Washindi wa uchaguzi kwenye kura za maoni za Ubunge wa CHADEMA waliopita kwenye majimbo yao ni kama ifuatavyo:
1.Mshindi Jimbo la Kawe ni Halima Mdee mwenye kura 63 (71.5%).
2. Tarime Mjini mshindi ni Esther Matiko mwenye kura 80 (97. 6%)
3. Tarime Vijijini mshindi ni John Heche ambaye amepata kura 268 (99.2%) .
-Heche alikuwa Mgombea pekee na alihitaji tu kura za Ndio au Hapana, kwenye kura zilizopigwa, kura za Ndio ni 268 (99.2%),zilizoharibika ni 2 (0.74%) hakuna kura ya Hapana
4. Mshindi Jimbo la Bunda Mjini ni Ester Bulaya mwenye kura 126
5. Jimbo la Iramba mshindi ni Jesca Kishoa mwenye kura 134 (98%) .
- Jesca alikuwa Mgombea pekee na alihitaji tu kura za Ndio au Hapana, kwenye kura 136 zilizopigwa, kura za Ndio ni 134 (98%), zilizoharibika ni 2 na hakuna kura ya Hapana.
6. Jimbo la Isimani mshindi ni Patrick Ole Sosopi mwenye kura 115 (82.6%).
7.Mshindi jimbo la Mbeya Mjini ni Joseph Mbilinyi (Sugu) mwenye kura 294
- Sugu alikuwa ni Mgombea pekee na alihitaji tu kura za Ndio au Hapana ambapo amepata Ndio 294 na Hapana 5.
0 comments:
Post a Comment