Tuesday, 22 February 2022
Monday, 21 February 2022
NABII JOSHUA ASHINDA KWA KISHINDO URAIS UMOJA WA MITUME NA MANABII TANZANIA
NA MWANDISHI WETU
KIONGOZI Mkuu wa Huduma ya Sauti ya Uponyaji Tanzania,Dkt. Nabii Joshua Aram Mwantyala ametwaa asilimia 80 ya kura katika uchaguzi wa nafasi ya urais katika Umoja wa Manabii na Mitume nchini Tanzania (Unity of Apostles and Prophets Tanzania).
Ushindi huo umetokana na kura 179 alizopata huku akiwaacha mbali washindani wake akiwemo Mchungaji Ceasar Masisi aliyepata kura 42 na Mtume Joackim aliyepata kura nne kupitia uchaguzi uliofanyika katika Ukumbi wa Anatoglo uliopo Ilala, Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo, Askofu Profesa Rejoice Ndalima alimtangaza rasmi Dkt.Nabii Joshua Aram Mwantyala kuwa Rais wa Umoja wa Mitume na Manabii nchini Tanzania.
Aidha, mitume na manabii mbalimbali nchini walionesha imani kubwa juu ya Dkt. Nabii Joshua huku wakimpongeza na kuahidi kumpa ushirikiano mkubwa aweze kutekeleza jukumu lake la kuwaunganisha viongozi hao wa kiroho ili waweze kulihubiri neno la Mungu kwa ufanisi nchini.
Wakati huo huo akizungumza baada ya kutangazwa mshindi katika nafasi hiyo, Dkt. Nabii Joshua amesema kuwa, anakwenda kusimamia mambo makuu matatu ikiwemo kusimamia na kuhamasisha umoja kwa mitume na manabii.
"La kwanza, Bwana Yesu alitoa maelekezo siku chache kabla ya kuondoka kuhusu umoja, na matokeo ya umoja, tunaona kina Petro baada ya siku ile ya Pentekoste waliwainua viwete, kazi yangu itakuwa kuhakikisha ninasimamia na kuhamasisha umoja,kukesha na kuombea umoja wa mitume na manabii wa kanisa la Tanzania,"amesema Dkt.Nabiijoshua.
"Nina hakika katika umoja huo tutaenda mahali,tutasimama mahali aliposimama Petro alipomfuata Dorcas,"amesema.
Kiongozi huyo ambaye ni mzaliwa wa Mbeya akiwa amebatizwa kama Mpentekoste amesema ana zaidi ya miaka 20 katika wito akiwa ndiye kiongozi na mwanzilishi wa Huduma ya Haki Ministry makao makuu yakiwa mkoani Morogoro yenye matawi zaidi ya 200 nchini.
"Pili nitahakikisha umoja wetu unakuwa na faida kwa Taifa letu la Tanzania hasa katika kipindi hiki ambacho Taifa letu la Tanzania limempata Rais mwanamke, Mama yetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan. Debora hakwenda peke yake, kwa hiyo sisi tutakwenda na Debora wetu Rais wetu Mheshimiwa Samia kumsaidia kazi
"La mwisho nitahakikisha ninasimamia mitume na manabii kuhakikisha tunarudi katika misingi ya wazee wetu. Kitabu cha Malaki, Biblia inasema nitageuza mioyo ya watoto wawaelekee baba zao. Nitahakikisha tunawaenzi wazee wetu wakiwemo Baraza la Wapentekoste kwa kazi kubwa waliyoifanya, kwa sababu sisi ni matunda ya kazi yao,"amesema Dkt.Nabiijoshua,
MFAHAMU MGUNDUZI WA KWANZA WA SIMU
WAZIRI MKUU ARIDHIA KUONGEZA SIKU SABA KWA KAMATI MAALUMU YA KUCHUNGUZA MAUAJI MTWARA, KILINDI
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameridhia kuongeza muda wa siku saba kwa kamati maalum iliyopewa jukumu la kuchunguza mauaji yaliyofanyika Mtwara na Kilindi, Tanga.
Kamati hiyo iliyoanza kazi Februari 4, 2022 ilipaswa kukamilisha ripoti yake ndani ya siku 14, zilizoishia Februari 17, 2022. Lakini kutokana na ukubwa wa kazi na mahitaji ya kujiridhisha na baadhi ya masuala, kamati imeomba kuongezewa siku saba kuanzia Februari 17 hadi Februari 23, 2022.
Kamati hiyo iliundwa na Waziri Mkuu ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alilolitoa Februari 4, 2022 mjini Magu, Mwanza akiwa njiani kuelekea Musoma, Mara kwenye maadhimisho ya miaka 45 ya CCM.
Aidha, Mheshimiwa Waziri Mkuu anatoa wito kwa mamlaka husika kuendelea kutoa ushirikiano kwa kamati ili iweze kuikamilisha kazi hiyo kwa wakati na ufanisi
TANZANIA BARA, ZANZIBAR KUTEKELEZA KWA PAMOJA ANWANI ZA MAKAZI
Na Prisca Ulomi, WHMTH, Zanzibar
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa pamoja zinashirikiana kutekeleza mfumo wa anwani za makazi nchini kwenye mikoa yote 31 ya Tanzania Bara na Zanzibar ili iweze kukamilika ifikapo mwezi Mei mwaka huu kwa lengo la kufanikisha zoezi la sensa ya watu inayotarajiwa kuanza mwezi Agosti mwaka huu ambapo uzinduzi wa operesheni ya anwani za makazi na kikao kazi kwa ajili hiyo kimefanyika leo kwenye ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul Wakil, Zanzibar
Mgeni Rasmi wa kikao kazi na uzinduzi wa Operesheni ya Anwani za Makazi, Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema kuwa tuna viongozi katika kila ngazi, kila mmoja akifanya kazi yake vizuri hakuna mzanzibari atakosa taarifa kuhusu anwani za makazi na sensa ya watu na tumeona wataalam wetu wa ndani wametengeneza mfumo wa NaPA ambao unatupatia anwani za makazi ambapo tungetumia wataalam wa nje, Serikali ingetumia fedha nyingi sana
Ameongeza kuwa Serikali itagawa shilingi bilioni 28 kwenye mikoa yote 31 ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa ajiili ya utekelezaji wa anwani za makazi na ugawaji huo wa fedha hizo utazingatia ukubwa wa maeneo na mahitaji halisi ya eneo husika
“Fedha hizi zitakuja kwenye mikoa yenu, zikatumike kwa makusudi yaliyokusudiwa na tutazifuatilia kwa karibu, naamini viongozi ni wasikivu na mtatoa ushirikiano ipasavyo ili tufanikiwe utekelezaji wa jambo hili la anwani za makazi kwa kuwa hakutakuwa na muhali kwenye jambo hili na mmefanikiwa kwenye mazoezi makubwa na hili naamini nidhamu ya matumizi ya fedha itafanyika na tukitoka hapa tukawaelimishe wananchi wetu kuhusu jambo hili na tujumuishe kwenye ajenda zetu zote” amesisitiza Mhe. Abdullah
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi), Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed wakati akimkaribisha mgeni rasmi amesema kuwa masuala haya yanahitaji ushirikiano wa pamoja na ndio maana wote tuko hapa na baada ya kikao hiki kila mmoja achukue jukumu lake la kuhakikisha anwani za makazi na sensa ya watu inakamilika ipasavyo
“Ni lazima wananchi wajue kibao hiki kipo hapa kwa manufaa gani hivyo ni muhimu kujenga uelewa kwa wananchi ili malengo yaliyokusudiwa yaweze kupatikana”, amesisitiza Mhe. Mohammed.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye amesema kuwa mazoezi haya mawili ya utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi na sensa ya watu ni mazoezi mawili tofauti ila yanayotegemeana ambapo operesheni hii imelenga kuliongezea nguvu zoezi la sensa ya watu kwa sababu ya maagizo mliyotupatia kuwa zoezi la anwani za makazi linatakiwa kuisha mwezi wa tano na la sensa litaanza mwezi wa Nane mwaka huu
Waziri Nape ameongeza kuwa zoezi la anwani za makazi ni safari ya kuelekea Tanzania ya kidijitali kwa kuwa bila anwani za makazi Tanzania ya kidijitali haiwezakani kwa kuwa tayari dunia imeshaenda kidijitali, sisi ni sehemu ya dunia na kama tunataka kwenda kwenye Mapinduzi ya Nne ya Viwanda ni lazima tutekeleze mfumo wa anwani za makazi na Zanzibar ya kidijitali inawezekana
Amefafanua kuwa mfumo huu wa anwani za makazi ni mkataba baina ya CCM na wananchi kuwa ifikapo mwaka 2025 tuwe na awani za makazi na ni uamuzi mzuri kuwa jambo hili litekelezwe kwa miezi mitano badala ya miaka 5
“Zoezi la sensa haliwezi kutekelezwa vizuri bila anwani za makazi, hivyo tumeona ni vema mfumo wa anwani za makazi utekelezwe kwanza ili kufanikisha utekelezji wa sensa ya watu na makazi,” amesema Waziri Nape
Ameongeza kuwa utekelezaji wa mfumo huu wa anwani za makazi ungetekelezwa na wakandarasi ungetumia zaidi ya shilingi bilioni 700 ila Serikali itatumia shilingi bilioni 28 tu kwa kuwa mfumo huu wa operesheni ya anwani za makazi ni mali ya wananchi na utatekelezwa na wananchi wenyewe mpaka kwenye ngazi ya Serikali ya Mitaa/Shehia na utasimaimwa na watendaji wa Serikali ya Mitaa/Shehia wenyewe
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Amour Bakari amesema kuwa Wizara hizi zenye dhamana ya Mawasiliano ikiwemo Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ya Tanzania Bara zinawajibika kuhakikisha kuwa anwani za makazi zinatekelezwa kwa kuwa anwani za makazi zinawezesha mwananchi kupata, kupokea na kufikisha huduma au bidhaa hivyo tunapaswa kuwa na anwani za makazi kwa kuwa anwani ni nyenzo muhimu ya mawasiliano nchini na hadi sasa jumla ya shehia 30 kati ya shehia 338 za Zanzibar zina anwani za makazi ambayo ni sawa na asilimia 7 tu.
Katika kikao kazi hicho, wataalam wa kutoka Wizara na taasisi za SMZ waliwasilisha taarifa kuhusu hatua iliyofikiwa ya maandalizi ya Sensa ya Watu na Makaazi ya Mwaka 2022; Sensa ya Majengo; na taarifa ya utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi ambapo kwa upande wa Tanzania Bara, mtaalam wa TEHAMA, Fredrick Apina kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari aliwasilisha kwa viongozi hao namna mfumo wa NaPA unavyofanya kazi ikiwemo ukusanyaji wa taarifa na matumizi yake kwa mwananchi katika shughuli za kiuchumi na kijamii ambapo mfumo huu unamwezesha mwananchi kupata anwani za maeneo mbali mbali na huduma zinazotolewa mahali alipo au yaliyo jirani nae
Kikao kazi hicho kimehudhuriwa na Mawaziri, Makatibu Wakuu, Makamisaa wa Sensa; Makatibu Tawala wa Mikoa; Wakuu wa Wilaya; Makatibu Tawala wa Wilaya; Wakurugenzi wa Miji; Mabaraza ya Manispaa na Halamashauri za Wilaya; Wakurugenzi na Wakuu wa taasisi za Serikali uliofanyika kwenye ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul Wakil, Zanzibar.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
Sunday, 20 February 2022
Dk.Chaula Aitaka Ngos Kushirikiana Na Serikali Kuimarisha Uchumi Na Ustawi Wa Wananchi
Na WMJJWM, Tanga
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula ametoa wito kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kushirikiana na Serikali kuimarisha uchumi na Ustawi wa wananchi.
Dkt. Chaula akizungumza na Mashirika hayo katika Mkoani Tanga amesema Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO) ni moja ya chombo muhimu katika nchi hii kinachosimamia NGOs, hivyo kinatakiwa kisimamie vema Mashirika yake.
“KilaShirika lina majukumu lililokusudia, ikiwemo kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii, lengo Jamii ibadilike na kurudi kwenye maadili yake” amesema Dkt. Chaula.
Amesisitiza kila slShirika kuangalia sababu ya kujisajili, litekeleze majukumu yake na kufuata kanuni sheria na miongozo iliyopo, ikiwemo kuwasilisha taarifa za kila mwezi.
“Kwa hiyo tunapofanya kazi tunategemea matokeo ambayo kila mwananchi atafurahia uhuru wa nchi hii na Ustawi wa mtu mmoja mmoja utaimarika” Ameongeza Dkt. Chaula.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Tanga Saimon Mdende akiwasilisha taarifa ya shughuli zinazofanywa na Idara hiyo amesema mkoa unashirikiana kwa karibu na NGOs kutekeleza afua mbalimbali ikiwemo kielimisha Jamii madhara ya ukatili wa kijinsia na madawa ya kulevya.
Naye mmoja wa wamiliki wa NGOs ya Gift of Hope Foundation inayoshughulika na kutoa huduma ya ushauri nasaha kwa waathirika wa madawa ya kulevya Said Mbaga, amemueleza Katibu Mkuu malengo ya Taasisi hiyo ni kuhakikisha vijana hawaingii katika mkumbo wa kutumia madawa hayo na waathirika wanapata Huduma na kurudi katika hali zao za kawaida.
Awali, katika Mkutano huo Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri wa Wilaya ya Muheza, hiyo, Vije Mfaume alisema kwa mwaka 2021/22 Halmashauri imetenga jumla ya shilingi milioni 213 kutoka makusanyo ya ndani kwa ajili kutoa mikopo kwa wajasiriamali Wanawake, vijana na watu wenye Ulemavu na hadi sasa jumla ya sh. milioni 132 imetolewa.
Polisi Manyara Wakamata Gobore Haramu
Na Mwandishi wetu, Kiteto
JESHI la polisi Mkoani Manyara linamshikilia mkazi wa kata ya Hale Wilayani Korogwe Mkoani Tanga Omary Mohamed Chuma (52) kwa tuhuma za kufanya uhalifu akitumia silaha haramu.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi (ACP) Benjamin Kuzaga amesema tukio hilo limetokea Februari 15 saa 6 mchana katika kitongoji cha Losoiti kijiji cha Asamacha Kata ya Sunya Wilayani Kiteto.
Kamanda Kuzaga amesema Chuma ambaye ni mkulima na mkazi wa Hale alikamatwa na polisi wa doria akiwa na silaha hiyo haramu aina ya gorobe bila ya kibali kwenye kata ya Sunya.
Amesema mtuhumiwa huyo alikuwa anatumia silaha hiyo aina ya gorore hiyo yenye namba batili HD788-06 bila kibali kwa lengo la kufanyia uhalifu wilayani Kiteto.
“Silaha hiyo haramu iliyotengenezwa kienyeji ikiwa na stakabadhi ya bandia 241519 iliyotolewa June 27 mwaka 2016 wilayani Handeni mkoani Tanga,” amesema kamanda Kuzaga.
Amesema mtuhumiwa huyo anayeshikiliwa kwenye kituo cha polisi wilayani Kiteto, anatarajiwa kufikishwa mahakamani pindi uchunguzi wa tukio hilo utakapokamilika.
“Natoa wito kwa wananchi wote wanaotumia silaha zisizo na vibali wasalimishe kwenye vituo vya polisi popote walipo kwani bila hivyo polisi watawachukulia hatua,” amesema kamanda Kuzaga
Dk.Mpango Atoa Pole Msibani Kwa Malecela
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiongozana na mkewe Mama Mbonimpaye Mpango leo tarehe 20 Februari 2022 wamefika nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu Samwel Malecela Mtaa wa Kilimani Jijini Dodoma kutoa pole kufuatia kifo cha mtoto wake Dkt. Mwele Ntuli Malecela kilichotokea tarehe 10 Februari 2022 Geneva nchini Uswisi.
Akitoa neno la faraja kwa familia na waombolezaji mbalimbali waliojitokeza nyumbani hapo, Makamu wa Rais amewasihi kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu pamoja na kumuombea marehemu apate pumziko la Amani.
Makamu wa Rais amemtaja Dkt. Mwele kama shujaa aliejitoa kupigania Afya za wananchi wengine kupitia tafiti mbalimbali alizokuwa akizifanya zenye lengo la kusaidia jamii kupambana na magonjwa mbalimbali. Amesema Dkt. Mwele alifanya kazi iliyo njema na kuonekana katika jamii ndani na nje ya nchi.
Aidha Makamu wa Rais amesema katika kipindi cha uhai wake Dkt. Mwele Malecela aliinua jina la Tanzania kwa kuaminiwa kufanya kazi katika taasisi kubwa ya afya duniani. Amesema uwezo wa Dkt. Mwele katika kazi pia uliinua wanawake hapa nchini hivyo hapana budi kumshukuru Mungu kwa zawadi hiyo pamoja kumuombea ampokee ili apumzike kwa Amani.
ALIYEACHANA NA MME SUMBAWANGA NA KUOLEWA NA MWINGINE AJIFUNGUA MKONO WA MAMBA...AKOJOA MJUSI
Video Mpya : DIAMOND PLATNUMZ - GIDI