Saturday, 12 March 2016

HII HAPA LIST YENYE MAJINA YA WANAFUNZI WA ST.JOSEPH AMBAO TAARIFA ZAO ZINAMISS

Share:

TAARIFA KWA UMMA:TANGAZO KWA UMMA KUTOKA NACTE KUHUSU APPLICATION 2016/2017

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

TAARIFA KWA UMMA

TAREHE 11 MACHI 2016

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuutangazia umma kuwa waombaji wenye Stashahada (Ordinary Diploma – NTA Level 6) wanaoomba kujiunga na Shahada ya Kwanza zinazotolewa na  Vyuo Vikuu (Universities) au Vyuo Vikuu Vishiriki (Constituent Colleges of Universities) hawataweza kufanya hivyo sasa. Hii ni kwasababu Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) bado haijafungua rasmi Mfumo wa Udahili wa pamoja (CAS) unaoratibiwa kwa pamoja kati ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)  na  Tume ya Vyuo Vikuu (TCU). Tume ya vyuo vikuu inatarajia kufungua mfumo huo wa kudahili kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza mara baada ya matokeo ya kidato cha sita kutangazwa na Baraza la Mitihani la Tanzania
Share:

Maombi ya nafasi za mafunzo kozi za afya mwaka wa masomo Machi 2016/2017,deadline ni tarehe 31/3/2016 -masomo yataanza tare 28/4/2016

Share:

MAJINA YA NYONGEZA WANAFUNZI WA ST.JOSEPH WALIOHAMISHIWA CHUO KIKUU SUA,RUCO,MWENGE NA UDOM 2016

Share:

NAFASI MPYA ZA KAZI MARCH 2016-SEKRETARIETI YA AJIRA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

PropertyValue
Name:TANGAZO LA KAZI 11 MAR 2016-KISW
Description:Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 24 Machi, 2016
Filename:MARCH -KISWA1.pdf
Filesize: 322.19 kB
Filetype:pdf (Mime Type: application/pdf)
Creator:psrsweb
Created On: 03/12/2016 05:19
Viewers:Everybody
Maintained by:Editor
Hits:3795 Hits
Last updated on: 03/12/2016 05:19
Homepage:

Share:

New AUDIO | Queen Syrah - Ndege | Download

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
http://old.hulkshare.com/dl/4bfnof9hjlmo/Queen_Syrrah_-_Ndege.mp3?d=1
Share:

New AUDIO | G.nako Ft. Nikki wa II, Chin Bees - AROSTO | Download

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
http://old.hulkshare.com/dl/unu6gkvn6akg/G.nako_FT._Nikki_wa_II%2C_Chin_Bees_-_AROSTO.mp3?d=1
Share:

Official VIDEO | Sajna Vanilla - HOFU

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
https://youtu.be/LjuILnqJ3dY
Share:

Uchaguzi wa Meya Jiji la Dar kufanyika Kabla ya Tarehe 25 Mwezi Huu

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY



Hatimaye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene amemaliza mzozo wa uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es Salaam baada ya kuagiza ufanyike kabla ya Machi 25 na kutaja sifa za wapigakura.


Uamuzi huo wa kutangaza tarehe na sifa za wapigakura unaonekana kuwa ahueni kwa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ambavyo vilifurahia hatua kama hiyo, lakini wadau wa CCM wakafungua kesi iliyosababisha uchaguzi huo uahirishwe mara tatu.


Simbachawene, ambaye aliwahi kuagiza uchaguzi huo ufanyike kabla ya Februari 29 lakini ukakwama mara tatu, aliwaambia waandishi wa habari jana mjini Arisha kuwa uchaguzi huo utafanyika kwa kuzingatia kifungu cha 13 (1) cha Kanuni za Kudumu za Jiji.


Alisema watakaopiga kura katika uchaguzi huo ni madiwani wote wa halmashauri za jiji la Dar es Salaam ambazo ni Ilala, Temeke na Kinondoni, wabunge wa kuchaguliwa na wabunge wa viti maalumu ambao mchakato wa kuwapata ulianzia kwenye mamlaka za halmashauri hizo.


Simbachawene alisema wapigakura wengine watakuwa ni wabunge wa kuteuliwa na Rais, ambao ni Dk Philip Mpango, Balozi Agustine Mahiga, Dk Ackson Tulia, Profesa Joyce Ndalichako, Dk Abdallah Possi, Profesa Makame Mbarawa ambao ni wakazi wa jijini Dar es Salaam.


“Tunaomba vyama kuheshimu misingi ya demokrasia kwa kukubali matokeo ili kutosimamisha maendeleo ya jiji la Dar es Salaam,” alisema.


Taarifa ya tarehe ya uchaguzi huo na sifa za wapigakura imepokewa vizuri na viongozi wa Ukawa, ambao walitaka tamko hilo litolewe ndani ya siku saba na Serikali ibainishe sifa za wajumbe watakaoingia kupiga kura.


Kwa uamuzi huo wa Simbachawene, Ukawa, ambayo ina madiwani na wabunge kutoka vyama vya CUF na Chadema, itaingia kwenye uchaguzi ikiwa na wapigakura 87, huku CCM ikiwa na 76.


Akizungumza baada ya kupata taarifa hizo jana, Katibu wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kilewo alisema Simbachawene amesikia agizo lao walilotaka kupewa mapema tarehe ya uchaguzi huo.


“Kimsingi zile siku saba zilikuwa zinaisha leo (jana). Kwa hiyo Waziri Simbachawene ametumia busara. Hivyo ndivyo kiongozi anatakiwa kuwa,” alisema Kilewo.


Kilewo aliitaka CCM kujianda kisaikolojia, akisema wasitarajie ushindi kwa kuwa licha ya kuongezewa wajumbe, Ukawa bado wana hazina kubwa ya wajumbe.


“Tumeshapata taarifa kuwa wamepanga kuwakamata baadhi ya wajumbe wetu ili idadi ipungue. Nawaambia wasisithubutu kufanya mchezo huu bali wakubali yaishe na kuachia jiji,” alisema Kilewo.


Kwa takriban miezi miwili, uchaguzi katika jiji la Dar es Salaam umesimama kutokana na mvutano baina ya CCM na Ukawa, hasa wa uhalali wa wajumbe halali wa kupiga kura.


Kutokana na mgogoro huo, wabunge watatu wa Chadema, Halima Mdee wa Kawe, Mwita Waitara (Ukonga) na Said Kubenea (Ubungo) wameshtakiwa kwa tuhuma za kusababisha vurugu baada ya kusitishwa uchaguzi huo hivi karibuni kwa kutumia zuio hilo ambalo limebainika kuwa batili.


Akizungumzia zuio hilo, Simbachawene alisema lilikuwa ni batili kwa kuwa lilitolewa wakati tayari kesi ya msingi ilikuwa imetolewa uamuzi tangu Februari 23.
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MARCH 12 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY





Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger