Tuesday, 22 October 2019

Ofisa Takukuru atiwa mbaroni kwa madai ya kumuua Mkewe kwa Risasi

...
Ofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilayani Tunduru, James Paulo (27), anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuua kwa kumpiga risasi mke wake.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kufanya kitendo hicho usiku wa kuamkia Oktoba 21, mwaka huu, baada ya kutokea ugomvi kati yao.

Kamanda Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Maigwa, amethibitisha kuwapo kwa tukio hilo na kwamba chanzo cha kifo hicho ni ugomvi uliosababishwa na tukio la wivu wa kimpenzi.

Kamanda alimtaja mtu aliyeuawa kuwa ni Beatha Kufuru (25), ambaye alikuwa muuguzi katika Hospitali ya Wilaya ya Tunduru.

Kamanda Marwa ambaye alikuwa akizungumzia tukio hilo akiwa njiani kwenda Tunduru ili kujiridhisha na hali halisi, alisema mtuhumiwa huyo alimpiga risasi tatu kichwani na kusababisha kifo chake papo hapo.

Alisema polisi wanaendelea na uchuguzi wa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya kukamilika kwa taratibu za kisheria.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger