
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imewataka wananchi kupiga picha (Screen shot) ujumbe wowote katika mitandao ya kijamii unaopotosha kuhusu corona na kuwatumia.
Tangazo hilo linakuja siku chache baada ya tangazo la awali la kuwaonya wanaosambara taarifa au picha za masuala ya corona kwenye mitandao ya kijamii atachukuliwa hatua.
“Ukipokea au ukiona ujumbe unaochochea, kuzusha au kupotosha taarifa za corona katika group (kundi) lako au lolote lingine mtandaoni, piga picha ujumbe huo na namna ya aliyetuma na utume TCRA kupitia namba 0737 300 300 au Kwa barua pepe : nocorona@tcra.go.tz” ,linasema tangazo hilo.
"Maadmin wa Magroup ya Mitandao ya Kijamii ambao mitandao yao itabainika kuwa inatuma taarifa za uongo,uchochezi au uzushi kuhusu Ugonjwa Corona watawajibika,"Chukua Tahadhari', Tutumie Mawasiliano Kujiletea Maendeleo ",linaeleza tangazo jingine la TCRA.
"Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inatambua mchango wa watoa huduma za mawasiliano dhidi ya janga hili la mpito la ugonjwa wa Corona (Covid - 19). Taifa linawategemea mtuvushe salama kupitia huduma zenu. Tutumie Mawasiliano Kujiletea Maendeleo", - TCRA


0 comments:
Post a Comment