Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Shinyanga, Dotto Simon Joshua akimkabidhi Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu (kushoto) fomu ya kuomba ridhaa ya CCM kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Shinyanga, Dotto Simon Joshua leo Julai 16,2020 amerudisha fomu ya kuomba ridhaa ya CCM kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Akizungumza baada ya kurejesha fomu katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini kwa Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu, Dotto Simon Joshua amesema amefanya mambo mengi kupitia Jumuiya ya Vijana hivyo anakiomba chama chake kimpe nafasi ya Ubunge ili niweze kuwasaidia wananchi wa Jimbo la Shinyanga Mjini katika kuleta maendeleo katika Jimbo letu.
"Mimi kama Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini na Vijana wote wa Shinyanga Mjini ni Mashahidi wa mambo makubwa ambayo Mhe. Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli anayafanya katika nchi hii,nimeamua kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya Wanachama wa Chama cha Mapinduzi kuwa mgombea wa Ubunge wa Jimbo la SHINYANGA MJINI ili kuendeleza mazuri yote yanayofanya na yanayoendelea kufanywa na serikali ya CCM",amesema Joshua.
"Vijana wa Shinyanga mjini wameniamini na kuniomba kuomba ridhaa ya Kuwa mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini ili kukimbiza maendeleo ya Jimbo letu kwa ujumla",amesema.
0 comments:
Post a Comment