Saturday, 29 February 2020

Wananchi Washauriwa Kutochakaza Noti Na Sarafu

Gavana  wa Benki kuu ya Tanzania (BOT) Profesa. Frolens Luoga amewashauri wananchi kutumia vyema fedha bila kuziharibu wala kuzichakaza kutokana na ubora na uthamani wa utengenezaji wake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Prof. Luoga amesema, lazima fedha zitumike kwa uangalifu na kuwaasa wananchi kutumia fedha hizo bila kuzichakaza, kuzitupa wala kuziandika kwa kuwa fedha hizo zinapoharibiwa zinakuwa katika hatari ya kuharibiwa kabisa na mashine maalumu pindi zinapofika benki kuu, na kupelekea gharama ya kupata nyingine kupata fedha hiyo.

Profesa. Luoga amesema kuwa mabenki yana wajibu wa kusaidia benki kuu katika kutekeleza Sera ya Sarafu safi kwa kukusanya pesa zote zilizochafuka na zisizo na hali nzuri na kuzirudisha  benki kuu.

Amesema kuwa fedha ya nchi ina thamani kubwa hivyo lazima matumizi yake yawe ya uangalifu,

"Noti ya Tanzania inatengenezwa kwa gharama zaidi kwani inatengenezwa kwa pamba kwa asilimia 100 ukilinganisha na noti ya dola ambayo hutengenezwa kwa pamba kwa asilimia 75 ya pamba, na hiyo ni kutokana na matumizi" amesema.

Pia amesema kuwa Benki kuu itaendelea kushirikiana na vyombo vya dola katika kuwawajibisha wale wote watakaokutwa na hatia ya kuharibu pesa ambalo ni kosa la jinai.

"Kuchana noti ni kosa la jinai, wengi wamekuwa wakija benki kudanganya ili walipwe tumewabaini walioghushi na waliokamatwa wanachukulia sheria kwa kuwa hiyo sio biashara" Ameeleza Prof. Luoga.

Kuhusiana na malalamiko ya kupungua kwa pesa katika mzunguko Gavana huyo ameeleza kuwa;

" Kila asubuhi tunakutana na kuangaalia hali ya ukwasi katika mabenki na tunajua kila benki ina kiasi gani na tunaweza kutoa mkopo kwa mabenki ili waweze kufanya malipo" ameeleza

Amesema kuwa "Benki kuu inaangalia kiasi cha pesa katika  mabenki yote na kama benki haitakua na pesa tutaangalia ni kwanini na tutasaidia na ikitokea benki haina pesa kwa kutokidhi masharti kama benki tunachukua hatua nyingine" amesema Luoga.

Mwisho amewataka wananchi kutoghushi pesa ya nchi na kwa yeyote atakayekutwa na pesa bandia  atashtakiwa kwa  kosa la jinai na uhujumu uchumi.


Share:

DC Njombe Aagiza Kukamatwa Walimu Wafanyao Vitendo Vya Kikatili

Na Mwandishi Wetu Makambako
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Ruth Msafiri ameagiza kukamatwa kwa walimu mkoani Njombe watakaobainika kuwafanyia vitendo vya kikatiki wanafunzi ili kukomesha vitendo hivyo vinavyoendelea kutoka nchini.

Hayo yamebainika jana Makambako mkoani Njombe wakati msafara wa kijinsia kutokomeza ukatili ulipofika mkoani humo kwa ajili ya kutoa elimu ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Mhe. Ruth amesema kuwa Serikali haipingi adhabu ya viboko ila sio kutoa adhabu ya  viboko vya kupitiliza na kusababisha vilema na maumivu kwa wanafunzi.

Ameongeza kuwa suala la ukatili ni mapambano makubwa nchini hivyo jitihada zinahitajika kwa wananchi wadau na mashirika yasiyo ya kiserikali kuhakikisha wanaunganisha nguvu pamoja kuondokana na vitendo vya ukatili.

Mhe. Ruth amevitaka vyombo vya usalama kuacha kufanya ukatili kwa kuchelewesha kesi za vitendo vya ukatili wa kijinsia na kusababisha ukatili wa kihisia kwa wahanga wa vitendo hivyo.

“Vyombo vya usalama mnachelewesha kesi mnaomba rushwa nawaomba vyombo vys usalama msiwe kikwazo cha kutopatikana kwa haki ya wahanga wa vitendo vya ukatili” alisema.

Akizungumza kuhusu msaada wa kisheria unaotolewa na Shirika la Legal Serivces Facility Joseph Magazi amesema kuwa wameweka nguvu katika kuisidia jamii katika matatizo ya kisheria kwa kuwawezesha wasaidizi wa kisheria katika mikoa na wilaya kutoa elimu husika.

“Tumejipanga kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha tunaifikia jamii katika kutoa elimu itakayowezesha wenye matatizo mbalimbali ya kisheria kupata msaada na kuyatatua matatizo yao” alisema


Share:

Serikali kukataa rufaa kupinga hukumu ya ATCL kulipa Bilioni 69

Serikali imesema imeanza mchakato wa kukata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Uingereza dhidi ya Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL).

ATCL imeamriwa kulipa Dola 30.1 milioni (Sh69.23bilioni) kwa kampuni moja ya Liberia kama fidia baada ya kuvunjika kwa mkataba wa kukodisha ndege.

Kesi hiyo inahusu makubaliano yaliyofikiwa mwaka 2013 na aliyekuwa Mkurugenzi wa ATCL, David Mattaka ya kukodisha ndege aina ya Airbus kutoka kampuni ya Willis Trading.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Uingereza, Christopher Butcher aliiamuru ATCL kulipa fedha hizo pamoja na riba inayoweza kufikia dola 10 milioni (Sh23 bilioni) kwa kampuni hiyo ya Liberia, ambayo inajishughulisha na masuala ya kuuza na kukodisha ndege, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa.

Hata hivyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Adelardus Kilangi amesema kuwa mkataba wenyewe ulikuwa wa kifisadi wa kuitia nchi hasara.

Dk Kilangi alisema kuwa serikali imewasiliana na ofisi yake, ambayo imeanza mchakato wa kukata rufaa. 

“Tumeanza mchakato wa kukata rufaa na tunazingatia sheria na taratibu za Uingereza,” aliongeza.

Dk Kilangi alieleza kuwa hukumu hiyo imewashangaza kutokana na ukweli kuwa ndege yenyewe ilitumika kwa miezi saba tu. 

“Hawa watu wameibia nchi na tutapambana mahakamani kuhakikisha tunashinda kesi hii,” alisisitiza Kilangi.

Credit: Mwananchi


Share:

Afrika Kusini kuwarejesha raia wake waliopo Wuhan, China

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ameagiza kurejeshwa nchini humo raia 132 wa Taifa  hilo  waliopo kwenye mji wa Wuhan nchini China, mji  ambapo virusi vya corona vimeanzia.

Rais Ramaphosa ametoa agizo hilo baada ya kikao cha Baraza la Mawaziri nchini Afrika Kusini, kikao kilichofanyika kutokana na familia nyingi nchini humo zenye ndugu zao katika mji wa Wuhan kuomba ndugu zao wasaidiwe kurejea nchini humo.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Afrika Kusini imeeleza kuwa, ratiba kamili ya kurejeshwa kwa raia hao bado haijapangwa, lakini watakaorejeshwa nyumbani ni 132 kati ya 199 waliopo katika mji huo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, raia hao wote wanaotaka kurejea nyumbani hawajaambukizwa virusi hivyo vya corona na wala hawajaonyesha dalili zozote za kupata homa hiyo, lakini watakapofika Afrika Kusini watawekwa kwenye karantini kwa muda wa siku 21 ndipo waruhusiwe kwenda katika maeneo yao.

Serikali ya Afrika Kusini imeandaa Wataalam wa afya wa kutosha pamoja na askari ambao watahusika na zoezi lote la kuwarejesha raia wake wanaoishi Wuhan na kuwahudumia kwa wakati wote watakapokua kwenye Karantini.

Tayari Shirika la Ndege la Afrika Kusini limefuta safari zake za moja kwa moja kutoka nchini humo kwenda China.


Share:

Virusi Hatari Vya Corona Vyatua Nigeria

Serikali ya mji wa Lagos nchini Nigeria imethibitisha kuwa, kesi ya kwanza ya maambukizi ya virusi vya korona (COVID-19) imeripotiwa katika mji huo wa kibiashara na wenye idadi kubwa zaidi ya watu nchini humo.

Kamishna wa Afya wa mkoa wa Lagos, Akin Abayomi amesema, raia mmoja wa Italia aliingia nchini Nigeria jumanne kwa ziara ya kikazi akitokea Milan, na akaugua siku inayofuata. 

Amesema raia huyo alithibitishwa kuwa na virusi vya korona alhamis na taarifa kutolewa mara moja kwa Wizara ya Afya nchini humo.

Amesema mgonjwa huyo anaendelea vizuri na amelazwa kwenye Hospitali ya Magonjwa ya Kuambukiza iliyoko eneo la Yaba mjini Lagos. 

Pia amesema, wahudumu wa afya wanafanya jitihada kutambua watu wote waliowasiliana na mgonjwa huyo tangu alipowasili nchini Nigeria.


Share:

Mgumba:Tanzania ina utoshelevu wa chakula kwa zaidi ya asilimia 119

Na Amiri kilagalila,Njombe
Naibu waziri wa kilimo nchini Omary Mgumba amesema,Tanzania bado ina hali nzuri ya uwepo wa chakula kwa kuwa mpaka leo taifa lina utoshelevu wa chakula kwa zaidi ya asilimia 119.

Mgumba ametoa taarifa hiyo mkoani Njombe wakati wa kongamano la vijana katika kilimo mwaka 2020 lililowakutanisha takribani vijana 200 wa mikoa ya Njombe,Iringa na Ruvuma kwa lengo la kuwahamasisha vijana kujishughulisha na kilimo chenye tija nchini.

"Leo hii mpaka sasa kama taifa naomba niwaambie watanzania na vijana mlioko hapa tuna utoshelevu wa chakula zaidi ya asilimia mia moja na kumi na tisa"alisema Mgumba

Naibu waziri Mgumba amewaeleza vijana na watanzania kuwa kilimo kimeendelea kukuwa na kutoa mchango kwa uchumi wa nchi katika maeneo mbali mbali kwa kuwa takwimu zilizopo za mwaka 2018 zinaonyesha sekta ya kilimo inachangia asilimia 28.2 ya pato la taifa na sekta ndogo ya kilimo mazao inachangia zaidi ya asilimia 16.2 huku watanzania wanaoshiriki katika sekta ya kilimo wakiwa zaidi ya asilimia 58 na kusababisha kilimo kuwa na mchango mkubwa katika ajira.

Mgumba amesema wizara ya kilimo imeendelea kupata mafanikio makubwa kisera na taasisi ikiwemo kuanzisha mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja,na kusababisha ongezeko kutoka tani laki tatu na mbili mpaka kufikia tani laki nne na stini kwa mwaka.

Vile vile ametoa wito kwa vjana kujihusisha katika kilimo kwa kuwa nchi ya Tanzania ina eneo kubwa linalofaa kwa ajili ya kilimo.

"Nchi yetu ina eneo linalofaa kwa kilimo,ambalo linakadiliwa kuwa zaidi ya hekta milioni 44 linafaa kwa kilimo na mifugo hiyo ni fursa vijana mnatakiwa kuitumia,na kati ya hizo hekta milioni 29.4 zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji"alisema Waziri Mgumba

Aidha amezitaka halmashauri zote nchini kusimamia kikamilifu mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake vijana na walemavu,pamoja na kutoa mikopo ya kueleweka kwa vijana ili waweze kuwekeza kikamilifu katika kilimo.


Share:

BITEKO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KWENYE JIMBO LAKE LA BUKOMBE



Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Doto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Madini akizungumza na wakazi wa Kata ya Uyovu jimboni humo Februari 28, 2020 kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Buganzu.

Kabla ya mkutano huo, Biteko alikagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuwapongeza wananchi kwa kushirikiana kutekeleza miradi hiyo ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa na kuanzisha ujenzi wa Shule.
Baadhi ya wakazi wa Kata ya Uyovu jimboni Bukombe wakimsikiliza mbunge wao, Doto Biteko (hayuko pichani) ambaye pia ni Waziri wa Madini.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Madini alifika kukagua ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Lyobaika ambayo ujenzi wake umeanzishwa na wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Madini pia alikagua ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Kapwani inayojengwa kwa nguvu za wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Madini aliunga mkono juhudi za wananchi kwa kuahidi kuwasaidia ili kukamilisha miradi hiyo na mingine mingi jimboni Bukombe.
Tazama BMG TV hapa chini
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi February 29

















Share:

Friday, 28 February 2020

Serikali ya Tanzania Yaihakikishia Burundi Kwamba Kampuni ya Mbogo Mining ni Halali na Inafanya Shughuli Zake Zote Kwa Mujibu wa Sheria

Serikaki  ya Tanzania imewahakikishia wajumbe 11 wa kamati teule ya Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza kwamba wanaitambua Kampuni ya Mbogo Kampuni ya Mbogo  Mining & General Supply Ltd na shughuli zote inazofanya  nchini ni halali.

Kauli hiyo imetolewa  na baadhi ya mawaziri akiwamo  Waziri wa Madini, Doto Biteko , Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Stella Manyanya, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro katika vikao  vilivyofanyika kwa nyakati tofauti na wajumbe hao.

Rais Nkurunzinza aliteua kamati hiyo kuja Tanzania  na kukutana na viongozi wa Serikali ili kupata  taarifa sahihi  na uhalali wa kampuni hiyo ambayo inatarajiwa kukabidhiwa jukumu la  kusambaza vilipuzi nchini Burundi sambamba  na kushiriki mkutano wa kimataifa wa uwekezaji  katika sekta ya madini.

Akizungumza na wajumbe hao, Biteko alisema  Serikali ya Tanzania haina shaka na kampuni hiyo na haijawahi kukiuka au kwenda kinyume na vibali vinavyotolewa na wizara, hivyo aliwataka kuondoa wasiwasi na kuipatia kazi nchini Burundi.

 “Tunashukuru kwa ujio wenu maana shughuli ambazo zinafanywa na kampuni hii ni nyeti na zinaweza kuhatarisha usalama wan chi, lakini niwahakikishie kwamba tunafahamu kila kitu juu ya Mbogo Mining kwanza haijawahi kuleta shida tangu tunaipa vibali.

“Hapa nimeambatana na watalaamu ambao kila siku wanafanya nao kazi hivyo nawapa uhuru wa kuhoji kila kitu mnachotaka na majibu yatapatikana,” alisema

Kwa upande wa Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda , Manyanya ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Riziki Shamdoe na watalaamu wengine alisema  hawana wasiwasi na kampuni hiyo na inafahamika serikalini na wanashirikiana katika kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo.

“Mbogo Mining imeweka historia hapa nchini kwa namna inavyowekeza na hadi nje ya nchi, kitendo cha kufika kwenu Burundi  kimetuunganisha zaidi katika sekta ya viwanda na biashara na shughuli hii bila shaka itaongeza ajira kwa mataifa haya mawili,” alisema


Share:

Mahakama Kuu ya Kenya yatoa amri ya kusitishwa Safari zote za ndege kutoka China kwa Hofu ya Corona

Mahakama Kuu ya Kenya imetoa amri ya kusitishwa kwa muda ndege zote kutoka China zinazoingia katika nchi hiyo  kufuatia kesi kuhusu virusi vya Corona iliyowasilishwa na chama cha mawakili wa nchi hiyo.

Amri hiyo ya Mahakama Kuu ya Kenya inataka kusitishwa kuingia nchini humo ndege kutoka China kwa kipindi cha siku kumi.

Akitoa hukumu yake leo Jaji James Makau ameziagiza Wizara ya Usalama wa Ndani na ya Afya kuwatafuta abiria wote 239 waliowasili nchini Kenya kutoka China kupitia uwanja wa ndege wa  Kimataifa wa Jomo Kenyata mnamo Februari 26, na kuwatenga katika hospitali ya kijeshi.

Huku hayo yakijiri Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametoa agizo kuhusu virusi vya Corona kufuatia malalamiko ya umma kutoka kwa Wakenya kuhusiana na jinsi serikali inavyoshughulikia virusi hivyo hatari ambavyo vinaendelea kutikisa mataifa duniani.

Katika agizo lake Rais Uhuru Kenyatta anataka kamati ya kitaifa ya kushughulikia hali ya dharura kushughulikia mlipuko wa virusi vya Corona.

Rais pia ameagiza kukamilishwa kwa kituo cha kitaifa cha kuwatenga na kuwatibu wagonjwa mjini Nairobi katika kipindi cha siku saba.

Magazeti ya Kenya yameendelea kuangazia ghadhabu za Wakenya baada ya serikali kuruhusu ndege kutoka China kutua nchini humo.

Hatua hiyo pia imelalamikiwa sana katika mitandao ya kijamii baada ya ndege ya Shirika la Southern kuwasili nchini Kenya siku ya Jumanne iliyopita na kuruhusiwa kuingia nchini humo abiria 239.

Saa kadhaa kabla ya hatua hiyo, maafisa wa Kenya walikuwa wametangaza kurejeshwa kwa safari za ndege kuelekea China, licha ya hofu ya kusambaa kwa virusi vya Covid-19.


Share:

Maseneta Wa Ufaransa Kufanya Ziara Nchini




Share:

Mkutano Wa Mawaziri Wa SADC Wa Sekta Ya Ajira Na Kazi Kuanza Dar

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Tanzania inatakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Mawaziri na Wadau wa Utatu wa Sekta ya Ajira na Kazi kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajiwa kufanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 2 hadi 6 Machi 2020.

Mkutano huu ambao utafunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, umebeba kaulimbiu isemayo “Kukuza Soko la Ajira na Mahusiano Mema Sehemu za Kazi kwa Maendeleo Endelevu”.

Akizungumza na Kamati ya Maandalizi ya Mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa, Serikali ya Tanzania imejipanga vizuri kuwapokea Mawaziri 15 kutoka Nchi za SADC na kuwataka wajumbe wa Kamati hizo kukamilisha maandalizi kwa kuzingatia viwango ambavyo tayari vimewekwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC uliofanyika mwaka 2019 hapa nchini.

“Tanzania ni Mwenyekiti wa SADC kwa kipindi cha mwaka mmoja. Tumeendelea kuwa na Mikutano kadhaa ya kisekta tangu ulipofanyika Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC mwaka 2019. Nawahimiza tuendelee kuandaa mikutano hii kwa kufuata viwango vya juu vilivyowekwa na Mhe. Rais wetu wakati wa Mkutano huo na mingine iliyofuata hadi hapo tutakapokabidhi uenyekiti kwa nchi nyingine” alisisitiza Mhe. Mhagama.

Aidha, Mhe. Mhagama alipokea taarifa za utekelezaji wa majukumu ya kamati ndogo ndogo ikiwa ni pamoja na kupitia ratiba ya Mkutano ambapo mbali na kushiriki Mkutano huo, Mawaziri hao watapata fursa ya kufanya ziara katika maeneo kadhaa ikiwemo Chuo  Don Bosco Net Tanzania kilichopo Dar es Salaam kwa ajili ya kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na vijana wanaosoma chuoni hapo. Pia Mawaziri watatembelea maoneo mbalimbali ya kihistoria yaliyopo Bagamoyo lengo ikiwa ni kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania.

Kadhalika, Mawaziri hao watashuhudia uzinduzi wa Programu ya Taifa ya Mafunzo kwa Vitendo mahala pa kazi kwa vijana (Internship) utakaofanyika tarehe 5 Machi 2020 sambamba na ufunguzi rasmi wa Mkutano huo. Mkutano huu ni mwendelezo wa mikutano ya kisekta ya SADC ambayo itafanyika nchini kwa kipindi cha mwaka mmoja, kufuatia Tanzania kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo hadi mwezi Agosti 2020.

Mkutano wa Mawaziri ambao utatanguliwa na vikao vya maandalizi vya Makatibu Wakuu na Wataalam vitakavyofanyika kuanzia tarehe 2 Machi 2020, unatarajiwa kuhudhuriwa na washiriki kutoka nchi 16 wanachama wa SADC ikiwemo Tanzania.


Share:

Rais Magufuli Afanya Ziara Ya Kustukiza Kukagua Maendeleo Ya Ujenzi Wa Msikiti Wa Bakwata Kinondoni

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua makabati maalumu kwa ajili ya kuwekea viatu vya waumini wakati wa swala alipofanya ziara ya kustukiza kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Msikiti wa Bakwata unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Ijumaa 28, 2020


Share:

PICHA: Aliyekuwa Katibu Mkuu CHADEMA Dr. Vicent Mashinji Atambulishwa Rasmi CCM

Viongozi waandamizi watano kutoka vyama vya upinzani wametambulishwa  leo na kupokelewa rasmi kuwa wana CCM mbele ya Mwenyekiti wa Chama hicho Rais John Pombe Magufuli na wajumbe wa Kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Ofisi Ndogo ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam.

Kutoka kushoto ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Vincent Mashinji, aliyekuwa Meya wa jiji la Arusha kupitia CHADEMA Bw. Kalisti Lazaro,  aliyekuwa Meya wa Jiji la Mbeya kupitia tiketi ya CHADEMA Mchungaji David Mwashilindi .

Wengine ni aliyekuwa Mbunge wa Tandahimba kupitia CUF, Bw. Katani Ahmed Katani na aliyekuwa Naibu Meya wa Jiji la Mbeya kupitia tiketi ya CHADEMA Bw. Fanuel Kyanula


Share:

Video Mpya: Aslay – Rudi Darasani

Video Mpya: Aslay – Rudi Darasani


Share:

Video Mpya Ya Dogo Janja: – Nuru

Video Mpya Ya Dogo Janja:  – Nuru


Share:

Video Mpya Ya Nandy:– Na Nusu

Video Mpya Ya Nandy:– Na Nusu


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger