amesema ujenzi wa miundombinu yote utakamilika mwezi huu na kwamba wanatarajia bomba zitafika mwishoni mwa mwezi wa pili.

Ameahidi kuwa watatekeleza mradi huo kwa wakati kwa kuzingatia mkataba na kwamba wananchi pamoja na serikali watarajie kuapata maji kwa wakati.

Musa Ernest mkazi wa Badugu amesema upatikanaji wa maji katika kijiji hicho ni shida na kwamba kukamilika mradi huo utatatua kero ya maji kijijini hapo.


Share:

AMUUA BABA YAKE AKIMTUHUMU KUMROGA



Mkazi wa Kijiji cha Upungu Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Jacob Mlela (88) ameuawa kwa kukatwa na shoka kichwani, shingoni na mikononi na mtoto wake Michael Jacob kwa kile kinachotajwa kuwa ni imani za kishirikina.

Akizungumza na waandishi wa habari Jumatano Machi 2,2022 Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema kuwa tukio hilo limetokea juzi saa moja jioni katika eneo hilo, ambapo marehemu alishambuliwa akiwa nje ya nyumba yake na kukimbizwa hospitali ya Ndalla na kufariki dunia.

Amesema chanzo cha mauaji hayo ni imani za kishirikina, kwani mtuhumiwa ana tatizo la kuanguka kifafa na amekuwa akiamini kuwa baba yake ndio chanzo cha yeye kuugua ugonjwa huo.

"Mtoto anaugua ugonjwa wa kifafa ambao anaamini baba yake ndiyo chanzo cha yeye kuugua na kuchukua maamuzi hayo," amesema.

Mbali na baba yake, mtuhumiwa pia alimjeruhi ndugu yake, Magdalena Jacob ambaye kwa sasa anaendelea vizuri akiwa anapata matibabu.

Kamanda Abwao ametoa wito kwa wananchi mkoa wa Tabora kutoendekeza imani za kishirikina na wanapokuwa wanaumwa waende kuwaona wataalamu katika Vituo vya kutokea huduma.


CHANZO: Mwananchi
Share:

WATENDAJI RUWASA SIMIYU WACHAFUANA WAKISAKA MADARAKA,NAIBU WAZIRI AWAONYA

 

Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi amewaonya watendaji wa Mamlaka ya Maji Vijini, (RUWASA)  katika Halmashauri ya Wilaya ya Busega mkoani Simiyu, akiwataka kuacha mara moja tabia ya kuchafuana kwa lengo la kusaka madaraka na badala yake wafanye kazi kwa pamoja kuhakikisha miradi ya maji inayotekelezwa na Serikali kwenye maeneo yao inakamilika kwa wakati na wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama.

Mhandisi Maryprisca Mahundi ametoa onyo hilo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mkula wilayani Busega wakati akikagua mradi wa maji wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni mbili unaotekelezwa na Serikali kwa ajili ya kuhdumia wananchi wa vijiji vitano vya eneo hilo.

Amewataka watendaji hao kuanza kufanya kazi kwa pamoja ili kuleta tija na kudai kuwa tabia ya kuchafuana itasababisha halmashauri hiyo kuwapoteza  viongozi wenye uwezo wa kuwasaidia wananchi kupata maji…

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger