Wednesday, 1 July 2020

KIWANDA CHA KUSAFISHA DHAHABU MBIONI KUANZA JIJINI DODOMA



Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila (katika) akikagua moja ya nyaraka katika kiwanda cha Eyes Of Africa kilichopo jijini Dodoma alipofanya ziara yake ya kikazi, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Eyes of Africa Ferenc Molnar na kushoto ni Kamishina Msaidizi Sehemu ya Uongezaji Thamani, Bertha Luzabiko.
  Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila (kulia) akielekezwa kifaa cha kukatia dhahabu na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Eyes of Africa Ferenc Molnar

Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila (kushoto) akipewa maelezo na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Eyes of Africa Ferenc Molnar.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila (katika) akiongea jambo na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha Eyes Of Africa, kushoto ni Kamishina Msaidizi Sehemu ya Uongezaji Thamani, Bertha Luzabiko






Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila (kulia) akiwa kwenye picha ya pomoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Eyes of Africa Ferenc Molnar (katikati) na kushoto ni Kamishina Msaidizi Sehemu ya Uongezaji Thamani, Bertha Luzabiko



Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila (kulia) akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Eyes of Africa Ferenc Molnar.



Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila (kushoto) akipewa maelezo na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Eyes of Africa Ferenc Molnar.



Na Tito Mselem Dodoma,



Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, amefanya ziara ya kikazi katika Kiwanda cha Kusafisha Dhahabu ( Refinery) cha Eyes Of Africa Ltd kilichopo katika eneo la Area D pembezoni mwa Uwanja wa Ndege wa Jiji la Dodoma.

Ziara hiyo yenye lengo la kukagua hatua za ujenzi uliofikiwa na kiwanda hicho ambacho ni kiwanda cha kwanza nchini cha kusafisha madini ya dhahabu na fetha.

Kiwanda cha Eye Of Africa kinachomilkiwa na Ferenc Molnar ambaye ni raia wa Yugoslavia ni miongoni mwa kampuni nne zilizopewa leseni ya usafishaji wa madini ya dhahabu (Gold Refinery Licence) hapa nchini, kampuni nyingine ni pamoja na STAMICO-Mwanza, Geita Gold Refinery na African Ayes-Geita.

Katika ukaguzi huo, Prof. Msanjila aliambatana na Kamishina Msaidizi Sehemu ya Uongezaji Thamani, Bertha Luzabiko ambopo walifurahishwa na hatua iliyofikiwa na kampuni hiyo.

Prof. Msanjila amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Eye Of Africa Ferenc Molnar kuandika barua kwa Serikali kupitia Wizara ya Madini kuinisha mambo muhimu yanayotakiwa ili serikali isaidie katika kufanikisha mahitaji ya Kampuni hiyo.

Aidha, Prof. Msanjila, ameiahidi kampuni hiyo, kuhakisha inapata wateja kutoka sehemu mbalimbali hususan wachimbaji wadogo mara kampuni hiyo itakapo anza uzalishaji.

Pia, Prof. Msanjila amesema, mara baada ya viwanda vya usafishaji madini ya dhahabu kuanza kazi, Serikali itasitisha usafirishaji wa dhahabu ghafi kwenda kusafishwa nje ya nchi na badala yake madini ghafi yote yatasafishiwa nchini kabla hayajasafirishwa kwenda nje ya nchi.

Wakati huo huo, Prof. Msanjila amempongeza Molnar kwa hatua nzuri aliyoifika ikiwemo ufungwaji wa mashine mbalimbali za kusafisha madini ya dhahabu katika kiwanda hicho.

Kwa upande wake, Mkrugenzi Mtendaji wa Eye Of Afrika Ferenc Molnar, amesema mara baada ya kuanza kwa uzalisha kampuni yake itakuwa na uwezo wa kuzalisha kilo 40 za dhahabu kwa siku na itamtoza mteja asilimia 0.5 ya gharama ya mzigo utakaosafishwa kiwandani hapo.
Share:

TEKNOLOJIA KURAHISISHA USAHILI YAJA TANZANIA


July 1, 2020, Dar es Salaam, Tanzania
Kampuni ya usahili Tanzania imeunda na kuzindua mfumo wa kupima uwezo na ufanisi wa waajiriwa kupitia teknolojia.

 Zana hiyo iliyopewa jina la ‘Skills Assessment Tool’ au ‘Zana ya Tathmini ya Ujuzi’ imeundwa kwa lengo la kuwapunguzia waajiri changamoto wanazokumbana nazo katika mchakato wa usahili hasa katika kupitia mamia ya CV wakati wa mchakato wa kuajiri. 

Teknolojia ya Skills Assessment Tool inawezesha waajiri kuchuja maombi ya nafasi ya kazi na kuwawezesha kupata waombaji wachache pekee waliokidhi vigezo vya kazi husika. 

Waombaji watafanyiwa tahmini ya awali katika mchakato wa usahili kupitia Zana ya Tathmini ya Ujuzi, teknolojia ya tahmini ambayo hupima uwezo wa waombaji zaidi ya ilivyo kwenye wasifu (CV) zao. 

Zana hii huchuja uwezo wa msingi na stadi ngumu zinazohitajika kwa jukumu fulani lililotangazwa.

 Matokeo ya tahmini huwasilishwa kwa mwajiri kupitia mfumo wa kufuatilia waombaji (ATS), dashibodi ya mwajiri ambayo inayomwezesha kuchuja waajiri bora zaidi kulingana na vigezo tofauti, pamoja na alama za majaribio.

Akifafanua kuhusu teknolojia hii, Mkurugenzi Mtendaji wa BrighterMonday Tanzania Reshma Bharmal-Shariff amebainisha namna ambavyo waajiri wanavyojikuta katika wakati mgumu hasa pale wanapozungukwa na idadi kubwa ya waombaji wa kazi wasio na sifa stahiki. 

“Teknolojia imerahisisha upatikanaji wa taarifa na michakato ya kuomba ajira, hii imepelekea kwamba mtu yeyote anaweza kuomba kazi yoyote bila kujali vigezo mahsusi vya kazi husika. Hii inawasababishia maumivu Maafisa Rasilimali Watu kwani wanajikuta wana CV nyingi za kufanyia tathmini kabla ya kupata waombaji wachache watakaofaa kwa usahili. " Alielezea Reshma. 

"Hii ndio sababu tuliona haja ya kuwasaidia waajiri kutambua ni mwombaji gani mwenye ujuzi stahiki wa nafasi hiyo. Mwajiri sio lazima apitie mamia ya CV tena, kutafuta mwajiri fulani. Waombaji wenye sifa wapo, na teknolojia hii inampa uwezo mwajiri kumpata mwajiriwa sahihi kwa kubonyeza vitufe vichache katika kompyuta yake. Kupitia zana hii, mwajiri anaweza kutazama alama za mwombaji na vigezo vingine kama vile kiwango cha elimu na uzoefu. Kwa njia hii, mwajiri anaweza kulinganisha ustadi, sifa, na viwango vya uzoefu kwa muda mfupi",Reshma Bharmal-Shariff alihitimisha. 

Zana hii imeleta ufanisi mkubwa kwa waajiri nchini Tanzania kwani sasa wanaweza kuchagua waombaji wenye uwezo zaidi bila upendeleo, na kwa kutumia vigezo vinavyokidhi mahitaji ya mwajiri husika.

Share:

Programme Manager at Norwegian Church Aid

Job Summary Organization: Norwegian Church Aid; Position: Programme Manager Minimum Qualification: Bachelor Experience Level: Management level Experience Length: 5 years Job Description Background: Norwegian Church Aid (NCA) is a diaconal organization mandated by churches and Christian organizations in Norway to work with people around the world to eradicate poverty and injustice. In Tanzania, NCA works mainly with Faith […]

The post Programme Manager at Norwegian Church Aid appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Consultant TOR-Development of Climate Smart Agriculture technical manual and training aids

Job Summary The CRAFT project, in an effort to provide appropriate tools for farmers to adapt climate smart farming practices for increased productivity and income in an inclusive and climate resilient way; is seeking the services of a consultant firm to review and develop-without reinventing the wheel- climate smart agriculture training manuals for the following […]

The post Consultant TOR-Development of Climate Smart Agriculture technical manual and training aids appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Finance Manager – HP+ Tanzania

Finance Manager – HP+ Tanzania Company Overview: Palladium is a global leader in the design, development and delivery of Positive Impact – the intentional creation of enduring social and economic value. We work with foundations, investors, governments, corporations, communities and civil society to formulate strategies and implement solutions that generate lasting social, environmental and financial […]

The post Finance Manager – HP+ Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Human Resources Officer at Search for Common Ground

Responsible for coordination of Swahili Coast human resource activities in the areas of recruitment, remuneration and benefits administration, employee relations, training and development, performance management, employee data management and local HR policy formulation and implementation. Essential Duties and Responsibilities Responsible for dministration and implementation of global HR practices that support the global strategy In coordination […]

The post Human Resources Officer at Search for Common Ground appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Talented Music & Audio Producer at Alpha Records Co. Ltd

Position: Talented Music & Audio Producer Alpha Records Co. Ltd Job Summary Alpha Records is looking for a talented & Creative Audio and Music Producer, with a vision to create great music for Tanzania & the World. Experience Level: Mid level Experience Length: 3 years Job Description We are looking for a talented & Creative Audio […]

The post Talented Music & Audio Producer at Alpha Records Co. Ltd appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Zitto Kabwe amkaribisha Benard Membe ACT-Wazalendo

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, amemkaribisha aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Mwanachama wa CCM Bernard Membe, kuunganisha nguvu kupitia vyama mbadala hii ni mara baada ya yeye kufukuzwa uanachama ndani ya CCM.

Akizungumza jana  na mamia ya wafuasi wa chama hicho, katika eneo la Njia Nne, wilayani Kilwa, mkoani Lindi, Zitto alisema, anamkaribisha Membe ndani ya ACT- Wazalendo kwa mikono miwili

“Tunamtaka Membe kujiunga na chama chetu, ili kuihami demokrasia na kupigania haki za wananchi,” alieleza Zitto na kuongeza, “mtu yoyote anayeona ukandamizaji haufai, anapaswa kuungana na wenzake, kupinga vitendo hivyo.

"Ninajua bado anatetea haki yake ya uanachama huko ni hatua sahihi, hata hivyo muda wa kuleta mabadiliko katika nchi umewadia, ninamsihi afanye maamuzi ya kuunganisha nguvu kupitia vyama mbadala"


Share:

MBUNGE UMMY ALIVYOPAMBANA KUZIRUDISHA KWENYE CHATI KLABU ZA COASTAL UNION NA AFRICAN SPORTS

 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kushoto akipokea tuzo ya heshima kutoka kwenye Mwenyekiti wa Baraza la wazee la Klabu ya Coastal Union ikiwa ni kutambua mchango wake kuisaidia timu hiyo wakati ilipopanda daraja na kurudi Ligi kuu.

 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM)kulia akigawa vifaa vya michezo kwa timu za soka mkoani Tanga zilizokuwa zikishirika Ligi ya Banda Cup msimu uliopita ambapo vifaa hivyo alivitoa yeye.


WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga katika akiwa na baadhi ya viongozi wa timu ya Coastal Union wakati akipokwenda kuwakabidhi kiwanja eneo la Maweni Jijini Tanga kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya City Plan Consultants (T) Limited Dkt Juma Mohamed .


 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto  na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu katikati akiwa na viongozi wengine pamoja na timu ambazo alizikabidhi vifaa vya michezo jezi kwa ajili ya kushiriki Mashindano ya Banda Cup msimu uliopita.
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto  na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu katikati akiwa na mashabiki wa timu ya Coastal Union wakihamasisha ushindi wa timu ya Coastal Union kwenye mechi zao za nyumbani katika Ligi Daraja la kwanza.

NA MWANDISHI WETU,TANGA.
 
 
UNAPOZUNGUMZIA mafanikio ya soka kwa Mkoa wa Tanga huwezi kuacha kulitaja jina la Ummy Mwalimu ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa huo (CCM) na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambaye amefanya kazi kubwa kurudisha heshima ya michezo.

Sie sote ni mashahidi kwamba bila juhudi kubwa ambazo alizifanya kwa kushirikiana na viongozi wengine wa mkoa huo mkoani Morogoro wakati timu ya Coastal Union ikitafuta tiketi ya kureja Ligi kuu ingekuwa ni ndoto wana Tanga kushuhudia michuano hiyo mikubwa hapa nchini ikichezwa mkoani hapa.


Bila kujali jambo lolote licha ya kuwa na shughuli za kitaifa alilazimika kuungana na wana michezo mkoani Tanga kupiga kambi mkoani Morogoro ili kuhakikisha anatimiza ndoto zake za kuhakikisha anaandika historia ya kuirudisha Ligi kuu timu hiyo Kongwe hapa nchini ambayo ilishuka daraja kabla ya kurejea tena.

Licha ya kuipandisha timu hiyo ikiwa mkoani Morogoro lakini alilazimika kuisindikisha hadi mkoani Tanga akiwa na msafara mkubwa wa magari huku akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella eneo la Pongwe huku akiendelea kuisapoti timu hiyo katika Nyanja mbalimbali.

Hakuna asiyejua juhudi kubwa ambazo amezifanywa kuhakikisha anapambana kwa hali na mali ili timu hiyo inarudi Ligi kuu baada ya kushuka daraja mara kadhaa na kupoteza mwelekeo ambapo aliamua kulivalia njuga suala hilo na kusimama kidete na kufanikisha ndoto yake.

Katika makala hii leo Nataka japo nikueleza jambo utambua kwamba unapomzungumzia Mbunge Ummy Mwalimu amefanya nini kwenye kulipata mafanikio soka la Mkoa wa Tanga mpaka limefikia hapo lilipo lakini pia ameendelea kuwa bega kwa bega na timu kongwe za mkoa huo ambazo zilikuwa na historia ya soka.

Tukianzia kwa Klabu ya Coastal Union “Wagosi wa Kaya” ambao mwaka 1988 waliandika historia mkoani Tanga kwa kuchukua Ubingwa wa soka nchini ambao mpaka sasa imekuwa ni klabu ambayo ikiingia katika kumbukumbu za mabingwa wa nchi hii huwezi kuacha kuizungumzia.

Salimu Bawaziri ni Mjumbe wa Kamati ya Mipango na Fedha katika timu ya Coastal Union anaeleza kwamba mchango wa Mbunge Ummy ndani ya timu hiyo ni mkubwa na hauwezi kusaulika kwani amekuwa mstari wa mbele kuwasaidia tokea wakiwa Ligi daraja la kwanza mpaka akahakikisha timu inapanda daraja kwa kushirikiana na viongozi.

“Nakumbuka wakati tukiwa kule mkoani Morogoro tunapotafuta tiketi ya kupanda daraja mara kwa mara alikuwa anakuja kukutana na wachezaji na viongozi kwa kutoa motisha na hamasa kwa wachezaji kwa lengo la kuhakikisha tunapambana na kurejea Ligi kuu hivyo mchango wake ni mkubwa sana mpaka tulipo sasa na bado amekuwa akitusaidia”Anasema Bawaziri.

Anasema licha ya viongozi wengi kusaidia lakini Mbunge Ummy aliweza kuibeba timu hiyo tokea kipindi timu hiyo inashiriki Ligi daraja la kwanza hapa nchini na hakuweza kuiacha pekee bali alikuwa akifika kambini kwa kuzungumza na wachezaji kuwapa motisha jambo ambalo limechangia kwa asilimia kubwa kuweza kurudi ligi kuu.

“Kwa kweli msaada ambao ametusaidia ni mkubwa na hatuwezi kuusahau kufanya jitihada kubwa kwetu lakini pia kuweza kutusaidia kuweza kupata uwanja eneo la Maweni lenye ukubwa wa mita 7632 mkubwa ambao tutaanza kuufanyia kazi ambao huu utakuwa ni chachu kubwa kwa maendeleo ya timu yetu”Anasema


Hata hivyo anasema kuwa watahakikisha wanakuwa bega kwa bega naye kila wakati kutokana na mchango wake mkubwa ndani ya timu hiyo na historia ambayo ameiweka itakayodumu kwa vizazi na vizazi kwani kila watakapotumia eneo hilo lazima watakumbuka jambo hili kubwa lilifanywa na mbunge Ummy.

Hata hivyo Mbunge Ummy anaeleza dhamira yake ya kusaka eneo hilo ambapo anasema kubwa zaidi ni kuisaidia timu hiyo katika mipango iliyokuwa nayo kuanza kwenda vema huku wakijipanga kwa hatua nyengine lakini kubwa kwa kuwa na eneo lake ambalo watalitumia katika matumizi mbalimbali ikiwemo uwanja wa kuchezea.

““Nataka niwaambie Coastal Union tutaendelea kuwa pamoja katika harakati zetu za kuwania Ubingwa wa Ligi kuu labda niwahaidi kuwatafutia wadau pia niwaambie bado tunaendelea kutafuta wadau na nihaidi hata ile block yenye square mita 9600 yenye thamani milioni 48 nitafue wadau ili waweze kupata eneo hilo”Anasema

Anasema atasaidia kutafuta wadau ili kupata eneo hilo ambalo litakuwa kwa ajili ya matumizi ya ujenzi wa Hosteli,Gym ya Mazoezi na Ukumbi wa sherehe wa Coastal Union kwa sababu watu wa Tanga wana fanya sherehe na kitchen party kila siku

“Labda ndugu zangu wapenzi wa soka na wana michezo wenzangu jambo hilo limewezekana kutokana na mshikamano uliopo baina ya viongozi na wanachama huku wakiwataka kuuendeleza ili kuweza kupata mafanikio makubwa siku zijazo kwenye michuano ya ligi kuu”

Mbunge Ummy hakuishia hapo lakini pia anasisitizia timu hiyo kufanya vizuri kwa timu hiyo ndio imekuwa sababu ya kuwavuta wadau ambao wameweza kuwasaidia katika masuala mbalimbali hivyo wachezaji na walimu wana kazi kubwa ya kuhakikisha wanajipanga vema kwa ajili ya kufanya vizuri.

“Lakini pia eneo hilo la kiwanja ambacho tuliwakabidhiwa timu hiyo nitagharamia gharama za hati ya usajili mpaka kupata hati yenye jina la klabu ya Coastal Union na hivi karibuni nitakwenda kuwakabidhi rasmi kwa lengo la kuanza kuendelea na mipango yao “Anasema


Hata hivyo Mbunge huyo anatoa wito kwa wakazi wa Jiji la Tanga wanaotaka kuwekeza waende eneo la Pongwe ambalo lina viwanja 937 hivyo watumie nafasi hiyo kwa sababu timu ya Coastal Union wakiwa hapo itavutia lakini pia kuwepo kwa eneo kwa ajili ya zahanati kama walivyofanya kutoa kwa shule ya Msingi.

Hatua ya Mbunge Ummy kuikabidhi eneo timu hiyo kulipelekea Mwenyekiti wa Coastal Union Steven Mnguto kuishiwa na maneno ya kuzungumza huku akionyesha furaha yake isiyokuwa ya kifani kwake kwa kuisaidia timu hiyo lakini pia kuweza kurudisha heshima ya soka kwa mkoa huo.

“Mh Mbunge hapa nilipo nimeishiwa maneno ila nisema mama Ummy umetusaidia sana ulikuwa wapi siku zote kauli ya Mungu anasema nitakuwa muda na saa usizotarajia kila tunapofanyaa tukio kubwaa tunaona nyota inatuandama tulipata basi wakati tunapanda daraja kipindi kile safari hii tumepanda nyota nyengine imekuja kiwanja tuendelee kuomba na kushikamana”Anasema.

Hata hivyo naye Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tanga (TRFA) Saidi Soud anasema wao kama wasimamizi wa soka la mkoa wa Tanga wamehemewa na furaha kwa jambo hilo ambalo ni la kihistoria kutokana namna Waziri huyo alivyowashika mkono.


“Labda nisema Waziri Ummy ni mama wa kweli nakumbuka wakati unasema utatushika mkono huko mbele tulikuwa tunasuasua lakini ujio wako umesaidia kuvunja hata makundi yaliyokuwa yakirudisha nyuma maendeleo “Anasema.

Akizungumza katika Halfa hiyo, Mkurugenzi wa Kampuni ya City Plan Consultants (T) Limited Dkt Juma Mohamed anaeleza namna Mbunge Ummy alivyofanikisha upatikanaji wa eneo hilo ambapo anaeleza kwamba walipata ombi kutoka kwake na kuona namna ya kupata eneo la Michezo kwa timu ya Coastal Union.

Anasema baade waliweza kulijadili na kuliwasilisha kwa wadau ambao ni wananchi wa eneo la hapa na kuweza kupatikana kwa eneo hilo ambapo pia unaweza kutoa viwanja cha mpira hamsini kwa mia moja lakini panazaidi ya eneo la pitch ya mpira.

“Tulikubaliana kuhifadhi viwanja 16 upande block za chini kwani kuna masuala wanaendelea na majadiliano vitalipiwa kwa ajili ya kuweka maeneo mbalimbali ya michezo nah ii itafungua ukurasa mpya wa soka kwa mkoa “Anasema Dkt Juma.

Licha ya hivyo Mbunge Ummy aliweza kufanya ziara ya mara kwa mara kutetembelea kambi ya timu ya Coastal Union iliyokuwepo eneo la Saruji Jijini Tanga wakati timu hiyo ikishiriki daraja la kwanza na nikiwa kwenye nafasi ya tatu kwenye kundi B.


Baada ya kutembelea kambi hiyo aliwasisitizia wachezaji kuongeza jitihada na kujituma ili kushinda mechi nne zilizobakia kwa lengo la kujihakikishia nafasi ya kucheza ligi kuu ya Tanzania bara msimu wa mwaka 2018/2019 jambo ambalo lilifanikiwa na kuiwezesha timu kurudi ligi za juu.

“Katika nukuu ya maneno yake wakati huo ndugu zangu “Coastal Union ikipanda daraja na kucheza Premier League sio tu itawezesha vijana kupata kipato bali pia itachochea uchumi na maendeleo ya Jiji la Tanga mwisho wa kunukuu“

Katika kuhamasisha huko Mbunge Ummy aliwakabidhi shilingi milioni 3 na nusu kwa ajili ya mishahara ya wachezaji ya mwezi Desemba na gharama za chakula huku akihaidi kutoa zawadi y ash.milioni 2 kwa kila mechi watakayoshinda kati ya mechi nne zilizobaki.

Baada ya hatua hiyo Kocha Mkuu wa timu ya Coastal Union Juma Mgunda amemuhakikishia Mbunge Ummy kuwa vijana wapo tayari kufanya vizuri kwenye Ligi na hivyo hatutakuangusha katika michezo yao hiyo iliyosalia katika michuano ya Ligi Daraja la kwanza jambo ambalo walilfanikisha kwa asilimia kubwa na kurejea ligi kuu.

Pia walimshukuru Mbunge Ummy kwa kujitoa kwake ili kuhakikisha timu hiyo inapanda daraja ambapo tukio hilo la makabidhiano limehudhuriwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Tanga (TRFA) Said Soud na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Coastal Union Salim Bawaziri

“Motisha kwa wachezaji wa timu ya Coastal Union" 

Mbunge Ummy kwa kuonyesha kujali na kuwathamini wana michezo mkoani Tanga alilazimika kuwalipa wachezaji wa timu ya Coastal Union na African Sports mishahara kwa kipindi Fulani huku akihamasisha uwanjani.

Hatua hiyo inatajwa kwamba imechangia uwepo wa timu hiyo kwenye Ligi madaraja tofauti huku zikiendelea kufanya vizuri kutokana na uwepo wake ambao umekuwa na mchango mkubwa kwenye soka.

Wakati mwengine wana Tanga ambao wanakuwa wakijitokeza kwenye viwanja vya Mkwakwani wametakuwa ni mashahidi tosha Mbunge Ummy amekuwa akihudhuria mechi za timu hiyo licha ya kuwa nje ya mkoa huo kwa wakati huo lakini hulazimika kufika hata kipindi cha pili uwanjani ikiwa ni kuwahamasisha wanamichezo.

Kutembelea kambi ya wachezaji.

Ummy ni miongoni mwa viongozi wachache ambao kila wakati timu ya Coastal Union inapojiandaa kwa ajili ya kucheza na timu kubwa nchini ikiwemo Simba, Yanga na hata nyengine amekuwa akitinga kambini kuzungumza na wachezaji ikiwezekana kula nao chakula cha mchana huku akiwahamasisha suala la ushindi ni lazima.

Hatua hiyo imetajwa kwamba imechangia kwa asilimia kubwa wachezaji wa timu hiyo kupata hari kubwa ya kuweza kufanya vizuri katika michuano ya Ligi Daraja la kwanza na hatimaye kurudi Ligi kuu na kudumu mpaka wakati huo. 


Uhamasishaji.

Mbunge Ummy ambaye siku zote nimeshindwa nimfananishe na kiongozi gani hapa nchini amekuwa na desturi ya kila mechi zinapokuwa zikicheza timu kongwe za mkoa wa Tanga amekuwa akishirikiana na mashabiki na wapezi majukwaani kuhamaisha ushindi kwa staili ya kushangilia.

Staili hiyo ya ushangiliaji ilipelekea kuchangia kuwaibua mashabiki wengi wapya ndani ya timu hiyo ambao kila timu hiyo inapokuwa ikicheza mechi zake za nyumbani wanalazimika kufika uwanjani na kuujaza uwanja hali ambayo ilichangia kwa asilimia kubwa kwenye michezo ya nyumbani timu kufanya vizuri kutokana na hamasa.

Hata hivyo Mbunge Ummy hakuiacha nyuma Klabu ya African Sports ambao waliwahi kuwa mabingwa wa kombe la Muungano mwaka 1988 ambapo wakati huo taji hilo ndio lilikuwa kubwa zaidi nchini,michuano hiyo iliyoshirikisha timu za Bara na Visiwani na kumpata bingwa wa jumla wa nchi na pia wawakilishi wa michuano ya Afrika.

Bingwa wa Bara alikuwa anakwenda kucheza Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati pekee,lakini bingwa wa Muungano wakati huo alikuwa anacheza Klabu Bingwa Afrika na mshindi wa pili wa Ligi ya Muungano, alikuwa anacheza iliyokuwa michuano ya Kombe la Washindi Afrika, baadaye ikaongezeka na mshindi wa tatu akawa anacheza Kombe la CAF.

Pamoja na kushiriki michuano hiyo lakini miaka ya nyuma timu hiyo iliyumba na kushuka daraja kwa nyakati tofauti licha ya kurejea Ligi kuu lakini ilishindwa kuhimili mikimikii ya ligi hiyo na kujikuta wakishuka daraja wao na mahasimu wao Coastal Union na Mgambo Shooting kwa wakati mmoja.

Baada ya kushuka daraja wakajikuta wakishindwa kuhimili vishindo vya daraja la kwanza na kujikuta wakirudi kucheza Ligi daraja la pili walilopo mpaka wakati huu huku wakipambana kuhakikisha wanarejea walipotoka kwa kuweka mipango imara ambayo itawafikisha huko.

Kwa kuona hali ya timu hiyo Mbunge Ummy aliamua kujitosa na kuanza kuisaidia katika masuala mbalimbali ikiwemo vifaa vya vyenye thamani ya zaidi ya milioni 1.5 ikiwemo vyakula wakati wa kamb na motisha ikiwa ni mkakati kabambe wa kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri kwenye mashindano wanayoshiriki na hatimaye kucheza ligi daraja la kwanza msimu ujao.

Mbunge Ummy anasema vifaa hivyo vitakuwa ni chachu ya timu hiyo kuweza kufikia malengo yao huku akieleza dhamira yake kubwa ni kuhakikisha timu hiyo inarejea ligi daraja la kwanza na ile ya Coastal Union ihakikisha msimu ujao inarudi Ligi kuu.

“Niseme tu sisi tumejipanga kuhakikisha tunazirejesha timu hizi kwenye michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara tukianzia na timu ya Coastal Union lakini ndugu zangu African Sports mhakikishe mnarudi ligi daraja la kqwanza na baadae ligi kuu “Anasema

Akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo, Mwenyekiti wa Klabu ya African Sports, Awadhi Salehe Pamba anamshukuru Waziri Ummy kwa kuwasaidia msaada huo ambao utakuwa ni chachu kwao kuweza kufikia malengo yao kutokana na changamoto hiyo kwisha.

Alisema msaada uliotolewa na Mbunge Ummy utakuwa chachu kubwa kwao kuweza kufikia malengo yao waliojiwekea ya kuhakikisha wanarudi ligi kuu kwani ndio ndoto yao kubwa ambayo wamekuwa wakiiwaza kila wakati.

“Mbunge Ummy tukushukuru sana katika hili umetupa nguvu ya kuweza kupambana na tuna kuhaidia kuhakikisha tunairudisha timu Ligi daraja la kwanza na hatimaye ligi kuu.
Share:

Makamishna Wa Ardhi Watakiwa Kukutana Na Taasisi Zinazodaiwa Kodi Ya Pango La Ardhi

Na Munir Shemweta, WANMM SUMBAWANGA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewaagiza Makamishna Wasaidizi wa ardhi katika ofisi za mikoa kukaa na taasisi za serikali zinazodaiwa kodi ya pango la ardhi kuangalia namna bora ya kulipa madeni wanayodaiwa.

Dkt Mabula alitoa agizo hilo jana mkoani Rukwa wakati akizundua rasmi ofisi ya ardhi ya mkoa ikiwa ni mfululilizo wa uzinduzi wa ofisi za ardhi katika mikoa mbalimbali nchini. Tayari ofisi saba za ardhi katika mikoa ya Tanga, Arusha, Manyara, Singida, Iringa, Njombe na Songwe zimezinduliwa.

Alisema, mkoa wa Rukwa una taasisi za serikali pamoja na watu binafsi ambao kwa ujumla wao wanadaiwa zaidi ya shilingi bilioni moja kiasi alichokieleza kuwa ni kikubwa na fedha yake ingeweza kutumika katika shughuli za maendekeo kama vile ujenzi wa hospitali au barabara.

Alizitaja baadhi ya taasisi za serikali zinazodaiwa kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa Rukwa kuwa ni pamoja na Shirika la umeme Tanzania (Tanesco), Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) na Chuo Kikuu Huria na kubainisha kuwa katika kumuwezesha rais kufanya kazi ya shughuli za maendeleo kuna wajibu wa kulipa kodi ya pango la ardhi.

‘’Bilioni moja ni fedha nyingi sana nawaagiza Makamishna Wasaidizi wa mikoa kukutana na taasisi pamoja na watu wengine wanaodaiwa kodi ya pango la ardhi kukubaliana namna bora ya kulipa fedha wanazodaiwa vinginevyo taratibu za kisheria zitafuata’’ alisema Dkt Mabula

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Taasisi za serikali zinatenga fedha kwenye bajeti zake kwa ajili ya kulipia gharama mbalimbali ikiwemo kodi ya pango la ardhi na kutolipa kodi hiyo ni kutotimiza wajibu wa kulipa kodi ya ardhi.

Alisema, Wizara yake ilikutana na makampuni na taasisi za serikali zenye malimbikizo makubwa ya kodi ya pango la ardhi mkoani Dodoma na baada ya kukutana ndani ya mwezi mmoja zilikusanywa takriban bilioni ishirini na moja jambo linaloonesha kuwa taasisi hizo zinazo fedha kwa ajili ya kodi hiyo.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi Dkt Angeline Mabula alisema, wizara yake imeridhia kuanzishwa Baraza la Ardhi la Nyumba la wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa.

Hatua hiyo inafuatia Dkt Mabula kuridhishwa na juhudi za wilaya ya Nkasi katika kuanzisha baraza hilo ambapo alikagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi yake katika eneo la Namanyele wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa na kusema kuwa kwa sasa takriban mabaraza mia moja ya ardhi ya nyumba ya wilaya yameidhinishwa lakini ni mabaraza 55 ndiyo yanayofanya kazi.

Hata hivyo, aliongeza kwa kusema kuwa, wakati mchakato wa ofisi za baraza hilo ukiendelea mwenyekiti wa baraza la ardhi la wilaya ya Sumbawanga anaweza kupanga ratiba na kwenda kuendesha mashauri ya migogoro ya ardhi kwenye wilaya ya Nkasi kwa lengo la kupunguza mashauri hao.

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa, mkoa wake una baraza moja tu la ardhi la nyumba na wilaya huku mkoa mzima ukiwa umesajili jumla ya mashauri 308 ya migogoro ya ardhi kuanzia mwezi januari hadi juni mwaka huu.

Alisema, kufuatia hali hiyo iko haja ya kuanzishwa baraza la ardhi la wilaya ya Nkasi kwa kuwa wananchi wa wilaya hiyo wamkuwa wakipata taabu kutembea umbali mrefu na wakati mwingine hulazimika kusafiri kilomita 160 kufuata huduma ya baraza wilayani Sumbawanga.


Share:

Takukuru Manyara Yafanikiwa Kurejesha Fedha Zilizoporwa Na Mkuu Wa Shule

Na John Walter-Babati
Taasisi  ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Mkoani Manyara imefanikiwa kurejesha zaidi ya shilingi milioni nne za watumishi wa shule ya msingi Birsima, ambazo zilifanyiwa ubadhirifu na Mwalimu mkuu msaidizi wa shule hiyo, Aman Paul Mkeni.

Taarifa iliyotolewa na mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Holle Makungu imesema Fedha hizo zimekabidhiwa kwa wahusika na afisa wa TAKUKURU  dawati la Udhibiti Bi.Edda Senkondo  juni 30,2020.

Kwa mujibu wa mkuu wa TAKUKURU Manyara Holle Makungu, amesema Mkeni ambaye pia ni Mhasibu wa shule hiyo iliopo wilayani Babati, alishindwa kutimiza wajibu wake wa kuwalipa fedha hizo watumishi hao wasio walimu na kuzifanyia ubadhirifu.

Watumishi Waliokabidhiwa fedha zao kwenye mabano ni Ezekiel Rory (410,000), Daniel Jacob (1,400,000) na Melania Bayo (300,000).
 
Amesema wamefanikiwa kurejesha fedha hizo baada ya kupata malalamiko ndipo walipomtaka Mwalimu Mkeni  kuwasilisha fedha hizo.

Hata hivyo Makungu ameshauri uongozi wa shule hiyo umpe mwalimu mwingine mwenye uadilifu kazi ya kutunza fedha kwa kuwa Mwalimu huyo hastahili.


Share:

Waziri wa Fedha Dkt. Mpango Aridhishwa Na Ujenzi Wa Ofisi Ya Mkuu Wa Wilaya Buhigwe

Na: Josephine Majura na Peter Haule KIGOMA
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb), ameupongeza uongozi wa mkoa wa Kigoma na Wilaya ya Buhigwe  kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe inayojengwa katika eneo la Bwega, Tarafa ya Manyovu, wilayani Buhigwe mkoani Kigoma na kuagiza Jengo hilo likamilike kabla ya mwezi wa kumi ili wananchi wa wilaya hiyo waanze kupata huduma kwenye jengo hilo jipya.

Dkt. Mpango ametoa pongezi hizo alipotembelea na kukagua ujenzi wa jengo hilo jipya la Ofisi ya MKuu wa Wilaya mpya ya Buhigwe ambalo hadi kukamilika kwake litagharimu shilingi bilioni 1.1

“Nakupongeza Mkuu wa Wilaya na timu yako yote kwa usimamizi mzuri wa Fedha za Serikali, lazima tujenge Makao Makuu ya Wilaya ambayo yataishi kwa miaka mingi, kwa hiyo nimefurahi jengo ninavyoliona hata kama sio Mhandisi lakini ninaona lina ubora”. alisisitiza Dkt. Mpango.

Alimtaka Mkuu wa Wilaya kuendelea kusimamia rasilimali fedha  zinazotolewa na Serikali kama alivyofanya kwenye mradi wa ujenzi wa  Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ili thamani ya fedha za miradi inayotekelezwa ilingane na thamani ya fedha zilizotolewa.

Kwa upande wake, Meneja mradi huo Masawika Kachenje, akisoma taarifa ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe amesema kuwa hadi sasa kiasi cha shilingi milioni mia tano (500,000,000) ambazo Serikali zilitoa kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi huo  kimetumika kukamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi.

Aliongeza kuwa kiasi cha shilingi milioni (550,000,000), kimebaki ili kukamilisha kiasi cha sh. Bilioni 1.1 ikiwa ni gharama ya utekelezaji wa mradi wa  ujenzi  jengo zima, ambapo mipango ya Wilaya ilikuwa kukamilisha ujenzi huo ifikapo mwezi Julai tarehe 15 mwaka 2020.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali, Michaeli Ngayalina, amemshukuru Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango, kwa kutembelea na kukagua baadhi ya miradi inayotekelezwa kwa Fedha za Serikali na kuahidi kuzisimamia vizuri fedha zote zinazotolewa na Serikali kukamilisha miradi ya maendeleo.

Kanali Ngayalina, amemuomba Dkt. Mpango kusaidia upatikanaji wa Fedha zilizobaki ili waweze kukamilisha ujenzi wa ofisi hiyo kama ilivyopangwa kwenye ratiba.


Share:

Waziri Ummy : NHIF Tatueni Malalamiko Ya Upatikanaji Wa Baadhi Ya Dawa

Na.WAMJW,DSM
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) imetakiwa kutatua malalamiko ya upatikanaji wa baadhi ya dawa na vipimo kwa wananchi wenye bima ya afya.

Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa kikao na Menejimenti ya Mfuko huo katika ofisi ndogo za wizara zilizopo jijini, Dar es Salaam.

“Kumekuwepo na malalamiko ya upatikanaji wa baadhi ya dawa na vipimo kwa watu wenye kadi za bima pia ucheleweshaji wa malipo ya watoa huduma za afya” Alisema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy ameutaka mfuko huo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kujiunga na mfuko huo pamoja na mafao yanayotolewa katika vifurushi vya bima ya afya.

“Tatueni malalamiko yote kwa wakati ili wananchi wafurahie vifurushi vyote watakavyojiunga navyo”.Alisisitiza Waziri Ummy

Kikao hicho pia kiliangalia mwenendo wa utoaji wa huduma za bima za afya zinazotolewa na mfuko huo ambapo kilihudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa NHIF, Benard Konga, Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Grace Magembe, na Mfamasia Mkuu wa Serikali, Daudi Msasi.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano July 01























Share:

Tuesday, 30 June 2020

Job vacancies at HR World

HR World Limited on behalf of our reputable client (Sunflower Oil Extraction & Refining Plant Manyoni Singida) we are looking for well-qualified and experienced candidates to fill up the advertised vacancies as soon as possible. Kindly read Job Description on the website carefully before applying , only qualified candidates experienced in edible oil/food manufacturing Industry […]

The post Job vacancies at HR World appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

WATU WANNE WAUAWA KWA KUCHARANGWA MAPANGA MGODINI KAHAMA

Picha hauhusiani na habari hapa chini
Na Mwandishi wa Malunde 1 blog

Wafanyakazi wanne wa kiwanda cha uchenjuaji wa madini ya dhahabu(Plant) katika Mgodi mdogo wa Ntambalale, kijiji cha Wisolele Kata Segese Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga,wameuawa na mmoja kujeruhiwa kwa kucharangwa na mapanga na watu wasiojulikana kisha kutokomea na kaboni. 

Mwenyekiti wa mgodi wa Ntambalale Hamisi Mabubu amesema tukio hilo limetokea majira ya saa tisa usiku wa kuamkia leo Jumanne Juni 30, 2020 katika moja ya viwanda vya uchenjuaji wa madini. 

“Wafanyakazi watano wa kiwanda hicho, walivamiwa na kucharangwa na mapanga sehemu mbalimbali za miili yao na watu wasiojukulikana na kuwapora kaboni, Wafanyakazi wanne walipoteza maisha papo hapo na mmoja aliyejulikana kwa jina la Evary Mbuya akijeruhiwa. Bila shaka chanzo cha tukio hili ni tamaa ya kupata mali kwa haraka”, amesema.

Naye Diwani wa Kata ya Segese Joseph Mayala amesema alipata taarifa ya tukio hilo kutoka kwa mtendaji wake wa kata majira ya saa kumi usiku na walipofika kwenye tukio walikuta miili ya watu wanne na mmoja wao Evary Mbuya walimkimbiza katika Hospitali ya Halmashauri ya mji wa Kahama kwa ajili ya matibabu. 

Hata hivyo Mayala amesema matukio ya uvamizi wa viwanda cha uchenjuaji wa dhahabu yamekuwa yakitokea mara kwa mara hasa wakati wamiliki wa viwanda wakiwa na kaboni,na kuliomba jeshi la polisi kuongeza ulinzi na kudhibiti majanga haya yasiendelee kutokea. 

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Joseph Paul,amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa harakati za kuwatafuta na kuwatia nguvuni walitotenda tukio hilo zinaendelea na wakibainika watafikishwa katika vyombo vya sheria.
Share:

PROF. MAKUBI AIPONGEZA TMDA KUZINDUA TOLEO JIPYA LA MKATABA WA HUDUMA KWA WATEJA

Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Abel Makubi akikata Utepe kuashiria uzinduzi wa mkataba wa huduma kwa Wateja toleo la Nne wa TMDA, Kulia ni Kaimu Mkurgenzi Mkuu wa TMDA, Adam Fimbo na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Wizara (MAB) kwa TMDA, Eric Shitindi. Hafla iliyofanyika 29 Juni jijini Dar es Salaam.



Na Andrew Chale, Dar es salaam

MGANGA Mkuu wa Serikali, Profesa Abel Makubi amepongeza  Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), kwa kuzindua mpango mpya wa Huduma kwa Wateja ambao unaongeza ufanisi katika shughuli zake za kila siku baina ya taasisi na wateja wake.

Prof. Makubi amesema hayo jana 29 Juni, Jijini Dar es Salaam wakati akizindua toleo jipya la Nne la Mkataba wa Huduma kwa wateja lililoshuhudiwa pia na wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka Serikali, Wadau na washirika wa mradi wa FASTER (CRS, CHAI  na CSSC).

Akizungumza katika tukio hilo la uzinduzi, Prof. Makubi alitoa wito kwa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya kuwa na mkataba wa huduma kwa wateja kama wafanyavyo TMDA.

"Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jami, Jinsia, Wazee na Watoto inaendelea kutoa rai kwa Vituo vya Afya na Hospitali zote za Wilaya, Mkoa na Rufaa kuwa na dawati la Mkataba wa huduma kwa wateja.

"Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Afya zinapaswa kuwa na dawati la mkataba wa huduma kwa  Wateja  ili kurahisisha utoaji wa huduma bora  kwa wananchi." Alisema Prof. Makubi.

Aliongeza kuwa TMDA imekuwa na mipango mizuri katika utoaji wa  huduma kwa kuzingatia muda katika utoaji wa leseni kwa wadau mbalimbali kama ilvyoelezwa katika taarifa.

"TMDA imekuwa na mifumo mizuri ya viwango ambapo Shirika la Afya Duniani inatambua pamoja na jumuiya  mbalimbali hii inatokana na mikakati ya watendaji wa taasisi waliojiwekea ya kuhakikisha wanakwenda kutatua matatizo ya  huduma katika utoaji wa huduma zake" Alisema Prof. Makubi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurgenzi Mkuu wa TMDA, Adam Fimbo alisema waliweza kufanya mapitio ya Mkataba wa Huduna kwa wateja 'Clients Service Charter'  la kuandaa toleo la Nne (4) baada ya kutekeleza ule ulioandaliwa mwaka 2016.

"Mapitio ya Mkataba uliopita umechagizwa na mabadiliko mbalimbali  yamejitokeza katika kipindi cha miaka minne. Mabadiliko hayo ni pamoja na kubadilika majukumu ya iliyokuwa TFDA kwa masuala ya udhibiti  wa vyakula na vipodozi yalihamishiwa Shirika la TBS na kupelekea kubadilika kwa jina na kuwa TMDA." Alisema Fimbo

 Adam Fimbo alieleza kuwa wamefanikiwa kuweka mifumo ya TEHAMA ambapo umefanywa na TMDA na kurahisisha utoaji wa huduma.

"Toleo hili jipya la nne la mkataba wa huduma kwa wateja limepitiwa kwa kina na kupunguza maradufu muda wa utoaji ukilinganisha na Mkataba uliopita wa mwaka 2016.

Awali ilikuwa muda wa kusajili dawa zinazotoka nje ya nchi ulikuwa siku 240 kwa sasa umepungua hadi siku 180 za kazi. 

"Muda wa kusajili dawa zinazotengenezwa ndani ya nchi ulikuwa siku 120 Sasa umepungua hadi siku 60 na hio ni nusu ya siku zilizotengwa hapo awali. Muda wa usajili wa maeneo ya biashara za bidhaa zinazodhibitiwa na TMDA umepunguzwa kutoka siku 10 hadi 8.

"Pamoja na kupunguza siku za kuthamini na kusajili dawa, tumeweka pia utaratibu  rahisi wa kusajili dawa ambazo zimekwishasajiliwa kupitia Jumuiya zetu za Kikanda kama EAC na SADC pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO)." Alisema Fimbo. 

Aidha alipongeza wadau na washirika wa Maendeleo kupitia mradi wa FASTER, ambao ni Catholic Relief Services, CHAI na Christian Social Services Commission (CSSC) ambao walifanikisha kutolewa kwa mktaba huo wa huduma kwa wateja.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger