Wednesday, 10 July 2019

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATANO


Barcelona inamnyatia beki wa Manchester United na raia wa Sweden Victor Lindelof, 24, huku ikiwa beki wa Ajax Matthijs de Ligt anatarajiwa kujiunga na Juventus. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Real Madrid watalazimika kulipa dau litakalovunja rekodi la £162m kumsaini kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, kutoka Manchester United. (Marca)

Mkufunzi wa klabu ya Sheffield Wednesday Steve Bruce ataunga mkono ofa yoyote kutoka Newcastle baada ya kupigiwa upatu kumrithi Rafael Benitez. (Chronicle)

Naibu mkufunzi wa klabu ya Manchester City Mikel Arteta na mkufunzi wa Nice Patrick Vieira wameonywa kuhusu kazi ya Newvcastle na Benitez. (Sun)

Everton ni miongoni mwa klabu zilizo na hamu ya kumsaini kiungo wa kati wa Manchester City na Uingereza Fabian Delph, 29. (Sky Sports)

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anataka mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 26, kutokubali uhamisho wa kuelekea Inter Milan na badala yake kusalia katika uwanja wa Old Trafford next season. (Sun)

Arsenal wamepatiwa ofa ya kumsaini mshambuliaji wa Real Madrid na raia wa Dominican Republic Mariano Diaz, 25, kwa dau la chini la £18m. (Star)

Everton ina hamu ya kumsaini mshambuliaji kinda mwenye umri wa miaka 19- wa Itali Moise Kean, ambaye klabu yake ya Juventus inataka dau la £31m na kifungu cha kumnunua tena katika makubaliano yoyote. (Mail)

Fenerbahce inataka kumsaini mchezaji wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 30 Mesut Ozil kwa mkopo kutoka Arsenal. (Sky Sports)

Manchester United imewasiliana na Southampton kutaka kujua kuhusu juwepo wa kiungo wa kati wa Gabon mwenye umri wa miaka 25 Mario Lemina. (Sky Sports)

Bournemouth wamempatia kandarasi mpya ya miaka mitano mshambuliaji wa Uingereza Callum Wilson huku West Ham, Chelsea na Everton zikihusishwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27(Sun)

Liverpool wana matumaini kwamba mshambuyliaji wa Ubelgiji Divock Origi, 24, atatia saini ya kandarasi mpya Anfield. (ESPN)

Crystal Palace inakaribia kumsaini kwa mkataba wa kudumu mshambuliaji wa Swansea na Ghana Jordan Ayew, 27, ambaye alihudumu msimu uliopita akiwa kwa mkopo. (Sky Sports)

Mpango a West Ham kumsaini mshambuliaji wa Celta Vigo Maxi Gomez umefutiliwa mbali baada ya klabu hiyo kufeli kukubaliana kuhusu mpango wa malipo wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 raia wa Uruguay.. (Sky Sports)

The Hammers wamepatiwa ofa ya mshambuliaji wa Marseille Mario Balotelli, 28, kwa uhamisho wa bila malipo kama mbadala wa Wilson na Gomez. (Mirror)

Barcelona wana hamu ya kumsaini mshambuliaji wa Romania Ianis Hagi, mwanawe mchezaji wa zamani wa Barcelona Georghe Hagi, kutoka klabu ya Viitorul Constanta na kumtoa kwa mkopo kwa klabu ya Real Valladolid. (AS - in Spanish)

CHANZO.BBC SWAHILI
Share:

Katibu Mkuu Jumuiya Ya Madola Afanya Mazungumzo Na Prof. Kabudi – London,uingereza

Jumuiya ya Madola imeonesha kuridhishwa na namna Tanzania inavyotekeleza mageuzi ya kiuchumi,uwajibikaji na uawala bora kwa wananchi wake jambo ambalo jumuiya hiyo inalihimiza na kulisimamia kwa Nchi wanachama wake.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Bi Patricia Scotland wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi za sekretarieti ya jumuiya hiyo zilizopo London Nchini Uingereza.

Katika mazungumzo hayo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Bi Patricia Scotland ameeleza kuridhishwa na maelezo yaliyotolewa na Prof. Palamagamba John Kabudi kuhusu utekelezaji wa masuala ya demokrasia,utawala bora na utawala wa sheria pamoja na Haki za binadamu nchini Tanzania na kwamba Jumuiya hiyo inatambua  juhudi hizo na inaunga mkono hatua hiyo.

Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa mbali na kuhimiza utekelezaji wa utawala bora,haki za binadamu na utawala wa sheria pia Jumuiya ya Madola imelenga kukuza na kuwezesha biashara miongoni mwa nchi wanachama ikiwa ni pamoja na fursa zilizopo kupitia shirika la biashara la kimataifa (WTO) na mashirikiano ya biashara ya kikanda.

Amesema ni jukumu la nchi za Jumuiya ya Madola kuhakikisha uwepo wa amani na utulivu katika jumuiya hiyo ili kuiwezesha kupiga hatua za haraka za kimaendeleo na kuifanya  Jumuiya nzima kuendelea bila ya kuacha nchi nyingine nyuma kutokana na uwepo wa migogoro ama machafuko ya wenyewe kwa wenyewe miongoni mwa wanachama wa Jumuiya. Katika hili ameisifia Tanzania kwa kuwa na Amani na utulivu muda wote na pia kushiriki katika juhudi za kutatua migogoro kwa nchi zingine wanachama na wasio wanachama wa Jumuiya.

Kuhusu suala la mabadiliko ya tabia nchi,Katibu Mkuu huyo wa jumuia ya madola amesisitiza umuhimu wa ushirikiano miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ili kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi. Ameeleza kuwa Jumuiya hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania katika program mbalimbali zinazolenga kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi na masuala ya mazingira kwa ujumla.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. palamagamba John Kabudi amemhakikishia Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola kuwa Tanzania inaipa umuhimu mkubwa jumuiya hiyo na itaendelea kushirikiana nayo katika masuala ya ukuzaji wa uchumi, utawala bora hususani wakati huu ambapo Tanzania inafanya mageuzi ya kiuchumi katika kuelekea kuwa nchi ya uchumi wa kati.

Ameipongeza  jumuiya ya madola  kwa mpango maalum inayoandaa kwa ajili ya kukuza na kuongeza  biashara baina ya Tanzania na nchi nyingine wanachama wa jumuiya hiyo kwa ujumla jambo ambalo litafungua fursa biashara na masoko kwa bidhaa na mazao ya Tanzania. Amemuahidi Katibu Mkuu huyo kuwa Tanzania itashiriki ipasavyo katika mpango huo.

Katika mazungumzo hayo,  Waziri Kabudi pia amekubaliana na Bi Scotland kuangalia namna ya kuwasaidia vijana kuongeza ubunifu ili waweze kujiajiri na kuimarisha uchumi ili kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana huku akimpongeza Katibu Mkuu huyo kwa mageuzi makubwa anayoyafanya ndani ya jumuiya hiyo ili iweze kuwahudumia wanachama wake kwa ufanisi zaidi.

Profesa Palamagamba John Kabudi yuko London Nchini Uingereza kwa ziara ya siku nne kuhudhuria mkutano wa Mawaziri wa mambo ya Nje wa Jumuiya ya madola pamoja na mkutano wa Kimataifa kuhusu uhuru wa vyombo vya habari.


Share:

MTANDAO WA 4G WA TIGO KUWANUFAISHA WAKAZI WA KIBAIGWA-DODOMA


Mkurugenzi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Kanda ya Kaskazini, Aidan Komba (wa tatu kutoka kulia), akishirikiana na Diwani wa Kata ya Kibaigwa, Richard Kapinye, kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mnara wa mtandao wa 4G uliozindulliwa jana katika Mji wa Kibaigwa Wilaya ya Kongwa, Mkoani Dodoma.
Diwani wa Kata ya Kibaigwa Wilaya ya Kongwa, Mkoani Dodoma, Richard Kapinye akizungumza wakati wa uzinduzi wa rasmi wa mnara wa 4G wa kampuni ya Tigo katika eneo hilo.
Baadhi ya wakazi wa Mji wa Kibaigwa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma, walishiriki katika hafla ya uzinduzi wa mnara wa huduma ya 4G ya kampuni ya mawasiliano ya Tigo.

---
Katika jitihada zake za kuboresha mawasiliano na kurahisisha maisha ya watanzania kupitia teknolojia ya kidigitali, kampuni ya mawasiliano ya Tigo, imezindua mnara wa mawasiliano wa 4G katika mji wa Kibaigwa mkoani Dodoma.

Akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliohudhuriwa na wakazi wa mji huo, Mkurugenzi wa Tigo kanda ya kaskazini, Aidan Komba, alisema uboreshaji wa mtandao kutoka 3G kwenda 4G unatarajiwa kufungua fursa mpya za kibiashara ambazo zitakuza maendeleo ya kiuchumi katika eneo hilo.

“Kwa kuzingatia kwamba Kibaigwa ina shughuli nyingi muhimu za kiuchumi hususani za kilimo na ufugaji na pia ni kiunganishi muhimu na maeneo mengine ya nchi, sasa ni wakati wa wakazi wa Kibaigwa na vitongoji jirani kutumia Intaneti yenye kasi zaidi ili kuendeleza biashara na shughuli mbalimbali za kiuchumi,” alisema Komba.

Uzinduzi huu unaenda sambamba na ofa maalum kwa ajili ya wateja watakaobadili laini zao kwenda mtandao wa 4G. Wateja hawa watazawadiwa kifurushi cha 4GB cha Intaneti ya bure itakayotumika ndani ya siku 7.

Vilevile, wateja watakaonunua kifurushi chochote cha intaneti kwenye mitandao uliyoboreshwa kutoka 2G kwenda 3G watazawadiwa MB100 kila wanaponunua kifurushi.

Pia kufuatia uzinduzi huu, wateja sasa wataweza kunufaika na huduma mbalimbali za kibunifu kutoka Tigo kama vile “Saizi Yako” ambayo inawapatia wateja ofa mbalimbali za SMS, Intaneti na kupiga simu kulingana na mahitaji na matumizi ya mteja. Kwa mfano mteja anayetumia dakika nyingi zaidi kuliko Intaneti na SMS atapata kifurushi cha dakika za muda wa maongezi. Mteja anayetumia zaidi Intaneti kuliko dakika za maongezi na SMS atapata kifurushi cha Intaneti kinachoendana na matumizi yake.

Tigo inaendelea kuwekeza kwenye teknolojia ya kisasa hususani 4G+ ili kukidhi mahitaji makubwa ya data na Intaneti yenye kasi kutokana na ongezeko la matumizi ya simu janja za bei nafuu.
Share:

Waziri Mbarawa Afungua Mkutano Wa Bodi Za Maji Za Mabonde




Share:

Serikali Yapokea Gawio La Shilingi Bilioni 1 kutoka Benki ya Posta Tanzania (TPB)

Na Saidina Msangi na Farida Ramadhani, WFM, Dodoma
Serikali imepokea gawio la Shilingi Bilioni 1 kutoka Benki ya Posta Tanzania (TPB) linalotokana na faida ya uwekezaji wake wa asilimia 83 ya hisa  katika Benki hiyo katika mwaka wa fedha 2018/19.

Hafla ya makabidhiano ya Hundi kifani ya gawio hilo imefanyika jijini Dodoma, kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) ambaye alipokea kwa niaba ya Serikali, na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo Dkt. Edmund Mndolwa.

Akizungumza katika hafla hiyo Dkt. Mpango aliipongeza Benki hiyo kwa kutoa gawio kwa Serikali, na kuahidi kuwa fedha hizo zitatumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo nchini.

“Utoaji huu wa gawio ni kiashiria tosha kwa Serikali kuwa Benki inazidi kukua na kuwapa moyo watanzania na wawekezaji kuwa TPB inatoa huduma bora katika jamii”, alisema Dkt. Mpango.

Aliitaka Benki hiyo kuongeza wigo wa utoaji huduma ili kuwafikia wananchi hususani waishio vijijini pamoja na kutoa elimu kwa wananchi hao kuhusu umuhimu wa  kuweka akiba, kukopa sambamba na kurejesha mikopo kwa wakati.

“Riba katika benki zetu bado ni kubwa taasisi za fedha zione namna ya kuzipunguza sambamba na kutoa mikopo kwa kuzingatia kanzidata ya wakopaji ili kuepuka mikopo chechefu.”, alisisitiza Dkt. Mpango.

Aidha, Dkt. Mpango ameiagiza Benki hiyo kuendelea kuwapa wanawake  kipaumbele katika upatikanaji wa huduma za fedha na mikopo ili waweze kuendesha shughuli za maendeleo.

Pia Dkt. Mpango aliiagiza  TPB kusimamia uadilifu kwa watumishi wake na kuwa makini na kutoa taarifa za  miamala yenye mashaka ili kuzuia utakasishaji wa fedha haramu.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPB Dkt. Edmund Mndolwa alisema kuwa gawio hilo ni sehemu ya faida ya Sh. Bilioni 17.2 kabla ya kodi ambayo Benki yake imeipata katika mwaka wa fedha 2018/19. Pia ameeleza kuwa Benki hiyo itaendelea kutoa huduma bora ili kukidhi mahitaji ya wanahisa wake na wananchi kwa ujumla.

Aidha, Dkt. Mndolwa aliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa utendaji mzuri ambao umeiwezesha Benki hiyo kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi na kuahidi kuendelea kushirikiana nayo ili kukuza uchumi wa nchi.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano 10 July





















Share:

Tuesday, 9 July 2019

Picha : RAIS MAGUFULI AZINDUA HIFADHI YA TAIFA YA BURIGI CHATO MKOANI GEITA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla pamoja na viongozi wengine wakivuta utepe kuashiria uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi (Burigi -Chato National Park) ilioyopo Chato mkoani Geita. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali, Wakuu wa mikoa, Viongozi wa Vyama vya Siasa, Dini pamoja na Mabalozi mara baada ya kuzindua Hifadhi ya Taifa ya Burigi (Burigi -Chato National Park) ilioyopo Chato mkoani Geita. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Chato kabla ya kuzindua Hifadhi ya Taifa ya Burigi (Burigi -Chato National Park) ilioyopo Chato mkoani Geita. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu mara baada ya kumkabidhi Hundi ya Shilingi milioni kumi , kama shukrani katika mchango wake alioutoa katika utunzaji wa wa hifadhi mbalimbali ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Burigi (Burigi -Chato National Park) ilioyopo Chato mkoani Geita. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wafanyakazi wa TANAPA wakati akielekea kwenda kuzindua Hifadhi ya Taifa ya Burigi (Burigi -Chato National Park) ilioyopo Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka mara baada ya kuzindua Hifadhi ya Taifa ya Burigi (Burigi -Chato National Park) ilioyopo Chato mkoani Geita.
Wakuu wa Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara na Simiyu wakijadiliana jambo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi (Burigi -Chato National Park) ilioyopo Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama wakati Wimbo wa Taifa ukipigwa kabla ya kuanza kwa sherehe za uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi (Burigi -Chato National Park) ilioyopo Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Kikosi cha Jeshi Usu la kukabiliana na vitendo vya Ujangili pamoja na kulinda hifadhi za taifa kabla ya kuanza kwa sherehe za uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi (Burigi -Chato National Park) ilioyopo Chato mkoani Geita.
Kikosi cha Jeshi Usu cha kukabiliana na Vitendo vya Ujangili pamoja na kulinda hifadhi za Taifa kikipita mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya ukaguzi katika sherehe hizo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Tuzo ya Hifadhi bora ya Serengeti ambayo imekuwa ya kwanza katika Bara la Afrika kwa mwaka 2019 kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia sanamu ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yenye ujumbe maalum kuhusu umuhimu wa utunzaji wa mazingira ya wanyama pori.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla mara baada ya kumkabidhi Sanamu hiyo ya Baba wa Taifa. Rais Dkt. Magufuli ametoa maelekezo kuwa Sanamu hiyo aliyokabidhhiwa ijengewe eneo zuri katika hifadhi hiyo ya Burigi Chato ili watalii wakija waweze kumjua zaidi Muasisi wa Taifa letu Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. PICHA NA IKULU
Share:

Naibu Spika Ataka Misingi Ya Utafiti Kufuatwa Katika Uchapishaji Na Utangazaji Wa Taarifa

NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amesema misingi ya utafiti ni jambo muhimu na la msingi litakalopaswa kuzingatiwa katika uchapishaji na  utangazaji wa taarifa mbalimbali ili kuweza kulinda misingi ya amani iliyopo nchini.

Akizungumza leo Jumanne (Julai 9, 2019) Jijini Dar es Salaam katika Kongamano maalum la siku ya Amani lililoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF), Dkt. Tulia alisema uchapishaji na utangazaji wa taarifa yoyote haina budi kuwa na tija katika taifa.

Dkt. Tulia alisema katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na utamaduni uliozoeleka wa kutangaza na kuchapisha taarifa mbalimbali katika jamii kupitia vyombo vya habari pasipo na kuzingatiwa kwa misingi ya utafiti hatua inayoweza kuleta migongano isiyo na tija kwa taifa.

“Serikali ya Awamu ya Tano tunaona inatekeleza miradi mikubwa ya maendeleo, ikiwemo mradi wa umeme katika Mto Rufiji, sni wajibu wetu kulinda misingi ya amani iliyopo ili tuone matunda ya miradi hii katika nchi yetu” alisema Tulia.

Aidha Dkt. Tulia alisema ni wajibu wa misingi ya utafiti ikazingtiwa katika taaluma mbalimbali ikiwemo ya uandishi wa habari kwani wapo baadhi ya watu wanaofikiri kuwa wanaweza kuandika na kutangaza habari pasipo na kusomea taaluma hiyo, jambo ambalo si la kweli kwa kuwa uandishi wa habari ni taaluma nyeti na muhimu kama zilivyo taaluma nyingine.

Aliongeza kuwa ni wajibu wa Watanzania wote kusoma vitabu mbalimbali vilivyoandikwa na waasisi wa taifa vikiwemo vitabu vya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambavyo vimekuwa na wingi wa maarifa na  maelekezo yanayopaswa kuzingatiwa ili kuweza kujenga taifa lenye umoja, upendo na mshikamano.

Naye Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano Zanzibar, Imane Duwe alisema mfumo wa soko huria nchini yameleta mabadiliko makubwa katika tansia ya habari na mawasiliano ikiwemo matumizi ya mitandao ya kijamii, ambayo imekuwa imeleta hamasa kubwa kwa makundi mbalimbali ya kijamii ikiwemo vijana.

“Hapo awali mwandishi wa habari alipokuwa akitumwa kazi na mhariri wake ni lazima arudi na atoe taarifa kwa mkuu wake pamoja na habari au taarifa hiyo kuweza kufanyiwa uhariri kabla ya kuchapishwa na kutangazwa lakini kwa sasa hali ni tofauti kidogo, kwani tukio lolote linaweza kutumwa wakati huo huo kupitia vyombo vya kisasa zaidi vya mawasiliano” alisema.

Aliongeza kuwa vyombo vya habari vya zamani ikiwemo Magazeti, Redio na Televisheni kwa sasa navyo vimeingia katika ushindani mkubwa wa soko kwani kwa upande wao pia wameanzisha mitandao mbalimbali ya kijamii ili kuweza kuwa na njia za kisasa zaidi za mawasiliano.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku alisema ni wajibu wa Viongozi na Watanzania wajenge utamaduni wa kuheshimu tunu na misingi mikuu ya amani nchini ikiwemo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, misingi ya Azimio la Arusha ambayo iliasisiwa na Hayati Baba wa Taifa  Mwalimu Julius Nyerere.

Aidha aliongeza kuwa ili kuweza kujenga Taifa lenye misingi bora ya amani ni wajibu wa Serikali kupitia Viongozi kuwa na  matumizi na usimamizi bora wa rasilimali za taifa na kuhakikisha zinawanufaisha  wananchi wote pamoja na kuweka misingi imara katika ulinzi rasilimali hizo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Amani Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum alisema Tanzania inaweza kufikia na kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya viwanda iwapo Viongozi wataweka mkazo katika usimamizi wa rasilimali watu yenye kutambua umuhimu wa kulinda amani, weledi, uzalendo na kujiamini.

“Moja ya Nguzo muhimu katika kufikia uchumi wa viwanda ni mfanyakazi, hivyo ni wajibu kila mwenye dhamana hiyo kutimiza wajibu wake huku akiogopa kufanya vitendo vya ufisadi kwani hata katika vitabu takatifu vimezungumzia ufisadi ni jambo baya sana”  alisema Sheikh Salum.

MWISHO


Share:

Benki Ya Maendeleo Ya Afrika Kuipandisha Daraja Tanzania

Na Saidina Msangi na Josephine Majura, WFM, Dodoma
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) inatarajia kuipandisha daraja Tanzania kutoka katika hadhi ya kunufaika na Mfuko wa Maendeleo wa Benki (ADF) hadi kuwa na hadhi itakayoiwezesha Tanzania kuweza kupata rasilimali fedha zaidi kupitia dirisha la African Development Bank (ADB) la Benki ya Maendeleo ya Afrika.

Endapo Tanzania itafanikiwa kupandishwa hadhi, nchi itaweza kunufaika na ongezeko la fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika kutoka Dola za Marekani milioni 350 kwa mwaka hadi Dola za Marekani milioni 812 kwa mwaka.

Hayo yamesemwa Jijini Dodoma na Mwakilishi Mkazi wa Benki hiyo Dr. Alex Mubiru alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha na Mipango-Treasury Square.

Katika mazungumzo hayo, Dr. Alex ameeleza kuwa hatua hiyo ya kupandishwa hadhi ama kupandishwa daraja inatokana na uchumi wa nchi kufanya vizuri hususani katika maeneo ya kasi ya ukuaji wa uchumi na kuwa na deni himilivu.

“Hatua hiyo itaiwezesha Tanzania kupata fedha zaidi kutoka katika Benki hiyo na kuwezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo na vipaumble kwa Serikali” Alisisitiza Bw. Mubiru.

Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Bw. Alex Mubiru, amesema kuwa benki hiyo inajivunia kufanya kazi na Tanzania ambayo ni miongoni mwa nchi Waasisi wa Benki hiyo.

Katika mazungumzo yao, Dkt. Mpango ameeleza kuwa Serikali inajivunia kufanya kazi pamoja na Benki ya AfDB kwa kuwa benki hiyo imekuwa na masharti rafiki katika upatikanaji wa mikopo.

Dkt. Mpango amesema kuwa Benki hiyo ina mtazamo chanya katika maendeleo ya watu na kuwa dira katika mipango ya maendeleo na kuahidi kushirikiana nao vyema katika kukuza uchumi wa nchi.

Aidha, Waziri Mpango ameipongeza benki hiyo kwa kukubali kutekeleza miradi ya Ujenzi wa Barabara ya Mzunguko Dodoma (km110.2) kwa kiwango cha lami pamoja na ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Dodoma (Msalato) na kubainisha kuwa uamuzi huo ni mzuri kwani licha ya Dodoma kuwa ni Makao Makuu ya nchi lakini pia miundombinu hii itaunganisha na kuchochea ukuaji wa uchumi na biashara katika mikoa mingi nchini pamoja na nchi jirani.


MWISHO.


Share:

Serikali kujenga uwanja mkubwa wa mpira Chato

Serikali imetangaza kujenga uwanja mkubwa wa mpira wilayani Chato, mkoani Geita ili kukuza sekta ya michezo nchini na kuvutia watalii na wawekezaji. 

Uwanja huo unatarajiwa kuwa wa pili kwa ukubwa baada ya wa Benjamin Mkapa ulipo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nishati Medard Kalemani amesema hayo wakati akihutubia sherehe za uzinduzi wa Hifadhi ya taifa ya Burigi-Chato na kueleza kwamba uwanja huo utaitwa Chato Stadium na ujenzi wake unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

"Hivi karibuni tunajenga Uwanja wa mipra Chato Stadium ambao utatumika sana katika kuhamasisha Wawekezaji na hasa Watalii wanaotoka nje ya nchi yetu" amesema Waziri Medard Kalemani.


Share:

VIJANA WAUANA KWA MAPENZI

Kijana Fadhili Abdallah Mkunguja {23} mkazi wa Kijiji cha Ruchemi, Kata na Tarafa ya Milola, Mkoa wa Lindi, amefariki dunia baada ya kushambuliwa kwa kukatwa shingoni na kitu chenye ncha kali na mwenzake aitwae Issa Khalifa Mtumwa (20) katika ugomvi uliotokana na wivu wa kimapenzi.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, wameeleza kuwa mauaji hayo yamefanyika wakati wananchi kijijini hapo wakiwa katika sherehe za ngoma ya unyago, ambapo wamesema marehemu alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mchumba wa Issa Khalifa, aitwae Hawa Hamadi {15} na kufanikiwa kupata nae Mtoto mmoja.

"Issa na huyo Hawa ni mtu na mchumba wake, wanaishi nyumba moja kupika na kupakua na wamefanikiwa kupata mtoto wao mmoja", ameeleza mmoja wa mashuhuda ambao hawakutaka jina lake kutajwa.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Ruchemi, Ally Mussa Mkalola, amekiri kuwepo kwa taarifa hizo na yeye akizipokea kutoka kwa wasamalia wema kuwa mchumba wa Hawa amekutwa akiwa na Fadhili Abdallah wakielekea kichakani.

Mkalola amesema taarifa hiyo ilimfanya Issa kupandwa na hasira na kuamua kuwafuatilia huku akiwa ameshika panga mkononi, kwa ajili ya kwenda kumshambulia Fadhili ambaye kwa wakati huo alidaiwa kuwa na mchumba wake.

"Kitendo cha kumkuta Fadhili ameketi na mchumba wake pale chini ya mti, hakuuliza alichokifanya ni kumshambulia shingoni yule mgoni wake, huku yule msichana akitimua mbio kuelekea nyumbani kwao", amesema Mkalola.

Kamanda wa Polisi mkoani Lindi, ACP Prodansiana Protas alipoulizwa kuhusiana na mauaji hayo, amethibitisha kutokea na kueleza kuwa wanaendelea kumtafuta mtuhumiwa Issa Khalifa, ili sheria ichukue mkondo wake.
Chanzo - EATV
Share:

AUA MTU KWA KUSIKILIZA MUZIKI


Kushoto ni marehemu na kulia ni mtuhumiwa wa kesi ya mauaji

Michael Adams, Mkazi wa nchini Marekani anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kesi ya mauaji ya kijana mwenye umri wa miaka 17, kwa kumpiga na kumkaba hadi kufariki kwa sababu ya kusikiliza muziki.

Polisi wamesema tukio hilo limetokea katika eneo la Circle K , Peoria ave lililopo nchini Marekani, na mtuhumiwa mwenyewe Michael Adams amekiri kufanya tukio hilo na amewaambia maofisa wa polisi sababu ni marehemu alikua anacheza na kusikiliza muziki wa rap.

“Kijana huyo alikua anasikiliza muziki wa rap, na aina ya muziki huo unamfanya yeye kutokuwa salama na ameshambulia watu wengi ambao wanasikiliza muziki huo”, amesema mtuhumiwa huyo.

Aidha mwanasheria wa mtuhumiwa huyo amesema amemtetea mteja wake kuwa alikua anasumbuliwa na ugonjwa wa kiakili na aliachiwa kutoka jela siku 10 zilizopita kabla kufanya tukio hilo.

“Walimuachia kurudi mtaani bila ya kumpima afya yake, tiba na hata kumuwekea ulinzi. Huko ni kushindwa kwa idara hiyo na inatakiwa kufanyiwa marekebisho”.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger