Saturday, 28 March 2020

WAZIRI MKUU APOKEA MISAADA YA SH. BILIONI 1.185 KUKABILIANA NA CORONA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa fedha pamoja na vitu mbali mbali kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) wenye thamani ya sh. bilioni 1.185 kutoka kwa wadau.



Amewataka Watanzania wote waendelee kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo ili kuzuia usisambae zaidi nchini. “Hii ni vita kubwa inahitaji tupigane kwa lengo la kuzuia janga hili lisisambae zaidi nchini, hivyo tuzingatie maagizo ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kumtaka kila Mtanzania ashiriki kwenye vita hii”

Amepokea msaada huo leo (Jumamosi, Machi 28, 2020) katika ofisi ndogo ya Waziri Mkuu iliyoko Magogoni, jijini Dar Es Salaam. Waziri Mkuu amewashukuru wadau hao na kuwataka Watanzania waendelee kushirikiana na Serikali katika hatua zinazochukuliwa kukabiliana na ugonjwa huo.

Miongoni mwa wadau waliotoa msaada huo ni taasisi za kifedha ikiwemo benki ya UBA Tanzania  iliyotoa sh. milioni 230, CRDB sh milioni 150 na  NMB sh milioni 100. Wadau wengine ni  Karimjee Jivanjee Ltd na kampuni zake tanzu waliotoa sh. milioni 200 pamoja na kuhaidi kufanyia matengenezo kinga ya magari yote ya Toyota yanayotumika katika kukabiliana na COVID-19 kwa muda ya siku saba bure, Familia ya Karimjee imetoa jenereta la KVA 180 lenye thamani ya sh. milioni 75.

Wengine ni Watoa Huduma ya Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) ambao wametoa bidhaa mbalimbali zikiwemo magari ya matangazo yatakayotumika kutoa elimu kwa muda wa miezi minne kupitia kampuni ya Advent Construction, maji ya kunywa (Bakhressa Group), Billboard (Ashton Media) vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya sh. milioni 150.

Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) walitoa matanki 1,000 yenye thamani ya sh. milioni 25, huku kila moja likiwa na ujazo wa lita 250, matanki hayo yametengenezwa maalumu kwa ajili ya kunawia mikono, pia Kampuni ya GS1 Tanzania Limited imetoa vitakasa mikono chupa 1,600 zenye thamani ya sh. milioni nne.

Kadhalika, Tanzania Oxygen ltd imetoa msaada wa sh. milioni 158 ambapo wamehaidi kufanyia ukarabati kiwanda kikubwa cha kuzalisha oxygen, Mount Meru imetoa vitakasa mikono vyenye thamani ya sh. milioni mbili, Hospitali ya Aga Khan imetoa dawa, sabuni, vitakasa mikono na vifaa tiba vyenye thamani ya sh. milioni 10.220.

Pia, kampuni ya gesi ya Oryx imehaidi kutoa msaada wa kusambaza gesi kwa ajili ya kupikia na matumizi mengine katika hospitali kama kufulia na kwenye vituo vya kuwahifadhi watu wanaohisiwa kuwa pamoja wagonjwa wa COVID-19. Gesi hiyo ina thamani ya sh. milioni 25, Tredea Cosmetics Ltd wametoa vitakasa mikono vyenye thamani ya sh.  milioni 1.6.

Umoja wa Mama lishe-Ilala na Machinga  wa Kariakoo wametoa sabuni na vitakasa mikono vyenye thamani ya sh. milioni mbili. Wakati huohuo, Chemba ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Wakulima (TCCIA) wametoa shuka 50, magodoro10, sabuni za maji chupa 170 na vitakasa mikono chupa 400 vyote vikiwa na thamani ya sh milioni tano.

Baada ya kupokea misaada hiyo, Waziri Mkuu kwa niaba ya Rais Dkt. Magufuli aliwashukuru wadau hao kwa vitu mbalimbali walivyovitoa kwa ajili ya kupambana na COVID-19 kwani vifaa pamoja na fedha walizozitoa zitaisadia Serikali katika kukabiliana na ugonjwa huo.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema Serikali kwa upande wake inaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kupambana na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha hausambai zaidi nchini. Alitumia fursa hiyo kuwashukuru madaktari, wauguzi pamoja na wataalamu wengine kwa huduma wanazozitoa.

Kuhusu wadau wengine wanaohitaji kutoa misaada, Waziri Mkuu amesema Ofisi yake iko wazi pia wanaweza kupeleka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kwa wanalio nje ya nchi au sehemu yoyote wanaweza kutuma fedha kupitia akaunti  yenye Jina la: National Relief Fund Electronic  Akaunti Na: 9921159801

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Jeshi La Polisi Laanzisha Operesheni Maalum Katika Kukabiliana Na Wimbi La Wizi Wa Magari

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Katika kukabiliana na Wizi wa Magari,Jeshi la Polisi limeanzisha Operesheni maalum ambapo hadi sasa jumla ya Magari  ya wizi 130 ,Pikipiki 193 na vipuli 753 na watuhumiwa 128 wameshakamatwa

Hayo yamesemwa leo Machi 28,2020 jijini D  odoma na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai hapa nchini [DCI]   Kamishna wa Polisi ,Robert Boaz  wakati akizungumza na Waandishi wa Habari.

Kamishna Boaz amesema  uchunguzi unaendelea kufanyika ili kuweza kubaini wahalifu wa Makosa mbalimbali.

“Kipindi hiki tumeshuhudia dalili za ongezeko la makosa ya wizi wa magari na Matukio haya mara nyingi yamekuwa yakitokea usiku watu wakiwa wameegesha magari hayo na wezi wamebuni mbinu mbalimbali za kufungua na kuwasha magari hivyo jeshi la polisi limeanzisha operesheni Maalum ambapo hadi sasa jumla ya Magari ya Wizi 130 yameshakamatwa na uchunguzi unaendelea”amesema

Aidha Kamishna Boaz  amebainisha  kuwa katika kipindi cha  Miezi miwili ya kwanza kuanzia Januari hadi Februari Mwaka huu  hali ya uhalifu imezidi kupungua kutoka Matukio makubwa ya uhalifu  elfu tisa mia tano na sabini na mbili[9572] hadi Makosa   elfu tisa mia mbili sitini na tatu[9263 ] ambapo ni sawa na upungufu wa matukio mia tatu na tisa[309] ikiwa ni sawa na  asilimia  3.2%.

Kuhusu Makosa ya Usalama barabarani Kamishna Boaz amesema yamepungua kutoka 533 hadi makosa 425 sawa na upungufu wa makosa 108 sawa na asilimia 20.3% .

Pia  Kamishna Boaz ametoa tahadhari kwa wananchi kufuata taratibu pindi wanaponunua magari makuukuu ikiwa ni pamoja na kwenda kulikagua polisi hali itakayosaidia kujiepusha ununuzi wa magari ya wizi.


Share:

Watumishi wa Serikali mipakani waaswa kutoisaliti nchi yao kujiepusha na ugonjwa wa Corona

Katika hali ya kupambana na maambukizi ya ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona, Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewataka maafisa uhamiaji pamoja na watumishi wengine katika bandari za mkoa huo pamoja na mpaka wa nchi kavu kuacha tabia ya kupokea rushwa kutoka kwa wageni hasa katika kipindi hiki ambacho ni hatari kwa nchi.

Mh. Wangabo amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa kwani kuwapitisha wageni hao kwa kutumia rushwa kutasababisha nchi itaingia kwenye madhara makubwa ikiwemo kuliangamiza taifa na kuongeza kuwa kufanya hivyo ni sawa na usaliti kwa nchi, hivyo aliwataka watumishi hao kuwa wazalendo na nchi yao, kwani kutofanya hivyo kuna uwezekano wa kupitisha mgonjwa mmoja ambae ataweza kupelekea madhara makubwa katika nchi.

“Kwahiyo muwe makini sana, vitendo vya rushwa marufuku na kila jambo lichukuliwe kwa umuhimu na uzito mkubwa sana, kumbukeni kwamba kwenye mipaka ndipo mmebeba taifa, kwasababu atakayepitishwa pale bila ya kuzingatia taratibu zinazotakiwa, bila ya kuchunguzwa vizuri, bila ya kuulizwa ulizwa vizuri historia alikotokea na kumuweka katika “isolation room” kama itabidi kulingana na atakavyokuwa ameonekana, msipofanya hivyo mtu akapita, basi mjue kabisa kwamba analeta vifo katika nchi yet una huo utakuwa ni usaliti kwasababu umelisaliti taifa kwa kupitisha mtu ili aje atuue,” alisisitiza.

Mh. Wangabo ameyasema hayo alipotembelea katika bandari ya Kabwe iliyopo katika kata ya Kabwe, Wilayani Nkasi ili kukagua utekelezaji wa maelekezo ya serikali juu ya kuandaa maeneo maalumu kwaajili ya kuwaweka wageni kwa siku 14 pamoja na kuona kituo cha huduma ya afya kilichotengwa maalum kwaajili ya kuwapokea watu wanaodhaniwa kuwa na ugonjwa wa Corona kwa uangalizi zaidi ambapo katika ziara hiyo aliambatana na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa pamoja na wataalamu wengine.

Aidha, Mh. Wangabo ameutaka uongozi wa Wilaya kuhakikisha wanatoa elimu ya udhibiti wa ugonjwa wa Corona kwa wenyeviti wa vijiji vyote vilivyopo katika mwambao wa ziwa Tanganyika kwani imebainika kuwa mara kadhaa vijiji hivyo hutumika kama bandari zisizo rasmi kuingiza wageni wanaotoka katika nchi za Jamhuri ya Watu wa Kongo, Burundi pamoja na Zambia.

Wakati akitoa taarifa ya maandalizi ya kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo wa Corona Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Dkt. Hashim Mvogogo amesema kuwa majengo ya Hospitali ya Wilaya yamepangwa kutumika kuhifadhi wagonjwa watakaobainika kuwa na Virusi vya Corona baada ya siku 14 na pia kutumika kama kituo cha tiba endapo wagonjwa hao watatokea na kuongezeka na kuongeza kuwa kata 21 na vijiji 62 vimeshapewa elimu ya afaya ya kujikinga na ugonjwa huo huku wananchi wakionekana kuelewa na kuhamasika.

“Katika Kata tumetumia wasimamizi wa afya, ndio maana ukiangalia hata katika baadhi ya shule kabla hazijafungwa tulizifikia shule 42, kwahiyo tulianza “intervention” mapema kwa maana ile timu ya Wilaya hatukuweza kufika kwenye hizo sehemu lakini tulitumia wataalamu wetu ambao wako katika zile sehemu, kwahiyo kiujumla kama elimu kiwilaya wote, karibia kata zote wanahiyo elimu, lakini zile kata ambazo hatukufikia wataalamu kutoka ngazi ya wilaya, tunahitaji pia tuzifikie na sisi,” Alisema.

Kwa upande wake Mwangalizi wa Bandari ya Kabwe Mohamed Issa amesema kuwa mbali na kutenga nyumba mojawapo ya mtumishi kwaajili ya kuwahifadhi wageni watakaoingia nchini kwa siku 14, pia kuna boti maalum ambayo imeandaliwa kwaajili ya kufanya doria katika badari bubu zaidi ya nne zilizopo katika vya karibu na bandari hiyo ili kujihadhari na uingiaji holela wa wageni hao.

“Boti hii ni kwaajili ya kufanya “patrol” kwenye bandari bubu ambazo ni pamoja na Utinta, Kalila, Korongwe na Msalamba ndio bandari bubu ambazo zinatumiwa na wafanyabiashara ambao sio waaminifu wanaokwepa mapato ya serikali, kwahiyo hii boti itatusaidia kufika maeneo hayo kwa urahisi ili pia kulinda mapato ya serikali,” Alisema.
 
Katika Wilaya ya Nkasi kuna bandari bubu zaidi ya 12 ambazo hutumika na wageni kuingia nchini huku bandari rasmi zinaz otambulika ni 3 ikiwemo, Kirando, Kabwe na Wampembe ambapo bandari hiyo ya ipo katika hatua za mwisho kumalizika kutanuliwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 7.4 na ujenzi wake kufikia asilimia 95% hali iliyopelekea Mh. Wangabo kuwataka wananchi wa Mkoa wa Rukwa kuitumia bandari hiyo na fursa zake vizuri ili kujiingizia kipato.


Share:

Mabasi Yote Yanayoingia Na Kutoka Dodoma Kupuliziwa Dawa ili Kukabiliana Corona

Mkuu wa Wilaya (DC) ya Dodoma Mjini nchini Tanzania Patrobas Katambi ameagiza mabasi yote yanayoingia jijini humo kupigwa dawa za kuuwa wadudu ikiwa ni hatua ya kukakibiliana na virusi vya Corona.

Akizungumza jana Ijumaa Machi 27 2020, Katambi amewaagiza Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Dodoma Mjini na halmashauri ya jiji kuhakikisha mabasi yote yanayokwenda mikoani kupigwa dawa ya kuuwa wadudu kabla na baada ya safari.

Ameagiza pia kupigwa dawa kwa maeneo yote yenye mikusanyiko mikubwa ya watu.

Amewataka wakazi wa Dodoma kufuata masharti yaliyotolewa na wataalam wa afya ili kuepukana na ugonjwa huo.


Share:

Watano Watiwa Mbaroni Kwa Kumkata Mapanga Na Kisha Kumpora Afisa wa Serikali

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linawashikilia watu watano wanaodaiwa kumkata mapanga kichwani ofisa wa serikali na kupora nyumbani kwake mali zenye thamani ya Sh. milioni 3.7.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa, aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Juma John (27), mkazi wa Bungu A, Japhet Charles (25) na Victor William (23), wote wakazi wa Chanika.

Kamanda Mambosasa aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Joseph Charles (28), mkazi wa Mbezi Juu na Anthony Christian (40), mkazi wa Temeke jijini.

Alisema watuhumiwa hao walikamatwa usiku wa Machi 22 mwaka huu maeneo ya Tegeta wakiwa na silaha za jadi ambazo ni mapanga na marungu.

“Watuhumiwa hawa walivamia nyumbani kwa Victor Nyirenda ambaye ni ofisa wa serikali na kumjeruhi kichwani kisha kupora simu mbili, kompyuta mpakato mbili aina ya HP, pochi na bahasha iliyokuwa na Sh. 500,000,” alisema.

Alibainisha kuwa watuhumiwa hao waliiba vitu vyenye thamani ya Sh. milioni 3.7 na baada ya taarifa kulifikia Jeshi la Polisi, ufuatiliaji ulianza na kuwakamata wote.

Kamanda Mambosasa alisema juzi walikamata watuhumiwa wengine wanne waliopokea vitu vya wizi kutoka kwa wahalifu wanaofanya matukio ya uvunjaji.

Alisema baada ya upekuzi kufanywa kwenye maduka ya watuhumiwa, walikamata kompyuta mpakato tatu, simu 10, luninga, deki na chaji za kompyuta.

Kamanda Mambosasa pia alisema jeshi hilo limekamata silaha mbili aina ya shotgun Pump Action na Maker Four.

Alisema silaha aina ya Shotgun Pump Action yenye namba za usajili 011822114, mali ya Kampuni ya Ulinzi ya OK Security, ilipotea katika mazingira ya kutatanisha.

Kamanda Mambosasa alisema katika tukio hilo, wamewakamata walinzi wawili wa kampuni hiyo ambao ni Akili Mlatoni (31), mkazi wa Mtoni Mtongani na Isack Junia (22), mkazi wa Mwananyamala Ujiji.

Alisema silaha hiyo iliibwa Machi 19 mwaka huu katika Kanisa la EAGT City Centre Mtoni Mtongani.

Alisema silaha ya pili imekutwa imetelekezwa katika ghala la Kampuni ya Enka Enterprises na kwa sasa wanaendelea kumsaka mmiliki wake.


Share:

Arusha Yazindua Zoaezi La Kupuliza Dawa Mabasi Ya Abiria Ili Kukabiliana Na Corona

Jiji la Arusha nchini Tanzania limeanza operesheni ya  kuyafanyia usafi  magari ya abiria kwa kuyapulizia dawa ya kuzuia virusi ugonjwa wa corona.

Shughuli ya kuyapulizia dawa imeanza jana  Ijumaa Machi 27,2020 na kuongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Fabian Daqarro.

Mhe.Gabriel Daqaro amesema kuwa operesheni hiyo ya upulizaji wa dawa utakuwa endelevu na utashirikisha wadau ambao tayari wameanza kutoa michago yao kuwezesha zoezi hilo.

Aidha Daqarro amewataka wananchi kutokuwa na taharuki na hofu pamoja kuzusha maneno ya upotoshaji juu ya ugonjwa huo bali waachie mamlaka husika kutoa taarifa pamoja na elimu.


Share:

Vigogo 6 Halotel Kortini Kwa Utakatishaji Fedha

Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel Son Nguyen (46), na vigogo wengine watano wa Viettel Tanzania wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka 10 yakiwemo ya kuisababishia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), hasara ya zaidi ya Sh bilioni 78

Washtakiwa wengine ni Nguyen Minh (40) na Vu Tiep Mameneja wa Halotel, Ha Than (39) Mtaalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) wa Halotel, Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni hiyo, Nguyen Cong na Kampuni ya Viattel.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa jana mahakamani hapo na wakili wa Serikali Mkuu Monica Mbogo  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, imedaiwa kati ya Juni 8, 2017 na Machi 26,2020 huko Mikocheni washtakiwa waliongoza genge la uhalifu ili kujipatia faida.

Katila shtaka la pili ikidaiwa siku na mahali hapo na katika  maeneo mengine ya nchi ya Tanzania washtakiwa kwa  pamoja walitumia masafa ya redio bila kupata kibali kutoka TCRA.

Imeendelea kudaiwa kuwa kati ya Julai 7,2016 na Machi 26, mwaka huu maeneo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Vietnam washtakiwa kwa pamoja walitengeneza mfumo ambao ulitumia huduma za mawasiliano zinazojulikana kama Virtual Private Network (VPN) kinyume na taratibu.

Aidha washitakiwa hao wanadaiwa kukwepa kulipa kodi kwa TCRA kwa kutumia mitambo ya mawasiliano yaliyounganisha Viettel Tanzania na Vietnam  kinyume na sheria na pia wanadaiwa kutumia masafa ya redio bila kupata kibali cha TCRA ambapo waliisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh bilioni 75.

Katika shtaka la sita washtakiwa hao wanadaiwa kati ya Julai 7, 2016 na Machi 26, mwaka huu kwa kutumia mitambo ya VPN waliisababishia TCRA hasara ya Sh bilioni 3.03 huku pia wakidaiwa kutakatisha Sh bilioni 3.03 wakati wakijua fedha hizo ni zao la makosa ya kuongoza genge la uhalifu.

Hata hivyo washitakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote mahakamani hapo kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu ambazo kwa kawaida kusikilizwa mahakama Kuu.
 
 Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 9, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa wamerudishwa rumande.


Share:

MWANAMKE AJIUA KARANTINI YA CORONA


Sehemu ya Shule ambayo imetengwa maalum, kwa watu wanaoingia Kenya kutoka nchi zilizoathiriwa na Virusi vya Corona.

Mwanamke mmoja raia wa Afrika kusini amejitia kitanzi kwenye karantini ya Shule ya Ufundi nchini Kenya (KITI), iliyopo Mjini Nakuru, eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya watu wanaoingia nchini humo kutoka Mataifa yaliyoripotiwa kuwa na ugonjwa wa Virusi vya Corona.

Jeshi la Polisi nchini humo kupitia kwa Kamishna wa Nakuru George Natembeya, amethibitisha kuwa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 27, alijitoa uhai kwa kujinyonga na kwamba Polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha hatua hiyo.

Akizungumzia tukio hilo Waziri wa Afya kaunti ya Nakuru Dkt Kariuki Gichuki, amesema mwanamke huyo aliingia nchini Kenya Machi 25 mwaka huu na alitakiwa kusalia eneo hilo kwa siku 14, kabla ya kukutwa chumbani kwake akiwa amefariki dunia.
Share:

Kenya yaanza kutekeleza amri ya kutotoka nje wakati wa usiku ili Kukabiliana na Corona

Amri ya kutotoka nje nchini Kenya kuanzia saa moja usiku hadi saa kumi na moja alfajiri ilianza kutekelezwa majira ya saa moja jana huku wafanyakazi wa huduma muhimu pekee wakiruhusiwa kuwa nje usiku.

Jana majira ya saa kumi na mbili Wakenya wengi mjini Nairobi walionekana wakiharakisha kuelekea nyumbani hatua iliyosababisha msongamano mkubwa katika barabara kadhaa huku wale waliokuwa wakitumia usafiri wa umma wakionekana kusubiri katika vituo vya magari hayo licha ya muda kuyoyoma.

Magari machache ya abiria mashuhuri kwa jina la ‘Matatu’ nchini Kenya yaliyokuwepo yalitumia fursa hiyo kujitengezea fedha baada ya kuongeza nauli huku baadhi yao yakikiuka agizo jipya la kupunguza idadi ya abiria ndani ya magari hayo ili kuwaepusha maambukizi ya virusi vya Corona.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kenya Hillary Mutyambai alionya jana kwamba wale watakaopatikana nje ya nyumba zao baada ya saa moja usiku watakabiliwa iwezekanavyo.

Hata hivyo mjini Mombasa na Eldoret mpango huo ulianza kwa mkosi baada ya maafisa wa polisi kukabiliana na wakaazi saa mbili kabla ya amri hiyo kuanza kutekelezwa.


Credit:Parstoday



Share:

Serikali Yapiga Marufuku Kuuza Ethanol Nje ya Nchi Ili Kuvilinda Viwanda vya Kuzalisha Vitakasa Mikono




Share:

Ofa: Jipatie Sabufa Hii Kwa 250,000 Tu, Na Tv Kuanzia 200,000 Tu. Soma Tangazo Lote

TAFADHALI SOMA TANGAZO LOTE KABLA HUJAPIGA SIMU. Bongo Deco Electronics ni duka la vifaa mbalimbali kkama tv, Friji, Home theater, na vingine vingi. Sasa wanakuletea sabufa hii yenye spika 5 na warranty ya mwaka 

1. Sabufa hii ni nzuri sana na inadumu sana.
Sabufa hii ina bluetooth, inashika radio mbalimbali, unaweza iunganisha na Tv, Deki au kingamuzi, pia ina seheemu ya Flash, Memory Card. 

Warranty yake ni mwaka 1. Kwa wakazi wa Dar unaweza kuja kuifata mwenyewe dukani au piga simu 0658184797 au 0752184797 tukuletee BURE kama upo Dar na utalipia 250,000 radio ikikufikia.

KWA WATU WA MIKOA MINGINE AMBAO MNGEPENDA KUPATA HUDUMA HII KUNA NJIA 2
1. MTUMIE HELA NDUGU YAKO ALIEPO DAR AJE AKUCHUKULIE HALAFU AKUTUMIE WEWE MKOANI.

2. UTUME HELA YA USAFIRISHAJI TUKUTUMIE SISI HADI HUKO MKOANI
 
SABUFA HII BEI 250,000 TU.

TV IPO KWENYE OFA NI 32INCH MPYA KWA 295,000 TU.

PIA TUNAUZA TV ZENYE WARRANTY YA MWAKA 1. Usafiri na kufungiwa ukutani ni BURE kwa Dar. Piga 0658184797 / 0752184797. Warranty mwaka 1 na Tupo KINONDONI STUDIO PEMBENI YA KITUO CHA MWENDOKASI. MKOANI TUNATUMA KWA GHARAMA ZA MTEJA MWENYEWE AU MTUMIE HELA NDUGU YAKO ALIEPO HUKU AJE AKUCHUKULIE.

SAMSUNG TV ZISIZO SMART
24inch 380,000
32inch 500,000
40inch 850,000
43inch 1,000,000

SAMSUNG SMART TV
32inch 630,000
40inch 1,000,000
43inch 1,100,000
43inch 4k 1,250,000
49inch 1,400,000
49inch 4k 1,550,000
50inch 4k 1,600,000
55inch 4k (Sio curved) 2,300,000
55inch 4k curved 2,350,000
65inch 4k 3,700,000
65inch 4k curved 3,800,000
75inch 5,000,000
 
LG TV (SIO SMART)
32inch 500,000
43inch 900,000
49inch 1,300,000

LG TV SMART TV
32inch 650,000
43inch 1,050,000
43inch 4k 1,200,000
49inch 1,400,000
49inch 4k 1,550,000
55inch 1,850,000
55inch 4k 2,200,000
65inch inch 3,200,000
75inch 4,500,000
 
HISENSE TV (SIO SMART)
32inch 450,000
40inch 620,000
43inch 800,000
49inch 1,100,000

HISENSE SMART TV
32inch 500,000
40inch 730,000 
43inch 850,000
43inch 4k 900,000
49inch 1,200,000
55inch 4k 1,600,000
65inch 4k 2,200,000

SONY TV (SIO SMART)
32inch 600,000
40inch 950,000
43inch 1,150,000

SONY SMART TV
32inch 800,000
40inch 1,150,000
43inch 1,350,000
49inch 1,800,000
55inch 4k 2,600,000
65inch 4k 5,550,000
BOSS TV (SIO SMART)
24inch 290,000
32inch 400,000 (zmeisha)
40inch 550,000 (zmeisha)

BOSS SMART TV
43inch 750,000
49inch 900,000
55inch 1,250,000 (zmeisha)

PINETECH TV (SIO SMART)
17inch 200,000
22inch 260,000
24inch 300,000
32inch 380,000

PINETECH SMART TV
32inch 480,000 (zmeisha)
43inch 750,000
55inch 1,300,000 (zmeisha)

SOYI TV (SIO SMART)
21inch 205,000
24inch 280,000
32inch 360,000
42inch 580,000

SOYI SMART TV
32inch 405,000
42inch 650,000
50inch 900,000
GOODVISION TV
32inch 300,000 OFA
42inch 600,000

GOODVISION SMART TV
32inch 430,000
42inch 650,000
50inch 900,000
55inch 1,200,000
STAR X TV (SIO SMART)
24inch 290,000
32inch 380,000
40inch 550,000 (zmeisha)
43inch 650,000
50inch 950,000

STAR X SMART TV
32inch 450,000
43inch 750,000
50inch 1,000,000
50inch 4k 1,050,000
55inch 1,250,000
65inch 2,000,000

UBEY TV SIO SMART
17inch 200,000
19inch 210,000
22inch 255,000
24inch 290,000
32inch 300,000 OFA
39inch 550,000

UBEY SMART TV
32inch 350,000 OFA
43inch 690,000
50inch 4k 880,000
55inch 1,150,000
65inch -2,000,000

 TCL (HITACHI) [sio smart]
32inch 470,000
43inch 750,000

TCL SMART TV
32inch 500,000
43inch 850,000
50inch 1,200,000
55inch 4k 1,500,000
65inch 2,800,000


Share:

Naibu Waziri Mabula Achoshwa Na Bajeti Za Upimaji Ardhi Halmashauri Za Mkoa Wa Kagera

Na Munir Shemweta, WANMM KAGERA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameonesha kutoridhishwa na kiasi cha fedha kilichotengwa na halmashauri nane za mkoa wa Kagera kwa ajili ya shughuli za kupanga, kupima na kumilikisha ardhi katika maeneo ya halmashauri hizo.

Hali hiyo inafuatia Naibu Waziri Mabula kuwahoji wakurugenzi wa halmashauri za mkoa wa Kagera kutaka kujua kila halmashauri ya mkoa huo imetenga kiasi gani cha fedha kwa ajili ya shughuli za upangaji, upimaji na umilikishaji ardhi katika bajeti ijayo ya mwaka 2020/2021 ikiwa ni juhudi za kuhakikisha maeneo yote yanapimwa ili kuondoa migogoro ya ardhi na kuongeza mapato kupitia sekta ya rdhi.

Akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Kagera jana Dkt Mabula alibaini halmashauri mbili za Misenyi na Kyerwa katika mkoa wa Kagera ndizo angalau zilizoonekana kutenga shilingi milioni 30 kwa kila moja kwa ajili ya shughuli za upangaji na upimaji ardhi katika maeneo yao.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa halmashauri ya Misenyi  Innecent Mkandara halmashauri yake imetenga milioni  50 kwa ajili ya shughuli za ardhi na milioni 30 kati ya hizo zitatumika kwa kazi ya upimaji huku mkurugenzi wa Kyerwa Shadrack Magamba akieleza halmashauri yake kutenga milioni 30 kwa kazi za upimaji sambamba na milioni 25 kwa ajili ya upimaji vijiji.

Halmashauri nyingine za mkoa huo zimetenga chini ya milioni 30 huku halmashauri ya Karagwe ikiwa ya mwisho kwa kutenga milioni 13 huku Mkurugenzi wake Godwin Kitonga akieleza kuwa sehemu kubwa ya halmashauri inayofanyika shughuli ya urasimishaji.

Dkt Mabula alisema kiasi kilichotengwa na halmashauri za mkoa wa Kagera katika kazi ya upangaji, upimaji na umilikishaji ardhi ni kidogo sana na hakioneshi kama wakurugenzi wake wana nia ya dhati ya kupima maeneo yao kwa kasi inayotarajiwa na wizara wakati halmashauri hizo ndizo zenye mamlaka ya upangaji kwenye maeneo yake.

Hata hivyo, Naibu Waziri wa Ardhi alisema katika kuhakikisha maeneo yote yanapangwa na kupimwa tayari wizara imeanzisha utaratibu wa kuzikopesha halmashauri fedha isiyo na riba kwa ajili ya shughuli za kupanga, kupima na kumilikisha maeneo ambapo kwa mwaka huu wa fedha  unaoisha halmashauri 24 zilikopeshwa na nne kati ya hizo ndizo zilizofanikiwa kurejesha mkopo huo kwa asilimia mia moja.

‘’Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021 Wizara ya Ardhi inatarajia kupatiwa bilioni saba kwa ajili ya kuzikopesha halmashauri, ni vizuri wakurugenzi mkatumia fursa hiyo kwa kuandika andiko litakalowawezesha kupata mkopo huo kulingana na maombi’’ alisema Dkt Mabula.

Sambamba hilo, aliwataka wakurugenzi wa halmashauri za mkoa wa Kagera kuhakikisha maeneo yote ya umma yanapimwa kufikia mwezi julai mwaka huu na kupatiwa hati ili kuondoa changamoto ya kuvamiwa na kupunguza migogoro ya ardhi ianyosababishwa na mipaka.

Akigeukia suala la mapato yatokanayo ya kodi ya pango la ardhi, Dkt Mabula alisema mkoa wa Kagera unaweza kuwa mkoa wa mwisho na kufuatiwa na ule wa Rukwa kwa kukusanya mapato kidogo ya sekta ya ardhi. Hali hiyo inafuatia kuelezwa kuwa hadi sasa mkoa huo umekusanya shilingi milioni 801 kati ya bilioni 3.3 ilizotakiwa kukusanya ambazo ni sawa na asilimia 23.

‘’Kwa mtindo huu hatuwezi kufika, tukisimamia vizuri sekta hii kwa kukusanya kodi ya ardhi tutamsaidia mhe rais kusimamia miradi ya kimkakati ambayo mingi inaendeshwa kwa fedha za ndani na sekta ya ardhi ikisimamiwa vizuri inaweza kukusanya fedha kuliko sekta nyingine’’ alisema Mabula.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi March 28

















Share:

Friday, 27 March 2020

Picha : FUSO YAGONGANA NA GARI NDOGO ROUND ABOUT USIKU HUU SHINYANGA MJINI…SPIDI KALI YATAJWA

Kumetokea ajali katika Mzunguko wa Barabara’ Round About’ ya Japanese Corner Mjini Shinyanga ambapo Fuso lenye Namba za usajili T609 COL kugongana na gari dogo aina ya IST lenye namba za usajili T435 DGL leo Ijumaa Machi 27,2020 majira ya moja na nusu usiku huu.



Mashuhuda wa tukio waliozungumza na Malunde 1 blog wamesema chanzo ni mwendo kasi wa dereva wa lori hilo ambaye baada ya kufika katika Round About hiyo gari lilimshinda na kugonga gari ndogo na kupinduka katika eneo.


“Hili Lori lilikuwa katika speed kali likitokea barabara ya Lubaga na dereva alipofika katika Round About alijaribu kufunga breki lakini kutokana na mwendo kasi aliokuwa nao gari lilimshinda na kupinduka mara kadhaa na kugonga gari ndogo”,wamesema mashuhuda.

“Ndani ya lori kulikuwa na wanaume watatu na kwenye gari ndogo kulikuwa na mwanamke,wote wamekimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu”,wameongeza.

Malunde 1 blog imeshuhudia miundo mbinu ya Round About hiyo ikiwa imeharibika kutokana na ajali hiyo huku askari wa usalama barabarani wakiwa eneo la tukio kuongoza magari kuepusha foleni na kuondoa wananchi waliofurika katika eneo hilo kushuhudia ajali hiyo.

Tutakutaarifu zaidi baada ya kuzungumza na Mamlaka zinazohusika ikiwemo jeshi la polisi kwa  taarifa zaidi kuhusu ajali hiyo..Endelea kutembelea Malunde 1 blog.
Muonekano wa Lori baada ya kupata ajali katika eneo la Round About eneo la Japanese Corner Mjini Shinyanga . Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mashuhuda wakiwa eneo la tukio
Muonekano wa lori baada ya ajali
Muonekano wa gari ndogo baada ya ajali Round About Shinyanga Mjini
Share:

WAJUMBE WATATU YANGA WAJIUZULU, WAWILI WASIMAMISHWA

Wajumbe watatu wa Kamati ya Utendaji Yanga wametangaza kujiuzulu nafasi zote walizokuwa nazo , huku wengine wawili wakisimamishwa kwa utovu wa nidhamu, ikiwa siku chache tangu Kampuni ya GSM kutishia kusitisha huduma zake klabuni.


Waliotangaza kujiuzulu na maamuzi yao kukubaliwa na kikao cha Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo ni Rodgers Gumbo, Said Kambi na Shija Richard, huku waliosimamishwa kwa muda usiojulikana ni pamoja na vigogo wa Kamati ya Usajili, Frank Kamugisha na Salim Rupia.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger