Thursday, 16 July 2020

MDAU WA MAENDELEO JOSEPH GORYO 'MUDDY' ACHUKUA NA KUREJESHA FOMU YA UDIWANI CCM-LAMADI

...


Mdau wa Maendeleo Mkoa wa Simiyu, Joseph Goryo 'Muddy' akionesha fomu yake aliyoichukua kutia nia kiti cha Udiwani ndani ya CCM Lamadi.
Mdau wa Maendeleo Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, Joseph Goryo 'Muddy' ametia nia kuwania kiti cha Udiwani ndani ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Kata ya Lamadi.

Goryo amechukua na kurejesha fomu hiyo na kwa sasa anasubiria hatua nyingine zaidi ndani ya Chama chake.


Goryo amekuwa mdau mkubwa wa Maendeleo kwa kusaidia masuala ya kijamii ikiwemo kutoa misaada ndani na nje ya mkoa wake huo wa Simiyu pia ni Mfanyabiashara, Mkulima na mfugaji.

Hata hivyo Goryo hakuwa tayari kuzungumzia hatua yake hiyo akiomba Wanahabari na wadau wasubirie muda muafaka ukifika  ataeleza kwa kina katika nia yake hiyo ya kuwatumikia wana Lamadi kupitia nafasi ya Udiwani endapo atapitishwa na chama na kisha kugombea.

Goryo amekuwa na shauku ya kuona safari ya Lamadi mpya yenye maendeleo ya kisasa inatimia.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger