Wednesday, 22 May 2019

WAFANYAKAZI WA MAJI TAKA WAFARIKI DUNIA KWA KUTUMBUKIA KWENYE LINDI LA CHOO

...
Wafanyakazi wanne wa kampuni ya Maji safi na Taka ya Mavoko Water (Mavwasco) wamefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye (chamber)lindi la choo.

 Mkasa huo umetokea Jumanne, Mei 21,2019 katika kijiji cha makazi duni cha Kwa Mang'eli pembezoni mwa Mto Athi Kaunti ya Machakos nchini Kenya wakati wafanyakazi hao wa kampuni ya Maji safi na Taka ya Mavoko Water (Mavwasco) walipokuwa kazini. 

Wafanyakazi hao wa Kampuni ya Maji na Maji taka Mavoko Kaunti ya Machakos na walitumbukia wakiwa wa Mang'eli.

Maafisa wa polisi, zima moto, wananchi na maafisa wengine wa mkoa walishirikiana na chifu wa Mavoko Nzau Komo katika shughuli za kuiopoa miili hiyo.

 Kulingana na chifu, wanne hao walishindwa kujiokoa na walikosa hewa safi ingawa ripoti ya uchunguzi wa daktari utathibitisha kilichowaua.

 "Tunashuku wafanyakazi hao wa Mavwasco walikosa hewa safi na kufariki dunia, bado hatujajua chanzo cha vifo hivyo," alisema. 

Ripoti zaidi ni ya Trizah Mwikali, Ripota wa TUKO. 
Via>>Tuko
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger