Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema imeanza
kutekeleza mikakati mipya ya ukusanyaji wa mikopo ya elimu ya juu kutoka
wadaiwa ambayo itaongeza wastani wa ukusanyaji wa Tshs 2.6 bilioni za
sasa hadi kufikia Tshs 8 bilioni ifikapo mwezi Julai mwaka huu.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Jerry Sabi ameyasema hayo leo
(Jumatano, Machi 30, 2016) jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea
mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii iliyotembelea
ofisi za Bodi hiyo zilizopo Mwenge.
“Hadi mwezi uliopita
(Februari, 2016) tulikuwa tunakusanya wastani wa shilingi bilioni 2.6
kwa mwezi, lakini sasa tumeongeza kasi na mikakati mipya ambayo
itawezesha kukusanya shilingi bilioni 6 mwezi Aprili na shilingi bilioni
8 ifikapo mwezi Juni mwaka huu,” amesema Bw. Sabi aliyeteuliwa kushika
nafasi hiyo na miezi miwili iliyopita.
HESLB ilianzishwa ilianza
kazi mwaka 2005 ili kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji na pia
kukusanya mikopo kwa wanufaika. Hadi sasa, zaidi ya shilingi 2.1
trilioni zimetolewa kwa wanufaika na kati ya fedha hizi, mikopo iliyoiva
na inayopaswa kukusanywa ni shilingi 258 bilioni ambazo wanufaika wake
wamemaliza au kusitisha masomo yao na vilevile kumaliza muda wa
kujipanga kuanza kulipa (grace period).
Kwa mujibu wa Bw. Sabi,
hadi sasa, HESLB imekusanya shilingi 91 bilioni kati ya shilingi 258
bilioni zilizoiva na hivyo kupaswa kukusanya.
Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji huyo alikuwa akijibu hoja zilizotolewa na Wajumbe wa Kamati
hiyo waliokutana na watendaji wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Mafunzo ya Ufundi na HESLB wakiongozwa na Waziri Prof. Joyce Ndalichako
na Naibu wake Mhandisi Stella Manyanya.
Bw. Sabi alitaja
mikakati mipya iliyobuniwa na HESLB kuwa ni pamoja na kuimarisha mtandao
baina ya Bodi na waajiri kutoka sekta binafsi na umma ambao unalenga
kubaini na kukusanya kiasi cha shilingi 7.02 bilioni kwa mwaka kutoka
kwa wanufaika 136,252.
“Tunapata ushirikiano mkubwa kutoka kwa
taasisi za Serikali na sasa tumejipanga kupitia upya mitandao ya waajiri
kwa kushirikiano na taasisi kama Chama cha Waajiri (ATE), Mfuko wa
Sekta Binafsi (TPSF) na Shirikisho la Asasi zisizo za Kiserikali (TANGO)
ili kuhuisha takwimu zetu kuhusu waajiri ili kukusanya taarifa za
wadaiwa wapya kwa haraka,” alifafanua Bw. Sabi.
Mikakati mingine
ni kutoa elimu na kuimarisha ushirikiano na wadau mahsusi kama Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Usimamizi wa Mashirika ya Hifadhi
za Jamii (SSRA), Wakala wa Usajili wa Makampuni (BRELA), Kituo cha
Uwekezaji Tanzania (TIC), Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa
Hesabu Tanzania (NBAA) na vyama vya kitaaluma.
Akizungumza katika
mkutano huo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma
Kaskazini Bw. Peter Serukamba ameitaka HESLB kuongeza kasi ya kudai
mikopo iliyoiva na kuutaka uongozi wa HESLB kuandaa orodha ya wadaiwa
wote na kuiwasilisha kwa kamati ili ifanyiwe kazi.
“Ni lazima
kuwe na fedha ili kuwezesha kutoa mikopo kwa wahitaji wengine
...haiwezekani mtu anapata mkopo halafu halipi...andaeni orodha ya wote
walionufaika na mikopo ambayo itaonyesha nani halipi, nani analipa na
nani amemaliza na tutaamua tufanye nini,” alisema Serukamba.
HESLB
ilianzishwa mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai mwaka 2005 kwa
lengo la kutoa mikopo kwa watanzania wahitaji waliopata nafasi za masomo
katika vyuo vya elimu ya juu na kukusanya mikopo iliyoiva kutoka kwa
wadaiwa walionufaika na mikopo tangu mwaka 1994.
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY Dada wa marehemu akilia baada ya mdogo wake kujinyonga.
STORI: Dustan Shekidele, Wikienda
Morogoro: Mshtuko! Mwanafunzi wa wa darasa la tano katika Shule ya
Msingi Mchikichini ‘B’ ya mjini hapa, Anosisye Gidion (12), ameacha
viulizo kibao baada ya kujinyonga kwa kutumia kitenge cha mama yake,
Judith Kilalu ‘Mama Kapipi’.
Tukio hilo la kuhuzunisha lilijiri
mwishoni mwa wiki iliyopita, majira ya saa 1:00 asubuhi nyumbani kwao
maeneo ya Mji Mpya mjini hapa.
Kitenge cha mama yake alichotumia kujinyongea.
Kwa mujibu wa
mashuhuda wa tukio hilo, Ashura na rafiki wa marehemu, Hussein walisema
kuwa chanzo cha denti huyo kujinyonga kilidaiwa kuwa ni kitendo cha mama
yake kumchapa na kumtishia kumpeleka polisi baada ya kuchukizwa na
kitendo chake cha kurudi nyumbani saa 6:00 usiku huku akidaiwa kuonekana
akiwa na kundi haramu la vibaka la Kizazi Jeuri.
Mama mzazi akilia kwa uchungu.
“Anosisye
alichelewa kurudi nyumbani, ilipofika saa 4:00 usiku, mama yake aliamua
kumtafuta akaambiwa alionekana akiwa na lile kundi lililokupora wewe
(mwandishi wetu) maeneo ya Stendi ya Daladala ya Mji Mpya,” alisema
mmoja wa mashuhuda hao huku akirekodiwa.
Mashuhuda wakifuatilia tukio hilo.
Kwa
upande wake, mama mzazi wa denti huyo aliyeangushiwa zigo la lawama juu
ya kifo cha mwanaye alisema: “Mwanangu alichelewa kurudi nyumbani
usiku. Nilizunguka kumtafuta, nikaambiwa alionekana akiwa na Kizazi
Jeuri hivyo nilimchapa sana na kumtisha kukicha nitampeleka polisi.
“Kulipokucha aliandaa nguo za shule, cha ajabu nimemkuta amejinyonga. Inauma sana jamani.”
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Makaburi B, Amiri Kombo
aliyekuwepo eneo la tukio alithibitisha kutokea kwa tukio hilo katika
mtaa wake.
Polisi wakichukua mwili wa marehemu kwaajili ya uchunguzi.
Wazazi
wanahofia watoto wao kujiunga na kundi hilo lililomvamia mwandishi wetu
na kumpora kamera na simu ambao aliwafungulia jalada la kesi namba
MOR\RB\140\2016 hivyo wanasakwa na polisi.
Minister for Education and Vocational Training Joyce Ndalichako.
St Joseph University of Tanzania (SJUIT) will run next
academic year due to start in October without new students, succumbing
to pressure by the nation’s high academic overseer organization,
Tanzania Commission for Universities (TCU) that barred the new entry
pending settlements of academic discrepancies.
The academic hitches defying TCU standards that led to the latest
intake freeze in a row of other sanctioned harassments involving closure
of the Catholic Church-run Songea and Arusha campuses, included an
allegedly poor quality education.
The decision by TCU at the SJUIT Luguruni campus in Dar es Salaam
comes barely a month after it revoked the registration of the subsidiary
campus in Songea and Arusha for failure to meet the quality assurance
standards.
The Luguruni campus was then spared, pending the release of
evaluation report from TCU before the commencement of the second
semester this week.
However, it was all not that bad news for the struggling university
as TCU released the evaluation report this week, saying it would not
revoke approval of the remaining Luguruni and Boko campuses in Dar es
Salaam.
“TCU has made its evaluation and found out that the existing
challenges at the Luguruni campus can be solved at the university’s
administrative levels under our supervision” the TCU Executive Secretary
Professor Yunus Mgaya told the Guardian on Sunday on Friday.
“We allow commencement of their daily academic activities on a
condition that they do not enroll new students for this academic year
until the outlined challenges are settled,” he said.
The Commission, among others, has ordered the university authority
to equip the institution with an adequate number of qualified lecturers
including Ph.D. holders and professors, to increase the number of
workshops, laboratories and other facilities.
Earlier, students at the university staged a strike in a protest
against high tuition fees and low quality education, but the Minister
for Education and Vocational Training Joyce Ndalichako ordered them to
go back to classes, amid pledges she would work with the university
authorities to address their claims.
However, Professor Mgaya confirmed to this paper that TCU is
currently scrutinizing the International Medical and Technological
University (IMTU) on its way to Kampala International University (KIU),
the two institutions notoriously chronic in violation of the
commission’s values centred on the provision of quality education.
“This is the nationwide exercise to awaken universities into
proper implementation of their duties and challenging them into
delivering quality university education,” he said.
He said a team of experts from the Ministry of Health, Community
Development, Gender, Elderly and Children, a professor from Muhimbili
University of Health and Allied Sciences (MUHAS) and TCU started
evaluation processes at IMTU earlier this week.
He said the report on IMTU may be released to public if so deemed
necessary, noting the commission was especially keen in inspecting a
number of universities whose records call for consistent scrutiny.
“We cannot do it all alone because it is an exercise that needs a
lot of human resources, that’s why we have to involve professors and
officials from relevant ministries in this,” said Prof. Mgaya.
In February TCU revoked accreditation of St Joseph University
College of Agricultural Science (SJUCAST) and St Joseph University
College of Information (SJUCIT) based in Ruvuma region and Saint Joseph
Arusha Campus barely five years since its establishment, citing gross
underperformance.
Following the revocation, more than 3,603 students of the three
constituent colleges were transferred by TCU to other higher learning
institutions with immediate effect.
According to section 5(1) of the Universities Act, Cap.346 of the
Laws of Tanzania, the Commission is mandated among other things, to
oversee and regulate quality as well as the general management and
performance of universities.
Taarifa
zilizotufikia hivi punde zinasema, Gari lenye namba za usajili T598 BEL
Toyota Landcruser,limepata ajali maeneo ya Mbezi Beach Africana, Dereva
hajafahamika kutokana na kuungua .Gari lipo Polisi Kawe.