Sunday, 29 March 2020

Korea Kaskazini yafyatua baharini Makombora Mawili

Korea Kaskazini imefyatua leo kile kilichoonekana kuwa ni makombora mawili ya masafa mafupi katika pwani yake ya mashariki, ikiwa ni jaribio la nne la aina hiyo katika mwezi huu wakati ulimwengu ukipambana na janga la virusi vya corona. 

Taarifa ya pamoja ya Wakuu wa Jeshi la Korea Kusini imesema makombora mawili yalifyatuliwa kuelekea mashariki kutokea mji wa bandari wa Wonsan na kuanguka katika Bahari ya Japan, inayofahamika pia kama Bahari ya Mashariki. 

Wizara ya Ulinzi ya Japan imesema makombora hayo hayakuvuka mipaka yake ya baharini au kufika katika kanda ya kipekee ya kiuchumi ya nchi hiyo. 

Korea Kaskazini wiki moja iliyopita ilifyatua makombora mawili ya masafa mafupi. 

Siku moja baadaye, chombo cha habari cha nchi hiyo yenye silaha za nyuklia kikatangaza kuwa Rais wa Marekani Donald Trump alimtumia barua kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ikielezea kwa kina mpango wa kukuza mahusiano. 

Credit: DW


Share:

Alliance One Yatoa Vifaa Vya Ujenzi Vya Milioni 23.9 Kwa Wilaya Mbili Za Mkoa Wa Tabora

NA TIGANYA VINCENT
KAMPUNI ya Tumbaku ya Alliance One Tanzania (AOTTL)  imeukabidhi uongozi wa Mkoa wa Tabora vifaa mbalimbali vikiwemo vifaa ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni 23.9.

Msaada huo umekabidhiwa jana na Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Kampuni hiyo David Mayunga kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri katika halfa iliyofanyika Ofisini kwake.

Mayunga alivitaja vifaa vilivyotolewa ni Bati 270, Saruji mifuko 300  na nondo 320.

Alisema msaada huo kwa ajili ya ujenzi wa mabweni na vyoo  katika Wilaya ya Tabora na Wilaya ya Uyui kwa ajili ya kuwasaidia watoto wa kike.

Mayunga alisema Wilaya ya Tabora imepewa mifuko 200 ya saruji na nondo 240 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 8.6.

Alisema msaada huo ni kwa ajili ya ujenzi wa mabweni katika Shule ya Sekondari ya Itojanda na Ndevelwa zote za Manispaa ya Tabora.

Mayunga alisema kwa upande wa Wilaya ya Uyui wamekabidhi mabati 250 , mifuko 100 ya saruji na nondo 80 kwa ajili ya kuunga mkono ujenzi wa Mabweni ya watoto wa kike katika Sekondari ya Idete na kumalizia majengo ya shule mpya ya Nsimbo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mwanri aliwataka Idara Wakuu wa Wilaya zote zilizopata msaada huo  kuhakikisha vifaa hivyo vinatumika kwa malengo ya kutoa mazingira mazuri ya watoto wa kike kupata elimu.

Alionya kuwa hatasitakuchua hatua kwa watendaji wote waliopewa vifaa ambao watavitumia kwa maslahi binafsi.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala aliishukuru Kampuni ya Alliance One kwa msaada huo ambao utawasaidia kuongeza kampeni yake ya kujenga mabweni kwenye shule mbalimbali ili kuwa kinga watoto wa kike na mimba.

Alisema hatua hiyo ni muhimu katika kukabiliana na watoto kutembea umbali mrefu kwenda shuleni na huku njiani wakikutana na vishwawishi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya alisema msaada waliopata utasaidia kumalizia mbweni ya wasichana  katika Shule ya Idete ambayo walikuwa washaanza kujenga chini ya Kampeni ya Nishike mkono kuwasaidia watoto wa kike wapate elimu.


Share:

Maafisa Ustawi Na Maendeleo Ya Jamii Watakiwa Kutoa Elimu Kwa Ya Kujikinga Na Corona

Na Mwandishi wetu, Arusha
Wizara ya Afya kupitia Idara kuu ya maendeleo ya Jamii imeanza kutoa mafunzo kwa Wataalamu wa Ustawi wa Jamii pamoja na Maendeleo ya Jamii kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuelimisha Jamii kuhusu ugonjwa unaoenezwa na Virusi vya Corona.

Akifungua mafunzo hayo kwa maafisa wa Wilaya na kata zote za Mkoa wa Arusha jana tarehe 28/03/2020 jijini Arusha, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Bw. Hargeney Chitukuro amewataka kutumia fursa hiyo kuwaelimisha wananchi kwa usahihi kuhusu maambukizi na namna ya kujikinga na ugonjwa wa Corona bila hofu.

Bw. Chitukuro amesema kuwa, tangu ugonjwa huo ulipoingia Mkoani Arusha, mafunzo mbalimbali yameshatolewa kwa wataalamu na kuwaelekeza namna ya kuelimisha jamii jinsi ya kujikinga.

“Katika kipindi cha takribani wiki mbili tangu ugonjwa huu uingie tayari tumeshatoa mafunzo kwa wataalamu wa Afya 240 kwenye Wilaya zetu na Halmashauri zote. Kwa mafunzo ya leo tunatarajia kuwafikia wataalamu wa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Jamii zaidi ya 185” amesema.

Amewaomba pia wadau wote kuelekeza nguvu zao kushirikiana na Serikali katika kufanikisha ukarabati wa kituo cha dharura Mkoani Arusha pamoja na kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya kujikinga.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii, Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii Patrick Golwike ametoa wito kwa Maafisa hao ili kuepusha msongamano watumie Redio za Jamii zilizopo kwenye maeneo yao kuelimisha jamii.

“Baadhi ya Halmashauri zina Televisheni zao pamoja na Redio za kijamii. Vyombo hivi vikitumika vizuri kwenye kusambaza elimu ya kujikinga na virusi vya Corona ili kuepuka msongamano, zitakuwa ni sehemu mojawapo ya kusaidia kufikisha ujumbe” amesema.

Akitoa mada kwa washiriki hao, Dkt. Meshack Chinyuli kutoka Wizara ya Afya, kitengo cha Elimu kwa Umma amewasisitiza kutumia takwimu sahihi zinazotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na hapa nchini ni Wizara ya Afya.

Awali akitoa lengo la mafunzo hayo kwa washiriki, Afisa Ustawi wa Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya, Idara ya Maendeleo ya Jamii Zakia Mohamed amesema kuwa mafunzo hayo yatawajengea uelewa wa kufahamu njia za maambukizi, dalili zake na inapotokea mtu amepata dalili ni wajibu wa maafisa hao kuelekeza wapi pa kwenda kupata huduma.

Akishukuru kwa niaba ya washiriki, Afisa maendeleo ya Jamii Mkoa Bi. Blandina Mkini amewahimiza Maafisa hao kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha kuwa Mkoa wa kwanza kuundoa ugonjwa huo hapa nchini.

“Sasa tutakuwa kifua mbele kwa sababu tuna tuna uwezo wa kumueleza mwananchi kuhusu ugonjwa huu na kukanusha upotoshaji” amesema.

Mgonjwa wa kwanza kuripotiwa nchini alitokea Mkoa wa Arusha hapo tarehe 16 Machi, 2020 ambaye amepona na hadi sasa wagonjwa waliothibitishwa ni 13.

MWISHO


Share:

NHC Yatakiwa Kukamilisha Ujenzi Jengo La Kitega Uchumi Mutukula

Na Munir Shemweta, WANMM MISENYI
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi DkT Angeline Mabula amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kukamilisha haraka mradi wake wa ujenzi wa Jengo la Kitega Uchumi lililopo mpaka wa Tanzania na Uganda eneo la Mutukula wilaya ya Misenyi mkoani Kagera ili kuliwezesha shirika kupata faida kupitia jengo hilo.

Dkt Mabula alitoa agizo hilo juzi wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo akiwa katika ziara yake mkoani Kagera kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo sambamba na kufuatilia utekelezaji maagizo aliyoyatoa kuhusiana na wa sekta ya ardhi.

Alisema, mradi wa jengo la kitega uchumi unaoendelea eneo la Mutukula uko sehemu nzuri ya mpakani mwa Tanzania na Uganda na kuna muingiliano mkubwa wa kibiashara hivyo ni vizuri Shirika la Nyumba likaona haja ya kuharakisha ujenzi wake ili kutoa fursa kwa taasisi na wawekezaji kupanga kwenye jengo hilo.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, mji wa Mutukula umechangamka na una mzunguko mzuri wa biashara hatua inayosababisha kuwepo mvuto kwa wafanyabiashara na wawekezaji katika eneo hilo na kukamilika kwake kutaiwezesha NHC   kupata wapangaji na kujipatia mapato.

‘’Naagiza Miradi yote ya Shirika la Nyumba la Taifa inayoweza kuliingizia Shirika mapato likiwemo hili la kimkakati lazima iishe ili NHC iingize mapato na kujiendesha kibiashara’’ alisema Dkt Mabula

Kwa upande wake Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mikoa ya Kagera na Geita Benit Masika alisema shirika lake liko katika jitihada kubwa za kuhakikisha mradi huo wa jengo la kitega uchumi Mtukula unakamilika mapema na kubainisha kuwa kwa sasa ujenzi wake umefikia asilimia 88 na utakapokamilika litapangishwa kwa taasisi zilizoonesha nia ya kupanga zikiwemo za kifedha kama vile mabenki.

Aidha, Nabu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliitaka halmashauri ya wilaya ya Misenyi mkoani Kagera kutumia vizuri fursa ya kuwa eneo la mpakani kwa kuhakikisha inakamilisha zoezi la kupanga, kupima na kumilikisha viwanja ili wananchi waweze kujenga nyumba nzuri na zenye sura ya nchi ya Tanzania.

Alisema, halmashauri ya Misenyi wakati wa kupanga mji huo ihakikishe inakuwa na soko la mazao zikiwemo ndizi ili kuwawezesha watanzania kuuza bidhaa zao nchini Uganda tofauti na sasa ambapo tegemeo kubwa lipo upande wa Uganda na kuwataka watanzania kubadilika kwa kuitumia fursa ya kuwa eneo la mpakani kuchangamkia kuwekeza katika ardhi.


Share:

Waziri Mkuu Majaliwa Atembelea Hospitali Ya Wilaya Ya Kibaha Iliyotengwa Kuwahudumia Wagonjwa Wa Corona

Waziri Mkuu, Kaasim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  (wa tatu kulia) wakati alipokagua hospitali ya wilaya ya kibaha iliyopo eneo la Lulanzi  ambayo imetengwa kwa ajili ya kuwahuduma kwa wagonjwa wa Coroma, Machi 28, 2020.  Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo  na wa pili kushoto ni  Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Muhammad Bakari.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Share:

Ulega: “Marufuku Kufunga Minada Kisa Corona.”

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega ametembelea mnada wa mifugo wa Pugu na soko la samaki ferry jijini Dar es Salaam na kutoa agizo la serikali kwa wakurugenzi wote nchini kutofunga minada ya mifugo na samaki kwa sababu ya maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid – 19, badala yake amewataka kushirikiana na watalaamu wa afya ili kuhakikisha shughuli zinazofanywa katika minada hiyo zinafanywa kwa tahadhari ikiwemo ya watu kunawa mikono wakati wa kuingia na kutoka katika minada hiyo kwa kutumia maji tiririka yenye dawa.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili March 29













Share:

Saturday, 28 March 2020

WANAKIJIJI 6 WANUSURIKA KUFA KWA KUSHAMBULIWA NA FISI WALIYEMZINGIRA WAMUUE SHINYANGA

Picha haihusiani na habari hapa chini
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Watu sita wamenusurika kufa kwa kushambuliwa na fisi baada ya kumzingira wakitaka kumuua katika kijiji cha katika kijiji cha Mwangh’alanga, kata na tarafa ya Samuye, wilaya na mkoa wa Shinyanga. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Deborah Magiligimba amesema tukio hilo limetokea Ijumaa Machi 27,2020 majira ya saa nne. 

“Chanzo cha tukio hilo ni watu hao kuvamiwa na fisi huyo baada ya kumzingira wakitaka kumuua. Hata hivyo wananchi walifanikiwa kumuua fisi huyo”,amesema Kamanda Magiligimba. 

Amewataja waliojeruhiwa kujeruhiwa na fisi kwa kung'atwa maeneo mbalimbali ya miili yao katika tukio hilo kuwa ni Zengo Jitonja , Nkuba Deteba , Juma Salaganda, Limbu Mihambo , Dutu Mdese na John Matana wote wakazi wa kijiji cha Mwangh’alanga Samuye 

Amesema majeruhi watano kati yao wamepata majeraha madogo madogo na hivyo wamepatiwa matibabu hospitalini na kuruhusiwa na hali zao zinaendelea vizuri. 

“Majeruhi mmoja Zengo Jitonja (56), amelazwa katika hospitali ya rufaa mkoa Shinyanga baada ya kujeruhiwa na fisi huyo mikononi na mdomoni na hali yake siyo mbaya sana”,ameongeza Kamanda Magiligimba.
Share:

VISA VYA MAAMBUKIZI YA CORONA VIRUS VYAONGEZEKA UGANDA NA KENYA, WAWILI WAPONA.

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES

CHANZO:BBC SWAHILI

Kenya imethibitisha visa saba zaidi vya maambukizi ya ugonjwa wa coronavirus, huku Uganda ikiandikisha visa vingine vitano vya ugonjwa huo hatari.
Akizungumza katika kikao na wanahabari siku ya Jumamosi, waziri wa Afya nchini Kenya Mutahi Kagwe amesema kwamba idadi hiyo inaongeza visa vya maambukizi nchini Kenya kufikia 38, huku mtu mmoja akiripotiwa kufariki naye mwingine akipona maambukizi hayo.
Waziri Kagwe amesema kwamba kufikia sasa mji mkuu wa Nairobi unaongoza kwa maambukizi ya visa 28.
Amesema kwamba kati ya visa hivyo saba kuna Wakenya wanne raia wawili wa DR Congo na raia mmoja wa China.
Ameongezea kwamba idadi hiyo ni miongoni mwa watu 81 ambao walifanyiwa vipimo katika maabara tofauti nchini katika kipindi cha saa 24.
Maambukizi ya virusi vya corona yaongezeka kote duniani huku China yakipunguaHaki miliki ya picha
Image caption


Amesema wanne kati ya visa hivyo ni watu wenye historia ya kusafiri katika mataifa yenye idadi kubwa ya maambukizi huku mmoja akiripotiwa kusafiri hadi Mombasa nao wengine wawili wakiambukizwa na visa vya awali.
Vilevile waziri huyo alikuwa na habari njema pale aliposema kwamba wagonjwa wawili waliokuwa wakiugua virusi hivyo wamepona.
''Mgonjwa wetu wa kwanza na watatu wamepona virusi hivyo , watafanyiwa vipimo vingine katika kipindi cha saa 48 , tuna matumaini kwamba vipimo hivyo vya pili vitabaini kwamba wamepona kabisa ili kuruhusiwa kutoka katika vituo vyetu vya tiba'', alisema.

Nairobi inaongoza kwa maambukizi

Amesema kwamba visa vyote saba vinatoka katika kaunti ya Nairobi ikiwa ndio inayoongoza , ikifuatiwa na kilifi visa 6, Mombasa visa 2 huku kajiado na Kwale zikiwa na kisa kimoja kila moja.
Aidha waziri huyo amesisitiza umuhimu wa kujitenga akisema mwanae na mpwa wake wametengwa ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.
''Mimi mwenyewe nina mwanangu ambaye amewekwa karantini . Pia nina mpwa wangu ambaye amewekwa karantini . Tunachosisitiza ni kwamba wakati mtu anapowekwa katika karantini anajilinda yeye na maisha ya wengine'', alisema Kagwe bila kutoa maelezo zaidi.
Image caption

Nchini Uganda

Wakati huohuo Idadi ya watu waliopata maambukizi ya virusi vya corona nchini Uganda imeongezeka na kufikia 23 kutoka 18 baada ya watu wengine watano kukutwa na maambukizi siku ya Ijumaa.
Kati ya sampuli 227 zilizofanyiwa vipimo siku ya Ijumaa watu 222 hawakupatikana na virusi vya corona huku watu watano wakipatikana na ugonjwa huo, alisema Dkt. Jane Ruth Aceng katika chapisho lake la mutandao wa twitter.
''Waganda tafadhalini fuateni maelezo na mikakati ya kuzuia kusambaa kwa virusi hivi. Tunaweza kuzuia maambukizi ya virusi hivi pamoja'', alisema afisa huyo.
Haki miliki ya picha
Hata hivyo Aceng hakutoa maelezo ya watu walioambukizwa.
Rais Museveni alisema kwamba kutokana na visa hivyo vipya huenda kukawa na umhimu wa kuchukua hatua kali zaidi ili kuzuia maambukizi kulingana na ujumbe wa twitter uliotumwa na katibu wake wa maswala ya habari bwana Don Wanyama .
Maafisa wa afya wanasema kwamba watu wote 14 waliothibitishwa hapo awali kuwa na virusi hivyo wanaendleea vyema katika hospitali ya Entebbe Grade B , Hospitali ya Mulago na hospitali kuu ya Adjumani.
Je utajilinda vipi?
jinsi ya kulinda dhidi ya virusi
Presentational white space

Presentational white space
Tumia kitambaa kuziba
Iwapo huna tishu tumia sehemu yako ya mkono
Jizuie kugusa macho yako , pua na mdomo iwapo hujaosha mikono
Jiepushe na watu ambao ni wagonjwa
Presentational white space

Je dalili ni zipi?

Presentational white space
Hizi ndizo ishara za ugonjwa huu
Presentational white space

Nifanyeje iwapo sijisikii vyema?

Piga simu ili upate usaidizi
Presentational white space
Pia unaweza kushauriwa usalie nyumbani
Presentational white space


Unaweza kufanyiwa vipimo vya virusi
Share:

Meya Manispaa Ya Iringa Ang'olewa Madarakani

Baraza la Madiwani la Manispaa ya Iringa limemwondoa Meya wa Manispaa ya iringa-Chadema Alex Kimbe baada ya kupiga kura ya kutokuwa na imani nae kufuatia tuhuma mbalimbali za matumizi mabaya ya madaraka

Kimbe ambaye anatokana na chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema ameng’olewa madarakani leo Jumamosi Machi 28, 2020 katika kikao maalum cha madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa hiyo.

Akitangaza matokeo ya kura zilizopigwa, mwenyekiti wa kikao ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa, Joseph Ryata amesema wajumbe waliohudhuria kikao ni 26 na kura 14 zimeridhia kumuondoa meya huyo.

Miongoni mwa tuhuma ambazo alikuwa anakabiliwa nazo Kimbe ni matumizi mabaya ya madaraka ikiwamo kufanya uamuzi bila kuzingatia kanuni za kudumu za Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.


Share:

WAZIRI MKUU APOKEA MISAADA YA SH. BILIONI 1.185 KUKABILIANA NA CORONA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa fedha pamoja na vitu mbali mbali kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) wenye thamani ya sh. bilioni 1.185 kutoka kwa wadau.



Amewataka Watanzania wote waendelee kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo ili kuzuia usisambae zaidi nchini. “Hii ni vita kubwa inahitaji tupigane kwa lengo la kuzuia janga hili lisisambae zaidi nchini, hivyo tuzingatie maagizo ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kumtaka kila Mtanzania ashiriki kwenye vita hii”

Amepokea msaada huo leo (Jumamosi, Machi 28, 2020) katika ofisi ndogo ya Waziri Mkuu iliyoko Magogoni, jijini Dar Es Salaam. Waziri Mkuu amewashukuru wadau hao na kuwataka Watanzania waendelee kushirikiana na Serikali katika hatua zinazochukuliwa kukabiliana na ugonjwa huo.

Miongoni mwa wadau waliotoa msaada huo ni taasisi za kifedha ikiwemo benki ya UBA Tanzania  iliyotoa sh. milioni 230, CRDB sh milioni 150 na  NMB sh milioni 100. Wadau wengine ni  Karimjee Jivanjee Ltd na kampuni zake tanzu waliotoa sh. milioni 200 pamoja na kuhaidi kufanyia matengenezo kinga ya magari yote ya Toyota yanayotumika katika kukabiliana na COVID-19 kwa muda ya siku saba bure, Familia ya Karimjee imetoa jenereta la KVA 180 lenye thamani ya sh. milioni 75.

Wengine ni Watoa Huduma ya Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) ambao wametoa bidhaa mbalimbali zikiwemo magari ya matangazo yatakayotumika kutoa elimu kwa muda wa miezi minne kupitia kampuni ya Advent Construction, maji ya kunywa (Bakhressa Group), Billboard (Ashton Media) vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya sh. milioni 150.

Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) walitoa matanki 1,000 yenye thamani ya sh. milioni 25, huku kila moja likiwa na ujazo wa lita 250, matanki hayo yametengenezwa maalumu kwa ajili ya kunawia mikono, pia Kampuni ya GS1 Tanzania Limited imetoa vitakasa mikono chupa 1,600 zenye thamani ya sh. milioni nne.

Kadhalika, Tanzania Oxygen ltd imetoa msaada wa sh. milioni 158 ambapo wamehaidi kufanyia ukarabati kiwanda kikubwa cha kuzalisha oxygen, Mount Meru imetoa vitakasa mikono vyenye thamani ya sh. milioni mbili, Hospitali ya Aga Khan imetoa dawa, sabuni, vitakasa mikono na vifaa tiba vyenye thamani ya sh. milioni 10.220.

Pia, kampuni ya gesi ya Oryx imehaidi kutoa msaada wa kusambaza gesi kwa ajili ya kupikia na matumizi mengine katika hospitali kama kufulia na kwenye vituo vya kuwahifadhi watu wanaohisiwa kuwa pamoja wagonjwa wa COVID-19. Gesi hiyo ina thamani ya sh. milioni 25, Tredea Cosmetics Ltd wametoa vitakasa mikono vyenye thamani ya sh.  milioni 1.6.

Umoja wa Mama lishe-Ilala na Machinga  wa Kariakoo wametoa sabuni na vitakasa mikono vyenye thamani ya sh. milioni mbili. Wakati huohuo, Chemba ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Wakulima (TCCIA) wametoa shuka 50, magodoro10, sabuni za maji chupa 170 na vitakasa mikono chupa 400 vyote vikiwa na thamani ya sh milioni tano.

Baada ya kupokea misaada hiyo, Waziri Mkuu kwa niaba ya Rais Dkt. Magufuli aliwashukuru wadau hao kwa vitu mbalimbali walivyovitoa kwa ajili ya kupambana na COVID-19 kwani vifaa pamoja na fedha walizozitoa zitaisadia Serikali katika kukabiliana na ugonjwa huo.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema Serikali kwa upande wake inaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kupambana na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha hausambai zaidi nchini. Alitumia fursa hiyo kuwashukuru madaktari, wauguzi pamoja na wataalamu wengine kwa huduma wanazozitoa.

Kuhusu wadau wengine wanaohitaji kutoa misaada, Waziri Mkuu amesema Ofisi yake iko wazi pia wanaweza kupeleka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kwa wanalio nje ya nchi au sehemu yoyote wanaweza kutuma fedha kupitia akaunti  yenye Jina la: National Relief Fund Electronic  Akaunti Na: 9921159801

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Jeshi La Polisi Laanzisha Operesheni Maalum Katika Kukabiliana Na Wimbi La Wizi Wa Magari

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Katika kukabiliana na Wizi wa Magari,Jeshi la Polisi limeanzisha Operesheni maalum ambapo hadi sasa jumla ya Magari  ya wizi 130 ,Pikipiki 193 na vipuli 753 na watuhumiwa 128 wameshakamatwa

Hayo yamesemwa leo Machi 28,2020 jijini D  odoma na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai hapa nchini [DCI]   Kamishna wa Polisi ,Robert Boaz  wakati akizungumza na Waandishi wa Habari.

Kamishna Boaz amesema  uchunguzi unaendelea kufanyika ili kuweza kubaini wahalifu wa Makosa mbalimbali.

“Kipindi hiki tumeshuhudia dalili za ongezeko la makosa ya wizi wa magari na Matukio haya mara nyingi yamekuwa yakitokea usiku watu wakiwa wameegesha magari hayo na wezi wamebuni mbinu mbalimbali za kufungua na kuwasha magari hivyo jeshi la polisi limeanzisha operesheni Maalum ambapo hadi sasa jumla ya Magari ya Wizi 130 yameshakamatwa na uchunguzi unaendelea”amesema

Aidha Kamishna Boaz  amebainisha  kuwa katika kipindi cha  Miezi miwili ya kwanza kuanzia Januari hadi Februari Mwaka huu  hali ya uhalifu imezidi kupungua kutoka Matukio makubwa ya uhalifu  elfu tisa mia tano na sabini na mbili[9572] hadi Makosa   elfu tisa mia mbili sitini na tatu[9263 ] ambapo ni sawa na upungufu wa matukio mia tatu na tisa[309] ikiwa ni sawa na  asilimia  3.2%.

Kuhusu Makosa ya Usalama barabarani Kamishna Boaz amesema yamepungua kutoka 533 hadi makosa 425 sawa na upungufu wa makosa 108 sawa na asilimia 20.3% .

Pia  Kamishna Boaz ametoa tahadhari kwa wananchi kufuata taratibu pindi wanaponunua magari makuukuu ikiwa ni pamoja na kwenda kulikagua polisi hali itakayosaidia kujiepusha ununuzi wa magari ya wizi.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger