HOTELS AND LODGES FOR BOOKING AND TRANSPORT LOGISTICS FOR "TET" CONFERENCE PARTICIPANTS
The
National Council for Technical Education (NACTE), would like to inform
Participants who wishes to stay on the nearby Hotels and Lodges during
“TET” Conference to be held at NBAA- Accountants Professionals Centre -
Bunju area, Dar-es-salaam from 28th – 29th April, 2016.
The following are the list of Hotels and Lodges for booking;
Vero Inn Location: Tegeta - Nyuki Rooms rates: 40,000/=, 35,000/= Contact: 0716 168 343
Further; Participants buses will be allocated at two stations heading towards the conference venue as stipulated bellow; Station 1: Location: at Mwenge Puma Petrol Station Time of Departure: 7:00am Number of buses: Two Station 2: Location: at NACTE Headquarters Time of Departure: 7:30am Number of buses: One
For more information kindly contact these numbers; +255 684 006 409 Mwemezi, 756 600 124 Syoni and 685 818 108 Nkuliye
Sokoine University of Agriculture invites Applications from qualified Tanzanians and non-Tanzanians for admission to the Degree, Diploma and Certificate programmes offered by the University in the academic year 2016/2017. Read More:
HIZI NDIO SIFA ZA KUJIUNGA DIGRII MWAKA WA MASOMO 2016/2017SUA
APPLICATION SUA 2016/2017
Mwanafunzi wa kidato cha tatu, juzi alimkaanga
askari polisi anayedaiwa kumbaka kwa kuieleza Mahakama jinsi
alivyotendewa kitendo hicho katika kibanda cha ulinzi cha benki.
Akitoa
ushahidi mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Misungwi, Ruth Mkisi,
shahidi huyo alidai siku ya tukio askari huyo, Raphael Sixstus (30),
alimuita alipokuwa akipita karibu na Benki ya CRDB Tawi la Misungwi,
alipoitikia wito ghafla alivutiwa ndani ya kibanda hicho na kumbaka.
“Wakati
akinitendea kitendo hicho, alikuwa akinitishia kisu huku akiniambia
nikipiga kelele ataniua, niliogopa nikaa kimya ingawa niliumia na
kutokwa damu nyingi sana,”alidai shahidi huyo.
Akiongozwa
na Mwendasha Mashtaka wa Polisi, Doreth Mgenyi, mwanafunzi huyo mwenye
umri wa miaka 16 alidai kabla ya kumbaka, mshtakiwa huyo alimvua nguo
zote za ndani.
Awali, Mwendesha mashtaka alipokuwa akimsomea
makosa mshtakiwa huyo alidai kuwa Novemba 20, mwaka jana, akiwa eneo la
lindo katika Benki ya CRBD Tawi la Misungwi, alimbaka mwanafunzi huyo
saa 1.00 usiku wakati akitoka mashine kusaga unga katika maeneo ya
Bomani.
Hakimu Mkisi aliahirisha kesi hiyo hadi leo
itakapoendelea kusikilizwa kwa upande wa mashtaka kuita mashahidi
wengine. Mshtakiwa yuko nje kwa dhamana.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetahadharisha uwepo wa mvua
kubwa na upepo mkali unaozidi kasi ya kilomita 40 kwa saa iliyotarajiwa
kuanza jana hadi keshokutwa.
Sambamba na upepo huo, taarifa hiyo
ya TMA imesema mvua za zaidi ya milimita 50 zinatarajiwa kunyesha huku
bahari ikitarajiwa kuwa na mawimbi makubwa yanayozidi mita 2.0
Taarifa
hiyo imeelezwa kuwa hali hiyo imesababishwa na mgandamizo mdogo wa hewa
katika Pwani ya Tanzania unaotakana na kimbunga cha Fantala.
Maeneo
yaliyotajwa na TMA kwamba yataathiriwa na hali hiyo ni mikoa ya Tanga,
Dar es Salaam, Morogoro, Lindi, Mtwara, Unguja na Pemba na kwamba mvua
hizo pia zinatarajiwa kusambaa hadi katika maeneo ya mikoa ya
Kilimanjaro na Mashariki mwa Manyara.
Ofisa Habari wa TMA,
Monica Mutoni aliwataka wakazi wa maeneo hayo na watumiaji wa bahari
kuchukua hatua stahiki ili kuepuka uwezekano wa kupata madhara
yanayoweza kujitokeza.
“Mvua hizi ni kama zile zilizonyesha wiki
iliyopita. Wajibu wetu ni kutoa taarifa pale tunapoona kiwango cha juu
cha mvua na upepo ili watu wachukue tahadhari. Kwa watumiaji wa bahari
umakini uzidi kuongezeka kwani mawimbi yatakuwa makubwa na upepo wa
bahari utakuwa kilomita 30 kwa saa,” alisema Mutoni.
Ripoti iliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG) Profesa Musa Juma Assad imezichanganya Hospitali ya Taifa
Muhimbili na Bohari ya Dawa (MSD), huku Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akihitaji maelezo ya kina kuhusu
mkanganyiko huo.
Ummy ameitaka MSD kuandika maelezo ya kina kwa
maandishi, kuhusu vifaa vya Sh2 bilioni ambavyo viko njiani kwenda
Muhimbili kwa miaka minne sasa, kabla wizara yake haijatoa tamko rasmi.
Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu jana alisema bohari
haina mzigo wowote ulio njiani kuelekea Muhimbili bali imekuwa
ikisambaza dawa zake nchi nzima.
Bwanakunu alisema tatizo
lililojitokeza ni mfumo wa kompyuta ambao unaonyesha mzigo upo njiani,
hivyo muamala katika kompyuta unavyoshindwa kukamilika, mzigo lazima
uonekane upo njiani.
“Mwaka 2012 tulibadilisha mfumo wa kompyuta
kutoka wa awali mpaka tunaotumia sasa, hivyo kuna miamala ilihitaji
kubadilishwa, mwaka huu tulifanya zoezi la kukamilisha baadhi na si kwa
Muhimbili pekee kwa mfano kuna mzigo unatoka MSD Ubungo kwenda Mulebaukifika kule mtu anashindwa kuingiza kwenye mfumo kwamba
umepokelewa,” alisema Bwanakunu.
Alifafanua kwamba majibu ya MSD
kwa CAG yalieleza kuwa walitengeneza timu ya uchunguzi na baadhi ya watu
walichukuliwa hatua, “nimeshachukua hatua za haraka baada ya kupata
hiyo ripoti, tangu mwanzoni mwa mwaka huu wale ambao hawakujaza hiyo
miamala tulishawachukulia hatua, hakuna mali iliyopotea MSD.”
Taarifa
zaidi zinaeleza kwamba kuna ripoti ya Muhimbili ambayo inaonyesha katika
vitabu kwamba kuna mzigo ambao Muhimbili iliununua kutoka MSD, lakini
haujafika, lakini Bwanakunu alipoulizwa alisema hakuna vitabu
vinavyoonyesha kuwa Muhimbili inadai vifaa tiba na dawa MSD.
Kaimu
Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru
alisema kwa taarifa alizonazo mpaka sasa CAG alifanya ukaguzi katika
vitabu vya MSD na si wao na alipouliza vifaa viko wapi alijibiwa kuwa
vinakwenda MNH.
Alisema kuwa Watanzania wawe na subira na kwamba
watapewa majibu kesho (leo), baada ya Muhimbili kupekua kwa kina vitabu
vya mwaka 2012, ili kujiridhisha iwapo vifaa vilipokelewa au havikuwahi
kununuliwa Muhimbili.
“Hiyo ripoti tumeiona leo Jumanne. Hayo mambo
yametokea mwaka 2012 huwezi kuwa na jibu la kila kitu, kesho tunataka
tukapitie hiyo ripoti kwa sababu ni ukaguzi wa MSD, tukaangalie vitabu
hivyo vifaa vilifika?” Alisema Museru.
Naye Waziri Ummy Mwalimu
alisema katika ripoti hiyo kuna hoja mbili ambazo ni MSD na TFDA, huku
akifafanua kwamba amezungumza na Mkurugenzi wa MSD lakini hajaridhika na
majibu na kumtaka aandike maelezo ya kina.
“Nimetaka maelezo ya
maandishi kutoka kwa MSD na TFDA kuhusu ripoti ya CAG tumekubaliana na
Katibu Mkuu walete maandishi ndiyo tutatoa msimamo rasmi wa wizara, kwa
upande wa MSD ndiyo maana tuliweka pembeni wale wakurugenzi wanne sababu
ya changamoto hii ambayo CAG amekutana nayo,” alisema Ummy.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameivunja
Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kumsimamisha kazi
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt. Ally Yahaya Simba kutokana na
kutosimamia ipasavyo Mkataba wa utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa
mawasiliano ya simu (TTMS), na kusababisha nchi kupoteza mapato ya
takriban shilingi bilioni 400 kwa mwaka.
Rais Magufuli amechukua
hatua hiyo leo tarehe 26 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam baada
ya kufanya kikao cha kazi kati yake na viongozi na wataalamu kutoka
Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Wizara ya fedha na Mipango na
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Tarehe 22
Machi, 2013 Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) iliingia mkataba na
kampuni ya SGS juu ya uwekaji, uendeshaji na uhamishaji wa mapato ya
simu ambapo kampuni hiyo ilipaswa kutekeleza vipengele vitano lakini
mpaka sasa kampuni ya SGS haijaanza kutekeleza kipengele kidogo
kinachohusiana na uthibiti wa mapato ya simu za ndani (Offnet), hali
ambayo imesababisha serikali kukosa mapato yanayokadiriwa kuwa shilingi
bilioni 400 kwa mwaka.
Pamoja na kuivunja bodi ya TCRA
inayoongozwa na Profesa Haji Semboja na Kumsimamisha kazi Mkurugenzi
Mkuu wa TCRA Dkt. Ally Yahaya Simba, Rais Magufuli pia amemuagiza Waziri
wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa Mnyaa kumteua
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo mara moja.
Aidha, Rais
Magufuli amewataka Waziri Prof. Mbarawa, Katibu Mkuu na Naibu Katibu
katika wizara hiyo kuchukua hatua mara moja ili mfumo wa ukusanyaji wa
mapato ya simu kwa simu za ndani (Offnet) uanze kufanya kazi, na nchi
ipate mapato yanayostahili kukusanywa.
“Waziri hakikisha
unachukua hatua mara moja, nataka tukusanye mapato yote ya serikali
yanayostahili na sitasita kuchukua hatua dhidi ya yoyote
atakayekwamisha jambo hili” Amesisitiza Rais Magufuli.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU Dar es salaam 26 Aprili, 2016
Rais John Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 3,551, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya Muungano wa Tanzania.
Taarifa
iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja
Jenerali Projest Rwegasira ilisema wafungwa 580 wataachiwa huru, huku
wengine 2,971 watapunguziwa moja ya sita ya vifungo vyao.
Alisema
rais ametoa msamaha huo kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya ibara
ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aliwataja
watakaonufaika na msamaha huo kuwa ni wafungwa wenye ugonjwa wa ukimwi,
kifua kikuu na saratani ambao wapo kwenye hatua za mwisho. Wengine ni
wazee wenye umri wa miaka 70 na kuendelea, wajawazito na wale waliongia
na watoto gerezani.
Wafungwa wengine watakaonufaika na msamaha
huo ni wenye ulemavu wa akili ambao wamethibishwa na jopo la waganga
kuwa wana tatizo hilo.
Katibu mkuu wa wizara hiyo alisema
msamaha huo hautawagusa wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa au
kifungo cha maisha jela.
Pia, wafungwa wanaotumikia kifungo kwa
makosa ya usafirishaji na matumizi ya dawa za kulevya, upokeaji na
utoaji rushwa, matumizi mabaya ya madaraka, unyang’anyi kwa kutumia
silaha na kubaka ni miongoni mwa waliokosa msamaha huo.
Wengine
ambao hawataguswa na msamaha huo ni wale wanaotumikia vifungo kwa makosa
ya kupatikana na silaha, wizi wa magari na pikipiki, kuwapa mimba
wanafunzi na ubadhirifu wa fedha za Serikali.
Wafungwa wengine
watakaoendelea kubaki magerezani ni wale waliohukumiwa kutokana na
usafirishaji wa nyara za Serikali na ujangili, utekaji wa watoto,
biashara ya binadamu, kukutwa na viungo vya binadamu na waliojaribu
kutoroka wakiwa chini ya ulinzi.
Katika maadhimisho ya Uhuru
yaliyofanyika Desemba 9, 2015, Rais Magufuli aliwasamehe wafungwa 2,336,
kati ya hao 117 waliachiwa huru huku 2,219 wakipunguziwa moja ya sita
ya vifungo vyao.
Kwa idadi hiyo mpaka sasa wafungwa 5,887
wamenufaika na msamaha wa Rais Magufuli tangu aingie madarakani baada ya
kushinda katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, 2015.
Mke
wa Rais mstaafu wa Kenya, mama Lucy Kibaki amefariki dunia . Lucy
alifariki katika hospitali ya Bupa Cromwell mjini London alikokuwa
amelazwa.
Alisafrishwa hadi mjini Landon wiki moja iliopita kwa matibabu.
Akithibitisha
kifo chake rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa kenya
imesikitishwa na kifo cha mama Lucy mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai
Kibaki.
Katika taarifa iliotumwa katika vyombo vya habari Uhuru amesema bi Lucy amekuwa mgonjwa kwa kipindi cha mwezi mmoja .
Amesema
kuwa Kenya imempoteza mwanamke aliyechangia mengi katika maendeleo ya
taifa la Kenya hususan katika vita dhidi ya ugonjwa wa ukimwi.
Rais ametuma risala za rambi rambi kwa mtangulizi wake Mwai Kibaki pamoja na familia yake.