Sunday, 7 November 2021

MWANAFUNZI AKUTWA AMEFARIKI HOSTELI

...

Familia moja mjini Kisii Nchini Kenya imeziomba mamlaka za uchunguzi kubaini kilichomuua mtoto wao wa kiume aliyekutwa amefariki kwenye kitanda chake ndani ya bweni lao shule yao.

Taarifa zinaeleza kuwa marehemu Enock Morara ambaye alikuwa mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Upili ya St.Paul Amasago eneo la Keumbu, kaunti ya Kisii alilala kama kawaida lakini hakuamka kama wenzake walivyoamka na baadaye akagundulika amefariki.

Uchunguzi wa kitabibu uliofanyika katika hospitali ya Rufaa ya Kisii bado haujabaini chanzo cha kifo cha mtoto huyo.

Wakati huo huo, maofisa wa Polisi nao wanaendelea na uchunguzi zaidi kuhusu kifo cha mwanafunzi huyo.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger