Friday, 20 November 2020
GGML, NEEC WAANZISHA MAFUNZO KWA WAFANYABIASHARA 500 GEITA
Balozi Nyamanga: Bunge la Umoja wa Ulaya Halijatoa Azimio lolote Kuhusu Tanzania
Na Immaculate Makilika- MAELEZO
Serikali kupitia Balozi wa Tanzania nchini Ubeligiji na Mwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Ulaya imesema kuwa Bunge la Umoja wa Ulaya halijatoa azimio lolote kuhusu Tanzania kupitia kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Bunge hilo.
Akizungumza mapema leo kupitia televisheni ya Taifa (TBC), Balozi wa Tanzania nchini Ubeligiji na Mwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Ulaya Jestus Nyamanga alisema kuwa kuna taarifa za upotoshaji na zisizo na ukweli wowote zinazosambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii zikidai kuwa Bunge la Umoja wa Ulaya jana Novemba 19 limeazimia kusitisha misaada na mikopo kutoka umoja huo na mashirika yake, kwa nchi ya Tanzania sambamba na kuiwekea vikwazo.
Halikadhalika taarifa hizo za upotoshaji zinadai kwamba Bunge hilo la Umoja wa Ulaya limeazimia kuiwekeza vikwazo Tanzania na kuzuia kuuza bidhaa zake katika nchi za Umoja wa Ulaya.
“Novemba 19 asubuhi hapa Ubeligiji, Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Ulaya ilikutana katika kikao chake cha kawaida, moja ya masuala yaliyojadiliwa ilihusu Tanzania na hali ilivyo baada ya Uchaguzi Mkuu kukamilika, huu ni utaratibu wa kawaida kabisa wa Kamati hiyo kuijadili nchi ambayo ni mdau wao mkubwa wa maendeleo mara tu baada ya Uchaguzi Mkuu kukamilika”, alisema Balozi Nyamanga
Balozi Nyamanga alifafanua kuwa kikao hicho ni kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na si Bunge lote na hata hivyo kikao hicho kilitoa nafasi kwa wabunge kutoa mawazo yao na kujadili kuhusu hali ya Tanzania baada ya Uchaguzi Mkuu ambapo ni wabunge watano tu ndio walitoa mawazo yao kati ya wabunge 71 wa Kamati hiyo. Ambapo hilo lina idadi ya wabunge 705 na hivyo halijatoa azimio lolote kuhusu Tanzania.
Alibainisha kuwa pia kuna taarifa ambazo si za kweli zinazoenezwa na watu wenye nia mbaya na Tanzania zikidai kwamba Bunge hilo la Umoja wa Ulaya limeazimia kuifutia Tanzania msaada wa euro milioni 626 ambazo Tanzania inapewa na Umoja wa Ulaya kila mwaka, si kweli kwamba Umoja huo unaipa Tanzania fedha hizo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi. Aidha Serikali inaendelea kutekeleza miradi yake mbalimbali.
“Hakuna mjadala wala majadiliano yanayoendelea katika Umoja wa Ulaya wala hakuna azimio lililowekwa na Kamati hiyo ya Bunge, wala kuizuia Tanzania kuuza bidhaa zake katika nchi hizo za Umoja wa Ulaya, hata hivyo naomba niwahakikishie watanzania wenzangu kwamba uhusiano wa Tanzania na Umoja wa Ulaya ni mzuri sana kwa zaidi ya miaka 45 sasa na tunaendelea kushirikiana katika masula mbalimbali yanayohusu maendeleo kwa pande zote mbili”, alisema Balozi Nyamanga.
Mwisho.
Dkt. Abbasi awataka viongozi wa Michezo kuandaa mikakati Mikubwa kuendeleza Michezo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, leo Alhamisi, Novemba 19, 2020, jijini Dar es Salaam, amefungua semina ya wadau wa michezo kutoa maoni na kisha kuridhia Kanuni za Kitaifa za Kutekeleza Mkataba wa Kimataifa wa Kupambana na Matumizi ya Dawa za kusisimua misuli na Kuongeza Nguvu Michezoni.
Akizungumza Katika semina hiyo, Dkt. Abbasi, amewataka wanamichezo wa Tanzania kujiamini kwa kufanya mazoezi na kujiandaa badala ya kutumia dawa za kusisimua misuli ambazo zimepigwa marufuku duniani katika michezo mbalimbali ambayo Tanzania hushiriki.
Aidha amevitaka vyama na mashirikisho ya michezo nchini kuja na mikakati makini ambayo Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Dkt. John Pombe Magufuli, itaona namna ya kuisaidia kwani Mhe Rais ameshatangaza dhamira ya kusaidia sana sekta ya michezo.
“ Viongozi wa mashirikisho na vyama vya Michezo mnatakiwa kuwa wabunifu na kuandaa mikakati ya kukuza na kuendeleza michezo nchini, kwa kuwa Serikali iliyoko madarakani chini Rais Magufuli imejitolea kuinua na kuisaidia Sekta ya Michezo”, amesema Dkt.Abbasi.
Dkt. Abbasi ameongeza kuwa katika warsha hiyo alisisitiza kuwa kila kiongozi wa chama cha michezo atimize wajibu wake, kwa kutoa maoni ili kuepusha kero ya wanamichezo kufungiwa kushiriki michezo kwa sababu ya Matumizi ya Dawa za kusisimua misuli na kuongeza nguvu na kuliletea aibu taifa.
Kwa upande wa Katibu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania Bw.Philbert Bayi aliipongeza Serikali kwa kufanikisha kusainiwa kwa mkataba wa Kupinga matumizi na mbinu haramu michezoni mwaka 2017 na sasa Serikali imetimiza ndoto hiyo ambayo imedumu kwa miaka kumi sasa.
Mwisho
Biden : Trump anatuma ujumbe wa vitisho
Rais mteule wa Marekani, Joe Biden amelaani kitendo cha, Donald Trump kutokukubali kuwa ameshindwa katika uchaguzi wa rais na kwamba amekuwa akituma ujumbe mbaya sana kuhusu Marekani.
Biden amesema, alikuwa na uhakika kuwa, Trump alikuwa anajua kuwa asingeshinda na kila kitu kilionekana wazi, kwa kuwa alikuwa hajitumi kabisa katika majukumu yake.
Biden alikuwa akiongea katika mkutano wa simu na Magavana, wakiwemo wa Democrats na Republicans, kuhusu janga la corona.
Alihojiwa kuhusu suala la Trump kutokubali ushindi wake, Biden amesema rais anatuma ujumbe wa kutisha kwa dunia nzima kuhusu jinsi demokrasia inavyofanya kazi na hilo anapaswa kulikumbuka kwa kuwa amekuwa rais ambaye hawajibiki katika historia ya Marekani.
Kulikuwa na marudio ya kuhesabu kura za uchaguzi wa rais katika Jimbo la Georgi, na Biden alipata ushindi katika jimbo hilo, Trump alifungua kesi ya madai ya wizi wa kura.
Madai yake yote ya kisheria yaligonga mwamba na kushindwa kufanya mabadiliko yoyote.
Serikali Itaendelea Kuboresha Sekta Ya Nishati Kwa Kasi
Na. Beatrice Saanga-MAELEZO
Nishati ni sekta muhimu sana kwa wananchi na maendeleo ya nchi kwa ujumla hususani kuelekea katika uchumi wa viwanda kwa kuhakikisha kuwa umeme wa uhakika unazalishwa na na kuwafikia wananchi walio wengi ili waweze kufikia ndoto zao za kuanzisha na kumiliki viwanda na kuweza kuinuka kuinua kipato cha familia zao na kuleta maendeleo ya nchi.
Aidha, nishati ya umeme inasalia kuwa muhimu sana katika maendeleo na ukuaji wa uchumi duniani kote hasa kutokana na uhitaji mkubwa wa nishati katika matumizi ya kila siku na uzalishaji viwandani ambapo inahitajika katika kuendesha mitambo na mikubwa na katika viwanda vidogo vinavyomilikiwa na wajasiriamali wadogo.
Katika kipindi cha 2019/19, Wizara ya Nishati kwa imekuwa na vipaumbele vingi hasa katika kuhakikisha kwamba umeme wa uhakika unapatikana ili kuwezesha ukuaji wa uchumi wa nchi ambapo Serikali ya Rais John Pombe Magufuli imejitahidi kuongeza uzalishaji wa umeme kwa kutekeleza miradi mikubwa ikiwemo mradi wa kuzalisha umeme katika Mto Rufiji ambao ukikamilika utakuwa na MW 2,100 uliopo wilayani Rufiji na miradi ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia ya Kinyerezi I – Extension MW 185, Kinyerezi II MW 240, Somanga Fungu MW 330 ulioko mkoani Lindi pamoja na MW 300 ulioko katika mkoa wa Mtwara.
Aidha, Serikali imeimarisha mifumo ya usafirishaji wa umeme mkubwa nchini ikiwa ni pamoja na kuendelea na utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini unaosimamiwa na Wakala wa Usambazaji Umeme Vijijini (REA), mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania) na kuendeleza miradi ya nishati jadidifu (jotoardhi, upepo na umeme-jua).
Jitihada za Serikali katika kuimarisha nishati zimeiwezesha kutekeleza miradi mingi ya kusafirisha umeme ambapo imepelekea kupunguza matumizi ya umeme wa mafuta na kuwezesha kuokoa kiasi cha shilingi bilioni, 719 kwa mwaka. Mafanikio hayo yamewezekana katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kuanzia 2019/20.
Wakati Tanzania inaelekea kutimiza azma ya kuwa nchi ya uchumi wa viwanda na kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa katika ya Mwaka 2025 Serikali kupitia, Wizara ya Nishati imelenga kuzalisha umeme wa MW 5,000, mwaka 2020 na kuongezeka hadi kufikia kufikisha MW 10,000 ifikapo mwaka 2025.
Mahitaji ya umeme nchini yameendelea kuongezeka kutokana na kukua kwa shughuli za kiuchumi zinazohitaji nishati ya umeme wa kutosha, wa uhakika na wenye gharama nafuu pamoja na kuimarishwa kwa mifumo ya usafirishaji na usambazaji wa umeme ili kupunguza tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme wa jumla ya MW 2,100 kwa kutumia maji (Hydro Power Plant) katika Bonde la Mto Rufiji ni kichocheo muhimu katika kuwezesha Tanzania kufikia azma yake ya kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 ampapo utekelezwaji wa mradi huu unategemewa kupunguza kama si kuondoa kabisa tatizo la umeme nchini
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais John Pombe Magufuli itahakikisha inasimamia ipasavyo na kuimarisha miundombinu ya nishati kwa kuhakikisha upatikanaji wa huduma za umeme unaboreshwa ili kukabiliana na changomoto mbalimbali za uimarishaji wa Mikakati ya utoaji wa huduma ya nishati ya Umeme.
Katika hotuba yake wakati wa akizindua Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dodoma, tarehe, 13, Novemba 2020 Rais John Pombe Magufuli alisema Serikali yake inaenda kuwezesha upatikanaji wa umeme katika vijiji vyote ambavyo bado havijafikiwa na umeme na kuondoa kabisa tatizo la umeme vijijini.
“Kuhusu umeme pia, kwenye miaka mitano ijayo, tumepanga kufikisha umeme kwenye vijiji vyote ambavyo bado havijafikishiwa umeme, ambapo idadi yake haizidi 2,384. Kwenye miaka mitano iliyopita, kwa takwimu za hadi jana tumefikisha umeme kwenye vijiji 9,884 kutoka vijiji 12,018 mwaka 2016. Nchi yetu ina vijiji 12,280”alisema Rais Magufuli.
Alibainisha kuwa kwenye miaka mitano ijayo Serikali yake imejipanga kukamilisha mradi wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Nyerere ambalo linategemewa kuzalisha megawati 2,115 ambapo Tanzania inakusudia kupata umeme wa kutosha kupitia mradi huo ambao unatarajiwa kupunguza bei ya umeme kwa wananchi.
Aliitaja miradi mingine ambayo Serikali inakusudia kuanza ujenzi wake katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuwa ni pamoja na ujenzi wa miradi mingine ya umeme wa maji Ruhudji utakaokuwa na MW 358, Rumakali MW 222, Kikonge MW 300, umeme wa gesi Mtwara MW 300, Somanga Fungu MW 330,Kinyerezi III MW 600 na Kinyerezi IV MW 300. Aliongeza kuwa Serikali pia inakusudia kutekeleza miradi mingine midogo midogo ambayo kwa pamoja inakusudiwa kuzalisha umeme MW 1,100 kwa kutumia Nishati jadidifu (jua, upepo,jotoardhi)
Katika miaka mitano ijayo Serikali itakamilisha miradi hiyo na kuwezesha upatikanaji wa umeme katika maeneo mbali mbali ya nchini, hali itakayopelekea kuimalika kwa shughuli za viwanda, kuongeza uzalishaji, pamoja na kupelekea kupanda kwa uchumi wa taifa pia Serikali itaendelea kuhamasisha matumizi ya gesi asilia na gesi ya mitungi majumbani, kwenye taasisi, viwanda na magari ili kupunguza uharibifu wa mazingira na athari za mabadiriko ya tabianchi. MWISHO
OFA OFA ....Funga mwaka na kumiliki kiwanja cha ndoto zako! Kwa mkopo nafuu kabisa usio kuwa na riba wala dhamana yoyote ile
Funga mwaka na kumiliki kiwanja cha ndoto zako! Kwa mkopo nafuu kabisa usio kuwa na riba wala dhamana yoyote ile.
Sasa unaweza kumiliki kiwanja kilicho pimwa na chenye hati kwa kulipa kidogo kidogo ndani ya mwaka mzima yaani miezi 12 na zaidi ya mwaka mmoja kwa viwanja vyetu vya Kigamboni (Gezaulole)
Hii ni ofa kabambe kwa wateja wetu wote wa viwanja hasa kwa msimu huu wa siku kuu za krismasi na mwaka mpya.
Viwanja vyetu vipo maeneo yafuatayo;
- Goba (kisauke) bei 35,000 kwa Sqm
- Madale (Flamingo) bei 40,000 kwa Sqm
- Bunju "A" (kinondo - mji mpya) bei 25,000 kwa Sqm
- Kerege (matumbi) bei 17,000 kwa Sqm
- Mbweni (kiharaka) bei 25,000 kwa Sqm
- Kigamboni (Gezaulole) bei 18,000 kwa Sqm (ofa ya hivi viwanja ni kwamba mteja atalipia laki tano tano tu kila mwezi mpaka atakapo kamilisha malipo yake husika)
- Mbezi (Luguruni) bei 35,000 kwa Sqm
- Goba (lastanza) bei 45,000 kwa Sqm
NB: Viwanja vyetu vyote vimepimwa na vina hati, mteja atakabidhiwa hati miliki ya kiwanja chake husika mara tu baada ya kukamilisha malipo yake husika.
- Ofisi yetu ipo jengo la Mwenge towet opposite na Mlimani city.
Tupigie: 0757712776 / 0656489722 / 0783389952
BENKI YA CRDB YATOA MSAADA TAULO ZA KIKE KWA SHULE YA SEKONDARI YA OLD TANGA JIJINI TANGA
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa kushoto akimkabidhi msaada wa taulo za kike Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga(RAS) Judica Omari katika kwa ajili ya wasichana kwenye shule ya Sekondari Old Tanga zenye thamani ya Milioni 5,kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Old Tanga Kasimu Ndumbo wa kwanza kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salim Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa akizungumza wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari akizungumza wakati wa halfa hiyo
AFISA Elimu Mkoa wa Tanga Mayansa Hashimu akizungumza wakati wa halfa hiyo
Meza kuu wakiwa wamesimama wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kupokea msaada huo
Sehemu ya walimu na wanafunzi wa shule ya Sekondari Old Tanga wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye halfa hiyo
Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Old Tanga akitumbuiza kwenye halfa ya makabidhiano hayo
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Old Tanga wakiiimba wimbo wa Taifa kabla ya kupokea msaada huo
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari, Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa alisema kwamba wametoa msaada huo kupitia kampeni maalumu ya Hedhi Salama kwa elimu bora.
Alisema kwamba Benki ya CRDB inachukua kwa uzito sana suala la uwezeshwaji mtoto wa kike,mwanamke hatua ambayo imepelekea benki yao kutunga na kutekeleza sera na mikakati inayolenga kuhamaisha usawa wa kijinsia na kutengeneza mazingira rafiki kwa mwanamke.
Meneja huyo alisema kwamba ndani ya benki yao wamefanya hivyo wakiamini kuwa ukimuewezesha mwananke umeiwezesha jamii na hivyo ndio moja ya siri kubwa ya mafanikio kwenye benki hiyo.
Alisema benki hiyo waliamua kuanzisha mpango huo lakini kwa bahati kubwa shule ya Sekondari Old Tanga wakawa ni miongoni mwa shule ambazo wanaanza nazo.
“Pamoja na jitihada zinazofanywa na wadau mbalimbali ikiwemo serikali bado mahudhuria ya watoto wa kike mashuleni hayaridhishi na hivyo kupelekea kutokufanya vizuri katika masomo yao “Alisema
Alisema changamoto hiyo kwa kiasi kubwa imechangia watoto wengi wa kike wakati wanapoingia kwenye kipindi chao cha hedhi kutokuwa na uwezo wa kuwa na taulo bora za kike inawalazimu kukaa nyumbani na kushindwa kwenda shule na kukaa nyumbani mpaka watakapomaliza .
Meneja huyo alisema lakini au kuvaa vitambaa ambavyo sio salama kwa afya zao ambapo alieleza kwamba utafiti uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Binadamu NIMR unaonyesha kuwa katika wilaya 14 za Tanzania Bara ulibaini kuwa asilimia 15 ya wanafunzi wa kike wanashindwa kuhudhuria shule katika siku zao za hedhi.
Alisema katika ya hizo asilimia 42 inachangiwa na ukosefu wa vifaa vya hedhi na 34 asilimia hofu ya kujichafua kwa sababu hana kitu sahihi cha kujistiri huku asilimia 26 inatokana na miundombinu isiyokuwa rafiki wakati akiwa kwenye kipindi cha siku zake.
“Kutokana na changamoto hiyo benki ya CRDB tuliamua kuanzisha kampeni maalumu ijulikanayo Hedhi Salama kwa elimu bora inayolenga kutatua changamoto wanazopata watoto wa kike kwa kutoa msaada wa taulo za kike kwenye shule mbalimbali nchi nzima”Alisema
Aliongeza kwamba wao kama benki wanaamini upatikanaji wa taulo za kike ni muhimu kwa mahudhurio ya mtoto wa kike shuleni na kupata haki yake ya msingi wa elimu sawa na mtoto wa kiume
Awali akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari aliwashukuru Benki ya CRDB kutoa msaada huo ambao utasaidia katika kuboresha masomo yao.
“Kwa kweli niwashukuru sana na kuwapongeza uongozi wa Benki ya RCD kwa kutambua umuhimu wa huduma hii kwa mtoto wa kike kwenye mkoa wa Tanga nimefurahihwa sana kwa kujali na kutoa mahitaji haya ambayo ni muhimu kwa vijana wetu wa kike”Alisema Ras Judica.
Aidha alisema kwamba serikali ya awamu ya tano nchini ya Rais Dkt John Magufuli inatoa kipaumbele kwenye kuboresha elimu na shule nyingi zimepewa kipaumbele cha hali ya juu.
Alisema katikampango wa elimu ya bila malipo imeongeza zaidi idadi ya wanafunzi kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha kwanza na ufadhili huo ambao umepatikana ni mkubwa kutokana kwa serikali ya awamu ya tano huku akieleza kwamba kwa mkoa wa Tanga umeendelea kupokea msaada huo.
Katibu Tawala huyo alisema kila mwezi kwa mkoa wa Tanga wanapokea kiasi cha sh.Bilioni 1 kwa ajili ya kuendesha mpango wa elimu bure katika shule na mpango huo unasaidia katika kutoa posho mbalimbali kwa ajili ya uwezeshwaji wa wanafunzi, wakuu wa shule wanawezeshwa
Alitaja pia uwezeshwaji wa walimu wakuu pamoja na maafisa elimu kata ambao ni viongozi muhimu katika kuhakikisha elimu bora inapatikana mkoani
“Katika ngazi ya shule fedha hizo pia zinatumika kwenye masuala ya kujenga taaluma, kufanya ukarabati, utawala, kununua vifaa, usimamizi mitihani katika hiyo fedha pa asilimia 10 inatumika kwenye kununua mahitaji mbalimbali kwa ajili ya kumuwezesha mtoto wa kike kuweza kufanya ufaulu mzurina kuweza kukaa shuleni kwa utulivu”Alisema
Thursday, 19 November 2020
Kilimo Mseto Ni Ukombozi Wa Uhakika Wa Chakula Nchini
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya leo amewasili mkoani Mara na kuzindua maonesho ya siku tatu ya kuhamasisha wakulima na wafugaji nchini kutumia kilimo mseto ili kuongeza uhakika wa chakula na kipato.
Maonesho ya Kilimo Mseto yanafanyika mjini Musoma kwa kuwashirikisha wakulima, wafugaji na wavuvi chini ya uratibu wa shirika la Vi Agroforestry pamoja na taasisi za serikali na wadau wa sekta ya kilimo.
” Nimekuja hapa Mara kuwatia moyo wakulima waendelee kujikita katika kilimo mseto kwa kuwa kinafanya vema katika kuhakikisha kaya na taifa linajitosheleza kwa chakula” alisema Kusaya.
Kusaya aliongeza kusema wizara ya kilimo inaendelea kujanga mazingira wezeshi kwa wakulima kupata elimu na teknolojia bora ili kilimo kiwe na tija na kukuza uchumi hivyo uwepo wa maonesho haya una mchango mkubwa kwa wakulima.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Mara Kalorine Mthapula amesema mkoa huo unaendelea na kazi ya kuhamasisha wakulima kujikita katika kwenye shughuli za kilimo na kuwa kupitia maonesho ya kilimo mseto wana uhakika uchumi wa mkoa utaendelea kukua.
Katibu Tawala mkoa huyo alieleza kuwa pamoja na maonesho ya kilimo mseto mkoa huo umeanzisha viwanja maalum vya Nanenane vinavyojulikana kama Mama Maria Nyerere wilayani Butiama kwa lengo la kutumika kufanya maonesho ya kilimo,mifugo na uvuvi ii elimu iwafikie wananchi wengi kwa ukaribu.
” Kila tarehe 15 Septemba mkoa wa Mara huadhimisha siku iitwayo Mara Day kwa lengo la kuhamasisha kilimo, mifugo na uvuvi kupitia viwanja vetu vya Nanenane vya Mama Maria Nyerere huko Butiama ambapo pia siku hiyo hutumika kuhamasisha uhifadhi endelevu la bonde la mto Mara” alisema Mthapula.
Naye Mkurugenzi wa shirika la Vi Agroforetry Thadeus Mbowe alisema maonesho ya mwaka huu yamesheni teknolojia mbalimbali za kilimo mseto kupitia washirika wenza wakiwemo watafiti na wataalam wa kilimo wanaotoa elimu kwa wananchi.
” Lengo kuu la maonesho haya ni kueneza mchango wa kilimo mseto katika kuboresha maisha na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi na kuendeleza mjadala wa uhitaji wa sera ya Taifa ya kilimo mseto” alisema Mbowe.
Kauli mbiu ya maonesho ya Kilimo mseto mwaka huu inasema ” Kilimo mseto kwa usalama wa chakula na kipato”.
Kilimo mseto ni kilimo kinachopambana na mabadiliko ya tabia nchi yanayoathiri kilimo.
Mwisho
Imeandaliwa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Kilimo
MUSOMA
Procurement Officer at Christian Social Services Commission
Background: The Christian Social Services Commission (CSSC) is an ecumenical body established in 1992 by the Christian Council of Tanzania and the Tanzania Episcopal Conference, to coordinate and facilitate the delivery of social services (health and education) by the member churches in Tanzania. For 28 years, CSSC has been serving and coordinate a network of […]
The post Procurement Officer at Christian Social Services Commission appeared first on Udahiliportal.com.
Watu watatu wafariki Uganda katika ghasia za uchaguzi
Polisi nchini Uganda imethibitisha vifo vya watu watatu kutokana na machafuko yaliyozuka alasiri ya Jumatano kufuatia habari za kukamatwa kwa mgombea urais Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine
Machafuko hayo yalisambaa katika miji kadhaa na kusababisha watu wengi kujeruhiwa kutokana na risasi na mabomu ya kutoa machozi. Hii imewalazimu wagombea wawili kwa kiti cha urais kusitisha kampeni zao hadi pale mwenzao atakapoachiwa.
Wagombea hao wamesema ni vigumu kwao kuendelea na kampeni huku mgombea mwingine akiwa anaendelea kunyanyaswa na polisi kwa madai yasiyo na msingi.
Bobi Wine alikamatwa jana Jumatano Mashariki mwa eneo la Luuka baada ya polisi kumshtumu kwa kosa la kusababisha mikusanyiko ya watu ikiwa ni uvunjaji wa miongozo ya kukabiliana na virusi vya corona iliowekwa na Tume ya Uchaguzi.
Na punde tu baada ya wafuasi wake kupata taarifa, walianza kuandamana wakidai aachiliwe huru. Mgombea mwingine, Patrick Amuriat Oboi, pia amekamatwa.
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini Aahidi Kufuatilia ili kujua aliyemtorosha Nabii Bushiri na Mkewe
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema kuwa kutoroka kwa Nabii wa Malawi na mke wake nchini humo ni jambo ambalo analifuatilia kwa karibu na ameahidi kuchukua hatua baada ya kupata taarifa za kina.
Nabii Shepherd Bushiri na mke wake Mary, wanakabiliwa na mashtaka ya ulaghai na utakatishaji wa fedha nchini Afrika Kusini.
Wawili hao walitoroka nchini Afrika Kusini wiki liyopita na kujisalimisha kwa polisi nchini Malawi baada ya Afrika Kusini kutoa kibali cha kukamatwa kwao.
Kupitia televisheni ya eneo, Rais Ramaphosa amesema tukio la wawili hao kutoroka "halikutakiwa kutokea".
"Bila shaka tutachukua hatua," Rais alijibu alipoulizwa ikiwa serikali inapanga kufanya lolote.
Baadhi ya taarifa zinasema kuwa muhubiri huyo aliyejitangaza mtume pamoja na mke wake walitoroshwa nchi humo kwa njia haramu na genge la watu ambalo linahusika na uuzaji wa magari yaliyoibwa nchini Afrika Kusini na kupelekwa Malawi.
Pia kuna baadhi ya vyombo vya habari Afrika Kusini vilivyosema kuwa nabii huyo alitoroka kwa kutumia ndege ya rais.
Hata hivyo serikali zote mbili zimekanusha madai hayo.
PRINCIPAL PLANNING OFFICER II Transfer Vacancies at Mwalimu Nyerere Memorial Academy
The Mwalimu Nyerere Memorial Academy invites application from suitably qualified Public Servants who wish to transfer to the Mwalimu Nyerere Memorial Academy. Establishment of the Academy The Mwalimu Nyerere Memorial Academy (MNMA) is a public higher learning institution which was established by an Act of Parliament No. 6 of 2005. The Origin of the Mwalimu […]
The post PRINCIPAL PLANNING OFFICER II Transfer Vacancies at Mwalimu Nyerere Memorial Academy appeared first on Udahiliportal.com.
ASSISTANT LIBRARIAN TRAINEE Transfer Vacancies at Mwalimu Nyerere Memorial Academy
The Mwalimu Nyerere Memorial Academy invites application from suitably qualified Public Servants who wish to transfer to the Mwalimu Nyerere Memorial Academy. Establishment of the Academy The Mwalimu Nyerere Memorial Academy (MNMA) is a public higher learning institution which was established by an Act of Parliament No. 6 of 2005. The Origin of the Mwalimu […]
The post ASSISTANT LIBRARIAN TRAINEE Transfer Vacancies at Mwalimu Nyerere Memorial Academy appeared first on Udahiliportal.com.
PERSONNELS ADMINISTRATIVE OFFICER II Transfer Vacancies at Mwalimu Nyerere Memorial Academy
The Mwalimu Nyerere Memorial Academy invites application from suitably qualified Public Servants who wish to transfer to the Mwalimu Nyerere Memorial Academy. Establishment of the Academy The Mwalimu Nyerere Memorial Academy (MNMA) is a public higher learning institution which was established by an Act of Parliament No. 6 of 2005. The Origin of the Mwalimu […]
The post PERSONNELS ADMINISTRATIVE OFFICER II Transfer Vacancies at Mwalimu Nyerere Memorial Academy appeared first on Udahiliportal.com.