Monday, 23 March 2020

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu March 23























Share:

Sunday, 22 March 2020

Waziri Wa Kilimo Afuta Mikutano Yote Ya Wadau Wa Kilimo Iliyopangwa Kufanyika Mwezi Machi Na Aprili 2020 Ili Kujiepusha Na Corona

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Kutokana na kuwepo kwa ugonjwa wa homa kali ya mapafu ujulikanao kama corona Wizara ya Kilimo imeamua kufuta mikutano yote ya wadau wa mazao ya kilimo iliyopangwa kufanyika kati ya mwezi Machi na Aprili, 2020 hadi hapo baadae maelekezo yatakapotolewa na kuziagiza Bodi za mazao na Taasisi zote zinazohusika na mazao kuendelea na matayarisho ya nyaraka na miongozo mbalimbali itakayotumika katika msimu wa mwaka 2020/2021.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 22 Machi 2020 Ofisini kwake Jijini Dodoma na kuongeza kuwa Serikali haitajihusisha na upangaji wa bei za mazao ya wakulima kuanzia mwaka 2019/2020, badala yake vyama vya ushirika na wakulima wote kwa kushirikiana na wadau mbalimbali vimeagizwa kupanga bei za mazao kwa kuzingatia bei za masoko ndani na nje ya nchi. 

Kutokana na kuwepo kwa ugonjwa wa corona, minada yote itakayoendeshwa kwenye vyama vya ushirika vya korosho, kahawa, tumbaku, mkonge, pamba, n.k lazima mikusanyiko isiwe mikubwa na watu wakae mbali kati ya mita 2 na kuendelea kati ya mtu na mtu ili kupunguza msongamano.

Aidha, taasisi za Wizara ya Kilimo zinazoshughulika na mazao, zinatakiwa zianze matayarisho ya kuanza kununua mazao mbalimbali, Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA na taasisi ya Bodi ya Mazao Mchanganyiko zinatakiwa kujipanga kwa ajili ya kuanza ununuzi kwa mwaka 2019/2020.

Vile vile vyama vya ushirika wa mazao mbalimbali kama mahindi, mchele, choroko, dengu, mbaazi, kahawa, tumbaku, pamba, korosho n.k vinatakiwa kuanza maandalizi ya ununuzi wa mazao hayo kwa msimu ujao.  Pia wanunuzi wa mazao kama pamba, kahawa n.k wanatakiwa kulipa tozo za ushirika na Halmashauri kama ilivyokubalika katika vikao vya wadau haraka iwezekanavyo.

Kuhusu Muhtasari wa uchambuzi wa ukaguzi wa Vyama vya Ushirika uliofanyika katika kipindi cha miezi sita kuanzia Julai-Disemba 2019 amesema kuwa katika kipindi cha miezi sita jumla ya vyama 3,160 vimekaguliwa. Kati hivyo vyama vikuu ni 35, vyama vya mazao (AMCOS)  ni 1,882, vyama vya akiba na mikopo (SACCOS) 1,059 na vinginevyo ni 184.

Katika Daftari ya Mrajis wa vyama vya ushirika linaonesha kuwa kuna vyama vya ushirika 11,149 ambapo Vyama 3,436 vitafuta rasmi tarehe 17 April 2020.

Ameyataja matokeo ya ukaguzi huo uliohusisha vyama 4413, vyama 69 vimepata hati inayoridhisha, Vyama 1545 vimepata hati ya mashaka, Vyama 330 vimepata hati isiyoridhisha huku vyama 1216 vikiwa vimepata hati mbaya.

Waziri Hasunga amesema kuwa Kwa kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi inaamini kuwa ushirika ndiyo chombo pekee cha kumsaidia mwananchi mnyonge ili kuweza kupata bei nzuri za mazao yao, kuwaunganisha wakulima na kuwa na maisha mazuri, ikiwa ni pamoja na kuondoa umsakini wa wanyonge, ametoa maagizo 13

Ameiagiza Tume ya Maendeleo ya Ushirika kuanza kutoa elimu ya ushirika kwa vyama vyote nchini kwa namna ya kusimamia na kuviongoza vyama hivyo. Mafunzo ya kutunza kumbukumbu za vyama, mali, fedha na kutengeneza hesabu za mwaka pamoja na kufanya ukaguzi maalumu ndani ya mwezi mmoja kwa vyama vikuu 16 vilivyopata hati isiyoridhisha au mbaya.

Ameiagiza Tume ya ushirika katika kipindi cha miezi miwili kupitia vyama  vyote vilivyopata hati mbaya ambavyo ni vyama 1,216 na kuhakisha vinarekebisha mahesabu yao na kujibu hoja za ukaguzi sawasawa kadhalika kuhakikisha kwamba wanafuatilia taarifa ya uchunguzi maalumu ya vyama vyote vinavyotajwa kwenye ripoti kwa kufanya ubadhilifu wa fedha za vyama, Vyama hivyo ni pamoja na Chama cha msingi cha IKUZU (AMCOS), Chama cha KIREKA (AMCOS), chama cha Mkombozi (AMCOS), chama cha Minaki (AMCOS) na chama cha KABERA (AMCOS).

Pia ameitaka Tume ya ushirika kukamilisha miongozo na kanuni za namna ya kupata viongozi wenye elimu, sifa na uzoefu wa kutosha ndani ya miezi mitatu ili kuweza kuajiri watu wenye weredi, mafunzo na maadili ya uongozi na kuharakisha zoezi la kubadilisha Sheria ya Ushirika ili Serikali iwe na mkono, na kumuweza CAG kufanya ukaguzi wa nje wa vyama vya ushirika vyote na uwezo wa kusimamia maendeleo ya ushirika nchini.

Waziri Hasunga ameitaka Tume ya Ushirika kuhakikisha kuwa kila mwanachama wa ushirika anakuwa na akaunti ya benki ili kurahisisha mfumo wa malipo ya fedha zao na Kila makusanyo ya mapato ya ushirika au tozo za ushirika sharti zilipwe kupitia akaunti ya benki ya chama husika na malipo yote yatolewe kupitia benki.

Pia, ameitaka Tume kuhakikisha kuwa Vyama inatengeneza hesabu za fedha za mwaka kwa kuzingatia weledi na kanuni za utayarishaji wa hesabu za ushirika za kimataifa na Katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 vyama vya korosho vyote vinapaswa kukaguliwa na CAG kwa kuwa korosho yote ilinunuliwa na taasisi ya serikali.

Kadhalika, Waziri Hasunga ameagiza kuwa Vyama vikuu vyote kuajiri mameneja wa vyama wenye sifa na weledi unayohitajika katika kusimamia mali za ushirika kulingana na ukubwa wa chama kimapato huku akisema kuwa Tume inapaswa kuimarisha kitengo cha ukaguzi wa ndani ili kuvisimamia vyama vya ushirika kikamilifu.

Katika hatua nyingine Waziri Hasunga amewataka Watumishi wa TTume ya Ushirika kuanza kubadilika ili kujenga ushirika imara na wenye matumaini kwa wananchi. Uzembe, rushwa, ubadhirifu na kutofanya kazi sawasawa ni muhimu vikapigwa vita.

Ripoti inaonesha kuwa hali ya vyama vya ushirika inaendelea kuwa mbaya kinyume na matarajio ya Serikali. Mambo yaliyosababisha hali hiyo ni pamoja na Uelewa mdogo wa viongozi wa vyama vya ushirika katika kutengeneza hesabu za ushirika, Ubadhirifu wa makusudi wa mali na fedha za ushirika unaofanywa na baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika; na Uzembe wa makusudi na kusababisha upotevu wa mazao ya wakulima;

Mambo mengine yaliyosababisha ni pamoja na Udhaifu wa mifumo ya ukusanyaji wa mapato na madeni; Uelewa mdogo wa wanachama wa vyama wa kuchukua hatua na Uongozi na usimamizi mbovu wa vyama vya ushirika katika ngazi mbalimbali.

MWISHO


Share:

Tumia Mwika Kujitibu Busha, Nguvu za Kiume

Mwika ni dawa  ya asili ya nguvu za kiume yenye kutibu matatizo kwa wakati mmoja ;

(1)Nguvu za kiume
(2) Kunenepesha Maumbile
(3)Kuchelewe kufika kileleni

Yajuwe matatizo yanayosababisha upungufu wa nguvu za kiume

(1) Ngiri ya kupanda na kushuka
2.Korondani moja kuvimba
3.Tumbo kuunguruma kujaa gesi
4.Kisukari
5.Presha
6.Kiuno kuuma
7.Kutopata choo vizuri 

Pia tunatibu kisukari siku (14) vidonda vya tumbo siku (30), Miguu kufa ngazi, kuwaka moto .

Pia tunayo dawa ya mvuto wa mpenzi hata yupo mbali amekuacha atarudi na kutimiza ahadi zote mvuto wa biashara.

Wasiliana nasi kwa namba 0747100745 (Whatsap/ Kupiga kawaida)


Share:

WAGONJWA WA CORONA WAFIKIA 12 TANZANIA..RAIS MAGUFULI AHUTUBIA TAIFA

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania,  Dkt. John Pombe Magufuli amesema watu 12 wamebainika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona nchini Tanzania.
Katika hotuba yake kwa Taifa kiongozi mkuu huyo wa nchi leo Jumapili Machi 22, 2020 amebainisha kuwa kuanzia kesho Jumatatu Machi 23,2020 wasafiri watakaoingia Tanzania kutoka nchi zenye maambukizi ya corona watawekwa katika eneo maalum kwa siku 14 kwa gharama zao wenyewe.

“Mpaka sasa nchi yetu imebaini wagonjwa 12 ambao wamethibitika kuambukizwa corona. Kati yao wanne ni raia wa nje na wanane ni raia wa Tanzania. Wagonjwa wote isipokuwa mmoja ametoka kwenye nchi zilizokuwa na maambukizi ya ugonjwa huo.”

“Kuanzia kesho Machi 23 wasafiri wote watakaoingia nchini kutoka kwenye mataifa yaliyoathirika zaidi na ugonjwa huu watalazimika kufikia sehemu zilizotengwa na kukaa huko kwa siku 14 kwa gharama zao wenyewe”,amesema Rais Magufuli.

Share:

Rais Magufuli ataka Watanzania wasitishane Kuhusu Corona na badala yake wachukue tahadhari

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Watanzania kutotishwa na janga la ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (Covid-19) na badala yake waendelee kuchapa kazi na kujenga uchumi huku wakizingatia tahadhari zote za kujikinga kuambukizwa ugonjwa huo kama zilivyotolewa na wataalamu.

Mhe. Rais Magufuli amesema hayo leo tarehe 22 Machi, 2020 alipohudhuria Ibada ya Jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Paulo wa Msalaba, Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma, iliyoongozwa na Paroko wa Parokia hiyo Padre Onesmo Wisi.

Katika salamu zake katika Ibada hiyo, Mhe. Rais Magufuli amesema kuwepo kwa ugonjwa wa Corona isiwe sababu ya kutishana kiasi cha kumsahau Mwenyezi Mungu, hivyo ametoa wito kwa Wakristo na Waumini wa madhehebu mengine kumrudia Mwenyezi Mungu ili aepusha janga hili, badala ya kumwacha shetani atawale.

Mhe. Rais Magufuli amekemea tabia za baadhi ya watu wanaofanya mzaha juu ya ugonjwa huu ama kuwatia hofu wananchi kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, na badala yake ametaka Watanzania waendelee kuchapa kazi huku wakizingatia tahadhari.

“Watu tusitishane, tunatishana mno. Niwaombe ndugu Wakristo na Watanzania kwa ujumla wa Madhehebu yote, huu ndio wakati mzuri sana wa kumtegemea Mungu kuliko wakati wote, tuendelee kuchapa kazi, tuendelee kuujenga uchumi wetu, hatuwezi kusalimu amri kwa ugonjwa huu wa Corona na kushindwa kumtegemea Mungu na tukashindwa kuendeleza uchumi wetu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Amewashukuru viongozi wa Dini kwa kuungana na Serikali katika kuwahamasisha wananchi kuchukua tahadhari na ametoa wito kwa viongozi hao kuendelea kuliombea Taifa ili Mwenyezi Mungu aepushe balaa hili la Corona.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chamwino
22 Machi, 2020


Share:

Italia yavunja tena rekodi, watu 793 wafa siku moja kwa corona

Kwa mara nyingine tena Italia imevunja rekodi ya watu wengi zaidi waliokufa siku moja kutokana na maambukizi ya kirusi hatari cha corona kiasi kwamba katika kipindi cha masaa 24, watu 793 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa COVID-19 nchini humo.

Shirika la ha habari la Tasnim limelinukuu shirika la habari la AFP likitangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, Wakala wa Kuwalinda Raia wa Italia ulisema jana kuwa, idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na kirusi cha corona nchini humo ilikuwa ni 793 katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita na hadi kufikia jana watu 4800 walikuwa wameshafariki dunia nchini Italia kutokana na kirusi hicho.

Wakala huo wa kulinda raia nchini Italia pia umesema, hadi kufikia jana karibu watu 53600 walikuwa wameshaambukizwa ugonjwa wa COVID-19 ikiwa ni ongezeko la watu 6500 ikilinganishwa na tangazo lililotolewa juzi Ijumaa.

Italia hivi sasa ndiyo yenye idadi kubwa zaidi ya watu waliofariki dunia kutokana na ugonjwa wa COVID-19 na imeipiku hata China ulikoanzia ugonjwa huo. Hadi hivi sasa watu 3,255 wamefariki dunia kwa ugonjwa huo nchini China.

-Parstoday


Share:

Wadaiwa Sugu Kodi Ya Ardhi Kuanza Kuburuzwa Mahakamani Jumatatu

Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi itaanza kuwafikisha mahakamani wadaiwa wote sugu wa kodi ya pango la ardhi kuanzia kesho (tarehe 23 Machi 2020) katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni jitihada za Wizara hiyo kuhakikisha wamiliki wote wa ardhi wanalipa kodi kwa mujibu wa sheria.

Uamuzi wa kuwafikisha mahakamani wadaiwa hao unafuatia kushindwa kulipa madeni yao hata baada ya kupelelekewa ilani ya madai inayowataka kulipa madeni ya Kodi ya Pango la Ardhi ndani ya wiki mbili baada ya kupokea hati ya madai.

Malengo ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ni kukusanya shilingi bilioni 180 kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato ya ardhi. Vyanzo hivyo ni Kodi ya Pango la Ardhi, Ada za Upimaji Ardhi, Usajili wa Hati na Nyaraka pamoja na Ada zinazotozwa kupitia Mabaraza ya Ardhi ya Nyumba ya Wilaya.

Takriban wiki mbili sasa Maafisa kutoka Wizara ya Ardhi kwa kushirikiana na Watumishi walioko mikoani wamesambazwa maeneo mbalimbali nchini katika operesheni maalum ya kusambaza ilani za madai kwa wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi.

Akizungumza katika mahojiano maalum leo tarehe 22 Machi 2020 jijini Dodoma, Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Denis Masami alisema uamuzi wa kuwafikisha Mahakamani wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi unatokana na wadaiwa hao kushindwa kulipa madeni yao hata baada ya kupelekewa ilani za madai.

Alisema siku ya kesho (tarehe 23 Machi 2020) jumla ya mashauri 847 yatapelekwa katika Mabaraza ya Ardhi ya Nyumba ya wilaya katika mikoa ya Dar es Salaama, Mwanza na Lindi.

‘’Kesho tutapeleka Mashauri 847 katika Mabaraza ya Ardhi katika mkoa wa Mwanza mashauri 450, Lindi 121 na Dar es Salaam Ilala 200 na Temeke 76 na lengo hapa ni kuhakikisha tunakusanya kodi yetu ya pango la ardhi kama sheria ya umiliki ardhi inavyoelekeza’’ alisema Masami.

Mkuu huyo wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema, zoezi la kuwafikisha mahakamani wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi ni endelevu na kuwataka wamiliki wa ardhi waliopewa ilani za madai kuhakikisha wanalipa madeni ndani ya wiki mbili na kushindwa kufanya hivyo kutasababisha kufikishwa kwenye Baraza la Ardhi la Nyumba la Wilaya na huko maamuzi yake ni kupigwa mnada mali za mdaiwa kufidia deni.

Wakati wa uzinduzi mkakati maalum wa Wizara ya Ardhi wa kuongeza maduhuli ya serikali kupitia kodi ya pango la ardhi uliofanyika jijini Dodoma hivi karibuni, Kamishna wa Ardhi Nathaniel Nhonge aliwaeleza Watendaji wa serikali za mitaa wakiwemo Wenyeviti kuwa wizara yake itaanza kuwafikisha mahakamani wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi katika maeneo yote nchini.

Alisema, opresheni hiyo itaendeshwa na Maofisa wa Wizara ya Ardhi, watendaji wa sekta ya ardhi katika mikoa na halmashauri kwa ushirikiano na Wenyeviti Mitaa ili kurahisisha kuwafikia wamiliki wa ardhi wasiolipa kodi ya ardhi kwa wakati

Aliwataka watendaji wa serikali za mitaa na wenyeviti kushiriki kikamilifu katika operesheni hiyo sambamba na kusimamia uendelezaji maeneo kutokana na jukumu hilo kuwa kwao na kubainisha kuwa, kushindwa kuendeleza jukumu hilo kutasababisha migogoro ya rdhi na miji kuendelezwa kiholela.


Share:

Rais Magufuli Asali Ibada Ya Jumapili Katika Kanisa La Mtakatifu Paulo Wa Msalaba Jimbo Kuu Katoliki La Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waumini wa Kanisa la Mtakatifu Paulo wa Msalaba Jimbo kuu la Dodoma na Watanzania katika Ibada ya jumapili iliyoongozwa na Paroko wa kanisa hilo Padre Onesmo Wissi, ambapo Mhe. Rais amewataka Watanzania kutotishwa na ugonjwa Corona na badala yake wamtangulize Mungu mbele kwa Maombi huku wakizingatia tahadhari zote za kujikinga na ugonjwa huo. Machi 22, 2020.



Share:

Uganda Yaripoti Mgonjwa Wa Kwanza Wa Corona, Museven Kulihutubia Taifa Leo

Wizara ya Afya Uganda imethibitisha kisa cha kwanza cha corona, mgonjwa ni Mwanaume Raia wa Uganda mwenye umri wa miaka 36 ambae ameingia Uganda akitokea Dubai 

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amesema kuwa ifikapo saa 10:00 jioni ya Machi 22, 2020, atalihutubiwa Taifa la Uganda na kueleza ni hatua gani watachukua ili kukabiliana na kuenea kwa ugonjwa hatari unaosababishwa na Virusi vya Corona.
 
Rais Museveni ameyaandika hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter

"Kutokana na uthibitisho wa kisa kimoja cha mgonjwa wa COVID-19 nchini Uganda, leo saa 10:00 jioni, nitalihutubia Taifa juu ya hatua gani zaidi za kuchukua ili kupunguza kuenea kwa ugonjwa huu. Asante." ameandika Rais Museveni.


Share:

NHIF TANGA YATUA KILINDI KUHAMASISHA WANANCHI JUU YA VIFURUSHI VIPYA

< div class="separator" style="clear: both; text-align: center;">  MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akizungumza na waumini wa kanisa la Adventist (Wasabato) wakati akihamasisha juu ya vifurusi vipya vya mfuko huo katika halmashauri ya wilaya ya Kilindi mkoani Tanga
  MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akitoa elimu kwa mfanyabiashara wa viatu wilayani Kilindi kuhusu umuhimu wa kujiunga na bima ya afya wakati wa uhamasishaji wananchi juu ya vifurushi vipya katika halmashauri ya wilaya hiyo.
 AFISA Metekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Macrina Clemence  kulia akiwa na Mhasibu Mwandamizi wa NHIF Tanga Fredrick Mtangoo wakihamasisha mpango wa bima ya afya kwa wakazi wa mji wa Songe wilaya ya Kilindi wakatiuhamasishaji wananchi juu ya vifurushi vipya katika halmashauri ya wilaya hiyo.

 AFISA Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Tanga Josephine John akitoa elimu kwa wananchi wa mji wa Songe wilaya ya Kilindi wakati uhamasishaji wananchi juu ya vifurushi vipya katika halmashauri ya wilaya hiyo.
 AFISA Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Tanga Josephine John akitoa elimu kwa wananchi wa mji wa Songe wilaya ya Kilindi wakati uhamasishaji wananchi juu ya vifurushi vipya katika halmashauri ya wilaya hiyo.

 AFISA Metekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Macrina Clemence kulia akitoa elimu kwa wafanyabiashara wa soko la Songe wilayani Kilindi  juu ya vifurushi vipya katika halmashauri ya wilaya hiyo.
 AFISA Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Tanga Josephine John kushoto akitoa elimu kwa mfanyabiashara kwenye mji wa Songe wilaya ya Kilindi

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) umepiga kambi wilayani Kilindi Mkoani Tanga kwa ajili ya zoezi la uhamasishaji wananchi juu ya vifurushi vipya katika halmashauri ya wilaya hiyo.


Uhamasihaji huo ulifanyika kwenye maeneo  makao makuu ya  wilayani hiyo Songwe kwenye maeneo ya kanisani, msikitini,sokoni ,vituo vya bodaboda na stendi ya mabasi lengo kubwa kuwapa uelewa wananchi umuhimu wa kujiunga na mfuko huo.


Akizungumza wakati wa uhamasishaji huo Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu alisema kwamba lengo la kufika wilayani humo ni kuwafikia wananchi na kuzungumza nao juu ya umuhimu wa mfuko huo.


Alisema kwamba wananchi wengi,wafanyabiashara ndogondogo ,wananchi wa kawaida  walifikiria bima ya Afya ni kwa ajili ya viongozi,wakubwa na waajiriwa lakini wao wamefika kuwaeleza kwamba mfuko huo ni kwa ajili ya wananchi wote.


Meneja huyo alisema kwamba hivi sasa wana fao la Jipimie ambalo wamefika wilayani humo kuzungumza na wananchi katika maeneo yao ya biashara kuhusu umuhimu wa kujiunga nao.


“Kubwa zaidi wafanyabiashara wanapaswa kutambua kwamba ili waweze kuendeela na biashara zao ni muhimu kuwa na bima ya afya watatibiwa wakati wanapoumwa na hawatamaliza mitaji yao kwa sababu gharama za matibabu hazitawasumbua “Alisema Meneja huyo .


Aidha alisema pia alisema familia wakati mwengine zimekuwa zikiingia kwenye matitizo wakati mtoto anapoungua,mama hivyo ni fursa nzuri ya wananchi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanajiunga na bima ya afya ili waweze kunufaika na matibabu wakati wanapougua.


Akizungumzia mpango huo,Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilindi Bakari Kingalangala alisema kwamba mpango wa bima ya afya ni muhimu sana kwa jamii kwa sababu watu ambao hawana bima ya afya wanapoungua wanatoa fedha nyingi sana kugharamia matibabu na wakati mwengine kuyumba kiuchumi.


Alisema lakini wanapokuwa na bima ya afya inawasaidia kuweza kupata matibabu bila kuwaza kwamba watapata wapi fedha za kwenda kupata matibabu wanapoungua.


“Bima ya Afya ni muhimu sana kwa jamii kwa sababu mimi mwenyewe nimewaona watu ambao hawana uwezo wakipata mateso wakifika vituo vya afya, hospitalini kama huna bima unatoa fedha nyingi sana lakini ukiwa nayo inakusaidia kutibiwa na unaepuka gharama kubwa”Alisema.


Mwenyekiti huyo alisema kwamba  wayakuwa wahamasishaji kuwaeleza viongozi wa chama ngazi ya wilaya, kata  na vijiji umuhimu wa kujiunga na mpango wa bima ya afya ili kuweza kunufaika na huduma za matibabu pindi wanapougua.
Share:

Serikali Imewataka wanaouza Bidhaa za Kujikinga dhidi ya Covid-19, Kuuza kwa Bei iliyoko Sokoni

Na. Mwandishi Wetu-MAELEZO
Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto na Taasisi mbalimbali za Serikali imejipanga vyema kukabiliana na changamoto zinazohusiana na mapambano dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa Corona (Covid-19).
 
Katika kuhakikisha changamoto hizo zinatatuliwa jana Waziri Innocent Bashungwa ametembelea viwanda vinavyozalisha sabuni na Vitakasa mikono vilivyoko Jijini Dar es Salaam kuangalia bei ya bidhaa hiyo na kuwaagiza wafanyabiashara kuuza kuendana na bei iliyoko sokoni.
 
Katika mazungumzo na Waandishi wa Habari yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam, Waziri Bashungwa alisema kuwa maelekezo yaliyotolewa na Serikali yanalenga kuwasaidia wananchi kujua hatua stahiki zinazopaswa kuchukuliwa ili kujinga na Covid-19.
 
“Watanzania wote tunawiwa kuwa na mchango katika kupambana dhidi ya kuenea Covid-19, watalaam kutoka tume ya Ushindani (FCC), katika maeneo ya kuuzia barakoa (face masks), vikinga mkono (gloves), vitakasa mikono na kemikali za usafi wa mazingira (Hand sanitizer and surface disinfectant) katika eneo la Dar es Salaam watalaam wamebaini kuwepo kwa uhaba na changamoto ya kupanda bei kwa bidhaa hizo”, Alisema Waziri Innocent Bashungwa.
 
Waziri Bashungwa Amewataka wafanyabiashara kuacha njama za makusudi za kuficha bidhaa hizo kwa kigezo cha kuadimika hali ambayo inasababisha kupungua kwa uwezo wa kujikinga na kudhibiti ugonjwa huo wa Covid-19 kwa kuzuia maambukizi mapya.
 
Aidha Waziri Bashungwa alisema kuwa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), limebainisha kuwepo na umuhimu wa wazalishaji wa bidhaa za kujikinga na maambukizi mapya ya Covid-19, hususani kwa wazalishaji wa Vitakasa mikono (Hand Sanitizer)  kuzingatia viwango vilivyoweka na Shirika hilo.
 
“Kiwango kilichowekwa kwa uzalishaji wa vitakasa mikono ni Na. TZS 1650: 2014, kiwango hiki kinahusisha pia uwepo wa kileo (alcohol) ya walau asilimia 60 kuwezesha vitakasa mikono kuweza kufanya kazi iliyokusudiwa, kwa hiyo nawaelekeza TBS kushirikiana na wazalishaji waliopo na wapya ili kukidhi matumizi ya bidhaa hizo ili kuwawezesha wananchi kupata bidhaa yenye kiwango bora ili kudhibiti janga hili,” Alisema Waziri Bashungwa.
 
Alibainisha kuwa Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na taasisi zake imeendelea kufanya ukaguzi na uchunguzi sokoni ili kubaini endapo kuna vitendo vyovyote vya udanganyifu au vinavyokiuka sheria zinazosimamiwa na taasisi hizo ikiwemo TBS  katika kuzalisha, kuingiza,  kusambaza na kuuza bidhaa hizo.
 
Aliongeza kuwa kumekuwepo na udanganyifu wa bei za bidhaa hizo za kujinga dhidi ya Maambukizi ya Covid-19, hususani vitakasa mikono, kwa mujibu wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD), mil.250 inauzwa Tsh. 5,500, lakini baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakiuza kwa Tsh. 20,000, huku mil. 60 ikiuzwa Tsh. 2,500 lakini kwenye baadhi ya maduka  wanauza  kwaTsh.8,000, na amewataka wafanyabiashara kuuza kulingana na bei iliyoko sokoni.
 
“Nawaelekeza TBS na FCC kuendeleo kuchunguza bei,  uzalishwaji, uingizwaji wa bidhaa unaozingatia viwango vya ubora na ushindani  wa soko ili bidhaa hizi zipatikane kwa urahisi , zikidhi matarajio ya matumizi na zipatikane kwa bei ya soko, kwahiyo kwa wafanyabiashara wanaouza bidhaa hizo kwa bei ya juu wakibainika wafutiwe leseni ili tuone wataenda kuuza wapi”, Alisema Bashungwa
 
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango nchini TBS, Dkt. Yusuph Athuman Ngenya amewataka wananchi kuepuka habari za utengenezaji wa Vitakasa mikono, ikihusisha uwepo wa kiwango cha Alcohol kwa asilimia 60 ambacho ndiyo kiwango cha chini cha kutengeneza bidhaa hiyo ili iweze kupambana na Covid-19.
 
“Kuhusu ubora na kiwango cha chini cha Alcohol kwenye vitakasa mikono ni asilimia 60 ambacho kimebainishwa kwenye kiwango cha 1650: 2014 cha TBS, lakini pia tunahusika kwa kiasi kikubwa kudhibiti bidhaa zinazoingia nchini kwahiyo tumejipanga kulinda ubora wa vitakasa mikono hasa vinavyotoka nje ya nchi ili kupata bidhaa bora kwa matumizi ya wananchi kujikinga na Covid-19,” Alisema Dkt.Athuman.
 
Mwisho



Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili March 22













Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger