Tuesday, 21 February 2017
Monday, 20 February 2017
HIZI HAPA HABARI KALI SIKU YA LEO JUMATATU FEB 20 2017
MAGAZETI YA LEO JUMATATU FEB 20 2017,BONYEZA HAPO>>>>>https://goo.gl/nx8imK
MANENO YA PRFO.J BAADA YA KWENDA GEREZA ALILOFUNGWA MBUNGE LIJUAKALI,SOMA ZAIDI HAPO>>>>>>>>>>>https://goo.gl/P00daq
MH.MBOWE ASAKWA NA JESHI LA POLISI KILA KONA APEWA MASAA 48 AJISALIMISHE,SOMA ZAIDI HAPO>>>https://goo.gl/MxB3jP
MKAZI WA MKOA WA MWANZA KWIMBA AANZISHA KIWANDA CHA KUTENGENEZA GONGO,SOMA ZAIDI HAPO>>>>>>>https://goo.gl/Qh7hOL
Siri yafichuka wanawake wengi kujifungua kwa upasuaji
Aidha, imeelezwa kuwa baadhi ya hospitali zinalazimisha upasuaji kama njia ya kutafuta fedha, jambo lililoelezwa kuwa ni kinyume cha maadili ya tiba nchini.
Gazeti hili limezungumza na madaktari mbalimbali, wakiwemo madaktari bingwa wa wanawake na wanajamii kwa ujumla kuhusu sababu mbalimbali zinazohusishwa na hali halisi ya uzazi wa wanawake kwa sasa.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, Dk Erasto Rite alisema njia ya upasuaji kwa mjamzito inayotumika kuzalisha mtoto mmoja au zaidi (caesarean section), hutumika kipindi ambacho uhai wa afya ya mama na mtoto upo hatarini.
Alisema takwimu zinaonesha kwamba ongezeko kubwa la njia ya upasuaji kwa wajawazito ambapo ni kati ya asilimia 16.4 mpaka 28 ya akinamama wanaojifungua, huku idadi ikiwa juu kwa kina mama wanaoishi mijini ikilinganishwa na wanaoishi vijijini.
Dk Rite alisema hiyo inachangiwa na kubeba ujauzito katika umri mkubwa, kukua kwa teknolojia na baadhi ya kina mama wenyewe kuchagua njia hiyo.
Alisema kwa upande wa kina mama wanaoishi vijijini, njia hiyo imeanza kuongezeka kutokana na baadhi yao kutumia dawa za kienyeji za kuongeza uchungu (dawa za wepesi), ambazo husababisha wengi kuishia kufanyiwa upasuaji.
Alisema hiyo pia huchangiwa na dawa hiyo kutolewa bila vipimo na pia wengi wanatumia dawa hizo wakati hakustahili kupewa na hivyo kumsababisha kupata uchungu mkali unaohatarisha maisha yake na kulazimika kupasuliwa.
Kwa upande wake, daktari wa magonjwa ya wanawake katika Hospitali ya Regency Dar es Salaam ambaye hakutaka kutajwa jina gazetini, alisema hali hiyo huchangiwa na mfumo wa mabadiliko ya maisha kipindi cha nyuma na ilivyo sasa.
Alisema zamani wanawake walikuwa wakila vyakula vya asili na kufanya shughuli mbalimbali ambazo zilikuwa kama mazoezi ya kumsaidia kuuweka mwili sawa, lakini kwa sasa ni tofauti, wanawake wengi hula vyakula ambavyo havina mpangilio maalumu na hawajishughulishi kuweka mwili sawa.
Aidha, alisema sababu nyingine inayochangia wanawake kufanyiwa upasuaji ni shinikizo la damu au mtoto kukaa vibaya au mtoto kuwa mkubwa na hivyo kushindwa kutoka kwa njia ya kawaida.
Alisema hiyo ndiyo hasa dharura inayotakiwa kuzingatiwa mjamzito kufanyiwa upasuaji na si vinginevyo. Mkazi wa Kinondoni Dar es Salaam, Juliana Joseph ambaye amejifungua watoto wawili kwa njia ya upasuaji, alisema alitamani kujifungua kwa njia ya kawaida, ila tatizo kubwa linalomsumbua wakati akiwa mjamzito ni shinikizo la damu na hivyo madaktari humshauri kwamba ili kuokoa maisha yake na ya mtoto ni lazima kufanyiwa upasuaji.
“Wakati nikiwa hospitali moja ya binafsi nilipokuwa najifungua mtoto wangu wa kwanza, alitokea mama mmoja akiwa ameshapata uchungu, madaktari walimshauri hawezi kujifungua kawaida kwa kuwa mtoto ni mkubwa ila walibishana sasa mama yule alikataa upasuaji akalazimisha kusukuma mtoto.
“Kutokana na hali kuwa mbaya na mtoto kukaa njiani muda mrefu, mtoto alizaliwa amechoka sana na baada ya kuzaliwa alikaa kwenye mashine ya kupumulia siku mbili na ya tatu akafariki, hivyo niliamini kwamba mama yule alichangia kumuua mwanawe, hivyo tunaposhauriwa na madaktari tukubali na tusibishane nao kwa kuwa siamini kama inawezekana mtu mwenye uwezo wa kujifungua kawaida ukalazimishiwa upasuaji, hiyo ni imani potofu,” alisema Juliana.
Naye Amini Salum alisema amejifungua mtoto kwa njia ya upasuaji na hiyo imesababishwa na mtoto wake kukaa vibaya na hivyo kushindwa kutoka kwa njia ya kawaida.
Kwa upande wake, mganga wa wanawake katika Hospitali ya Tumbi wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani ambaye hakuwa tayari kutaja jina gazetini, alisema upasuaji unapaswa kufanyika pale inapotokea tatizo kwa mjamzito na si kitu kinachopendwa na madaktari kumfanyia mtu.
Hata hivyo, alisema zipo taarifa kuwa, baadhi ya wanawake huomba kufanyiwa upasuaji hasa katika hospitali binafsi kwa kile kinachodaiwa hawataki kuharibu maumbile yao ya uzazi.
“Sijui nani aliwaambia maumbile yanaharibiwa kwa kuzaa kwa njia ya asili.
Huo ni utaratibu aliyouweka Mungu mwenyewe hata vitabu vitakatifu vinaeleza.
Uke huwa kama mpira na hutanuka wakati wa kujifungua na baada ya muda mfupi, hurejea katika hali yake, sasa hii dhana potofu sijui wameitoa wapi,” alisema daktari huyo.
Kuhusu hospitali binafsi, alisema wapo wanaowashauri wajawazito kufanyiwa upasuaji kwa tamaa za fedha, jambo ambalo ni kinyume cha maadili ya kazi yao na kuwataka kuzingatia maadili na kufanya upasuaji inapobidi lakini kama mjamzito hana tatizo lolote la dharura linalohitaji upasuaji, aachwe ajifungue kawaida.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake katika Hospitali ya Aga Khan ya Dar es Salaam, Dk Munawar Kaguta alisema wanawake wengi wa mjini wanaomba wenyewe madaktari kuwazalisha kwa upasuaji.
Dk Kaguta alisema hayo hivi karibuni katika mahojiano na gazeti hili kuhusu masuala ya uzazi.
Alifafanua kuwa wanawake wa mjini wanadanganywa na taarifa mbalimbali wanazozipata katika mitandao mbalimbali ya kijamii, ambazo zinaonesha kuwa kujifungua kwa kawaida ni hatari.
“Hawa wanawake wa mjini wanadanganywa na mitandao ambayo wanaingia kutafuta taarifa za uzazi, mwisho wa siku wakija hospitali wanaomba wao wenyewe kufanyiwa upasuaji kutoa mtoto,” alisema Dk Kaguta.
Daktari huyo alisema mbali na taarifa za mitandaoni, pia wanashawishiana na kupeana taarifa nyingine zisizo sahihi, wakielezana athari nyingi zinazoweza kumpata mama anapojifungua kawaida, ikiwa ni pamoja na kupata uchungu mkali wakati wa kujifungua.
Alisema pamoja na sababu zote hizo madaktari wengi huwazungusha na wanapolazimisha sana wakienda hospitali kwa ajili ya kujifungua mwisho wanajifungua wenyewe kwa njia ya kawaida.
Dk Kaguta alisema kila jambo lina madhara yake, alisema mwanamke kupata uchungu wakati wa kujifungua ni kawaida na kwamba hapa nchini hakuna wataalamu wa kutosha kwa ajili ya dawa za kupunguza uchungu.
“Dawa zipo lakini tatizo wataalamu wa kuzichoma, zina utaalamu wake na ambao kwa hapa nchini sio wengi,” alisema Dk Kaguta na kuongeza kuwa wataalamu hao wakipatikana wa kutosha na dawa zifike mpaka katika hospitali za serikali itasaidia kupunguza idadi ya wanaojifungua kwa upasuaji.
Dk Kaguta alisema upasuaji wowote ni hatari kwani dawa zinazotumika kumfanya mtu asipate maumivu wakati wa kufanyiwa upasuaji na pia kumlaza zinaweza kusababisha moyo kusimama ingawa haina madhara mengi kwa mtoto.
“Upasuaji wowote ni hatari, hatari zaidi zile dawa zinaweza kusababisha moyo kusimama, maumivu ya mgongo, kovu kuchelewa kupona na kuendelea kuuma ingawa hakuna hatari zaidi kwa mtoto,” alisema Dk Kaguta.
Hata hivyo, Dk Kaguta alishauri kama mjamzito hana tatizo lolote na pia mtoto amepimwa na kukuta hana tatizo na ana uzito wa kawaida ni bora kujifungua kawaida kwa kuwa ni salama na asili zaidi. Imeandikwa na Regina Kumba, Lucy Ngowi na Hellen Mlacky.
MANENO YA PRFO.J BAADA YA KWENDA GEREZA ALILOFUNGWA MBUNGE LIJUAKALI
January
11 2017 Mbunge wa Jimbo la Kilombero Morogoro kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ Peter Lijualikali alihukumiwa na
Mahakama ya wilaya kifungo cha miezi sita jela bila kulipa faini kwa
kosa la kufanya vurugu kipindi cha uchaguzi wa Mwenyekiti wa halmashauri
ya wilaya ya Kilombero.
Leo
February 19 2017 Mbunge wa Mikumi Joseph Haule maarufu Profesa J
amekwenda kumtembelea gerezani Ukonga Dar es salaam na baada ya kutoka
hapo akaandika yafuatayo.
Sunday, 19 February 2017
HII HAPA REPORT YA WANASAYANSI KUHUSU KUWEPO KWA BARA LA NANE DUNIANI
Wanasayansi wafahamisha kuwa bara la 8 lawezekana kuwa lipo chini ya bahari ya Pasifiki.
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa katika jarida la Marekani la 'Geological Society of America' ni kwamba bara hilo limepewa jina la Zealandia .
Bara hilo lililokubalika na wanasayansi linasemekana kupatikana katika upande wa Kusini Magharibi mwa bahari ya Pasifiki.
Liko na ukubwa wa kilomita milioni 5 za mraba sawa na thuluthi ya ardhi ya bara la Australia .
Wanasayansi wamesema kuwa bara hilo limefinikwa na maji ya bahari .
Zijue Namba Maalum za Magari ya Viongozi, Serikali na Taasisi za Umma kwa Ujumla..!!!
Ukiona mtaani gari zimeandikwa ktk plate number kama ifuatavyo usiumize kichwa jua ni hivi:
1. Ngao-Rais, makamu wa rais na waziri mkuu
2. S-Spika wa bunge
3. JM- Jaji mkuu
4. JR- Jaji wa mahakama ya rufaa
5. JK- Jaji Kiongozi
6. J- Jaji wa mahakama kuu
7. XXXX-Mkuu wa majeshi(CDF)
8. CAG-Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali
9. CS- Katibu mkuu kiongozi
10. W mwanzoni inaashiria waziri kisha kifupi cha wizara yake hufuata
11. NW-Naibu waziri
12. DFP-Donor's Fund project
13. ST-Serikali ya Tanzania kisha herufi nyingine hufuata
14. SMZ-Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar
15. PT-Police of Tanzania
16. SM-Serikali za mitaa
17. CD- Magari ya ubalozini
18. SU-Shirika la umma.
19. gari za jeshi pia zina namba zake ambazo zina vifupi vya JW
20. MT-Magereza Tanzania
21. CGP-Commissioner General of Prison(Mkuu wa Magereza)
22. Gari nyingine za umma zina namba zaidi ya moja kwa kazi maalum
NYONGEZA:
Gari za biashara zina plate number nyeupe na zile za matumizi binafsi plate number ya njano.
MUGABE ANAWEZA KUPIGIWA KURA HATA AKIWA MAITI...
Mke
wa Rais mkongwe wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amesema kuwa mumewe ni
mashuhuri sana hivi kwamba anaweza kupigiwa kura hata akiwa maiti.
Bwana Mugabe, ambaye atakuwa na umri wa miaka 93 mnamo Jumanne,
ametangaza mara kadhaa kuwa atagombea kiti cha Urais katika uchaguzi
mkuu wa mwaka ujao.
Grace Mugabe ana miaka 40 mchanga kwa mumewe.
Aliambia mkutano wa chama tawala cha ZANU-PF kuwa hata mumewe akifariki,
bado jina lake litawekwa kwenye karatasi za kupiga kura.
Alisema watu wa Zimbabwe wanampenda rais wao sana, hivi kwamba wangempigia kura hata akiwa maiti.
Bi Mugabe amekuwa mkosoaji mkuu wa wakosoaji wa mumewe na kwa wale walio na tamaa ya kumrithi.
Inadhaniwa kuwa alikuwa mstari wa mbele wa kumwachisha kazi aliyekuwa makamu wa rais, Joice Mujuru mwaka 2014.
Bwana Mugabe, ambaye siku hizi haonekani sana hadharani, ametawala Zimbabwe tangu taifa hilo kuwa huru miaka 37 iliyopita.
Via>>BBC
MAELFU WAJITOKEZA KUMZIKA MCHEZAJI BONNY MWANDANJI
Maelfu
ya wakazi wa mkoa wa Mbeya wamejitokeza katika mazishi ya mchezaji wa
zamani Geoffrey Bonny Mwandanji aliyefariki dunia juzi na kuzikwa katika
makaburi ya kanisa Katoliki Makandana wilayani Rungwe.
Akizungumza wakati wa mazishi baba mzazi wa marehemu,Bonifasi Mashamba
alisema amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mwanae na kuongeza kuwa
aliishi na watu vizuri jambo lililochangia watu wengi kujitokeza
kumuuguza ikiwa ni pamoja na misaada mbali mbali.
Naye Mjomba wa marehemu, Innocent
Sigonda alisema marehemu alikuwa akisumbuliwa na kansa ya mapafu pamoja
sukari ilikuwa ikishuka mara kwa mara.
Mwenyekiti wa tawi la Yanga mkoa wa Mbeya Lusajo Kifamba alisema
marehemu alikuwa mwanachama wao hivyo uongozi unasikitika kumpoteza
mwanachama wake ambaye alikuwa akitoa msaada wa kiufundi kila
alipotakiwa.
Naye mwakilishi wa uongozi wa yanga makao makuu Shadrack Nsajigwa
alisema marehemu aliishi naye kama ndugu kwani walisaidiana na kupeana
ushauri.
Alisema marehemu alikuwa na kipaji cha mpira pia alikuwa anajituma hivyo alikuwa mfano wa kuigwa kwa vijana waliopo.
Aliongeza kuwa wachezaji wa zamani ni hazina kwa taifa hivyo ni vyema wakatunzwa na kuthaminiwa.
Aidha alitoa wito kwa wachezaji wengine kujipanga kimaisha ili baada ya
kustafu wasisubiri kuomba misaada pindi wapatapo matatizo.
Alisema in vyema pia kuanzisha vyama vya kuwasaidia kama wachezaji wastaafu.
AMIRI JESHI MKUU RAIS DKT MAGUFULI ATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WAPYA WA JWTZ IKULU DAR
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride wakati wa
sherehe za Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la
Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini
Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Magufuli akitunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi
la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu
jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Magufuli akiweka saini katika hati ya Kamisheni muda mfupi kabla
ya Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania
na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es
salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Magufuli akiweka saini katika hati ya Kamisheni muda mfupi kabla
ya Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania
na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es
salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli akiwasili Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la
Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya
Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
Kikundi cha ngoma cha JWTZ kikitumbuiza kwa ngoma ya Chaso ya Pemba
wakati Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt
John Pombe Magufuli alipotunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la
Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya
Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Magufuli, Makamu wa rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe
Kassim Majaliwa, Waziri wa ulinzi nja Jeshi la Kujenga taifa Dkt Hussein
Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Juma Kijazi na viongozi wengine
katika picha ya pamoja baada ya Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa
Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika
viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.PICHA
NA IKULU
Saturday, 18 February 2017
Mwanamke asimulia alivyobakwa na askari Msumbiji
Wakati Serikali ikiahidi kufanya
uchunguzi wa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu katika kutimua
Watanzania nchini Msumbiji, mwanamke mmoja amesema alibakwa na askari
watatu kabla ya kuwekwa mahabausu ambako alikaa siku tatu bila kula.
Mwanamke huyo, aliyejitambulisha kwa jina la Halima (si jina lake
halisi) ni mmoja kati ya zaidi ya Watanzania 180 ambao wamekuwa
wakitimuliwa nchini Msumbiji tangu mwanzoni mwa wiki na wengi wakidai
wana hati halali za kuishi nchi hiyo jirani na wengine kulalamikia
vitendo vya ukiukwaji haki wakati wa utekelezaji wa operesheni hiyo.
Tayari Serikali imesema kuwa itafanya uchunguzi wa madai hayo, ambayo
yanaweza kuharibu uhusiano wa muda mrefu wa Tanzania na Msumbiji.
Halima anasema
walianza kufukuzwa usiku wa Jumamosi ya Februari 11, muda ambao askari
hao waliutumia kumfanyia kitendo hicho.
Halima anasema kuwa alisikia
watu wakivunja geti la nyumba waliyokuwa wakiishi na kudhania ni
majambazi, kumbe walikuwa ni askari ambao waliwalazimisha kutoa nyaraka
zao zote za kuishi Msumbiji pamoja na pesa.
“Niliwasikia wakivunja geti
nikamwambia mume wangu watakuwa ni majambazi kumbe askari, mume wangu
akajificha chini ya uvungu, lakini wakamtoa na baadaye kututoa ndani na
kuanza kutupiga.”
Anasema baada ya kipigo walilazimishwa kuzoa mali
zao kutoka ndani na zikawekwa kwenye gari la polisi na kisha kuwafunga
mikono na baadaye kuwapeleka mahabusu.
“Cha kushangaza tulibebeshwa vitu
wenyewe kuweka kwenye gari pasipo kuelezwa sababu baada ya hapo askari
akanivuta nyuma ya nyumba na kuniingilia kimwili. Nikajua ni mmoja,
lakini waliendelea hadi wakafikia watatu,” alisema.
“Ninaona aibu
walinibaka kwa njia ya kawaida tofauti na taarifa za wengine wanaosema
tulibakwa kinyume na maumbile, si kweli. Nawaomba waelewe hatukubakwa
kinyume na maumbile kama wanavyosema ilikuwa kawaida.”
Hata hivyo
anaeleza baada ya hapo waliwekwa mahabusu kwa siku tatu pasipo kula,
hali iliyowalazimu kunywa maji yaliyokuwa yamewekwa chooni.
“Tulikaa
mahabusu siku tatu, hamna kula wala kunywa, chooni tulienda kwa mtutu
tukalazimika kunywa maji ya chooni kwa sababu hakukuwa na jinsi na njaa
ilizidi. Kwa hiyo inabidi useme unakwenda chooni ili ukanywe maji,”
alisema Halima.
Kutokana na hali hiyo, Halima anashangazwa na kauli ya
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Susan Kolimba kwamba waliorudishwa
hawakuwa na nyaraka huku kaimu balozi wa Tanzania nchini Msumbiji
akiwatangazia wengine kuondoka ndani ya siku tano.
“Kweli mtu utathubutu
vipi kuishi nchi ya watu bila kibali? Hata kaimu balozi na yeye
anatukana, kwamba hatujaingia na documents (nyaraka)? Ilibidi atutetee
lakini katukana. Mungu atatulipia,” alisema.
Mwanamke mwingine
aliyewekwa mahabusu kabla ya kurudishwa nchini, Mary Makundi anasema
askari wa kiume walimwambia awape fedha na alipowajibu kuwa hana,
walimpekua na kuzikuta.
Anasema walizichukua fedha hizo pamoja na simu
kabla ya kumpiga na kutaka kumbaka.
“Walivunja mlango wakanikuta.
Wakaniambia niwape nyaraka zangu. Nikawapa nikijua wanazikagua tu na
kuniacha, lakini cha kushangaza walizichana mbele yangu na kunitaka
niwape pesa na simu. Nikawaambia sina wakanipiga na kunikagua hadi
sehemu za siri na kuchukua pesa na simu,” alisema Mary.
“Baada ya hapo
walinipiga kwanza kabla ya kunifunga mkono. Askari mmoja akataka
kunibaka, nikamwambia kuwa hata kama hawatutaki nchini kwao, hawawezi
kuniingilia bila kinga.
“Nilipoona hali imekuwa mbaya, nilisema wacha
nigombane nife kwa silaha, lakini si kubakwa.”
Mtanzania mwingine
Mohamedi Said ni mmoja wa wafanyabiashara walioambiwa waondoke pasipo
kuchukua chochote na anadai kuacha mali zake zote pamoja na nyumba
aliyojenga.
“Polisi walikuja ghafla wakatuambia wageni wote tunatakiwa
tuondoke. Hapa nina vibali vyote mpaka leseni ya biashara, lakini
imebidi niondoke kwa sababu ya usalama wangu,” alisema Said.
“Hakuna
anayejua sababu mpaka sasa. Nimekuja nyumbani kufuatilia haki yangu kwa
sababu mpaka kibali cha kujengea ninacho.
“Mpaka sasa amekuja kaimu
balozi kutoka ubalozi wa Tanzania na amesema kwa ripoti aliyopewa
ametupa siku tano tuondoke. Hatujui kwanini siku tano. Utahamishaje vitu
kwa siku tano au kumtafuta mnunuzi wa nyumba kwa siku tano kwa sababu
imenibidi niache duka kubwa na gari,” alisema Said.
Akizungumzia tukio
hilo, mwenyekiti wa Kijiji cha Kilambo kilichopo mpakani na Msumbiji,
Mohamed Mkama alisema wananchi wa kijiji chake wamekuwa wakishirikiana
na wanakijiji wa vijiji jirani vya Msumbiji, lakini tukio hilo
limewashangaza.
Amesema mara nyingi wamekuwa wakitembeleana na hata
wengine kutoka upande wa Msumbiji kuja kutibiwa Tanzania kutokana na
ujirani mwema uliopo.
“Kijiji changu kina vitongoji vitano ambavyo
tumekuwa tukishirikiana na kijiji cha upande wa pili kwa muda mrefu na
wengine wana vitambulisho vya uraia mwema, lakini tunashangaa kwanini
wanarudishwa pasipo kuelezwa sababu,” alisema Mkama.
Ofisa uhamiaji Mkoa
wa Mtwara, Rose Mhagama alisema idadi ya Watanzania waliorudi na
kusajiliwa katika mpaka wa Kilambo ni watu 221 hadi kufikia jana mchana.
Thursday, 16 February 2017
NECTA yasitisha mtihani wa udahili kwa kidato cha kwanza Jambo Blog 10
BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA) limesitisha mpango wa kuwafanyia mtihani wa udahili wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu katika shule za sekondari za serikali uliokuwa ufanyike Februari 28, mwaka huu.
Naibu Katibu Mtendaji wa Necta, Athumani Salumu alisema hayo juzi kwenye kikao cha wadau wa sekta ya elimu Mkoa wa Morogoro alipokuwa akihitimisha mada yake kwa wajumbe wa kikao hicho kilichoongozwa na mkuu wa mkoa huo, Dk Stephen Kebwe.
Salumu alisema mpango wa kuwafanyia mtihani wa udahili wanafunzi hao ulitokana na matakwa yaliyowasilishwa Necta na baadhi ya wakuu wa shule za serikali wakipendekeza kupitia maofisa elimu wa mikoa na wilaya kuwa wanafunzi wa kidato cha kwanza waliochaguliwa na kupangiwa shule zao wengi hawana sifa na uwezo wa kumudu masomo.
Naibu Katibu Mtendaji wa Necta alisema wakuu wa shule walikuwa wakiomba kupata idhini ya kuwafanyia mtihani wanafunzi ili kubaini uwezo wao na kwamba baraza liliwasiliana na maofisa elimu mkoa na wilaya likiwataka kuwasilisha orodha ya idadi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza waliopangiwa kwenye shule ya zao.
Alisema baada ya kufahamika idadi ya wanafunzi hao, baraza ndilo litatunga maswali ya mitihani yenye kuzingatia mfumo na vigezo maalumu na kutumiwa wakuu wa shule hizo ili kuusimamia kwa lengo la kuweka uzani sawa wa mtihani huo.
Alisema moja ya masharti ni kwamba mtihani huo ulitakiwa ufanyike kwa wanafunzi wa kidato hicho kwa shule zote za serikali siku moja na kwa muda uliopangwa.
Hata hivyo, alisema baada ya kuwatumia masharti hayo, wakuu wa shule hizo walishindwa kuwasilisha orodha ya wanafunzi kwa maofisa elimu wa mikoa na wilaya ili itumwe Necta na kutokana na mazingira hayo, baraza limeamua kusitisha kuwadahili wanafunzi wa kidato cha kwanza na kuitaka mamlaka inayosimamia elimu kuendelea na utaratibu wao wa kawaida.
“Necta imewasiliana na wahusika kwa barua rasmi ya kusitisha mtihani huo ambao ulipangwa ufanyike Februari 28, mwaka huu na wanafunzi wote waliopangiwa kidato cha kwanza shule mbalimbali za serikali zikiwemo za bweni, waendelee na masomo kama yalivyopangwa,” alieleza Naibu Katibu Mtendaji wa Necta.
Novemba mwaka jana, serikali ilitangaza kuwa wanafunzi 526,653 sawa na asilimia 94.8 ya waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka jana, wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za sekondari za serikali katika awamu ya kwanza huku 28,638 wakishindwa kupangiwa shule katika awamu ya kwanza.
Kati ya wanafunzi hao, wasichana ni 268,052 sawa na asilimia 94.5 ya wasichana waliofaulu na wavulana ni 258,601 sawa na asilimia 95.2 ya wavulana waliofaulu.
Chanzo: Habari Leo