Saturday, 21 March 2020

Wanaoongeza bei vifaa vya kujikinga na Corona kuchukuliwa hatua za kisheria

Serikali imeiagiza Tume ya Ushindani wa Kibiashara na Shirika la Ubora wa Viwango (TBS) kufanya msako na kuwachukulia hatua wafanyabiashara watakaobainika kuongeza bei kwa makusudi kwa lengo la kujipatia faida kubwa katika kipindi hiki kigumu cha mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

Agizo hilo limetolewa leo Machi 21, 2020 na Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa ambapo pia amewaonya wafanyabiashara walioficha bidhaa za vitakasa (sanitizers) na barakoa (mask) kuacha mara moja huku akiwatoa hofu Watanzania kuhusu upatikanaji wa bidhaa hizo na kuongeza kuwa Serikali inafanya kila linalowezekana kuhakikisha bidhaa zinapatikana kirahisi na kwa bei nafuu.


Share:

Makonda : Mwananchi hauna mamlaka ya kutangaza mtu mwenye corona

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewataka wananchi wa mkoa huo kutojifanya wajuaji kwenye jambo la kutangaza ugonjwa wa corona.

Akizungumza na waandishi wa habari jana alisema watu wa mkoa wake ndio wanaongoza kwa kujifanya wajuaji na kutoa taarifa za wagonjwa wakati sio jambo sahii.

“Sasa niwaombe msilete ujuwaji kwenye janga hili la corona tujifanye wajinga kidogo”

“Mwananchi hauna mamlaka ya kutangaza mtu mwenye corona … wenye mamlaka anayo Waziri wa Afya, Waziri Mkuu na Rais, hata mimi  hamjanisikia nikitangaza kwenye mkoa wangu kuna wagonjwa wangapi?”alisema Makonda

Pia alisema kuwa watu wanatakiwa kuwa watulivu ili Mungu afanye miujiza yake.

“Tunaweza kula na kusherekea Pasaka bila corona hili litapita kama matatizo mengine yalivyopita.”

“Naomba tusifanye jambo la kunyanyapaa watu wenye corona na tusitumie mitandao ya kijamii kuwajaza hofu.”

“Sio unamwona mtu hospitali unaanza kutangaza kuwa anaumwa corona magonjwa yapo mengi, corona haijasitisha magonjwa mengine mtu anaweza kwenda hospitali kwa magonjwa mengine”alisema Makonda

Aidha amewataka watu kuacha kwenda sehemu za starehe  na kwamba wakitaka kunywa wafanye hivyo majumbani kwao na familia zao.


Share:

Tumia Mwika Kujitibu Busha, Nguvu za Kiume

Mwika ni dawa  ya asili ya nguvu za kiume yenye kutibu matatizo kwa wakati mmoja ;

(1)Nguvu za kiume
(2) Kunenepesha Maumbile
(3)Kuchelewe kufika kileleni

Yajuwe matatizo yanayosababisha upungufu wa nguvu za kiume

(1) Ngiri ya kupanda na kushuka
2.Korondani moja kuvimba
3.Tumbo kuunguruma kujaa gesi
4.Kisukari
5.Presha
6.Kiuno kuuma
7.Kutopata choo vizuri 

Pia tunatibu kisukari siku (14) vidonda vya tumbo siku (30), Miguu kufa ngazi, kuwaka moto .

Pia tunayo dawa ya mvuto wa mpenzi hata yupo mbali amekuacha atarudi na kutimiza ahadi zote mvuto wa biashara.

Wasiliana nasi kwa namba 0747100745 (Whatsap/ Kupiga kawaida)


Share:

BLOGA MBARONI KWA KUCHAPISHA MTANDAONI TAARIFA ZENYE KUZUA HOFU KUHUSU CORONA

Mwendeshaji wa Mitandao ya Kijamii Bloga (Blogger) Robert Alai anashikiliwa katika kituo cha polisi cha Muthaiga nchini Kenya kufuatia madai ya kuchapisha ujumbe wa kuzua hofu miongoni mwa watu mitandaoni kuhusu Virusi vya Corona (Covid-19).

 Bloga huyo aliagizwa kufika katika Idara ya Upelelezi mnamo Ijumaa, Machi 20,2020 kuandikisha taarifa kufuatia ujumbe wa kuzua hofu aliouchapisha mitandaoni kuhusu janga la coronavirus  kabla ya kukamatwa na kusafirishwa hadi kituo cha polisi cha Muthaiga.

 Bloga Robert Alai atalazimika kulala kizuizini wikendi nzima kwa madai alichapisha ujumbe wa kuzua hofu mitandaoni kuhusu janga la coronavirus. 

 Inadaiwa kwamba, Alai alichapisha ujumbe kwenye ukurasa wa Twitter kwamba watu kadhaa wameaga dunia Mombasa baada ya kuambukizwa virusi vya corona. 

Mshukiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatatu kujibu mashtaka hayo.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe kwenye kikao na waandishi wa habari mnamo Alhamisi alionya kwamba serikali itamchukulia hatua kali yeyote ambaye atasambaza ujumbe wa kupotosha kuhusu maradhi hayo. 

"Ningependa kuwaomba wananchi kujiepusha na kusambaza jumbe zozote za kupotosha. Uvumi umekuwa ukisambazwa mitandaoni kwamba Nairobi itafungwa na kwamba tutawatuma watu mashambani.....haya ni mambo yasiyo ya ukweli. Uvumi huo unapaswa kukomeshwa haraka," Kagwe alisema. 

 Hii sio mara ya kwanza kwa bloga huyo kujipata pabaya kwani mwaka jana Juni, alikamatwa kwa madai ya kusambaza picha za polisi waliouawa katika shambulizi la kigaidi Wajir.

 Alishtakiwa kwa usaliti na kutoa habari za kijasusi na baada ya kuzuiliwa kwa wiki mbili aliachiliwa kwa dhamana ya KSh 300,000 baada ya kukana mashtaka.

Chanzo- TUKO
Share:

MSANII KENNY ROGERS AFARIKI DUNIA


Msanii Kenny Rogers (81) raia wa Marekani, amefariki Dunia akiwa nyumbani kwake.

Kwa mujibu wa familia yake kifo cha Msanii huyo ni cha kawaida na wala hakihusishwi na jambo lolote .

Rogers, alitamba kwa nyimbo zake nyingi zikiwemo The Gambler, Lady, Islands in the Stream na Lucille, huku akiwa ameuza rejodi zaidi ya Milioni na kushinda tuzo 3 za Grammy.

Kama muigizaji ametokea kwenye filamu ya Six Pack mwaka 1982 na katika tamthilia kadhaa maarufu za runinga kama The Gambler franchise, Christmas in America na Coward of the County.
Share:

BIBI WA MIAKA 80 ABAKWA HADI KUFA, AKATWA VIUNGO

Picha haihusiani na habari hapa chini
Kikongwe anayekadiriwa kuwa na zaidi ya miaka 80, mkazi wa Kijiji cha Shaurimoyo wilayani Babati, amebainika kubakwa na kuuawa na hatimaye kukatwa vidole na watu waliomfanyia unyama huo.

Kikongwe huyo alikutwa amekufa Machi 8, 2020 baada ya kufanyiwa ukatili na watu wasiojulikana.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kikongwe huyo alikutwa amekatwa vidole na kitu chenye ncha kali na kubakwa hali ambayo inaelezewa kuwa huenda ilisababisha kupoteza maisha. 

Bibi huyo (jina linahifadhiwa) pia alikutwa akiwa amekatwa sehemu ya unyayo jambo ambalo limehusishwa na imani za kishirikina.

Majirani wa bibi huyo aliyekuwa akiishi peke yake, walisema mwili wake pia ulikutwa ukiwa umekatwa sikio na vidole vya mkono. 

Mwenyekiti wa Kijiji cha Shaurimoyo, Dismas Dodo, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema baada ya kupata taarifa kutoka kwa wanakijiji, alichukua hatua ya haraka ya kuwasiliana na Jeshi la Polisi Kituo Kdogo cha Magugu.

Diwani wa Kisangaji, Adamu Ipingika, akiwa kwenye msiba wa kikongwe huyo juzi, alikemea kitendo hicho na kuwataka wanakijiji kutoa ushirikiano kwa polisi ili watuhumiwa waliofanya uhalifu huo wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kisangaji, John Jacob, alisema katika mwezi huu, mtoto wa miaka minne alibakwa katika kijiji hicho na mtuhumiwa mwenye miaka 30 lakini alikamatwa na kufikishwa katika Kituo Kidogo cha Polisi Magugu.

Soma zaidi <<HAPA>>
Share:

Binti wa Miaka 18 Atoa Mimba Gesti

Polisi Mkoa wa Morogoro nchini Tanzania inamshikilia Rehema Fabiani (18), mfanyakazi wa Mgahawa wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) akidaiwa kutoa mimba akiwa katika nyumba ya kulala wageni ya EM mjini Morogoro.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Ijumaa Machi 20, 2020 Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa alisema binti huyo alikutwa katika nyumba hiyo akiwa tayari katoa mimba na kusababisha kifo cha kichanga chenye jinsi ya kiume.

Mutafungwa alisema tukio hilo limetokea Alhamisi Machi 19, 2020 saa 3 asubuhi katika nyumba hiyo ya kulala wageni eneo la mtaa wa Amani kata ya Mjimkuu.

Alisema binti huyo alifika katika nyumba hilo na kupanga chumba namba saba na siku iliyofuata asubuhi muhudumu wa nyumba hiyo alisikia kelele kutoka ndani ya chumba hicho na kumgongea.

Kamanda huyo anasema baada ya kufungua mlango wa chumba na kuingia ndani alimkuta binti huyo akilalamika maumivu makali ya tumbo na kumuhoji ambapo alimweleza alikuwa ametumia dawa za kutibu ugonjwa wa UTI.

Alisema baada ya kuhojiwa kwa kina binti huyo alisema aliingia katika nyumba hiyo ya kulala wageni tangu Machi 15, 2020 akiwa na lengo la kuharibu ujauzito aliokuwa nao na alieleza alitumia dawa za aina mbalimbali bila mafanikio na kwamba ndipo Machi 18, 2020 akabadilishiwa dawa na kutimiza lengo lake.


Share:

Upinzani waitaka serikali kufunga mipaka kujikinga na corona

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, imeitaka serikali kuhakikisha inafunga mipaka yote ili kutoruhusu wageni na hata Watanzania waliopo nje ya nchi kwa lengo la kutoleta maambukizi mapya ya virusi vya corona.

Aidha, imesema wageni hao waruhusiwe pale inapobidi kuingia na serikali iwaweke kwenye karantini kwa gharama zao kwa siku 14 kama taratibu za kitabibu zinavyoelekeza.

Waziri Kivuli wa Afya, Cecilia Paresso ametoa rai hiyo jana Ijumaa Machi 20, ambapo amesema hii ni kwa sababu wagonjwa wote waliothibitika kuwa na virusi hivyo ni wale waliotoka nje ya nchi na si waliokuwa hapa nchini.

“Tunatambua athari za kufunga mipaka ya nchi katika wakati huu wa utandawazi wa kibiashara na kiuchumi. Hata hivyo, afya na uhai wa binadamu haiwezi kulinganishwa na thamani ya kitu chochote.

“Ni vema kwa sasa tusiangalie na kuwaza tu faida za muda mfupi katika za utalii, biashara na uchumi kwa kuacha mipaka wazi jambo ambalo litakuja kutufanya tujute baadaye kama Taifa.

“Hata hivyo tumeshangaa kupitia vyombo vya habari kumsikia Mkuu wa Mkoa wa Arusha akieleza umma kuwa dereva aliyemwendesha Mtanzania wa kwanza aliyegundulika na virusi vya corona kuwa hana maambukizi yoyote, jambo la kujiuliza hapa je siku 14 zimetimia? Kwani ni takribani siku nne tu zimepita tangu dereva huyo atafutwe na kupatikana,” amesema.

Kutokana na hali hiyo, amesema Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka serikali na viongozi waliopo madarakani kutoleta mzaha kwenye suala hilo na pengine ikawa bora zaidi kuwaachia wasemaji wa jambo lenyewe kuweza kulitolea ufafanuzi kuliko hivi sasa hali inayoleta mkanganyiko wa matamko kutoka kwa kila mtu.


Share:

Waganga Wakuu Watakiwa Kukagua Utayari Wa Kukabiliana Na Corona Kwenye Vituo Vya Kutolea Huduma Za Afya

Na. Majid Abdulkarim, Singida
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia maswala ya Afya, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt.Dorothy Gwajima amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri watoke ofisini kukagua utayari wa vituo vya kutolea huduma za Afya katika kukabiliana na virusi vya COVID-19(CORONA) na kuhakikisha vituo vilivyotengwa katika kila Halmashauri nchini vinakidhi vigezo vya kutoa matibabu ya COVID-19(CORONA).

Dkt.Gwajima amesema kuwa taarifa ya zoezi hilo itumwe kila baada ya masaa 24 Ofisi ya Raisi, TAMISEMI kukiri kuwa viongozi hao walifika kituo gani na yatakonayo na ziara hiyo ni yepi katika kituo husika.

Dkt.Gwajima ameagiza hayo leo akiendelea na ziara yake ya kukagua matayarisho ya vituo kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wa COVID-19 (CORONA) katika halmashauri za Singida, Ikungi na Manyoni mkoani Singida.

Aidha Dkt.Gwajima amesisitiza kuwa kila mjumbe wa Kamati ya Afya Halmashauri apewe vituo vya kuvifuatilia kila siku kwani ni sehemu ya moja wapo ya majukumu yao na hususan kipindi hiki ambapo nchi inapambana na maradhi haya.

“kila Mkuu wa Kituo ahakikishe amewashirikisha watumishi wote, Kamati ya Afya ya Kituo na Wahudumu wa Afya Ngazi ya jamii katika kupanga na kutekeleza mikakati ya kupambana na Covid-19(CORONA)”,ameeleza Dkt.Gwajima.

Pia Dkt.Gwajima ameongeza kuwa Kamati za Afya ya Msingi ngazi ya mkoa na halmashauri zihakikishe kila mjumbe anao mpangokazi wake wa ufuatiliaji na uhamasishaji juu ya ugonjwa huu ili kuleta uelewa kwa jamii mfano, Afisa Biashara anatakiwa kuhakikisha wafanya biashara wote wanaelewa vizuri dhana nzima ya kujikinga ili biashara zao zisiwe chanzo cha kuchochea maambukizi.

Katika ziara hii, Dkt Gwajima ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Manyoni kwa jinsi ambavyo wamezingatia maelekezo na kuyafanyia kazi ikiwemo matayarisho ya vituo kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wa COVID-19 (CORONA) kwa ushirikiano na viongozi wa jamii ngazi zote wakiwemo Mhe Diwani Kata ya Chikuyu, Mtendaji wa Kata, Mtendaji wa Kijiji cha Mwiboo na Mwenyekiti wa Kijiji hicho.

Naye Diwani wa Kata ya Chikuyu wilayani Manyoni Bw.Benjamini Kamwoga amesema kuwa, wananchi wa Chikuyu wako bega kwa bega na serikali yao katika kupambana dhidi ya ugonjwa huu.

“Ili kuonyesha kuwa janga hili ni letu sote kesho wananchi watakuja kwa awamu ili kusafisha mazingira ya kituo hiki ikiwa ni sehemu moja wapo ya kuaanda mazingira rafiki ya kupambana na ugonjwa huu” amesema Bw.Kamwaga.

Kwa kuhitimisha Dkt Gwajima amewapongeza watumishi wote wa sekta ya afya,  wananchi na wadau wote kwa ujumla kwa jinsi wanavyojitoa katika vita dhidi ya Covid-19. Amewataka wataalamu kuendelea kushirikiana na wadau wote ngazi zote za jamii.


Share:

Jinsi Bosi wa TAKUKURU Tanga na msaidizi wake walivyonasa kwenye mtego wa rushwa

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU inapenda kuufahamisha umma kwamba, watumishi wake wawili akiwemo Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga, wamesimamishwa kazi kuanzia  Machi 20, 2020 ili kupisha uchunguzi dhidi yao. Hatua hii imefikiwa leo baada ya watumishi hao:

(i)Christopher Mariba – Aliyekuwa Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga na

(ii) Hilton Njau – Afisa Uchunguzi Mkuu kutoka ofisi ya TAKUKURU mkoa wa Tanga, kuhusishwa na tuhuma za kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa mmoja wa watuhumiwa waliokuwa wakichunguzwa na TAKUKURU.

Kosa hili ni kinyume na Kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007.

Ndugu Waandishi wa Habari,
Kama ambavyo nimekuwa nikiuleza umma mara kwa mara, chombo hiki ndicho chenye dhamana ya kuongoza mapambano dhidi ya rushwa nchini – jukumu ambalo tumepewa kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya Mwaka 2007.

Kwa msingi huo, watumishi wa TAKUKURU wanapaswa kuwa na uadilifu na weledi wa hali ya juu wakati wote wanapotekeleza majukumu haya nyeti kwa mustakabali wa maendeo na ustawi wa Taifa letu.

Ndugu Waandishi wa Habari,
Ili kuhakikisha kuwa chombo hiki hakichafuliwi, ipo SERA ya ndani ya chombo hiki YA KUTOMVUMILIA MTUMISHI YEYOTE ANAYETUHUMIWA KUJIHUSISHA NA VITENDO VYA RUSHWA. Hivyo basi, kwa msingi huo, watumishi hawa wamesimamishwa kazi kuanzia leo Machi 20, 2020 ili kupisha uchunguzi dhidi yao na uchunguzi huo utakapokamilika hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa.

Wakati uchunguzi huu ukiendelea, nimemteua Dkt Sharifa Bungala kukaimu nafasi ya Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Tanga kuanzia  Machi 20, 2020.

BRIG. JEN JOHN MBUNGO (ndc)
KAIMU MKURUGENZI MKUU – TAKUKURU


Share:

Watatu Wakamatwa Kwa Kuua Na Kufukia Mwili Katika Shamba La Mahindi

NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
JESHI la Polisi mkoani Pwani, kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji wamefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 51, raia wa Ethiopia waliokuwa wameingia nchini kupitia bandari bubu ya Makurunge katika wilaya  ya Bagamoyo.
 
Idadi hiyo inafikia wahamiaji haramu 100 baada ya wengine 49 kukamatwa juzi ,Kidomole,Fukayose.
 
Kamanda wa polisi mkoani hapa,Wankyo Nyigesa alieleza, raia hao wamekabidhiwa kwa vyombo vya dola kwa taratibu za kisheria .
 
“Raia hawa wamekamatwa usiku wa kuamkia march 20 huko Makurunge, kata ya Makurunge, Tarafa ya Yombo, Wilaya ya Bagamoyo”alifafanua Wankyo.
 
*AKAMATWA AKISAFIRISHA VIROBA VITANO VYA  BANGI*
Jeshi hilo, linamshikilia Ally Hashimu Athumani ,mkazi wa Malela – Morogoro kwa kosa la kusafirisha bangi viroba vitano. 
 
“Mnamo march 20 ,majira ya saa 12:00 huko maeneo ya Maili moja, Kata ya Maili moja,Wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani Jeshi la Polisi baada ya kupokea taarifa kutoka kwa raia wema  walimkamata mtuhumiwa huyo akisafirisha kiasi hicho cha bangi kutoka Morogoro kuelekea Dar Es  Salaam kwa kutumia gari yenye namba za usajili *T.688 CZK* ,Toyota Carina nyeupe”:.
Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili aweze kujibu tuhuma zinazomkabili.
 
WATATU WAKAMATWA KWA KUUA NA KUFUKIA MWILI KATIKA SHAMBA LA MAHINDI
Mnamo tarehe 10/03/2020 majira ya saa 14:30 hrs huko maeneo ya  Kibindu, Kata ya Kibindu,Tarafa ya Chalinze katika Wilaya ya kipolisi Chalinze, Mkoa wa Pwani *Bw. Chacha Chacha Machangu,* Miaka 27,Mkurya, mkazi wa Kibindu alimfumania mke wake (jina linahifadhiwa ) akiwa na mwanaume mwingine na mara baada ya tukio hilo alimshambulia kwa kumkata kata na mapanga sehemu mbalimbali za mwili na kumsababishia majeraha yaliyopelekea kifo cha mama huyo usiku wa tarehe 10/03/2020.
 
Baada ya tukio la kifo cha mama huyo Bw Chacha Machangu kwa kushirikiana na ndugu zake ambao ni *Emmanuel Chacha Machangu,* Miaka 19,Mkurya na *Hamis Chacha Machangu*, Miaka 22, Mkurya,wote wakazi wa Kibindu walichimba shimo katika shamba la mahindi na kuufukia mwili wa mama huyo.
 
Mnamo tarehe 19/03/2020 Jeshi la Polisi (M) Pwani lilipata taarifa ya tukio hilo na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wote watatu waliojihusisha na tukio hilo na wao wenyewe kwa ridhaa yao walionesha mahali shimo lilipo.Baada ya Jeshi la Polisi kufukua ulipatikana mwili wa marehemu ambao ulifanyiwa uchunguzi na daktari kisha kufanyiwa mazishi kwa heshima zote.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi March 21

















Share:

Friday, 20 March 2020

WAKUU WA WILAYA, WAKURUGENZI WAPEWA AGIZO ZITO WANAFUNZI WANAOZAGAA HOVYO ...CORONA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo ameagiza Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi na Wakuu wa shule nchini, kuhakikisha wanasafirisha wanafunzi waliokosa usafiri badala ya kuwaacha wakizagaa hovyo.

Machi 17, mwaka huu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alifunga shule zote za msingi na sekondari kwa siku 30 kutokana na tishio la ugonjwa wa Corona.

Agizo hilo amelitoa leo Machi 20, 2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma. 

Amesema baadhi ya mikoa wanafunzi wameonekana kuzagaa na wengine kulala kwenye vituo vya mabasi kutokana na viongozi hao kutotekeleza agizo la kuhakikisha wanasafiri kwa usalama na amani hadi makwao.

"Kama kuna shida wakuu wa shule wawasiliane na wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama ambao ni wakuu wa wilaya, haileti picha nzuri kuona wanafunzi wamezagaa vituoni wakitafuta usafiri jambo ambalo linadhihirisha kuwa wakuu wa shule hawakujipanga vizuri," amesema.

Ametoa pongezi kwa Mkuu wa Shule ya Kilakala iliyopo Morogoro na Mkuu wa Shule ya Dodoma Sekondari kwa kuweka utaratibu mzuri wa kusafirisha wanafunzi hao.
CHANZO- NIPASHE
Share:

BITEKO AWATAKA WACHIMBAJI MADINI KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA

Baadhi ya wachimbaji wadogo wa Almasi katika Kata ya Maganzo Wilaya Kishapu mkoani Shinyanga (kulia), wakisalimiana na Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa kwanza kushoto) alipotembelea eneo la kuchenjulia mabaki ya mchanga wa almasi (makinikia) kutoka mgodi wa Mwadui/ Williamson Diamonds Ltd. Wachimbaji hao wamechukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kwa kuvaa vikinga pua na mdomo (mask).
Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) akisalimiana na baadhi ya viongozi wa mgodi wa Mwadui/ Williamson Diamonds Ltd (kushoto) alipotembelea mgodi huo kujionea zoezi la utoaji nje mabaki ya mchanga wa almasi (makinikia) kwa ajili ya kuchenjuliwa upya na wachimaji wadogo.
 Mkuu wa Wilaya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Talaba (katikati) akionesha namna sahihi ya kutakasa mikono kwa kutumia sabuni maalum (hand sanitizer) ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.
 Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wilayani Kishapu kukagua eneo la mchanga wa almasi uliotolewa na mgodi wa Mwadui (Williamson Diamonds Ltd).
 Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wilayani Kishapu akitoka kukagua eneo la mabaki ya mchanga wa almasi uliotolewa kwa wananchi na mgodi wa Mwadui (Williamson Diamonds Ltd) ili kuchenjuliwa upya.
Waziri wa Madini, Doto Biteko akikagua vizimba vilivyoandaliwa kwa ajili ya shughuli ya kuchenjua mabaki ya machanga wa almasi (makinikia) katika eneo la Maganzo wilayani Kishapu. 
Zoezi la utoaji mabaki ya mchanga wa almasi (makinikia) kwa ajili ya kuchenjuliwa upya na wananchi katika eneo la Maganzo limeanza Machi 19, 2020.
 Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wilayani Kishapu akikagua eneo ambalo wananchi watakuwa wakitakasa mikono yao kwa sabuni maalum (hand sanitizer) kabla ya kuingia eneo la kuchenjulia mabaki ya mchanga wa almasi (makinikia) ikiwa ni tahadhari dhidi ya virusi vya Corona.
 Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) akikagua vifaa vya kupima ubora wa almasi katika eneo la mnada wa uuzaji madini hayo lililopo katika mgodi wa Mwadui unaomilikiwa na kampuni ya Williamson Diamonds Ltd.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Mwadui/ Williamson Diamonds Ltd, Ayound Mwenda (kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusu vifaa vya kupimia ubora wa alamsi mgodini hapo.


Na George Binagi-GB Pazzo, Shinyanga

Waziri wa Madini, Doto Biteko amewataka wachimbaji wa madini nchini Tanzania kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa mafua, kikohozi na homa kali ya Corona ambao umesababisha athari ikiwemo vifo katika mataifa mbalimbali duniani.

Biteko alitoa tahadhari hiyo Machi 19, 2020 alipotembelea eneo la kuchenjulia mabaki ya mchanga wa almasi (makinikia) uliotolewa na mgodi wa Mwadui (Williamson Diamonds Ltd) kwa wachimbaji wadogo ambapo alifurahishwa na matayarisho mazuri ya eneo hilo ikiwemo tahadhari dhdi ya virusi vya Corona kabla ya zoezi la kuchenjua mchanga huo halijaanza rasmi.

“Tuendelee kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kwa kuepuka kushikana mikono ovyo, lakini pia tuzingatie matuzi sahihi ya viziba pua na mdogo (mask) pamoja na kutakasa mikono kwa kutumia sabuni maalum (hand sanitizer)” alisisitiza Biteko wakati akisalimiana na baadhi ya wachimbaji wadogo wa almasi katika eneo la Maganzo.

Aidha Biteko aliwakumbusha wafanyabishara na wachimbaji wadogo wa almasi kufanya shughuli zao kwa kuzingatia sheria na kanuni za madini ikiwemo kuuza madini yao kwenye masoko huku wakijiepusha na utoroshaji madini kwani yeyote atakayeshindwa kufanya hivyo ataangukia mikononi mwa sheria na kuishia kufungwa jambo ambalo asingependa litokee.

“Ni marufuku kutunza kinyemela madini nyumbani kwako bila kuwa na nyaraka kutoka kwa maafisa wetu wa madini, sisi tukikukamata hayo madini yatakuwa mali halali ya Serikali” Biteko aliwatahadharisha wafanyabishara na wachimbaji wa almasi.

Awali akizungumzia zoezi la utoaji nje mchanga wa almasi, Katibu Mkuu wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa Shinyanga (SHIREMA), Greygory Kabusi alisema maandalizi yamekamilika na vikundi 700 vya wachimbaji wadogo wa almasi vyenye wanachama 10 kila kimoja vinatarajiwa kuanza shughuli ya kuchenjua mchanga huo na hivyo kujipatia kipato.

Naye Mkuu wa Wilaya Kishapu, Nyabaganga Talaba alisema Serikali inafuatilia kwa ukaribu zoezi la uchenjuaji mchanga huo ili kuchukua tahadhari za kiusalama hususani katika kipindi hiki cha maambukizi ya virusi vya Corona.

Tazama video hapa chini

Share:

Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Mwezi Huu Access Bank, EXIM Bank, KCB Bank, NMB Bank, NBC Bank, Vodacom, Tigo, CRDB Bank

Share:

Dereva Wa Basi La Isamilo Afariki Dunia Akiwa Safarini

Dereva wa Basi la Isamilo lenye namba za usajili T609 CQB Scania linalofanya safari zake kutoka Mwanza kwenda Mbeya Sebastian Mathias (43) mkazi wa Mwanza amefariki dunia wakati akiendelea na safari kutoka Mbeya kwenda Mwanza.           

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga, Deborah Magiligimba amesema tukio hilo limetokea leo Ijumaa Machi 20,2020 saa nne asubuhi.

Kamanda Magiligimba amesema Sebastian wakati akitoka Mbeya kwenda Mwanza alikuwa akijisikia vibaya walipofika Singida ndipo hali yake ilibadilika wakawa wamebadilishana na dereva mwenzake.

"Sebastian alitoka Mwanza kwenda Mbeya akiwa anajisikia vibaya. Huwa wapo madereva wawili,wameenda hadi Mbeya,wakati wanatoka Mbeya kwenda Mwanza Sebastian alikuwa anaendelea kujisikia vibaya, walipofika Singida akawa anajisikia vibaya zaidi ndipo akabadilishana na yule dereva mwenzake",amesema Kamanda Magiligimba.

"Wamefika Tinde leo saa nne asubuhi akawa amezidiwa sana, wakambeba kwenda kwenye Kituo cha Afya Tinde,baada ya kumfikisha,Daktari akabaini kuwa tayari Sebastian Mathias alikuwa amefariki dunia",ameeleza Kamanda Magiligimba

Amesema kwa kuwa gari lina madereva wawili, dereva mwingine ameendelea na safari kwenda Mwanza na maiti imehifadhiwa katika kituo cha afya cha Tinde.


Share:

Wanaume waliombaka mwanamke ndani ya basi wanyongwa India

India imewanyonga hadi kufa wanaume wanne walioshitakiwa kwa kosa la kumbaka na kumuua mwanafunzi mmoja ndani ya basi mnamo mwaka 2012. 

Mwanamke huyo aliyekuwa na miaka 23 alibakwa wakati basi lilipokuwa likiendelea na safari mjini New Delhi. 

Watu hao wamenyongwa mapema hii leo katika gereza la Tohar Jail mjini New Delhi hii ikiwa ni kulingana na shirika kubwa la habari nchini humo la Press Trust of India, lililonukuu mamlaka za gereza. 

Wanaume hao walimbaka mwanamke huyo aliyekuwa akitokea kutazama sinema na kumuumiza vibaya kwenye sehemu zake za siri kwa kutumia kipande cha chuma. 

Tukio hilo baya kabisa liliibua maandamano kote nchini India na kuwachochea wabunge kuongeza ukali wa adhabu dhidi ya kesi za unyanyasaji wa kingono. 

Adhabu ya mwisho ya kunyongwa ilitolewa mwaka 2013 nchini India.

-DW


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger