Friday, 18 October 2019

AUAWA KWA KUPIGWA RISASI YA MAKALIO KAHAMA

...
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kijana aitwaye Mishael Masatu (29) amefariki dunia baada ya kujeruhiwa kwa kupigwa risasi kwenye makalio na mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi iitwayo Serengeti Security Services Ltd, mkazi wa mtaa wa Malunga akiwa kazini kwenye yard ya magari katika kisima cha mafuta cha PetroAfrica mtaa wa Mbulu Kahama Mjini.

Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao tukio hilo limetokea Oktoba 16,2019 majira ya tisa alfajiri.

"Mlinzi wa kampuni ya Ulinzi ya Serengeti Security Services LTD  Isumail Hassan (20) mkazi wa mtaa wa Malunga akiwa kazini hapo kisimani, alifyatua risasi moja kutoka kwenye bunduki aina ya Shortgun yenye namba HP.9-1.  007710112 mali ya Kampuni ya Serengeti Security Services LTD na kumjeruhi matakoni mtu aliyekutwa na kitambulisho chenye jina la Mishael Z. Masatu(29), mkazi wa Nyihogo mtaa wa Sazia ambaye aliingia kwenye yard hiyo bila kibali",ameeleza Kamanda Abwao.

 "Chanzo cha tukio ni majeruhi kuingia kwenye yard bila kibali na kudhaniwa kuwa ni mwizi. majeruhi alianza kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Halmashauri Mji wa Kahama na baadaye alifariki dunia",amesema Kamanda Abwao.

Amesema askari mlinzi  anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Wilaya Kahama wakati upelelezi unaendelea.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger