Thursday, 24 February 2022

MKAZI WA MTONGANI ASHINDA MILIONI 10 ZA BIKO

Meneja wa Bank ya CRDB Tawi la Palm Beach Primier jijini Dar es Salaam, Pendo Kitula kulia akishirikiana na balozi wa Biko Kajala Masanja kushoto kumkabidhi mshindi wao wa biko Ahmad Ally Mbwana jumla ya sh milioni 10 alizoshinda kutoka kwenye droo kubwa zinazofanyika kila Jumapili. Picha na Mpigapicha Wetu.
Balozi wa Biko Kajala Masanja kushoto akifurahia jambo na mshindi wake Ahmad Ally Mbwana aliyeshinda sh milioni 10 za bahati nasibu ya Biko na kukabidhiwa jana kwenye Bank ya CRDB, Tawi la Palm Beach Primier, jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa Biko wa sh milioni 10, Ahmad Ally Mbwana, akionesha tabasamu pana baada ya kuibuka kidedea kwenye droo kubwa ya biko iliyofanyika Jumapili. Picha na Mpiga picha wetu.


Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mkazi wa Mtoni Mtongani, wilayani Temeke, mkoani Dar es Salaam, Ahmad Ally Mbwana, ameibuka Milionea wa biko baada ya kushinda sh milioni 10 za droo kubwa inayofanyika kila Jumapili kwa kucheza live kwa kuingia www.biko.co.tz au kwa namba ya Kampuni ya 505050 na kumbukumbu namba 2456.


Biko ni mchezo unaochezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi unachezwa kwa kufanya miamala kuanzia sh 1000 na kuendelea ambapo Watanzania wamekuwa kuanzia sh 2500 hadi Milioni 5 papo kwa hapo pamoja na droo kubwa za kila Jumapili.


Mbali na wanaocheza kwa kupitia www.biko.co.tz, pia wanaotumia simu za kawaida nao wataendelea kucheza kama zamani kwa kutumia namba ya Kampuni 505050 na kumbukumbu namba 2456 na wote kujishindia kuanzia sh 2500 hadi milioni tano papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa zinazofanyika kila Jumapili.
Share:

WATUMISHI SITA WAFUKUZWA KAZI HALMASHAURI YA SHINYANGA


Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngasa Mboje akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Februari 23,2022. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngasa Mboje akizungumza kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Nice Munissy. Wa Kwanza kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Dkt. Christina Mzava akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Isaack Sengelema.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga limewafukuza kazi Watumishi Sita kutokana na makosa mbalimbali ya kiutumishi.

Uamuzi huo umetangazwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngasa Mboje wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Februari 23,2022.

Mboje amesema Baraza la Madiwani limewafukuza watumishi hao baada ya kupitia utetezi wao na baadhi yao hawajaonekana kutokana na kutokuwepo kwenye maeneo yao ya kazi.

“Baraza la Madiwani limewafukuza kazi watumishi sita wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, kutoka Idara ya Afya watumishi wawili wamefukuzwa kazi na kutoka Idara ya Utawala waliofukuzwa kazi ni wanne”,amesema Mboje.

Mbali na watumishi hao sita kufukuzwa kazi, pia watumishi wengine wawili Baraza hilo limeagiza wakatwe asilimia 15 ya mishahara yao na watafanya hivyo kwa muda wa miaka mitatu.

Watumishi Idara ya Afya waliofukuzwa kazi ni Daktari Fidelis Benedict Mushi wa Kituo cha afya Nindo na Andrew Israel Mwakisambwe ambaye ni Mteknolojia Maabara Kituo cha Afya Salawe.

Watumishi wanne kutoka Idara ya Utawala waliofukuzwa kazi ni Maafisa Watendaji wa Vijiji ambao Charles Dominick Mayunga (Bukene), Mercy Gasper Kyando (Kilimawe), Omary Hamis Omary (Igembya) na Robert Surika Mbuti (Mwabagehu).

Soma pia : 

HALMASHAURI YA SHINYANGA YAPOKEA SH. MILIONI 900 KUPANGA, KUPIMA NA KULIPA FIDIA VIWANJA



Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI FEBRUARI 24,2022














Share:

DC MBONEKO ATEMBELEA UJENZI MRADI WA RELI YA KISASA SGR

 

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, ametembelea kuona shughuli za maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha Tano kutoka Mwanza hadi Isaka, pamoja na kusikiliza kero za wananchi na wafanyakazi na kuzitafutia ufumbuzi, ambapo ujenzi huo unapita kwenye maeneo mbalimbali wilayani Shinyanga.


Mboneko amefanya ziara hiyo leo Februari 23,2022, akiwa ameambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya, pamoja na Naibu Meneja wa mradi wa Reli ya kisasa Mhandisi Alex Bunzu kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC), ambao ndiyo wasimamizi wa mradi huo ambao unatekelezwa na Wakandarasi kutoka China.

Akizungumza kwenye ujenzi huo wa mradi wa Reli ya kisasa,Mboneko ameagiza vijana ambao wanatoka kwenye maeneo husika mradi ambapo unapopita wapatiwe ajira, na siyo kupewa vijana kutoka maeneo mengine.

“Mradi huu wa ujenzi wa Reli ya kisasa ujenzi unachukua muda wa miaka mitatu kukamilika, hivyo tunataka wananchi wa maeneo husika ambao wanapitiwa na mradi huu wanufaike nao ikiwamo  vijana kupata ajira, na siyo kupewa ajira vijana kutoka maeneo mengine na wakati eneo hilo la mradi kuna vijana wengi na hawana ajira,”alisema Mboneko.

“Na nyie vijana ambao mmepata ajira kwenye mradi huu wa Reli ya kisasa hasa madereva acheni wizi, sababu kumekuwa na wimbi kubwa sana la wizi wa mafuta, huko ni kuhujumu mradi huu, na ninatoa onyo la mwisho mkiiba tena mafuta tunafukuza kazi madereva wote,”aliongeza.

Alisema pia Madereva wanapokuwa wakiiba mafuta hayo na kuwauzia wananchi na kutunza ndani ya nyumba zao ni kutengeneza janga jingine, ambalo linaweza kusababisha maaafa makubwa kwa wananchi kulipukiwa na mafuta hayo.

Aidha Mboneko, aliagiza  wananchi ambao bado hawajalipwa Fidia waliopisha maeneo yao kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo wa Reli ya kisasa walipwe wote pesa zao, na kuwatoa wasiwasi wananchi kuwa hakuna ambaye hatalipwa pesa yake ya Fidia bali wote watalipwa, huku akiwataka pesa hizo wazitumie kwa maendeleo ikiwamo kujenga nyumba bora.

Katika hatua nyingine Mboneko aliagiza suala la mikataba mibovu ya wafanyakazi litafutiwe ufumbuzi wa haraka, pamoja na upewaji wa chakula bora na cha uhakikisha ili kutodhoofisha Afya za wafanyakazi.

Pia aliagiza ujenzi wa nyumba za makazi kwa ajili ya wafanyakazi wa Mradi huo wa Reli ya kisasa zijengwe kwa kasi inayotakiwa na kwa kuzingatia ubora, huku akiwataka wanawake ambapo mradi huo unapita wachangamkie fursa ya kuuza vyakula kwenye ujenzi huo na kupata pesa.

Kwa upande wake Naibu Meneja wa mradi huo wa Reli ya kisasa (SGR) Mhandisi Alex Bunzu, alisema maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa wilaya watayafanyia kazi, likiwamo suala hilo la ulipwaji wa Fidia, na upewaji wa mikataba mizuri, huku akibainisha kuwa pia kuna kamati ilishaundwa ambayo itapita kukusanya maoni na malalamiko ya wafanyakazi na kutafutiwa ufumbuzi.

Bunzu aliwataka pia vijana ambao wanafanyakazi kwenye ujenzi huo wa Reli ya kisasa, wawe wazalendo na nchi yao na kuacha tabia ya wizi wa vitu mbalimbali, ambapo kumekuwa na wizi mkubwa sana, huku akisema mradi huo utakamilika 2024 wenye gharama ya Sh.Trilioni 3.062.

 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akisikiliza malalamiko ya wananchi wa kijiji cha Maskati wilayani humo, ambao wanapitiwa na mradi wa Reli ya kisasa (SGR) ambapo walikuwa wakidai hawajalipwa fidia na ukosefu wa ajira kwa vijana wao, na kuahidi kutatua malalamiko yao yote.

Naibu Meneja wa mradi huo wa Reli ya kisasa (SGR) Mhandisi Alex Bunzu, akizungumza kwenye ziara hiyo ya Mkuu wa wilaya na kuahidi changamoto zote zitafanyiwa kazi.

Baadhi ya wafanyakazi katika mradi huo wa Reli ya kisasa, wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko juu ya utatuzi wa malalamiko yao.

 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na Wakandarasi ambao wanatekeleza mradi huo wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha tano, na kuwataka wazingatie maelekezo ya ajira na kufuata sheria za nchi, pamoja na kuongeza kasi ya ujenzi wa mradi huo ili ukamilike kwa wakati.

 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiendelea na ukaguzi wa maendeleo ujenzi wa Reli ya kisasa.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (wapili kushoto) akisikiliza maelezo ya ujenzi wa nyumba za makazi kwa ajili ya wafanyakazi wa Reli hiyo ya kisasa (SGR), ambazo zipo Luhumbo wilayani Shinyanga, akitoa maelezo hayo ni Naibu Meneja wa mradi huo wa Reli ya kisasa (SGR) Mhandisi Alex Bunzu.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kushoto) akiwa na Naibu Meneja wa mradi wa Reli ya kisasa (SGR) Mhandisi Alex Bunzu, akikagua ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa mradi huo wa Reli ya kisasa.

Ukaguzi ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa Reli ya kisasa (SGR) ukiendelea.

Ukaguzi ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa Reli ya kisasa (SGR) ukiendelea.

Ukaguzi ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa Reli ya kisasa (SGR) ukiendelea.

Ukaguzi ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa Reli ya kisasa (SGR) ukiendelea.

Ukaguzi ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa Reli ya kisasa (SGR) ukiendelea.

Ukaguzi ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa Reli ya kisasa (SGR) ukiendelea.

ujenzi wa nyumba hizo ukiendelea.

ujenzi wa nyumba hizo ukiendelea.

ujenzi wa nyumba hizo ukiendelea.

Ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha Tano ukiendelea.

Ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha Tano ukiendelea.

Ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha Tano ukiendelea.

Ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha Tano ukiendelea.

CHANZO - SHINYANGA PRESS CLUB BLOG



Share:

Wednesday, 23 February 2022

ASKARI POLISI AKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA


Polisi wa kike kutoka nchini Jamaica, amekamatwa na dawa za kulevya aina ya Cocaine gramu 1,350 akiwa amezificha sehemu mbalimbali za mwili wake, wakati akijaribu kuingia nazo nchini Marekani.

Polisi huyo, Shelian Cherine Allen mwenye umri wa miaka 42, amekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Fort Lauderdale-Hollywood International Airport, muda mfupi baada ya kuwasili akitokea Montego Bay, Jamaica.

Kwa mujibu wa maafisa wa polisi, mwanamke huyo amekutwa na dawa hizo akiwa amezificha kwenye sehemu zake za siri, kwenye sidiria aliyokuwa amevaa huku pia akiwa amemeza takribani kete 90 tumboni mwake.

Endapo atakutwa na hatia, mwanamke huyo anaweza kuhukumiwa kifungo cha takribani miaka 40 jela.
Share:

WAKULIMA NZEGA WAPO TAYARI KWA UJENZI NA UKARABATI WA MRADI WA UMWAGILIAJI IDUDUMO


Mhandisi Mwinchuma Tengeneza (kulia) akimkabidhi kablasha la eneo la kazi ya Ujenzi na Ukarabati wa miundombinu, katika skimu ya kilimo cha Umwagiliaji Idudumo mwakilishi wa Kampuni ya Ujenzi ya Explicit Main Constructors Ltd Bw. Basil Clement (kushoto).

****

Na Mwandishi wetu - Nzega

Wakulima katika Halmashauri ya mji wa Nzega Mkoani Tabora, wameonesha kuwa tayari na kutoa ushikiano kwa ujenzi na ukarabati wa mradi wa kilimo cha Umwagiliaji Idudumo unaofadhiliwa na Serikali kwa silimia mia.

Wakiongea kwa nyakati tofauti katika makabidhiano ya eneo la kazi katika skimu hiyo, Bw. Pascal Maganga ambaye ni mkulima wa zao la mpunga katika skimu hiyo alisema, ujenzi na ukarabati wa miundombi katika skimu hiyo utasaidia wakulima kulima zaidi ya mara moja katika misimu tofauti ya mvua, tofauti na sasa ambapo ukosekanaji wa miundombinu unapelekea mashamba kujaa maji na kutokulima kwa wakati na kuweza kuleta madhara kwa mazao.

“Naamini kuwa baada ya ujenzi na maboresho haya, kwa heka awali mkulima kama alikuwa anapata gunia thelathini (30) ila baada ya maboresho haya tutavuna zaidi .” Alisee Mkulima hiyo.

Akiongea wakati wa makabithiano hayo, Meneja mradi huo Mhandisi Juma Kibori kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji alisema, eneo la skmu hiyo ya kilimo cha Umwagiliaji yenye ukubwa Hekta 300, na kujikita zaidi katika kilimo cha mpunga lenye chanzo chake cha maji ya Bwawa la Idudumo, lilikuwa likitumia njia za asili na sasa itajengewa mfereji mkubwa wa kupeleka maji mashambani wenye urefu wa mita 1500, vigawa maji sita, makaravati matano na mifereji ya upili yenye urefu wa mita zaidi ya mia sita.



Aliendelea kusema kuwa, awamu hiyo ya kwanza ya ujenzi na ukarabati wa skimu hiyo utakaogharimu zaidi ya shilingi milioni 700, unaotegemea kuchukua miezi nane, utaboresha miundombinu na kusaidia wakulima kuwa na kilimo cha uhakika.

Wa pili kutoka kulia, Meneja Mradi wa Ujenzi na Ukarabati wa Skimu ya Umwagiliaji Idudumo Bw. Juma Kibori akiwaonesha wawakilishi wa viongozi wa Halmashauri ya Nzega mji na wataalam ramani ya ujenzi na ukarabati wa neo la mradi
Sehemu ya eneo la Bwawa Idudumo, ambalo litafanyiwa ukarabati katika awamu nyingine ya mradi.

Share:

CHUO CHA TAIFA CHA UTALII CHAZINDUA MAFUNZO KWA WADAU WA SEKTA YA UTALII RUVUMA


Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii Dkt. Shogo Mlozi Akizugumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku tano ya UVIKO 19 kwa wadau wa Sekta ya Utalii yaliyofanyika Februari 21,2022 Katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Manispaa Mji wa Songea.
Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Steven Ndaki akizungumza alipokuwa akifungua rasmi mafunzo hayo akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge.
Dkt. Naiman Mbise Mratibu wa Mradi wa Mradi Mafunzo kwa watoa huduma katika mnyororo wa Sekta ya Utalii nchini chini ya Mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19, akizungumza wakati wa ufunguzi huo.
Mratibu wa Mafunzo hayo Mkoa wa Ruvuma Elina Makanja akizumzia jinsi walivyojipanga Katika kutoa mafunzo hayo Mkoani humo.
Wadau mbalimbali wa Sekta ya Utalii Mkoa wa Ruvuma wakifuatilia hotuba mbalimbali za ufunguzi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii Dkt. Shogo Mlozi (wa kwanza Kushoto aliyekaa), katibu tawala wa mkoa wa Ruvuma Steven Ndaki (Katikati) na Mratibu wa Mafunzo hayo Mkoa wa Ruvuma Elina Makanja wakiwa kwenye Picha ya pamoja na watumishi wa Chuo cha Taifa cha Utalii.


Na: Mwandishi wetu, SONGEA.

Chuo cha Taifa cha Utalii kimezindua mafunzo ya siku tano ya UVIKO 19 kwa wadau zaidi ya 140 waliopo kwenye mnyororo wa huduma za utalii katika Mkoa wa Ruvuma ili kuwajengea uwezo wa namna ya kujikinga katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo wakati wanapotoa huduma kwa wageni pindi wanapotembelea maeneo yao.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika Februari 21,2022 Katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Mji wa Songea Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii Dkt. Shogo Mlozi Sedoyeka amesema kuwa Mafunzo hao yamefadhiliwa na MPANGO WA TAIFA WA MAENDELEO KWA USTAWI WA TAIFA NA MAKABILIANO DHIDI YA UVIKO 19 kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii.


Dkt. Sedoyeka amesema kuwa Chuo kimeamua kutoa mafunzo hayo kwa wadau wa utoaji wa huduma za Utalii baada ya kubaini kuwa baadhi yao walikuwa bado hawana uelewa wa kutosha kuhusiana na Uviko 19 pindi wanapowahudumia watalii .


Amesema kuwa Chuo kinatoa mafunzo hayo kwa wadau muhimu katika mnyororo wa utalii ili wadau hao waweze kuboresha huduma zao na thamani ya pesa inayotolewa na mgeni au mtalii kuonekana. chuo kinatoa mafunzo hayo kwa watoa huduma hao kwa kuwa wengi wao hawana weledi wa utoaji huduma hasa wakati huu wa janga la UVIKO-19 ili kujikinga wao wenyewe pamoja na wageni wanaopata huduma zao.


Aidha, Dkt. Sedoyeka amesema mafunzo haya kwa mkoa wa Ruvuma yamekuja wakati sahihi ambapo kuna shughuli mbalimbali za utalii wa makumbusho, kupanda milima, fukwe n.k lakini watoa huduma kutokuwa na uelewa mpana na wa kibunifu wa kutoa huduma hizo.


Pia amesema mafunzo yanatolewa katika mikoa nane ikijumuisha Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya, Mara na Mwanza. mbapo mpaka sasa mafunzo yamekamilika mkoa wa Lindi na Mtwara; yanaendelea mkoa wa Ruvuma na Njombe kwa siku tano,na badae kufikia mikoa mingine minne.

Katika hatua nyingine Dkt. Sedoyeka amempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo ambazo zinawezesha kukabiliana na Uviko 19 kwenye jamii pamoja na kwamba mpango huo unanesha nia madhubiti ya Serikali ya awamu ya sita Katika kukabiliana na janga hilo.


Kwa upande wake katibu tawala wa mkoa wa Ruvuma Steven Ndaki ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa huo Brigedia Wilbert Ibuge kwenye uzinduzi huo katika nafasi ya mgeni rasmi amesema kuwa sekta ya utalii imekuwa ikitoa fursa mbalimbali ikiwemo suala la ajira hivyo inatakiwa kuizingatia kikamilifu .


Ndaki amesema kuwa katika kipindi cha janga kubwa la Corona utalii uliyumba katika Nchi mbalimbali hivyo kwa sasa inatakiwa kuitumia elimu ya Uviko 19 ipasavyo ili kulinda watalii na jamii kwa ujumla .


Naye Maajabu Mbogo Afisa Utalii katika pori la Limbaramba ambaye ni mmojawa washiriki wa mafunzo hayo amesema kuwa mafunzo hayo yataleta neema ya kuongezeka kwa watalii na kuifanya Serikali iweze kupata mapato kupitia watalii hao.


Hata hivyo Mbogo amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka fedha za Uviko19 katika Sekta hiyo na kwamba RAIS ameangalia maslahi mapana ya nchi hasa katika kuikomboa Sekta ya Utalii nchini ambao imeathirika na Jana hilo kwa kiasi kikubwa.


Katika mafunzo hayo jumla ya mada Sita zitatolewa wakufunzi mbalimbali kutoka Chuo cha Taifa cha Utalii na mafunzo hayo yatafikia kilele chake ijumaa Februari 25,2022.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger