Afisa wa polisi wa trafiki anauguza majeraha kwenye uso wake baada ya kushambuliwa na raia alipokuwa kazini.
Kisa hicho kimefanyika Jumapili Novemba 7,2021 katika mzunguko wa magari eneo la Kariokor jijini Nairobi nchini Kenya ambapo Afisa huyo alikuwa akisaidia kuelekeza magari wakati jamaa mmoja aliibuka ghafla na kumtwanga ngumi usoni.
Kutokana na ngumi hiyo nzito aliyopigwa na mhuni huyo, Askari poli alishikwa na kizunguzungu na kuanguka huku akivunja damu na ndipo Msamaria Mwema akamkimbiza hospitali
Kwa mujibu wa DCI, afisa huyo alikuwa katika mzunguko wa Kariokor jijini Nairobi wakati kisa hicho kilifanyika.
Taarifa ya DCI ilisema afisa huyo alikuwa akisaidia kufungua foleni/ msongamano wa magari kabla ya jamaa huyo kuibuka ghafla na kumuangushia ngumi nzito.
"Afisa huyo alikuwa akisaidia kuelekeza magari katika mzunguko wa Kariokor wakati mwanaume huyo alimshambulia kwa kumpiga ngumi na kisha kutoweka huku akimwacha afisa huyo amepasuka usoni karibu na jicho," DCI walisema.
Msamaria mwema aliyeshuhudia kisa hicho alimkimbiza afisa huyo hospitalini ambapo alipokea matibabu na kuruhusiwa kuondoka.
Ni kisa ambacho kiliwaacha madereva katika mzunguko huo kwa mshangao huku msongamano mkubwa wa magari ukishuhudiwa. Makachero wa DCI wanaendelea kuchunguza kisa hicho ili aliyetekeleza uvamizi huo kukamatwa.
Yeyote aliye na habari ametakiwa kusaidia makachero kumtia mbaroni mhuni huyo ili ashtakiwe kwa kosa hilo.
Chanzo - Tuko News
0 comments:
Post a Comment