Thursday, 3 January 2019

WAKATI MBOWE NA MATIKO WAKISOTA GEREZANI,PROFESA SAFARI AISHANGAA SERIKALI

  Wakati Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko wakiendelea kusota mahabusu yapata mwezi mmoja na nusu sasa, Wakili anyewatetea Profesa Abdallah Safari amehoji katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhusu rufaa iliyokatwa na upande wa mashtaka katika Mahakama ya Rufani. Mbowe na Matiko wanasota mahabusu baada ya Mahakama ya Kisutu kuwafutia dhamana yao...
Share:

JUMLA YA MASHAURI 118 YAMEPOKELEWA NA MAHAKAMA YA WATOTO KISUTU NA KUFANYIWA KAZI 2018

Mahakama ya watoto ya Kisutu imepokea jumla ya mashauri 118 ya jinai na makosa 295 ya madai yalipokelewa na kufanyiwa kazi kwa mwaka 2018. Hayo yamebainishwa na hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu Bi. Agness Mchome wakati akimpa maelezo katibu mkuu wizara ya Afya ,maendeleo ya jamii,Jinsia,wazee na watoto  idara kuu maendeleo ya jamii Dkt John Jingu alipotembea mahakama ya...
Share:

BINTI AJINYONGA KISA KAZUIWA KWENDA KWENYE MKESHA WA MWAKA MPYA

Mwaka Mpya wa 2019 umeanza na visa vya watu wawili wilayani Tarime mkoani Mara kufariki dunia kwa nyakati tofauti akiwemo msichana mkazi wa Mtaa wa Nkende, Elizabeth Magige (14) aliyejinyonga kwa kamba kwa madai ya kuzuiliwa na bibi yake kwenda kwenye sherehe za Mwaka Mpya. Aidha, mkazi wa Kijiji...
Share:

KOCHA MBELGIJI WA SIMBA AWASHA TAA NYEKUNDU,ATANGAZA REKODII HII WALIYOEWEKA YANGA

WAKATI timu ya Yanga ikiwa haijafungwa hata mchezo mmoja katia mechi za ligi kuu soka Tanzania Bara,Kocha mkuu wa Mabingwa wa Ligi kuu hiyo Timu ya Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems amesema nao wao watahakikisha  katika mechi zao 24 za Ligi Kuu Bara zilizobaki, hawatafungwa kwenye uwanja wao wa nyumbani kwa lengo la kuipiku Yanga na kutetea ubingwa wao. Kocha huyo ambaye anasifika kwa “Fomesheni’ ...
Share:

VYAMA 10 VYA UPINZANI NCHINI KUIBURUZA SERIKALI YA JPM MAHAKAMANI,NI KUPINGA MSWAADA HATARI

NI VITA mpya sasa unaweza ukasema ni mara baada ya Vyama 10 vya upinzani nchini kupitia muungano wao vimepanga kwenda fungua kesi Mahakamani Kuu ya Tanzania kupinga muswada wa sheria ya vyama vya siasa kujadiliwa na Bunge kwa ajili ya kuupitishwa kuwa sheria. Kesi hiyo ya kupinga mswaada huo ambao unatajwa ni hatari zaidi imefunguliwa Desemba 20,2018 ikitarajiwa kuanza kusikilizwa kesho Ijumaa Januari...
Share:

UMOJA WA VYAMA 10 VYA UPINZANI NCHINI TANZANIA VIMEFUNGUA KESI MAHAKAMA KUU TANZANIA.

Na. Jovine Sosthenes. Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, Naibu Katibu Mkuu CUF bara, Joram Bashange pamoja na viongozi wengine wa vyama mbalimbali vya siasa vya upinzani leo Januari 3 wamethibitisha kufungua kesi katika Mahakama kuu ya Tanzania kwa ajili ya kupinga muswada wa sheria ya vyama vya siasa kujadiliwa Bungeni kwa minajiri ya...
Share:

HARMONIZE ATOA MSAADA KWA WALEMAVU

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka lebo ya WCB iliyochini ya Diamond Platnumz, Harmonize alimaarufu Kondeboy ameamua kutoa msaada kwa walemavu jijini Dar Es Salaam maeneo ya Kariakoo. Msanii huyo ameamua kurudisha shukrani hizo kwa mashabiki zake ambao wana matatizo mbalimbali hasa walemavu...
Share:

WADAU WA SOKA SHINYANGA WALIA NA TFF UKATA VILABUNI

Wadau wa soka Mkoani Shinyanga wameliomba Shirikisho la mpira wa miguu nchini(TFF) kuvinusuru vilabu vinavyoshiriki ligi kuu soka Tanzania bara,kwa kutafuta mdhamini mkuu atakayeondoa hali ya ukata kwa vilabu shiriki katika mzunguko wa pili msimu huu wa 2018/19.  Wakati baadhi ya timu zinazoshiriki...
Share:

CCM NJOMBE YAAHIDI KUNYAKUA VIJIJI NA MITAA YOTE KATIKA UCHAGUZI MDOGO 2019

  Na Amiri kilagalila Jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM mkoa wa Njombe umeahidi chama hicho kuibuka kidedea katika uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka 2019 kutokana na kukubalika kwa chama hicho mkoani humo. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake wakati akitoa salamu za mwaka mpya katibu wa hamasa na chipukizi UVCCM mkoa...
Share:

WATOTO WAWILI WAFARIKI WAKIOGELEA BAHARINI KUSHEREHEKEA MWAKA MPYA

Watu wawili ambao ni wanafunzi wa shule ya Msingi Mgao Mkoa wa Mtwara wameokotwa wakiwa wamefariki dunia pembezoni mwa mwambao wa Bahari ya Hindi. Uchunguzi wa Daktari imebainisha kuwa vifo hivyo vimetokana na kukosa hewa baada ya kuzama kwenye maji. Kamanda wa Polisi mkoani Mtwara, Kamishna msaidizi...
Share:

MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU INATARAJIA KUSIKILIZA KESI YA MALINZI NA WENZAKE KWA SIKU TATU MFULULIZO.

DAR ES SALAAM Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kusikiliza ushahidi wa kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili aliyekuwa Rais wa (TFF) Jamal Malinzi na wenzake kwa siku tatu mfululizo. Hayo yameelezwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya kesi hiyo kuitishwa leo kwa ajili ya kutajwa. Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi January 16, 17 na 21, 2019 kwa ajili ya kuendelea na...
Share:

VYAMA 10 VYA UPINZANI VYAFUNGUA KESI KUPINGA MUSWADA WA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA TANZANIA

Vyama 10 vya upinzani nchini Tanzania kupitia muungano wao vimefungua kesi Mahakamani Kuu ya Tanzania kupinga muswada wa sheria ya vyama vya siasa kujadiliwa na Bunge kwa ajili ya kuupitishwa kuwa sheria. Kesi hiyo imefunguliwa Desemba 20,2018 ikitarajiwa kuanza kusikilizwa kesho Ijumaa Januari...
Share:

MBOWE,MATIKO KUENDELEA KUSOTA MAHABUSU HADI JANUARI 17..MAWAKILI WAHOJI KWA NINI?

Wakati Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko wakiendelea kusota mahabusu, Wakili anayewatetea Profesa Abdallah Safari amehoji katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhusu rufaa iliyokatwa na upande wa mashtaka katika Mahakama ya Rufani. Mbowe na Matiko wanasota...
Share:

ZITTO KABWE : WABUNGE WAPENDA SIFA ,MAKASUKU WANATUKWAMISHA BUNGENI

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo ameeleza kuwa wingi wa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) bungeni kuna kwamisha maslahi ya wananchi kutokana kutumia wingi wao kupitisha yanayowapendeza watawala. Akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye Ofisi za Chama cha CHAUMA akiambatana na viongozi...
Share:

ZAHERA : LIVERPOOL WANA NAFASI YA KUICHAPA MAN CITY LEO

Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera ametoa mtazamo wake kuelekea mchezo mkali wa EPL leo kati ya vigogo Manchester City na Liverpool. Akizungumza katika mahojiano na Kipenga Extra ya East Afrika Radio inayoruka Jumatatu mpaka Ijumaa, kuanzia saa 6:00 mpaka...
Share:

RAIS MSTAAFU JACOB ZUMA KUINGIA STUDIO KUREKODI NGOMA

Rais mstaafu wa Afrika Kusini Jacob Zuma, anakusudia kuingia studio hivi karibuni, kurekodi albam ambayo itakuwa na nyimbo za mapambano. Taarifa hiyo imetolewa na Thembinkosi Ngcobo ambaye ni Mkuu wa Hifadhi ya Utamaduni na Burudani, na kusema kwamba wamefikia uamuzi huo baada ya kuona hakuna msanii...
Share:

HIKI NDICHO KINACHOMUUMIZA KICHWA WAZIRI LUGOLA KATIKA WIZARA YAKE.

  Na Allawi Kaboyo Bukoba. WAZIRI wa Mambo ya ndani ya nchi Kangi Lugola,amesema kitu kinachomuumiza kichwa katika wizara yake ni Idara ya huduma za uangalizi na probesheni licha ya kuwa na watumshi wengi katika wizara hiyo. Alitoa kauli hiyo Jana wakati akipokea taarifa za idara hiyo Mkoani Kagera ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake mkoani humo kwa muda wa siku saba atakaoumaliza....
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger