Monday, 9 November 2020

Rais Dkt. Mwinyi ateua Makamu wa Pili wa Rais

 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemteua Hemed Suleiman Abdulla kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee imeeleza kwamba Rais Dkt. Hussein Mwinyi amemteua Hemed Suleiman Abdulla kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa mujibu wa uwezo aliyopewa chini ya Kifungu Namba 39 (1) na 39 (2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Kabla ya Uteuzi huo Hemed Suleiman Abdulla alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.

Uteuzi huo umeanza leo tarehe 08 Novemba, 2020.


 


Share:

DIWANI MTEULE AFARIKI DUNIA KWA KUTEKETEA KWA MOTO NDANI YA NYUMBA


Picha haihusiani na habari hapa chini

Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV- Pwani

DIWANI Mteule wa Kata ya Kikongo wilayani Kibaha Vijijini katika Mkoa wa Pwani Fatma Ngozi pamoja na mjukuu wake mwenye umri wa miezi kati ya saba na nane Ajivin Hamis wamefariki baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kuteketea kwa moto usiku wa kuamakia leo Novemba 9,2020.

Tukio la kuungua kwa nyumba hiyo na kusababisha vifo hivyo limetokea saa nane usiku wa kuamkia leo katika eneo hilo ambapo mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Michuzi TV na Michuzi Blog kwamba mbali ya kufariki kwa diwani mteule na mjukuu wake watu wengine watano wameokolewa kutoka kwenye nyumba hiyo.

Wamesema chanzo cha kuungua kwa nyumba hiyo bado hakijafahamika ingawa baadhi ya mashuhuda wanasema huenda ikawa imeungua kutokana na hitilafu ya umeme.Hata hivyo bado haijafahamika kilichosababisha kuungua kwa nyumba hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba uchunguzi zaidi kubaini chanzo cha moto huo ambao umesababisha vifo hivyo ili kubaini ukweli ,hivyo bado wanachunguza na watakapokamilisha uchunguzi watatoa taarifa.

Amesema maiti zimehifadhiwa katika Hospitali Mlandizi wakati wakiendelea na uchunguzi na baada ya hapo watakabidhi kwa ndugu kwa ajili ya shughuli za mazishi. Kwa upande wa majeruhi waliokolewa kwenye nyumba hiyo wanaendelea kupatiwa matibabu Hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha.

Hata hivyo ameomba wananchi kutoa ushirikiano na yoyote mwenye taarifa zitakazosaidia kukamilika kwa uchunguzi wa tukio hilo ni vema akaziwasilisha katika jeshi hilo wazifanyie kazi.Alipoulizwa chanzo cha moto huo amejibu ni mapema mno, wakikamilisha uchunguzi watafahamu kilichosababisha. 

CHANZO - MICHUZI BLOG
Share:

RAIS MAGUFULI AWATULIZA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WENYE WASIWASI WA KUTUMBULIWA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali katika Ikulu ya Chamwino mara baada ya kumuapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Lubango Kilangi leo tarehe 09 Novemba 2020. 
***
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amewataka watendaji ndani ya serikali kuchapa kazi na kuachana na wasiwasi wa kuhisi atawaondoa.

Magufuli ameyasema hayo leo Novemba 9, 2020 kwenye hotuba yake baada ya kumwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali Prof. Adelardus Kilungi Ikulu Chamwino, jijini Dodoma.

"Wakuu wa mikoa na wilaya msiwe na wasiwasi na inawezekana pasitokee mabadiliko yoyote labda kwa atakayestaafu au atakayefanya mambo ya hovyo, kama nilikuteua uwezo si bado ni ule ule najua wananisikia wachape kazi wasipochapa kazi shauri yao'', amesema",amesema Magufuli.

"RC unakuwa na wasiwasi gani labda kama 'performance' yako ilikuwa haifanyi kazi vizuri, nashangaa napata vimeseji kwamba Mh Rais nimejitahidi katika kipindi changu, kana kwamba kipindi chake nilimwambia kinaisha baada ya mimi kuapishwa", - ameongeza Rais Magufuli.
Share:

RAIS MAGUFULI AMUAPISHA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Lubango Kilangi alipokuwa akila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja wa Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya hafla fupi ya Uapisho wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Lubango Kilangi leo tarehe 09 Novemba 2020 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Lubango Kilangi muda mfupi baada ya kumuapisha leo tarehe 09 Novemba 2020 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Lubango Kilangi muda mfupi baada ya kumuapisha leo tarehe 09 Novemba 2020 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali katika Ikulu ya Chamwino mara baada ya kumuapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Lubango Kilangi leo tarehe 09 Novemba 2020. 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka mara baada ya hafla fupi ya Uapisho katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 09 Novemba 2020. PICHA NA IKULU
Share:

RAIS WA ZANZIBAR DK. HUSSEIN MWINYI AMTEUA ABDULLA KUWA MAKAMU WA PILI WA RAIS



Share:

DIJACSON LOYAL ALAMBA DILI LA UBALOZI 'MAZIWA HASWA'

 

Musician Dijacson Loyal


 Mwanamuziki Dijacson Loyal ajipatia dili nono la kuwa balozi wa Kampuni ya Hai Dairy Limited kutoka mkoani Kilimanjaro, kampuni ambayo imekuwa ikijihusisha kwa muda mrefu na bidhaa za maziwa na yoghut.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw. Donath Mboya akimkabidhi star huyo uwakilishi wa kutangaza bidhaa ya maziwa kutoka  kampuni hiyo amesema kwa muda mrefu wamekuwa wakimtizama Kijana huyo hit maker wa ngoma ya 'Corona Virus Tutakumaliza' na Kuvutiwa na harakati zake za kisanaa huku akiwashawishi vijana wengi kujituma na kuwekeza katika ujasiriamali na kujenga uzalendo katika mafanikio ya kujiajiri wenyewe.

Dijacson Loyal

Akizungumza baada ya kukabidhiwa jukumu la kuwa balozi wa Bidhaa ya Maziwa ya Kampuni hiyo Mwanamuziki huyo Amesema kuwa lengo kubwa siku zote ni kuitangaza Taifa na kuitangaza Taifa ni kuwaambia watu kuhusu yanayopatikana Tanzania ikiwa ni pamoja na makampuni bora yaliyojizatiti kuendeleza uchumi wa nchi na watu wake ikiwa ni katika kuchangia kukuza pato la Taifa na kutoa ajira kwa wananchil.

"Mimi niwaombe wananchi popote Mlipo tupendeni vya kwetu kuanzia leo jitafutie maziwa Haswaa na ujionee ladha halisi ya maziwa ya Kitanzania maziwa haswa , maziwa origina kwa afya bora ya familia , mie najivunia kuyatumia kila siku yananipa nguvu na  yananipa afya pia , tunapolitangaza taifa lolote tunaeleza yaliyopo ndani ya taifa mazuri yakuenziwa ikiwa ni pamoja na makampuni ya nyumbani yanayojituma na kutoa ajira kuchangia pato la taifa na kuhimili maendeleo ya nchi kwa ujumla wake 

niwaombe ndugu Watanzania na watu wote duniani tuweni na shauku na hamu ya kizalendo kwa kuvisapot taasisi zetu zawa kwakuwa ndivyo vyenye uchungu na dhamira ya dhati ya kuiendeleza nchi..." Alisema Dijacson Loyal .

Staa huyo tangu ameachia wimbo wake wa 'Corona Virus Tutakumaliza' amekuwa katika ubora wake huku akijizolea mashabiki kote ulimwenguni huku nyimbo hiyo aliyoiachia May 11 2020 ikifanya vizuri kote ulimwnguni na kuvunja rekodi ya kujikusanyia streams zaidi ya millioni moja katika kipindi kisichozidi saa 24 baada ya kuachia nyimbo hiyo (1,000,000 Streams worldwide in les than 24 hours..) .

Share:

DIJACSON LOYAL 'S BIOGRAPHY

 

Dijacson Loyal
 
Dijacson John Boniface Karengi Sr (born 22 October 1995) popularly known by his stage name Dijacson Loyal is a pop recording artist and entrepreneur from Tanzania , Africa.
He was born at Haydom Lutheran Hospital (HLH) The Hospital in the North of Tanzania, Near Arusha City. in his early music struggles Dijacson performed in some events inclunding Gongali Model Biogas Trainining on June 2020. click here to view his early performance



Dijacson Loyal 's 
'Corona Virus' 
Artwork
 
Dijacson Loyal is considered influential among his fans, and is said to be the most loved and decorated artiste of all the time in the world. He first Created his debut song in campaigning the fights against Covid-19 ‘Corona Virus Tutakumaliza ’ which was released on May 11 2020 worldwide. The song Scored over 1,000,000 Streams within Hours just from the release time. click here to see links to the song 'Corona Virus Tutakumaliza'


Dijacson carrying 
Nanofilter Water 
bottle after signing 
a deal with 
Gongali Model Ltd
in 2020.
On June 2020 Dijacson was given Nanofilter endorsement and took a deal to be a brand ambassador for Gongali Model Ltd representing their water community helping program 'NANOFILTER'


And on July 15 2020 Dijacson got Hai Dairy Investment endorsement for branding their dairy product 'Maziwa Haswa' , The Company invested on donating to Dijacson 's album launch and later five(5)singles before the contract ends.

Dijacson Loyal 
showing 
'Maziwa Haswa' 
bottle to the press 
conference.
 
The Hai Dairy Investment and Dijacson Loyal are working together until their contract ends, and here is the more information about the endorsement click here to read about the Contract deal when Dijacson Loyal was announced to be a brand Ambassador of 'Maziwa Haswa'

In 2013 Dijacson Completed his Secondary studies in Chief Sarwat Secondary School at Mbulu District , after high school studies Dijacson was too much interested in Media activities he liked working in the media stations as radio presenter or TV broadcaster because that was his childhood dreams.
before falling to the media activities Dijacson Joined some Computer studies institutions and later Journalism college where he got the media works concepts, but the challenge was how to get employed with a contract and build and rise his broadcasting carrier.

For while Dijacson suffered collecting news from the rural areas for some radio stations and online content creators.

On June 2018 Dijacson signed a Mini-wage contract and get paid a little wage in huge responsibilities at Arise and Shine Ministries working for their Local radio station Idea FM Radio 95.7 in Arusha region.

At the end of 2018 Dijacson officially moved to music as music was his life parts because when he was a young Child Dijacson loved singing some hip-hop freestyles and most interested in some catholic songs.
Dijacson Loyal
After leaving Media industry Dijacson puts his all efforts and works hard day and night for his music talent and many times he seems to get inspired by World Mega Star Diamond Platnumz , and as we are talking today Dijacson stays a number one fan of Diamond and lives him as all time role model.
Early 2020 Dijacson Announced to leave his Old Carrier for officially working in his music talent , he also announces to release his new song on April 2020 where he told media houses that the track he was expecting to release was officially what gonna introduce his talent to the Music industry in world.
A photo shows Dijacson Loyal
having a photopose with a
Nanofilter  re-usable bottle
Later , Dijacson Loyal Confirmed to release new first song 'Bendera' on April 13 2020 however the plan canceled due to the invasion of 'Covid-19' 'Corona Virus' , And after the pandemic Dijacson Loyal wrote a song about the fights of the world Governments against Covid-19 and named the song 'Corona Virus Tutakumaliza' after releasing the track on May 11 Dijacson went back to his old project 'bendera' for it to get released soon as he told some Media stations, Dijacson says in his tweet ‘I know you guys are ready for new project , Bendera is on the way ahead, get yours speakers ready for the play ……’.



Here are the major ways to catch Dijacson Loyal on Social Media and the web
Share:

BILIONI 66.8 KUTUMIKA UJENZI WA BARABARA YA TANGA HADI PANGANI

Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) Mkoa wa Tanga Mhandisi Alfred Ndumbaro akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani.


UJENZI wa kiwango cha lami wa barabara ya Tanga hadi Pangani yenye urefu wa kilomita 50 unatarajiwa kutumia bilioni 66.8 na utamalizika kwa kipindi cha miaka miwili.

Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) Mkoa wa Tanga Mhandisi Alfred Ndumbaro alisema kwamba tayari mkandarasi alikwisha kupatikana wa kampuni kutoka nchini China ya Chicco na amekwisha kuripoti eneo la kazi.

Alisema mkandarasi huyo hivi sasa anaendelea na maandalizi ya kujenga kambi ya wahandisi ambao watasimamia mradi huo na wafanyakazi wake katika maeneo ya Tongoni na Geza.

“Kama Serikali ilivyohaidi kujenga kiwango cha lami Barabara ya Tanga hadi Pangani kilomita 50 na tayari mkandarasi amekwisha kupatikana na amekwisha ripoti eneo la kazi kampuni kutoka china inatiwa Chicco”Alisema Meneja huyo.

Meneja huyo alisema tayari mkandarasi huy ameanza kusafisha kilomita 14 ambazo hazina matatizo na fidia na yupo eneo la kazi anaendelea kufanya kazi wakati huo anaendelea kujenga kambi za wahandisi pale Tongoni huku akimalizia kambi nyengine Geza .

Alieleza pia baadhi ya mitambo inaendelea kuletwa huku akiwataka wananchi kwenye maeneo yote washirikiana mkandarasi kuweza kumsaidia ili asiibiwe vifaa au mafuta wakati akitekeleza majukumu yake.

“Ujenzi huu pia utatoa fursa za ajira kwa wakazi wa Tanga wakati mradi huo ukianza ajira madereva, vibarua na tumemwambia achukua wananchi wanaoishi kwenye maeneo ambapo mradi unatekelezwa”Alisema Meneja huyo.
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu November 9



Share:

Sunday, 8 November 2020

TBS YATOA VYETI NA LESENI 177 KWA WAZALISHAJI WA BIDHAA NCHINI

Mkurugenzi Mkuu TBS, Dkt.Athuman Ngenya akizungumza katika hafla ya Utoaji vyeti na leseni kwa wazalishaji bidhaa na wajasiriamali wadogo iliyofanyika Makao Makuu ya Shirika la Viwango Tanzania TBS Jijini Dar es Salaam Wazalishaji wa bidhaa na wajasiriamali nchini wakiwa kwenye hafla ya Utoaji leseni na vyeti kwa wazalishaji waliokidhi Viwango.Hafla hiyo imefanyika leo hii Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu TBS, Dkt.Athuman Ngenya akitoa vyeti na leseni kwa wazalishaji wa bidhaa zilizokidhi Viwango pamoja na wajasiriamali.Hafla hiyo imefanyika leo hii Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Dar es Salaam.

****************************************

Shirika la Viwango Tanzania TBS, limetoa vyeti na leseni 177 kwa Wazalishaji wa bidhaa na wajasiriamali wadogo ambao bidhaa zao zimethibitishwa ubora baada ya kukidhi matakwa ya viwangokwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba 2020.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu TBS, Dkt.Athuman Ngenya amesema vyeti na leseni 177 zilizotolewa kati ya hizo,  leseni 1 ni ya mfumo wa usimamizi ubora na leseni, 146 za alama ya ubora na 30 ni vyeti kwa bidhaa zisizo na viwango vya Tanzania.

“Kati ya leseni na vyeti vilivyotolewa, 88 ni vya wajasiriamali wadogo. Vyeti na leseni hizo ni za bidhaa za vyakula, vipodozi, vifaa vya ujenzi, vilainishi, vitakasa mikono, vifaa vya umeme, vifaa vya makenika, magodoro, vibebeo pamoja na vifungashio”. Amesema Dkt.Ngenya.

Aidha, Dkt.Ngenya amesema kuwa majengo ya kuzalisha, kuhifadhi au kuuzia chakula na vipodozi pamoja na vyombo vinavyobeba bidhaa hizo (Mfano: magari ya kubebea vyakula) ni lazima visajiliwe na TBS ndipo viruhusiwe kutumika.

“Kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai mpaka Septemba mwaka huu tumekwisha sajili majengo 2139 ya biashara na ya kuhifadhia bidhaa za vyakula na vipodozi. Pia kwa kipindi hicho tumeweza kusajili jumla ya bidhaa 533 za vyakula na vipodozi”. Amesema Dkt.Ngenya.

Pamoja na hayo Dkt.Ngenya amewaasa wadau hao wa viwango kuendelea kuzalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya viwango kwa mustakabali wa afya na mazingira ya watumiaji kwa ujumla.

Share:

Kidato cha pili kuanza mtihani kesho


Jumla ya watainiwa 646,148 wa kidato cha pili kesho Novemba 9, wanatarajiwa kuanza mtihani wa upimaji wa kitaifa wa kidato cha pili huku kidato cha Nne wakianza mtihani wa taifa Novemba 23 hadi Desemba 11, mwaka huu.

Akitoa ratiba hiyo leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza Mitihani la Tanzania (NECT), Dk. Charles Msonde amesema mtihani wa upimaji wa darasa la nne unatarajiwa kufanyika kwenye shule 4,948 za Sekondari Tanzania Bara na kwamba maandalizi yote yamekamilika.

Amesema kati ya watainiwa hao, wavulana ni 301,831 sawa na asilimia 46.71 huku wasichana wakiwa 344,317 sawa na asilimia 53.29.

“Mitahini hii inanza kesho Novemba 9 hadi 20 mwaka huu, aidha, wapo watainiwa wenye mahitaji maalum 731 na kati yao 406 ni wenye uoni hafifu, 55 ni wasiona, watatu ni wenye ulemavu wa kusikia na 267 ni wenye ulemavu wa viungo vya mwili.

“Mwaka 2019 idadi ya watainiwa waliosajiliwa walikuwa 609,502, hivyo kuna ongezeko la jumla ya watainiwa 36, 646 sawa na asilimia 5.7 kwa mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana,”  amesema Dk. Msonde.

Amesema mtihani wa taifa wa kidato cha Nne na Maarifa(QT) utafanyika Novemba 23 hadi Desemba 11, mwaka huu katuka jumla ya shule za sekondari na vituo vya mitihani 6,727 Tanzania Bara na Zanzibar.

“Jumla ya watainiwa 490,103 wamesajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha Nne mwaka huu ambapo kati yao watainiwa wa shule ni 448,164 na watainiwa wa kujitegemea ni 41,939.

“Kati yao watainiwa wa shule ni 448,164 waliosajili, wavulana ni 213, 553 sawa na asilimia 47.7 na wasichana ni 234,611 sawa na asilimia 52.3.

“Aidha, wapo watainiwa wenye mahitaji maalum 893 na kati yao 425 ni wenye uoni hafifu , 60 ni wasioona, 186 wenye ulemavu wa kusikia na 222 ni wenye ulemavu wa viungo vya mwili,” alisema Dk. Msonde.


Share:

Viongozi Mbalimbali Duniani Waendelea Kumpongeza Joe Biden Kwa Ushindi


 Ushindi wa Joe Biden umepongezwa na viongozi mbalimbali duniani, wengi walieleza matumaini ya ushirikiano baina ya nchi baada ya miaka minne ya kuanguka kwa diplomasia chini ya Rais Donald Trump.

Wakati Trump akiendelea kupinga matokeo ya uchaguzi uliompa ushindi Biden, viongozi wengi duniani wameeleza wazi kuwa wanaunga mkono ushindi wa Biden na mgombea mwenza Kamala Harris.

Biden wa chama cha Democrats  amechaguliwa Rais wa 46 wa Marekani  baada ya kuhudumu kwa miaka 36 katika Baraza la Seneti la Marekani na miaka minane kama makamu wa Rais chini ya Rais wa zamani Barack Obama.

“Hongera! Nakutakia heri na mafanikio kutoka ndani ya moyo wangu,” amesema Angela Merkel, Kansela wa Ujerumani.

“Urafiki wetu hauna mfano pale tunapokabiliana na changamoto zetu kwa kipindi hiki,” alisema Markel katika ujumbe wa Twitter uliotolewa na Msemaji wa Serikali ya Ujerumani.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron ametuma salamu kupitia Twitter kuwa: “Wamarekani wamechagua Rais wao.

Hongera sana @JoeBiden na @KamalaHarris! Tunayo mengi ya kufanya kukabiliana na changamoto za sasa. Tushirikiane!”

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson pia amempongeza Biden na Harris kwa mafanikio yao ya kihistoria.

“Marekani ni mshirika wetu muhimu na ninatazamia kufanya kazi kwa karibu katika vipaumbele vyetu, kuanzia mabadiliko ya tabia nchi kwenda kwenye biashara na usalama,” alisema Johnson.

Waziri Mkuu wa Ireland, Michael Martin alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuandika katika twitter kuhusu uchaguzi. “ napenda kumpongeza Rais mteule wa Marekani @JoeBiden. Joe Biden amekuwa rafiki wa kweli wa nchi yake kipindi chote cha maisha yake na ningependa kufanya naye kati katika kipindi kijacho. Napenda pia kumkaribisha tena nyumbani muda mazingira yatakaporuhusu.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Ugiriki, Kyriakos Mitsotakis kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika: Hongera kwa Rais mteule wa Marekani @JoeBiden. Joe Biden amekuwa rafiki wa kweli wa Ugiriki na ninatumaini kwamba katika kipindi chake urafiki kati ya nchi zetu utashamiri."

Naye Rais wa Iraq, Barham Saleh alituma salamu zake za pongezi akimweleza Biden kama rafiki na mdau wa kuaminika  katika ujenzi wa Iraq iliyo bora. (Tunatazamia kufanya kazi pamoja kufanikisha malengo yetu na kuimarisha amani na usalama katika Mashariki ya Kati.”

Naye Rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri, alisema “Misri , ikiwa nchi ya Kiarabu yenye watu wengi, inatazamia kuendelea makubaliano ya nchi yetu na Marekani kwa manufaa ya nchi na zote mbili  na watu wake.


Share:

Mtumishi Hospitali Ya Rufaa Shinyanga Mbaroni Tuhuma Za Wizi Wa Vifaa Tiba


 JESHI la Polisi Mkoa wa Shinyanga linawashikilia watu wawili akiwemo Muuguzi wa Hospitali ya Serikali ya Rufaa mkoani Shinyanga wakituhumiwa kwa makosa ya wizi wa vifaa tiba vya hospitali hiyo ya mkoa vyenye thamani ya sh. milioni 26.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga ACP, Debora Magiligimba amewataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Madaraka Joseph (32) mkazi wa Mageuzi kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga ambaye pia ni muuguzi katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.

Mtuhumiwa mwingine aliyekamatwa ametajwa kuwa ni Suka Charles (42) mkazi wa Mtaa wa Buzuka Manispaa ya Shinyanga ambapo pia anamiliki zahanati ya iliyopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Akifafanua zaidi Kamanda Magiligimba amesema mnamo Oktoba 13, mwaka huu saa 12.00 jioni kulitokea wizi wa mashine mbili za kuangalia wagonjwa katika chumba cha upasuaji aina ya EDAN 1MB na DATA SCOP 1 zenye thamani ya shilingi milioni 26.

Kamanda Magiligimba amesema baada ya kutokea kwa wizi huo, Jeshi la Polisi lilianza kufanya uchunguzi ambapo lilibaini kuwa mtuhumiwa Madaraka Joseph ambaye ni mtumishi kwenye chumba cha upasuaji katika Hospitali ya mkoa ndiye aliyeiba vifaa tiba hivyo.

“Tulibaini baada ya kuiba vifaa hivyo alikwenda kuviuza kwa Suka Charles kwa makubaliano ya shilingi 4,000,000 na alitanguliziwa kiasi cha shilingi 2,000,000 hata hivyo tulimkamata Suka baada ya kumfanyia upekuzi nyumbani kwake maeneo ya Mhongolo wilayani Kahama na kufanikiwa kukamata vifaa hivyo,” alieleza Magiligimba.

Amesema pia Polisi walikamata vifaa vingine vinavyotumiwa na vifaa hivyo ikiwemo, Patient monitor S/N 301237 – M16 CO9160006-01, Patient monitor S/N PG 63700-B2, BP Machine Accessories (5), Cable wires Accessories (7), Medical molecular sieve, Oxygen Concentrator (1) Serial no. 598 na Oxygen Concentrator Intesty S/N 601-1.

Kamanda Magiligimba amesema watuhumiwa wote wawili wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika ambapo ametoa wito kwa watumishi wa umma kuacha tabia ya wizi wa mali za umma zinazosababishwa na tamaa ya mafanikio ya muda mfupi.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger