Baraza la Uuguzi na Ukunga nchini Tanzania, limeisimamisha kwa muda wa miezi mitatu leseni ya muuguzi, aliyemchoma sindano ya usingizi na kisha kumbaka, msichana mwenye umri wa miaka 16, aliyekuwa akimuuguza mama yake, katika hospitali ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora.
Inaelezwa kuwa muuguzi huyo Damiani Samson Mgaya, mnamo mwaka 2017, akiwa katika kituo cha Afya cha Igurubi , wilayani humo alishawahi kufanya tukio kama hilo, ambapo alipelekwa polisi na kisha mahakamani na hatimae aliachiwa huru na kurejeshwa kazini mwaka 2018.
Taarifa hiyo imetolewa leo Oktoba 18, 2019, na Msajili wa Baraza hilo Agnes Mtawa na kusema kuwa baada ya mtumishi huyo kurejeshwa kazini, alihamishwa kutoka kituo cha Afya cha Igurubi na kupelekwa katika hospitali ya Wilaya ya Igunga.
Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa baada ya kufanya ufuatiliaji, ilibainika kuwa mtumishi huyo alitoroka kituoni hapo na kuviomba vyombo vya ulinzi na usalama, vimsake popote alipo ili akamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria.
0 comments:
Post a Comment