Wednesday, 23 February 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO FEBRUARI 23,2022


>
Share:

Tuesday, 22 February 2022

TACAIDS, TPSF ZAINGIA MAKUBALIANO KUDHIBITI MAAMBUKIZI YA VVU MAENEO YA KAZI NA KUHIMIZA VYANZO VYA NDANI KUCHANGIA MFUKO WA ATF


Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt. Leonard Maboko akiwa pamoja na Mkurugenzi Idara ya Huduma kwa Wanachama kutoka TPSF, Zachy Mbena wakisaini makubaliano ya ushirikiano kati ya TACAIDS na TPSF yanayolenga ushirikiano katika kudhibiti maambukizi ya VVU, maeneo ya kazi pamoja na kuhimiza vyanzo vya ndani kuchangia mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI (ATF)

Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt. Leonard Maboko akiwa pamoja na Mkurugenzi Idara ya Huduma kwa Wanachama kutoka TPSF, Zachy Mbena wakionesha mkataba wa makubaliano waliosaini unaolenga ushirikiano katika kudhibiti maambukizi ya VVU, maeneo ya kazi pamoja na kuhimiza vyanzo vya ndani kuchangia mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI (ATF) Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt. Leonard Maboko akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano kati ya TACAIDS na TPSF yanayolenga ushirikiano katika kudhibiti maambukizi ya VVU, maeneo ya kazi pamoja na kuhimiza vyanzo vya ndani kuchangia mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI (ATF).Mkurugenzi Idara ya Huduma kwa Wanachama kutoka TPSF, Zachy Mbena akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano kati ya TACAIDS na TPSF yanayolenga ushirikiano katika kudhibiti maambukizi ya VVU, maeneo ya kazi pamoja na kuhimiza vyanzo vya ndani kuchangia mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI (ATF).

Wadau mbalimbali wakifuatilia hafla ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano kati ya TACAIDS na TPSF yanayolenga ushirikiano katika kudhibiti maambukizi ya VVU, maeneo ya kazi pamoja na kuhimiza vyanzo vya ndani kuchangia mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI (ATF).

Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt. Leonard Maboko akiwa pamoja na Mkurugenzi Idara ya Huduma kwa Wanachama kutoka TPSF, Zachy Mbena, mwakilishi wa Shirika la Kazi Duniani(ILO), Bi. Getrude Sima wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano kati ya TACAIDS na TPSF yanayolenga ushirikiano katika kudhibiti maambukizi ya VVU, maeneo ya kazi pamoja na kuhimiza vyanzo vya ndani kuchangia mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI (ATF).

Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt. Leonard Maboko akiwa pamoja na Mkurugenzi Idara ya Huduma kwa Wanachama kutoka TPSF, Zachy Mbena, Mwakilishi wa Shirika la Kazi Duniani(ILO), Bi. Getrude Sima wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano kati ya TACAIDS na TPSF yanayolenga ushirikiano katika kudhibiti maambukizi ya VVU, maeneo ya kazi pamoja na kuhimiza vyanzo vya ndani kuchangia mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI (ATF).

Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt. Leonard Maboko akiwa pamoja na Mkurugenzi Idara ya Huduma kwa Wanachama kutoka TPSF, Zachy Mbena, Mwakilishi wa Shirika la Kazi Duniani(ILO), Bi. Getrude Sima wakipata picha ya pamoja na watumishi wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano kati ya TACAIDS na TPSF yanayolenga ushirikiano katika kudhibiti maambukizi ya VVU, maeneo ya kazi pamoja na kuhimiza vyanzo vya ndani kuchangia mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI (ATF).

Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt. Leonard Maboko akiwa pamoja na Mkurugenzi Idara ya Huduma kwa Wanachama kutoka TPSF, Zachy Mbena, Mwakilishi wa Shirika la Kazi Duniani(ILO), Bi. Getrude Sima wakipata picha ya pamoja Wadau mbalimbali wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano kati ya TACAIDS na TPSF yanayolenga ushirikiano katika kudhibiti maambukizi ya VVU, maeneo ya kazi pamoja na kuhimiza vyanzo vya ndani kuchangia mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI (ATF).

********************

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) imesema bado zinahitajika juhudi kubwa katika kutunisha mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI(ATF) ili kufikia malengo ya kitaifa na kimataifa ya kumaliza UKIMWI ifikapo 2030.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Februari 22, jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt. Leonard Maboko, wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano kati ya TACAIDS na TPSF yanayolenga ushirikiano katika kudhibiti maambukizi ya VVU, maeneo ya kazi pamoja na kuhimiza vyanzo vya ndani kuchangia mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI (ATF).

Dkt. Maboko amesema kuwa kwa sasa asilimia 94 ya fedha ya Mapambano dhidi ya UKIMWI zinatoka kwa wafadhili huku fedha ya ndani ikiwa ni asilimia 6 tu.

"Ni kweli kwamba tunaendelea kutegemea wafadhili kwa kiasi cha asilimia 94, huku sisi tukichangia asilimia 6 pekee, hivyo lazima tufahamu kwamba ipo siku hawa wanaotushika mkono wataacha kutusaidia.

"Hivyo, ni jukumu letu kuangalia ni kwanamna gani tunashirikiana na sekta binafsi katika kutuwezesha kujitegemea kwenye mapambano haya dhidi ya UKIMWI," amesema Dkt. Maboko.

Kuhusu makubaliano hayo yaliyoingia na TPSF Dkt. Maboko amefafanua kuwa yanalenga kushirikiana katika kuhimiza sekta binafsi kuchangia katika mapambano dhidi ya UKIMWI.

“Kama tunavyofahamu kwamba TPSF ndiye muajiri mkubwa wa sekta binafsi kwa amana ya waajiri wote, hivyo makubaliano haya ni kuona ni kwa namna gani tunaweza kushirikiana katika kudhibiti maambukizi ya VVU na UKIMWI katika maeneo ya kazi pia kuhimiza uchangiaji wa fedha kwa vyanzo vya ndani ili kutunisha mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI(ATF).

“Lakini kusaidia kutoa elimu, kwa wafayakazi wao, umma, jamii inayowazunguka na kusaidia kufadhiri miradi mbalimbali ili kuona ni kwa namna gani sekta binafsi inakuwa na mchango kwenye mapambano haya,” amesema Dkt. Maboko.

Ameongeza kuwa pamoja na kwamba wafadhiri wanasaidia fedha za mapambano ya VVU lakini wamekuwa wakipunguza asilimia 5 kila mwaka.

Ameishukuru Kampuni ya Mgodi wa dhahabu ya Geita Gold Mining (GGML) kwa kuwa mstari wa mbele katika mapambano ya VVU kwa muda Mrefu. Amesema kuwa GGM na TACAIDS wamekuwa wakishirikiana kuhamasisha fedha za UKIMWI kupitia zoezi la kupanda mlima Kilimanjaro (kili challange) ambapo fedha zilizokuwa zinapatikana zilikuwa zinatumika katika afua mbalimbali za UKIMWI nchini,ikiwa ni pamoja na kusaidia makundi mbalimbali yaliyoko mkoani Geita

"GGM wamekuwa wakishirikiana na sisi kuhakikisha kuwa tunatokomeza janga hili, hivyo naomba Taasisi nyingine ziweze kuiga mfano huu," amesema Dk. Maboko.

Upande wake Mkurugenzi Idara ya Huduma kwa Wanachama kutoka TPSF, Zachy Mbena, amesema wao kama Sekta binafsi watashirikiana na Serikali kupitia TACAIDS kuhakikisha Mapambano dhidi ya UKIMWI hapa nchini yanasonga mbele.

Amesema miongoni mwa mikakati ni kuhakikisha sekta binafsi inaangalia ni namna gani inaweza kuzalisha ARV nchini ili kupunguza gharama za kuagiza dawa hizi nje ya nchi . "Kama ambavyo tuliweza kushiriki kwenye mapambano ya Uviko-19 basi hata kwenye UKIMWI inawezekana. Kwani tumeshuhudia kwa kiasi kikubwa nchi za Afrika ikiwamo Tanzania zikihimiza kutengeneza chanjo ya Uviko kwenye nchi zao basi hata ARVs inawezekana," amesema Mbena.

Naye mwakilishi wa Shirika la Kazi Duniani(ILO), Bi. Getrude Sima amsema waoa kama Umoja wa Mataifa(UN) walikuwa wakisubiri ushirikiano huo kwa muda mrefu kwani ushirikishwaji wa sekta binafsi ni muhimu zaidi.

"Matarajio yetu nikuona wadau hawa wakikaa kwa pamoja ili kuona ushiriki wao wa moja kwa moja, kwani tumeona mfano wanaweza kununua vifaa vya watu kujipima wenyewe hatua ambayo itakuwa na mchango katika kufikia 90 90 90.

"Pia mnaweza kuandaa hata bonanza mkaleta vipimo watu wakaja wakajipima pale, hivyo niwapongeze sana kwa hiki ambacho mmeanzisha kwani kinafungua uwanja mpana sana katika kukabiliana na Mapambano dhidi ya UKIMWI," amesema.

Upande wake mwakilishi wa Shirikisho la wenye viwanda nchini(CTI), Neema Ngodo amesema kuwa kuna faida nyingi kwa sekta binafsi kushirikishwa kwenye mapambano ya UKIMWI na kwamba jambo la msingi ni kupatiwa taarifa.

"Mtu akijua kwamba badala ya kulipa kodi TRA anaweza kuchangia kwenye mfuko wa UKIMWI (ATF) hili ni jambo zuri na wengi wataliunga mkono, jambo la msingi nikupatiwa Elimu," amesema Neema.
Share:

WIZARA YA ELIMU KWA KUSHIRIKIANA NA CANADA IMETOA KOMPYUTA 300 KWA VYUO VYA UALIMU KUONGEZA UBORA WA ELIMU NCHINI


WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda,akiangalia Kompyuta kabla ya kuzikabidhi kwa wakuu wa vyuo wakati wa hafla ya ugawaji Kompyuta kwa vyuo vya ualimu awamu ya tatu ambapo jumla ya Kompyuta 300 zimetolewa 


Na Dotto Kwilasa,Malunde 1 Blog-DODOMA.
WIZARA ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kwa kushirikina na Serikali ya Canada imedhamiria kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia katika Vyuo vya Ualimu ili kuongeza ubora wa elimu ,pamoja na kuwa na miundombinu rafiki kwa wanafunzi na walimu.

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Jijini Dodoma wakati wa hafla ya ugawaji Kompyuta kwa vyuo vya ualimu awamu ya tatu ambapo jumla ya Kompyuta 300 zimetolewa kupitia ufadhili wa Mradi wa kuendeleza Elimu ya Ualimu nchini (Teacher Education Support Project -TESP) unaogharimu Dola za Canada milioni 53.


Amesema kupitia mradi huo,mazingira ya kufundishia yataboreshwa ikiwa ni pamoja na miundombinu ya kujifunzia katika Vyuo vya Ualimu ili kuongeza ubora wa elimu ,pamoja na kuwa na miundombinu rafiki kwa wanafunzi na walimu hali itakayosaidia kuwepo ufaulu mzuri na kuzalisha walimu wenye ari ya kuendeleza vipaji vyao kwa vizazi vingine.

Amefafanua kuwa jumla ya vyuo 13 vimepata Kompyuta 50 ambapo ,Vyuo 4 kati ya hivyo vimepata Kompyuta 30 na Vyuo 9 Kompyuta 20 na kwamba Vyuo vyote 35 vitapatiwa Kompyuta Mpakato moja kwa ajili ya kusaidia idara zingine vyuoni.

“Leo mtapatiwa Kompyuta za Mezani na Kompyuta Mpakato na Mgao wa kompyuta hizi umezingatia uwiano kati ya wanachuo na vifaa vilivyopo katika Vyuo vyetu kwa sasa,”amesema.

Waziri Mkenda amevitaja Vyuo hivyo vya Ualimu vilivyopatiwa Kompyuta kuwa ni pamoja na Marangu,Kleruu,Vikindu,Patandi,Korogwe,Mpwapwa,Shinyanga,Ilonga,Tarime,Tandala,Butimba,Mtwara na Morogoro.

Amesema dhima ya Vyuo vya Ualimu nchini ni kuandaa walimu mahiri na wanaotosheleza mahitaji katika shule za Awali, Msingi na Sekondari.

“Kutokana na dhima hiyo, Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji katika Vyuo vyote vya Ualimu vya Serikali nchini mkazo ukitolewa katika uboreshaji wa miundombinu, vifaa vya kujifunzia na kufundishia na matumizi ya TEHAMA kama nyenzo muhimu katika ufundishaji na ujifunzaji,"amesema.

Pamoja na hayo ameeleza kuwa Uboreshaji huo utakwenda sawa na maendeleo makubwa katika matumizi ya Sayansi na Teknolojia katika ufundishaji na Ujifunzaji.

Kadhalika amesema Wizara itaendelea na ujenzi na ukarabati wa miundombinu katika Vyuo mbalimbali nchini ikiwemo ukamilishaji wa Chuo cha Kabanga, Ujenzi wa vyuo vipya vya Sumbawanga, Dakawa, Mhonda na Ngorongoro unaendelea na kwamba ukarabati na ujenzi wa baadhi ya miundombinu katika vyuo vya Morogoro, Mpwapwa, Tukuyu, Kasulu, Butimba na Patandi nao unaendeleana huku ukitarajiwa kukamilika mwaka wa fedha 2021/2022.

"Lengo letu ni moja nalo ni kuongeza thamani ya elimu nchini jambo tunalofanya kwa vitendo ambapo hadi sasa Wizara imetoa mafunzo ya matumizi ya Tehama katika kufundishia na kujifunzia kwa wakufunzi wote 2,300 kutoka Vyuo vya Ualimu vya Serikali yote 35,hali hii itasaidia kupunguza uwiano wa matumizi ya kompyuta kwa Wanachuo kutoka Wanachuo 28 kwa Kompyuta moja hadi kufikia Wanachuo 2 kwa Kompyuta 1 vyuoni,”amesema.

Katika hatua nyingine Prof. Mkenda amewaagiza wakuu wa vyuo hao kutunza Kompyuta hizo ambapo amesema zimenunuliwa kwa gharama kubwa hivyo kila Mkuu wa Chuo kuhakikisha kuwa zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ya kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji vyuoni.

Naye,Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga amesema licha ya juhudi zilizopo katika maboresho ya elimu, bado sekta hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa walimu nchini hivyo kunahitajika jitihada ili kuzaliwa walimu wengine wengi kupitia vyuo hivyo.

“Kila mwaka ni lazima tuzalishe walimu wa kutosha,Serikali ni kweli imewekeza ila bado kuna changamoto ya walimu bila walimu hatuwezi kutoka nyinyi ni chemchem ila tunaenda kubadilisha mitaala tutaangalia haya masuala ya teknolojia,”amesema.

Kwa upande wake,Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Prof. Caroline Nombo amesema mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Canada ambapo amedai mchango wa Canada katika mradi huo ni jumla ya Dola za Canada milioni 53.

Amesema mchango wa Serikali ya Tanzania ni katika kugharamia shughuli mbalimbali za uendeshaji wa vyuo ikiwemo gharama za malipo ya chakula kwa wanachuo na mafunzo ya ualimu kwa vitendo.

Prof.Nombo amesema dhumuni kuu la mradi huo ni kuendeleza elimu ya ualimu,kwa kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji kupitia uboreshaji wa miundombinu ya utoaji wa mafunzo ya ualimu katika vyuo vya ualimu vya Serikali 35.

“Utoaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia.Kuimarisha mifumo na miundombinu ya tehama.Kuwaendeleza kitaaluma na kuwajengea uwezo watendaji katika utoaji wa elimu ya ualimu,”amesema.

Amesema hadi kufikia Disemba mwaka 2021 jumla ya Dola za Canada milioni 42 sawa na asilimia 79.25 ya fedha zote za mkataba zilikuwa zimepokelewa kutoka kwa mfadhili wa mradi Globar Affars Canada hadi kufikia Disemba 2021 wastani wa utekelezaji wa malengo ya mradi ulikuwa ni asilimia 75.83.
Share:

BENKI YA CRDB YAWAPA SOMO LA FEDHA WAMACHINGA DAR ES SALAAM


Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi, Stephen Adili akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina ya Elimu ya Fedha kwa Wamachinga iliyoendeshwa na Benki ya CRDB leo tarehe 20/02/2022 katika ukumbi wa PTA Sabasaba. Mafunzo haya yamehudhuriwa na Shirikisho la Umoja wa Wamachinga mkoa wa Dar es salaam (Machinga Saccos) na baadhi ya wawakilishi wa wafanyabiashara hao kutoka Mikoa yote Tanzania ikiwa ni mwendelezo wa ushirikiano tulionao kati ya Benki yetu na wafanyabiashara wadogo (Wamachinga).
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki, Badru Idd akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina ya Elimu ya Fedha kwa Shirikisho la Umoja wa Wamachinga mkoa wa Dar es salaam lililoendeshwa na Benki ya CRDB leo tarehe 20/02/2022 katika ukumbi wa PTA Sabasaba, Dar es salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Umoja wa Wamachinga mkoa wa Dar es salaam, Steven Lusinde akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina ya Elimu ya Fedha kwa Shirikisho la Wamachinga mkoa wa Dar es salaam lililoendeshwa na Benki ya CRDB leo tarehe 20/02/2022 katika ukumbi wa PTA Sabasaba, Dar es salaam.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger