Thursday, 28 November 2019

Upembuzi Yakinifu Ujenzi wa Reli ya Kuunganisha Tanzania na Rwanda Wakamilika

Tanzania na Rwanda zinakamilisha mchakato wa ujenzi wa reli itakayounganisha mataifa hayo mawili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Hayo yamesemwa  Jana Jumatano November 27, 2019 na Rais Magufuli wakati akizungumza na wananchi wa Isaka Mkoani Shinyanga.

“Nimeshazungumza na Rais Kagame (Paul wa Rwanda) kuhusu utekelezaji wa mradi huu, upembuzi yakinifu umekamilika. Kinachofanyika sasa ni kutafuta fedha,” alisema Rais Magufuli. 

Reli hiyo itakayounganishwa na ile ya kati itaanzia bandari kavu ya Isaka wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Mradi huo ambao tayari hatua ya upembuzi yakinifu umekamilika utarahisisha usafirishaji wa mizigo kutoka bandari kavu ya Isaka kwenda nchi jirani.


Share:

Scholarship Mpya Kwa Watanzania | Commonwealth Shared Scholaships Tenable In The United Kingdom 2020

1.0 Call for Applications
The General public is hereby informed that, the Government of United Kingdom has opened a new Commonwealth Shared Scholarship to eligible Tanzanians to pursue Masters Studies in the United Kingdom for the academic year 2020. Interested candidates are highly encouraged to apply under the following six themes:-

1.Science and technology for development;
2.Strengthening health systems and capacity;
3.Promoting global prosperity;
4.Strengthening global peace, security and governance;
5.Strengthening resilience and response to crises; and
6.Access, inclusion and opportunity.

Further details on the eligible study Programmes can be accessed through the following link

2.0 Mode of Application
The online application system can be reached through the following link:<<BOFYA HAPA>>

Before making an online application you are advised to read the following guidelines found in the following link: <<CLICK HERE TO DOWNLOAD PDF>>

3.0 Submission
All applications must be submitted by 16.00 (GMT) on 18th December 2019 
 
Note:
It is important that applicants should read and understand all instructions when filling the application forms, attach all the required documents such as certified copies of academic certificates, transcripts, and birth certificates and submit them online through the above link.


Share:

Zaidi Ya Wakulima 500,000 Wamejengewa Uwezo Chini Ya Mfumo Shirikishi Wa Udhibiti Ubora Kwa Ajili Ya Soko La Ndani Na La Jumuiya Ya Afrika Mashariki

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Nchi mbalimbali Duniani zinajadili na kuweka mikakati ya kuendeleza kilimo-hai. Mwaka 2010, Umoja wa Afrika kupitia Marais wake, ulipitisha Azimio la mpango na mkakati wa kilimo-hai kuelekea ajenda yake ya miaka 50 ijayo (Agenda 2063), na kuzitaka nchi zote kuchukua hatua kutekeleza azimio hilo.

Katika kufikia azimio hili la Umoja wa Afrika, Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau imefanikiwa kuwa na Sera ya Kilimo iliyohusisha kilimo-hai kwa upana wake na uwekezaji kwenye viwanda vinavyo chakata mazao ya kilimo-hai.

Hii inaenda sambamba na jitihada za Serikali ya awamu ya tano chini ya Mheshimiwa Rais John Pombe Joseph Magufuli ya kutaka Tanzania ifikie uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 kupitia sera ya viwanda. Ambapo kumeanzishwa dawati la kilimo-hai katika idaya ya Maendeleo ya Mazao ili  kufikia idadi ya wakulima  na wafugaji 149,000 waliothibitishwa na kuingia katika fursa ya masoko ya bidhaa za kilimo-hai kimataifa, wanaozalisha kwenye eneo la hekta takribani 278,000.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo jana tarehe 26 Novemba 2019 wakati akifungua kongamano la kitaifa la kilimo-hai la siku mbili linalofanyika Jijini Dodoma na kuongeza kuwa zaidi ya wakulima 500,000 wamejengewa uwezo chini ya mfumo shirikishi wa udhibiti ubora (participatory guarantee system - PGS) kwa ajili ya soko la ndani na la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Ameongeza kuwa kilimo-hai Duniani katika mataifa mbalimbali kinakua kwa kasi kubwa. Inakadiriwa kuwa soko la bidhaa na mazao ya kilimo-hai duniani ni wastani wa Euro 89 bilioni ambapo hiyo ni fursa kubwa kwa kwa Tanzania kwani ni nchi ya tatu kati ya tano barani Afrika zinazoongoza kwa kuwa na eneo na idadi kubwa zaidi zilizo thibitishwa katika mfumo huo wa kilimo-hai, ikiongozwa na Uganda na Ethiopia na kufuatiwa na Kenya na Jamhuri ya Kidemokrsi ya Kongo (DRC).

Waziri Hasunga amesema kuwa kufuatia kupitishwa kwa mtaala mpya unaojumuisha stadi na programu za kilimo-hai katika vyuo vya mafunzo ya kilimo na vyuo vikuu kikiwemo SUA, inatarajiwa idadi hiyo ikiongezeka mara dufu. Vyama vikuu vya ushirika – KCU, KNCU na KDCU pamoja na makampuni kama Biore, Biosustain, Biolands na OLAM  wamewezesha nchi yetu kufikia mafanikio hayo.

Pia, ametoa mwito kwa wadau wa kilimo-hai nchini kufanya kazi kwa karibu na Wizara na Taasisi zake na Serikali yote kwa ujumla ili kwa pamoja kuwezesha upatikanaji wa uhakika wa chakula na lishe na masoko utakao boresha maisha ya watanzania walio wengi kwenye sekta ya kilimo.

Amesema kuwa baadhi ya changamoto katika kuendeleza kilimo-hai nchini ni pamoja na uhakiki (certification) wa mazao hayo kuwa ya kilimo hai, fedha kwa ajili ya uwekezaji katika kilimohai kibiashara, kutoyafikia masoko maalumu (niche market) hususani katika nchi za Ulaya kutokana na kutokidhi vigezo vya masoko hayo na tishio la mabadiliko ya tabianchi ambayo ni fursa katika kuendelea kilimohai nchini.

Waziri Hasunga amewahakikishia wadau wote waliohudhuria katika mkutano huo kuwa Wizara ya kilimo itaendelea kushirikiana nao kwa karibu hivyo wasisite kuwasilisha mapendekezo yao wakati wowote ili Serikali iyashughulikie kwa maslahi ya kuendeleza kilimo-hai nchini.

Kadhalika, amewasihi wadau wote kupitia kongamano hilo, kujadili na kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo ili kuweza kuongeza uzalishaji kupitia kilimo-hai.



Share:

Waziri Ummy Asema Serikali Inaendelea Na Mchakato Wa Kuboresha Sera Mpya Ya Afya

Na.Faustine Gimu Galafoni.Dodoma
Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mhe. Ummy mwalimu amesema serikali inaendelea na mchakato wa kuboresha sera mpya ya afya  ili kuimarisha huduma  za afya nchini badala ya kuendelea na sera iliyopo kwasasa ambayo imepitwa na wakati.
 
Waziri Ummy amesema hayo  jana Nov.27,2019 jijini Dodoma wakati akifungua Kongamano  la sita la   afya nchini  lijulikanalo  “TANZANIA HEALTH SUMMIT “ambapo pamoja na mambo mengine ameendelea kusisitiza  dhamira yake ya kuwasilisha bungeni muswaada utakao lazimisha kila mtanzania kuwa na bima ya Afya.
 
Waziri Ummy amesema Sera ya Afya ya Mwaka 2017 imejikita zaidi katika masuala ya tiba na si kinga hivyo Sera Mpya ya mwaka 2019/2020 itajikita zaidi katika Masuala ya kinga kwani kinga ni bora kuliko tiba.

Aidha ,Waziri Ummy amesema katika sera Mpya ya Afya ya Mwaka 2019/2020 itaangalia mktadha wa kuwafikia wananchi huduma ya Afya yaani Afya kwa wote kwa kuangalia vigezo muhimu vya uhitaji  tofauti ya na sera ya iliyopo ambapo inasema zahanati kila kijiji bila kuangalia mzigo wa Magonjwa ama geografia ya eneo husika.

Kwa upande wake Rais wa Kongamano la Afya nchini Tanzania, Dokta Omary Chillo  amesema Lengo la kongamano hilo ni kujadili changamoto mbalimbali zilizopo katika sekta ya afya na namna ya kukabiliana nazo ili kuleta ufanisi zaidi katika utendaji kazi.

Kongamano la sita la Afya Mwaka 2019 limeanza Nov.27 hadi  28,2019  huku likiandaliwa na Taasisi  sita ambazo ni  Wizara ya Afya Tanzania,Wizara ya Afya  Upande wa Zanzibar ,Ofisi ya Rais TAMISEMI ,Tume ya Huduma za kijamii ya Kikristo,Baraza la Waislam Tanzania[BAKWATA]  na Tindwa Medical Services   na kaulimbiu ni ufanisi na Matokeo katika utoaji wa huduma za Afya.

Mwisho.


Share:

Benki Ya Biashara Na Maendeleo Mashariki Na Kusini Mwa Afrika Yaleta Neema Kwa Wafanyabishara Wa Tanzania

Na Josephine Majura, Dar es Salaam
Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), imeahidi neema kwa Wafanyabiashara nchini kwa kuwapatia mikopo nafuu itakayowawezesha kusafirisha na kuuza bidhaa za kilimo nje ya nchi

Hayo yameelezwa na Mwakilishi wa Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Bw. Lloyd Muposhi, wakati ujumbe wa Benki hiyo uliopo nchini kwa ziara ya kikazi, ulipokutana na  kufanya mazungumzo na  Wafanyabiashara wanaojihusisha na uuzaji wa mazao hayo nje ya nchi ikiwemo  nafaka, chai, kahawa na katani.

Bw. Muposhi, ameeleza kuwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili yalikua mazuri yenye kujenga ambapo kwa mwaka ujao wa fedha ameahidi benki hiyo itawawezesha wafanyabishara ama sekta binafsi kimtaji ili waweze kukuza mitaji yao na kufanya biashara ya ushindani na yenye tija.

Kwa upande wake Mkurenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Bw. Edwin Rutageruka ameishukuru Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuratibu mkutano huo na kuwakutanisha Wafanyabiashara na Uongozi wa Benki ya Biashara na Maendeleo ambapo wamepata muda wakubadilishana uzoefu na kujadili mambo mbalimbali zikiwemo changamoto mbalimbali zinazokabili usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi, uzoefu wa kufanya biashara pamoja na ukosefu wa mitaji.

Bw. Edwin alisema changamoto kubwa iliyopo kwa Wafanyabiashara wa ndani ni ukosefu wa mitaji kwa kuwa ni gharama kubwa  kusafirisha bidhaa kwenda nje ya nchi hivyo iwapo TDB wataanza kutoa ufadhili kwa Wafanyabiashara wa Tanzania watakuwa wamewasaidia sana kuondokana na tatizo hilo.

Naye mmoja wa Wafanyabiashara walioshiriki katika mkutano huo Mkurugenzi wa ALASKATANZANIA, Bi. Jennifer Bash ameipongeza Serikali kwa kuandaa mkutano huo kwani umetoa fursa ya kubadilishana uzoefu kati ya Wafanyabiashara hao na uongozi wa benki hiyo.

Alieleza kuwa changamoto kubwa inayowakabili Wafanyabiashara wengi ni uhaba wa fedha na mitaji hivyo mkutano huo umetoa mwanga kwao kwa kuwa wamezungumza mambo mengi ambayo iwapo yatatekelezwa yatapunguza ombwe lililopo la ufanisi wa biashara kwa wafanyabiashara wengi.

Mkutano huo umefanyika Dar es Salaam ambapo ulihusisha Uongozi kutoka Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Wataalamu kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE).


Share:

Rais Magufuli apiga marufuku halmashauri kukopa benki.

Rais Magufuli amewapiga marufuku Wakurugenzi  Watendaji wa Halmashauri zote nchini kuacha  mara moja kukopa fedha kwenye taasisi za fedha kwa madai ya kufanya miradi ya maendeleo.

Ametoa kauli hiyo Jumatano Novemba 27, 2019 wilayani Bukombe mkoani Geita wakati akihutubia mkutano wa hadhara, Rais Magufuli amewaagiza iwapo wapo ambao wameshachukua fedha hizo kuzirudisha na kuvunja mikataba waliyoingia.

“Kama kuna mkurugenzi yeyote amekopa fedha azirudishe, mwenye mamlaka ya kukopa kwa niaba ya Serikali ni paymaster general wa Serikali ambaye ni Wizara ya Fedha pekee.”

“Anayekopa ajiandae kutoka. Naamini Wakurugenzi wamenielewa, nimepita Kahama Mkurugenzi ananiambia anataka kukopa kutoka TIB (Benki ya Uwekezaji Tanzania) kwa ajili ya kujenga stendi, haiwezekani fedha za wananchi kuchezewa, ovyo”  alisema Rais Magufuli




Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi November 28























Share:

Wednesday, 27 November 2019

Walimu 4,046 wa shule za msingi na sekondari wafukuzwa kazi

Katibu Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Winifrida Rutaindurwa amesema jumla ya walimu 4,046 wa shule za msingi na sekondari wamefukuzwa kazi kutokana na makosa mbalimbali yakiwemo utoro kazini, kukiuka maadili na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi.

Rutaindurwa ameyasema hayo jana  katika mkutano wa siku mbili uliolenga kuwajengea uwezo Makatibu Wasaidizi wa TSC kutoka Wilaya zote Tanzania Bara uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, jijini Dodoma.

Katika Maelezo ya kumkaribisha Naibu Waziri (Elimu) wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mwita Waitara, Rutaindurwa alisema kuwa tangu TSC ianze kufanya kazi mwezi Julai, 2016 walimu 7,123 walifunguliwa mashauri ya kinidhamu baada ya kukiuka maadili ya kiutumishi.

“Mheshimiwa Naibu Waziri katika makosa yaliyotendwa kwa kipindi cha miaka mitatu, makosa 5,447 yalikuwa ya utoro kazini, makosa 1,290 kukiuka maadili, makosa 162 uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi na makosa mengine kwa ujumla wake yalikuwa 224”, alieleza Rutaindurwa

Alifafanua kuwa TSC imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kiutumishi kwa mujibu wa Sheria Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Walimu ambapo walimu  4,046 walifukuzwa kazi, walimu 930 walipewa onyo/karipio, walimu 284 walipunguziwa mshahara, walimu 244  walisimamishiwa nyongeza ya mshahara, walimu 237 walishushwa cheo na walimu 14 walipewa adhabu ya kufidia hasara.

Alieleza kuwa walimu wengi walikutwa na makosa ya utoro wakati wa zoezi la uhakiki wa watumishi kwa kuwa waliondoka kwenye vituo vyao vya kazi bila kufuata taratibu na kuruhusiwa na waajiri wao, hivyo walichukuliwa hatua za kinidhamu.

“Wengi wa walimu waliotiwa hatiani kwa makosa ya utoro, walikuwa wameenda masomoni bila kupata ruhusa kutoka kwa waajiri wao na zoezi la uhakiki wa watumishi lilipofanyia ndipo ikagundulika kuwa ni watoro na mchakato wa kuwachukulia hatua za nidhamu ukaanza,” alisema.

Akifungua Mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Naibu Waziri anayeshughulikia elimu katika ofisi hiyo, Mhe. Mwita Waitara alieleza kuwa TSC bado ina kazi ya kufanya ili kuhakikisha walimu wanakuwa na uelewa wa kutosha juu ya taratibu za kiutumishi ili wajiepushe na makosa ya kinidhamu.

Aliweka bayana kuwa Serikali haijivunii kuwafukuza kazi walimu wake iliyowaajiri yenyewe ikizingatiwa kuwa bado kuna changamoto ya upungufu wa walimu katika maeneo mbalimbali nchini.

“Kwa kweli tunasikitika kuwa idadi ya walimu waliofukuzwa kazi ni kubwa, lakini ni lazima watumishi wa umma muelewe kuwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais wetu mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli haina huruma kabisa na watumishi wazembe wasiozingatia Maadili na Miiko ya kazi yao”, alisema Mhe. Waitara.

Pamoja na hayo, Mhe. Waitara alieleza kuwa walimu wamekuwa na kero na malalamiko mbalimbali yanayosababishwa na kutowajibika kikamilifu kwa baadhi ya watendaji wa wanaoshughulikia masuala yao.

Alieleza baadhi ya kero hizo kuwa ni kucheleweshwa kwa malipo ya kusafirisha mizigo kwa walimu waliostaafu, walimu waliostahili kupandishwa madaraja kutopandishwa kwa wakati, Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kukataa kupitisha barua za walimu wanaoomba kuhama kutoka Wilaya moja kwenda nyingine na walimu kutotendewa haki katika mashauri ya nidhamu.

Kutokana na changamoto hizo, Naibu Waziri alipiga marufuku tabia ya baadhi ya Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ya kuzuia kupitisha barua za walimu wanaoomba uhamisho na kueleza kuwa wao sio wenye mamlaka ya kutoa uamuzi wa ombi la mwalimu anayetaka kuhamia wilaya nyingine.

“Ni marufuku kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuzuia kupitisha barua za walimu wanaoomba uhamisho. Wao wanapaswa kupitisha, kuweka maoni yao na kuruhusu maombi hayo yaende kwa mhusika aliyeandikiwa. Mwenye mamlaka ya kukubali au kukataa ombi la uhamisho wa mwalimu ni  Katibu Mkuu, TAMISEMI,” alisisitiza Mhe. Waitara.

Aidha, Mhe. Naibu Waziri aliiagiza TSC kwa kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuandaa orodha ya walimu waliostahili kupandishwa madaraja lakini hawakupandishwa na kuiwasilisha TAMISEMI ili taratibu nyingine ziweze kufanyika.


Share:

Naibu Waziri Masauni Aagiza Mkuu wa Chuo cha Polisi Dar Aondolewe na Ashushwe Cheo

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni amemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Sirro kufanya mabadiliko ya uongozi kwenye Chuo cha Polisi Dar es Salaam kutokana na kukiuka maagizo yake katika ujenzi wa mabweni chuoni hapo.

Pia, Masauni amemuelekeza IGP Sirro kumuondoa Mkuu wa Chuo hicho, Antony  Ruttashuburugukwa na kumshusha cheo kutokana na kosa hilo.

Akizungumza leo Jumatano Novemba 27, 2019 akiwa chuoni hapo, Masauni amesema alielekeza katika ujenzi huo watumike wafungwa kufanya kazi za vibarua ili kuokoa fedha lakini mkuu huyo wa chuo hakutekeleza agizo hilo.

“Rais alikubali kutupatia Sh700 milioni kwa ajili ya ujenzi wa mabweni, tuliangalia na kuona tunaweza kuokoa Sh210 milioni za kuwalipa vibarua kwa kuwatumia wafungwa.”

“Nilizungumza na kamishna wa magereza akasema hilo linawezekana hivyo nikamuelekeza mkuu wa chuo kufanyia kazi suala hilo lakini leo nimekuja nakuta hali hii hakuna wafungwa,” amesema Masauni

Wakati Masauni anakagua ujenzi huo alikuta vijana wakifanya kazi na alipowahoji walimuleza kuwa wao ni vibarua wanaolipwa kwa siku.


Share:

Rais Magufuli Ampongeza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Kwa Kuchapa Kazi Vizuri

Rais Magufuli  amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga (RC), Zainabu Tellack kwa kumwakilisha vema kwa kusimamia kikamilifu nafasi yake  na kupambana na rushwa.

Akizungumza na wananchi eneo la Isaka Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga leo Jumatano Novemba 27, 2019, Rais Magufuli amemtaka mkuu huyo wa mkoa kuchapa kazi na kuendelea kupiga vita vitendo vya rushwa kwenye eneo lake.

“Mkuu wa mkoa wewe unafanya kazi nzuri sana; endelea kufanya kazi. Wewe ndiye mwakilishi wangu hapa na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa...ndio maana nimewasimamisha kazi RPC na RCO. Sijui walikuwa wanakudharau kwa sababu wewe ni mwanamke?” amesema Rais Magufuli

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo siku chache baada ya kuagiza kusimamishwa kazi kwa Kamanda wa Polisi mkoa (RPC) wa Shinyanga, Richard Abwao, Mkuu wa Upelele wa mkoa (RCO), John Rwamlema na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wa mkoa huo, Jumbe Samson kwa tuhuma za utovu wa nidhamu na uhujumu uchumi.

Kusimamishwa kazi kwa vigogo hao wa mkoa kulitokana na madai ya kushindwa kutekeleza maelekezo ya mkuu wa mkoa kuhusu hatua za kisheria dhidi ya kampuni moja inayozalisha pombe kali inayodaiwa kukwepa kodi.


Share:

Picha : RAIS MAGUFULI AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA ISAKA - KAHAMA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Isaka Mkoani Shinyanga wakati akielekea Kahama. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kahama mkoani Shinyanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kahama mkoani Shinyanga.
Wananchi wa Kahama wakishangilia mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili katika Wilaya hiyo wakati akitokea Mkoani Dodoma.
PICHA NA IKULU
Share:

JAMAA AUA MPENZI WAKE BAADA YA KUMKUMBUSHIA AHADI YA NDOA

Na Asna Kaniki, Mwananchi 
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Paschal (24), anadaiwa kumuua mpenzi wake, Rosemary Gallus (34) mkazi wa Gongo la Mboto kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali tumboni na kisha kujiua sababu ikidaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Kamanda wa polisi wilaya ya Ilala, Zuberi Chembela alisema tukio hilo lilitokea Ijumaa iliyopita ambapo kijana huyo alikwenda nyumbani kwa Rosemary kwa lengo la kumaliza tofauti zao baada ya kugombana.

“Wawili hao walikuwa wakiishi pamoja na wamezaa mtoto ambaye ana mwaka na miezi kadhaa, ugomvi wao ulianza baada ya binti kukumbushia kuhusu ahadi yao ya ndoa, mwanaume alisita hivyo binti alianza kutomuamini na ugomvi ukaanzia hapo,” alisema Chembela alipokuwa akizungumza jana kwa njia ya simu.

Hata hivyo baada ya kijana huyo kusita kutoa msimamo wake kuhusu kufunga ndoa binti aliamua kuondoka nyumbani alipokuwa akiishi na mzazi mwenzie na kwenda kupanga Gongo la mboto.

Alisema kwa kuwa marehemu hao walikuwa wazazi, waliendelea kuwasiliana na kijana huyo alipafahamu alipopanga mpenzi wake na hatimaye alikwenda kwa ajili ya kuzungumza na kumaliza tofauti zao.

“Badala ya usuluhishi ikawa ugomvi tena huku mwanaume akimtuhumu mwanamke kuwa anamsaliti kisha kumchoma na kitu chenye ncha kali tumboni mara mbili na kisha yeye mwenyewe kujichoma kitu tumboni mara mbili.”

Alisema kwamba baada ya hapo majirani walisikia mtoto akilia ambapo siyo kawaida yake ndipo walipokwenda kugonga hata hivyo hawakujibiwa, kwa kuwa mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani, ndipo baadaye walipoamua kuuvunja mlango huo.

Kamanda Chembela alisema majirani hao walipofika ndani walimkuta mtoto pembeni ya maiti za wazazi wake huku akiwa analia.

Kutokana na tukio hilo, Kamanda Chembela amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kama alivyofanya kijana huyo ambapo alidai kuwa ni kinyume cha sheria.
CHANZO - MWANANCHI
Share:

Live : RAIS MAGUFULI AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA KAHAMA MUDA HUU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Kahama Mkoani Shinyanga
Share:

RAIS MAGUFULI : ......KUSUSIA UCHAGUZI NAYO NI DEMOKRASIA

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kitendo cha kususia uchaguzi na kujitoa katika uchaguzi pia ni demokrasia huku akikisitiza kuwa maendeleo hayana chama na kwamba Watanzania wanatakiwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa. 

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Jumatano Novemba 27,2019 wakati akizungumza na wananchi wa Isaka wilayani Kahama mkoani Shinyanga. 

Rais Magufuli ametumia fursa hiyo kukipongeza Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Novemba 24,2019 ambapo baadhi ya Vyama vya Upinzani nchini Tanzania vilisusia uchaguzi huo 

“Ninapenda kuwashukuru sana ndugu zangu wa Isaka mmemaliza chaguzi, Nimeambiwa Chama Cha Mapinduzi kimepasua vizuri. Hongereni sana,maendeleo ndugu zangu hayana chama na demokrasia hata kujitoa nayo ni demokrasia,kususia uchaguzi nayo ni demokrasia”,amesema Rais Magufuli. 

“Kwa hiyo nawapongeza kwa ushindi mkubwa mlioupata chama cha mapinduzi lakini maendeleo hayana chama ni lazima tushikamane wote kujenga taifa letu,tunachohitaji ni maendeleo,ukileta maji,wote watakunywa,uwe CCM, uwe CHADEMA,ukileta bandari hapa kila mmoja atafanya biashara”,ameongeza Rais Magufuli. 

“Naomba Watanzania tutangulize mbele maslahi ya taifa letu,tuwe wamoja,tujenge Tanzania yetu”,amesema Rais Magufuli.
Share:

Shahidi Aeleza Mahakama Adhabu Ilivyosababisha Ulemavu Wa Mgongo Kwa Mwanafunzi

Kesi ya jinai inayomkabili Mwalimu Focus Mbilinyi , dhidi ya Jamhuri kwa tuhuma za kumpiga Mwanafunzi na kumsababishia ulemavu, imeendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Njombe, ambapo mashahidi wawili wa upande wa Jamhuri wamefika mahakamani hapo kuwasilisha ushahidi wao.

Kesi hiyo namba 141 ya mwaka 2019, inayomkabili aliyekuwa Mwalimu wa Shule ya Msingi Madeke, Focus Mbilinyi, imeendelea kusikilizwa mahakamani hapo chini ya Hakimu Irvan Msaki na Wakili wa Serikali Elizabeth Malya.

Shahidi wa Kwanza Given Nyanginywa, ameiambia Mahakama kwamba mnamo tarehe 21 March, Mwalimu Focus Mbilinyi, alitoa Hesabu 10 na baadae alitoa adhabu kwa wanafunzi wote waliokosa na miongoni mwa walioadhibiwa siku hiyo ni pamoja na Hosea Manga, ambaye alipigwa viboko 10 huku akiwa amening’inizwa dirishani kwa mtindo wa miguu juu kichwa chini, ambapo baada ya Hosea kupigwa viboko hivyo, alianguka chini na kushindwa kunyanyuka.

Kwa Upande wake shahidi namba 4 Daktari Silvery Mwesige, ameiambia Mahakama kwamba, Mtoto Hosea Manga walimpokea takribani wiki mbili, baada ya kupata matatizo akitokea Hospitali ya Ikonda.

Ameiambia Mahakama pia baada ya vipimo kufanyika walibaini kuwepo kwa mgandamizo chini ya uti wa mgongo, uliopelekea kupishana kwa pingili za uti wa mgongo na kusababisha mfumo wa damu kushindwa kupenya kwenda sehemu za chini za mwili wa mtoto huyo.

Licha ushahidi huo kuwasilishwa mahakamani hapo pamoja na kielelezo cha Ripoti ya Matibabu ya mtoto huyo, mawakili upande wa utetezi walipinga kielelezo hicho kwa madai ya kwamba, ripoti hiyo ya matibabu imewasilishwa na mtu ambaye hajaiandaa, pingamizi ambalo Mahakama imelitupilia mbali.

Kesi hiyo imesikilizwa kwa zaidi ya masaa sita,  ambapo baadaye Mahakama ilikikubali kielelezo hicho kilichowasilishwa na Daktari silvery Mwesige, kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kitengo cha mifupa MOI, na kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 2, 2019.

Kesi hiyo ni ya pili kufunguliwa kwa tukio lililomkuta mtoto Hosea Manga.

Kesi ya awali namba 83 ya mwaka 2017 ilifutwa kutokana na daktari aliyemtibu kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili kushindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi licha ya kuitwa mara nane.


Share:

Live : RAIS MAGUFULI AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA ISAKA - KAHAMA MUDA HUU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi mbalimbali waliomsubiri njiani Isaka 
Share:

Majibu Ya Rais Magufuli Baada Ya Mwananchi Kumtaka Aachie Fedha, Maisha Magumu

Rais Magufuli amewataka Watanzania kufanya kazi kwa bidii na waache kulalamika kwamba hawana fedha wakati hawajitumi.

Magufuli ametoa kauli hiyo leo Novemba 27, katika eneo la Shelui wilayani Igunga mkoani Tabora akiwa njiani kuelekea Shinyanga baada ya mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Abel Mbinga kumlalamikia maisha magumu.

“Rais unafanya kazi nzuri sana, lakini fedha hakuna mheshimiwa, watu wana hali mbaya, akina mama wananyang’anywa TV, friji kwa ajili ya mikopo midogomidogo, tunaomba uachie fedha, mtaani, hali ngumu, mengine yote hatuna shida na wewe, yakikamilika haya hata ukitawala milele,” amesema Abel.

Majibu ya Rais Magufli: “Usipofanya kazi hela zitaisha tu, ukitaka hela fanya kazi, wapo watu wanalima sasa hivi, baadaye watapata pesa, wewe umekaa kijiweni unataka pesa ikukute hapo? Labda ukaoe mwanamke mwenye pesa. Cha bure hakipo, hata mimi sina, kinachotakiwa ni kuchapa kazi, maandiko yanasema asiyetaka kazi na asile.

“Kalime viazi au matikiti, ukiyaweka hapa barabarani yataliwa tu, ukitaka vya bure hupati, nenda hata machimboni utapata kazi, unataka mkono wako uwe soft (laini)… pesa hakuna, mimi sikuja hapa kuleta hela, nimekuja kuwaambia Watanzania ukweli.

“Serikali inatafuta pesa kwa ajili ya kujenga hospitali, barabara, maji na miradi mingine ya maendeleo. Siwezi kutafuta pesa kwa ajili ya kukulisha wewe na mke wako, na ukikosa (pesa) na mke anakukimbia….. Hata Ulaya wanafanya kazi wasiwadanganye wapo wanaolala kwenye mashimo. Mimi nimekwenda Ulaya wapo wenye shida kuliko huku, bahati mbaya kwao kuna baridi. Ukitaka kutengeneza maisha yako chapa kazi,”


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger