Monday, 30 March 2020
ZITTO KABWE ATAJA MAMBO 8 KUKABILIANA NA CORONA
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ametoa mapendekezo manane kupitia barua aliyomwandikia Rais John Magufuli, kuhusu nini kifanyike katika kuzuia maambukizi mapya ya ugonjwa wa corona.
Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini, kwenye barua hiyo alitoa pia ushauri juu ya namna nzuri ya udhibiti wa maambukizi ya ugonjwa huo, ambao umekuwa tishio katika nchi nyingi duniani.
Kwanza, Zitto alipendekeza kuwapo kwa umoja wa kitaifa ambao utawaweka Watanzania pamoja kwa vitendo hali itakayofanikisha kupambana na ugonjwa huo.
“Hakuna wakati nchi yetu inahitaji umoja kama wakati huu. Wewe kama mkuu wa nchi una wajibu mkubwa wa kuwaweka Watanzania pamoja kwa vitendo. Tukiwa wamoja tutaweza kupambana na corona na kushinda pamoja na ikibidi kushindwa tushindwe pamoja,” alisema Zitto na kuongeza:
“Corona haitambui itikadi zetu za vyama, dini zetu wala makabila yetu. Corona inaua mashekhe na makasisi, wanasiasa na wananchi wa kawaida, wanadiplomasia na wanamichezo na mbaya zaidi inaua hata wataalamu wa afya kama madaktari na manesi. Nakusihi sana, uunganisha nchi yetu sasa bila kuchelewa,” alisema Zitto.
Pili, Zitto alipendekeza wataalamu kupewa nafasi katika kuongoza mapambano na kwamba viongozi kuepuka kutoa maeneo ya jumla.
“Ni muhimu sana sisi viongozi kuepuka kutoa maneno ya jumla ambayo yanawapa wananchi wetu matumaini hewa, hivyo kusababisha hatari zaidi.
“Tutoe nafasi kwa wataalamu wa afya kutuongoza katika mapambano haya ya kudhibiti corona. Ni lazima sasa, maneno tunayoyasema kwa umma na maamuzi tunayoyachukua katika kudhibiti mlipuko huu yazingatie ushauri wa wataalamu ,” alisema Zitto.
Tatu, alipendekeza serikali kuweka nguvu kubwa kwenye kupima wananchi ili kuwatambua wenye maambukizi, kuwatenga wasiambukize wengine, kuwatibu na kuwafutilia maendeleo yao.
Zitto alisema kazi ya upimaji iwe kampeni endelevu na kwamba serikali itumie vipimo ilivyosaidiwa sambamba na kutumia fedha za dharura ambazo Bunge lilizipitisha kwenye bajeti ya mwaka 2019/2020 kununua vipimo vingi zaidi ili kupima wananchi.
Nne, Zitto alipendekeza kuwapo na uwazi wa takwimu za maambukizi mapya, wagonjwa mahututi na vifo kwani suala hilo ni muhimu sana katika kukabiliana na ugonjwa huo.
Tano, Zitto alipendekeza kuepukwe maelekezo yanayopinga na kueleza kuwa hatua zichukuliwe kusimamisha vikao vyote vya kiserikali ikiwamo Bunge na Mahakama.
“Serikali ilichukua hatua muafaka kufunga shule na vyuo kote nchini ili kuzuia maambukizi. Hata hivyo, tunatuma ujumbe gani kwa wananchi, na hasa watoto wetu wanapoona wao wamefunga shule, lakini viongozi wanahutubia makumi ya watu hadharani? Wanapata ujumbe gani wanapoona Bunge linaendelea na vikao?” Alisema Zitto.
Sita, alipendekeza mahabusi na wafungwa waachiliwe na warudi nyumbani ama kumalizia vifungo au kusubiri upelelezi wa kesi zao.
Saba, Zitto alipendekekeza kufungwa kwa mipaka ya nchi kwa muda ili kudhibiti maambukizi, na kwamba kwa kufanya hivyo kutasaidia kuzuia maambukizi zaidi.
“Ni lazima kuzuia msongamano wa watu kwenye huduma za usafiri wa umma kwa kuagiza vyombo vya usafiri vya Jeshi la Wananchi, Polisi na hata watu binafsi kutoa huduma ya usafiri wa umma kwa uangalifu mkubwa,” alisema Zitto.
Nane, Zitto alipendekeza kuundwa kwa timu ya wachumi waliobobea waliopo ndani na nje ya serikali watakaofanya uchambuzi wa kina wa hali ya uchumi wa nchi na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua.
Sita wajeruhiwa na fisi Shinyanga
Watu sita wa familia moja wakazi wa kijiji cha mwangalanga kata ya Samuye wilayani Shinyanga wamejeruhiwa kwa kung’atwa na fisi katika maeneo mbalimbali ya miili yao na ikidaiwa watu hao wamejeruhiwa na fisi huyo baada ya kumzingira kwa lengo la kumuua
Tukio hilo lilitokea Machi 27, saa 10 jioni, katika kijiji cha Mwangalanga wakati fisi huyo alipovamia kijiji hicho na wananchi kumzingira kwa kumpiga na kusababisha watu hao sita kujeruhiwa.
Taarifa iliyotolewa juzi na Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Deborah Magiligimba, ilisema baada ya watu hao kujeruhiwa walikimbizwa hospitali kupatiwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.
Aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni Zengo Jitonja, Nkuba Deteba, Juma Salaganda, Limbu Mihambo, Dutu Mdese, na John Matanda.
"Watu hawa wakati wakiwa wamemzingira fisi huyo na kuanza kumshambulia, aliwang'ata sehemu mbalimbali za miili yao, majeruhi watano walipata majeraha madogo na wemeruhusiwa kutoka hospitali," alisema Magiligimba.
"Majeruhi mmoja Nzengo Jintonja, ambaye alijeruhiwa vibaya kwa kung'atwa mikononi na mdomoni, yeye alikimbizwa na kulazwa katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Shinyanga na hali yake siyo mbaya sana," aliongeza.
Alisema fisi huyo ameshauawa na wananchi walioendelea kumshambulia kwa kumpiga.
Jiko La Mkaa Lasababishavifo Vya Watu Wanne Shinyanga
Wakazi wanne wa kitongoji cha Ngilimba ‘B’ kata ya Ulowa halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga wamefariki dunia baada ya kuvuta hewa yenye sumu iliyosababishwa na mkaa waliouwasha kwenye jiko na kisha kuliweka ndani ya nyumba yao ili kujikinga na baridi.
Akungumza na Waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba alisema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Machi 28 mwaka huu ambapo wanafamilia hiyo waligundulika kupoteza Maisha ndani ya nyumba yao wakiwa wamelalala baada ya kuvuta hewa yenye sumu.
Kamanda Magiligimba aliwataja waliofariki dunia ni pamoja Masanja Emmanuel (35) ambaye ni baba wa familia hiyo, Mngole Masanja (25) mkewe, Holo Masanja,(05) na Matama Masanja (03) wote wakazi wa Ngilimba.
“Tukio hili limesababishwa na mvua iliyonyesha Machi 27 iliyoambatana na baridi kali ndipo marehemu hao waliamua kulala na jiko la mkaa ndani ya nyumba yao na kusababisha mgandamizo wa hewa kuwa mdogo uliosababisha wavute hewa yenye sumu ya carbon monoxide”,amesema Magiligimba.
Miili ya marehemu hao imekabidhiwa ndugu zao kwa ajili ya taratibu za mazishi baada ya kufanyiwa uchunguzi wa daktari.
Mwisho.
Sunday, 29 March 2020
SUMAYE AKABIDHIWA RASMI KADI YA UANACHAMA CCM

Na .Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Dkt BASHIRU ALLY leo Machi 29,2020 amemkabidhi rasmi kadi ya uanachama wa chama hicho Waziri mkuu mstaafu FREDRICK SUMAYE huku akiahidi kufanya sherehe ya kumpokea mwanachama huyo mara baada ya tishio la Virusi vya Corona litakapoisha.
Makabidhiano hayo yamefanyika jijini Dodoma ambapo amesema siku zote chama kinapopokea mwanachama mpya kinafanya sherehe lakini kutokana na uwepo wa virusi hivyo wamesitisha sherehe hiyo kwa sasa.
Amesema SUMAYE amekabidhiwa kadi Dodoma kwa sababu Chama hicho ni chama cha kitaifa nasio chama cha watu.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kadi SUMAYE amesema amefurahi amerudi rasmi kwenye chama chake na sasa ni mwanachama kamili.
Amesema wakati anaondoka CCM alisema anaondoka akiwa hana chuki na chama,hana chuki na aliyekuwa mwenyekiti wa CCM wakati huo dokta JAKAYA KIKWETE na hana chuki na mgombea aliyeteuliwa wakati huo dokta JOHN MAGUFULI
Kwa upande wake Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM MIZENGO PINDA amesema amefurahi kwa kuwa wakati wanaondoka CCM alipata shida sana.
Mfanyabiasha Afariki Dunia Kwa Mshtuko Wa Kuunguliwa Maduka Samunge Jijini Arusha
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Mtu mmoja amefariki dunia Mara baada ya moto mkubwa kuzuka na kuunguza soko la Samunge jijini Arusha baada ya kufika na kushuhudia maduka yake yote yakiwa yameketea na moto.
Mtu mmoja amefariki dunia Mara baada ya moto mkubwa kuzuka na kuunguza soko la Samunge jijini Arusha baada ya kufika na kushuhudia maduka yake yote yakiwa yameketea na moto.
Akiongea na waandishi wa habari Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
Aidha wakati zoezi la kuzima moto likiendelea mtu mmoja aliyefahamika kwa majina ya James Peter Temba, 57 Mfanyabiashara na mkazi wa Moshono ambaye ni mmoja kati ya wamiliki wa vibanda vilivyoungua ndani ya Soko hilo, alifika eneo hilo na kukuta vibanda vyake vimeungua.
Kaimu kamanda Koka alieleza kuwa majira ya saa 23:30hrs, katika soko la Samunge, lililopo Mtaa wa NMC, kata ya Kati, Tarafa ya Themi, katika Halmashauri ya Jiji la Arusha, moto ambao bado chanzo chake hakijajulikana uliwaka na kuteketeza vibanda vya Soko hilo ambavyo idadi na thamani yake bado haijajulikana.
Ameeleza kuwa vibanda hivyo vilikuwa vinamilikiwa na wafanyabiashara wa Soko hilo ambavyo vilijengwa kwa Mabati, Mbao na Mabanzi. Mara baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Wananchi walifanikiwa kuzima moto huo ambao haukuleta madhara kwa binadamu.
Mtu huyo alipata mshtuko na kuanguka chini na kuzimia ambapo alichukuliwa na kupelekwa katika Hospital ya Mkoa ya Mount Meru na alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu.
Hata hivyo Uchunguzi unaendelea ili kubaini thamani halisi ya mali zilizoungua pamoja na chanzo cha moto huo.
Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mount Meru kwa uchunguzi zaidi wa Daktari.
Natoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa haraka pindi wanapoona majanga kama haya ya moto kwa Jeshi la Polisi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kudhibiti matukio kwa haraka kabla ya kuleta madhara makubwa.
Alitoa wito kwa wananchi na kuwaomba pamoja na wafanyabiashara kuwa watulivu wakati vyombo vya Ulinzi na Usalama vikifanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo halisi cha tukio hilo
Mbunge wa Moshi Vijijini, Antony Komu Atangaza Kujiondoa CHADEMA
Mbunge wa Moshi Vijijini, Antony Komu leo Machi 29, 2020 ametangaza kujiondoa kwenye Chama cha Demokrasia na Maendeleo mara baada ya kipindi chake cha ubunge kuisha na kusema atahamia chama cha NCCR Mageuzi.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika Hotel ya Nepherland Magomeni Jijini Dar es salaam, Komu amedai kuwa anaamini Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) kitatumia busara kumuacha amalizie majukumu yake ya kibunge kwa muda uliobakia kwani bado anahitaji kuwatumikia wananchi wake.
MFANYABIASHARA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUSHUHUDIA LIVE VIBANDA VYAKE VIKITEKETEA KWA MOTO SOKO LA SAMUNGE
Na Ahmed Mahmoud - Arusha
Mfanyabiashara aitwaye James Peter Temba, 57 Mfanyabiashara na mkazi wa Moshono amefariki dunia baada ya kufika na kushuhudia vibanda/maduka yake yote yakiwa yameteketea na moto kutokana na moto mkubwa kuzuka na kuunguza soko la Samunge jijini Arusha.
Akiongea na waandishi wa habari Sokoni hapo Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Koka Moita amesema tukio hilo limetokea jana usiku majira ya saa 23:30 katika soko la Samunge, lililopo Mtaa wa NMC, kata ya Kati, Tarafa ya Themi, katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Amesema chanzo cha moto huo uliowaka na kuteketeza vibanda vya Soko hilo hakijajulikana na idadi na mpaka sasa thamani ya mali zilizoteketea haijajulikana.
"Wakati zoezi la kuzima moto likiendelea mtu mmoja aliyefahamika kwa majina ya James Peter Temba, 57 Mfanyabiashara na mkazi wa Moshono ambaye ni mmoja kati ya wamiliki wa vibanda vilivyoungua ndani ya Soko hilo, alifika eneo hilo na kukuta vibanda vyake vimeteketea kwa moto alipata mshtuko na kuanguka chini na kuzimia ambapo alichukuliwa na kupelekwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru na alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu",ameeleza Kamanda..
Ameeleza kuwa vibanda hivyo vilikuwa vinamilikiwa na wafanyabiashara wa Soko hilo ambavyo vilijengwa kwa Mabati, Mbao na Mabanzi. Mara baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Wananchi walifanikiwa kuzima moto huo ambao haukuleta madhara kwa binadamu vimeungua.
Hata hivyo Uchunguzi unaendelea ili kubaini thamani halisi ya mali zilizoungua pamoja na chanzo cha moto huo.
Soko la Samunge likiteketea kwa Moto kama lilivyokutwa na kamare ya matukio jijini Arusha usiku wa kuamkia leo picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.
Soko la Samunge likiteketea na Moto usiku wa kuamkia leo jijini Arusha ambapo imeelezwa kuwa thamani ya Mali iliyoteketea bado haijajulikana huku mfanyabiashara Mmoja akifariki kwa mshtuko Mara baada ya kukuta maduka yake matatu yameungua.
JIKO LA MKAA LAUA WATU WANNE WA FAMILIA WAKIJIKINGA NA BARIDI YA MVUA SHINYANGA
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Watu wanne wa familia moja wamefariki dunia baada ya kuvuta ya hewa yenye sumu ya Carbon monoxide iliyotokana na mkaa waliowasha kwenye jiko la mkaa kisha kulala ndani ya nyumba yao wakijikinga na baridi katika kitongoji cha Ngilimba ‘B’ kijiji cha Ngilimba kata ya Ulowa halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea Machi 28,2020 ambapo ndugu hao wa familia moja waligundulika kuwa wamefariki dunia wakiwa nyumbani kwao wamelala baada ya kuvuta hewa yenye sumu ya Carbon Monoxide.
“Chanzo cha tukio hilo ni kwamba siku hiyo mvua kubwa ilinyesha kijijini hapo na kupelekea uwepo wa baridi nyumbani kwa marehemu hao na ndipo wakati wakijiandaa kulala waliacha jiko la mkaa likiwa limewashwa ndani ya nyumba na kufunga mlango na dirisha hali iliyo pelekea mgandamizo wa hewa kuwa mdogo ndani ya nyumba yao na kuvuta hewa hiyo iliyokuwa na sumu ya carbon monoxide”,amesema Kamanda Magiligimba.
“Waliofariki dunia ni Masanja Emmanuel (35), Mngole Masanja (25), Holo Masanja,(05) na Matama Masanja wote wakazi waNgilimba wote wa familia moja”,ameeleza Kamanda Magiligimba
Amesema miili ya marehemu imekabidhiwa ndugu kwa ajili ya mazishi baada ya kufanyiwa uchunguzi wa daktari.
PRISCA KIBASA MWANAMKE ASIYEOGOPA KUZUNGUKA USIKU KUIMARISHA ULINZI SHIRIKISHI
Na Dinna Maningo - Tarime
Ni saa tisa alasiri nawasili nyumbani kwa Prisca Kibasa mwenye umri wa miaka (56) ambaye ni Mwenyekiti wa mtaa wa Kibasa kata ya Sabasaba wilaya yaTarime mkoani Mara kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Ananikaribisha huku usoni kwake akionekana mtu mwenye furaha.Lengo la kufika kwake nikutaka kufahamu ni kwa namna gani anawatumikia wananchi ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama wa mtaa.
Licha ya kwamba baadhi ya wanawake hawajitokezi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwa uoga waliojijengea kutokana na dhana zilizopo ndani ya jamii kuwa mwanamke hana haki kuzungumza mbele ya watu au kuwaongoza wanaume lakini hali hiyo ni tofauti kwa mama Kibasa.
Mama Kibasa ambaye amekuwa kiongozi ngazi ya kitongoji na Mtaa tangu mwaka 2004 hadi sasa ni kiongozi akihakikisha anaimarisha ulinzi na usalama kwa wananchi na mali zao na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili.
Je Kwanini Mwenyekiti huyo anaitwa Prisca Kibasa na mtaa nao unaitwa Kibasa?
"Wakati tunagawa mitaa nilikuwa ni Mwenyekiti nikasema kwanini niite majina mengine nikaita jina langu hata nije kukumbukwa kwa hilo na nilipoita na wengine nao wakajiitia majina yao kama mtaa wa Nyangai,Chomete,na mtaa wa Nyarusai kwa hiyo ndiyo ujue kuwa mwanamke akiamua kufanya jambo inawezekana na wengine wakaiga kutoka kwako",anasema Kibasa.
Kibasa anaeleza historia yake ya uongozi ambapo anasema kuwa amekuwa mwenyekiti wa Kitongoji cha Serengeti kwa awamu mbili mfululizo tangu mwaka 2004 hadi 2014.
"Wakati huo ilikuwa ni halmashauri moja ya wilaya mimi nilikuwa ndiyo mwanamke peke yangu niliyechaguliwa hadi nilikuwa najishangaa nikisimama kuzungumza mbele ya wanaume nilikuwa naona aibu, lakini baadae nilizoea nikajiamini kwanini nijishushe nawakati nimegombea sawa na wanaume" anasema Kibasa.
Kibasa anaeleza kuwa licha ya kuwa kiongozi mwanamke pekee wananchi walimpa ushirikiano kutokana na ujasiri wake na kujituma uliofanikisha kuleta maendeleo kutokana na ushawishi baina yake na wananchi.
"Mimi si Mkurya kabila langu ni mrangi wa Kondoa niliolewa na mkurya pamoja nakwamba mimi ni mkabila tena musagane mwanamke ambaye sikukeketwa bado wananchi waliniona nafaa wakanichagua. Kitongoji chetu kilikuwa na wananchi 490 walinichagua kwa sababu mimi sipendi rushwa na sina ubaguzi huduma yangu wanahifurahia",anasema.
Anaongeza"Nilipokuwa mwenyekiti wa kitongoji tulifanikiwa kujenga madarasa shule ya msingi Sabasaba,darasa moja shule za Sekondari Nyamisangura,Rebu na Nkende, kuimarisha ulinzi shirikishi na shughuli zingine za kimaendeleo".
Akizungumzia suala la ulinzi shirikishi anasema kuwa pamoja na yeye kuwa kiongozi mwanamke hakusita kutembea usiku akiwa ameambatana na wanaume kuhakikisha wanazunguka maeneo yote ya kitongoji kuimarisha ulinzi.
Anasema kuwa wakati wa zamu ya ulinzi aliwaandaa wananchi na kuwapanga kwa makundi kisha kupita kwenye maeneo ya giza na vichochoro vyote jambo ambalo lilifanikisha baadhi ya wahalifu kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
"Tulikuwa tunaanza ulinzi saa sita usiku nachagua watu kwa zamu nilivaa mavazi yangu Suruali,kofia na jaketi kisha tunaenda kulinda,lazima na mimi Mwenyekiti niende maana ukiacha waende wenyewe wapo baadhi ya wananchi si wazuri watatumia muda huo kufanya uhalifu kama kuwaibia simu wapita njia,kabla ya kuanza ulinzi tunakutana nyumbani kwangu nawapanga makundi matatu yenye watu sita tunaondoka kila kundi linaenda sehemu yake kufanya ulinzi.
"Tulikuwa tunalinda hadi saa kumi kisha tunakutana mahali ambapo tumepanga kukutana ili kuona kama tuko wote, kwakweli tulifanikiwa sana maana tulikuwa tunawapata wezi, maeneo mengine tulikuta vitu vilivyoibwa vimetunzwa ,wakati wa ulinzi tuliwapa Polisi Taarifa na walifika kubeba na kuwakamata wezi, kabla ya kuwakabidhi Polisi tulikuwa tunawapa kwanza kichapo",anasema Kibasa.
Mbali na kuwa Mwenyekiti wa Kitongoji mwaka 2019 katika uchaguzi wa Serikali za mitaa Mama Kibasa aliibuka tena na kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa mtaa wa Kibasa na alifanikiwa kupita katika kura za maoni kupitia chama cha CCM dhidi ya wapinzani wake.
"Nilishindana na wanaume wawili mwanamke nilikuwa mimi peke yangu na nikawashinda na sasa mimi ni mwenyekiti wa mtaa japo napata changamoto kuwa hatukuchaguliwa na wananchi lakini hainikatishi tamaa mimi ndiyo mwenyekiti wao bahati nzuri wengi wananikubali".
"Kuna mwananchi mmoja waligombana nikamwita kwa barua alikataa kuja akasema hanitambui kwakuwa ninajiamini nikamwambia sasa utanitambua kuwa mimi ni mwenyekiti na kufikisha ngazi za juu alivyoona nimekuwa mkali alikuja kuomba radhi kwa kuwa alikiri kosa nikamsamehe nilitaka nimwonyeshe kuwa hata mwanamke ana uwezo wa kujisimamia",anasema Kibasa.
Mahende Kangoye mkazi wa mtaa wa Kibasa anasema Mwenyekiti huyo anafaa kuongoza kwa kuwa ni mtu anayejali watu na kwamba hakuna changamoto inayotokea akashindwa kuitatua,anasisitiza kuwa kadri siku zinavyokwenda mila kandamizi zinapungua.
Kangoye anasema kuwa baadhi ya wanawake ni waoga kusimama mbele za watu hali inayosababisha wasigombee,anasema usipokuwa jasiri huwezi kuongea au kushauri jambo kwenye mikutano.
Anaongeza kwamba mila ya Kabila la Wakurya mwanamke hawezi kufanya jambo bila ruhusa ya mme wake na wengine ukataliwa na ukijichukulia maamuzi yao hufukuzwa nyumbani hali inayosababisha wengine kuacha kugombea.
"Wapo baadhi ya wanaume wakiona mwanamke anaongea jukwaani wanasema huyu mwanamke ni shida nyumbani mara atakuwa ana sauti nyumbani, ukienda kwenye vikao ukachelewa anadhani ulikuwa kwa wanaume",anasema.
Anaongeza" ni vyema wanaume waelimishwe watambue kuwa hata mwanamke anaweza kuongoza na kuna wanawake wana uwezo lakini niwaoga anajiuliza kuwa nikipata uongozi je nitahimili mikikimikiki ya vijana, nitaweza kweli anaamua kuacha" anasema Kangoye.
Katibu wa Umoja wa Wanawake Chama cha Mapinduzi (UWT) wilaya ya Tarime Sauda Kashombo anasema kuwa kuna haja ya elimu kuendelea kutolewa ili kuwapa fursa kugombea na kwamba wasiwe na hofu kwani uongozi si nguvu bali ni akili.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Tarime Mkaruka kura anasema kuwa baadhi ya wanawake hawajiamini kuwa wana uwezo wa kugombea na wanaume na kwamba Chama cha Mapinduzi hutoa kipaumbele kwa wanawake lakini baadhi yao wanashindwa baada ya kutopigiwa kura wakati wa kura za maoni na kwenye uchaguzi.
Lilian Liund ni Mkurugenzi wa Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) anasema kuwa ushindi wa wanawake kwenye chaguzi hutegemea uamuzi wa wapiga kura,wanawake kwa wanaume, na kwamba wanawake ndiyo ujitokeza kwa wingi kupiga kura ikilinganishwa na wanaume.
Liund anatoa rai kwa wanawake na wanaume kuwapigia kura wanawake wenye uwezo na wenye kubeba ajenda ya ukombozi wa mwanamke,kuhakikisha wanahamasisha wanawake wenye uwezo wanajitokeza kugombea,Kushawishi vyama kuteua wanawake,kuwapa moyo wanawake waliojitokeza kuwania viti vya uchaguzi na kuwapigia kura.
FULL POWER , ZATI 50 SULUHISHO LA KUDUMU NGUVU ZA KIUME NA UUME MDOGO

Sababu za upungufu wa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume
⇒Ngiri,
⇒Henia
⇒Kisukari
⇒Tumbo kujaa gesi
⇒Kutopata choo vizuri
⇒Utumiaji madawa kwa muda mrefu
⇒Unywaji wa pombe kupita kiasi
⇒Msongo wa mawazo
⇮⇒Haya yote hupelekea mwili kutokuzalisha homoni ya gesrtogine au kuwa chache na kushindwa kupata mzunguko mzuri wa damu na vichocheo vingine kama madini ya zinki ambayo hukufanya kuwa na msisimko na kufanya kuwa na muda mrefu na nguvu za kutosha.
FULL POWER
⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.
⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa
⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.
Zati 50
⇨ Inarutubisha maumbile ya uume na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4
⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.
Pia tunatibu Magonjwa mengine Kama
Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonga vya tumbo,Kisukari,Magonjwa sugu ya zinaaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kungoa
Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga.
Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27


MATUKIO YA ZIARA YA KIMASOMO YA WASHINDI WA SHINDANO LA CMSA KWA VYUO VIKUU NA TAASISI ZA ELIMU YA JUU

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA)
Nicodemus Mkama akizungumza na wanafunzi (hawapo pichani) wakati wa
ziara ya mafunzo ya washindi wa shindano la vyuo vikuu na Taasisi za
Elimu ya Juu kwa mwaka 2019 linaloendeshwa na CMSA.

Baadhi ya washindi wa Shindano linaloendeshwa na CMSA kwa vyuo vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu kwa mwaka 2019.

Watendaji wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA)
wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa mamlaka hiyo (hayupo pichani)wakati
wa ufunguzi wa ziara ya kimasomo kwa washindi.

Ofisa wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) akiwafundisha wanafunzi
vinara wa shindano la vyuo vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu kwa mwaka
2019.

Ofisa wa Soko la Hisa Dar es Salaam(DSE)wakiongea na wanafunzi.

Mkurugenzi wa Utafiti,Sera na Mipango CMSA, Alfred Mkombo (wa kwanza
kulia) na Mkurugenzi wa Usimamizi na Maendeleo ya Masoko CMSA,Exaut
Julius.

Mkurugenzi wa Utafiti,Sera na Mipango CMSA, Alfred Mkombo
akiwasilisha mada katika ziara ya wanafunzi washindi wa shindano la
CMSA kwa vyuo vikuu.

Mmoja wa watendaji akizungumza na wanafunzi.
Waziri Mkuu Majaliwa Aridhishwa na Maandalizi ya Kituo Cha Kuhudia Wagonjwa wa Corona
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea eneo lililotengwa kwa ajili kuwahudumia watu watakaobainika kuwa na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) na amesema ameridhishwa na maandalizi.
Aliyasema hayo jana (Jumamosi, Machi 28, 2020) wakati akizungumza na wananchi wilayani Kibaha, Pwani baada ya kukagua hospitali ya wilaya ya Kibaha ambayo imetengwa kwa ajili ya kuwahudumia watu watakaogundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.
Alisema Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kukabilia na COVID-19, ambapo kwa sasa watu wote wanaoingia nchini kupitia viwanja vya ndege, vituo vya mabasi na bandari lazima wapimwe na wakigundulika wanamaambukizi wanawekwa kwenye maeneo maalumu kwa muda wa siku 14.
“Tunazingatia sana wale wanaotoka kwenye nchi ambazo zimeathirika sana wakiingia hapa Tanzania tunawazuia kwanza, tunawapima na tunafuatilia historia yake anatoka wapi na tunaangalia katika siku 14 amepita kwenye nchi zipi.”
Waziri Mkuu alisema wawaweka kwenye maeneo maalumu ili kuweza kuwapima kila siku na kujirishika kama hawana maambukizi kwani mtu anaweza kupimwa leo akaonekana yuko vizuri lakini ana maambukizi ambayo bado hayaonekani kwenye vipimo. Kama katika kipindi cha siku 14 mtu atabainika hana maambukizi anaruhusiwa kwenda kujiunga na familia.
Pia, alisisitiza wananchi waendelee kufuata maelekezo yaliyotolewa na Serikali kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kuzuia mikusanyiko na kwa wale wanaosafiri kwenye usafiri wa umma wasibanane kila mtu akae kwenye kiti.
Waziri Mkuu alisema wananchi wanapokwenda kufuata huduma kwenye masoko wahakikishe wanapeana nafasi baina ya mtu mmoja na mwingine na kabla hawajaingia katika maduka wanawe mikono kwa sabuni na maji tiririka ili kujikinga na maambukizi ya corona.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu alisema Serikali imeanza kuwachukulia hatua watu wote wanaopotosha kuhusu taarifa za ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19). “Aliyetangaza kuwa shule zinafunguliwa tumeshamkamata na atachukuliwa hatua.”
Hivyo aliwataka wananchi wajihadhari na taarifa zinazotolewa na watu ambao si wasemaji rasmi. Alisema taarifa kuhusu virusi vya corona itatolewa na Waziri Mkuu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Msemaji wa Serikali.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
Korea Kaskazini yafyatua baharini Makombora Mawili
Korea Kaskazini imefyatua leo kile kilichoonekana kuwa ni makombora mawili ya masafa mafupi katika pwani yake ya mashariki, ikiwa ni jaribio la nne la aina hiyo katika mwezi huu wakati ulimwengu ukipambana na janga la virusi vya corona.
Taarifa ya pamoja ya Wakuu wa Jeshi la Korea Kusini imesema makombora mawili yalifyatuliwa kuelekea mashariki kutokea mji wa bandari wa Wonsan na kuanguka katika Bahari ya Japan, inayofahamika pia kama Bahari ya Mashariki.
Wizara ya Ulinzi ya Japan imesema makombora hayo hayakuvuka mipaka yake ya baharini au kufika katika kanda ya kipekee ya kiuchumi ya nchi hiyo.
Korea Kaskazini wiki moja iliyopita ilifyatua makombora mawili ya masafa mafupi.
Siku moja baadaye, chombo cha habari cha nchi hiyo yenye silaha za nyuklia kikatangaza kuwa Rais wa Marekani Donald Trump alimtumia barua kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ikielezea kwa kina mpango wa kukuza mahusiano.
Credit: DW
Taarifa ya pamoja ya Wakuu wa Jeshi la Korea Kusini imesema makombora mawili yalifyatuliwa kuelekea mashariki kutokea mji wa bandari wa Wonsan na kuanguka katika Bahari ya Japan, inayofahamika pia kama Bahari ya Mashariki.
Wizara ya Ulinzi ya Japan imesema makombora hayo hayakuvuka mipaka yake ya baharini au kufika katika kanda ya kipekee ya kiuchumi ya nchi hiyo.
Korea Kaskazini wiki moja iliyopita ilifyatua makombora mawili ya masafa mafupi.
Siku moja baadaye, chombo cha habari cha nchi hiyo yenye silaha za nyuklia kikatangaza kuwa Rais wa Marekani Donald Trump alimtumia barua kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ikielezea kwa kina mpango wa kukuza mahusiano.
Credit: DW



































