Wednesday, 8 January 2020

Israel Yatoa Onyo Kama Itashambuliwa na Iran

...
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameonya kwamba nchi yake italipiza kisasi kwa yoyote atakayewashambulia, huku akirejelea matamshi yake ya kuiunga mkono hatua ya Marekani ya kumuua mkuu wa kikosi maalumu cha Iran Jenerali Qassemi Soleimani wiki iliyopita. 

Amesema mjini Jerusalem kwamba yoyote atakayewashambulia atakabiliwa na hatua kali ya kulipiza kisasi na kuongeza kuwa Israel inasimama kikamilifu na uamuzi wa rais wa Marekani Donald Trump na kuongeza kuwa anahitaji kupongezwa kwa kuchukua hatua hiyo kwa utaratibu, ujasiri na umadhubuti.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger