Sunday, 7 November 2021

MWENYEKITI WA CCM SAMIA SULUHU AFUNGA MAFUNZO YA MAKATIBU WA CCM

...

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifunga mafunzo ya makatibu wa wilaya na mikoa wa Chama hicho

Na Dotto Kwilasa, DODOMA.

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefunga mafunzo ya makatibu wa wilaya na mikoa wa Chama hicho katika ukumbi wa NEC Makao Makuu ya Chama Jijini Dodoma jana Jumamosi tarehe 6 Novemba, 2021.

Aidha mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku nne kuanzia tarehe 3 Novemba, 2021,yanatajwa na wanachama wa Chama hicho kuwa yataongeza tija na ari ya uongozi na hatimaye kifikia maendeleo ya pamoja.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya habari na Katibu wa uenezi wa Chama hicho Shaka Hamdu Shaka ,amesema Rais Samia ameridhia utaratibu wa mafunzo ndani ya Chama Cha Mapinduzi na kwamba utakuwa endelevu.

Aidha kutokana na umuhimu wake katika kukidhi mahitaji ya wakati na mabadiliko ya mwenendo wa siasa za Sasa,mafunzo hayo yatakuwa na manufaa katika kuleta mabadiliko ya kiutendaji na ufanisi.

Shaka amesema,mafunzo hayo ni nyenzo muhimu sana katika kuongeza weledi na ufanisi wakufikia malengo ya taasisi yoyote ile.

"Chama Cha Mapinduzi tutafanya utaratibu huu kuwa endelevu ili kukidhimahitaji ya wakati na mwenendo wa mabadiliko ya siasa za dunia,kutokana na mafunzo haya Mama Samia ametuonyesha namna ambavyo uongozi ni kushirikishana,lakini pia ametukumbusha kutimiza wajibu wetu kwa wakati,"amesema Shaka.

Licha ya hayo Shaka ameeleza Katika taarifa yake kwamba Katika mafunzo hayo Rais Samia amehimiza umoja,mshikamano na maelewano miongoni mwa viongozi na wanachama wa CCM ilikazi ya kuendelea kukiimarisha chama katika kuwatumikia wananchi iweniendelevu na ya kudumu.

"Tukifanya hivi hatimaye tutaleta tija hasa ikizingatiwa kuwa Chama ChaMapinduzi kimebeba matumaini makubwa ya watanzania katika kuwaleteamaendeleo endelevu ya kiuchumi,kijamii na kisiasa,"amefafanua.

Mbali na hayo ameeleza mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo wa kiutendaji Viongozi hao ikiwa ni pamoja na uweledi na ufanisi.

"Tuna imani sasa kwamba Watendaji wa CCM wa Mikoa na Wilaya katika kusimamia katiba ya chama,kanuni,ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025,maelekezo ya vikao na masuala mbalimbali ya kuisimamia serikali na ujenziwaTaifa,"amesisitiza.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Rais Samia Suluhu Hassan akipunga mkono kwa Watendaji wa Chama hicho ngazi ya mikoa na Wilaya jijini Dodoma
Katibu wa uenezi wa Chama hicho Shaka Hamdu Shaka akizungumza kwenye mafunzo hayo
Makatibu wa wilaya na mikoa wa CCM wakiwa Katika mkutano, ukumbi wa NEC Makao Makuu ya Chama Jijini Dodoma Jumamosi tarehe 6 Novemba, 2021.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger