Wednesday, 6 February 2019

MWILI WA MTOTO WATELEKEZWA KWENYE NDOO MAKAMBAKO

Na.Amiri kilagalila Wanawake mkoani njombe wametakiwa kuacha Tabia ya kutoa ujauzito na kutupa watoto wachanga wasio na hatia kwa kisingizio cha Ugumu wa Maisha kwani kufanya hivyo ni kinyume na matakwa ya Haki za Binadamu. Hayo yamesemwa na wananchi wa mtaa wa Mangula katika Halmashauri ya Mji wa Makambako mara baada ya kumkuta mtoto mchanga anayekadiliwa kuwa na miezi saba ambaye amewekwa kwenye ndoo na kutupwa na mama ambaye hajafahamika jina lake mpaka sasa katika eneo la uwanja wa amani mjini makambako. Aidha mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mangula…

Source

Share:

MAWAKILI WAOMBA ISOGEZWE MAHAKAMA KUU NJOMBE

Na.Amiri kikagalila Chama cha wanasheria Tananganyika (Tanganyika low society) pamoja na vyama vingine kikiwemo chama cha mawikili Afrika mashariki mkoani Njombe wameiomba serikali kusogeza mahakama kuu mkoani humo pamoja na kuongeza idadi ya watumishi wa mahakama ili kukabiliana na idadi ya ongezeko kubwa la mashauri mahakamani. Ombi hilo limetolewa na mawakili hao kwa mkuu wa mkoa wa Njombe CHRISTOPHER OLESENDEKA,wakati wa kilele cha siku ya sheria nchini yaliyofanyika kimkoa katika mahakama ya wilaya ya Njombe. “ili kuboresha swala la utoaji wa haki kwa wakati tungependa kupendekeza ongezeko la idadi ya…

Source

Share:

YANGA YAENDELEZA UZEMBE, YAAMBULIA SARE YA 0-0 NA SINGIDA UNITED


Yanga SC imeendeleza rekodi yake ya kutoshinda Uwanja wa Namfua mjini Singida, baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 na wenyeji, Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo jioni.

Huo unakuwa mchezo wa tatu mfululizo wa Ligi Kuu, Yanga ikicheza bila kushinda ikitoka kufungea 1-0 na Stand United Shinyanga na kutoa sare ya 1-1 na Coastal Union Tanga, baada ya mwanzo mzuri katika mzunguko wa kwanza ikiongoza kwa tofauti ya tisa.

Kwa matokeo hayo, Yanga inajiongezea pointi moja tu na kufikisha 55 katika mechi ya 22, sasa ikiizidi point inane Azam FC, ambayo hata hivyo ina mechi mbili mkononi.

Mchezo wa leo ulikuwa mkali na timu zote zilishambuliana kwa zamu, lakini zilikosa maarifa ya kumalizia tu.

Mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo kwa mara nyingine leo ameendelea kucheza chini ya kiwango chake tangu amerejea kutoka kwao, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wiki tatu zilizopita.

Nahodha Ibrahim Ajibu alianzishiwa benchi leo kabla ya kuingia kipindi cha pili, lakini naye kwa mara nyingine hakuwa na mchezo mzuri, huku kocha Mkongo, Mwinyi Zahera akimuanzisha chipukizi Gustavo Simon katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye mvua kali kwa dakika 10 za mwisho.

Mechi nyingine za leo Tanzania Prisons imeshinda 2-1 dhidi ya Mbao FC Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, Kagera Sugar imefungwa 1-0 na Mbeya City Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Stand United imeifunga 2-0 Ndanda FC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Lipuli FC imeshinda 1-0 dhidi ya KMC Uwanja wa Samora, Iringa na JKT Tanzania imeshinda 3-1 dhidi ya Biashara United Uwanja wa Meja Isamuhyo, Mbweni .

Kikosi cha Singida United kilikuwa; Said Lubawa, Jonathan Daka, Mohammed Abdallah, Salum Kipaga, Kennedy Juma, Yussuf Kagoma, Boniface Maganga, Kenny Ally, Habibu Kiyombo/Frank Mkumbo dk83, Mathew Michael/Rajab Zahir dk71 na Athanas Mdamu/Geoffrey Mwashiuya dk64.

Yanga SC; Ramadhani Kabwili, Paulo Godfrey, Mwinyi Mngwali, Kelvin Yondani/Andrew Vincent ‘Dante’ dk59, Abdallah Hajji ‘Ninja’, Feisal Salum/Ibrahim Ajibu dk67, Deus Kaseke, Thabani Kamusoko, Heritier Makambo, Matheo Anthony/Pius Buswita dk59 na Gustavo Simon.
Chanzo - Binzubeiry blog
Share:

Picha : AGPAHI YAKABIDHI MAGARI KUKABILIANA NA UKIMWI SHINYANGA, RC AMWAGA SIFA

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Zainab Telack ameipongeza Asasi ya kitaifa inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia, Ariel Glaser Pediatric AIDS Health Initiative (AGPAHI) kwa jitihada inazozifanya  katika kuboresha utoaji wa huduma za Virusi Vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI mkoani Shinyanga.

Telack ametoa pongezi hizo leo Jumatano Februari 6,2019 wakati akipokea magari mawili aina ya Nissan Patrol yenye thamani ya shilingi milioni 186.5 yaliyotolewa na AGPAHI kwa ajili ya kusaidia utoaji wa huduma za VVU na UKIMWI katika halmashauri za wilaya za Kahama Mji na Ushetu.

Alisema AGPAHI wamekuwa wadau bora katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI na kuwaomba kuendelea kushirikiana na serikali katika kuwahudumia wananchi.

Alisema kutokana na juhudi zinazofanywa na wadau kwa kushirikiana na serikali takwimu za maambukizi ya UKIMWI mkoani Shinyanga zimepungua kutoka asilimia 7.4 mwaka 2011/2012 hadi kufikia asilimia 5.9 mwaka 2016/2017.

“Kazi mnayofanya ni ya kujenga familia za Watanzania,niwashukuru sana kwa ushirikiano mkubwa mnaotupatia,naomba tuendelee kushirikiana”,alisema Telack.

“Leo nimepokea magari haya mawili na sasa idadi ya magari yaliyotolewa na AGPAHI mkoani hapa tangu ilipoanza kazi zake,yanakuwa manne,naomba mtupatie pia magari kwa ajili ya Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga kwani napo bado wananchi wanahitaji elimu ya VVU na UKIMWI”,aliongeza Mkuu huyo wa mkoa.

Aidha aliahidi kuwa, magari hayo yatatumika kwa malengo yaliyokusudiwa huku akiwataka Wataalamu wa afya kutumia magari kuwafikia wananchi wengi zaidi yakiwemo maeneo ya wachimbaji madini na kuwaelimisha kuhusu masuala ya VVU na UKIMWI.

Akikabidhi magari kwa mkuu wa mkoa, Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa alisema magari hayo yatasaidia katika kuboresha utoaji wa huduma na kuongeza tija katika kuboresha huduma za VVU na UKIMWI.

“Tunatambua kuwa wilaya ya Kahama ina kiwango kikubwa cha maambukizi ya VVU, ndiyo maana tumeona vyema tutoe magari Kahama Mji na Ushetu kwani uhitaji ni mkubwa ili kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI tukishirikiana na serikali”,alisema Dk. Sekela.

“Mbali na kutoa magari,pia tulishatoa pikipiki,baiskeli,kujenga na kukarabati vituo vya kutolea huduma,kutoa ajira kwa watumishi na kuwapatia mafunzo mbalimbali ya utoaji huduma za VVU na UKIMWI katika vituo 107 kwenye halmashauri ambazo tunasaidia huduma mkoani Shinyanga”,alisema.

Aidha alieleza kuwa, katika kipindi cha kuanzia Januari 2017 hadi Disemba 2018,AGPAHI imefanikiwa kupima VVU watu 905,724 mkoani Shinyanga ,25,106 walionekana kuwa na maambukizi ambapo watu 27,724 wanaoishi na VVU (110%) walianzishiwa dawa za kufubaza makali ya VVU ‘ARVs’.

“Katika kipindi hicho pia akina mama wajawazito 140,173 walipimwa VVU ambapo 6,555 walionekana kuambukizwa,WAVIU wamama 6,481 (98.9%) walianzishiwa dawa na watoto 4,877 (96%) walizaliwa bila maambukizi”,alifafanua Dk. Sekela.

Magari hayo yamekabidhiwa na AGPAHI kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR) chini ya Vituo vya Kudhibiti Magonjwa na Kinga (CDC). 

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack akizungumza wakati Asasi ya AGPAHI ikikabidhi magari mawili yenye thamani ya shilingi milioni 186.5 kwa ajili ya kusaidia utoaji wa huduma za VVU na UKIMWI katika halmashauri za wilaya za Kahama Mji na Ushetu. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa, kulia ni Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Muonekano wa magari yaliyo magari mawili yaliyotolewa na AGPAHI kusaidia utoaji wa huduma za VVU na UKIMWI katika halmashauri za wilaya za Kahama Mji na Ushetu.

Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa (kushoto) akishikana mkono na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack wakati wa makabidhiano ya magari.
Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa akimweleza jambo Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack wakati akimkabidhi funguo za moja ya magari hayo ili akague.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Zainab Telack akijiandaa kuingia ndani ya gari wakati Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akiwasha gari. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Zainab Telack akiwa amekaa ndani ya gari wakati Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akiwasha gari.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Zainab Telack akijaribu kuendesha gari.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Zainab Telack akikabidhi ufunguo wa gari kwa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Ushetu, Michael Augustino Matomora (wa kwanza kushoto mwenye suti nyeusi) na Mwenyekiti wa halmashauri ya Ushetu, Juma Kimisha (katikati).
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Zainab Telack akimkabidhi ufunguo wa gari Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Kahama Mji, Anderson Msumba (kushoto).
Kushoto ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Ushetu, Juma Kimisha akipokea kadi ya gari.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Zainab Telack na Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa wakikabidhiana hati za makabidhiano ya magari.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Zainab Telack (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa wakisaini hati za makabidhiano ya magari mawili aina ya Nissan Patrol yenye thamani ya shilingi milioni 186.5.
Mratibu wa Mradi AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Dk. Gastor Njau (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Ushetu, Michael Augustino Matomora nao wakisaini hati za makabidhiano ya magari.
Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa akimkabidhi Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack nyaraka za mpango mkakati wa AGPAHI wa miaka mitano (2018-2022) kupambana na VVU na UKIMWI.
Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa (kulia) akieleza mafanikio ya AGPAHI hadi kufikia Septemba 2018 ambapo alisema watu 395,777 wanapatiwa huduma za VVU na UKIMWI katika vituo vya kutolea huduma katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara. Watu 248,000 wakiwemo watoto 13,600 wanatumia dawa za kupunguza makali ya VVU.
Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Dk. Rashid Mfaume akiishukuru AGPAHI kwa kuendelea  kushirikiana na serikali katika kutoa huduma za VVU na UKIMWI.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Share:

RAIS MAGUFULI : SIJAINGILIA MUHIMILI WA MAHAKAMA WALA BUNGE


Rais John Magufuli ameueleza umma kwamba, katika uongozi wake hajawahi kuingilia kazi za muhimili wowote. 

Akizungumza leo tarehe 6 Februari 2018 kwenye Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam amesema, hajaingilia muhimili wa Mahakama wala Bunge.

“Katika uongozi wangu, mimi nimejitahidi sana kutoingilia muhimili wowote, sijaingilia muhimili wa Bunge. Hata mtu akikutukana unazima Tv (televisheni),” amesema Rais Magufuli na kuongeza; “sijaingilia muhimili wa mahakama.”

Ameitaka mahakama pia kutokubali kuingiliwa na mammlaka yoyote.

“Najua nina fahamu kuwa wapo wanaoingilia kwa hasira tu lakini nyie musiruhusu kuingiliwa,” amesema na kuongeza; Kila muhimili ujisimamie wenyewe kwa mujibu kwa Katiba ya Nchi.

Kwenye maadhimisho hayo Rais Magufuli amesema, serikali itaendelea kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na mhakama na kwa sasa inaendelea kushughulikia changamoto hizo.

“Changamoto zinazowakabili zisiwakatishe tamaa, hakuna kazi isiyo na changamoto. Hata tukimaliza za sasa zitajitokeza zingine,” amesema.

Rais Magufuli ameshauri wananchi wasome sheria ili kuweza kuzijua na kuwa, idara za mahakama na wadau wasaidie wananchi kutafsiri sheria.

“Nawasihi wananchi wasome sheria walau kwa uchache, idara ziwasaidie wananchi kutafsiri kwa lugha ya Kiswahili,” amesema na kuwaomba wananchi kutojichukulia sheria mkononi.

Rais Magufuli ameonesha kukerwa na tabia ya baadhi ya wapelelezi wanaopeleleza kesi zilizo na vidhibiti vilivyo wazi.

“Mtu unakuta ameshikwa na meno ya tembo, dawa za kulevya halafu eti upelelezi unaendelea. “Eti lazima tupeleke kwa Mkemia Mkuu na yanapoendelea kukaa huko wanasema ni majivu.”

Kiongozi huyo wa nchi amewataka majaji, mawakili kutenda haki kwa kuwa, wanaposimamia haki kazi yao inapata Baraka kutoka kwa Mungu.

“Wapelelezi kapelelezeni haraka, unapokiona kitu kipo unakwenda kupeleleza nini? Mtu ameiba na kitu anacho bado unakwenda kupeleleza.

“Unakwenda kupeleleza ili kujua wakati anaiba alikuwa ameinama ama amelala?” amehoji Rais Magufuli.

Amesema, wanasheria wana pande mbili, upande wa mshitaki na mshitakiwa na kwamba, wakati mwingine wanasheria huzungumza namna ya kuruka vipengele ili mshtakiwa aachwe huru.

“Mjue kuwa hamzikosei roho zenu tu bali mnamkosea Mungu. Kesi zingine zina ushahidi wa kutosha lakini zinafutwa,” amesema Rais Magufuli.

Amemsifu Prof. Ibrahim Juma, Jaji Mkuu kwa kueleza ukweli kuhusu changamoto za mahakama ambapo ameahidi kuzifanyia kazi kadri atavyoweza kupata wasaa.

“Ndio maana nikakwambia baada ya kumaliza hotuba yako, unikabidhi ili niendelee kupitia na nitayoweza kutatua haraka nitatue na mingine yanaweza kusubiri mpaka pale hali itakaporuhusu,” amesema.

Rais Magufuli amesema, ni muhimu kujenga jamii yanye kuheshimu haki, kudumisha amani na kuondoa migogoro kwenye jamii.

“Tupo hapa leo na tumekaa kwa amani kwa kuwa, zipo sheria zinatulinda, zisingekuwepo pengine tusingekuwa hivi leo,” amesema.
Chanzo - Mwanahalisi Online
Share:

ALIYEUAWA KWA KUPIGWA RISASI KANISANI SINGIDA AZIKWA,JAFO ALAANI

Nteghenjwa Hosseah, Itigi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amelaani vikali vitendo cha watumishi wa umma kutumia nguvu nyingi dhidi ya wananchi hali inayopelekea kuletea machafu kwenye jamii na hata kupelekea mauaji ya wananchi wasiokuwa na hatia.

Jafo amelaani vitendo hivyo wakati wa mazishi ya marehemu Isaka Petro aliyefariki Jumamosi katika vurugu zilizotokea katika kanisa la Waadiventisti Wasabato Itigi kundi Namba Two na kuzikwa nyumbani kwao kijiji cha kazikazi kata ya Kitaraka; Mazishi hayo pia yamehudhuriwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Singida pamoja na Wilaya ya Manyoni.

Jafo amesema tukio hilo lilitokea sio agizo la Serikali na waliotekeleza wamefanya kwa utashi na akili zao binafsi na hawakuagizwa na mtu yeyote na zaidi wametenda kinyume cha maadili ya utumishi wa umma.

“Hakuna namna tunaweza kusema vinginevyo kuhusu tukio hili zaidi ya kuwa tukio baya na la kusikitisha sana kuwahi kutokea kwa wananchi wetu, tena likiwa limetekelezwa na watumishi wa Serikali inasikitisha sana nawasihi watumishi wa umma tutangulize utu mbele katika kila kazi tunazozifanya”

Aliongeza kuwa watumishi wa umma haijalishi unafanya kazi gani katika mazingira gani lakini hakikisha unatanguliza ubinadamu kwanza ili tulinde maisha yetu na ya wale tunaowahudumia haipendezi wewe ukawa chanzo cha mtafaruku katika jamii tusaidie kuwaunganisha wananchi na kuwafanya kuwa kitu kimoja na sio kuwa chanzo cha ugomvi na mafarakano.

Kwa taarifa nilizopewa na nimezithibitisha ni kuwa wote waliohusika na tukio hili wameshakamatwa na vyombo vya Ulinzi na Usalama bado vinaendelea na taratibu zao alisema Jafo.

Katika msiba huo Waziri Jafo akiwa na viongozi wa Mkoa wa Singida alitoa pole kwa familia ya marehemu sambamba na rambirambi pia alishirikiana na ndugu, jamaa na marafiki katika shughuli zote za mazishi ya marehemu Isaka Petro nyumbani kwao Kazikazi.

Akizungumza katika mazishi hayo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amesema kuwa msimba huo ni pigo kwa Serikali pamoja na wananchi wote wa kijiji cha Kazikazi.

“Serikali inawahudumia wananchi walio hai na sio wafu sasa mwananchi wetu anapotutoka tena kwa kifo cha kwa namna hii na sisi tunapata pigo kwa sababu dhamira yetu ya kufikisha huduma bora kwake haitafikiwa”

Sisi kama Serikali tuna wajibu wa kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya wananchi wetu kufanya shughuli zao kwa usalama wa hali ya juu sasa wajibu huu unapotekelezwa kinyume na taratibu zetu ni makosa ninatoa na kila mtu atawajibika kwa kadiri ya kosa lake alisema Dkt. Nchimbi.

Aidha Dr Nchimbi aliwaeleza wananchi wa kazikazi pamoja na Kitaraka kuwa wale wote wanaolima katika Shamba la Kitaraka waendelee na shughuli zao kama kawaida na wasilipe ushuru wa shilingi elfu ishirini kama ilivyokuwa hapo awali mpaka hapo yatakapokuja maelekezo mengine.

“Watumishi wa halmashauri mupeleke ujuzi na pembejeo kwa wakulima wadogo wa shamba la Kitaraka na sio kwenda kuwabugudhi kwa kuwadai ushuru nyie endeleeni na wawekezaji wenu wakubwa kwa kadiri ya makubalino mliyoingia lakini hawa wananchi wanaolima ekari moja moja waacheni waendelee na kilimo chao” alisema Dkt. Nchimbi.

Naye Mchungaji wa Kanisa la Waadiventista Wasabato Itigi Kundi Namba Two Manigina F.S Manigina aliwaasa wanakijiji cha kazikazi kutokua na kisasi na kumuomba Mungu ili tukio kama hilo lisitokee tena katika kijiji chao.

“Visasi ni vya Mungu nyinyi msiweke visasi na mtu ila endeleeni na maisha yenu kama kawaida na Mungu atazidi kuwashushia baraka zake katika kazi zenu” alisema Mchungaji Manigina.

Katika vurugu zilizotokea siku ya jumamosi katika kijiji cha kazikazi eneo la Kanisa la Waadiventista Wasabato Kundi Namba Two baina ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi akiwa na askari wa wanyamapori na baadhi wa wananchi wa kijiji hicho zilipelekea kifo cha kijana Isaka Petro mwenye umri wa miaka 28.

Marehemu ameacha mke na watoto watatu.
Share:

BABA NA MWANAE WAKAMATWA KWA KUMPIGA NA KUMNG'OA MENO ASKARI POLISI


Polisi huko Homa Bay nchini Kenya wamewatia mbaroni baba na mwanae wa kiume kwa kumpiga hadi kumng’oa meno afisa wa polisi aliyekuwa ameenda kumkamata mshukiwa mwingine aliyehusishwa na mzozo wa shamba katika mtaa wa Ka Peter, Homa Bay.

Kwa mujibu wa ripoti ya Taifa Leo, Februari 4,2019, Boniface Oremo (48) na mwanae Collins Oremo (22) walimvamia afisa huyo kwa mawe na kumsababishia majeraha mabaya. 

Inaelezwa kuwa afisa huyo alikuwa ameandamana na wenzake wawili wakati baba na mwanawe walipoanza kuwarushia mawe ili kuwazuia kufanya kazi yao.

 Kulingana na ripoti hiyo, mmoja wa maafisa hao wa polisi alipoteza baadhi meno yake baada ya jiwe lililorushwa kumpata mdomoni. 

Naibu Chifu wa Kata ya Asego Tom Ondiek alisema kwamba wawili hao walikamatwa baadaye wakiwa mafichoni katika mitaa mbalimbali mjini Homa Bay.

 Walikuwa wamejificha baada ya kupata taarifa kwamba polisi walikuwa wakiwasaka.

OCPD wa Homa Bay Sammy Koskey alisema kuwa, afisa wa polisi alijeruhiwa amelazwa hospitalini na anaendelea kupokea matibabu huku washukiwa hao wakisubiri kufikishwa kortini.

 Kwa sasa washukiwa hao wanaendelea kuzuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Homa Bay. 
Share:

NAPE NNAUYE : TUJIFUNZE KIDOGO KUWEKA AKIBA YA MANENO HASA TUNAPOSHUTUMIANA BILA SABABU

Mbunge wa Mtama Nape Nnauye amewataka Wanasiasa kujiwekea utaratibu wa kuwa na akiba ya maneno pindi wanapozungumza mambo ikiwemo kupinga jambo.

Nape aliyasema hayo jana wakati akichangia mapendekezo katika taarifa mbili za Kamati ikiwemo Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii kwa mwaka 2018 pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji.

Alisema kwa niaba ya wananchi wa jimbo la Mtama wanamshukuru Rais John Magufuli kwa kukubali maombi yao ya kufuta mashamba yaliyotelekezwa.

“Tujifunze kidogo kuweka akiba ya maneno hasa tunaposhutumiana bila sababu. Wakati wa uchaguzi tulipeleka kwa Rais maombi ya kufuta baadhi ya mashamba yaliyotelekezwa,” alisema.

Alisema miongoni mwa mashamba hayo ambayo Rais alikubali ombi lililopelekwa kwake na yeye na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ni shamba namba 37 lililopo eneo la Maumbika jimbo la Mtama mkoani Lindi.

“Wakati mwingine tunapolishwa maneno tukaseme tuweke akiba ya maneno ya nani anapinga nini na anasema nini? Itatusaidia sana kwa sisi wanasiasa tukiweka akiba ya maneno,” alisema.

Jumatatu, Nape aliandika barua kwenda kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai ya kujiuzulu nafasi ya uenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii na hadi sasa bado haijafahamika sababu ya kujiuzulu kwake.
Share:

UDOM:APPLICATION FOR ADMISSION INTO PhD AND MASTER BY THESIS PROGRAMMES FOR ACADEMIC YEAR 2018/2019 BATCH II

APPLICATION FOR ADMISSION INTO PhD AND MASTER BY THESIS PROGRAMMES FOR ACADEMIC YEAR 2018/2019 BATCH II
Applications are invited for admission into various postgraduate programmes for the academic year 2018/19.

PhD PROGRAMMES
UDOM offers PhD by thesis in the fields of Business and Economics Studies, Social Sciences, Education, Humanities, Public Health, Nursing, Medicine, Natural Sciences, Computer Science, Telecommunications Engineering, Information System, Environmental Engineering and Mining Engineering.

ADMISSION CRITERIA
A candidate to be admitted under Master degree by Research only minimum GPA should be 3.5, and for PhD the applicant should possess Master’s degree (Minimum GPA should be 3.0) in the area intended to register for studies.
Applicant for either Master or PhD degree programme should present a concept paper outlining what to be researched in the intended discipline.

HOW TO APPLY
• Applicants are required to complete application procedures Online via the link application.udom.ac.tz or through UDOM website: www.udom.ac.tz.

• Application fee is Tsh 50,000/= (Non Refundable) to be paid through TIGO PESA, AIRTEL MONEY, M PESA, NMB, EXIM BANK or CRDB. Modalities of payment will be given after successful registration into the application system.

IMPORTANT NOTES
a) The closing date for submission of completed application is on Tuesday 5th March 2019
b) Successful applicants will be notified by the end of March, 2019.
c) For enquiry please contact: graduate@udom.ac.tz.

Successful candidates are expected to commence studies in April 2019.

The post UDOM:APPLICATION FOR ADMISSION INTO PhD AND MASTER BY THESIS PROGRAMMES FOR ACADEMIC YEAR 2018/2019 BATCH II appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

UDSM: Applications For Admission Into Postgraduate Programmes for the 2018/2019 and 2019/2020 Academic Years

The University of Dar es Salaam invites applications for admission into its postgraduate programmes for the 2018/2019 and 2019/2020 Academic Years.

Note: All PhD programmes are offered by thesis except few which are offered by both delivery modes (thesis, coursework and dissertation) as shown in the programme list.

Applicants are required to complete all stages as shown on the guideline for Online Application through the link: udsm.admission.ac.tz

NB: Applicants who would like to pursue their postgraduate programmes either by thesis, short term or as occasional students should indicate if they would like to be admitted in the second semester of 2018/2019 academic year commencing in March 2019 or in the first semester of 2019/2020 academic year beginning in October 2019.

Deadline for Application is on 29th March 2019
Successfully applicants will be notified by the end of March for the programmes that commences in March 2019, and July 2019 for the rest of the programmes which will commence in October 2019

Click the attached document for more Information.

 Attachment20190205_054712_UDSM_Applications for admission into Postgraduate Programmes.pdf

The post UDSM: Applications For Admission Into Postgraduate Programmes for the 2018/2019 and 2019/2020 Academic Years appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA TANZANIA LEO FEBRUARI 6,2019.

Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Februari 6, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.

Source

Share:

AGPAHI YATOA MSAADA WA MAGARI YA MILIONI 186 KUSAIDIA UTOAJI WA HUDUMA ZA VVU NA UKIMWI MARA



Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa (kushoto) na Mkuu wa mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima, wakifungua moja ya magari yaliyotolewa na AGPAHI mkoani Mara kwa ajili ya kusaidia utoaji wa huduma za VVU na UKIMWI katika halmashauri za wilaya za Bunda na Rorya, Februari 5,2019.


Mkuu wa mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima, akifungua moja ya magari hayo kwa ajili ya ukaguzi. Nyuma yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa.
Mkuu wa mkoa wa Mara, Mh. Adam Malima akifurahia wakati wa kufungua gari.
Mkuu wa mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima, akisaini ya kushuhudia mkataba wa makabidhiano ya magari hayo.
Mkuu wa mkoa wa Mara, Mh. Adam Malima, akisisitiza matumizi bora ya gari kwa uongozi wa halmashauri ya Bunda.
Mkuu wa mkoa wa Mara, Mh. Adam Malima, ndani ya moja ya magari yaliyotolewa na AGPAHI.
Mratibu wa AGPAHI mkoa wa Mara, Bi Alio Hussein, akisaini makubaliano ya makabidhiano ya magari hayo.
Picha ya pamoja baada ya magari kukabidhiwa kwa halmashauri za Bunda na Rorya
***
Asasi ya kitaifa inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia, Ariel Glaser Pediatric AIDS Health Initiative (AGPAHI),leo imetoa msaada wa magari mawili yenye thamani ya jumla ya shilingi milioni 186 kwa ajili ya kusaidia utoaji wa huduma za VVU na UKIMWI katika halmashauri za wilaya za Bunda na Rorya, mkoani Mara.

Akikabidhi magari hayo aina ya Nissan Patrol kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, mjini Musoma, Februari 5,2019, Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk.Sekela Mwakyusa, amesema asasi hiyo imenunua magari hayo ili kukabiliana na changamoto ya usafiri hivyo kuboresha utoaji wa huduma za VVU na UKIMWI katika halmashauri husika.

“Usafiri umekuwa ni changamoto kwa halmashauri nyingi. Kwa kutambua hilo, kwa awamu, tumekuwa tukizipatia halmashauri misaada ya vifaa vya usafiri kama vile magari, pikipipiki na baiskeli hivyo kwa awamu kwa kuzingatia upatikaji wa fedha na uhitaji wao. Mwaka jana pekee AGPAHI ilinunua vyombo vya usafiri vyenye jumla ya shilingi bilioni1.2,” anasema Dk. Mwakyusa.

Mkurugenzi Mtendaji amesema AGPAHI ambayo kwa sasa inahudumu katika mikoa ya Mara, Mwanza, Simiyu na Shinyanga n imuumini mzuri wa upatikanaji wa huduma bora za VVU na UKIMWI. 

Kwa mantiki hiyo kwa ufadhili wa watu wa Marekani kupitia Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR) chini ya Vituo vya Kudhibiti Magonjwa na Kinga (CDC) ,AGPAHI imekuwa ikifanya mambo mbalimbali kuboresha utoaji wa huduma hizo.

“Ili kuhakikisha kuwa kunakuwa na huduma bora za VVU na UKIMWI, tumefanyia ukarabati majengo 158 ya kutolea huduma ili kuwawezesha wengi kupata huduma hizo na katika mazingira mazuri, tumenunua vifaa tiba vyenye jumla ya thamani ipatayo sh. Bilioni 4 na kuviweka kwenye maeneo ya kutolea huduma katika mikoa tunayofanyia kazi,” amesema.

Aidha amesema kwa kutambua kuwa huduma hizo ni muhimu kutolewa na watu wenye utaalamu nazo, AGPAHI imesaidia watumishi 7,121 kupata mafunzo mbalimbali ya utoaji wa huduma za VVU na UKIMWI. 

“Watumishi 457 waliwezeshwa kupata ajira hivyo kupunguza upungufu wa wafanyakazi wa kada ya afya nchini”.

Akizungumzia mafanikio yatokanayo na huduma za AGPAHI mkoani Mara, Dk. Sekela amesema kuwa asasi hiyo kwa kusaidiana na serikali imekuwa ikitoa huduma kwenye vituo 122 vya kutolea huduma na kupata mafanikio makubwa.

“Kuanzia Januari 2017 hadi Disemba mwaka 2018, tulifanikiwa kupima VVU watu 494,188 ambapo 15,748 walionekana kuwa na maambukizi. Watu14,804 ya watu hao walioonekana kuishi na VVU ambao ni sawa na 94% walianzishiwa dawa za kupunguza makali ya VVU,” amesema Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI.

Kwa upande wa kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, Dk. Mwakyusa amesema AGPAHI iliendelea kusaidia utoaji huduma hizo mkoani hapa na katika kipindi hicho akina mama wajawazito108,696 walipimwa VVU ambapo 2,057 walionekana kuambukizwa. Wamama1,867 (asilimia 90.8) walianzishiwa dawa hivyo kufanikisha kuzaliwa kwa watoto 2,000 (asilimia 96.5) walizaliwa bila maambukizi.

Amesema katika kipindi hicho hicho cha Januari 2017 na Disemba 2018, watu 35,398 wanaotumia dawa za kupunguza makaliya VVU walipimwa kipimo cha wingi wa virusia mbapo 28,670 ambao ni sawa na 81% walionekana kuwa idadi ya virusi vilivyofubazwa.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mheshimiwa Adam Malima, aliishukuru AGPAHI kwa msaada wake wa hali na mali katika kuboresha afya za watanzania, hususan za watu wanaoishi na VVU.

Mkuu huyo alisema kuwa AGPAHI imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia serikali kuboresha afya ya wananchi wake mkoani mwake.

“Ukienda sehemu nyingi za kutolea huduma hutaacha kuona kazi nzuri ya AGPAHI, kama siyo majengo waliyoyakarabati ili kuyawezesha kutoa huduma bora, basi utaona vifaa tiba, vitendea kazi mbalimbali na hata watumishi waliopata mafunzo au ajira kutokana na AGPAHI”,amesema Malima.

Akikabidhi magari hayo kwa halmashauri za Rorya na Bunda, Mkuu wa mkoa alizitaka halmashauri hizo kuhakikisha kuwa magari hayo yanatumiwa kwa shughuli iliyokusudiwa.

“Tunataka siku AGPAHI wakirudi kukagua kazi zao, basi waone kuwa magari haya yaliweza kutuongezea tija katika shughuli za VVU na UKIMWI", ameongeza.
Share:

Tuesday, 5 February 2019

MWILI WA MTOTO WAKUTWA DAMPO IRINGA

Mtoto anayekadiliwa kuwa umri wa miezi 7 amekutwa ameuawa kikatili na mwili wake kutelekezwa katika kontena la taka lililopo soko la kihesa manispaa ya iringa. Akizungumza na mtandao huu Mwenyekiti wa Mtaa wa Sokoni AGUSTINO KIMULIKE amesema kuwa dampo hilo linatumika na mitaa  mitatu hivyo kama serikali wanaendelea kushirikiana na wananchi ili kumbaini mwanamke aliyefanya kitendo  hicho. Kwa upande wake Mtendaji wa Kata ya Kihesa SWEBE DATUS amesema kuwa wananchi wanapaswa kukomesha matukio kama hayo kwani yanaleta sifa mbaya katika jamii. Nao baadhi ya wananchi wa Mtaa huo Kata ya…

Source

Share:

SERIKALI YAWAGEUKIA WAMILIKI WA MACHAPISHO

Serikali imetoa notisi ya siku 24 kwa wamiliki wa machapisho (magazeti na majarida) ambayo bado hayajahuisha leseni zao kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 kuhakikisha wanahuisha leseni hizo hadi ifikapo Machi 21, 2019 vinginevyo hayataruhusiwa kuchapishwa. agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi leo Jijini Dodoma wakati akiongea na Wanahabari kuhusu utekelezaji wa masuala mbalimbali ya Serikali ikiwemo utekelezaji wa Sheria ya Huduma ya Habari. “Kwa mujibu wa Sheria mpya ya Huduma za Habari ya Mwaka…

Source

Share:

CCM NJOMBE YAADHIMISHA MIAKA 42 YA CHAMA KWA KUPANDA CHAI

Na.Amiri kilagalila Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Njombe kimeungana na wananchi wa kijiji cha uliwa kata ya Ihungilo mkoani Njombe katika zoezi la upandaji wa miche ya chai ili kukuza na kuendeleza zao hilo la kimkakati mkoani humo pamoja na kuadhimisha miaka 42 ya chama hicho tangu kilipozaliwa. Akizungumza wakati wa zoezi hilo, katibu wa siasa na uenezi wilaya ya Njombe HITLA BENJAMINI MSOLA amesema kuwa chama hicho kimeamua kufanya maadhimisho hayo kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji hicho ili kuakisi ukombozi wa uchumi wa Tanzania. “kwanza tumefikisha miaka…

Source

Share:

MAPACHA WAZUA GUMZO BAADA YA KUOA MWANAMKE MMOJA

Mapacha wa kiume wamevunja rekodi nchini Afrika Kusini baada ya kufunga pingu za maisha na mwanamke mmoja.

 Ndugu hao wawili walipiga picha pamoja na mke wao huku wamevalia ngozi za chui. 

Mwanamke huyo alikuwa kati kati yao huku akiilaza mikono yake kila pande kwenye mapaja ya waume zake.

 Huku waume hao wakionyesha furaha kwa tabasamu kubwa, mwanamke huyo alionekana kama aliyechanganyikiwa.

Katika picha kadhaa zilizochapishwa katika mtandao wa Twitter na Catchvibe Moatshe, harusi hiyo iliyofanyika Jumamosi, Februari 2 iliwaacha wengi wakishangaa kuhusu jinsi ndugu hao wawili walikubaliana kumuoa mwanamke mmoja.

 Baadhi walikataa wakidai kuwa mke mmoja hawezi kukubali kuolewa na wanaume wawili.

 Walidai kuwa mume mwengine alikuwa nao kwa ajili ya picha tu wala si kwa ndoa. Suala hilo limesalia kuwa kitendawili, wengi wakijiuliza maswali bila majibu. 

Share:

Picha : RAIS MAGUFULI AKINUNUA NA KUNYWA MADAFU MTAANI DAR



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisaidiwa na Katibu Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole kunywa Dafu alilonunua kwa mjasiriamali Paschal Sabas mara baada a kukagua ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega Uchumi la CCM (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5,2019.Picha na Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akinywa Dafu alilonunua kwa mjasiriamali Paschal Sabas mara baada a kukagua ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega Uchumi la Ccm (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasikiliza Wajasiriamali wadogo Paschal Sabas Mjasiliamali wa Madafu pamoja Dunia Seleman Simba Mjasiliamali wa Miwa mara baada ya kukagua ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega Uchumi la CCM  (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimlipa pesa Paschal Sabas Mjasiliamali wa Madafu mara baada kununua Madafu yake, alipotembelea ili kukagua ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega Uchumi la CCM  (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimlipa pesa Paschal Sabas Mjasiliamali wa Madafu mara baada kununua Madafu yake, alipotembelea ili kukagua ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega Uchumi la CCM  (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimlipa pesa Paschal Sabas Mjasiliamali wa Madafu mara baada kununua Madafu yake, alipotembelea ili kukagua ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega Uchumi la Ccm (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5,2019.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufguli na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole wakimsikiliza Msimamizi wa Ujenzi wa ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega wa Kitega Uchumi la CCM  (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5,2019.


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufguli na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole akitoa maelekezo kwa Msimamizi wa Ujenzi wa ukarabati wa Mradi wa Jengo la Kitega wa Jengo la Kitega Uchumi la Ccm (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5,2019.
Picha na Ikulu
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger