Monday, 14 October 2019

Ndege mpya Dreamliner ya ATCL yafanyiwa majaribio Marekani

...
Ndege  mpya ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) aina ya Boeing 787-8 5H-TCJ Dreamliner ipo katika hatua za mwisho nchini Marekani kuja nchini, ambako inaundwa.

Jana, ofisa wa kitengo cha habari cha kampuni ya Boeing, Jennifer Schuld alituma picha za ndege hiyo aina ya Boeing 787-8 na kueleza kuwa ipo kwenye majaribio.

“Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania imeanza majaribio ya kuruka leo. Ndege hii 787 inaitwa Rubondo Island,” aliandika ofisa huyo kwenye ujumbe alioutuma kwenye akaunti yake ya Twitter ikiwa sambamba na picha kadhaa za ndege hiyo.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger