Mama mzazi wa kijana Hamza Mohammed aliyeshambulia na kuua askari wanne kwa risasi kabla ya yeye kuuawa kwa kupigwa katika maeneo ya Ubalozi wa Ufaransa, Bi. Sofia Hassan Askari amefariki dunia.
Bi. Sofia amefariki jana Jumapili, Novemba 7, 2021 na anatarajia kuzikwa kesho saa 7 mchana kwa mujibu wa taarifa za kifamilia.
Jina la Askari ni la utani ambalo alipewa kutokana na mume wake kuwa askari (miaka ya nyuma) wakati akiishi katika maeneo ya Upanga jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment