Sunday, 7 July 2019

Rais Magufuli ampa Rais Kenyatta tausi wanne

Rais Magufuli amemzawadia Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ndege aina ya tausi kama kumbukumbu ya uhusiano, urafiki na ujirani mwema baina ya nchi hizo mbili.

Magufuli ametoa zawadi hiyo  Jumamosi Julai 6, 2019 wilayani Chato mkoani Geita na kumpatia Kenyatta aliyekuwa nchini Tanzania kwa ziara binafsi ya siku mbili.

“Nimeguswa sijawahi kugawa tausi kwenye nchi yoyote kwa sababu wana historia ya nchi yetu. Kwa  heshima kubwa na mahusiano  yaliyopo kati ya Tanzania na Kenya, nimekubali na hili nataka kulisema wazi.

“Najua watu wataandika lakini hili limenigusa kutoka moyoni, nitatoa tausi wanne watapelekwa Kenya kwa Kenyatta,” alisema Magufuli huku akitabasamu.



Share:

Serikali Yaikabidhi Mwauwasa Ujenzi Wa Mradi Wa Maji Kwimba

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amekabidhi ujenzi wa mradi wa maji wa Shilima Wilayani Kwimba kwa Mamlaka ya Maji Mwanza (MWAUWASA) baada ya Mkandarasi Kampuni ya Palemon Construction Ltd ya Mwanza kushindwa kukamilisha kwa wakati.

Makabidhiano hayo yalifanyika hivi karibuni katika Kijiji cha Shilima na kushuhudiwa na watendaji mbalimbali wa Serikali na mamia ya wananchi wa Shilima na maeneo ya vijiji vya jirani.

Akizungumza kabla ya kukabidhi mradi, Waziri Mbarawa alieleza kwamba ujenzi wake ulianza tangu mwaka 2013 na kwamba ulipaswa kukamilika ndani ya miezi sita lakini hadi sasa mradi huo haujakamilika.

Alisema Serikali iliamua kusitisha mkataba na Mkandarasi ambaye alishindwa kutekeleza ujenzi wa mradi kama ilivyo kwenye makubaliano.

Mara baada ya kuukabidhi mradi huo, Profesa Mbarawa aliiagiza MWAUWASA kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha ujenzi unakamilika ndani ya Siku 60 ili kuwaondolea mateso ya muda mrefu wanachi wa maeneo hayo hasa ikizingatiwa kwamba mradi ulipaswa kukamilika tangu mwaka 2013.

“Tunataka wataalam hawa wafanye kazi usiku na mchana na baada ya miezi miwili wananchi wapate maji safi na salama, uwezo tunao, tunaweza kumaliza tatizo la maji hapa kwa muda mfupi sana,” alisema Profesa Mbarawa.

Aliongeza kuwa kuna miradi ipatayo 88 kote nchini ambayo ujenzi wake ulianza kati ya Mwaka 2010 hadi 2015 ambayo ilipaswa kuwa imekwisha kamilika lakini hadi hivi sasa bado inasuasua na huku akiutolea mfano mradi huo wa Shilima.

Alibainisha kwamba Serikali kupitia Wizara ya Maji imeamua kuwa na utaratibu mpya wa kuzikabidhi Mamlaka za Maji miradi ambayo ujenzi wake una changamoto inayosababisha isikamilike kwa wakati.

“Tumeamua kubadilisha utendaji wa Sekta ya Maji, kila mahala tatizo ni maji, hili halikubaliki, tumejipanga na tunadhamira ya dhati kuhakikisha kero hii inakuwa historia kote nchini,” alisema Waziri Mbarawa.

Kuhusu utaratibu huo mpya, Profesa Mbarawa alibainisha kuwa ni wa nchi nzima na kwamba wakandarasi wanaoshindwa kutekeleza miradi waliyokabidhiwa kwa wakati hawatovumiliwa na watanyanganywa na itakabidhiwa kwa Mamlaka za maji kwenye maeneo husika.

“Tumeamua miradi yote yenye changamoto tutaisimamia wenyewe na tutahakikisha inafanya kazi. Wananchi wamechoka kuendelea kuisubiri miradi hii ikamilke, fedha nyingi zinapotea, Serikali haitokubaliana na Mkandarasi anaechelewesha ujenzi wa mradi tayari tumefanya hivi Rungwe na sasa tumefanya hapa Shilima,” alisema Profesa Mbarawa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga alisema wamepokea agizo hilo la kutekeleza mradi huo ambao umesuasua kwa kipindi kirefu na kwamba wataukamilisha kwa wakati kama ilivyoagizwa.

“Tunaahidi hadi kufikia Septemba 3, 2019 tutakuwa tumeukamilisha mradi kwani itakuwa tayari ni Siku 60 na wananchi wataanza kupata majisafi na salama kutoka Ziwa Victoria,” alisema Mhandisi Sanga.

Aidha, kwa mujibu wa Mhandisi wa Maji, Wakala wa Maji Vijijini Wilaya ya Kwimba, Mhandisi Boaz Pius ni kwamba mradi huo utakapokamilika utahudumia wakazi 16,675 kutoka vijiji vinne ambavyo ni Shilima chenye wakazi 7,526, Mhande chenye wakazi 1,967, Kasang’wa wakazi 2,730 na Kijiji cha Izizimba “A” chenye wakazi wapatao 4,452.

Mhandisi Boas aliongeza kwamba kukamilika kwa mradi huo pia kutaweza kuhudumia vijiji vya Sangu, Gurumwa, Mwalubungwe na Kikubiji, ambapo bomba kuu linapita.


Share:

FILAMU YA 'MIMI SIYO MWEHU' KUTIKISA ZAIDI YA 'LAANA YA MKE'


Unaikumbuka ile Filamu ya Laana ya Mke iliyoigizwa na wasanii kutoka mkoa wa Shinyanga ambayo hivi karibuni ilifanikiwa kushinda Tuzo ya Heshima Filamu Bora yenye maudhui ya kitaifa Kanda ya Ziwa???.

Sasa ni hivi?!! Baada ya Filamu ya Laana ya Mke kutikisa....Wasanii wa Filamu mkoa wa Shinyanga wanakuletea filamu nyingine kali imepewa jina la " MIMI SIYO MWEHU".... Ndiyo!!  Mimi siyo Mwehu ni bonge la filamu yenye tungo zenye manufaa katika jamii zenye kuelimisha, kuonya,kuburudisha zilizojaa mafunzo ya uhalisia wa maisha halisi katika jamii za Kiafrika.

Mwandaaji wa Filamu hiyo, Ibrahim Juma Songoro maarufu 'Songoro Gadafi' ambaye ni Mwenyekiti wa Bongo Movie Shinyanga ameiambia Malunde1 blog kuwa filamu ya 'Mimi Siyo Mwehu' inalenga kuelimisha jamii inayowachukulia watu wasio na kipato,waliochoka kimaisha, kiuchumi na kiafya mawazo yao au ushauri wao haustahili bali ni wendawazimu.

"Mimi Sio Mwehu ni filamu iliyosheheni Misemo ya hekima itakayomfanya mtazamaji asichoke kuitazama katika maisha yake, washiriki wakuu kwenye filamu hii iliyoongozwa na Director Dave Skerah ni Juma Ibrahim Songoro, Goodness Mndeme na Fadhili Mungi".

"Naapa kurudisha heshima ya tasnia ya Filamu Tanzania kwa kuwaletea Filamu zenye tungo zenye manufaa katika jamii kwa lengo la kuelimisha, kuonya na kuburudisha kwa kuangalia uhalisia wa maisha ya jamii zetu za Kiafrika",amesema Songoro.

Amesema Filamu ya 'Mimi Siyo Mwehu' itazinduliwa hivi karibuni na kuwaomba mashabiki wa filamu kujiandaa kupokea Filmu hii yenye ubora wa hali ya juu.

Na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Songoro

Goodness 
Share:

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AWATAKA WANANCHI KUTUNZA VYANZO VYA MAJI,ARIDHISHWA NA UHIFADHI WA MAZINGIRA NA VYANZO VYA MAJI MUHEZA

MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Mkinga Mark Yona

 KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 Mzee Ally akivishwa skafu na vijana wa skauti mara baada ya kuwasili wilayani Muheza.
 MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati akiwa na viongozi mbalimbali mara baada ya mwenge kuwasili kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza Like Gugu na Mbunge wa Jimbo la Muheza( CCM) Balozi Adadi Rajabu kushoto ni  KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 Mzee Ally
 MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto akihamasisha kushiriki kuimba kwa pamoja nyingi mbalimbali za mwenge wakati wakiiusubiri
 MMOJA kati ya wakimbiza Mwenge Kitaifa akiweka mwenge mara baada ya kukimbizwa kwenye miradi mbalimbali
 Mwenge wa Uhuru 2019 ukikimbizwa wilayani Muheza
 MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kulia akiteta jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri Bakari Mhando
 KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 Mzee Ally katikati akionyeshwa namna ya utunzaji wa mazingira unavyoifanyika wakati alipotembelea na kukagua mradi wa shughuli za uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji Kijiji cha Shembekeza.
 KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 Mzee Ally kushoto akimkabidhi cheki ya Sh.Milioni moja Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbaramo Mussa Salimu ikiwa ni mchango uliotoka Halmashauri kuunga mkono ujenzi wa Hosteli kwenye shule ya Msingi Mbaramo kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalumu anayeshuhudia katikati ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo
 MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akiwakabidhi zawadi mbalimbali wakimbiza Mwenge wa Uhuru 2019

KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 Mzee Ally amewataka wananchi wanaoishi karibu na vyanzo vya maji wilayani Muheza mkoani Tanga kuhakikisha wanavitunza ili viweze kuwa endelevu.

Alitoa kauli hiyo mara baada ya Mwenge wa Uhuru kukagua mradi wa shughuli za uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji ikiwemo kukagua mabanda ya wadau wa mazingira na kupanda miti eneo maalumu lillotengwa Kijiji cha Shembekeza.

Akiwa kwenye eneo hilo kiongozi huyo alionyeshwa kuridhishwa na namna mradi wa uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji ambao umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uharibifu wa vyanzo vya maji.

Alisema kwani Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kutekeleza miradi hiyo kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji hivyo ni muhimu kulindwa na kuendelezwa kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Kiongozi huyo alisema suala la upatikanaji wa maji limekubwa na changamoto nyingi ikiwemo matumizi mabaya ya fedha za serikali huku baadhi ya waka ndarasi wamekuwa wakichukua muda mrefu kukamilika miradi hiyo na hata wengine kukamilisha chini ya kiwango.

“Lakini pia niwaambie kwamba sio jambo jema kufanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji ikiwemo ukulima, ufugaji na kujenga karibu na vyanzo hivyo tushirikiane kuhakikiha tunatunza vyanzo vya maji ili vielendee kumudu kwqa vizazi vya sasa na vijazo”Alisema Kiongozi huyo.

Awali amkizungumza wakati akisoma taarifa ya miradi itakayozinduliwa na mwenge ikiwemo kukaguliwa Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo alisema kwamba miradi yenye thamani ya Bilioni 29.471.7 huku akieleza kwamba mwenge huo umekimbizwa kwenye miradi na shughuli mbalimbali.

Alisema wakati wa mkesha wa mwenge huo huduma mbalimbali zilitolewa ikiwemo upimaji vvu ambapo walipimwa watu 448 ambapo kati yao wanaume 307 na wanawake 141 na waliokutwa na maambukizi ni wanaume wawili na wanawake wawili

Wakati huo huo Mpiga picha wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Muka Sabuni amepongeza na viongozi wa mbio hizo kutokana na namna aliyoweza kutengeneza mabango yenye picha zao wakati ulipoongia wilayani Muheza.

Hatua ya mmoja ya wakimbiza Mwenge ni kushangazwa na ubinfu uliotumiwa na mpiga picha huyo kwa kuweka picha zao kwenye mabango yaliyokuwa yamebeba ujumbe wa mwenge wilayani humo.

Kutokana na hali hiyo mmoja wa wakimbiza Mwenge hao Kenon alitumia muda wa makabidhiano baina ya Muheza na Pangani ndipo aliposimama na kumtambulisha huku akionyeshwa kufurahishwa na utendaji wake na kuiwataka viongozi wa wilaya hiyo kuendelea kumtumia kwenye shughuli mbalimbali. 
Mwisho 
Share:

HALMASHAURI TARIME YAPATA HATI SAFI...BILIONI 1.5 ZAVUKA MWAKA BILA KUTUMIKA


Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima akizungumza kwenye kikao cha madiwani

Na Dinna Maningo,Tarime.
Zaidi ya shilingi Bilioni 1.5 zinadaiwa kuvuka mwaka pasipo kutumika katika Halmashauri ya wilaya ya Tarime jambo linalodaiwa kukwamisha uendeshaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Hayo yalielezwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Tarime ambaye pia ni Diwani kata ya Nyamwaga Misiwa Yomami kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Tarime cha kujadili Taarifa ya mpango kazi na majibu ya Menejimenti kuhusu hoja za ukaguzi zilizoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za Serikali kwa mwaka unaoishia Juni 30,2018.

Yomami alisema pamoja na Halmashauri hiyo kupata hati safi ,kuna fedha Bilioni 1.5 zimevuka mwaka bila kutumika kutokana na kucheleweshwa.

"Tunaomba Serikali itatue hii ni changamoto inayokwamisha utendaji pesa zote hizo zinavuka mwaka bila kutumika zingekuja kwa wakati zingesaidia kukamilisha masuala mbalimbali kwa wakati ,lakini pamoja na changamoto zinazojitokeza naipongeza Halmashauri kwa kupata hati safi",alisema Yomami.

Akisoma Taarifa ya mpango kazi kuhusu hoja za Ukaguzi Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Apoo Tindwa alitaja hati halmashauri ilizopata katika kipindi cha mwaka 2013-2018 ,ambapo mwaka 2013/2014 Halmashari ilipata Hati safi,2014/2015 Hati yenye shaka,2015/2016 Hati Safi,2016/2017 Hati safi na 2017/2018 Hati safi,na katika Miradi ya Maendeleo kwa kipindi cha miaka hiyo imepata Hati safi ikiwemo miradi ya TASAF,ASDP, na HBF.

Tindwa aliongeza kuwa katika kutekeleza mkakati kwa ajili ya kuzuia hoja, kuna changamoto ambazo Halmashauri inahitaji kuzitatua ili kufikia lengo la kuondoa hoja ikiwemo fedha za maendeleo na matumizi ya kawaida kutopokelewa kwa wakati kutoka hazina,tatizo la kukatika kwa mtandao wa mawasiliano na upungufu wa Watumishi katika Idara za Halmashauri.

Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima aliwataka Madiwani kushikamana ikiwa ni pamoja na kujadili,kuangalia mapungufu na kuzifanyia kazi hoja za CAG ili kusiwepo na hoja nyingi za ukaguzi.

January 2019 Halmashauri hiyo iliingia katika tuhuma nzito ambapo mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima akiongea na Madiwani aliihituhumu Halmashauri kwa matumizi mabaya ya fedha za miradi ya maendeleo ambazo ni mapato ya ndani Bilioni 9.5 kutoka Mgodi wa Dhahabu wa ACACIA uliopo Nyamongo tangu mwaka 2015-2018.

Malima aliunda Tume ya uchunguzi wa fedha hizo ikiongozwa na Katibu wake Mwita Chacha iliyoanza kazi Januari 28,2019 na kukamilisha uchunguzi Febuari 25,2019 na mwezi Aprili 2019 Tume hiyo mbele ya Madiwani na RC Malima ilieleza na kukiri uwepo wa ubadhilifu wa matumizi mabaya ya fedha ya Bilioni 15 kati ya hizo Bilioni 9.4 ni mapato ya Mgodi.

Kupitia tume hiyo aliiagiza Taasisi ya Kupambana na Rushwa Takukuru kumchungunza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Apoo Tindwa huku Watumishi wengine 4 wakisimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi.

Share:

Vijana wapewa elimu kuhusu kuanzisha biashara ili kujikwamua na uchumi

Na.Mwandishi Wetu-DSM
Vijana wapewa elimu kuhusu kuanzisha biashara ili kujikwamua na uchumi kwa  kuchangamkia fursa zilizoko kwenye maeneo yao na kujua umuhimu wa kodi katika biashara ili kuwezesha taifa kupata mapato na wao kupata faida. 

Akizungumza katika Semina ya Vijana iliyoandaliwa na Umoja wa Vijana Tanzania (TYVA), Afisa Elimu na Huduma kwa Walipa Kodi kutoka TRA, Isihaka Sharifu alisema kuwa Serikali imerekebisha baadhi ya Sheria za kodi hususani kwa vijana wanaofungua kampuni au biashara mpya. 

Sharifu alisema kuwa kwa sasa Sheria ya kodi imejikita kuwasaidia vijana wanaoanzisha kampuni na biashara mpya kwani imeweza kugusa msamaha wa kodi kwa miezi sita tofauti na awali ambapo biashara mpya zilikuwa zinalipiwa kodi baada ya miezi mitatu. 

“ Kwa sasa Sheria inasema ukiwa unafungua biashara yako au kampuni mpya kwa sasa unatakiwa kulipa kodi baada ya miezi sita, kwa hiyo hii itawasaidia vijana wengi ambao wanania ya kuanzisha biashara, nawasihi vijana wenzangu tumieni Fursa hiyo kujikwamua kiuchumi”, Alisema Sharifu. 

Katika Semina hiyo ambayo kauli mbiu yake ilikuwa ‘Nguvu ya Kodi’ Sharifu alipaeleza kuwa TRA inatekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano kuwakwamua vijana hasa wajasiriamali wadogo ambao wanafanya biashara zao kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini. 

Alisema kuwa kodi inayotozwa kwa wafanya biashara wenye mauzo kuanzia milioni 0 hadi 100 imegawanyika katika makundi manne ambayo ni mauzo kuanzia 0 mpaka milioni 4 ambao hawatozwi kodi, mauzo ya milioni 4 mpaka 7.5 wanatozwa 100,000, milioni 7 mpaka 11 wanatozwa  250,000 na milioni 11 mpaka 14 wanatozwa 450,000 tofauti na hapo zamani ambapo walikuwa wanatozwa 546,000, kwa hiyo vijana wanatakiwa kuchangamkia fursa hiyo. 

Kwa upande wake, Afisa Vijana kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Temeke, Anna Marika alisema kuwa vijana wanatakiwa kuwa wazalendo kwa kutimiza wajibu wao kwenye suala la kulipa kodi kama Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli anavyoagiza. 

“Nimefurahi kwa Semina hii kwani watoa mada wamekuja na Mada nzuri zinazoelimisha ulipaji Kodi, wito wangu kwa vijana ni kwamba wanatakiwa kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi kama Rais alivyoagiza kuchukua vitambulisho ili wasipate shida kwenye maeneo yao ya kufanyia Biashara”, Alisema Marika. 

Marika aliongeza kuwa kwa Wilaya ya Temeke wamejikita zaidi katika kuwasaidia vijana, wanawake na walemavu kujikwamua kimaisha kama Ofisi ya Rais –TAMISEMI ilivyoagiza kuwa asilimia 10 ya mapato ya halmashauri ijikite kwenye kuwasaidia vijana, wanawake na walemavu. 

Alisema Wilaya ya Temeke imetanga asilimia nne kwa vijana, asilimia  nne kwa wanawake na asilimia mbili kwa walemavu, huku wakilenga kuboresha utoaji wa huduma kwa kutoa vifaa vya kazi kwa vikundi mbalimbali kama vile pikipiki, Chelehani,vifaa vya mziki na magari ya kuzoa takataka na kusomba matofali. 

Alitolea mfano wa kikundi cha wanawake waliopewa chelehani 50 na wataanza kurejesha mikopo baada ya miaka miwili na wakimaliza mkopo vifaa vile vinakuwa mali ya kikundi. 

“Niombe sasa kwa wale vijana ambao mnaisha Temeke, haijarishi unatoka Wilaya gani hapa Dar es Salaam au mkoani, mkirudi kwenu kachangamkieni fursa hii ili kuwawezesha kujikimu kimaisha na kupata faida kubwa ya kuendesha uchumi wenu”, Alisistiza Marika.


Share:

Toa Mikunjo Usoni,Michirizi,Makovu, Kuza Nywele zako na Hawa Jamaa

Kessy_product_cosmetics:

            🍅🥒🍒👇

1- Kutoa Mvi Sugu Pia Zakuzala @130,000/

2-Kuza Nywele Na Kuzijaza Bila Kukatika@120,000/

3-Tengeneza Umbo Lako
4-Toa Mikunjo Uson Makonyanz(Ngozi Yakuzeeeka)90,000/

5-Toa Kitambi Na nyama Za pemben

6-Punguza Mwili Mzima @130,000/

7-Ongeza Unene Wa Mwili @100,000/

8-Towa Michirizi (Strech Mark)90,000/

9-Kutoa Alam, Chunusi,makovu Madoa@80,000/

10-Toa Ndevu Na Vinyweleo@100,000/

11-Ongeza Mguu Kam Bia@100,000/

12-Kama Umepoteza Hamu Yakula @100,000/

13-Towa Weusi Mapajani Mikononi@80,000/

14-Pata Mikanda Yakutowa Tumbo Kabisa *wakawaid@100,000/

*wenye Daw@150,000/

*waumeme@200,000/

15-Ngiri Ainazote@90,000/

16-Rudisha Nywele Kichwani(Kipara@15,000

17-Toa Harufu Sehem mbaya kwapani@100,000/

            🍍🍒🥬👇

Akikisha Unaongea Na Kessy Kwa Maelekezo

Tunapatikana Dar, K Koo,posta, Sinza

_+225_

0719955528

0756259180

0785371237

*Delivery  Popote Ulipo


Share:

Kigwangallah Ampa Makavu January Makamba...."Ni Dharau na Kujionesha tu"

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla ameonesha kutoridhishwa na kauli ya Waziri wa Mazingira, January Makamba akiieleza TANAPA kuwa hawawezi kuanza utaratibu wa kutumia magari maalumu ya umeme (Cable Cars), kwa ajili ya watalii wanaotembelea mlima Kilimanjaro.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Waziri Kigwangalla amehoji baadhi ya maswali kwenda kwenye mamlaka ya mazingira, akieleza kuwa watu hao wamekuwa wakishiriki zaidi kwenye makongamano na si uhalisia wa kulinda mazingira.

"Watu wa mazingira wanataka kuingilia kati mradi wa cable cars KILIMANJARO. Lengo letu ni kukuza utalii, kuongeza mapato na kuboresha experience ya watalii wetu nchini. Tusipokuwa wabunifu tunatukanwa kutokutumia vizuri vivutio vyetu, tukiamka wanakuja ‘speed governors’.

"Hivi kuna nchi ngapi zimeweka Cable Cars kwenye milima yake?, hizi haziharibu mazingira?, Cable inapita juu inaharibu mazingira gani?. Zaidi ya hekari 350,000 za misitu zinapotea kila mwaka nchini, ipi ni hatari kubwa?, watu wa mazingira wamechukua hatua gani zaidi ya makongamano tu?", amesema Kigwangalla.

Hivi karibuni wakati TANAPA ilieleza mpango wake wa kuja na namna mpya ya usafiri kwa watalii wanaotaka kwenda kutembelea mlima Kilimanjaro, Waziri wa Mazingira, January Makamba akasema suala hilo haliwezi kufanyika mpaka pale NEMC watakapo thibitisha.

"Inabidi watu wa Mazingira tupitishe na kutoa cheti kwanza kabla hawajaanza. Na tutafanya 'studies' ili kujua madhara kwa mazingira na uthabiti wa 'mitigation measures", alisema Makamba


Share:

Waziri Kamwelwe azindua treni ya Majaribio SGR

Na Grace Semfuko,MAELEZO.
Serikali imeanza mchakato wa ununuzi wa vichwa 22 vya treni, mabehewa 1,430 ya mizigo na Mabehewa 60 ya Abiria vitakavyotumika kwenye uendeshaji wa Reli ya kisasa ya SGR ambayo ujenzi wake unaendelea.

Yapi Merkez inajenga Reli ya SGR awamu ya kwanza kutoka Dar Es Salaam hadi Morogoro ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 56 na awamu ya pili kutoka Morogoro hadi Makutupora Mkoani Singida ikiwa imefikia asilimia 52 zote zikiwa na urefu wa zaidi ya kilomita 722 na zinajengwa kwa gharama ya fedha za ndani shilingi Trilioni 7.2.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe wakati akizindua Safari ya kwanza ya majaribio ya Treni ya Wahandisi kwenye eneo la Soga lililopo Kibaha Mkoani Pwani.

Injinia Kamwelwe alisema mpango wa sasa wa Serikali ni kuwa na Seti tano za Treni  za SGR zitakazokuwa na behewa nane za abiria, mpango ambao unalenga kuimarisha  sekta ya usafirishaji wa reli.

“Ndugu zangu Watanzania, leo hii tumezindua majaribio ya njia ya reli yetu, hii inamaana kwamba tupo katika mipango ya kuhakikisha reli inakamilika kwa wakati, tumetembea kilomita 20 za majaribiop, reli ni salama kabisa, haina kikwazo,sasa tumeanza mchakato wa kununua vichwa vya treni 22 na mabehewa yake 60 ya Abiria na 1,430 ya Mizigo” alisema Waziri Kamwelwe.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania TRC Masanja Kadogosa amesema zoezi la majaribio ya awali ya treni ya wahandisi ni hatua muhimu ya kuhakikisha reli hiyo inapitika bila kikwazo kwani inakagua na kuimarisha miundombinu ya reli hiyo.

Alisema zoezi hilo la awali limekuja kufuatia kukamilika kwa baadhi ya maeneo ya kupita treni kuanzia Soga Wilayani Kibaha Mkoani Pwani, kuelekea Morogoro na kuongeza kuwa treni rasmi kwa ajili ya kupita reli hiyo itawasili hivi karibuni.

Zoezi la majaribio ya uendeshaji wa Reli ya kihandisi ulishuhudiwa na Waziri Kamwelwe, Maafisa wa Shirika la Reli Tanzania TRC pamoja na Waandishi wa Habari ambao walitembea na treni hiyo kwa kilomita 20. 

Mwisho.


Share:

Halmashauri kuu CCM Njombe yatoa maagizo haya kwa serikali

Na Amiri kilagalila-Njombe
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Njombe imetoa maelekezo kwa mkuu wa mkoa wa Njombe na Mkuu wa Wilaya ya Njombe kukutana haraka iwekezanavyo na wadau wa usafirishaji wa abiria mkoani humo ili kutatua changamoto inayowakumba wananchi wanaosafiri kwa mabasi kushindwa kushushwa  katikati ya mji wa Njombe baada ya stendi kuu mpya kuanza kufanya kazi.

Akizungumzia baadhi maazimio ya kikao cha  halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Njombe iliyokutana siku chache zilizopita na kujadili utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015/2020 kwa mwaka wa fedha 2018/19, katibu wa siasa na uenezi wa CCM mkoa wa Njombe, Erasto Ngole amesema CCM imesikia kilio cha wananchi juu ya adha wanayoipata abiria wanaposhindwa kushushwa na mabasi ya abiria katikati ya mji na hivyo imeagiza lazima kuwepo na kituo cha mabasi katikati ya mji wa Njombe.

“Chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe tumempa maelekezo mkuu wa mkoa pamoja na mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa halmashauri ya mji waite mkutano mkubwa wa wadau wanaohusika na usafiri,ili waweze kuangalia namna bora ya kuondoa haya manung’uniko,na sisi tumetoa mapendekezo kati kati ya mji lazima kuwe na kituo cha kushusha na kupakia abiria,haiwezekani kabisa mwananchi akapitishwa mjini kusiwe na kituo hata kimoja”alisema Ngole

Katika hatua nyingine kuhusu swala la vitambulisho vya ujasiriamali amesema chama kimetoa maelekezo  kwa serikali ya mkoa wa Njombe kuzingatia utaratibu wa ugawaji wa vitamburisho hivyo.

“Imeonekana kwa sasa yameorodheshwa makundi mbalimbali na watu wanagawiwa vitambulisho ili viishe,mheshimiwa Rais alisema wanaotakiwa kuwa na vitambulisho ni wafanyabiashara wadogo wadogo wenye mauzo chini ya milioni nne kwa mwaka kwa hiyo ni lazima tuzingatie hilo na halmashauri kuu ya mkoa imekazia hilo”aliongeza Ngole

Aidha kuhusu ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Njombe kuelekea tarafa ya Lupembe hadi mpakani na mkoa wa Morogoro, Ngole amesema chama cha mapinduzi kimeitaka serikali kuanza ujenzi wa barabara hiyo mara moja kwa sababu wananchi wanaoishi maeno hayo wamekuwa wakipata adha kubwa ya usafiri kutokana na miundombinu ya barabara kuwa mibovu.

Kwa upande wake mwenyekiti wa jumuia ya umoja wa vijana mkoa wa Njombe (UVCCM) Nehemia Tweve ametoa wito kwa vijana kuona fulsa mbali mbali zilizopo katika mkoa huo ikiwemo utalii licha ya kilimo na ufugaji ambazo zimezoeleka na wengi




Share:

Misri Yatupwa Nje Afcon Kwa Kuchapwa Bao 1-0 Na Afrika Kusini

Mabingwa watetezi Cameroon na wenyeji Misri wameyaaga mashindano Jumamosi Juni 6 baada ya kutolewa kwenye siku ya pili ya hatua ya mtoano.

Cameroon na Misri ndio waliocheza fainali ya Kombe la Maifa ya Afrika (Afcon) miaka miwili iliyopita ambapo Cameroon ilitwaa ubingwa.

Hata hivyo timu hizo mbili zimeyaaga mashindano baada ya Cameroon kufungwa 3-2 dhidi ya Nigeria jijini Alexandria.

Misri wamepigwa mbele ya mashabiki elfu sabini jijini Cairo na Afrika Kusini kwa goli moja tu lililofungwa na Thembinkosi Lorch katika dakika ya 85.

Afrika Kusini ambao walifuzu katika raundi ya mtoano kama timu ya tatu kwenye kundi lao baada ya kushinda mchezo mmoja tu haikupigiwa upatu katika mechi ya hiyo dhidi ya Misri inayoongozwa na mshambuliaji wa Liverpool Mo Salah.

Umakini wa safu ya ulinzi wa Afrika Kusini  ndio imekuwa chachu ya ushindi baada ya kuhimili vishindo na mikiki ya safu ya ushambuliaji ya Misri ambayo iliibuka na ushindi kwenye mechi zote tatu za makundi.


Share:

Iran Yatishia Kuitandika Kwa Makombora Uingereza

Mjumbe wa baraza la wataalamu wa Iran, Ayetullah Muhammed Ali Musevi, amesema Iran itajibu mapigo kwa makombora kutokana na kitendo cha uongozi wa Gibratar ambayo ni sehemu ya Uingereza, kuikamata meli ya mafuta ya Iran.

Akiongea na shirika la habari la Fars Musevi ameionya Uingereza kutokana na kitendo cha meli ya mafuta ya Iran kukamatwa katika mlango bahari ya Gibrata.

Musevi alikumbushia jinsi Iran ilivyoidungua ndege isiyoendeshwa na rubani ya Marekani baada ya kukiuka na kuingia katika anga la Iran bila ruhusa, kisha akasema kwamba kamwe Iran haitakubali kuonewa na kuhusiana na suala la meli yao kushikiliwa watatoa majibu muafaka.

Musevi alisema anatangaza waziwazi Uingereza ni budi iogope kushushiwa makombora na Iran.

Baada ya Uongozi wa Gibrata ambayo ipo chini ya Uingereza kuikamata meli ya mafuta ya Iran iliyokuwa ikipeleka shehena Syria siku ya alhamisi, Iran ilielekeza vitisho vya kuipiga kwa makombora Uingereza.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili 7 July















Share:

Lugola Asema Polisi Wanaoshirikiana Na Mafisadi Kudhulumu Ardhi Ya Wananchi Maskini, Dawa Yao Imeiva

Na Felix Mwagara, Mwibara (MOHA)
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema baadhi ya polisi wasiokuwa waaminifu nchini wanaoshirikiana na mafisadi kudhulumu ardhi ya wananchi maskini, sasa dawa yao imeiva. 

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Haruzale, Kata ya Nyamihyolo, Jimbo la Mwibara, Bunda akiwa katika ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo jimboni mwake, Lugola amesema amepokea malalamiko mengi ya ardhi katika jimbo lake na sehemu mbalimbali nchini.

Amesema mafisadi wa ardhi hukimbilia kufungua kesi vituoni wakilazimisha kwa kutumia fedha ardhi iwe mali yao wakiwatumia polisi wasiokuwa waaminifu ili kufanikisha matwaka yao.

“Haiwezekani tabia hii ikachekewachekewa na kuonekana ni kawaida, nimekemea sana katika mikutano yangu hapa Mwibara na sehemu zinginezo hapa nchini, nitahakikisha napambana na mafisadi pamoja na polisi hao wasiokuwa waaminifu,” alisema Lugola.

Waziri Lugola alisema kila kukicha anapata malalamiko mengi kutoka sehemu mbalimbali nchini kuwa mafisadi wanaendelea kuwaonea wananchi maskini kwa kupora ardhi wakidai wao ndio wamiliki halali. Aliongeza kuwa, utumia polisi wasiokua waaminifu kuwakandamiza wananchi ambao hawana nguvu ya kifedha na kufanikiwa kudhulumu ardhi zao.

“Dawa yao ilikuwa jikoni, sasa imeiva, siwezi mwangusha Mheshimwa Rais Dkt. John Magufuli, Serikali hii haichezewi hata siku moja, sasa nitawashughulikia ipasavyo,” alisema Lugola.

Aidha, Lugola aliwataka wananchi wa Mwibara kuhifadhi vyakula vizuri ili kuepusha janga la njaa kwa hapo baadaye na kusababisha wananchi kuja kuteseka kwa ukosefu wa vyakula na kusababisha mateso katika familia. 

“Tutunzeni vyakula vyetu, msitumie hovyo, kuweni makini na matumizi ya vyakula, sitaki nije kuona mnateseka na njaa, hakikisheni mnatunza vyakula kwa ajili ya matumizi ya baadaye, ogopeni njaa kama ukoma,” alisema Lugola. 

Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo, alifanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo akikagua madarasa ya shule ya msingi pamoja na zahanati.


Share:

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Asifu Maonesho Ya 43 Ya Sababsaba Jijini Dar

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete amezipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kwa maandalizi mazuri ya Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere.

Akizungumza  Jumamosi (Julai 6, 2019) mara baada ya kutembelea na kukagua mabanda mbalimbali ya washiriki wa Maonesho hayo, Rais Mstaafu Kikwete alisema hizo ni dalili njema kwa maonesho hayo kwa kuwa yamekuwa bora zaidi ya maonesho yaliyofanyika mwaka jana.

Aidha aliongeza kuwa maonesho ya mwaka huu, yameonesha dhamira ya dhati ya Serikali katika kujenga uchumi wake kupitia viwanda, kwa kuwa katika maonesho ya mwaka huu malighafi nyingi za kilimo zimepewa kipaumbele na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali.

“Maonesho ya mwaka huu yamekuwa bora zaidi, kwani tumeshuhudia malighafi nyingi za kilimo zikipewa kipaumbele na hii imekuwa ni dalili njema na point (alama) tunayotakiwa kuifikia kwa sasa” alisema Kikwete.

Awali akitembelea Banda la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Rais Mstafu Kikwete alilitaka jeshi hilo kuwa wabunifu kwa kuzalisha bidhaa bora zitakazoweza kutumika nje ya Tanzania hususani bidhaa za ngozi ikiwemo viatu vinavyozalishwa na Jeshi hilo.



Share:

Prof.Mbarawa kuzivunja bodi za mamlaka ya maji na kuwaondoa katika nyazifa wakurugenzi wazembe.

NA SALVATORY NTANDU
Serikali imesema  haitasita kuzivunja Bodi za Usimamizi wa Maji na kuwaondoa katika nyazifa,  Wakurugenzi wa Mamkala hizo watakaobainika  kushindwa kukusanya mapato na kusababisha kushindwa kujiendesha ikiwa ni pamoja nakukosekana kwa   huduma ya maji kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa jana wakati akizungumza na watumishi wa Mamkala ya majisafi na Usafi wa Mazingira mjini kahama(KUWASA) nakusema kuwa,mamlaka za maji  hapa nchini nyingi zinashindwa kujiendesha na kusababisha  kwa wananchi kukosha huduma hiyo muhimu.

Amesema ofisi yake inahitaji  kupata taarifa za ukusanyaji wa mapato(akra) kila baada ya miezi mitatu na nisipoyapata navunja bondi ya maji na kumuondoa mkurugenzi kwenye nafasi yake na kumpatia mwingine mwenye uwezo wa kukusanya mapato na kupeleka huduma ya maji kwa wananchi.

"Nimevunja bodi na kumuondoa mkurugenzi wa mamlaka ya maji Morogoro kutokana na kushindwa kukusanya mapato na kusababisha huduma ya maji kwa wananchi kukosekana, na nitafanya hivyo pia kwenye mamlaka ambazo zitashindwa kukusanya mapato bila kujali mwenyekiti wake wa bodi ni rafiki yangu" Amesema Prof.Mbalawa.

Hata hivyo Prof Mbarawa amesema mamlaka za maji zimekuwa zikisuasua kupeleka huduma ya maji hata kilometa mbili kwa wananchi na badala yake wamekuwa wakiomba fedha wizarani na huku wamekuwa wakitoa huduma na kukusanya mapato na kushindwa kutatua kero za wananchi.

Hata hivyo Prof. Mbarawa amesema adhima ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2020  asilimia 85 ya vijiji vyote nchini view vinapata maji safi na salama hivyo kuzitaka mamlaka hizo kuongeza mitandao ya maji ili kuongeza mapato na kusogeza huduma hiyo kwa wananchi.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Kahama(KUWASA )Meja mstaafu Bahati Matala amesema, atahakikisha anaongeza mapato kwenye mamlaka yake kwa kupanua mtandao wa maji na kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima.

Amefafanua kuwa, fedha itakayopatikana kwenye ukusanyaji wa akra za maji atahakikisha apeleka huduma ya maji kwa wananchi nakuongeza kwa wale wafanyakazi ambao watabainika kuwaunganishia huduma ya maji wateja kinyemela hata sita kuwaondoa kazini.


Share:

Rais Wa Kenya Uhuru Kenyatta Amaliza Ziara Yake Binafsi Ya Siku Mbili Chato Mkoani Geita Na Kurejea Nchini Kwake

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amerejea nchini kwake  baada ya kumaliza ziara ya siku mbili Tanzania.

Kenyatta ameondoka katika Uwanja wa Ndege wa Chato jana  mchana akisindikizwa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Rais Kenyatta aliwasili Chato  Ijumaa ikiwa ni ziara yake binafsi baada ya kualikwa na Rais Magufuli.

Mara baada ya kuwasili alizungumza na wananchi akisisitiza umoja katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ili kuendeleza ushirikiano.

Pamoja na mambo mengine, kiongozi huyo alimjulia hali mama mzazi wa Rais Magufuli, Suzana.



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger