Tuesday, 25 February 2020

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne February 25



















Share:

Monday, 24 February 2020

Vifo Vya Wajawazito Kipindi Cha Kujifungua Vyapungua Hospitali Ya Rufaa Ya Mkoa Temeke

Na. Catherine Sungura - Dar es Salaam
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa temeke imejipanga kuokoa maisha ya wakina mama, wajawazito hususan katika kipindi cha kujifungua, kutimiza lengo hilo imeboresha miundombinu yake, vifaa tiba pamoja na kuimarisha huduma za afya kwenye ngazi za msingi.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, wakati wa ziara yake ya kikazi hospitalini hapo, ambako alikwenda kwa lengo la kusikiliza maoni na changamoto kutoka kwa wananchi na watumishi wa hospitali hiyo.

“Mwaka 2018 walikuwa na vifo 19 vya wajawazito na 2019 walikuwa na vifo 8 tu, lakini kwa takwimu za kuanzia Novemba 2019 hadi leo hakuna mwanamke mjamzito aliyekuja hospitalini hapa na kupoteza maisha, niwapongeze madaktari, wauguzi na watoa huduma wote wa hapa kwa hatua hii," amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa jitihada za makusudi, kuwekeza kwenye huduma za afya nchini sambamba na ujenzi wa vituo vya afya na ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa.

“Sasa hivi hapa temeke kuna huduma za kibingwa za meno ambapo zamani haikuwepo," amesema.

Waziri Ummy amesisitiza Wizara ina mpango pia wa kuhakikisha huduma zote za kibingwa zinazohitajika zinakuwepo kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa.

Hata hivyo amesema kuwa wanawake 15 kati ya wanawake 100 ndio ambao huhitaji kupelekwa kujifungulia kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa hususan wale wenye changamoto za ujauzito, kwa mfano mtoto amekaa vibaya au viashiria vya uzazi pingamizi.

Kwa upande  wa vipimo waziri huyo amesema kuwa Wizara yake imeongeza vipimo vya utra sound hivi sasa serikali imeboresha vituo vya afya na kwamba vipimo hivyo vinaanza kutolewa kuanzia ngazi za vituo vya afya vya umma na hospitali za wilaya nchini.

Amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma kuanzia ngazi ya msingi na hospitali za rufaa za mikoa ni kwa wagonjwa watakaopata rufaa.

“Kwa yeyeote atakayefanya makusudi kukorofisha vipimo ili watu waende kupima kwenye vutuo binafsi tutawachukulia hatua kwani ni wahujumu uchumi, tunataka vipimo vyote vifanyike ndani ya hospitali ila pale mashine haipo tutaruhusu, lengo letu ni kujitosheleza kwa vipimo vyote kwenye vituo vya afya vya umma," amesisitiza Waziri Ummy.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Yudas Ndungile amesema kuwa kutokana na maboresho ya miundombinu, wataalam na vifaa tiba kwa mkoa huu wameweza kupunguza vifo vipatavyo arobaini kwa mwaka ukilinganisha na vifo186 mwaka 2018 hadi vifo 140 mwaka 2019 na matarajio yao ni kupunguza zaidi.

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke Dkt. Meshack Shimwela amesema kuwa  hospitali hiyo imeondoa msongamano wa wajawazito kwa kuwa hivi sasa wananchi wengi wanafuata mfumo wa rufaa.

"Hivyo wakina mama wajawazito wanaofika kwenye hospitali hii ni wale wenye changamoto ya uzazi kwa maana hiyo wengi wanajifungulia kwenye ngazi za chini ambapo huduma za afya nazo zimeboreshwa," amesema.

MWISHO


Share:

Madalali Na Waendesha Minada Wasiofuata Sheria Kukiona Cha Moto

Na Ramadhani Kissimba, WFM, Dar Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James mewaonya madadali na waendesha minada Tanzania Bara kuacha mara moja kufanya biashara hiyo bilaa kujisajili kwani watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Bw. James ametoa onyo hilo Jijini Dar es Salaam wakati akizundua Mfumo Mpya wa Kieletroniki wa utoaji leseni za udalali na uendeshaji wa minada ya hadhara Tanzania Bara ambapo watoa huduma hiyo kuanza sasa wanatakiwa kujisajili kupitia mfumo huo kwa njia ya mtandao wa Internet ama kupitia simu zao za kiganjani.

‘’Napenda kuwafikishia taarifa hii wananchi wote, hasa Madalali na waendesha minada, kuwa Wizara ya Fedha na Mipango itaendelea kufuatilia na kuchukua hatua kali kwa wote watakaojuhusisha na shughuli za udalali na uendeshaji wa minada bila kuwa na leseni halali’’ alisema Bw. James.

Aliziagiza Taasisi zote za Serikali kufanya kazi na Madalali na waendesha minada ambao wanatambulika kisheria na kwa kufanya hivyo watakuwa wameisaidia Serikali kujipatia mapato yatakayotokana na ada ya leseni itakayolipwa na wafanyabiashara ya udali na waendesha minada.

“Mfumo huu utapunguza changamoto zilizokuwepo hapo awali ambazo zilikuwa zinatumia mlolongo mrefu wa kupata leseni kwa kuwa mfumo huo  umeunganishwa na Mfumo wa Malipo wa GePG ambapo mwombaji ataweza kulipia ada ya leseni kwa kutumia benki, mawakala au simu za kiganjani na hivyo kurahisisha na kuboresha ulipaji, kupunguza gharama za ulipaji na kuongeza uwazi na udhibiti wa Fedha za Umma.

Bw. James aliutangazia Umma kuwa kuanzia  tarehe 24 Februari, 2020 maombi yote ya leseni za Udalali na Uendeshaji wa Minada Tanzania Bara yawasilishwe kupitia Mfumo wa Utoaji wa Leseni za Udalali na Uendeshaji Minada ambao unapatikana katika tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango (www.mof.go.tz);

Awali, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Bw. Chotto Sendo, amesema biashara ya udalali na uendeshaji wa minada hapa nchini imekuwa ikikua kwa kasi na hivyo kutengeneza ajira, kuongeza kipato pamoja na kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi.

Bw. Chotto aliongeza kuwa leseni za Udalali na uendeshaji wa minada Tanzania Bara zinatolewa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa mujibu wa sheria ya waendesha minada ya Mwaka 1928 iliyorejewa Mwaka 2002, na Wizara imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kutatua changamoto zinazowakabili wadau hawa ili kuwawezesha kufanya shughuli zao kwa ufanisi.

Wakizungumza kwa niaba ya madalali, Mwenyekiti wa Chama cha Mdalali wa Mahakama Bi. Mwamvua Kigulu na Mwenyekiti wa madalali Binafsi Bw. Phidel Katundu, wameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kwa kubuni mfumo huo utakao wapunguzia gharama ya kufuata huduma ya usajili jijini Dodoma.

Wameiomba Serikali kudhibiti madalali wasio na leseni au wale wasiosajiliwa kwa kuwa wanaikosesha Serikali mapato pamoja na kuchafua taswira ya biashara ya udalali nchini.

Wamemwomba Katibu Mkuu Bw. Doto James kupitia upya Sheria ya Udalali ya Mwaka 1928 ambayo wamesema imepitwa na wakati na inakwaza shughuli za udalali nchini ikiwemo urasimu wa ufanyakazi kazi zao kutoka kwa mamlaka za Serikali Kuu hasa makatibu Tawala wa Wilaya ambao wanataka kupata vibali kutoka kwao kabla ya kutekeleza kazi zao za udalali katika maeneo husika.
 
MWISHO


Share:

Agribusiness Advisor at Rikolto [ Mpanda ]

Agribusiness Advisor in Mpanda Rikolto in East Africa (formerly known as VECO) is part of the Rikolto network, an international NGO with more than 40 years of experience in partnering with farmer organisations and food chain actors across Africa, Asia, Europe and Latin America. Rikolto aims to contribute to the development of a dynamic, sustainable and inclusive agricultural sector… Read More »

The post Agribusiness Advisor at Rikolto [ Mpanda ] appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Watumishi Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Watakiwa Kutunza Siri

Na Felix Mwagara, MOHA.
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima amewataka watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kufanya kazi kwa kushirikiana, uwajibikaji na kutunza siri za ofisi kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi Tawi la NIDA, Kailima alisema mafanikio ya Mamlaka hiyo ni pamoja na kushirikiana katika utendaji wa kazi ili kuleta weledi, na pia kuepuka kutoa siri za ofisi kwa mujibu wa utaratibu wa utumishi wa umma.

Pia aliwakumbusha watumishi hao kutoka Makao Makuu ya NIDA na Ofisi zake Mikoani, kuhakikisha uwajibikaji unakuwepo kwa upande wa mwajiri na mwajiriwa kwa kufanyiwa kazi kile kinachotakiwa kufanyiwa kazi na kisichohitajika kuifanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria.

“Tukoseane kwa nia ya kuboresha, tusikoseane kwa nia ya kubomoa kwa sababu ya kupata fursa hii ya kuwa na haki na hadhi sawa, na pande zote mbili ziwajibike kuwajibishana,” alisema Kailima.

Aliongeza kuwa, watumishi wanapaswa kupewa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za mamlaka na masuala yanayowahusu kwa utaratibu wa ofisi au unaoidhinishwa na Mkurugenzi Mkuu na si vinginevyo.

“Muhakikishe mnatoa huduma kwa wananchi sehemu zote nchini kwa weledi, maafisa wafike mapema katika maeneo ya kazi na kutoa vitambulisho vya Taifa mapema, na wananchi waridhike na huduma hiyo mnayoitoa, kwa hatua hiyo mtapunguza malalamiko ya wananchi,” alisema Kailima.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dkt. Arnold Kihaule alitoa mafanikio ya Mamlaka yake hadi kufikia Desemba mwaka 2019, alisema NIDA imefanikiwa kusajili wananchi 21,511,321, Wageni wakaazi, 19,311 na Wakimbizi 274,000 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

“Pia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa imezalisha namba za utambulisho 16,211,654 na kutoa vitambulisho 5,787,869, na vimewafikia wananchi ilipofika mwezi Desemba 2019,” alisema Dkt. Kihaule.

Kikao cha Baraza hilo cha siku moja pia kilipitia Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2019/20 kwa Kipindi cha kwanza cha Mwezi Julai hadi Desemba na Makadirio ya Bajeti ya Mamlaka kwa Mwaka wa Fedha 2020/21.


Share:

Chief Country Compliance Officer / Senior Manager at Citi Bank

Chief Country Compliance Officer / Senior Manager  Locations: Dar es Salaam, Dar es Salaam Region Job Function: Compliance and Control Employee Status: Regular Job ID: 20162416 Oversees the Citi Compliance Risk Management Program for a medium to smaller franchise country and/or multiple countries including regulated branches, legal entities and other affiliates. The Citi Country Compliance Officer (CCCO) is… Read More »

The post Chief Country Compliance Officer / Senior Manager at Citi Bank appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Advisor Health at GIZ

Advisor Health  As an international cooperation enterprise for sustainable development with worldwide operations, the federally owned Deutsche Gesellschaft fur Internationale Zusammenarbeit (GIZ) GmbH supports the German Government in achieving its development-policy objectives. The GIZ program “Improving Healthcare in Tanzania” is looking to fill the position of Advisor Policy Development and Coordination in the Health Sector. Duty station: Dodoma… Read More »

The post Advisor Health at GIZ appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

BREAKING: Madiwani 11 wa CHADEMA wakiongozwa na Meya wa Jiji la Mbeya wahamia CCM

Madiwani 11 wa Chadema Halmashauri  ya Jiji la Mbeya akiwemo Meya wa Jiji hilo wamejiuzulu na kuhamia CCM leo Jumatatu Februari 24, 2020.

Katibu Mkuu wa CCM, Bashiru Ally amesema kati ya Madiwani hao, 10 ni Madiwani wa Kuchaguliwa na Mmoja ni wa Viti Maalumu huku timu hiyo inayoongozwa na Meya ikiwa na Viongozi Watatu wa Juu wa CHADEMA.

Amesema kuwa Madiwani hao wanatoka katika Jiji la Mbeya kwenye Halmashauri inayoongozwa na CHADEMA na Mbunge wa Jimbo hilo ni Joseph Mbilinyi (Sugu) na kuwa huo ni ugeni mkubwa tangu aanze kupokea Wageni.

Aidha, amesema ameongea na Madiwani hao na kumueleza kwanini wanafanya uamuzi huo wakati huo na amefurahi sana maana kazi yake ni kuifanya CCM kutoa ushawishi na kupata wafuasi kila kona ya Nchi.


Share:

BREAKING: Erick Kabendera Aachiwa Huru Kwa Masharti Ya Kulipa Fidia Au Kifungo Cha Miezi 3

Mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera amehukumiwa kulipa faini Sh100 milioni baada kukiri kosa la  utakatishaji fedha na pia kulipa faini ya Sh250,000 au kwenda jela miezi mitatu kwa kukiri kukwepa kodi,pamoja na fidia ya shilingi milioni 172. 

Mapema leo, Kabendera aliyekuwa akikabiliwa na makosa matatu, alifutiwa kosa lake alilokuwa akidaiwa Kuongoza Genge la Uhalifu.

Hukumu imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega baada ya Kabendera kusota korokoroni tangu alipofikishwa mahakamani hapo Agosti 5, 2019.

Kabendera anatakiwa kulipa kiasi cha Sh.Mil 173 ndani ya miezi 6, huku kiasi cha Sh.Mil 100 akiwa tayari ameshaingiza katika akaunti ya Serikali.

Kabendera kwa sasa yupo huru, huku akitakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha.


Share:

Mwandishi wa habari , Erick Kabendera Atiwa Hatiani Kwa Mashitaka Mawili

Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtia hatiani mwandishi wa habari , Erick Kabendera.

Uamuzi huo wa mahakama umetolewa leo Jumatatu Februari 24, 2020 baada ya Kabendera kukiri mashtaka yake mawili ya kukwepa kodi na kutakatisha Sh173 milioni.

Uamuzi huo umetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega baada ya upande wa mashtaka kumsomea maelezo ya awali ya mshtakiwa huyo.

Kabendera ambaye ni mwandishi wa habari wa kujitegemea alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Agosti 5, 2019 akikabiliwa na mashtaka matatu

Leo amefutiwa shtaka la kuongoza genge la uhalifu na kubaki na mashtaka mawili ya kukwepa kodi na kutakatisha zaidi ya Sh173.2 milioni.



Share:

Finance Manager at Basil & Alred

Finance Manager  On behalf of our client, a leading, highly innovative company, providing professional events and entertainment services with presence in numerous parts of the world. We are seeking to recruit two high caliber candidates for the position of Finance Manager and Human Resources Manager, Procurement and Logistics Officer at SOS Children’s Villages February, 2020 Position Title: Finance… Read More »

The post Finance Manager at Basil & Alred appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Tanzania Finance and Strategy Lead at One Acre Fund Tanzania

Job Summary The Finance and Strategy lead will own planning and financial analysis for the country, rotate through several departments, and work on special projects direction for our country director; all in order to drive impact and sustainability in the country. Minimum Qualification: Bachelor Experience Level: Management level Experience Length: 2 years Job Description 50% Finance and Strategy: Decide the Long-Term… Read More »

The post Tanzania Finance and Strategy Lead at One Acre Fund Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Benki ya CRDB yapongezwa kuisaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ukusanyaji wa zaidi ya shilingi bilioni 25 sekta ya Utalii

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuwa kinara katika kuisaidia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kukusanya mapato katika sekta ya Utalii. Mwaka jana Benki ya CRDB kupitia mifumo yake ya kidijitali iliweza kukusanya kodi na tozo kwa watalii na wageni zinazofikia dola za kimarekani milioni 12 kutoka dola laki 4 mwaka 2014 ambapo ni ongezeko la takribani asilimia 3000.

Akizungumza katika Semina maalum iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa ajili ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na viongozi wengine wa taasisi za Serikali Mheshimiwa Zuberi Ali Maulid, alisema Benki ya CRDB imekuwa kiungo muhimu katika uchumi wa Zanzibar hususani katika kuweka miundo mbinu thabiti ya huduma za kifedha kwa Wazanzibari na wageni.

“Benki ya CRDB ni mshirika muhimu katika uchumi wa Zanzibar, hususan kipindi hiki tukiwa tunakwenda kukamilisha Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2020. Serikali inafurahishwa sana na namna ambavyo tumekuwa tukishirikiana na Benki hii katika kuhakikisha tunafikia malengo tuliyojiwekea,” alisema Mhe. Zubeir Maulid.

Mheshimiwa Zubeir Maulid alisema moja ya mafanikio makubwa ambayo Serikali imeyapata kutokana na ushirikiano baina yake na Benki ya CRDB ni kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato ambao unatokana na uunganishwaji wa mifumo ya kidijitali ya malipo ya Benki ya CRDB. “Mwaka jana wametusaidia kukusanya zaidi ya dola za kimarekani milioni 12, hiki ni kiwango kikubwa sana ambacho kinatokana na ufanisi wa mifumo hii ya kidijitali ya Benki ya CRDB,” alisema Mhe. Zubeir Maulid.

Mhe. Zubeir Maulid alisema kuongezeka kwa ukusanyaji huo katika sekta ya utalii kunasaidia kuongeza kwa Pato la Taifa, na hivyo kuiongeza serikali uwezo katika utoaji wa huduma za kijamii. Pia alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inafurahishwa na ushiriki wa Benki ya CRDB katika sekta nyengine za maendeleo ikiwamo kilimo, biashara na viwanda pamoja na ujenzi wa miundombinu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela alisema kwamba Benki ya CRDB imedhamiria kufanya kazi kwa karibu zaidi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kufikia malengo ya kujenga nchi yenye uchumi wa kati kupitia uwezeshaji katika miradi mbalimbali ya maendeleo. 

"Tunafahamu Serikali imejipanga kuleta mapinduzi katika sekta zote za maendeleo na sisi tumeweka mikakati ya ushiriki wetu katika kuisaidia Serikali kuanzia sekta ya kilimo, utalii, ujenzi, uchakataji wa mazao na uwekezaji kwenye viwanda,” alisema Nsekela huku akibainisha kuwa benki hiyo pia imejipanga pia kuwezesha sekta binafsi ambayo ni mshirika wa maendeleo wa Serikali nchini.
 
Nsekela alisema usahili wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Tabianchi (GCF) ulioipata Benki hiyo mwishoni mwa mwaka jana umesaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza uwezo wa benki hiyo kutoa mikopo ambapo sasa hivi inaweza kutoa hadi dola za kimarekani milioni 250 kwa mradi mmoja.

“Hizi ni fedha nyingi sana ambazo tumedhamiria kuzielekeza katika miradi ya maendeleo nchini kwa kushirikiana na Serikali na sekta binafsi,” aliongezea Nsekela.

Semina hiyo maalum kwa ajili ya Wajumbe na Baraza la Wawakilishi na Viongozi wa Serikali Zanzibar ambayo ilikuwa na kauli mbiu ya “Pamoja Kujenga Uchumi”, ililenga katika kujadiliana namna ya kuboresha ushirikiano kati ya Serikali na Benki ya CRDB katika kufanikisha miradi ya maendeleo nchini pamoja na kusogeza huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi ili kuchochea ukuaji wa uchumi.



Share:

Human Resources Manager at Basil & Alred

Human Resources Manager   On behalf of our client, a leading, highly innovative company, providing professional events and entertainment services with presence in numerous parts of the world. We are seeking to recruit two high caliber candidates for the position of Finance Manager and Human Resources Manager, Position Title: Human Resources Manager Reports to: Chief Operations Officer Job Location: Dar… Read More »

The post Human Resources Manager at Basil & Alred appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Ongezeko La Sangara Ziwa Victoria Laishtua Ccm,yatoa Maagizo Mazito

CHAMA cha Mapinduzi kimeshtushwa na ongezeko kubwa la samaki aina ya Sangara ikiwa ni miaka mitatu tu tangu Serikali ya awamu ya tano kuanza operesheni za kudhibiti uvuvi haramu katika Ziwa Victoria na kutaka Serikali kuchukua hatua za haraka kutafuta masoko ya uhakika ya samaki ndani na nje ya nchi.

Wakizungumza kwenye ziara ya Wajumbe wa Sektetarieti ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu baadhi ya Wavuvi katika Mwalo wa Nyamikoma wilayani Busega wamesema awali kabla ya operesheni kuanza walikuwa wakisafirisha wastani wa tani 6 za samaki kwa mwezi lakini tangu Serikali ilipoamua kuchukua hatua za kudhibiti uvuvi haramu samaki wameongezeka na sasa wanasafirisha wastani wa tani 60 kwa mwezi.

Mwenyekiti wa Kikundi cha Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi ‘BMU’ Mwalo wa Nyamikoma wilayani Busega mkoani Simiyu , George James alisema ongezeko hilo kubwa la samaki pia limepunguza bei ya Sangara kutoka wastani wa shilingi 9,000  kwa kilo hadi kufikia shilingi 4,000 kwa kilo.

Mbali na mafanikio hayo pia wavuvi hao wameiomba Serikali kuwasaidia kupata mtambo wa kutengeneza barafu katika eneo hilo kwani kwa sasa wanalazimika kusafiri hadi jijini Mwanza umbali wa zaidi ya kilomita 150 kufuata barafu.

Hivyo walimuomba Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu kumfikishia shukrani Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli  kwa uongozi wake imara hasa katika usimamizi wake wa rasilimali za uvuvi na kwamba sasa samaki ni wengi na kwamba ombi lao kubwa ni kusaidiwa kupata soko baada ya ongezeko hilo la samaki.

Akizungumza katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mwalo wa Nyamikoma wilayani Busega, Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu, Haula Kachwamba  aliitaka Serikali kupitia Dawati la Sekta Binafsi lililoko Wizara ya Mifugo na Uvuvi kufika katika mwalo huo wa Nyamikoma ili kuwaunganisha wavuvi hao na taasisi za kifedha kuweza kupata mtambo wa kutengeza barafu.

Pia ameitaka Serikali kutanua wigo wa kuwatafutia masoko ya samaki wavuvi hao ili kunufaika na fursa kubwa ya ongezeko hilo la samaki aina ya Sangara kwa kupeleka katika masoko ya mikoa ya mbali na Ziwa Victoria pamoja na nchi za jirani za Kongo, Zambia, Burundi, Rwanda, Malawi na Msumbiji.

Kuhusu vita dhidi ya uvuvi haramu, Katibu huyo alisema Ilani ya CCM imeitaka Serikali kudhibiti uvuvi ili kupata uvuvi endelevu na kuongeza kipato cha mwanchi mmoja mmoja na kuiletea fedha za kigeni Serikali kutokana na mauzo ya samaki nje ya nchi na kupongeza juhudi kubwa zilizofanywa na Rais Dk. John Magufuli katika kusimamia rasilimali hizo za uvuvi.

“Tunaishukuru Serikali kwa kuamua na kusimamia operesheni Sangara ambayo ilisimamiwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi operesheni hii imezaa matunda kama mlivyotoa ushuhuda kwamba operesheni hii mliipinga sana lakini sasa mnaona matokeo yake”alisema.

Aliongeza kuwa CCM inaamini katika kusimamia sheria na kwamba hatua zote zilizochukuliwa na Serikali katika kudhibiti uvuvi haramu zililenga kunufaisha watanzania wengi tofauti na hapo awali ambapo watu wachache ndio waliokuwa wakinufaika kupitia uvuvi haramu.

“Niipongeze sana Serikali yetu kwa kukubali kutukanwa, kuzuliwa maneno mengi kupata kashfa nyingi lakini bado waliendelea kusimamia msimamo wa kulinusuru ziwa letu kwenye ilani yetu tumesema tutahakikisha tunadhibiti uvuvi haramu ili tuweze kupata samaki wa kutosha kwa ajili ya watanzania sisi CCM tunaomba msiishie hapa endeleeni kudhibiti uvuvi haramu ili matunda yazidi kuongezeka siku hadi siku”alisema Katibu wa CCM

Katika hatua nyingine, Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Busega, David Palanjo aliongoza zoezi la uteketekezaji wa shehena ya nyavu haramu zilizokamatwa kwenye operesheni hiyo katika wilaya za Magu na Busega na kutoa wito kwa wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali katika kudhibiti uvuvi haramu.


Share:

Hatima Ya Tundu Lissu Kuhusu Ubunge Wake Kujulikana Kesho

Mahakama Kuu kesho itaanza kusikiliza maombi ya aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, kumruhusu kwenda Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi wa Spika wa Bunge, Jobu Ndugai, kumvua nafasi ya ubunge wa jimbo hilo.

Juni 20, mwaka jana, Spika alitangaza kumvua Lissu ubunge kwa madai ya kutotimiza masharti ya kuendelea kuwa mshiriki katika shughuli za Bunge.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Msemaji wa familia ya Lissu, Wakili Alute Mughway, alisema Mahakama Kuu Masjala ya Dar es Saalam, Februari 25, mwaka huu, itasikiliza maombi ya Lissu, endapo atakubaliwa kwenda Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi wa kuvuliwa nafasi yake ya ubunge.

Mughway alisema, Lissu alipeleka ombi hilo Septemba mwaka jana dhidi ya Spika Ndugai kumvua nafasi yake ya ubunge na kutangaza Jimbo la Singida Mashariki kuwa wazi.

Septemba 9, 2019, Mahakama Kuu, ilitupilia mbali ombi la Lissu la kupinga kuvuliwa ubunge.

Akitoa uamuzi huo, Jaji Sirilius Matupa, alisema maombi ya Lissu hayatekelezeki kwa sababu mleta maombi alitakiwa kufungua kesi ya kupinga uchaguzi mahakamani, badala yake alipeleka maombi ya kutaka kupinga uamuzi wa Spika.

Msemaji huyo wa familia, Mughway, alisema Lissu, hajaridhishwa na uamuzi wa Mahakama Kuu, hivyo amepeleka maombi mengine kuruhusiwa kwenda Mahakama ya Rufani kutolea uamuzi kama hukumu ya Jaji Matupa ni sahihi kisheria.

Alisema maombi hayo, kwa mara ya kwanza yalitajwa Desemba mwaka 2019, na Februari 25, mwaka huu yatakwenda kusikilizwa.

Akizungumzia Lissu kurejea nchini kutokana na kukamilisha matibabu yake, alisema atarudi baada ya muda kidogo, kwa kuwa anasubiri uchunguzi wa mwisho wa madaktari kuangalia kama matibabu aliyopewa yamekidhi viwango.

Licha ya kuzungumza hayo, alisema Lissu alikuwa na mpango wa kurejea nchini kuendelea na shughuli zake, lakini kinachomkwamisha ni kuhofia ulinzi na usalama wake.

Credit: Nipashe


Share:

EXPRESSION OF INTEREST FOR EXTERNAL ANNUAL FINANCIAL AUDIT AND LEGAL SERVICES | Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (UMATI)

Job Summary The successful External Auditor will cover the Association Head Office, the Static Clinics Offices and Association’s investment private entity limited by shares. The audit will be in conformity with Generally Accepted Accounting Standards and International Standards of Auditing (“ISA”). The findings and recommendations shall include an action plan for UMATI and accounting improvements depending on findings… Read More »

The post EXPRESSION OF INTEREST FOR EXTERNAL ANNUAL FINANCIAL AUDIT AND LEGAL SERVICES | Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (UMATI) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger