Saturday, 11 December 2021

BADEA Kuipaisha Tanzania Kimaendeleo Kwa Sh. Trilioni 7 Miaka Mitano Ijayo


Na Benny Mwaipaja, Cairo
BENKI ya Maendeleo ya Kiarabu (BADEA) imeahidi kuipatia Tanzania mikopo yenye masharti nafuu pamoja na misaada inayokadiriwa kufikia dola za Marekani bilioni tatu sawa na takribani shilingi za Tanzania trilioni 7 katika kipindi cha miaka mitano ijayo kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ahadi hiyo imetolewa Jijini Cairo Nchini Misri na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Dkt. Sidi Ould Tah alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

“Tumekuwa na majadiliano ya kina na yenye tija na Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania pamoja na ujumbe wake ambapo tumejadili mambo mengi ya msingi kwa ajili ya uhusiano wetu kama Benki na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tuko tayari kutoa fedha hizo” alisema Dkt. Tah.

Alifafanua kuwa fedha hizo zitatolewa katika kipindi cha miaka 5 ya utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo katika maeneo matano ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, elimu, kilimo, kuimarisha sekta binafsi pamoja na kuwajengea uwezo wataalam.

“Tunampongeza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na Watanzania kwa ujumla kwa kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa n chi yake na sisi tunaahidi kwamba tutashirikiana naye katika mipango yake ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Kwa Upande wake Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba aliishukuru Benki hiyo kwa kuamua kutoa kiasi hicho kikubwa cha fedha ambacho kitasaidia kuwaletea wananchi maendeleo ya haraka kupitia miradi ya kimkakati waliyokubaliana kupatia fedha hizo.

Alisema kuwa BADEA ni wadau wakubwa wa maendeleo nchini ambapo mpaka sasa wametoa mikopo na misaada inayofikia zaidi ya dola za Marekani bilioni 2.24 kwa ajili ya ujenzi wa miradi ukiwemo mradi mkubwa wa maji uanaoanzia Mwanga kwenda Same mkoani Kilimanjaro.

Dkt. Mwigulu alisema kuwa mikopo na misaada ya dola za marekani bilioni 3 zitakazotolewa na Benki hiyo katika kipindi cha miaka 5 ijayo zitatumika kuboresha Nishati, ujenzi wa miradi zaidi ya 14 ya kilimo cha umwagiliaji, ufugaji na ujenzi wa barabara zitakazofungua fursa za kiuchumi kwenye maeneo yanayozalisha bidhaa zikiwemo za kilimo.

“Fedha hizi ambazo BADEA watatupatia zitatumika pia kuendeleza sekta binafsi ambapo benki zitapatiwa sehemu ya fedha hizo kwa ajili ya kutoa mikopo yenye riba nafuu kwenye sekta za uzalishaji na kukuza ajira kwa vijana na wanawake kupitia shughuli mbalimali ikiwemo biashara na shughuli nyingine za ujasiliamali” alisema Dkt. Nchemba.

Naye Waziri wa Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt. Jamal Kassim Ali alisema kuwa Zanzibar itanufaika na sehemu ya fedha hizo za mikopo nafuu na misaada ambapo kiasi cha dola za Marekani milioni 450 kitatumika kutekeleza miradi kadhaa ya kimkakati.

Aliitaja baadhi ya miradi ambayo fedha hizo zitaelekezwa kuwa ni Ujenzi wa Uwanja wa Ndege Kisiwani Pemba ukihusisha njia ya kurukia ndege na jengo la abiria, ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Binguni, ujenzi wa vyuo vya ufundi vitano vya VETA pamoja na maghala ya kuhifadhia mafuta.

Dkt. Ali alisema kuwa hatua hiyo itachangia kusisimua zaidi uchumi wa nchi na pia kukuza ajira ambazo ni changamoto kubwa hivi sasa na kuishukuru Benki hiyo ya Maendeleo ya nchi za Kiarabu BADEA kwa uamuzi huo wa kutoa fedha kuchangia maendeleo ya nchi.


Share:

DREAMS Champion– Kagera 6 Job Opportunitiesn at MDH

DREAMS Champion (6 Posts)   JOB ADVERT – KAGERA SUBGRANTEE VACANCY ANNOUNCEMENT Management and Development for Health (MDH) is a non-profit, non-governmental organization whose primary aim is to contribute to address public health priorities of the people of Tanzania and the world at large. These priorities include: communicable diseases such as HIV/AIDS, Tuberculosis and Malaria; Reproductive, […]

This post DREAMS Champion– Kagera 6 Job Opportunitiesn at MDH has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

ART Nurse – Tabora 28 Job Opportunities at MDH

ART Nurses (28 Posts)   JOB ADVERT – TABORA SUBGRANTEE VACANCY ANNOUNCEMENT Management and Development for Health (MDH) is a non-profit, non-governmental organization whose primary aim is to contribute to address public health priorities of the people of Tanzania and the world at large. These priorities include: communicable diseases such as HIV/AIDS, Tuberculosis and Malaria; Reproductive, […]

This post ART Nurse – Tabora 28 Job Opportunities at MDH has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

ART Nurse – Kagera 13 Job Opportunity at MDH

ART Nurses (13 Posts)   JOB ADVERT – KAGERA SUBGRANTEE VACANCY ANNOUNCEMENT Management and Development for Health (MDH) is a non-profit, non-governmental organization whose primary aim is to contribute to address public health priorities of the people of Tanzania and the world at large. These priorities include: communicable diseases such as HIV/AIDS, Tuberculosis and Malaria; Reproductive, […]

This post ART Nurse – Kagera 13 Job Opportunity at MDH has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Clinical Officer – Kagera 19 Job Opportunities at MDH

Clinical Officers (19 Posts)   JOB ADVERT – KAGERA SUBGRANTEE VACANCY ANNOUNCEMENT Management and Development for Health (MDH) is a non-profit, non-governmental organization whose primary aim is to contribute to address public health priorities of the people of Tanzania and the world at large. These priorities include: communicable diseases such as HIV/AIDS, Tuberculosis and Malaria; Reproductive, […]

This post Clinical Officer – Kagera 19 Job Opportunities at MDH has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI DESEMBA 11,2021

Magazetini leo Jumamosi December 11 2021













Share:

TIC YASHIRIKI ZOEZI LA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KUADHIMISHA MIAKA 60 YA UHURU

Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kanda ya Kaskazini Bw. Daudi Riganda akiwa kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro katika kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru tarehe 9 Disemba, 2021.
Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kanda ya Kaskazini Bw. Daudi Riganda akiwa kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro katika kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru tarehe 9 Disemba, 2021.
Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kanda ya Kaskazini Bw. Daudi Riganda akiwa kwenye eneo la Kibo alipokuwa akipanda Mlima Kilimanjaro katika kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru tarehe 6 Disemba, 2021.
Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kanda ya Kaskazini Bw. Daudi Riganda akiwa njiani kuelekea kilele cha Mlima Kilimanjaro katika kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru tarehe 7 Disemba, 2021.
Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kanda ya Kaskazini Bw. Daudi Riganda alipokuwa akianza kupanda Mlima Kilimanjaro katika kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru tarehe 5 Disemba, 2021.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai akiwapokea waliokuwa wamepanda Mlima Kilimanjaro katika kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru tarehe 10 Disemba, 2021.

***
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Stephen Kagaigai amehitimisha zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru. 

Hitimisho hilo limeenda sambamba na kuwapokea watu  mbalimbali waliopanda Mlima Kilimanjaro wakiongozwa na aliyeshika bendera Kanali Martin Msumali na Staff Surgent Samwel Chacha ambao walienda kusimika bendera ya Tanzania kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro tarehe 10 Disemba, 2021.

Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kanda ya Kaskazini Bw. Daudi Riganda ameiwakilisha vyema TIC kwa kuweza kupanda na kufika kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Bw. Riganda amekuwa kati ya watu 79 waliofanikiwa kufikia  kilele cha Mlima Kilimanjaro ambapo waliopanda awali walikuwa 150.

Riganda amesema kuwa safari ya kupanda mlima Kilimanjaro ilianza tarehe 5 Desemba, 2021 kutokea Geti la Marangu hadi kambi ya Mandara ambapo ilichukua masaa 4 kwa kusafiri urefu kwa futi 8,858. Siku ya pili safari ilianza Mandara hadi kambi ya Horombo kwa kusafiri urefu wa futi 12,205 ambayo ilichukua masaa 6.

 Siku ya tatu safari ilianza Horombo hadi Mawenzi ridges kwa kusafiri urefu wa futi 14,400 kwa ajili ya kuzoea mazingira ya hewa (climatization) kabla ya kupanda zaidi mlima kuelekea Kibo. Siku ya nne safari ilianza Horombo hadi kambi ya Kibo kwa kusafiri urefu wa futi 15,530 safari ambayo ilichukua masaa 6. 

Siku ya tano safari ilianza Kibo Hut hadi kilele cha Mlima Kilimanjaro (Uhuru Peak) kupitia Gilman's Peak na Stella Peak kwa kusafiri urefu wa futi 19,341 ambayoilichukua masaa 10.

 Siku ya sita safari ilianza kurudi Geti la Marangu.

Bw. Riganda amesema kuwa alienda na kauli mbiu ya WEKEZA TANZANIA ARDHI YENYE MLIMA KILIMANJARO (INVEST IN TANZANIA THE LAND OF MOUNT KILIMANJARO).

Bw. Riganda amesema kuwa amefurahia sana safari hiyo kwani ameweza kukutana na baadhi ya vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje kama vile BBC (Salim Kikeke), ITV, TBC, na wengine waliokuwa katika ziara hiyo. 

Vilevile amefanya mahojiano na balozi wa hiyari wa utalii kutoka Marekani Mr. Macon Dunnagan ambae amemweleza fursa za uwekezaji tulizonazo Tanzania na akaahidi kuwa atazitangaza hizo fursa hizo. Mr. Dunnagan amepanda Mlima Kilimanjaro zaidi ya mara arobaini na tano (45)

Hafla hiyo imehudhuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Stephen Kagaigai, Mwenyekiti wa Bodi wa TANAPA Jenerali George Waitara, Katibu Tawala wa Wilaya ya Moshi Bi. Angelina Marko na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Sekta binafsi na Makampuni mbalimbali ya utalii.
Share:

Friday, 10 December 2021

BASHUNGWA- VYAMA VYA MICHEZO TUMIENI TAIFA CUP KUWAPATA WACHEZAJI WA BORA WA TAIFA.



***********

Na John Mapepele.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Innocent l. Bashungwa ametoa wito kwa vyama vya kitaifa vya michezo, kutumia mashindano ya Taifa CUP 2021 kuchagua vipaji vya wachezaji na kuviendeleza ili kupata vipaji vitakavyounda timu za Taifa za michezo mbalimbali kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.

Mhe. Bashungwa ameyasema hayo, leo Desemba 10,2021 wakati alipokuwa akifungua mashindano ya Taifa CUP 2021 kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Amesema azma ya Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wa Tanzania, wanashiriki kikamilifu katika shughuli za michezo kwa kuwa michezo inatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi hususan kwenye Marnie ya uchumi, siasa na jamii.

“Kimsingi michezo ni ajira, amani, mshikamano, afya na furaha. Kutokana na umuhimu huu wa sekta ya michezo, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeamua kwa dhati kabisa, kwa kusaidiana na Vyama vya Michezo chini ya Baraza la Michezo la Taifa, kuanzisha shindano la Taifa Cup ambalo lilikuwa halipo kwa miaka kadhaa”. Amefafanua Mhe. Bashungwa.

Amesema, mashindano ya Taifa Cup 2021 yameshirikisha michezo michezo mitatu ambayo ni soka, netiboli na riadha pamoja na michezo ya jadi.

Ameongeza kuwa amefarijika kuona wananchi wa pande mbili za Muungano wameendelea kuunganishwa na mashindano haya na wanashirikiana vyema, kupitia sekta ya michezo, ambapo amesisitiza kuwa ana amini kuwa katika mashindano haya, kutakuwa ushindani mkubwa katika michezo yote mitatu, na aliyejiandaa vema ndie atakaye kuwa mshindi.

Kupitia hotuba yake amemshukuru Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa dhamira yake ya dhati ya kutaka kuona sekta ya michezo, pamoja na sekta za Utamaduni na Sanaa, zinapiga hatua kubwa kwa manufaa ya Watanzania.Amepongeza kamati ya maandalizi ya mashindano haya na viongozi wa mikoa yote iliyoleta timu zao kwenye mashindano haya, bila kujali changamoto mbalimbali katika kuandaa ikiwa ni pamoja na maandalizi ya timu, na kuzisafirisha mpaka hapa Dar es Salaam.

Ametoa rai kwa wanamichezo wanaoshiriki mashindano hayoambao bado hawajachanja, kwenda kuchanja ili kujikinga na ugonjwa wa Uviko 19 na amewakumbusha watanzania wote kuchukuwa hatua za kujikinga na maambukizi ya virusi vya korona, kwa kuwa ugonjwa huo bado upo ambapo amesisitiza kuwa ni wajibu wa kila mwananchi kunachukua hatua madhubuti, kadiri ya maelekezo ya wataalamu wetu wa afya.
Share:

WILAYA YA MISENYI YAKAMILISHA MIRADI YA UVIKO 19 KABLA YA MUDA ULIPANGWA



HALMASHAURI ya Wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera imefanikisha usimimizi wa fedha za miradi ya maendeleo ya  Uviko 19 iliyo tolewa na serikali kuu ,ambapo imeweza kutekeleza asilimia 95 ya miradi  53 ya vyumba vya madarasa ya sekondari kabla ya muda uliowekwa  ifikapo Desemba 15 Mwaka huu.

Hayo yamedhibitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ya Misenyi ,Waziri Kombo mara baada ya  ziara yake na wataalamu wa Halmshauri hiyo kukagua miradi ambayo inatekelezwa.

Kombo amesema kuwa Halmashauri yake ilipewa Bilioni moja na milioni 60 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo ikiwemo ujenzi wa madarasa 53 ya wanafunzi wa kidato cha kwanza watakaoanza kidato cha kwanza mwakani na madarasa 10 ya shule shikizi za msingi.

Amesema mafanikio hayo ni kutokana na ufatiliaji wa karibu na wa mara kwa mara ulioenda sambamba na ushirikiano kati ya viongozi wote kuanzia walimu ambao walipewa jukumu la kusimamia mafundi,viongozi wa Wilaya,Chama mpaka Mkoa jambo ambalo limeleta tija kubwa.

Amesema kuwa uwepo wa madarasa hayo umewapunguzia mzigo wakurugenzi kwani ni jambo ambalo lilikuwa linawatesa kwamba watayajengaje ila kupitia fedha za Serikali itasaidia kuondoa changamoto hiyo na kuwasaidia wanafunzi kusoma bila shida.

‘’Tunamshukuru Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha kwa ajili ya miradi hii kwenye Halmashauri yetu,tulikuwa hatulali tulifatilia kwa karibu na kuna wakati tulitumia ukali kwa wasimamizi lakini lengo lilikuwa ni kutimiza maagizo tuliyopewa na hatimaye leo tumemaliza kabla ya wakati na kwa viwango vya juu’’amesema Kombo

Kwa upande wao wataalamu ngazi ya  Halmashauri hiyo katibu kamati ya ufatiliaji miradi ya uviko 19 ,Gozberth  Bernard na mhandisi Lucy Nshoma wamesema kuwa mradi huo ulikuwa na usimamizi mzuri na wenye viwango bora vilivyotolewa na serikali.

Wakizungumza kwa nyakati fofauti wananchi wa Wilaya ya Misenyi wamesema kuwa wanaishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa jinsi ilivyoleta maendeleo kwenye jamii hususani madarasa ambayo yatasaidia Watoto wao kupata elimu bora.
Share:

WANAOTUHUMIWA KUMUUA MWALIMU WAKAMATWA MUSOMA



JESHI la Polisi Mkoani Mara limefanya Operesheni maalumu kwenye Halmashauri zote na kukamata watuhumiwa 22 wakiwemo Wawili ambao wanahusishwa na mauaji ya Mwalimu Dickson James (27) wa Shule ya Msingi Busambara wilayani Musoma mkoani Mara.

Mwili wa James ulikutwa umetelekezwa mashambani, Disemba 7 Mwaka huu, majira ya saa 2 usiku katika Kitongoji cha Nyakato, Kijiji cha Nyang’oma huku mikono yake ikiwa imefungwa kwa kamba.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, SP Longinus Tibishubwamu, marehemu aliibiwa Pikipiki yake yenye Namba za usajili MC 179 CYQ aina ya Super Tiger.

Operesheni hiyo iliyoanza 26 Oktoba hadi 09 Disemba Mwaka huu majini na nchi kavu, imewezesha kukamatwa mali mbalimbali za wizi zikiwemo Pikipiki 12, Magodoro 11 likiwemo Moja la Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kwangwa.
Share:

KIJANA ATUPWA JELA KWA KUMBAKA NA KUMTOROSHA BINTI WA MIAKA 14




KIJANA, Hamad Ali Hamad (25) mkazi wa Chake Chake, Pemba ameanza kutumikia kifungo cha miaka 14 gerezani baada ya kupatikana na hatia katika kesi ya kubaka na kutorosha msichana mwenye umri wa miaka 14.

Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu wa Mahakama ya Chake Chake, Abdallah Yahya Shamuhuna.

Awali akisoma hati ya mashtaka, Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya DPP, Juma Mussa alidai mshtakiwa alimchukuwa binti huyo aliye chini ya uangalizi wa wazazi wake na kumpeleka nyumbani kwake, jambo ambalo ni kosa chini ya sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.

Alidai kitendo cha kumtorosha binti huyo na kumuweka nyumbani kwake, kwa kiasi kikubwa kimesababisha usumbufu kwa wazazi wake pamoja na kumkosesha kwenda shule kwa muda.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Shamuhuna alisema ameridhishwa na upande wa utetezi ukiongozwa na mashahidi saba na kumtia hatiani mshtakiwa huyo kwa kosa la kutorosha na kumbaka binti huyo ambaye yupo chini ya uangalizi wa wazazi wake.

“Kubaka ni kosa kwa mujibu wa sheria chini ya mwenendo wa makosa ya jinai, ambapo mtuhumiwa atatumikia chuo cha mafunzo (gerezani) miaka 14 na kumlipa fidia muhusika Sh milioni 2,” alisema hakimu huyo.

Serikali ya Zanzibar imeanzisha mahakama maalumu ya udhalilishaji wa kijinsia na kuanzia Januari hadi Septemba, mwaka huu imewatia hatiani washtakiwa 20 na kuwahukumu kifungo cha miaka 14 hadi 30, huku kesi zikisikilizwa kwa haraka.
Share:

KIFAA CHA KUSAIDIA WATU KUJIUA CHAZUA UTATA




Mtengenezaji wa kifaa cha kujiua alisema ana uhakika kinaweza kutumika nchini Uswizi kuanzia mwaka ujao.

Sarco iliomba ushauri wa mtaalamu wa sheria, na akaihakikishia kuwa kifaa hicho hakikiuki sheria za Uswizi.

Lakini wanasheria wengine walihoji usahihi wa msimamo wake. Shirika la Dignitas, ambalo linahusika na suala la kusaidiwa kujiua, lilisema hakuna uwezekano kuwa kifaa hicho "kukubalika kwa kiasi kikubwa". Kujiua kwa kusaidiwa ni halali nchini Uswizi. Na watu 1,300 walikufa, kwa njia hiyo mnamo 2020.

Mkanganyiko wa kisheria

Njia inayotumika kwa sasa Uswizi ni kumpa mtu anayetaka kujiua majimaji, yakimeng'enywa maisha yake yataisha.

"Vidonge vya kujiua" vinaweza kuwekwa popote, vimejaa nitrojeni, na hupunguza haraka viwango vya oksijeni. Husababisha mtu kupoteza fahamu, na kisha kufa ndani ya dakika 10.

Kifaa kinaweza kuendeshwa kutoka ndani, na kina kitufe cha dharura cha kusaidia kutoka humo.

Sarco ilimwomba mtaalamu wa sheria Daniel Herlmann, profesa mshiriki katika Chuo Kikuu cha St. Gallen, kuthibitisha ikiwa matumizi ya kifaa cha kujitoa uhai yalikiuka sheria za Uswizi.

Aliambia BBC kuwa alidhani kifaa hicho "si kifaa cha matibabu" na kwa hivyo hakiko chini ya Sheria ya Bidhaa za Tiba.

Pia inaaminika kuwa haikiuki sheria zinazohusiana na matumizi ya nitrojeni, silaha au usalama wa bidhaa. Alihitimisha kuwa "Sheria za Uswizi hazishughulikii kifaa hiki."

"Uswizi imekuwa na sera ya kusaidiwa kujiua kwa miaka 35," Dignitas aliambia BBC. "Kwa kuzingatia matendo haya ya kitaalamu hatuwezi kufikiria kuwa kifaa cha kuokoa maisha kinaweza kukubaliwa au kuvutiwa na Uswizi."

CHANZO - BBC SWAHILI
Share:

UTEKELEZAJI WA KAMPENI KABAMBE YA MAZINGIRA WASHIKA KASI

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mohammed Khamis Abdulla akikabidhi Mpango Kazi wa Kampeni Kabambe ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira na Mwongozo wa Tuzo ya Taifa ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira kwa Bw. Seif A. Seif Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Kampeni Kabambe ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira katika kikao kilichofanyika leo tarehe 10/12/2021 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Bw. Seif A. Seif Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Kampeni Kabambe ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira akionyesha Mpango Kazi wa Kampeni Kabambe ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira na Mwongozo wa Tuzo ya Taifa ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira mara baada ya kukabidhiwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mohammed Khamis Abdulla leo tarehe 10/12/2021, jijini Dar es Salaam.
Bw. Seif A. Seif Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Kampeni Kabambe ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira akiendesha kikao mara baada ya kupokea Mpango Kazi wa Kampeni Kabambe ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira na Mwongozo wa Tuzo ya Taifa ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira leo tarehe 10/12/2021, jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mohammed Khamis Abdulla (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati Maalumu ya Kampeni Kabambe ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira kutoka katika taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Sekta Binafsi, Serikali Kuu, Mashirika ya Umma, Mashirika ya Kimataifa, Asasi Zisizo za Kiserikali, na Taasisi za Fedha. Kushoto ni Bw. Seif A. Seif Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Kampeni Kabambe na Bw. Faraja Ngerageza Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.


******************


Na Lulu Mussa, Dar es Salaam


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo leo tarehe 10 Disemba, 2021 amekabidhi Mpango Kazi wa Kampeni Kabambe ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira na Mwongozo wa Tuzo ya Taifa ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira kwa wajumbe wa Kamati Maalumu ya Kampeni Kabambe ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira katika kikao kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.


Katika hotuba yake iliyosomwa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mohammed Khamis Abdulla, amesema Lengo la Kampeni hiyo ni kuelimisha na kuhamasisha ushiriki wa jamii na uwajibikaji wa mamlaka za usimamizi katika hifadhi na usafi wa mazingira ili kuleta ustawi wa jamii ya watanzania na maendeleo endelevu.


Katika kufanikisha utekelezaji wa Kampeni hiyo, Ofisi ya Makamu wa Rais imeandaa Mpango Kazi wa Kampeni Kabambe ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira wa Kipindi cha Miaka Mitano 2021-2026, Mwongozo wa Tuzo ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira na Rasimu ya Mkakati wa Kutafuta Fedha za kuwezesha utekelezaji wa Kampeni Kabambe ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira.


“Nyaraka hizi ni vitendea kazi vya Kamati hii Maalumu pamoja na jamii ya watanzania katika utekelezaji wa Kampeni hii. Hivyo ninawakabidhi rasmi nyaraka hizi muhimu kama ishara ya kuwa kazi imeanza rasmi. Niwaombe mtoe uzito wa pekee katika kutekeleza majukumu hayo ya hiari ili kuwezesha kufikiwa kwa lengo la Kampeni” Jafo alisisitiza.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Kampeni Kabambe Bw. Seif Ally Seif amesema kwamba, ni imani yake kuwa utekelezaji wa Kampeni hiyo utaanza mara moja na kuwa Kamati yake iko tayari kuungana na Serikali katika kuwezesha utekelezaji wake kwa ufanisi mkubwa.


Kampeni Kabambe ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira ilizinduliwa tarehe 5 Juni, 2021 wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani na Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kampeni hii itakuwa endelevu na itatekelezwa katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2021 hadi 2026.


Wajumbe hawa wa Kamati Maalumu wanatoka katika taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Sekta Binafsi, Serikali Kuu, Mashirika ya Umma, Mashirika ya Kimataifa, Asasi Zisizo za Kiserikali, na Taasisi za Fedha.
Share:

Mradi Wa Jnhpp Kutekelezwa Kwa Weledi, Ufanisi, Wakati Na Gharama Zilizopangwa


Na Dorina G. Makaya – Rufiji, Pwani.

Waziri wa Nishati Mhe. January Yusuf Makamba amesema Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme wa  maji la Julius Nyerere (JNHPP) unatekelezwa kwa weledi, ufanisi, wakati na gharama zilizopangwa

Waziri Makamba ameyasema hayo tarehe 07 Novemba 2021, akiwa kwenye ziara ya kikazi na Waziri wa Nyumba, Huduma na Makazi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri Mhe. Mhandisi Assem Hafez El Gazar walipotembelea Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere (JNHPP)  tarehe 07 Desemba, 2021.

Ameeleza zaidi kuwa, Serikali kupitia Wizara ya nishati inasimamia mradi huo mkubwa wa Ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme wa maji la Julius (JNHPP) na kuwa mradi huo unagharamiwa kwa fedha za Watanzania shilingi trilioni 6.558 na utazalisha umeme wa Megawatt 2,115.

Waziri Makamba pia amekumbushia kuwa, Ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme wa  maji la Julius Nyerere (JNHPP),  ni muhimu na ni mradi mkubwa wa kimkakati kwa nchi yetu. “Sisi kama wasimamizi tumepewa jukumu na Rais wetu Mhe Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha kwamba mradi huu unatekelezwa kwa weledi, ufanisi, wakati na gharama zilizopangwa” alisema Waziri Makamba.

Alikumbushia kuwa, wakandarasi wa mradi huu wametoka katika nchi ya Misri na kuwa ziara hiyo ya Waziri wa Nyumba, Huduma na Makazi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri Mhe. Mhandisii Assem Hafez El Gazar, aliyepewa dhamana ya kusimamia Ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme wa maji la Julius (JNHPP), inaonyesha namna ambavyo Serikali ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri ilivyochukulia kwa uzito wa hali ya juu katika kuhakikisha kwamba Mradi unatekelezwa kwa weledi, ufanisi, wakati na gharama zilizopangwa


“Tumekuja hapa leo kukagua maendeleo ya mradi, kuangalia tulipofikia, kuangalia kama kuna changamoto kwa upande wa Serikali ya Tanzania na Serikali ya Misri ili tuweze kutatua na kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huu.” Alisema Waziri Makamba.

Waziri January Makamba amesema, baada ya kutembelea mradi, wameona mradi unaendelea vizuri pamoja na changamoto chache zilizopo za Mradi kutokwenda kwa kasi kama iliyokuwa imepangwa. Lakini, alieleza kuwa si jambo la ajabu kutokea kwa miradi mikubwa kama huo kuchelewa kukamilika.

Amesema, jambo jema ni kuwa, mradi uko katika hatua nzuri ya utekelezaji na iwapo italazimu kuongeza muda basi utakuwa ni muda unaokubalika na hakutakuwa na gharama za ziada.

“Sisi tumepewa kazi ya kuhakikisha kwamba mradi unatekelezwa na kukamilika kwa kuzingatia usalama na ubora na kutuhakikishia upatikanaji wa umeme wa uhakika. alisisitiza Waziri Makamba.

Waziri Makamba ameeleza zaidi kuwa, Wizara ya Nishati ingependa pakiwa na changamoto zo zote basi zijadiliwe kidugu kwa kuzingatia matarajio ya viongozi wakuu. wa nchi zote mbili pasipo kuviziana, kushtakiana na kuingiza madai ya kisheria na kuwa  nia iwe kumaliza tofauti ndogo ndogo zozote zilizopo kwa maelewano.

Nae Waziri wa Nyumba, Huduma na Makazi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Mhe. Mhandisi Assem Hafez El Gazar amesema, Mradi wa JNHPP ni muhimu sana kwa nchi zote mbili za Tanzania na Jamhuri ya Kiarabu ya Misri.

Amebainisha kuwa, wakati alipoteuliwa kushika nafasi hiyo ya Uwaziri wa Nyumba, Huduma na Makazi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, maelekezo ya kwanza aliyopewa na Raisi Al Sisi ni kusimamia utekelezaji wa Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere (JNHPP)

Waziri El Gazar ameuelezea Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere (JNHPP) kuwa ni mradi utakaosaidia kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizo mbili na kuwa, ukitekelezwa vizuri utajenga imani kwa watanzania kuwa. Jamhuri ya Kiarabu ya Misri ni nchi yenye uwezo wa kutekeleza miradi mingine mikubwa ambayo Tanzania itatazamia kuijenga baadaye.

Aidha, Waziri huyo wa Nyumba, Huduma na Makazi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri Mhe. Mhandisi Assem Hafez El Gazar, amewataka wakandarasi wajitahidi kukamilisha mradi huo kwa wakati na ubora unaokubalika.



Share:

Medical Specialist II (Oncology)(Re-advertised) at Muhimbili National Hospital at Muhimbili National Hospital

POST: MEDICAL SPECIALIST II (ONCOLOGY)(RE-ADVERTISED) – 1 POST   POST CATEGORY(S):  HEALTHCARE AND PHARMACEUTICAL EMPLOYER: Muhimbili National Hospital APPLICATION TIMELINE: 2021-12-07 2021-12-20 JOB SUMMARY NA DUTIES AND RESPONSIBILITIES i.To provide routine specialized medical services for in-patients and out patients; ii.To supervise ward rounds and advice on appropriate medication; iii.To participate in the training of student doctors in their […]

This post Medical Specialist II (Oncology)(Re-advertised) at Muhimbili National Hospital at Muhimbili National Hospital has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

AJALI YA LORI YAUA WATU ZAIDI YA WATU 53


Takriban watu 53 wamefariki na makumi wengine kujeruhiwa baada ya lori walilokuwa wakisafiria kupata ajali mbaya kusini mwa Mexico , mamlaka imesema.

Takriban watu 100, wanaodaiwa kuwa wahamiaji kutoka Marekani ya kati walikuwa ndani ya lori hilo wakati lilipopindukia na kugonga daraja katika jimbo la Chiapas.


Picha kutoka eneo la ajali zinaonesha waathiriwa wakiwa wametapakaa barabarani karibu na lori hilo lililopindukia.


Pia kulikuwa na miili iliopangwa ardhini ikiwa imefunikwa nguo nyeupe.


''Ni mojawapo ya ajli mbaya zaidi kutokea nchini Mexico , huku watu wengine 58 wakiwa wamejeruhiwa , wengine wakiwa na majereha mabaya'', alisema Luis Manuel Garcia , mkuu wa kitengo cha utetezi wa raia wa Chiapas.


Alisema kwamba waathiriwa walikuwa pamoja na wanaume, wanawake, na watoto. Uraia wao haujathibitishwa , lakini maafisa wa eneo hilo wanasema kwamba wengi wa waliokuwa ndani ya lori hilo ni wahamiaji kutoka mataifa ya Honduras na Guatemala.


Lori hilo liliripotiwa kuendeshwa kwa kasi kabla ya kupoteza mwelekeo katika kona na kugonga daraja la raia katika barabara kuu inayoelekea katika mji mkuu wa jimbo la Chiapas , Tuxtla Gutierrez.


Chiapas , ambalo ni jimbo linalopakana na Guatemala , ni kituo cha wahamaji wengi wasio na vibali wanaoelekea Marekani.



Mamia ya maelfu ya wahamiaji wanaotoroka umasikini na ghasia Marekani ya kati hujaribu kuvuka kupitia Mexico kila mwaka kwa lengo la kuwasili Marekani.


Wengi wao hulipa watu wanaofanya magendo , ambao huwasafirisha kinyume cha sheria wakiwa wamejazana katika malori hatari katika safari hiyo ya muda mrefu.


Mpaka wa Marekani na Mexico ni mojawapo ya mipaka hatari zaidi duniani kulingana na data kutoka kwa shirika la wahamiaji duniani IOM.


Mwaka huu pekee takriban watu 650 wamefariki katika mpaka huo, wakijaribu kuvuka , ikiwa ni zaidi ya mwaka wowote ule tangu IOM ilipoanza kuweka rekodi zake.


Pia kuna vifo vingi katika safari hiyo hatari kuelekea mpakani , hatahivyo, vifo hivyo ni vigumu kuvirekodi, ilisema IOM katika taarifa yake.


Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador alielezea ajali hiyo kuwa ya uchungu na kuandika katika twitter kwamba 'anajutia ajali hiyo'.

CHANZO- BBC SWAHILI
Share:

Programme Coordinator/ Coordinatrice de Programme at Danish Refugee Council

DRC has been implementing emergency response projects in Tanzania since the onset of the Burundi refugee crisis in 2015 in three refugee camps in the Kigoma Region at the border with Burundi. DRC’s integrated projects for refugees, asylum seekers and host communities comprise sectors such as Camp Coordination and Camp Management (CCCM), Protection, Water, Sanitation […]

This post Programme Coordinator/ Coordinatrice de Programme at Danish Refugee Council has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger